Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa, 2020
This provision gives the short title of the rules and says they apply to election advertising for political parties.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa, 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the rules and says they apply to election advertising for political parties. Kanuni hizi zimetungwa ili kuwaongoza watoa huduma wote wa maudhui Tanzania Bara. This section defines key terms used in the regulations, including “advertisements,” “Authority,” “online content service,” and related election-broadcasting terms. Every content service provider must ensure election news and related political coverage are fair, accurate, balanced, and free from personal presenter opinions or inflammatory content. Mtoa huduma za maudhui lazima ahakikishe vipindi na uwasilishaji wake vinatii masharti yaliyoorodheshwa kuhusu maudhui ya uchaguzi na tabia ya lugha.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa, 2020
Showing 22 of 22
- 1
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the rules and says they apply to election advertising for political parties.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa, 2020. Matumizi na Mawanda Tafsiri Sura ya.172 Sura ya 172 - 2
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zimetungwa ili kuwaongoza watoa huduma wote wa maudhui Tanzania Bara.
2. Kanuni hizi zitatumiwa na kuwaongoza watoa huduma wote wa maudhui Tanzania Bara. - 3
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the regulations, including “advertisements,” “Authority,” “online content service,” and related election-broadcasting terms.
3. Katika Kanuni hizi isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Sheria” maana yake ni Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania; “matangazo” maana yake ni utangazaji wa habari zozote kwa ajili ya malipo au mtangazaji kupata kitu chochote cha thamani kwa madhumuni ya- (a) kuuza kwa hadhira bidhaa au huduma yoyote; (b) kuishawishi hadhira kuamini au kufanya tendo; au (c) kutangaza bidhaa, huduma, imani, kufanya tendo, mtu au shirika; “maudhui ya matangazo” maana yake ni ujumbe wa malipo unaotokea katika maudhui ya vipindi kwa madhumuni ya kuuza, kutoa taarifa au kushawishi watu kuhusu bidhaa, huduma au imani fulani; “Mamlaka” maana yake ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria; “blogu au tovutiblogu” maana yake ni tovuti inayojumuisha 3 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa uzoefu, mtazamo, maoni ya mwandishi au kikundi cha waandishi ikiwa ni pamoja na habari mpya, matukio, majarida, matangazo na picha, video na miunganiko ya tovuti nyingine; “mmiliki wa blogu” maana yake ni mwandishi au kikundi cha waandishi kinachomiliki na kuendesha blogu na matendo mengine yoyote yanayohusiana na blogu; “huduma za utangazaji” maana yake ni maudhui yanayorushwa hewani kwa njia ya huduma za mawasiliano ya kielektroniki ambayo yanakusudiwa kupokelewa moja kwa moja na umma kwa ujumla; Sura ya 343 “mgombea” ina maana kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Uchaguzi ya Taifa; Sura ya 343 “kampeni” ina maana kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Uchaguzi ya Taifa; Sura ya 172 “Kamati ya Maudhui” maana yake ni Kamati iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 27 cha Sheria; “malalamiko” maana yake ni maelezo yoyote ya kutoridhika na bidhaa au huduma inayotolewa na mtumiaji, mwenendo mbaya katika utoaji huduma na maudhui yasiyokubalika katika maadili ya utangazaji; “huduma za maudhui” maana yake ni huduma zinazotolewa kwa njia ya matamshi au sauti nyingine, matini,au picha zikiwa isipokuwa pale ambapo zinatangazwa kwa njia ya mawasiliano binafsi; tulivu au jongevu “mtoa huduma za maudhui” maana yake ni mtu mwenye leseni ya huduma ya maudhui iliyotolewa na Mamlaka; “mlalamikaji” maana yake ni mtu anayetoa malalamiko kwa Mamlaka dhidi ya maudhui yaliyotangazwa na mtoa huduma za maudhui ambayo yamedhuru maslahi yake; “Mkurugenzi Mkuu” maana yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka; “mawasiliano ya kielektroniki” maana yake ni mawasiliano ya redio au kama ifaavyo, mawasiliano ya habari katika mfumo wa matamshi au sauti nyingine, data, matini, au picha kwa kutumia nishati ya elektromagnetiki elekezi au sielekezi; “uchaguzi” ina maana kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Uchaguzi ya Taifa; “siku ya uchaguzi” ina maana kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Uchaguzi ya Taifa; “wakati wa uchaguzi” maana yake ni kipindi kati ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi chini ya masharti ya sheria husika ya uchaguzi na siku ya mwisho ya kupiga kura; “kipindi cha uchaguzi” maana yake ni kipindi chochote 4 Sura ya 343 Sura ya 343 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa kinachohusiana na uchaguzi wa ofisi ya Rais, Bunge au