Tanzania Act or statute

Parliament of Tanzania

SHERIA YA HUDUMA NDOGO YA FEDHA

This section gives the Act’s short title: the Microfinance Services Act, 2018. Kifungu hiki kinafafanua maneno muhimu yanayotumika katika Sheria hii, ikiwemo “Benki,” “taasisi,” “watoa huduma ndogo za fedha,” na istilahi…

accountingaccounting recordsadministrative sanctionsappeal procedureappealsapplication processapplication processingapplication refusalapplication reviewBanking and financebranch operationsbusiness administrationbusiness premisesBusiness registrationcapitalcapital requirementscollateral enforcementcomplaints handlingcompliancecompliance noticeconsumer protectioncontract termscorporate statuscredit reportingcustomer identificationcustomer information secrecydebt collectiondefinitionsdisclosure exceptionsdistributionsdividendsdocumentation requirementsEmployment lawenforcementfedha ndogofinancial institution supervisionfinancial literacyfinancial reportingBanking and financefinancial statementsinformation requestsinformation sharinginstitutional migrationinterestinterest ratesinternal auditinternal controlsinternal financial managementlicense applicationlicense cancellationlicense issuancelicense refusallicense revocationlicense validitylicensed service restrictionsBusiness registrationlicensing/applicationlicensing/exemptionsliquidity requirementslocal participation compliancemanagement takeovermicrofinancemicrofinance classificationmicrofinance institution operationsmicrofinance institutionsmicrofinance providersmicrofinance regulationmicrofinance service providersmicrofinance servicesmicrofinance supervisionnotificationpenaltiespolicy oversightpreparation of accountspublic administrationpublic disclosurepublic noticereapplicationrecord disclosurerecord keepingrecordkeepingregister maintenanceregistersregistrationregistration cancellationregistration certificateregistration processregistryregulatory complianceregulatory delegationregulatory inspectionregulatory powersregulatory reportingreportingsmall finance servicessupervisionsupervision and regulationsuspicious transaction reportingtransitional compliancetransitional provisionsuendelevu wa mtoa hudumauwezeshaji

Publicly available, excluded from search-engine indexing

This page remains available for direct research for the following reasons:

  • The record does not meet this release's canonical indexing criteria. (market-indexing-disabled)
  • The record does not meet this release's canonical indexing criteria. (emergency-noindex)

Professional statute overview

Enactment structure, operative effect and source provenance

Official source

01

Purpose and legislative effect

“This section gives the Act’s short title: the Microfinance Services Act, 2018.”

This section gives the Act’s short title: the Microfinance Services Act, 2018. Kifungu hiki kinafafanua maneno muhimu yanayotumika katika Sheria hii, ikiwemo “Benki,” “taasisi,” “watoa huduma ndogo za fedha,” na istilahi nyingine za huduma ndogo za fedha. Huduma ndogo za fedha zinaweza kufanywa tu na taasisi zinazotambuliwa na kuanzishwa ipasavyo chini ya sheria husika na Sheria hii, na lazima zifuatwe kwa masharti ya Sheria hii. Sheria hii inaweka madaraja manne ya watoa huduma ndogo za fedha, na taasisi zinazopokea amana chini ya Daraja la 1 zitasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabenki na Taasisi za fedha. A microfinance service provider must have business premises with a correct address, and may not open or close premises without approval from the Bank or the delegated authority.

02

How the instrument operates

  1. 01

    Start with the recorded version

    Legal dates not recorded. The date shown identifies this source expression and should not be treated as proof that no later change exists.

  2. 02

    Locate the controlling provision

    Use the provision map, part headings and full-text filter to move from the broad subject to the exact legal language.

  3. 03

    Read conditions and exceptions together

    Keep subsections, definitions, provisos and cross-references in context before drawing a legal conclusion.

  4. 04

    Verify currency and official wording

    Confirm later legislation, commencement notices and corrections with the official publisher before advice, filing or reliance.

03

Research entry points

Selected provisions across the instrument. Open any row to continue with the exact stored text.

2

This section gives the Act’s short title: the Microfinance Services Act, 2018.

Section 1

Maombi ya leseni kwa Daraja la 2

Mtu anayetaka kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha Daraja la 2 lazima aombe leseni kutoka Benki na aweke maombi yake pamoja na taarifa na nyaraka zinazohitajika.

Section 17

33

The Bank or Commissioner may cancel a registration certificate if the stated conditions are met, and if it is cancelled they must notify the provider in writing, direct the provider to stop operations, and remove the provider’s name from the register.

Section 32

48

Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kukagua mtoa huduma ndogo za fedha, na mtoa huduma lazima aonyeshe vitabu, kumbukumbu na nyaraka na atoee taarifa zinazoombwa. Pia, mtu yeyote anayekwamisha ukaguzi au kukataa kuonyesha vitu vinavyohitajika anatenda kosa.

Section 47

04

Source and current-law status

Source record view

Source record from oagmis.oag.go.tz · Legal dates not recorded

Verify current force

The source record does not state a definitive current-law status. Check the official publisher and later amendments before relying on this text.

Source-indexed provision map

Sections and provisions

Search by section, heading, part or exact legal wording. Every result remains linked to the stored source record.

Showing 61 of 61 provisions

Provision 56Offence 4Short title
§ 12Short title

This section gives the Act’s short title: the Microfinance Services Act, 2018.

1. Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018. Matumizi Tafsiri Sura 342
§ 3Jina la SheriaProvision

Kifungu hiki kinafafanua maneno muhimu yanayotumika katika Sheria hii, ikiwemo “Benki,” “taasisi,” “watoa huduma ndogo za fedha,” na istilahi nyingine za huduma ndogo za fedha.

3.-Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Benki” maana yake ni Benki Kuu ya Tanzania; “benki” maana yake ni kama ilivyo kwenye Sheria ya Usimamizi wa Mabenki na Taasisi za Fedha; “vikundi vya kifedha vya kijamii” maana yake ni kikundi kilichoundwa kwa pamoja na kusimamiwa na wanachama wenyewe na kusajiliwa chini ya Sheria hii kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha ikijumuisha ukusanyaji wa amana kutoka kwa wanachama wake na utoaji mikopo kwa wanachama wake lakini haijumuishi: 6 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha (a) vikundi vya kijamii vya kusaidiana vilivyoundwa kwa madhumuni ya kinga na ustawi wa jamii na kiuchumi wa wanachama wake ambavyo havipokei amana na havitoi mikopo kwa wanachama wake kwa kufanya shughuli za biashara ya huduma ndogo za fedha; (b) vikundi vya watu wenye maslahi maalum, vilabu na vyama vinavyokusanya michango ya fedha kutoka kwa wanachama wake au vinavyopokea misaada ya hisani vilivyoundwa na kusajiliwa chini ya Sheria ya Vyama vya Hiari kwa madhumuni ya kuimarisha hali za kiuchumi kwa wanachama wake lakini havifanyi biashara ya huduma ndogo za fedha; na (c) vikundi vya muda mfupi vinavyoundwa kwa madhumuni ya kupokea michango au upokeaji wa fedha kwa shughuli za kidini au matukio ya kijamii ikijumuisha ndoa au shughuli za familia za kimila zinazofanywa na watu au vikundi; “kampuni inayotoa mikopo” maana yake ni kampuni iliyosajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni na yenye leseni ya kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha; “Chombo cha ubadilishanaji wa taarifa za mikopo” maana yake ni taasisi maalumu kwa ajili ya kukusanya na kuuza taarifa za wakopaji binafsi na makampuni; “Tume ” maana yake ni Tume ya Maendeleo ya Ushirika Sura ya 212 Sura. 211 Tanzania iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Ushirika; “Mlaji”maana yake ni mteja au mwanachama wa taasisi inayotoa huduma ndogo za fedha ambaye anajipatia au ana lengo la kujipatia huduma zitolewazo na taasisi ya huduma ndogo za fedha; “Mamlaka Kasimishwa” maana yake ni taasisi ya umma iliyokasimishwa mamlaka na Benki Kuu ya Tanzania kutekeleza majukumu na mamlaka ya Benki Kuu chini ya sheria hii; “taasisi” maana yake ni shirika, ubia, udhamini, chama, wanahisa, ushirikiano wa pamoja wa mitaji, ushirika, umiliki binafsi, kikundi au aina nyingine yoyote ya taasisi ambayo haijaorodheshwa katika tafsiri hii lakini inatambulika kama taasisi ikiwa ni pamoja na 7 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha Serikali au wakala wa Serikali au taasisi za Serikali; “mtoa huduma ndogo za fedha wa kigeni” maana yake ni mtoa huduma ndogo za fedha aliyesajiliwa Tanzania ambaye wamiliki wake wengi au wanahisa wake wengi ni wageni; “taasisi ya fedha” maana yake ni taasisi iliyosajiliwa chini ya sheria husika ambayo ina leseni ya kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha kwa mujibu wa Sheria hii; “biashara ya huduma ndogo za fedha” maana yake ni biashara ya huduma ndogo za fedha inayohusisha kupokea na kutokupokea amana na inajumuisha shughuli ambazo zimeainishwa katika kifungu cha 4; “mkopo mdogo wa karadha” maana yake ni mkopo unaotolewa kwa njia ya vifaa ambavyo wastani wa thamani yake hauzidi shillingi milioni kumi na muda wa kurejesha mkopo usiozidi miezi 24; “mkopo mdogo” maana yake ni mkopo unaotolewa kwa kama biashara ndogo, kaya na watu binafsi itavyoainishwa katika kanuni; Sura. 394 “huduma ndogo za bima" ina maana iliyotolewa katika Sheria ya Bima; “watoa huduma ndogo za fedha” maana yake ni taasisi au mtu ambaye amesajiliwa au amepewa leseni ya kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha chini ya Sheria hii ikijumuisha watoa huduma ndogo za fedha wanaochukua na wasiochukua amana kama walivyoainishwa chini ya kifungu cha 5 cha Sheria hii; “Waziri” maana yake Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha; Sura. 423 “utakasishaji fedha haramu” ina maana iliyotolewa katika Sheria ya Utakasishaji wa Fedha Haramu; “sehemu ya biashara” maana yake ni tawi, ofisi, wakala au ofisi inayohamishika ya mtoa huduma ndogo za fedha inayotoa huduma kwa umma; 8 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha “Rejesta” maana yake ni rejesta ya watoa huduma ndogo za fedha ilivyorejewa katika kifungu cha 54 cha Sheria hii; Sura. 211 “SACCOS” maana iliyotafsiriwa katika Sheria ya Vyama vya Ushirika. Biashara ya huduma ndogo za fedha SEHEMU YA PILI WATOA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

Part

SEHEMU YA PILI

§ 45Provision

Huduma ndogo za fedha zinaweza kufanywa tu na taasisi zinazotambuliwa na kuanzishwa ipasavyo chini ya sheria husika na Sheria hii, na lazima zifuatwe kwa masharti ya Sheria hii.

