SHERIA NDOGO ZA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA ZA MWAKA 2020
Hii ni kichwa cha Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya Ruangwa za Mwaka 2020, kikifuatiwa na neno la kuanza sehemu ya tafsiri.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO ZA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA ZA MWAKA 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Hii ni kichwa cha Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya Ruangwa za Mwaka 2020, kikifuatiwa na neno la kuanza sehemu ya tafsiri. This section defines key terms used in these bylaws, including authorized officer, food, council, household, wastewater, resident, director, waste, solid waste, and agent. Wamiliki na wakazi wanatakiwa kusafisha maeneo yanayozunguka nyumba, viwanja au biashara zao, kuondoa uchafu kwenye mifereji ya maji, na kushiriki usafi wa mazingira kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi au siku nyingine itakayopangwa na Halmashauri. Property owners must keep their premises free of standing water, wastewater, rubbish, and other materials that could breed mosquitoes or other harmful insects. Mwenye biashara ya upuliziaji dawa za kuua wadudu au wanyama waharibifu katika eneo la Halmashauri lazima awe na cheti kinachotambuliwa na Serikali, awe na leseni hai ya Halmashauri, asimamie upuliziaji chini ya Afisa Afya, na atoe cheti kilichosainiwa na Afisa Afya baada ya kupuliza.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO ZA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA ZA MWAKA 2020
Showing 8 of 8
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Hii ni kichwa cha Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya Ruangwa za Mwaka 2020, kikifuatiwa na neno la kuanza sehemu ya tafsiri.
1. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya Ruangwa za Mwaka 2020. Tafsiri - 2 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi, isipokuwa pale muktadha utahitaji
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in these bylaws, including authorized officer, food, council, household, wastewater, resident, director, waste, solid waste, and agent.
2. Katika Sheria Ndogo hizi, isipokuwa pale muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote atakayeteuliwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa dawa, hii ni pamoja na: - (a) kitu chochote kinachotumika katika matengenezo ya chakula; (b) kitu chochote kinachoongeza ladha ya chakula; au (c) kitu chochote kinachobadili rangi ya chakula; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Sura 191 Ruangwa; “kaya” maana yake ni familia inayojumuisha baba, mama, mtoto au watoto na mtu mwingine yeyote anayeishi na familia hiyo au watu wanaokaa katika nyumba moja na kuishi kama familia au mtu yeyote anayeishi peke yake 1 Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) katika chumba au nyumba; “maji taka” maana yake ni ile iliyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote anayeishi katika eneo la Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri au anafanya biashara katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “taka” maana yake ni ile iliyoanishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” Maana yake ni ile iliyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni, taasisi au shirika aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira - 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Wamiliki na wakazi wanatakiwa kusafisha maeneo yanayozunguka nyumba, viwanja au biashara zao, kuondoa uchafu kwenye mifereji ya maji, na kushiriki usafi wa mazingira kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi au siku nyingine itakayopangwa na Halmashauri.
3.- (1) (2) (3) Kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba anafanya usafi wa mazingira yanayozunguka makazi au eneo lake hadi mwanzo wa mipaka ya barabara ya mbele ya eneo lake. Kila mmiliki wa nyumba, kiwanja au eneo la biashara atakuwa na wajibu wa kuondoa uchafu kama vile mchanga, majani, nyasi au vitu vingine vinavyofanana na hivyo kwenye mifereji ya kupitisha maji inayozunguka au kupita kando ya nyumba, kiwanja au eneo la biashara yake. Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1) na cha (2), kila mkazi atakuwa na wajibu wa kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira katika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi au katika siku itakayopangwa na Halmashauri. (4) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu hiki atakuwa ametenda kosa. Wajibu wa kuondoa na kudhibiti - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Property owners must keep their premises free of standing water, wastewater, rubbish, and other materials that could breed mosquitoes or other harmful insects.
4.- (1) Mmiliki wa nyumba, kiwanja au eneo la biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa katika eneo 2 Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) mazalia ya mbu. lake hakuna mkusanyiko wa maji, maji machafu, takataka au kitu chochote cha majimaji au kigumu ambacho kinaweza kuruhusu kuwepo kwa mazalia ya mbu au wadudu wengine wenye madhara kwa afya ya binadamu. (2) Mtu yeyote ambaye bila sababu za msingi, atakiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1), atakuwa ametenda kosa. Upulizaji dawa - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Mwenye biashara ya upuliziaji dawa za kuua wadudu au wanyama waharibifu katika eneo la Halmashauri lazima awe na cheti kinachotambuliwa na Serikali, awe na leseni hai ya Halmashauri, asimamie upuliziaji chini ya Afisa Afya, na atoe cheti kilichosainiwa na Afisa Afya baada ya kupuliza.
