Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya Monduli za Mwaka 2020
This provision gives the short title of the by-laws and introduces the interpretation section.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya Monduli za Mwaka 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the by-laws and introduces the interpretation section. This section defines key terms used in the by-law, including appointed officer, food, council, household, wastewater, resident, director, and agent. Wamiliki na wakazi wa nyumba, viwanja au biashara lazima wasafishe mazingira ya karibu na waondoe uchafu kwenye mifereji; wakazi pia lazima washiriki kwenye usafi wa mazingira kila mwisho wa mwezi au siku itakayowekwa na Halmashauri. Wamiliki wa nyumba au maeneo ya biashara lazima waweke taa yenye mwanga nje ya jengo na kuiwasha usiku. Mmiliki wa nyumba, kiwanja au eneo la biashara lazima ahakikishe eneo lake halina maji, taka, au vitu vingine vinavyoweza kuruhusu mazalia ya mbu au wadudu hatari. Mtu yeyote anayekiuka sharti hilo bila sababu za msingi anatenda kosa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya Monduli za Mwaka 2020
Showing 33 of 33
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the by-laws and introduces the interpretation section.
1. Sheria Ndogo hizi itajulikana kama Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya Monduli za Mwaka 2020. Tafsiri - 2 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale itakavyoelekezwa
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including appointed officer, food, council, household, wastewater, resident, director, and agent.
2. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale itakavyoelekezwa vinginevyo; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote atakayeteuliwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa dawa, hii ni pamoja na: - (a) kitu chochote kinachotumika katika matengenezo ya chakula; (b) kitu chochote kinachoongeza ladha ya chakula; au (c) kitu chochote kinachobadili rangi ya chakula; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya 1 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) Monduli; “kaya” maana yake ni familia inayojumuisha baba, mama, mtoto au watoto na mtu mwingine yeyote anayeishi na familia hiyo au watu wanaokaa katika nyumba moja na kuishi kama familia au mtu yeyote anayeishi peke yake katika chumba au nyumba; “maji taka” maana yake ni kinyesi au mkojo na uchafu mwingine kama maji ya kuoga na maji ya kupigia deki, kuosha vyombo, maji yanayotokana na uchafu kutoka vituo vya mafuta, vituo vya kuoshea magari na viwandani ambapo yana kemikali au yasiyokuwa na kemikali na ambayo hayajasafishwa; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote anayeishi katika eneo la Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri au anafanya biashara katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; na “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni, shirika aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. taasisi au - 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Wamiliki na wakazi wa nyumba, viwanja au biashara lazima wasafishe mazingira ya karibu na waondoe uchafu kwenye mifereji; wakazi pia lazima washiriki kwenye usafi wa mazingira kila mwisho wa mwezi au siku itakayowekwa na Halmashauri.
3.- (1) Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira (2) Kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba anafanya usafi wa mazingira yanayozunguka makazi au eneo lake hadi mwanzo wa mipaka ya barabara ya mbele ya nyumba yake. Kila mmiliki wa nyumba, kiwanja au eneo la biashara atakuwa na wajibu wa kuondoa uchafu kama vile mchanga, majani, nyasi au vitu vingine vinavyofanana na hivyo kwenye mifereji ya kupitisha maji 2 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) (3) (4) inayozunguka au kupita kando ya nyumba, kiwanja au eneo la biashara yake. Bila kuathiri masharti ya Kanuni ndogo ya (1), na (2) kila mkazi atakuwa na wajibu wa kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira katika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi au katika siku itakayopangwa na Halmashauri. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Kanuni hii atakuwa ametenda kosa. - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba au maeneo ya biashara lazima waweke taa yenye mwanga nje ya jengo na kuiwasha usiku.
4. (1) Uwekaji taa za nje ya nyumba na upakaji rangi Kila mmiliki wa nyumba au eneo la biashara atakuwa na wajibu wa kuweka taa yenye mwanga nje ya jengo analoishi au analolitumia kwa shughuli za biashara na atatakiwa kuiwasha wakati wa usiku. (2) Mtu yeyote ambaye, bila sababu za msingi atakiuka masharti ya Kanuni ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba, kiwanja au eneo la biashara lazima ahakikishe eneo lake halina maji, taka, au vitu vingine vinavyoweza kuruhusu mazalia ya mbu au wadudu hatari. Mtu yeyote anayekiuka sharti hilo bila sababu za msingi anatenda kosa.