4.-(1) Biashara ya huduma ndogo za fedha itafanywa na taasisi za huduma ndogo za fedha ambazo: (a) zimeanzishwa kwa mujibu wa Sheria zao husika na zinazotambulika chini ya Sheria hii; na (b) zimeanzishwa na kutambuliwa chini ya Sheria hii. (2) Taasisi za huduma ndogo za fedha chini ya kifungu kidogo cha (1) zitafanya biashara ya huduma ndogo ya fedha kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii. (3) Bila ya kuathiri ujumla wa kifungu kidogo cha (2), biashara ya huduma ndogo za fedha zitakazofanywa chini ya Sheria hii zitajumuisha- (a) kupokea fedha, kwa njia ya amana au riba inayotokana na amana au mikopo na ambayo inakopeshwa kwa wanachama au wateja; (b) kupokea akiba na kutoa mikopo au huduma nyingine za kukopesha kwa wajasiriamali wadogo na kaya za kipato cha chini au watu binafsi; (c) kutoa mikopo midogo, akiba, bima ndogo, mikopo midogo ya karadha, pensheni ndogo na mikopo midogo ya nyumba; (d) huduma za kuhawilisha na malipo ya fedha ikijumuisha huduma ndogo za fedha kwa njia ya mtandao; (e) ufanyaji wa biashara ya huduma ndogo za fedha za bidhaa ikijumuisha utoaji wa mikopo ya bidhaa; (f) kutoa huduma ya elimu ya fedha; na 9 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha (g) huduma nyingine zinazofanana na hizo kama zitakavyoainishwa katika kanuni. Aina za watoa huduma ndogo za fedha
§ 56Provision

Sheria hii inaweka madaraja manne ya watoa huduma ndogo za fedha, na taasisi zinazopokea amana chini ya Daraja la 1 zitasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabenki na Taasisi za fedha.

5.-(1) Kwa madhumuni ya Sheria hii, kutakuwa na madaraja manne ya watoa huduma ndogo za fedha kama ifuatavyo:- (a) Daraja la 1, litajumuisha taasisi za huduma ndogo za fedha zinazochukua amana; (b) Daraja la 2 litajumuisha taasisi za huduma ndogo za fedha zisizochukua amana kama vile kampuni na wakopeshaji binafsi wanaotoa mikopo ya fedha; (c) Daraja la 3, litajumuisha Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOs); na (d) Daraja la 4, litajumuisha vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha; (2) Taasisi za huduma ndogo za fedha zinazopokea amana chini ya kifungu cha (1)(a) zitasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabenki na Taasisi za fedha.
§ 67Provision

A microfinance service provider must have business premises with a correct address, and may not open or close premises without approval from the Bank or the delegated authority.

6.-(1) Kila mtoa huduma ndogo za fedha atapaswa kuwa na sehemu ya biashara au sehemu za biashara zenye anwani sahihi kwa ajili ya kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha. (2) Kwa kuzingatia kifungu hiki, mtoa huduma ndogo za fedha hataruhusiwa kufungua au kufunga sehemu ya biashara bila kupata idhini ya Benki au Mamlaka Kasimishwa. (3) Mtoa huduma ndogo za fedha ambaye atashindwa kuzingatia masharti ya kifungu hiki, atakuwa anatenda kosa. Sura 342 Sehemu ya biashara Uendeshaji wa taasisi za huduma ndogo za fedha

Part

Sehemu ya

§ 78Provision

Microfinance institutions must follow operating instructions issued by the Bank or appointed authority when their operating rules conflict with microfinance business.

7.-(1) Taratibu za uendeshaji wa taasisi za huduma ndogo za fedha zitakuwa kama itakavyoainishwa katika sheria zao anzilishi au katiba zinazoanzisha taasisi husika. (2) Bila ya kujali kifungu kidogo cha (1), Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza, iwapo itajiridhisha kuwa utaratibu wa uendeshaji wa taasisi ya huduma ndogo za fedha unakinzana na biashara ya huduma ndogo za fedha, 10 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha itatoa maelekezo ya jumla au mahsusi kwa taasisi ya huduma ndogo ya fedha kuhusu uendeshaji wake na maelekezo hayo yatapaswa kutekelezwa. Uwajibikaji wa watoa huduma ndogo za fedha
§ 89Provision

Mtoa huduma ndogo za fedha lazima awajibike kwa benki au mamlaka nyingine husika anapofanya biashara ya huduma ndogo za fedha.

8. Mtoa huduma ndogo za fedha atapaswa, kwa dhumuni la kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha, kuwajibika kwa Benki Mamlaka Kasimishwa au mamlaka nyingine yoyote kwa mujibu wa sheria zinazotumika. Kiwango cha chini cha mtaji
§ 910Provision

Mtoa huduma ndogo za fedha chini ya Sheria hii lazima atimize kiwango cha chini cha mtaji kitakachoainishwa katika kanuni.

9. Mtoa huduma ndogo za fedha anayefanya biashara ya huduma ndogo za fedha chini ya Sheria hii, atapaswa kutekeleza matakwa ya kuwa na kiwango cha chini cha mtaji kama itakavyoainishwa katika kanuni. Kiwango cha chini cha mali zinazobadilis hi-ka kirahisi kuwa fedha taslim
§ 1011Provision

Mtoa huduma ndogo za fedha lazima awe na kiwango cha chini cha mali zinazoweza kubadilishwa haraka kuwa fedha taslimu, kwa kiwango kitakachoainishwa katika kanuni.

10.-(1) Mtoa huduma ndogo za fedha atapaswa kuwa na kiwango cha chini cha mali zinazobadilishika kirahisi kuwa fedha taslim kama itakavyoainishwa katika kanuni. (2) Kwa dhumuni “mali zinazobadilishika kirahisi kuwa fedha taslim” maana yake ni- la kifungu hiki, (a) noti na sarafu ambazo ni fedha halali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; (b) bakaa zilizopo katika benki au taasisi za huduma ndogo ya fedha; (c) dhamana na hatifungani za Serikali ambazo ni rahisi kuuzika kupitia Benki; au (d) mali nyingine kama Benki au Mamlaka Kasimishwa itakavyobainisha. Kuhama madaraja kwa watoa huduma ndogo za fedha
Section 10Verify source
§ 11Biashara ya huduma ndogo za fedhaProvision

A microfinance institution may move to another class if it applies and meets the criteria in the regulations, and the Bank may assess, approve, set conditions, and enforce the move.

11.-(1) Taasisi yoyote ya huduma ndogo za fedha inaweza, kwa kutuma maombi na kukidhi vigezo vilivyoainishwa katika kanuni, kuhama kutoka Daraja moja la watoa huduma ndogo za fedha kwenda Daraja jingine. (2) Endapo taasisi ya huduma ndogo za fedha inahama kwenda daraja jingine, taasisi hiyo itapaswa kusimamiwa kwa mujibu wa sheria zinazohusika na daraja husika pamoja na Sheria hii. 11 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha (3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, vigezo vya kuhama daraja kwa taasisi ya huduma ndogo za fedha vitajumuisha- (a) kiwango cha chini cha mtaji kinachokidhi kuhamia daraja husika; (b) idadi ya wanachama na wateja inayokidhi kuhamia daraja husika; (c) aina ya shughuli ya huduma ndogo za fedha inayofanywa; na (d) vigezo vingine vitakavyoainishwa katika kanuni. vyovyote kama (4) Bila ya kujali masharti ya kifungu hiki, Benki inaweza, kabla ya kutoa idhini ya kuruhusu taasisi ya huduma ndogo za fedha kuhama kwenda daraja jingine, kufanya tathmini ili kujiridhisha uendelevu wa huduma za taasisi hiyo baada ya kuhamia daraja jingine. (5) Endapo baada ya kufanya tathmini, Benki itajiridhisha kwamba taasisi ya huduma ndogo za fedha inakidhi vigezo vya kuhama, inaweza kutoa maelekezo ya kuiruhusu taasisi hiyo kuhama kwa kuzingatia vigezo na masharti yatakayotolewa na Benki. (6) Endapo taasisi ya huduma ndogo za fedha, bila sababu za msingi, itashindwa kutekeleza maelekezo yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (5), Benki itachukua hatua stahiki ili kuhakikisha maelekezo yake yanatekelezwa. SEHEMU YA TATU MASHARTI YANAYOHUSU MASUALA YA UTAWALA Majukumu ya Benki
Section 11Verify source

Part

SEHEMU YA TATU

§ 12Majukumu ya BenkiProvision

Benki lazima isimamie na kufuatilia taasisi na biashara za huduma ndogo za fedha, na itimize majukumu mengine ya udhibiti na usimamizi yaliyoorodheshwa.

12.-(1) Benki itakuwa na jukumu la kusimamia na kufuatilia taasisi za watoa huduma ndogo za fedha zinazofanya biashara ya huduma ndogo za fedha kwa mujibu wa Sheria hii. (1), (2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha majukumu ya Benki yatakuwa ni kudhibiti na kusimamia uendeshaji wa biashara ya huduma ndogo za fedha kwa mujibu wa Sheria hii na sheria nyingine husika. 12 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha (3) Bila ya kuathiri masharti ya jumla ya vifungu vidogo vya (1) na (2), Benki itakuwa na majukumu yafuatayo- (a) kutoa leseni kwa watoa huduma ndogo za fedha waliokidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria hii; (b) kushauri na kutoa taarifa kwa Waziri kuhusu masuala ya biashara ya huduma ndogo za fedha; (c) kuanzisha na kusimamia kanzidata ya watoa huduma ndogo za fedha; (d) kukagua, kufuatilia na kutathmini utendaji wa biashara ya huduma ndogo za fedha; (e) kutoa nyaraka na miongozo kwa watoa huduma ndogo za fedha; (f) kutathmini na kutoa idhini kwa watoa huduma ndogo za fedha kuhama daraja moja kwenda jingine; (g) kuhakikisha malalamiko yanayohusu biashara ya fedha yanashughulikiwa huduma ndogo za ipasavyo; (h) kuhakikisha ulinzi kwa watumiaji wa huduma ndogo za fedha ikijumuisha kutoa adhabu kwa ukopeshaji usiofuata misingi na taratibu sahihi za ukopeshaji; (i) kuhakikisha kuwa taarifa za mikopo ya biashara ya huduma ndogo za fedha zinakusanywa, kusambazwa na kupatikana kwa urahisi; na majukumu kama itakavyotakiwa kwa ajili ya kudhibiti na kusimamia biashara ya huduma ndogo za fedha. (j) kutekeleza mengine Mamlaka ya Benki
Section 12Verify source
§ 13Mamlaka ya BenkiProvision

Benki ina mamlaka ya kusimamia, kukagua, na kuchunguza shughuli na nyaraka za watoa huduma ndogo za fedha.