Mamlaka za mitaa na vipindi vingine kama- (a) kuhimiza au kushawishi au kuonekana kuhimiza au kushawishi wapigakura kupigia kura chama cha siasa au mtu yeyote wakati wa uchaguzi; (b) kusaidia kufanya utetezi kwa mgombea au kwa chama cha siasa; au (c) kuarifu mikutano iliyofanywa au itakayofanywa inayohusiana na uchaguzi; “maoni ya mpigakura mshiriki” maana yake ni tathmini ya mchakato wa kupiga kura kupitia mitazamo au maoni ya wapigakura wakati wakiondoka katika kituo cha kupigia kura; “habari za upotoshaji” maana yake ni habari au picha ambazo zimetengenezwa kuonyesha ni za ukweli lakini si za ukweli; “hotuba za chuki” maana yake ni maelezo yoyote kwa maneno, hotuba, picha, yanayodhalilisha, kukashifu au kushusha hadhi ya mtu au kikundi kwa msingi wa mbari, ukabila, dini au ulemavu; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya utangazaji; “mtandaoni” maana yake ni mazingira ambayo mawasiliano yanapatikana kupitia mtandao ambapo jamii inaweza kupata mtandao ama bila malipo au kwa malipo na ambayo yameanzia au kukusudiwa kutumika Tanzania; “huduma ya maudhui mtandaoni” maana yake ni maudhui yanayotangazwa kwa umma kupitia tovuti za intaneti, programu tumizi za kompyuta, majukwaa, blogu, tovutiblogu, blogu ndogondogo, akaunti ya umma, zana za ujumbe mfupi wa papo hapo, matangazo ya moja kwa moja mtandaoni, mikusanyiko na majukwaa mengine yanayohusiana; “mtoa maudhui mtandaoni” maana yake ni mtu yeyote anayetoa huduma za maudhui mtandaoni; “jukwaa mtandaoni” maana yake ni kituo cha intaneti ambapo watu wanaweza kupata habari, burudani, elimu, dini au taaarifa nyingine kupitia televisheni, redio, mtandao wa kijamii na blogu za mtandaoni; “mawasiliano kwa redio” maana yake ni mawasiliano ya kielektroniki kupitia masafa ya redio; “utangazaji wa uchaguzi wa vyama” maana yake ni vipindi vinavyotolewa kwa vyama vya siasa au wagombea kuwaelezea wapigakura juu ya sera zao. “upigaji simu” maana yake ni vipindi vya redio na televisheni ambapo umma unaruhusiwa kushiriki na kutoa maoni 5 Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa GN NO. 755 Conted kwa njia ya simu; “matangazo ya kisiasa” maana yake ni matangazo ya kulipia yanayokusudiwa kuendeleza maslahi ya chama chochote cha siasa; Sura ya 343 “chama cha siasa” ina maana kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Uchaguzi ya Taifa; “ujumbe wa vyama vya siasa” maana yake ni ujumbe wowote kutoka katika mikutano wa kisiasa, mazungumzo ya kisiasa, mdahalo wa kisiasa na mkutano wa chama na waandishi na la chama katika kampeni za uchaguzi; tamko “kipindi” maana yake ni maudhui mubashara au yaliyorekodiwa yanayojumuisha picha, sauti au yote yanayorushwa kwa madhumuni ya utangazaji kwa umma; “kipindi cha chama cha siasa” maana yake ni matangazo yenye maudhui ya kisiasa yanayowashawishi watu kufanya uamuzi na uteuzi wa kisiasa wanapopiga kura; “arafa” maana yake ni ujumbe mfupi wa maandishi kupitia vifaa vya mawasiliano ikiwemo simu za mkononi. Jukumu la kuripoti SEHEMU YA PILI UTANGAZAJI WA HABARI
Part
SEHEMU YA PILI
- 4
AI-assisted research summary: Every content service provider must ensure election news and related political coverage are fair, accurate, balanced, and free from personal presenter opinions or inflammatory content.
4. Kila mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba - (a) matangazo yote ya habari wakati wa uchaguzi mkuu yanaripotiwa na kutangazwa kwa uadilifu na kutoupendelea upande wowote, kwa usawa na ulinganifu kwa vyama vyote; (b) ushughulikiaji wa matukio ya kila siku, pamoja na masuala ambayo ama yana mabishano miongoni mwa umma au ni suala la mdahalo wa umma, uwe wa haki kwa wahusika wote na kwamba suala linalotangazwa liwasilishwe kwa njia yenye uadilifu na bila kuupendelea upande wowote; (c) taarifa za kisiasa ziwasilishwe bila mtangazaji kuonyesha maoni binafsi; (d) taarifa ya chama cha siasa inayojumuishwa katika utangazaji wa habari iwe ni taarifa ya ukweli yenye mashiko yaani iwe mpya, yenye mvuto na inayostahili kutangazwa katika vyombo vya habari; (e) umbe wa vyama vya siasa unatangazwa kwa ufupi na bila maoni ya mtangazaji; (f) hataruhusu matangazo yoyote ya uchochezi, kashfa na yenye kuleta mgawanyiko katika jamii; (g) Taarifa zinazotolewa kuhusu utaratibu wa uchaguzi na nafasi za wagombea zinapaswa ziwe sahihi, haki 6 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na zenye ulinganifu; (h) utangazaji wa uchaguzi unadhamiria kusisitiza umuhimu wa uchaguzi na kuhimiza ushiriki wa wananchi wote katika mchakato wa uchaguzi; na (i) wakati wa kipindi cha uchaguzi habari zilenge masuala muhimu na maslahi ya wananchi na siyo kutawaliwa na matukio ya vyama vya siasa au wagombea. uwasilishaj i wa vipindi - 5
AI-assisted research summary: Mtoa huduma za maudhui lazima ahakikishe vipindi na uwasilishaji wake vinatii masharti yaliyoorodheshwa kuhusu maudhui ya uchaguzi na tabia ya lugha.