5. (1) Wajibu wa kuondoa na kudhibiti mazalia ya mbu Mmiliki wa nyumba, kiwanja au eneo la biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa katika eneo lake hakuna mkusanyiko wa maji, maji machafu, takataka au kitu chochote cha majimaji au kigumu ambacho kinaweza kuruhusu kuwepo kwa mazalia ya mbu au wadudu wengine wenye madhara kwa afya ya binadamu. (2) Mtu yeyote ambaye bila sababu za msingi, atakiuka masharti ya Kanuni ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Upulizaji dawa - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Anayefanya biashara ya kupulizia dawa za kuua wadudu au wanyama waharibifu katika eneo la Halmashauri lazima awe na cheti kinachotambuliwa na Serikali na leseni hai, asimamie chini ya Afisa Afya wakati wa upuliziaji, na atoee cheti kilichosainiwa baada ya kupulizia.
6. (1) Mtu yeyote anayeendesha biashara ya upuliziaji dawa ya kuuwa wadudu au wanyama waharibifu katika eneo la Halmashauri atatakiwa: (a) kuwa na cheti cha taaluma kinachotambuliwa 3 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) na Serikali na leseni hai kutoka Halmashauri; (b) kusimamiwa na Afisa Afya wakati wa upulizaji; na (c) kutoa cheti baada ya kupuliza dawa kilichosainiwa na Afisa afya. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Kanuni ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Matengene zo na maegesho ya magari, pikipiki na mitambo - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo lazima yafanyike kwenye karakana, gereji au eneo lililoruhusiwa baada ya kupata kibali cha Halmashauri.
7. (1) Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yatatakiwa kufanyika kwenye karakana, gereji au maeneo yaliyoruhusiwa baada ya kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri. (2) Mtu yeyote: (a) hatoruhusiwa kutengeneza gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo halikutengwa kwa shughuli hiyo; au (b) kuegesha gari bovu kwenye njia ya miguu, mtaa, uchochoro, mtaro, maeneo ya wazi au barabarani. (3) Mtu yeyote atakayekiuka, bila sababu za msingi, masharti ya Kanuni ndogo ya (2) atakuwa ametenda kosa. . Utengenez aji, na uuzaji vyakula. - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Watu wanaotengeneza, kupika, kuchemsha, kuchoma, au kuuza chakula ndani ya eneo la Halmashauri lazima wazingatie masharti ya afya na wawe na kibali cha Afisa Afya wa Halmashauri.
8.- (1) Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa: (a) kutimiza masharti na kanuni za afya; na (b) kuwa na kibali kutoka kwa Afisa Afya wa Halmashauri. (2) Mtu yeyote atakayekiuka, bila sababu za msingi, masharti ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. Machinjio na maduka - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: No one may slaughter livestock for commercial purposes outside a slaughterhouse, sell meat outside authorized butcher shops or while uninspected, or transport meat commercially from a slaughterhouse without an approved special meat vehicle.
9. (1) Mtu yeyote hatoruhusiwa: 4 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) ya nyama (a) kwa madhumuni ya kibiashara kuchinja mifugo katika maeneo yasiyokuwa machinjio; (b) kuuza nyama ya aina yoyote katika maeneo yasiyokuwa maduka ya nyama au katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri; (c) kuuza nyama isiyokaguliwa na mtaalamu wa mifugo au mtaalamu wa afya; na (d) kusafirisha nyama kwa madhumuni ya kibiashara toka machinjioni bila kutumia gari nyama la maalumu lililoidhinishwa na Halmashauri. kusafirishia (2) Kila mmiliki wa duka la kuuzia nyama atatakiwa kuhakikisha yafuatayo: (a) duka lake ni jengo la kudumu lililosakafiwa kwa marumaru nyeupe hadi urefu wa futi sita kutoka usawa wa sakafu; (b) duka lake lina maji safi, misumeno ya kukatia nyama na vyuma vya kutundikia nyama; (c) duka lake lina kabati la vioo na jokofu la kuhifadhia nyama na mizani ya kupimia nyama; (d) duka lake lina pipa au kifaa cha kuhifadhia takataka; (e) muuzaji ana vazi jeupe pamoja na aproni nyeupe na kofia nyeupe; (f) muuzaji anapima afya kila baada ya miezi sita; na (g) duka lake lina karo la maji machafu. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Kanuni ndogo ya (1) na (2) atakuwa ametenda kosa. - 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba za kulala wageni, hosteli, shule, vituo vya afya, au nyumba za biashara lazima wakaguliwe na Afisa Afya na wapate kibali cha Halmashauri kabla ya kuanza biashara.