13. Katika kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria hii, Benki itakuwa na mamlaka ya- (a) kuchunguza au kuhoji uendeshaji wa shughuli za watoa huduma ndogo za fedha; (b) kukagua na kuchunguza vitabu vya hesabu, kumbukumbu, taarifa na nyaraka nyingine yoyote ya watoa huduma ndogo za fedha; (c) kutaka na kupewa taarifa zinazohusu shughuli za watoa huduma ndogo za fedha; 13 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha (d) kuelekeza usimamizi bora wa shughuli za watoa huduma ndogo za fedha; (e) kuingia, kwa muda wowote muafaka, kwenye eneo lolote la biashara la mtoa huduma ndogo za fedha au eneo lolote ambalo inaaminika, kwa sababu za msingi, kwamba vitabu vya hesabu, kumbukumbu au nyaraka za biashara ya mtoa huduma ndogo za fedha katika namna yoyote zinatunzwa; (f) kufungua au kuagiza kufunguliwa kwa chumba au kasha la kuhifadhia fedha au kifaa kingine ambapo kunashukiwa, kwa sababu za msingi, kwamba kuna amana, vitabu vya hesabu, kumbukumbu au nyaraka za mtoa huduma ndogo za fedha; (g) kumuagiza afisa yeyote, mwajiriwa au wakala yeyote wa mtoa huduma ndogo za fedha kutoa au kuwasilisha maelezo au nyaraka zinazohusu usimamizi au shughuli za mtoa huduma ndogo za fedha; na (h) kutekeleza kama itakavyokuwa lazima kwa utekelezaji bora wa majukumu yake chini ya Sheria hii. mamlaka mengine Kukasimisha mamlaka na majukumu ya Benki
Section 13Verify source
§ 1415Provision

Benki may delegate some of its duties and powers by Government Gazette notice, but not its duties and powers about supervision and regulation of Daraja la 2 institutions unless the Minister approves otherwise.

14.-(1) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu na mamlaka yake ya udhibiti na usimamizi chini ya Sheria hii na kwa kuzingatia masharti na taratibu mahsusi ambazo zitawekwa na Benki, Benki inaweza, kwa notisi itakayotangazwa kwenye Gazeti la Serikali, kukasimisha majukumu au mamlaka yake yoyote kama ifuatavyo: (a) kwa majukumu na mamlaka ya watoa huduma ndogo za fedha waliopo katika Daraja la 3, kwa Tume; na (b) kwa majukumu na mamlaka ya watoa huduma ndogo za fedha waliopo katika Daraja la 4, kwa mamlaka za serikali za mitaa. (2) Mamlaka Kasimiwa chini ya kifungu kidogo cha (1), zinapaswa kutekeleza majukumu na mamlaka yake kwa mujibu wa masharti, taratibu na maelekezo mengine yoyote yatakayotolewa na Benki mara kwa mara. 14 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha Sura ya 287 na 288 Jukumu la Waziri (3) Mamlaka au jukumu lolote lililokasimishwa chini ya kifungu hiki, litakapotekelezwa na Mamlaka Kasimiwa litachukuliwa kama limetekelezwa na Benki. (4) Ukasimishaji wa mamlaka chini ya kifungu hiki hautazuia Benki kutekeleza mamlaka na majukumu yake yaliyokasimishwa. (5) Bila ya kuathiri kifungu kidogo cha (1), isipokuwa pale Waziri atakapoidhinisha vinginevyo, Benki haitakuwa na mamlaka ya kukasimisha majukumu na mamlaka yake yanayohusu udhibiti na usimamizi wa taasisi za watoa huduma ndogo za fedha katika Daraja la 2. (6) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, tafsiri ya neno “mamlaka za serikali za mtaa” ina maana iliyotolewa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji).
Section 14Verify source
§ 15Kukasimisha mamlaka na majukumu ya BenkiProvision

Waziri ana jukumu la kutunga sera na kusimamia utekelezaji wa sera ya biashara ya huduma ndogo za fedha, na anaweza kuomba taarifa au nyaraka na kutunga kanuni kwa ajili ya utekelezaji bora.

15.-(1) Waziri atakuwa, kwa madhumuni ya kuhakikisha uwepo wa mazingira wezeshi ya kisera kwa biashara ya huduma ndogo za fedha, na jukumu la kutunga sera na kusimamia utekelezaji wake. (2) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1), Waziri atatekeleza yafuatayo- (a) kuweka mazingira wezeshi ya kusaidia ustawi wa biashara ya huduma ndogo za fedha; (b) kuhakikisha biashara ya huduma ndogo za fedha inakuwa endelevu; (c) kutoa maelekezo kwa Benki katika utekelezaji wa sera ya biashara ya huduma ndogo za fedha; (d) kuhakikisha uwepo wa uendelezaji, uwazi na uwajibikaji katika biashara ya huduma ndogo za fedha; na (e) kutekeleza jukumu jingine lolote kwa utekelezaji bora wa Sheria hii. (3) Katika kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria hii, Waziri anaweza, baada ya kushauriana na Mawaziri husika, kuhitaji au kutaka kupatiwa taarifa au nyaraka zinazohusu biashara ya huduma ndogo za fedha kutoka Wizara, taasisi au ofisi yoyote na Wizara, taasisi au ofisi hiyo itapaswa kutekeleza. (4) Waziri anaweza, kwa kushauriana na Waziri 15 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha mwenye dhamana na ushirika au kadri itakavyokuwa, Waziri mwenye dhamana na mamlaka za serikali za mitaa, kutengeneza kanuni kwa ajili ya utekelezaji bora wa majukumu yake chini ya Sheria hii. SEHEMU YA NNE UTOAJI LESENI KWA WATOA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA WA DARAJA LA 2 NA 3 Katazo la kutoa huduma ndogo za fedha bila leseni
Section 15Verify source

Part

SEHEMU YA NNE

§ 1617. Maombi ya leseni kwa Daraja la 2Provision

A person must not carry out any microfinance service activity unless licensed under the Act.

16.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu cha 28 cha Sheria hii, mtu hapaswi kufanya shughuli yoyote ya kutoa huduma ndogo za fedha isipokuwa kama mtu huyo amepatiwa leseni kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu hiki atakuwa ametenda kosa na iwapo atapatikana na hatia- (a) kwa Daraja la 2, atapata adhabu ya faini isiyopungua shilingi milioni ishirini na isiyozidi shilingi milioni mia moja kifungo kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja; au (b) kwa Daraja la 3, atapata adhabu ya faini isiyopungua shilingi milioni kumi na isiyozidi shilingi milioni hamsini au kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja. (c) kwa Daraja la 3, atapata adhabu ya faini isiyopungua shilingi milioni kumi au kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja. Maombi ya leseni kwa Daraja la 2
Section 16Verify source
§ 17Maombi ya leseni kwa Daraja la 2Provision

Mtu anayetaka kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha Daraja la 2 lazima aombe leseni kutoka Benki na aweke maombi yake pamoja na taarifa na nyaraka zinazohitajika.

17.-(1) Mtu anayekusudia kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha chini ya Daraja la 2 atapaswa kuomba leseni kutoka Benki kama itakavyoainishwa katika kanuni. (2) Maombi ya leseni chini ya Daraja la 2 yatapaswa kuwasilishwa Benki kama kupitia zitavyoonyeshwa katika kanuni, na maombi hayo yatapaswa kuwa na taarifa za mwombaji, biashara ya huduma ndogo za fomu maalum 16 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha fedha husika, mahala au sehemu ya biashara na taarifa nyingine kama itakavyohitajika kwa madhumuni hayo. (3) Maombi yatakayowasilishwa chini ya kifungu kidogo cha (1), yatapaswa kuambatishwa na- (a) nakala iliyothibitishwa ya hati ya usajili iliyotolewa kwa mujibu wa sheria husika; (b) ada ya maombi iliyoainishwa ambayo haitarejeshwa; na (c) taarifa au kama itakavyohitajiwa na Benki kwa madhumuni ya maombi hayo. nyingine nyaraka Maombi ya leseni kwa Daraja la 3 Sura ya 211 (4) Benki utaratibu wa maombi ya yanayohusu wakopesshaji binafsi wa fedha. itatengeneza kanuni zitakazoainisha leseni na masuala mengine
Section 17Verify source
§ 18Maombi ya leseni kwa Daraja la 3Provision

Anayetaka kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha chini ya Daraja la 3 lazima aombe leseni kwa Benki au Mamlaka Kasimiwa.

18.-(1) Mtu anayekusudia kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha chini ya Daraja la 3 atapaswa kuomba leseni kutoka Benki au Mamlaka Kasimiwa kwa utaratibu utakaowekwa katika kanuni. (2) Maombi ya leseni chini ya Daraja la 3 yatapaswa kuwasilishwa Benki au kwa Mamlaka Kasimiwa kupitia fomu maalum na maombi hayo yatapaswa kuambatanishwa na- (a) nakala iliyothibitishwa ya hati ya usajili iliyotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika; (b) ada ya maombi iliyoainishwa ambayo haitarejeshwa; na (c) taarifa au kama itakavyohitajika na Benki au Mamlaka Kasimiwa kwa madhumuni ya maombi ya leseni. nyingine nyaraka Utoaji wa leseni kwa mtoa huduma ndogo za fedha wa kigeni
Section 18Verify source
§ 19Utoaji wa leseni kwa mtoa huduma ndogo za fedha wa kigeniProvision

Mtoa huduma ndogo za fedha wa kigeni anayetaka kufanya biashara lazima aombe leseni kwa Benki.