5. Kila mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba vipindi na uwasilishaji wake- (a) unafuata masharti ya Sera, Sheria na Kanuni zinazosimamia uendeshaji wa vyombo vya habari vya kielektroniki; (b) haujihusishi na kumkashifu au kumwaibisha mgombea au mtu mwingine yeyote au kauli yoyote mbaya kuhusu uadilifu wa mtu yeyote; (c) hautoi ushawishi wa kisiasa wala kuegemea misingi ya jinsia, mbari, rangi, dini au mahali pa asili; (d) usiwe na viashirio vya lugha ya kashfa, chuki au kufuru au lugha yoyote inayoweza kuchochea vurugu au uasi; (e) usiwe na kauli zozote zinazoweza kuumiza hisia za mtu yeyote kwa sababu ya jinsia, jinsi, mbari, rangi, tabaka, imani, ulemavu au mahali pa asili; (f) una maudhui ya siasa ambapo vyama vinataka kuelezea sera, vipindi na malengo yao; (g) una maudhui ya siasa ambayo yameainishwa ipasavyo na hayatawasilishwa kwa njia ambayo inapotosha hadhira kuamini kwamba vipindi hivyo ni vya mtazamo mwingine wowote; (h) pale ambapo mtangazaji wa kipindi au mwendesha mjadala anapokutana na wanasiasa wakati akitekeleza majukumu yake ya kitaaluma, kukutana huko kusifikie au kusisababishe kuaminika kwamba yeye ama ni mwanachama au muunga mkono wa chama chochote cha siasa; (i) unafuata maagizo yaliyotolewa katika Sheria ya Uchaguzi; (j) unaepuka hisia yoyote ya kupendelea upande mmoja katika matangazo yote na hayataathiriwa na maslahi ya kisiasa au mengineyo; 7 Sura ya 343 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa Mhojiwa kutambuli wa ipasavyo Vipindi vya kuchangia kwa simu TS.Na.134 la 2018 TS.Na.538 ya 2020 TS.Na.134 la 2018 TS.Na.538 ya 2020 - 6 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: Watoa huduma za maudhui na waendesha mijadala katika vipindi vya kisiasa lazima wahakikishe mahojiano yana ridhaa, yanabaki kwenye mada, na hayaoneshwi kwa njia ya kupotosha au ya kudhalilisha.
6. Pale ambapo mtoa huduma za maudhui anapofanya mahojiano katika kipindi cha kisiasa atahakikisha kwamba- (a) mhojiwa anayetambulishwa kama mwakilishi wa ipasavyo awe ameteuliwa chama siasa kuzungumza kwa niaba ya chama; cha (b) mhojiwa katika kipindi cha siasa hatahojiwa bila ya ridhaa yake; (c) waendesha mijadala katika vipindi kama hivyo wazuie na wahakikishe kwamba wahojiwa wanajikita kwenye mada iliyochaguliwa;vipindi havipotoshi kwa kuwa na lugha ya dhihaka au udhalilishaji; (d) toleo lililohaririwa au kufupishwa la mahojiano haliwasilishwi vibaya au kupotosha maoni na mchango wa mhojiwa; (e) mahojiano yasihaririwe ili yaonekane yanamhusisha mchangiaji na mtazamo fulani ambao hawezi kuufuata na ambao hakupewa nafasi ya kutoa maoni katika kipindi au makala. - 7
AI-assisted research summary: Mtoa huduma za maudhui lazima ahakikishe vipindi vya moja kwa moja vya simu vinakuwa vya haki, sahihi, visivyoegemea upande wowote, na vinaheshimu faragha ya wapiga simu.