10. (1) Uendeshaji wa biashara ya hoteli na hosteli Kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni, hosteli, shule, kituo cha kutolea huduma za afya au nyumba ya biashara kabla ya kuanza biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha: (a) jengo lake limekaguliwa na Afisa Afya; na (b) amepata kibali cha Halmashauri cha kufanya shughuli husika. 5 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) (2) Kibali cha kuendesha biashara ya nyumba ya kulala wageni, hosteli, shule, kituo cha kutolea huduma za afya au nyumba ya biashara kitatolewa baada ya Halmashauri kujiridhisha kuwa mahitaji yafuatayo yamezingatiwa: - (a) jengo lina mwanga na hewa ya kutosha; (b) jengo lina nafasi na vifaa vya kutosha; (c) uimara wa jengo; (d) jengo lina mfumo imara wa uondoshaji wa maji taka, miminika na taka ngumu; (e) usafi wa jumla wa jengo na vifaa vyake; (f) jengo lina vyoo na mabafu ya kutosha kwa jinsia zote; (g) jengo lina vifaa vya zima moto; (h) tanki la kuhifadhia maji safi; (i) vyoo na bafu vimesakafiwa kwa vigae au marumaru na kuta zake zimewekwa vigae kiasi cha futi sita toka usawa wa sakafu; (j) kwa nyumba za kulala wageni na hosteli, uwepo wa vyandarua. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Kanuni ndogo (4) ya (1) atakuwa ametenda kosa. Bila kuathiri masharti ya Kanuni ndogo ya (3), wakati wowote Halmashauri ikijiridhisha kuwa mmiliki hajakidhi masharti ya afya inaweza kuzuia utoaji wa huduma husika mpaka hapo mmiliki atakapokuwa amekidhi masharti ya kiafya yaliyotolewa na Halmashauri. Ukaguzi wa afya. - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge a health inspection fee before issuing or renewing a business licence.
11. Halmashauri itatoza ada ya ukaguzi wa afya kabla ya kutoa au kuhuisha leseni ya biashara. Eneo la kutupa taka - 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: The Council must set aside a waste disposal area, provide special waste containers, and offer waste collection service for a fee. Anyone who dumps waste or litter in prohibited places commits an offence.
12. (1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa: - (a) kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupia taka; (b) kuweka vyombo maalum vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye 6 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) dampo. (2) Mtu yeyote atakayetupa taka au uchafu wowote au kuacha takataka au uchafu kwenye nyumba, uchochoro, kiwanja, mfereji wa maji ya mvua, barabara au mahali popote pasipotengwa kwa shughuli hiyo atakuwa ametenda kosa. - 13 Verify source ↗
Section 13
AI-assisted research summary: Halmashauri must encourage and recognize community waste-collector groups, and may enable them to carry out solid waste control and environmental cleanliness activities in streets after they contract with the Council.
13. Vikundi vya wazoa taka Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika mitaa baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. - 14 Verify source ↗
Section 14
AI-assisted research summary: Mmiliki wa gari la abiria linaloingia eneo la Halmashauri lazima awe na chombo cha kuhifadhi taka na ahakikishe abiria wanakitumia.
14. (1) Kila mmiliki wa gari la abiria litakaloingia katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhi taka na kuhakikisha kwamba kila abiria anatupa taka kwenye chombo hicho. Magari ya abiria kuwa na vyombo vya kuhifadhia takataka (2) Endapo abiria atatupa takataka nje ya chombo cha usafiri, mmiliki au dereva au kondakta atachukuliwa kuwa ametenda kosa na atawajibika kulipa kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini chini ya utaratibu wa kufifilisha kosa au kushtakiwa mahakamani chini ya Sheria Ndogo hii. Uhifadhi maji taka - 15 Verify source ↗
Section 15
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara lazima wawe na karo la kuhifadhi maji taka, wanyonye maji taka karo likijaa, na wasimwage au kuelekeza maji taka sehemu zisizoruhusiwa.
15. (1) Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara anatakiwa: - (a) kuhakikisha kuwa analo karo la kuhifadhi maji taka; (b) kunyonya maji taka pale karo linapojaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye 7 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote isiyotengwa kuhifadhia maji taka. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Kanuni ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. - 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: The Council must charge monthly waste collection fees, and payers must pay by the 30th of each month to the authorized officer.