19.-(1) Mtoa huduma ndogo za fedha wa kigeni anayetaka kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha atapaswa kutuma maombi ya leseni kwa Benki. (2) Utaratibu wa maombi chini ya kifungu kidogo cha (1) utaainishwa kwenye kanuni. (3) Endapo mtoa huduma ndogo za fedha wa kigeni atafanya biashara ya huduma ndogo za fedha nchini, mtoa 17 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha huduma ndogo za fedha huyo atapaswa kuzingatia sheria husika za ushirikishwaji wa wazawa ikijumuisha ajira na mafunzo. Upitiaji wa maombi
Section 19Verify source
§ 20Upitiaji wa maombiProvision

Baada ya kupokea maombi chini ya Sheria hii, Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kuyashughulikia maombi ndani ya muda utakaowekwa na kanuni, ikiwa maombi yamekidhi matakwa ya kisheria yaliyoainishwa.

20. Baada ya kupokea maombi chini ya Sheria hii, Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza, ndani ya kipindi kitakachoainishwa katika kanuni, kuyafanyia kazi maombi iwapo yamezingatia ili kujiridhisha yaliyopokelewa matakwa ya kisheria yaliyoainishwa. Utoaji leseni
Section 20Verify source
§ 21Utoaji leseniProvision

Ikiwa Benki au Mamlaka Kasimiwa itaridhika kwamba mwombaji ametimiza matakwa yote ya leseni, lazima itoe leseni na imsajili mtoa huduma ndogo za fedha katika rejesta.

21. Endapo Benki au Mamlaka Kasimiwa itaridhika kuwa mwombaji amekidhi matakwa yote ya kupewa leseni chini ya Sheria hii, Benki au Mamlaka Kasimiwa itapaswa: Uhalali wa leseni Kukataa maombi ya leseni Maombi mapya na kukata rufaa (a) kutoa leseni kwa mwombaji yenye vigezo na masharti kama Benki au Mamlaka Kasimiwa itakavyoona inafaa; na (b) kusajili mtoa huduma ndogo za fedha aliyepewa leseni katika rejesta.
Section 21Verify source
§ 22Uhalali wa leseniProvision

Leseni iliyotolewa chini ya Sheria hii ni halali kuanzia tarehe iliyotolewa, na hubaki halali isipokuwa ifutwe na Benki au Mamlaka Kasimiwa.

22. Leseni iliyotolewa chini ya Sheria hii itakuwa halali kuanzia tarehe iliyotolewa na itakuwa halali isipokuwa kama itafutwa na Benki au Mamlaka Kasimiwa.
Section 22Verify source
§ 23Kukataa maombi ya leseniProvision

Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kukataa kutoa leseni ikiwa mwombaji hakukidhi masharti au ametoa taarifa zisizo sahihi; ikikataa, lazima imjulishe mwombaji sababu kwa maandishi ndani ya siku 7.

23.-(1) Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kukataa kutoa leseni iwapo- (a) mwombaji ameshindwa kukidhi vigezo na masharti ya kupata leseni; au (b) mwombaji ametoa zinazopotosha. taarifa zisizo sahihi au (2) Endapo Benki au Mamlaka Kasimiwa itakataa kutoa leseni, itapaswa ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya uamuzi wake, kumtaarifu mwombaji kwa maandishi sababu za kukataa. ambaye maombi
Section 23Verify source
§ 24Maombi mapya na kukata rufaaProvision

An applicant whose application was rejected may apply again if the problems that caused the rejection have been fixed or otherwise addressed.

24.-(1) Mwombaji yake yatakataliwa anaweza kuomba upya, iwapo mapungufu yaliyokuwa msingi wa kukataliwa kwa maombi ya awali au mapitio ya maombi yamerekebishwa au vinginevyo yameshughulikiwa. 18 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha Ufutaji wa leseni Utaratibu wa kufuta leseni (2) Mwombaji asiyeridhika na uamuzi ya Benki au Mamlaka Kasimiwa chini ya kifungu kidogo cha (1) anaweza, ndani ya siku ishirini na moja kuanzia tarahe ya uamuzi- (a) iwapo ni Mamlaka Kasimiwa, kukata rufaa kwa Benki; au (b) iwapo ni Benki, kukata rufaa kwa Waziri. (3) Mtu ambaye hataridhishwa na uamuzi wa Waziri chini ya kifungu hiki, anaweza kutafuta nafuu kwenye mahakama yenye mamlaka stahiki.
Section 24Verify source
§ 25Ufutaji wa leseniProvision

Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kufuta leseni ya mtoa huduma ndogo za fedha kwa notisi ikiwa ipo sababu zilizoelezwa, na lazima ichapishe jina la aliyefutiwa leseni ndani ya siku 14.

25.-(1) Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza, kwa kutoa notisi kwa mtoa huduma ndogo za fedha, kufuta leseni pale ambapo mtoa huduma ndogo za fedha- (a) atasitisha biashara ya huduma ndogo za fedha; (b) atakiuka vigezo na masharti yaliyowekwa kwenye leseni; (c) atafilisika au vinginevyo kufutwa; (d) atafutiwa usajili chini ya sheria husika; au (e) atakiuka masharti ya Sheria hii. (2) Benki au Mamlaka Kasimiwa, ndani ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya kufutwa leseni, itapaswa kuchapisha jina la mtoa huduma ndogo za fedha aliyefutiwa leseni katika Gazeti la Serikali na gazeti linalosambazwa kwa wingi kwa umma.
Section 25Verify source
§ 26Utaratibu wa kufuta leseniProvision

Ikiwa mtoa huduma ndogo za fedha anakiuka masharti ya leseni, Benki au Mamlaka Kasimiwa lazima itoe notisi ya maandishi; mtoa huduma lazima ajibu kwa maelezo ya marekebisho; na ikishindikana, leseni inaweza kufutwa na kuna njia za rufaa.

26.-(1) Endapo mtoa huduma ndogo za fedha atakiuka vigezo na masharti ya leseni iliyotolewa, Benki au Mamlaka Kasimiwa itatoa notisi ya maandishi kwa mtoa huduma ndogo za fedha inayobainisha ukiukwaji uliofanyika na muda ambao ukiukwaji huo unapaswa kurekebishwa. (2) Baada ya mtoa huduma ndogo za fedha kupokea notisi ya ukiukwaji, atapaswa kuwasilisha kwa Benki au Mamlaka Kasimiwa maelezo kuhusu marekebisho ya ukiukwaji au kasoro iliyofanyika . (3) Endapo mtoa huduma ndogo za fedha atashindwa kurekebisha au kusahihisha makosa ndani ya muda ulioainishwa katika notisi au hatawasilisha maelezo yanayojitosheleza, Benki au Mamlaka Kasimiwa itafuta 19 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha leseni iliyotolewa na kumtaarifu ipasavyo mtoa huduma ndogo za fedha kwa maandishi. (4) Mtoa huduma ndogo za fedha ambaye hakuridhika na uamuzi wa Benki au Mamlaka Kasimiwa ya kufuta leseni, anaweza- (a) iwapo uamuzi ulifanywa na Benki, kukata rufaa kwa Waziri; na (b) iwapo uamuzi ulifanywa na Mamlaka Kasimiwa, kukata rufaa kwa Benki. (5) Mtu ambaye hataridhishwa na uamuzi wa Waziri chini ya kifungu hiki, anaweza kutafuta nafuu kwenye mahakama yenye mamlaka stahiki.
Section 26Verify source
§ 27Matokeo ya kufuta leseniProvision

If a microfinance service provider’s licence is revoked, the Bank or delegated authority must remove its name from the register and issue written directions to stop operations and handle user or member assets and liabilities within the stated time.

27.-(1) Endapo leseni ya mtoa huduma ndogo za fedha itafutwa kwa mujibu wa Sheria hii, Benki au Mamlaka Kasimiwa itapaswa kufuta jina la mtoa huduma ndogo za fedha kutoka kwenye kwa maandishi itamwelekeza mtoa huduma ndogo za fedha- rejesta na (a) kusimamisha shughuli zake kuanzia tarehe ya kufutwa kwa leseni; (b) kusimamia na kushughulikia ndani ya muda utakaoainishwa, masuala yote yanayohusu mali na madeni ya watumiaji au wanachama. Matokeo ya kufuta leseni (2) Endapo mtoa huduma ndogo za fedha atashindwa kutekeleza maelekezo yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1), Benki itakuwa na mamlaka ya kuchukua hatua stahiki kulinda haki za watumiaji au wanachama. SEHEMU YA TANO USAJILI WA WATOA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA WA DARAJA LA 4 Usajili wa watoa huduma ndogo za fedha chini ya Daraja la 4
Section 27Verify source

Part

SEHEMU YA TANO

§ 2829Provision

An applicant who wants to operate a Grade 4 microfinance business must submit a registration application to the Bank or the delegated authority.

28.-(1) Mtu anayekusudia kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha chini ya Daraja la 4 atapaswa kuwasilisha Benki au Mamlaka Kasimiwa maombi ya kusajiliwa kwa utaratibu utakaoanishwa katika kanuni. (2) Maombi ya kusajiliwa yatawasilishwa Benki au katika Mamlaka Kasimiwa kwa kutumia fomu maalum na maombi hayo yatapaswa kuambatanishwa na- 20 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha (a) nakala mbili za katiba zilizotiwa saini na wanachama wa mwombaji; (b) azimio la wanachama la kuanzisha na kusajili kikundi cha huduma ndogo za fedha ambalo limesainiwa na wanachama wote; (c) muundo wa kikundi unaopendekezwa na majina ya viongozi yanayopendekezwa na mwombaji; (d) barua ya utambulisho kutoka kwenye kata au serikali ya kijiji inayomtambulisha mwombaji; na (e) nyaraka au taarifa nyingine zozote ambazo Benki au Mamlaka Kasimiwa zitazihitaji.
Section 28Verify source
§ 2930Provision

Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kukataa kumwandikisha mwombaji ikiwa hajakidhi vigezo vya usajili au ametoa taarifa zisizo sahihi; ikikataa, lazima ifahamishe sababu kwa maandishi ndani ya siku 7.