5.- (1) Mtu yeyote anayeendesha biashara ya upuliziaji dawa ya kuuwa wadudu au wanyama waharibifu katika eneo la Halmashauri atatakiwa:- (a) kuwa na cheti cha taaluma kinachotambuliwa na Serikali pamoja na leseni hai kutoka Halmashauri; (b) kusimamiwa na Afisa Afya wakati wa upulizaji; na (c) kutoa cheti baada ya kupuliza dawa kilichosainiwa na Afisa Afya. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Sehemu hii inapiga marufuku kutengeneza au kuegesha magari, pikipiki na mitambo katika maeneo yasiyoruhusiwa, na inaweka masharti ya matengenezo na uuzaji wa chakula ndani ya eneo la Halmashauri.
6.- (1) Matengenez o na maegesho ya magari, pikipiki na mitambo cha (1), atakuwa ametenda kosa. Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yatatakiwa kufanyika kwenye karakana, gereji au maeneo yaliyoruhusiwa baada ya kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri. (2) Mtu yeyote:- (a) hataruhusiwa kutengeneza gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo halikutengwa kwa shughuli hiyo; au (b) kuegesha gari bovu kwenye njia ya miguu, mtaa, uchochoro, mtaro, maeneo ya wazi au barabarani. (3) Mtu yeyote atakayekiuka, bila sababu za msingi, masharti ya kifungu kidogo cha (2), atakuwa ametenda kosa. . Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, Utengenezaj 7. 3 Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) i na uuzaji vyakula. Machinjio na maduka ya nyama kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa: (a) kutimiza masharti na kanuni za afya; na (b) kuwa na kibali kutoka kwa Afisa Afya wa Halmashauri. - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Section 8 bans several meat-related acts, requires meat-shop owners and some food-business owners to meet health and inspection rules, and sets offences and penalties for breaches.
8.- (1) Mtu yeyote hatoruhusiwa:- (a) kuchinja mifugo kwa madhumuni ya yasiyokuwa katika maeneo kibiashara machinjio; (b) kuuza nyama ya aina yoyote katika maeneo yasiyokuwa maduka ya nyama au katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri; (c) kuuza nyama isiyokaguliwa na mtaalamu wa mifugo au mtaalamu wa afya; na (d) kusafirisha nyama kwa madhumuni ya kibiashara toka machinjioni bila kutumia gari maalumu nyama la lililoidhinishwa na Halmashauri. kusafirishia (2) Kila mmiliki wa duka la kuuzia nyama atatakiwa kuhakikisha yafuatayo: (a) duka lake ni jengo la kudumu lililosakafiwa kwa marumaru nyeupe hadi urefu wa futi sita kutoka usawa wa sakafu; (b) duka lake lina maji safi, misumeno ya kukatia nyama na vyuma vya kutundikia nyama; (c) duka lake lina kabati la vioo na jokofu la kuhifadhia nyama na mizani ya kupimia nyama; (d) duka lake lina pipa au kifaa cha kuhifadhia takataka; (e) muuzaji ana vazi jeupe pamoja na aproni nyeupe na kofia nyeupe; (f) muuzaji anapima afya kila baada ya miezi sita; na (g) duka lake lina karo la maji machafu. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) na (2) atakuwa ametenda kosa. Uendeshaji wa biashara 9. (1) Kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni, hosteli, 4 Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) ya hoteli na hosteli shule, kituo cha kutolea huduma za afya au nyumba ya biashara kabla ya kuanza biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha: (a) jengo lake limekaguliwa na Afisa Afya; na (b) amepata kibali cha Halmashauri cha kufanya shughuli husika. (2) Kibali cha kuendesha biashara ya nyumba ya kulala wageni, hosteli, shule, kituo cha kutolea huduma za afya au nyumba ya biashara kitatolewa baada ya Halmashauri yafuatayo yamezingatiwa:- kujiridhisha kuwa (a) kuwepo kwa hewa ya kutosha katika jengo; (b) kuwepo kwa nafasi na vifaa vya kutosha; (c) uimara wa jengo; (d) kuwepo kwa mfumo imara wa uondoshaji wa maji taka, miminika na taka ngumu katika jengo; (e) usafi wa jumla wa jengo na vifaa vyake; (f) uwepo wa vyoo na mabafu ya kutosha kwa jinsia zote; (g) kuwepo na vifaa vya kuzimia moto; (h) kuwepo na tanki la kuhifadhia maji safi; (i) vyoo na bafu vimesakafiwa kwa vigae au marumaru na kuta zake zimewekwa vigae kiasi cha futi sita toka usawa wa sakafu; na (j) kwa nyumba za kulala wageni na hosteli, uwepo wa vyandarua. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu cha (1) (4) atakuwa ametenda kosa. Bila kuathiri masharti ya kifungu cha (3), wakati ikijiridhisha kuwa mmiliki wowote Halmashauri hajakidhi masharti ya afya inaweza kuzuia utoaji wa huduma husika mpaka hapo mmiliki atakapokuwa amekidhi masharti ya kiafya yaliyotolewa na Halmashauri. Upimaji wa afya (1) 10 .- Kila mmiliki wa hoteli, mgahawa, baa, bucha, sehemu za kuokea mikate, nyumba ya kulala wageni na grosari au mtu yeyote anayetengeneza chakula kwa ajili ya kuuza atatakiwa kuhakikisha mhudumu wake 5 Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) amepima afya kila baada ya miezi sita. (2) Mmiliki yeyote atakayebainika kuruhusu mhudumu kufanya kazi bila kupimwa afya yake atatakiwa kulipa kiasi cha shilingi elfu hamsini na kuhakikisha mhudumu huyo anapimwa afya. (3) Ada ya upimaji wa afya itakuwa shilingi elfu sita. Eneo la kutupa taka 11 . (1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa:- (a) kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupia taka; (b) kuweka vyombo maalum vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. (2) Mtu yeyote atakayetupa taka au uchafu wowote au takataka au uchafu kwenye nyumba, kuacha uchochoro, kiwanja, mfereji wa maji ya mvua, barabara au mahali popote pasipotengwa kwa shughuli hiyo atakuwa ametenda kosa. Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi Jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika mitaa baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Vikundi vya wazoa taka 12 . (1) 13 . Magari ya abiria kuwa na vyombo vya kuhifadhia takataka Kila mmiliki wa gari la abiria litakaloingia katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhi taka na kuhakikisha kwamba kila abiria anatupa taka kwenye chombo hicho. (2) Endapo abiria atatupa takataka nje ya chombo cha usafiri, mmiliki au dereva au kondakta atawajibika 6 Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) kulipa kiasi cha shilingi elfu hamsini chini ya utaratibu wa kufifilisha kosa au kushtakiwa mahakamani. Uhifadhi maji taka (1) 14 .- Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara anatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa analo karo la kuhifadhi Ada ya utozaji taka 15 . maji taka; (b) kunyonya maji taka pale karo linapojaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote isiyotengwa kuhifadhia maji taka. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. Halmashauri itatoza ada ya uzoaji taka kila mwezi kutoka kwa kila kaya, wamilliki wa nyumba za biashara, taasisi na kampuni zilizopo ndani ya eneo la Halmashauri kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi. Ada ya kila mwezi italipwa kila tarehe 30 ya kila mwezi ndani ya mwezi husika na italipwa kwa Afisa Mwidhiniwa ambaye atatoa stakabadhi ya malipo yatakayolipwa na atajaza katika rejista ya wazalishaji taka. taka atashindwa kulipia Endapo mzalishaji wa gharama ya huduma ya uzoaji taka kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo, Halmashauri itamtaka kulipa deni hilo na adhabu ya asilimia hamsini ya ada anayostahili kulipa. Endapo mzalishaji taka atashindwa kulipa gharama ya huduma kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) itachukuliwa kuwa ametenda kosa chini ya Sheria Ndogo hizi. 7 (2) (1) (2) (3) (4) Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) Wajibu wa kuwa na choo na kukitumia Vyoo vya umma 16 . 17 . Kila mmiliki wa jengo la makazi au la biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba jengo lake lina choo safi, imara na madhubuti na kuhakikisha kuwa kinatumika wakati wote. Halmashauri inaweza kujenga vyoo vya umma au kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu au taasisi kujenga vyoo vya umma vitakavyotoa huduma kwa malipo katika maeneo ambayo Halmashauri itaona kuwa kuna haja ya kufanya hivyo. Vyoo vya muda katika mkusanyiko 18 . (1) (2) (1) Ilani ya kujenga choo 19 . Mtu, kikundi au taasisi yenye lengo la kukutanisha watu kwa muda maalum katika eneo ambalo halina choo cha kudumu itatakiwa kujenga vyoo kwa matumizi ya wakati huo kwa idhini na usimamizi wa Halmashauri. Mtu, kikundi au taasisi itakayokiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa imetenda kosa. Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika kuwa nyumba yoyote haina choo, choo kilichopo kimejaa au hakifai binadamu, Afisa Mwidhiniwa atatoa ilani ya siku thelathini kwa mmiliki wa nyumba akiainisha masharti ya kurekebisha hali hiyo. kwa matumizi ya (2) Mmiliki wa nyumba atakayeshindwa kutekeleza masharti ya Ilani iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. (3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Halmashauri inaweza kuamuru nyumba au jengo hilo lisitumike kwa shughuli za makazi au biashara hadi hapo hali hiyo itakapokuwa imerekebishwa. Ilani ya kuondoa kero (1) 20 . Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote atatoa ilani ya siku saba kwa mmiliki wa nyumba, mpangaji, mtumiaji au mtu 8 Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) yeyote anayehusika akimtaka kuondoa kero hiyo. (2) Mtu yeyote atakayeshindwa kutekeleza masharti ya ilani aliyopewa ndani ya muda ulioainishwa kwenye ilani atakuwa ametenda kosa. Halmashauri inaweza kuteua kampuni au kikundi cha jamii kutekeleza majukumu yake isipokuwa majukumu mahsusi ya Mkurugenzi, Afisa Mwidhiniwa na Afisa Afya chini ya Sheria Ndogo hizi. Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hizi atahukumiwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hizi kiasi cha shilingi laki mbili iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiyari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. Uteuzi wa Wakala Adhabu Kufifilisha kosa 21 . 22 . 23 . 9 Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) JEDWALI LA KWANZA (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 15(1)) ADA YA UZOAJI TAKA Aina ya biashara Ada ya mwezi Nyumba za kuishi au makazi kwa kaya Nyumba za kulala wageni Maduka Mgahawa, baba au mama lishe Hoteli, baa na grosari Vibanda au meza za biashara Wachoma chips, kuku na nyama Saluni Gereji Fundi seremala, samani Wauza mbao au karakana za kuranda mbao Ofisi na Taasisi mbalimbali Mashine za kusaga na kukoboa Sh. 2500/= Sh. 5000/= Sh. 3000/= Sh. 2000/= Sh. 5000/= Sh. 2000/= Sh. 3000/= Sh. 3000/= Sh. 5000/= Sh. 5000/= Sh. 5000/= 3000/= 3000/= Na. 1 2 3
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: Hii fomu inaeleza kukiri kosa kwa hiari na kulipa shilingi laki mbili ili kumaliza kosa badala ya kufikishwa mahakamani.
10. 11 12 10 Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 23) JEDWALI LA PILI KUFIFILISHA KOSA Mimi……………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, kuwa Tarehe ………Mwezi………. Mwaka………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha………………. cha Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa za Mwaka 2020. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri, niko tayari kulipa kiasi cha shilingi laki mbili na kutekeleza wajibu wangu badala ya kushitakiwa mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI KWELI NA NINAYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe………………………………. ya Mwezi…………………. Mwaka………………… Jina…………………………………………Saini……………………………… ……… Mbele ya: Jina………………………………………...Cheo……………………………… ……. Saini………………………………………Tarehe……………………………… …… 11 Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Tangazo la Serikali Na.598 (Linaendelea.) Nembo ya Halmashauri imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio la Mkutano wa Halmashauri uliopitishwa na kufanyika tarehe 15/8/2019 na umeandikwa mbele ya:- ANDREA G. CHEZUE Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Ruangwa RASHID NAKUMBYA, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya,Ruangwa. NAKUBALI, L.S Dodoma, 01 Julai, 2020 SELEMANI S. JAFO (MB.), WN OR-TAMISEMI Dodoma 12
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO ZA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA ZA MWAKA 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in