16. (1) Ada ya utozaji taka (2) (3) (4) Halmashauri itatoza ada ya uzoaji taka kila mwezi kutoka kwa kila kaya, wamilliki wa nyumba za biashara, taasisi na kampuni zilizopo ndani ya eneo la Halmashauri kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la kwanza la Sheria Ndogo hizi. Ada ya kila mwezi italipwa kila tarehe 30 ya kila mwezi ndani ya mwezi husika na italipwa kwa Afisa Mwidhiniwa ambaye atatoa stakabadhi ya malipo yatakayolipwa na atajaza katika rejista ya wazalishaji taka. Endapo mzalishaji wa taka atashindwa kulipia gharama ya huduma ya uzoaji taka kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo, Halmashauri itamtaka kulipa deni hilo na adhabu ya asilimia hamsini ya ada anayostahili kulipa. Endapo mzalishaji taka atashindwa, bila sababu za msingi, kulipa gharama ya huduma kwa mujibu wa Kanuni ndogo ya (3) atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria Ndogo hizi.
Part
Jedwali la kwanza la Sheria Ndogo hizi.
- 17 Verify source ↗
Section 17
AI-assisted research summary: Wamiliki wa majengo ya makazi au ya biashara lazima wahakikishe jengo lina choo safi, imara na kinachotumika wakati wote.
17. Wajibu wa kuwa na choo na kukitumia Kila mmiliki wa jengo la makazi au la biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba jengo lake lina choo safi, imara na madhubuti na kuhakikisha kuwa kinatumika wakati wote. Vyoo vya umma - 18 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kujenga vyoo vya umma au kumruhusu
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kujenga vyoo vya umma au kuruhusu watu binafsi, vikundi au taasisi kuvisanifu katika maeneo ambayo inaona yanahitajika.
18. Halmashauri inaweza kujenga vyoo vya umma au kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu au taasisi kujenga vyoo vya umma vitakavyotoa huduma kwa malipo katika maeneo 8 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) ambayo Halmashauri itaona kuwa kuna haja ya kufanya hivyo. - 19 Verify source ↗
Section 19
AI-assisted research summary: Watu, vikundi au taasisi zinazoandaa mkusanyiko wa muda katika eneo lisilo na choo cha kudumu lazima zijenge vyoo vya muda kwa idhini na usimamizi wa Halmashauri.
19. (1) Vyoo vya muda katika mkusanyik o Mtu, kikundi au taasisi yenye lengo la kukutanisha watu kwa muda maalum katika eneo ambalo halina choo cha kudumu itatakiwa kujenga vyoo kwa matumizi ya wakati huo kwa idhini na usimamizi wa Halmashauri. (2) Mtu, kikundi au taasisi itakayokiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa imetenda kosa. - 20 Verify source ↗
Section 20
AI-assisted research summary: Ikigundulika nyumba haina choo, choo kimejaa, au hakifai, Afisa Mwidhiniwa atatoa ilani ya siku 30 ya kurekebisha hali hiyo; mwenye nyumba akishindwa kutekeleza masharti ya ilani atakuwa ametenda kosa, na Halmashauri inaweza kuzuia nyumba isitumiwe kwa makazi au biashara hadi itakaporekebishwa.
20. (1) Ilani ya kujenga choo Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika kuwa nyumba yoyote haina choo, choo kilichopo kimejaa au hakifai binadamu, Afisa Mwidhiniwa atatoa ilani ya siku thelathini kwa mmiliki wa nyumba akiainisha masharti ya kurekebisha hali hiyo. kwa matumizi ya (2) Mmiliki wa nyumba atakayeshindwa kutekeleza masharti ya Ilani iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. (3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Halmashauri inaweza kuamuru nyumba au jengo hilo lisitumike kwa shughuli za makazi au biashara hiyo hadi imerekebishwa. itakapokuwa hapo hali - 21 Verify source ↗
Section 21
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa must give a seven-day notice to remove any nuisance found in an inspected area, and the council may stop a house or building from being used until the problem is fixed.