29.-(1) Kwa kuzingatia kifungu cha 28 cha Sheria inaweza kukataa hii, Benki au Mamlaka Kasimiwa kumsajili mwombaji iwapo- (a) ameshindwa kutimiza vigezo vya usajili; au (b) ametoa taarifa zisizo sahihi au zinazopotosha. (2) Endapo Benki au Mamlaka Kasimiwa imekataa kumsajili mwombaji chini ya kifungu hiki, itapaswa ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya uamuzi wake, kumjulisha mwombaji kwa maandishi sababu za kukataa kumsajili. (3) Mwombaji ambaye maombi yake yamekataliwa kwa mujibu wa kifungu hiki anaweza kuwasilisha maombi mpya kwa kuzingatia sababu za kukataliwa kwa maombi yake na maombi hayo yatashughulikiwa kama maombi mapya na yatafuata taratibu zote za maombi. (4) Mtu ambaye hataridhishwa na uamuzi chini ya kifungu hiki anaweza- (a) kwa uamuzi uliyofanywa na Mamlaka Kasimiwa, kata rufaa kwa Benki; na (b) kwa uamuzi uliyofanywa na Benki, kata rufaa kwa Waziri.
Section 29Verify source
§ 3031. Matokeo ya usajiliProvision

After registering a class 4 microfinance service provider, the bank or delegated authority must issue a registration certificate.

30.-(1) Benki au Mamlaka Kasimiwa mara baada ya kufanya usajili wa mtoa huduma ndogo za fedha chini ya Daraja la 4, itatoa kwa mtoa huduma huyo hati ya usajili. (2) Hati ya usajili inayotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1) itajumuisha- (a) jina na anwani ya mtoa huduma ndogo za fedha; 21 Kukataa maombi ya usajili kwa Daraja la 4 Hati ya usajili Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha Matokeo ya usajili (b) tarehe na uhalali wa usajili; (c) eneo la shughuli au sehemu ya biashara ya mtoa huduma ndogo za fedha; na (d) vigezo na masharti mengine yatakayohitajika.
Section 30Verify source
§ 31Matokeo ya usajiliOffence

A registered microfinance service provider may operate as a corporate body, while any person or group doing Class 4 microfinance business without registration commits an offence.

31.-(1) Hati ya usajili itakuwa ndiyo ushahidi kwa mtoa huduma ndogo za fedha kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha kwa kuzingatia masharti ya katiba yake na Sheria hii. (2) Mtoa huduma ndogo za fedha aliyesajiliwa atakuwa na hadhi ya taasisi hodhi na kwa kutumia jina lake itaweza- (a) kushtaki na kushtakiwa; (b) kupata, kununua au kwa namna nyingine kuuza mali zinazohamishika au zisizohamishika; (c) kuingia mkataba; na (d) kutekeleza mambo yote ambayo yanaweza kufanywa na taasisi hodhi na ambayo ni ya lazima kwa ajili ya utekelezaji wa kazi na majukumu yake. (3) Mtu au kikundi chochote ambacho kinajihusisha na biashara ya huduma ndogo za fedha chini ya Daraja la 4 bila kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria hii anatenda au kinatenda kosa. Ufutaji hati ya usajili
Section 31Verify source
§ 3233Provision

The Bank or Commissioner may cancel a registration certificate if the stated conditions are met, and if it is cancelled they must notify the provider in writing, direct the provider to stop operations, and remove the provider’s name from the register.

32.-(1) Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kufuta hati ya usajili iwapo itajiridhisha kuwa: (a) vigezo na masharti yaliyowekwa katika hati ya usajili yamekiukwa; (b) mtoa huduma ndogo za fedha ameacha kutoa huduma; na (c) mtoa huduma ndogo za fedha anatoa huduma kinyume na masharti ya Sheria hii au sheria nyingine husika. (2) Endapo hati ya usajili imefutwa, Benki au Mamlaka Kasimiwa itafanya yafuatayo: (a) kumfahamisha mtoa huduma ndogo za fedha kwa maandishi sababu za kufutwa kwa usajili; (b) kumwagiza mtoa huduma ndogo za fedha kusitisha shughuli zake; na 22 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha (c) kufuta jina la mtoa huduma ndogo za fedha huyo katika rejesta. (3) Masharti ya kifungu cha 26 cha Sheria hii kuhusu taratibu za kufuta leseni yatatumika kwa kuweka marekebisho madogo stahiki katika kufuta hati ya usajili iliyotolewa chini ya Sheria hii. Uendelezaji na uwezeshaji watoa huduma ndogo za fedha
Section 32Verify source
§ 33Ufutaji hati ya usajiliProvision

Benki kwa kushirikiana na Baraza lazima ichukue hatua za kuendeleza watoa huduma ndogo za fedha wa Daraja la 4, ikiwemo kutoa elimu ya fedha, kusaidia maendeleo yao, kulinda maslahi na haki za wanachama na wanufaika, na kutumia programu za Serikali.

33.-(1) Kwa madhumuni ya kuendeleza ukuaji na uendelevu wa mtoa huduma ndogo za fedha katika Daraja la 4, Benki kwa kushirikiana na Baraza- (a) itatoa elimu ya masuala ya fedha kwa wanachama wa watoa huduma ndogo za fedha; (b) itaendeleza na kuingilia kati iwapo italazimika kwa kuwaendeleza watoa huduma ndogo za fedha; (c) italinda maslahi na haki za wanachama na wanufaika wa watoa huduma ndogo za fedha; (d) itatoa msaada kwa mtoa huduma ndogo za fedha kupitia programu mbalimbali za Serikali; (e) itafanya kazi nyingine kwa madhumuni ya kuendeleza na kuwawezesha watoa huduma ndogo za fedha. (2) Katika kifungu hiki "Baraza" maana yake ni Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoanzishwa chini ya Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi. la Taifa SEHEMU YA SITA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA WATOA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA (a) Usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Usimamizi wa biashara ya huduma ndogo za fedha
Section 33Verify source

Part

SEHEMU YA SITA

§ 3435Provision

Mtoa huduma ndogo za fedha anapaswa kusimamia shughuli, masuala ya fedha na biashara ya huduma ndogo za fedha.

34. Usimamizi wa shughuli, masuala ya fedha na biashara ya huduma ndogo za fedha utafanywa na mtoa huduma ndogo za fedha. Usimamizi na utwaaji
Section 34Verify source
§ 3536Provision

Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kuchukua usimamizi wa huduma ndogo ya fedha chini ya masharti fulani.

35.-(1) Bila ya kujali kifungu cha 34 na sheria nyingine husika, Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza 23 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha kutwaa usimamizi wa huduma ndogo ya fedha endapo- (a) Benki au Mamlaka Kasimiwa inaona kuwa mtoa huduma ndogo za fedha- (i) (ii) (iii) hana uwezo wa kifedha; hafanyi kazi zake kwa mujibu wa taratibu bora za kiutawala na kihasibu; na hazingatii sera sahihi za udhibiti wa viashiria vya hatari; (b) mtoa huduma ndogo za fedha ameshindwa kuzingatia masharti ya kiwango cha chini cha mtaji yaliyoainishwa na Sheria hii; (c) mtoa huduma ndogo anakataa kukaguliwa na Benki au Mamlaka Kasimiwa kama inavyotakiwa na Sheria hii; fedha za (d) leseni ya mtoa huduma ndogo za fedha imefutwa; (e) kuendelea kwa biashara hiyo ya huduma ndogo za fedha kutaathiri maslahi ya mteja wa huduma ndogo za fedha; au (f) mtoa huduma ndogo za fedha anafanya biashara ya huduma ndogo za fedha kinyume na Sheria hii. (2) Mdaawa katika mkataba na mtoa huduma ndogo za fedha hataondolewa wajibu wake kwa kigezo kwamba mtoa huduma ndogo za fedha yupo chini ya usimamizi ya Benki au Mamlaka Kasimiwa. (3) Gharama za usimamizi wa biashara ya huduma fedha wakati wa kipindi cha kutwaliwa ndogo za hazitabebwa na Benki au Mamlaka Kasimiwa. (4) Utaratibu wa usimamizi na utwaaji wa biashara ya huduma ndogo za fedha chini ya kifungu hiki utakuwa kama utakavyoainishwa katika kanuni. Shughuli zinazozuiliwa na zinazokuba- lika
Section 35Verify source
§ 3637Provision

Microfinance service providers must not provide services that are prohibited by this Act or any other Act. The Bank may set permitted and prohibited activities by regulation, and the Bank or delegated authority must take appropriate action if a provider fails, without good reason, to comply.

36.-(1) Mtoa huduma ndogo za fedha hatajihusisha na kutoa huduma yoyote iliyozuiliwa chini ya Sheria hii au sheria nyingine yoyote ya Bunge. (2) Benki, kupitia kanuni, itaainisha shughuli zinazoruhusiwa na zisizoruhusiwa kwa watoa huduma ndogo za fedha. 24 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha Ulipaji wa gawio au riba fedha (3) Endapo mtoa huduma ndogo za atashindwa, bila sababu ya msingi, kutekeleza masharti ya kifungu hiki, Benki au Mamlaka Kasimiwa itapaswa kuchukua hatua stahiki kama itakavyofaa kuhakikisha masharti yanazingatiwa.
Section 36Verify source
§ 3738Provision

Mtoa huduma ndogo za fedha lazima walipe wanahisa gawio au riba, au kutumia utaratibu mwingine wa mgao unaoruhusiwa, kwa mujibu wa sheria husika.

37.-(1) Mtoa huduma ndogo za fedha atapaswa kuwalipa wanahisa wake gawio au atafanya utaratibu mwingine wowote wa mgao au kuwalipa riba wanahisa au wanachama wake kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii na sheria nyingine husika. (2) Malipo ya gawio, riba na aina yoyote ya mgao chini ya kifungu kidogo cha (1), ikijumuisha kipindi cha malipo, itakuwa kwa namna itakavyoainishwa kwenye katiba au kwenye nyaraka nyingine husika za mtoa huduma ndogo za fedha. Vitabu vya mahesabu na kumbukumbu nyinginezo
Section 37Verify source
§ 3839Provision

Mtoa huduma ndogo za fedha lazima atunze vitabu sahihi vya mahesabu na kumbukumbu nyingine za biashara zinazoweza kuonyesha na kuelezea miamala na masuala ya kifedha.

