AI-assisted research summary: Hati hii inavunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia 31 Julai 2020.
Hati ya Kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka, 2020 ISSN 0856-033X JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Toleo Na. 29 13 Julai, 2020 TOLEO MAALUM to the Special Gazette of the United Republic of Tanzania No. 29 Vol. 101 dated 13th July, 2020 Printed by the Government Printer, Dodoma by order of Government TANGAZO LA SERIKALI NA. 532 la tarehe13/7/2020 KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA, 1977 (SURA YA 2) HATI (Imetolewa kwa mujibu wa Ibara ya 90(2)(a)) HATI YA KUVUNJWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA, 2020 KWA KUWA, imekusudiwa kufanyika Uchaguzi Mkuu katika mwezi wa Oktoba mwaka 2020; NA KWA KUWA, kwa mujibu wa kifungu cha 37 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, mchakato wa uteuzi wa wagombea katika Uchaguzi Mkuu na kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu, hauwezi kufanyika isipokuwa kama Bunge limekwisha kuvunjwa; NA KWA KUWA, kwa mujibu wa masharti ya aya ya (a) ya Ibara ndogo ya (2) ya Ibara ya 90 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka, 1977, Sura ya 2, Rais anaweza kulivunja Bunge kama limemaliza muda wa uhai wake kwa mujibu wa Ibara ya 65 ya Katiba au wakati wowote katika miezi kumi na mbili ya mwisho ya uhai wa Bunge; HIVYO BASI, MIMI, JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka niliyokuwa nayo chini ya Ibara ya 90(2)(a), sasa nalivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu tarehe 31 Julai, 1 Hati ya Kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka, 2020 2020 ili kutoa fursa kufanyika kwa mchakato wa uteuzi wa wagombea katika Uchaguzi Mkuu na kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu. Kutolewa kwa Hati hii kunathibitishwa na Saini yangu na Muhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tarehe 12, Julai, 2020. L.S Dodoma, JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI 12th Julai, 2020 Rais 2