21. (1) Ilani ya kuondoa kero Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote atatoa ilani ya siku saba kwa mmiliki wa nyumba, mpangaji, mtumiaji au mtu yeyote anayehusika akimtaka kuondoa kero hiyo. (2) Halmashauri inaweza kuamuru nyumba au jengo hilo lisitumike kwa makazi au biashara hadi hapo hali itakapokuwa imerekebishwa. 9 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) (3) Mtu yeyote atakayeshindwa kutekeleza masharti ya ilani aliyopewa ndani ya muda ulioainishwa kwenye ilani atakuwa ametenda kosa. Upimaji wa afya 22 (1) Kila mmiliki wa sehemu inayotoa huduma ya hoteli, mgahawa, baa, bucha, sehemu za kuokea mikate, nyumba za kulala wageni, grosari au mtu yeyote anayetengeneza chakula kwa ajili kuuza atatakiwa kuhakikisha kuwa wahudumu wake wanapima afya kila baada ya miezi sita na kulipa ada ya upimaji wa afya kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. (2) Mmiliki yeyote atakayekiuka mashartiya Kanuni ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Uteuzi wa wakala - 23 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kuteua kampuni,kikundi au mtu binafsi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuteua kampuni, kikundi, au mtu binafsi kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria Ndogo hizi. Pia, mtu yeyote akitiwa hatiani kwa kosa chini ya Sheria Ndogo hizi anaweza kupewa faini, kifungo cha miezi 12, au vyote viwili.
23. Mkurugenzi anaweza kuteua kampuni,kikundi au mtu binafsi kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria Ndogo hizi. Adhabu 24 Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hii atahukumiwa adhabu ya faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo cha miezi kumi na mbili au vyote viwili kwa pamoja. Kufililisha kosa - 25 Verify source ↗
Section 25
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii shilingi laki mbili ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalum ya Jedwali la Tatu.
25. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi laki mbili iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiyari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali laTatu la Sheria Ndogo hizi. - 26 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii inafuta Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa
AI-assisted research summary: This section repeals the Monduli District Council Health and Environmental Sanitation By-law, 2019.
26. Sheria Ndogo hii inafuta Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashuri ya Wilaya ya Monduli, 2019 na Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashuri ya Wilaya ya Monduli, 2019 . Kufutwa kwa Tangazo la Serikali Na.840 ya tarehe 8/11/2019 10 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) na Serikali Na.837 ya tarehe 8/11/2019 JEDWALI LA KWANZA (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 16(1)) SEHEMU YA I ADA YA UZOAJI TAKA AINA YA JENGO AU -BIASHARA ADA KWA MWEZI
Part
SEHEMU YA I
- 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: Section 11 lists categories of premises and activities, including household residential use, tea rooms, restaurants, private clinics, private health centers and hospitals, small industries or garages, hotels, and carpenter/workshop/metalworking premises.
11. Eneo la makazi kwa kaya Chumba cha kuuzia chai Mgahawa Wauza barafu Mgahawa mkubwa Nyumba za kulala wageni Zahanati binafsi Vituo vya afya (binafsi) Hospital (binafsi) Viwanda vidogo au garage Hoteli: Vyumba 1-10 Vyumba 11-20 Vyumba 21-30 Vyumba 31-40 Vyumba 41-50 Vyumba 51-60 Vyumba 61-70 Vyumba 71- na zaidi Fundi seremala/karakana/kuchoma vyuma 12 - 13 Verify source ↗
Maduka ya jumla
AI-assisted research summary: The text appears to list fee or charge amounts for general shops, retail shops, and a private primary school, but the rule itself is not clearly stated in this fragment.
13. Maduka ya jumla 14 Duka rejareja 11 2,000/= 2,500/= 3,000/= 2,500/= 5,000/= 10,000/= 5,000/= 7,500/= 10,000/= 5,000/= 20,000/= 40,000= 45,000= 60,000/= 70,000/= 80,000/= 90,000/= 100,000/= 5,000/= 12,000/= 6,000/= Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) Shule ya msingi(binafsi) - 18 Verify source ↗
Section 18
AI-assisted research summary: The text mentions private secondary schools and a local brewer as legally authorized, but it does not clearly state a rule.
18. Shule za Sekondari (binafsi) Local brewer(legal authorized) - 23 Verify source ↗
Duka la dawa
AI-assisted research summary: Section title: Duka la dawa (pharmacy shop).
23. Duka la dawa 24 Maduka makubwa ya dawa(phamarcy) - 43 Verify source ↗
Section 43
AI-assisted research summary: Section 43 lists supermarket categories: small supermarket and large supermarket.
43. Supermarket (ndogo) Supermarket (kubwa) - 46 Verify source ↗
Duka la kubadilisha fedha
AI-assisted research summary: This section is titled “Duka la kubadilisha fedha” and contains a list of monetary figures.