38. Mtoa huduma ndogo za fedha atatunza vitabu sahihi vya mahesabu pamoja na kumbukumbu nyingine zinazohusiana na biashara yake ambazo zinatosheleza, kuonyesha na kuelezea miamala aliyoifanya pamoja na masuala ya kifedha. Uandaaji wa mahesabu
Section 38Verify source
§ 3940Provision

Each microfinance service provider must prepare accounts every financial year using the specified standards.

39.-(1) Kila mtoa huduma ndogo za fedha kwa kila mwaka wa fedha atapaswa kuandaa mahesabu katika viwango vilivyoainishwa. (2) Viwango vilivyoainishwa kwa ajili ya kuandaa mahesabu ya biashara ya watoa huduma ndogo za fedha vitazingatia vigezo vya kitaifa vya utayarishaji wa taarifa za fedha. (3) Hesabu na taarifa nyingine za fedha za biashara ya huduma ndogo za fedha zitawasilishwa kwa kutumia shilingi ya Kitanzania na zitazingatia matakwa ya sheria husika. Ukaguzi wa mahesabu
Section 39Verify source
§ 40Usimamizi wa biashara ya huduma ndogo za fedhaProvision

Hesabu za biashara ya huduma ndogo za fedha lazima zikaguliwe angalau mara moja kwa mwaka, isipokuwa kwa watoa huduma wa Daraja la 4.

40.-(1) Hesabu za biashara ya huduma ndogo za fedha, isipokuwa kwa mtoa huduma ndogo za fedha wa Daraja la 4, zitakaguliwa angalau mara moja kwa mwaka na mkaguzi kwa namna ilitakavyoainishwa kwenye kanuni. (2) Bila ya kujali masharti ya kifungu kidogo cha 25 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha (1), hesabu na taarifa nyingine za fedha za watoa huduma ndogo za fedha kwa Daraja la 4 zitakaguliwa au kufuatiliwa kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni. (3) Endapo Benki au Mamlaka Kasimiwa itajiridhisha kwamba hesabu zilizokaguliwa za mtoa huduma ndogo za fedha hazijakidhi masharti ya Sheria hii au kanuni husika au zimejumuisha taarifa inayoweza kupotosha au iwapo hazijatangazwa kwa utaratibu ulioainishwa katika fomu, Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kumtaka mtoa huduma- (a) kuzifanyia marekebisho hesabu hizo zilizokaguliwa ili kutimiza matakwa ya Sheria; nyaraka (b) kurekebisha taarifa zinazopotosha; (c) kuchapisha upya hesabu zilizorekebishwa; na (d) kuwasilisha kwa Benki au kwa Mamlaka ziada Kasimiwa zinazohusiana na nyaraka au taarifa yoyote. (4) Endapo mtoa huduma ndogo za fedha, bila sababu ya msingi, atashindwa kutekeleza masharti ya kifungu hiki, Benki au Mamlaka Kasimiwa itachukua hatua stahiki kama itakavyoona inafaa ili kuhakikisha masharti yanatekelezwa. taarifa au za Uteuzi wa mkaguzi wa ndani Utoaji wa taarifa za fedha
Section 40Verify source
§ 4142Provision

Mtoa huduma ndogo za fedha lazima ateue mkaguzi wa hesabu wa ndani, na mtoa huduma wa Daraja la 4 lazima pia ateue mtu wa kusimamia ndani masuala ya fedha.

41.-(1) Mtoa huduma ndogo za fedha atateua mkaguzi wa hesabu wa ndani ambaye atakuwa na elimu na uzoefu ulioanishwa kwenye kanuni husika. (2) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), mtoa huduma ndogo za fedha kwa Daraja la 4 atateua mtu atakayekuwa na dhamana ya usimamizi wa ndani wa masuala ya fedha ya mtoa huduma huyo kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni.
Section 41Verify source
§ 4243Provision

Mtoa huduma ndogo za fedha lazima atoe taarifa za fedha na aweke nakala za hesabu zilizokaguliwa, mizania na akaunti ya faida na hasara kwa namna iliyoainishwa.

42.-(1) Mtoa huduma ndogo za fedha atatoa taarifa zake za fedha kwa Benki, Mamlaka Kasimiwa na wadau wengine kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni. (2) Bila ya kuathiri kifungu kidogo cha (1), mtoa huduma ndogo za fedha, kwa kipindi chote cha mwaka na katika sehemu ya biashara inayoonekana, ataweka nakala ya hesabu za fedha zilizokaguliwa kwa kipindi husika, nakala ya mizania ya hesabu na akaunti ya faida na hasara kwa 26 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha muundo na namna itakavyoainishwa na Benki au Mamlaka Kasimiwa. (3) Bila ya kujali masharti ya kifungu kidogo cha (1), Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kuainisha namna ambavyo mtoa huduma ndogo za fedha wa Daraja la 4 atakavyotoa taarifa zake za fedha. (4) Endapo mtoa huduma ndogo za fedha, bila sababu za msingi, atashindwa kutekeleza masharti ya kifungu hiki, Benki au Mamlaka Kasimiwa itachukua hatua stahiki kama ili kuhakikisha masharti yanatekelezwa. itakavyofaa
Section 42Verify source
§ 43Uteuzi wa mkaguzi wa ndaniProvision

Microfinance service providers must provide credit information in the manner set by regulations, and class 2, 3, and 4 providers must provide it to the credit information exchange body.

43.-(1) Mtoa huduma ndogo za fedha atatoa taarifa za mikopo kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni. (2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, taarifa za mikopo zitajumuisha taarifa zozote zikiwemo taarifa binafsi na historia ya mikopo ya mkopaji kama vile mwenendo wa urejeshaji wa mikopo, madeni ambayo hayajalipwa, madeni ya kodi na taarifa nyingine zozote za kibiashara. (3) Bila ya kujali vifungu vidogo vya (1) na (2), kwa madhumuni ya kuwezesha upatikanaji wa taarifa za mikopo, kila mtoa huduma ndogo za fedha wa Daraja la 2, 3 na 4 atatoa taarifa za mikopo kwa chombo cha ubadilishaji taarifa za mikopo (4) Mtoa huduma ndogo za fedha anaweza kupata na cha namna za mikopo kupitia za mikopo chombo kwa kutumia ubadilishanaji itakavyoainishwa kwenye kanuni. taarifa taarifa (5) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu hiki, udhibiti wa taarifa za mikopo utafanywa kwa mujibu wa Sheria ya Benki. (6) fedha atashindwa, bila sababu za msingi, kutekeleza masharti ya kifungu hiki, Benki au Mamlaka Kasimiwa itachukua hatua stahiki ili kuhakikisha masharti yanatekelezwa. Endapo mtoa huduma ndogo za Utoaji wa taarifa za mikopo Sura 197 (b) Usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Uwasilishaji wa taarifa
Section 43Verify source
§ 4445Provision

Mtoa huduma ndogo za fedha lazima apeleke taarifa za biashara yake kwa Benki au Mamlaka Kasimiwa kwa muda na namna itakavyobainishwa na Benki.

44.-(1) Mtoa huduma ndogo za fedha atawasilisha kwa Benki au kwa Mamlaka Kasimiwa taarifa za biashara 27 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha Upatikanaji wa taarifa za muda Usiri yake ya huduma ndogo za fedha kwa kipindi na kwa namna itakavyoainishwa katika Benki. (2) Endapo mtoa huduma ndogo za fedha, bila sababu za msingi, atashindwa kutekeleza masharti ya kifungu hiki, Benki au Mamlaka Kasimiwa itachukua hatua stahiki kama itakavyoona inafaa ili kuhakikisha masharti yanatekelezwa.
Section 44Verify source
§ 4546Provision

The Bank or delegated authority may obtain information about any microfinance service provider’s activities and may direct in writing that the information be submitted within the stated time.

45.-(1) Benki au Mamlaka Kasimiwa itakuwa na mamlaka ya kupata taarifa zinazohusu shughuli za watoa ya huduma ndogo za fedha wowote na inaweza kuelekeza, kwa maandishi, kwamba taarifa hiyo iwasilishwe ndani ya muda ulioanishwa kwenye maelekezo. (2) Endapo mtoa huduma ndogo za fedha, bila sababu za msingi, atashindwa kutekeleza masharti ya kifungu hiki, Benki au Mamlaka Kasimiwa itachukua hatua stahiki kama itakavyoona inafaa ili kuhakikisha masharti yanatekelezwa.
Section 45Verify source
§ 4647Provision

Benki, Mamlaka Kasimiwa, au mtoa huduma ndogo za taarifa lazima kwa ujumla ziitambue taarifa zilizopatikana chini ya Sheria hii kuwa siri na zisizotolewa kwa mtu yeyote, isipokuwa katika hali zilizoelezwa hapa.

46.-(1) Endapo Benki au Mamlaka Kasimiwa au mtoa huduma ndogo za taarifa iliyopatikana chini ya Sheria hii, taarifa hiyo itaichukuliwa kuwa ni siri na haitatolewa kwa mtu yeyote. fedha atakuwa na (2) Bila ya kujali kifungu kidogo cha (1), Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kutoa taarifa yoyote- (a) kwa mtu au taasisi iliyoidhinishwa endapo taarifa hiyo inahitajika na ni kwa ajili ya usimamizi au udhibiti na usiri wake utaendelea kulindwa; au (b) kwa mujibu wa sheria, amri ya mahakama au kwa ridhaa ya mtumiaji wa huduma ndogo za fedha husika. Ukaguzi wa biashara ya huduma ndogo za fedha
Section 46Verify source
§ 4748Provision

Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kukagua mtoa huduma ndogo za fedha, na mtoa huduma lazima aonyeshe vitabu, kumbukumbu na nyaraka na atoee taarifa zinazoombwa. Pia, mtu yeyote anayekwamisha ukaguzi au kukataa kuonyesha vitu vinavyohitajika anatenda kosa.