7.-(1) Mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba: (a) Kuna ulinganifu wa haki na usawa wa maoni yatolewayo na wachangiaji kwa simu juu ya masuala ya kisiasa kwa kuzingatia misingi ya vipindi mubashara vya kuchangia kwa simu ambayo ni haki, uadilifu, kutopendelea na ulinganifu; (b) anachukua hatua muhimu kuhakikisha kwamba hakuna mpiga simu au mchangiaji anayeshiriki katika vipindi vya kisiasa au vipindi vingine anayekiuka Kanuni za Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazaji wa Redio na Televisheni) za 2018, Kanuni za Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Mtandaoni) za 2020; (c) usiri wa wapiga simu unaheshimiwa na taarifa zao binafsi zinalindwa na namba zao za simu hazitolewi kwa mtu mwingine; (d) wapiga simu wanapitia katika mchakato wa uchunguzi kabla ya kwenda hewani mubashara katika kipindi, ambapo mchakato huo wa uchunguzi pia utajumuisha ucheleweshaji wa sekunde 3 hadi 5 kutoka studio hadi kituo cha kurushia matangazo ili kutoa nafasi ya kuhariri maudhui yoyote mubashara yanayokwenda kinyume na Kanuni za Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazaji wa Redio na Televisheni) za 2018, Kanuni za Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Mtandaoni) za 2020; 8 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa (e) vipindi vyote mubashara vinatangazwa kwa tahadhari na kuhakikisha kwamba taarifa zote ni sahihi na hazipotoshi ukweli; (f) watazamaji, wasikilizaji na wapiga simu wakati wa vipindi vya mubashara wanahudumiwa kwa heshima, uaminifu na haki; simu (g) vipindi vinavyoshirikisha hadhira ambapo hadhira na wapiga havitaruhusiwa wanashiriki kupandikiza taarifa au kutoa kauli zisizothibitishwa ambazo zinaweza kudhoofisha maslahi ya chama husika au mtu yeyote; (h) kuna matumizi stahiki ya arafa zinazotumwa na umma ili kuhakikisha usahihi, uadilifu, kutopendelea na ulinganifu. Mtangazaji atatahadharishwa na kujiandaa kumpinga Umma kushiriki katika midahalo ya kisiasa Mdahalo wa kisiasa Mtoa huduma za maudhui kuhakikisha ulinganifu kwenye midahalo mpiga simu ambaye atasema jambo lenye utata. - 8
AI-assisted research summary: Mtoa huduma za maudhui lazima aweke nafasi kwa umma kushiriki katika midahalo ya kisiasa kuhusu uchaguzi.
8. Mtoa huduma za maudhui atatoa fursa kwa umma kushiriki katika midahalo ya kisiasa inayohusiana na masuala ya uchaguzi na kuhakikisha kwamba, washiriki wa matangazo hayo ni lazima kadri iwezekanavyo wawe wawakilishi wa maoni tofauti na sekta mbalimbali za jamii. - 9
AI-assisted research summary: Mdahalo wa kisiasa lazima uwe na mwendeshaji na idadi sawa ya wawakilishi kutoka kila chama kinachoshiriki; vikao vinaahirishwa au vinaendelea kulingana na uwepo wa vyama.
9.-(1) Mdahalo wa kisiasa utakuwa na mwendeshaji na idadi sawa ya wawakilishi kutoka kwenye kila chama cha siasa kitakachoshiriki kujadili suala au masuala yanayohusiana. (2) Pale ambapo upande mmoja utashindwa kushiriki katika majadiliano au mahojiano yanayohusu vyama viwili, kipindi kitahirishwa mpaka vyama vyote viwili vishiriki vitakapowakilishwa. (3) Iwapo vyama zaidi ya viwili vinahusika, na endapo hakutakuwa na sababu ya msingi ya kutokuwepo kwa mwakilishi wa chama fulani ndani ya saa 24 kabla ya kipindi kuanza, majadiliano au mahojiano hayo yataendelea. - 10 Verify source ↗
11. Mtoa huduma za maudhui kuhakikisha ulinganifu kwenye midahalo
AI-assisted research summary: Mtoa huduma za maudhui lazima ahakikishe usawa, uwazi na uadilifu katika midahalo ya kisiasa; mwendesha mdahalo hapaswi kuonyesha upendeleo, na vyama au wagombea wana haki ya kujibu taarifa zisizo sahihi au zisizo za haki.