46. Duka la kubadilisha fedha 12 7,500/= 6,500/= 10,000/= 3,000/= 10,000/= 2,500/= 3,000/= 4,500/= 6,000/= 8,000/= 6,000/= 8,000/= 6,000/= 1,000/= 5,000/= 5,000/= 3,500/= 4,500/= 5,000/= 2,500/= 15,000/= 7,500/= 15,000= 10,000/= 5,000/= 7,500/= 15,000/= 10,000/= 10,000/= 75,000/= 5,000/= 7,500/= Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) - 47 Verify source ↗
Ofisi ya watumishi (1-10)
AI-assisted research summary: The section lists office-of-staff categories by size band: 1-10, 11-20, 21-50, and 51 or more.
47. Ofisi ya watumishi (1-10) 0fisi ya watumishi (11-20) Ofisi ya watumishi (21-50) Ofisi ya watumishi (51-na zaidi) - 58 Verify source ↗
Viwanda (taka nyepesi kwa trip)
AI-assisted research summary: The section lists fees for hospitals, based on bed ranges, and includes amounts in shillings.
58. Viwanda (taka nyepesi kwa trip) Hospitali Vitanda (1-10) Vitanda(11-20) Vitanda (21-30) Vitanda (31-40) Vitanda(41-50) Vitanda (51-60 Vitanda (61-70) Vitanda (71-80) Vitanda (81-90) Vitanda (91na zaidi) 2,000/= 3,500/= 4,500/= 7,500/= 10,000/= 1,000/= 5,000/= 3,000/= 10,000/= 2,000/= 8,000/= 4,000/= 5,000/= 5,000/= 20,000/= 10,000/= 12,000/= 20,000/= 30,000/= 40,000/= 50,000/= 60,000/= 70,000/= 90,000/= 100,000/= SEHEMU YA PILI ADA YA UNYONYAJI MAJITAKA Na
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Wahudumu fulani wa chakula na huduma za hoteli wanatakiwa kulipa ada ya upimaji wa afya, kujisajili kwa Halmashauri, na kupimwa afya kila baada ya miezi sita.
4. AINA YA BIASHARA Nyumba ya kuishi Taasisi Viwanda Kukodi gari nje ya Wilaya KIASI KWA SAFARI MOJA (TRIP) 35,000/= 50,000/= 100,000/= 500,000/= kwa siku bila gharama za mafuta JEDWALI LA PILI 13 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 22(1)) ADA YA UPIMAJI AFYA Aina ya Biashara Ada kwa miezi kila mhudumu wa hoteli,mgahawa,baa,bucha,sehemu za 18,000/= kila kuoke mikate,nyumba za kulala wageni,grosari au mtu anapopimwa yeyote anayetengeneza chakula kwa ajili kuuza kupima afya kila baada ya miezi sita na watalipa ada ya upimaji wa afya na kujisajili kwa Halmashauri ili kubainisha usalama wa afya yake kabla ya kutoa huduma kwa wateja kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Afya ya Jamii namba 1 ya mwaka 2009 .Kila mhudumu atapimwa afya yake kila baada ya miezi sita(6) JEDWALI LA TATU (Zimetungwa chini ya kifungu cha 25) HATI KUFILILISHA KOSA Mimi……………………. Nakiri kwa hiari yangu mwenyewe mbele ya …………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli/Afisa mwidhiniwa kwa niaba ya Mkurugenzi, kwamba Tarehe ………Mwezi………. Mwaka………. nilikutwa na kosa la kukiuka masharti ya Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ya Mwaka 2020, nipo tayari kulipa kiasi cha shilingi………………….na kutimiza wajibu wangu chini ya Sheria Ndogo hiyo badala ya kushtakiwa Mahakamani. Nathibitisha kwamba maelezo hapo juu ni kweli na nimeyatoa kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu Leo Tarehe…………………. ya Mwezi………………. Mwaka………………… 14 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) Jina…………………………………………Saini………………………………… Mbele ya: Jina………………………………………... Cheo……………………………………. Saini……………………………………… Tarehe…………………………………… 15 Sheria Ndogo za Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Tangazo Namba 778 (Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio la Mkutano wa Halmashauri ulioitishwa tarehe 24 mwezi juni mwaka 2017 Sheria Ndogo hizi za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli zimebandikwa mbele ya: STEPHEN A. ULAYA .……….……………………… Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Monduli …………………………………….. ISACK J. COPRIANO Mwenyekiti wa Halmshauri Halmashauri ya Wilaya ya Monduli. NAKUBALI Dodoma, 1st September, 2020 ……………………………… SELEMANI S. JAFO (MB) Waziri wa Nchi-0R-TAMISMI 16
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya Monduli za Mwaka 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in