47.-(1) Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza, kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni, kukagua mtoa huduma ndogo za fedha yeyote. (2) Itakuwa ni wajibu wa mtoa huduma ndogo za fedha kumwonyesha afisa yeyote aliyeruhusiwa kufanya ukaguzi, vitabu vyote vya hesabu, kumbukumbu na nyaraka nyingine zilizo chini ya mamlaka au uangalizi wa mtu huyo 28 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha na kutoa maelezo au taarifa yoyote inayohusu na shughuli za mtoa huduma ndogo za fedha kama ambavyo mamlaka ya ukaguzi itakavyohitaji katika muda utakaoainishwa. (3) Endapo Benki au Mamlaka Kasimiwa, baada ya kuzingatia ripoti ya ukaguzi chini ya kifungu kidogo cha (1), itabaini kwamba shughuli za mtoa huduma ndogo za fedha zinawaathiri wateja wake au zinafanywa kinyume na Sheria hii, inaweza, baada ya kumpa mtoa huduma ndogo za fedha haki ya kujieleza kuhusiana na ripoti hiyo, kuchukua hatua kwa namna itakavyoona inafaa, ikijumuisha- (a) kumzuia, kumsitisha au kumkataza mtoa huduma ndogo za fedha kulipa gawio; (b) kusitisha leseni kwa kipindi ambacho Benki au Mamlaka Kasimiwa itaona inafaa; (c) kuzuia uhamishaji wa faida yoyote ya mtoa huduma ndogo za fedha kwenda kwenye mtaji; (d) kumwelekeza mtoa huduma ndogo za fedha kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya afisa yeyote aliyehusika na kitendo hicho; (e) kumwelekeza mtoa huduma ndogo za fedha kuunda upya menejimenti yake; (f) kumwelekeza mtoa huduma ndogo za fedha, ndani ya muda ulioainishwa, kuwasilisha Benki au kwa Mamlaka Kasimiwa- (i) mpango wa urejeshaji wa mtaji; au (ii) mpango wa kurekebisha mapungufu yote kwa namna ambavyo Benki au Mamlaka Kasimiwa itajiridhisha; (g) kumzuia mtoa huduma ndogo za fedha asitoe bonasi, nyongeza ya mshahara na marupurupu mengine kwa uongozi wa juu wa menejimenti au kwa maafisa wa watoa huduma ndogo za fedha; (h) kuzuia ongezeko la mali au madeni ya huduma ndogo za fedha kwa namna itakavyoona inafaa; (i) kumtaka mtoa huduma ndogo za fedha kufanya au kuchukua hatua nyingine yoyote kama ambavyo Benki au Mamlaka Kasimiwa itakavyoona inafaa. (4) Mtu yeyote atakayemzuia afisa wa Benki au wa yeyote au mtu mwingine Mamlaka Kasimiwa 29 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha Usimamizi wa biashara ya huduma ndogo za fedha kwa Daraja la 4 aliyeidhinishwa kutekeleza majukumu yake chini ya kifungu hiki, au ambaye anapuuza au kukataa kuonyesha vitabu, kumbukumbu au kitu chochote ambacho afisa wa Benki au wa Mamlaka Kasimiwa au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa atakapohitaji kupatiwa kwa ajili ya ukaguzi, atakuwa ametenda kosa.
Section 47Verify source
§ 4849Provision

Benki au Mamlaka Kasimiwa lazima ifanye au iagize kufanyika usimamizi endelevu wa mtoa huduma ndogo za fedha wa Daraja la 4.

48.-(1) Benki au Mamlaka Kasimiwa itafanya au kuagiza kufanyika usimamizi endelevu wa biashara na shughuli za mtoa huduma ndogo za fedha wa Daraja la 4 kwa mujibu wa kanuni husika. (2) Endapo baada ya kufanya usimamizi chini ya kifungu kidogo cha (1), Benki au Mamlaka Kasimiwa itabaini mapungufu kwenye usimamizi wa biashara ya huduma ndogo za fedha, Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza- (a) kushauri au kumwelekeza mtoa huduma ndogo za fedha kurekebisha mapungufu ndani ya muda ulioainishwa; au (b) kumwelekeza mtoa huduma ndogo za fedha kuchukua hatua nyingine zozote ili kuhakikisha kwamba masharti ya Sheria hii yanatekelezwa. (3) Endapo mtoa huduma ndogo za fedha atashindwa, bila sababu za msingi, kutekeleza amri au maelekezo yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (2), Benki au Mamlaka Kasimiwa itachukua hatua stahiki kama itakavyoona inafaa ili kuhakikisha masharti yanatekelezwa. Uzingatiaji wa Sura ya 423
Section 48Verify source
§ 49Uwasilishaji wa taarifaProvision

Mtoa huduma ndogo za fedha lazima aweke utaratibu wa udhibiti wa ndani kwa ajili ya utambuzi wa wateja na kuripoti miamala inayotia shaka.

49.-(1) Mtoa huduma ndogo za fedha ataweka, ili kutekeleza Sheria za Kudhibiti Utakasishaji wa Fedha Haramu, utaratibu wa udhibiti wa ndani kwa lengo la utambuzi wa wateja na kutoa taarifa ya miamala inayotia shaka. (2) Benki au Mamlaka Kasimiwa itahakikisha kuwa kila mtoa huduma ndogo za fedha anatoa huduma kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1). 30 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha SEHEMU YA SABA ULINZI WA WATUMIAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA Misingi ya kumlinda mtumiaji wa huduma ndogo za fedha
Section 49Verify source

Part

SEHEMU YA SABA

§ 50Misingi ya kumlinda mtumiaji wa huduma ndogo za fedhaProvision

Watoa huduma ndogo za fedha lazima wafuate misingi ya ulinzi wa walaji, na masharti yanayowapa mtoa huduma uwezo wa kuongeza au kubadilisha riba au masharti ya mkopo ni batili.

50.-(1) Watoa huduma ndogo za fedha wanapaswa kufuata misingi ya ulinzi wa walaji kwa mujibu wa sheria zinazotumika na katika kanuni zilizotengenezwa chini ya Sheria hii. (2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (1), misingi fedha ya ulinzi wa walaji wa huduma ndogo za itakayoainishwa katika kanuni, itajumuisha- (a) vigezo na masharti ya mikopo au huduma zinazohusiana na hizo kuwa ya wazi, usawa, yanayosomeka na yanayolinda haki na maslahi ya watumiaji wa huduma ndogo za fedha au wanachama; (b) ushughulikiaji wa malalamiko na njia za utatuzi wa migogoro; (c) utoaji wa taarifa zote husika zinazohusu bidhaa na huduma zinazotolewa; (d) sharti la kuhakiki masharti ya viwango vya mikataba ya mikopo au makubaliano; (e) utoaji wa elimu ya fedha kwa wateja; (f) uwazi katika viwango vya riba, tozo au adhabu; na (g) misingi mingine yoyote la kuhakikisha usawa kwa watumiaji wa huduma ndogo za fedha. kwa lengo (3) Kwa mujibu wa kifungu hiki- na bidhaa uwazi wa “ulinzi kwa mtumiaji” inajumuisha misingi iliyokusudiwa kuhakikisha huduma zinazotolewa na watoa huduma ndogo za fedha, usawa na ulinzi wa maslahi na haki za mtumiaji pamoja na ushughulikiaji wa haki wa malalamiko na njia za utatuzi wa migogoro. (4) Bila ya kujali masharti ya kifungu kidogo cha (2) na (3), kigezo au sharti lolote litakalowekwa katika mkataba au nyaraka husika yoyote zinazodai kumpa mtoa huduma ndogo za fedha mamlaka ya kuweka au kubadilisha kiwango cha riba au masharti mengine yeyote ya mkopo litakuwa ni batili na halitatambulika kisheria. 31 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha fedha (5) Endapo mtoa huduma ndogo za atashindwa, bila sababu ya msingi, kufuata masharti ya kifungu hiki, Benki au Mamlaka Kasimiwa itachukua hatua itakayoona inafaa ili kuhakikisha utekelezaji wa masharti yaliyowekwa. Ukusanyaji wa madeni na fidia
Section 50Verify source
§ 51Ukusanyaji wa madeni na fidiaProvision

Madeni ya huduma ndogo za fedha yanakusanywa au kufidiwa kwa utaratibu utakaowekwa na kanuni, na kanuni hizo zinapaswa kuhitaji notisi ya maandishi, matumizi ya kukamata au kuuza mali ya dhamana kama njia ya mwisho, na muda wa kutosha wa notisi kabla ya kuuza au kuchukua mali.

51.-(1) Deni linalotokana na shughuli za biashara za huduma ndogo za fedha chini ya Sheria hii litakusanywa au litafidiwa kwa utaratibu utakaoainishwa kwenye kanuni. (2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo (1), kanuni zitakazotengenezwa chini ya kifungu hiki zitahakikisha- (a) hatua za ukusanyaji wa deni inaanzishwa kwa kutoa notisi inayojitosheleza ya maandishi kwa mdaiwa; (b) ukamataji wa mali ya mdaiwa au mali iliyowekwa dhamana kwa ajili ya kuuza ili kufidia deni utafanywa kama njia ya mwisho kabisa; na (c) muda wa kutosha unaainishwa kama notisi kwa mdaiwa kabla ya kuuza au kuchukua mali ya mdaiwa iliyowekwa dhamana. (3) Endapo mtoa huduma ndogo za fedha atashindwa, bila sababu ya msingi, kufuata masharti ya kifungu hiki, Benki au Mamlaka Kasimiwa itachukua hatua itakayoona inafaa ili kuhakikisha utekelezaji wa masharti yaliyowekwa. SEHEMU YA NANE MAKOSA NA ADHABU Adhabu ya ujumla
Section 51Verify source

Part

SEHEMU YA NANE

§ 5253Offence

A person who violates the Law’s provisions, when no specific penalty is set, commits an offence and may be fined or imprisoned depending on the grade.

52. Mtu atakayekiuka masharti ya vifungu vya Sheria hii ambapo hakuna adhabu mahsusi iliyowekwa, atakuwa ametenda kosa- (a) kwa Darala la 2 na 3, atahukumiwa kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tano na isiyozidi shilingi milioni ishirini au kifungo cha kipindi kisichopungua miezi mitatu na kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja; na (b) kwa Daraja la 4, atahukumiwa kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja na isiyozidi 32 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha Ufililishaji wa makosa shilingi milioni kumi au kifungo kisichopungua miezi mitatu na kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja.
Section 52Verify source
§ 53Adhabu ya ujumlaOffence

A person who admits an offence in writing may be ordered by the Bank or delegated authority to pay an immediate fine of up to half the normal penalty before a court hearing starts.