10. Ili kupata usawa wa hakika miongoni mwa hadhira, mtoa huduma za maudhui atahikikisha kwamba - (a) kila mgombea atakaribishwa kuwasilisha idadi ya kutosha na iliyo sawa kwa wafuasi, kwa namna kituo cha utangazaji kitakavyoamua; (b) wafuasi wa vyama watakaa kwa kutenganishwa kwa mujibu wa vyama vyao ili kumwezesha mwendesha mdahalo kuwashirikisha bila upendeleo; (c) mwendesha mdahalo, wakati wa kipindi au mwishoni hatatoa muhtasari au maoni ya mwa kipindi 9 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa kuonyesha upande anaounga mkono; (d) anavitendea haki vyama vyote vya siasa au wagombea na kuviwezesha katika hali ya usawa na uwazi; (e) vyama vya siasa au wagombea wana haki ya kujibu iwapo taarifa iliyotangazwa chini ya jukumu la uhariri wa chombo cha utangazaji ina maelezo yasiyo sahihi au ukosoaji usio wa haki kutokana na upotoshwaji wa ukweli; (f) fursa ya kujibu itatolewa ndani ya saa ishirini na nne (24) katika kipindi chenye hadhi na hadhira sawa; (g) hataruhusu washiriki walioalikwa katika midahalo ya kisiasa kukejeli mfumo wa uchaguzi. Mtoa huduma za maudhui mtandaoni - 11 Verify source ↗
Mtoa huduma za maudhui kuhakikisha ulinganifu kwenye midahalo
AI-assisted research summary: Mtu anayeandaa maudhui ya kutumika Tanzania Bara kwa Kiswahili au lugha yenye hadhira kubwa lazima asajiliwe na Mamlaka na ahakikishe taarifa zake ni sahihi, za kweli, na zinazochujwa kabla ya kutumwa au kuchapishwa.
11.-(1)Mtu anayeishi ndani au nje ya Tanzania anayeandaa maudhui yanayokusudiwa kutumika Tanzania Bara kwa kutumia lugha ya Kiswahili au lugha nyingine yoyote ambayo ina hadhira kubwa, atahakikisha kwamba- (a) amesajiliwa na Mamlaka; (b) anafuata masharti husika ya Sera, Sheria na kanuni nyingine; vyote vilivyoungana (c) maelezo na taarifa zinazotolewa katika majukwaa ya mtandaoni ni sahihi, zenye ukweli, na linganifu kwa chama vyama kinachojitegemea katika uchaguzi; jitihada kuhariri majadiliano yanayoelekea kuumiza hisia za mtu yeyote kwa kutumia lugha ya kashfa ambayo inaweza kuchochea vurugu, uasi au uvunjifu wa amani; (d) anafanya na za (e) anachukua tahadhari kuhakikisha usahihi katika kutangaza matokeo yoyote ya uchaguzi au kura za maoni (f) anachukua hatua za lazima kuchuja maelezo na taarifa kabla ya kuzituma au kuzichapa. SEHEMU YA TATU UTANGAZAJI WAKATI WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA KISIASA Kampeni za siasa
Part
SEHEMU YA TATU
- 12 Verify source ↗
Mtangazaji kutumia nafasi yake kuzuia hatari
AI-assisted research summary: Wakati wa kampeni za uchaguzi, mtoa huduma za maudhui lazima aweke uwiano katika vipindi vya siasa, na mwajiriwa wa kituo cha utangazaji aliye mgombea au aliyeajiriwa na mgombea au chama cha siasa lazima achukue likizo au aache kazi wakati wa kipindi cha uchaguzi.
12. Wakati wa kampeni za uchaguzi mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba- (a) ulinganifu katika vipindi vya siasa unafikiwa kwa uwasilishaji ulio sawa wa hoja mbadala, kinzani au yenye maslahi; 10 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa (b) suala la mjadala katika kipindi siasa linapendekezwa liwe la kufanana kati ya chama kimoja na kingine, isipokuwa pale ambapo suala limechaguliwa na vyama husika; cha (c) watu wanaozungumzia maoni mbalimbali ya chama watakuwa wa hadhi zinazolingana na wawe walioteuliwa na vyama vyenyewe; (d) pale ambapo haki ya kujibu inaporidhiwa, chama ambacho hakijaridhika kitapewa muda na fursa sawa ya kujibu katika muundo uleule wa kipindi kilichosababisha malalamiko hayo; (e) pale ambapo haki ya kujibu ya kwanza iliyotolewa inasababisha malalamiko mengine kipindi cha mdahalo au majadiliano kitaandaliwa; (f) vipindi vya uchaguzi wa vyama vya siasa vinaweza kurushwa hewani wakati wa uchaguzi tu; (g) pale ambapo mwajiriwa wa kituo cha utangazaji anakuwa mgombea au anaajiriwa na mgombea wa kisiasa, au chama cha siasa, atatakiwa kuchukua likizo wakati wote wa kipindi cha uchaguzi, au ataacha kazi katika kituo hicho. Idadi ya nafasi katika vipindi iwekwe bayana Kura za maoni zishughuliki we kwa tahadhari - 13 Verify source ↗
Idadi ya nafasi katika vipindi iwekwe bayana
AI-assisted research summary: Watoa huduma za maudhui wanaorusha vipindi vya uchaguzi lazima watenge kila siku nafasi za matangazo ya uchaguzi wakati wote wa kipindi cha matangazo ya uchaguzi.