53.-(1) Bila ya kujali vifungu vya Sheria hii vinavyohusu adhabu, iwapo mtu anakubali kwa maandishi kwamba ametenda kosa chini ya Sheria hii, Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza, kwa wakati wowote kabla ya kuanza kusikilizwa na mahakama yenye mamlaka, kuamuru mtu huyo kulipa faini ya papo kwa papo ya kiasi cha fedha kisichozidi nusu ya kiasi cha adhabu ambayo mtu huyo angeweza kuadhibiwa kukilipa kama angehukumiwa kwa kosa hilo. (2) Endapo kosa limefililishwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) na shtaka la kosa limeletwa dhidi ya mtuhumiwa kwa kosa hilo hilo, itakuwa ni ushahidi wa kutosha kwa mtuhumiwa kuithibitishia mahakama katika kiwango cha kuridhisha kuwa kosa analoshitakiwa nalo tayari lilishafililishwa chini ya kifungu kidogo cha (1). (3) Endapo mtu yeyote hataridhishwa na uamuzi uliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1), anaweza, ndani ya muda ulioainishwa, kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika Mahakama Kuu na masharti ya vifungu vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai vitatumika kwenye kila rufaa kana kwamba rufaa hiyo ni dhidi ya uamuzi uliyotolewa na Mahakama ya Wilaya katika kutekeleza majukumu yake ya msingi. (4) Endapo mtu ameshindwa kutekeleza uamuzi uliyotolewa chini ya kifungu hiki ndani ya muda uliyowekwa, Benki au Mamlaka Kasimiwa: (a) itamtaka, pamoja na kiasi kilichoamriwa, mtu kiwango riba huyo katika kitakachoainishwa katika kanuni; na kulipa (b) inaweza kutekeleza amri kwa namna ile ile ya mahakama katika kulipa kiasi amri ya kilichoamriwa katika amri hiyo. 33 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha SURA YA TISA MASHARTI YA JUMLA Daftari la watoa huduma ndogo za fedha itaagiza
Section 53Verify source
§ 5455Provision

The Bank or delegated authority must establish and maintain a register of licensed or registered microfinance service providers, and may update it when provider details change.

54.-(1) Benki au Mamlaka Kasimiwa kuanzishwa kwa Rejesta ya kumbukumbu ya watoa huduma ndogo za fedha wote waliopewa leseni au waliosajiliwa kwa mujibu wa Sheria hii. (2) Rejesta hiyo itajumuisha: (a) jina na anwani ya mtoa huduma ndogo za fedha; (b) maelezo ya leseni au usajili ikijumuisha tarehe ya leseni na nambe ya cheti kilichotolewa; na (c) taarifa nyingine kama itakavyoelekezwa na Benki. (3) Benki au Mamlaka Kasimiwa inaweza kufanya marekebisho yanayohusiana na mabadiliko ya maelezo yoyote ya mtoa huduma ndogo za fedha aliyesajiliwa.
Section 54Verify source
§ 5556Provision

Benki must publish the full names and addresses of listed microfinance service providers in the Government Gazette and another widely circulated newspaper, at least every six months or at other intervals it chooses.

55. Benki itapaswa, kwa madhumuni ya uwazi na kuendeleza uelewa kwa umma, kila baada ya miezi sita au katika vipindi ambavyo Benki itaamua, itachapisha katika Gazeti la Serikali na katika gazeti lolote lenye mzunguko mkubwa, majina na anwani kamili za watoa huduma ndogo za fedha- (a) waliopewa leseni au kusajiliwa kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha; (b) ambao leseni au hati zao za usajili zimefutwa; na (c) ambao kwa sababu yoyote ile wameacha kufanya biashara. Utangazaji wa watoa huduma ndogo za fedha Kinga kwa matendo yaliyofanywa au kutekelezwa kwa nia njema Sura ya 16 Sura ya 17
Section 55Verify source
§ 5657. Masharti ya mpitoProvision

Afisa au wakala wa Benki au Mamlaka Kasimiwa hapaswi kuwajibishwa au kushitakiwa kwa tendo au shughuli iliyofanywa katika kutekeleza au kudaiwa kutekeleza majukumu chini ya Sheria hii, bila kuathiri vifungu vilivyotajwa.

56. Bila ya kuathiri masharti ya kifungu cha 284A cha Sheria ya Kanuni za Adhabu na kifungu cha 3 cha Sheria ya Maafisa wa Umma (Urejeshaji wa Mikopo), hakuna tendo au shughuli itakayofanywa na afisa au wakala wa Benki au Mamlaka Kasimiwa katika kutekeleza au kudaiwa kutekeleza majukumu kwa mujibu wa Sheria hii, itamwingiza afisa huyo katika hatua, wajibu au madai yoyote. Masharti ya mpito
Section 56Verify source
§ 57Masharti ya mpitoProvision

Watu waliokuwa wakifanya biashara ya huduma ndogo za fedha kabla ya Sheria kuanza kutumika lazima waombe leseni au usajili ndani ya miezi 12 baada ya kuanza kutumika.

57. Mtu ambaye, kabla ya kuanza kutumika kwa Sheria hii, alikuwa anafanya biashara ya huduma ndogo za 34 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha fedha atawajibika ndani ya miezi kumi na mbili baada ya kuanza kutumika kwa Sheria hii, kuomba leseni au usajili kwa mujibu wa Sheria hii. Ushirikishwaj i wa wazawa
Section 57Verify source
§ 5859Provision

Mtoa huduma ndogo za fedha anayefanya biashara ya huduma hizo lazima azingatie sheria za kutoa kipaumbele kwa wazawa, ikijumuisha ajira na mafunzo kwa Watanzania.

58. Endapo mtoa huduma ndogo za fedha anafanya biashara ya huduma ndogo za fedha, mtoa huduma huyo atawajibika kufuata na kuzingatia sheria zinazotumika katika kutoa kipaumbele kwa wazawa ikijumuisha ajira na mafunzo kwa Watanzania. Dhima kwa matendo ya vikundi vya watu
Section 58Verify source
§ 5960Offence

If an offence is committed under this Act by a group, people involved in managing the group may be treated as having committed the offence if they knew about it, took part in it, or were associated with it.

59. Endapo kosa limetendwa chini ya Sheria hii na kikundi cha watu, ama kimesajiliwa au hakikusajiliwa na kikundi hicho kimetenda kosa kwa kufahamu au kushiriki au kuhusishwa na tendo au kosa lolote kwa upande wa mtu au watu wowote ambao wanahusishwa na usimamizi wa kikundi cha watu hao, mtu au watu hao watachukuliwa kuwa wametenda kosa. Kanuni
Section 59Verify source
§ 6061Provision

Benki inaweza kutengeneza kanuni za jumla za kutekeleza Sheria hii.

60.-(1) Benki inaweza kutengeneza kanuni za jumla kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya Sheria hii. (2) Bila ya kuathiri ujumla wa masharti ya kifungu kutunga kanuni inaweza (1), Benki kidogo cha zinazoainisha- (a) taratibu za maombi na fomu za kuanzisha, kusajili, na kuendesha huduma ndogo za fedha kwa Daraja la 2 na Daraja la 3; (b) matakwa na taratibu za uanzishaji, usajili na uendeshaji wa watoa huduma ndogo za fedha kwa Daraja la 4; (c) mambo ambayo yatasimamia shughuli za watoa huduma ndogo za fedha wa Daraja la 4; (d) masuala ya ukaguzi ikijumuisha uteuzi wa wakaguzi au maafisa waidhiniwa wa mamlaka ya kufanya ukaguzi; (e) ada mbalimbali zinazolipwa chini ya Sheria hii; (f) misingi ya kumlinda mtumiaji ikijumuisha taratibu za utatuzi wa migogoro na utoaji wa elimu ya fedha; (g) namna ambayo elimu ya fedha itatolewa na watoa huduma ndogo za fedha; 35 Tangazo la Serikali Na. 711 (Linaendelea.) Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha (h) malipo yatakayofanywa kuzingatiwa wanaoomba mikopo; na wanachama na masharti ya au wateja (i) masharti na namna ambayo gawio au aina kwa nyingine za faida zitakavyogawanywa wanachama au wateja; (j) uteuzi na sifa za mkaguzi wa ndani au mtu aliyeidhinishwa na mtoa huduma ndogo za fedha; (k) shughuli zinazoruhusiwa na zisizoruhusiwa kufanywa na mtoa huduma ndogo za fedha; (l) uwasilishaji, ukusanyaji na ubadilishanaji wa taarifa ikijumuisha taarifa za mikopo; (m) vigezo na taratibu za kuhama daraja kwa watoa huduma ndogo za fedha; (n) hatua mbalimbali za kiutawala kwa kukiuka masharti ya vifungu vya Sheria hii; (o) masuala yanayohusu biashara ya huduma ndogo za bidhaa zinazofanywa chini ya Sheria hii; (p) taratibu za uombaji wa leseni na masuala yanayohusu wakopeshaji binafsi wa fedha; (q) masharti na namna ya uendesdhaji wa biashara ya huduma ndogo za fedha kimtandao; na linaweza, au lolote ambalo (r) suala linahitaji Kutotumika kwa baadhi ya masharti kwa Daraja la 4 Vifungu vimeondo- lewa kuainishwa na Benki chini ya Sheria hii. (3) Kanuni zitakazotayarishwa chini ya kifungu hiki zitachapishwa katika Gazeti la Serikali.
Section 60Verify source
§ 61Ushirikishwaji wa wazawaProvision

Masharti ya vifungu vya 6(2), 9, 10, 35, 39, 44 na 47 hayatatumika kwa Daraja la 4.

61. Masharti ya vifungu vya 6(2), 9, 10, 35, 39, 44 na 47 hayatatumika kwa Daraja la 4. SURA YA KUMI MAREKEBISHO YATOKANAYO
Section 61Verify source
§ 6268. Vifungu vimeondolewaProvision

Sections 62–68 are removed.

62.-68. Vifungu vimeondolewa. ______________ 36
Section 62Verify source

Legislative relationships

0 referenced instruments

Names are derived from the stored provision headings and citation-enrichment layer. Treat this as a research index and verify each relationship against the source text.

No structured legislative relationships were detected

The statute remains fully searchable by provision. Consult the source text for amendments and cross-references that have not yet been indexed.

Recorded versions and source checkpoint

1 version available in this collection

Current-law checkpoint
  • Undated version · currentSwahili

Source-linked research

Ask AI about this statute

The overview, provisions, and source records above are public. Continue in a separate conversation with this statute’s jurisdiction and source version attached.

About this LexChat collection

Statute information is organised from identified legislative sources for professional research. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.