13. Kila mtoa huduma za maudhui anayerusha hewani vipindi vya uchaguzi atapaswa- (a) kutenga kila siku, wakati wote wa kipindi cha matangazo ya uchaguzi idadi ya nafasi za vipindi kwa ajili ya matangazo ya uchaguzi; (b) kufanya hivyo kwa mujibu wa mpangilio wa vipindi na kwa muda uliobainishwa na Kanuni hizi. - 14 Verify source ↗
Kura za maoni zishughulikiwe kwa tahadhari
AI-assisted research summary: Mtoa huduma za maudhui akiripoti matokeo ya kura za maoni lazima awajulishe umma chanzo, wakala, muda uliotumika, ukubwa wa sampuli na kiwango cha kasoro kinachoweza kujitokeza. Pia, matokeo ya kura za maoni kutoka kwa hadhira hayatachukuliwa kuwa ya kisayansi, na hakuna matokeo ya kura za maoni yatakayotangazwa ndani ya siku 30 kabla ya siku ya kupiga kura.
14.-(1) Kura zote za maoni zitashughulikiwa kwa tahadhari na katika kuripoti matokeo ya kura hizo mtoa huduma za maudhui atauarifu umma chanzo cha kura hizo, wakala, muda uliotumika kuendesha kura hizo, ukubwa wa sampuli na kiwango cha kasoro kinachoweza kujitokeza, inayolingana ichukuliwe wakati wa kushughulikia kura za maoni mara baada ya watu kupiga kura. tahadhari (2) kwa kuzingatia masharti yaliyoanishishwa katika kanuni ndogo ya (1), matokeo ya kura za maoni yanayotokana na arafa kutoka kwa hadhira hayatachukuliwa kama matokeo wakilishi ya kisayansi. (3) Hakuna matokeo ya kura za maoni yatakayotangazwa ndani ya siku thelathini (30) kabla ya siku ya kupiga kura. 11 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa tangazaji siku ya kupiga kura na kipindi cha kusubiri matokeo - 15 Verify source ↗
Utangazaji siku ya kupiga kura na kipindi cha kusubiri matokeo
AI-assisted research summary: Watoa huduma za maudhui na waandishi wa habari lazima waepuke matangazo na taarifa za upendeleo, za kukisia, za kashfa, na baadhi ya taarifa za uchaguzi wakati wa kipindi cha uchaguzi na kabla ya siku ya uchaguzi.
15- (1) Kwa madhumuni ya kuepuka migongano ya kimaslahi, wafanyakazi wa mtoa huduma za maudhui mwenye wadhifa wa kisiasa au kiongozi wa chama cha siasa au anayejishughulisha na kampeni za kisiasa au anayegombea ubunge, hawatoruhusiwa kutangaza au kushiriki katika kutoa uamuzi wa kiuhariri wakati wa kipindi cha uchaguzi. (2) Mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba, katika muda wa saa kumi na mbili kabla ya siku ya uchaguzi, hatatangaza jambo lolote linalohusiana na siasa ambalo linaweza kuvuruga ulinganifu wa kuzingatiwa wakati wote wa kipindi cha matangazo ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni hizi. (3) Mtoa huduma za maudhui hatakiwi kutumia maoni yake binafsi kama sehemu ya taarifa zozote na anatarajiwa kutoa matukio halisi na maelezo ya mashuhuda anaporipoti mara kwa mara mahudhurio katika vituo vya kupigia kura. (4) Mahojiano ya waangalizi yanaweza kutumiwa kwa ajili ya kuweka wazi upigaji wa kura. (5) Waandishi wa habari wanalazimika kutopendelea upande wowote na kuepuka utoaji wa taarifa za kukisia au kubuni. (6) Mtoa huduma za maudhui atahahakisha kwamba hakuna taarifa za kashfa zitakazotangazwa, na mwandishi wa habari lazima awe na uelewa wa sheria za kashfa za maandishi na za matamshi. (7) Mtoa huduma za maudhui hataruhusiwa kuutangazia umma kuanzia siku ya kupiga kura hadi siku ya mwisho ya kupiga kura katika vipindi vyake, mambo yafuatayo: (a) mjadala na uchambuzi wa masuala ya uchaguzi na kura za maoni; (b) matokeo au yanayosemekana kuwa matokeo ya upigaji kura katika jimbo la uchaguzi kabla ya kufungwa kwa vituo vyote vya kupiga kura katika jimbo hilo; (c) matokeo yoyote ya kura za maoni; (d) matangazo yoyote ya kisiasa ya kulipia na vipindi vingine vya kisiasa au vipindi vyovyote vya uchaguzi vilivyotayarishwa na, au kwa niaba ya, mgombea, chama cha siasa au mtu au chombo kingine. (e) matokeo ya kura zilizopita; na (f) maoni ya mpigakura mshiriki. Kutangaza matokeo ya uchaguzi - 16 Verify source ↗
Kutangaza matokeo ya uchaguzi
AI-assisted research summary: Content providers must publish election results as they become available and take special care to ensure the results are accurate. They must not broadcast opinions likely to incite violence or hatred based on race, ethnicity, gender, religion, or political stance.
16.-(1) Mtoa huduma za maudhui atakuwa na wajibu wa kuujulisha umma matokeo ya uchaguzi, kadiri yanavyopatikana: Ikizingatiwa kwamba, uangalizi maalumu ufanyike ili kuhakikisha usahihi wa matokeo yote yanayotangazwa. 12 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa Matangazo ya kisiasa (2) Mtoa huduma za maudhui hatatangaza maoni ambayo yanaweza kuchochea vurugu au kushawishi chuki kwa misingi ya mbari, kabila, jinsia, dini au msimamo wa kisiasa na ambayo yanajenga uchochezi wa kusababisha madhara. - 17 Verify source ↗
Matangazo ya kisiasa
AI-assisted research summary: Mtoa huduma za maudhui lazima itoe fursa sawa kwa vyama vya siasa na wagombea, na ifuate utaratibu wa wazi wa kugawa na kusimamia muda wa kampeni hewani.
17.-(1) Mtoa huduma za maudhui atatakiwa, pale inapostahili, kutoa fursa sawa na ya haki kwa vyama vya siasa na wagombea kutangaza vipindi vya uchaguzi na matangazo ya kisiasa ya kulipia ya vyama vya siasa. (2) Mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba, katika mazingira kama hayo anaandaa utaratibu wa wazi wa kukokotoa ugawaji wa muda wa kuwa hewani, pamoja na kuwa na kiasi cha muda na wakati wa kutangaza utakaotolewa kwa vyama vyote vya siasa au wagombea. (3) Hakuna tangazo lingine zaidi ya tamko la kulipia la kisiasa litakalotangazwa kwa nia ya kutekeleza madhumuni yoyote ya kisiasa. (4) Tamko la kisiasa la kulipiwa litakuwa la ukweli na la kueleweka, na litakuwa na jina la chama kinachohusika, jina la mzungumzaji, wakati na mahali pa tukio na halitaleta mtazamo hasi. (5) Hakuna kaulimbiu, wala miziki au nyimbo za aina yoyote kisiasa zitakazotangazwa kabla na baada ya tamko lolote la kisiasa la kulipiwa. zinazoweza vidokezo kuwa vya na (6) Mtoa huduma za maudhui hatarusha hewani kipindi cha uchaguzi cha chama chochote kabla au baada ya tangazo au tamko la kisiasa lililolipiwa na chama kingine cha siasa au mgombea mwingine. (7) Mtoa huduma za maudhui ataandaa utaratibu kuhusu namna ya kuwasilisha vipindi vya uchaguzi vya vyama na matangazo ya kisiasa ya kulipia, pamoja na maelezo bayana na muda, miundo ya vipindi na viwango vya kiufundi vinavyotakiwa: Ikizingatiwa kwamba, atapaswa kuutangaza utaratibu huo na kuwasilisha nakala kwa Mamlaka. (8) Mtoa huduma za maudhui ataanzisha mifumo na utaratibu wa wazi ili kuhakikisha kwamba matangazo ya kisiasa ya kulipia na vipindi vya uchaguzi vya vyama havihaririwi au kurekebishwa kwa uamuzi wa upande mmoja tu, bila ya ridhaa ya vyama au wagombea, isipokuwa pale ambapo mabadiliko hayo yanawezekana tu kama matangazo hayo au vipindi hivyo havifuati viwango vya uadilifu vya kiufundi, sheria za nchi au kanuni zozote za uchaguzi. (9) Pale ambapo chama cha siasa au mgombea, katika 13 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa Miongozo ya jumla Uuzaji wa muda wa kuwa hewani mazingira kama hayo, anakataa kuhariri au kurekebisha tangazo au kipindi, mtoa huduma za maudhui atakuwa na haki ya kukataa kurusha hewani tangazo au kipindi hicho. SEHEMU YA NNE UGAWAJI WA MUDA WA KUWA HEWANI
Part
SEHEMU YA NNE
- 18 Verify source ↗
Miongozo ya jumla
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinaweka taratibu za kugawa muda wa matangazo ya kisiasa na uchaguzi hewani, pamoja na masharti ya usawa, staha, na utunzaji wa rejesta.
18.-(1) Mwongozo wa jumla kuhusu ugawaji wa muda wa kuwa hewani utatumika katika matangazo yote ya vyama vya siasa kadri iwezekanavyo. (2) Wakati wa uchaguzi matangazo ya vyama vya siasa ratiba ya vipindi yatarushwa hewani kwa mujibu wa iliyoidhinishwa na Mamlaka. (3) Mwakilishi wa chama atazungumza na watazamaji katika mazungumzo yake bila kukatishwa juu ya suala au sera mbalimbali na muda wa mazungumzo hayo usiwe zaidi ya dakika arobaini na tano (45). (4) Muda wa kuwa hewani wa matangazo ya uchaguzi wa vyama utagawiwa na mtoa huduma za maudhui kwa vyama mbalimbali vinavyoshiriki katika uchaguzi kwa misingi ya vigezo vitakavyowekwa. 19 (1) Mtoa huduma za maudhui atakuwa huru kuuza muda wa kuwa hewani kwa madhumuni ya kampeni za kisiasa. (2) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (1), mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba- (a) sauti za wafanyakazi hazitatumika katika matangazo ya kisiasa; (b) matangazo ya kisiasa yatafuata viwango vya stara, staha, maadili na ukweli; (c) vyama vya siasa na wagombea vitapewa kadi yenye viwango sawa vya gharama na masharti pamoja na vipunguzo vinavyotokana na ukubwa wa ununuzi na bonasi ya muda wa matangazo; (d) kila inapowezekana, muda utagawiwa sawa kwa wagombea wote; (e) muda uliogawiwa kwa vyama, kadiri iwezekanavyo, utakuwa wenye thamani na viwango sawa; (f) kituo cha utangazaji kinatakiwa kutunza rejesta inayoonyesha ugawaji wa muda kwa kila chama pamoja na tarehe, jina la kipindi na maelezo mengine kama yanavyoweza kuhitajika; (g) wagombea na vyama vya siasa vitapewa fursa sawa za muda wa kuwa hewani usiolipiwa; 14 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa (h) kiasi cha muda unaogawiwa kwa propaganda za kisiasa na viwango vya malipo ya kutozwa kwa matumizi ya muda huo, vitalingana kwa vyama vyote na wagombea wote; (i) hakuna kipindi au mdhamini atakayeruhusiwa kumpinga waziwazi mgombea yeyote au chama cha siasa. SEHEMU YA TANO MALALAMIKO NA RUFAA Uwasilishaji wa malalamiko
Part
SEHEMU YA TANO
- 20
AI-assisted research summary: Malalamiko lazima yawasilishwe kwa mtoa huduma za maudhui ndani ya saa 48 baada ya suala kurushwa hewani, na mkataaji wa uamuzi anaweza kupeleka malalamiko yake kwa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ndani ya saa 48 baada ya uamuzi huo.
20.-(1) Malalamiko yatapaswa yawasilishwe kwa mtoa huduma za maudhui ndani ya saa arobaini nane (48) baada ya kurushwa hewani suala linalolalamikiwa. (2) Pale ambapo mlalamikaji hajaridhishwa na uamuzi uliotolewa na mtoa huduma za maudhui, atawasilisha malalamiko yake katika Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ndani ya saa arobaini na nane (48) baada ya uamuzi huo. (3) Kamati ya Maudhui itatakiwa, pamoja na mambo ili kuthibitisha hoja za kutetea haki ya kujibu mengine, malalamiko, itazingatia yafuatayo: (a) shtaka dhidi ya uadilifu na faragha; (b) uvunjaji wa kanuni za ulinganifu na haki; au (c) kukataliwa kurushwa hewani kwa matangazo ya siasa. Utaratibu wa kuwasilisha malalamiko - 21
AI-assisted research summary: Malalamiko rasmi kuhusu kipindi cha uchaguzi yanapaswa kuandikwa, yaoneshe taarifa zilizoainishwa, na kuwasilishwa moja kwa moja kwa Mamlaka ndani ya saa 48 baada ya uamuzi wa mtoa huduma wa maudhui.
21. Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine zozote, utaratibu wa kuwasilisha malalamiko kwenye Kamati ya Maudhui utakuwa kama ifuatavyo: (a) kwa maandishi na yaonyeshe: (i) kwamba malalamiko hayo ni rasmi kuhusu kipindi cha uchaguzi; (ii) jina la kipindi; (iii) chama au mgombea aliyehusishwa katika kipindi; (iv) kituo cha redio na televisheni au watoa huduma za maudhui mtandaoni ambao wamehusika kutangaza; (v) tarehe na muda wa tangazo au kipindi; (vi) masharti ya Kanuni hii yanayodaiwa kukiukwa na sababu zake; na (b) kuwasilishwa moja kwa moja kwa Mamlaka ndani ya saa arobaini na nane (48) baada ya uamuzi wa mtoa huduma za maudhui. 15 GN NO. 755 Conted Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa Rufaa Sura ya 172 - 22
AI-assisted research summary: A dissatisfied party or candidate may appeal the Authority’s decision to the Competition Tribunal.
22.-Pale ambapo chama cha siasa au mgombea hajaridhishwa na uamuzi wa Mamlaka, mlalamikaji anaweza kukata Rufaa kwenye Baraza la Ushindani dhidi ya uamuzi wa Mamlaka kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 45 cha Sheria. Kufutwa kwa TS.Na.228 la 2015 - 23 Verify source ↗
Uwasilishaji wa malalamiko
AI-assisted research summary: The 2015 Advertising Services (Content) Regulations for election advertising by political parties are repealed.
23. Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa) za mwaka 2015 zinafutwa. Dar es Salaam ……………., 2020 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania JAMES M. KILABA 16
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa, 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in