Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za mwaka 2020
Wamiliki na watunzaji wa hoteli/nyumba za kulala wageni ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya lazima wasajili wageni, walipe ushuru wa 10% ya mauzo ya kila chumba, waweke rekodi wazi wakati wa ukaguzi, na watoe huduma fulani za msingi kwa wageni.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za mwaka 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This page preserves the statute’s identified version, provision structure, official source link, and stored legal text for reading and research.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za mwaka 2020
Showing 1 of 1
- document Verify source ↗
Document text
AI-assisted research summary: Wamiliki na watunzaji wa hoteli/nyumba za kulala wageni ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya lazima wasajili wageni, walipe ushuru wa 10% ya mauzo ya kila chumba, waweke rekodi wazi wakati wa ukaguzi, na watoe huduma fulani za msingi kwa wageni.
Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya TANGAZO LA SERIKALI NA. 835 la tarehe 2/10/2020 SHERIA YA FEDHA YA SERIKALI ZA MITAA (SURA YA 290) ___________ SHERIA NDOGO __________ Zimetungwa chini ya kifungu cha 6(1) na 16(1) ___________ SHERIA NDOGO ZA USHURU WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI ZA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA ZA MWAKA 2020 Jina Eneo la kutumika Tafsiri 1 2 3 SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za mwaka 2020. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo; “Afisa mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa umma atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi. “daftari la wageni” maana yake ni kitabu maalumu kilichoandaliwa na Mmiliki au kilicho nunuliwa kwa lengo la kusajiri na kutunza kumbukumbu za Wageni wanaolala kwenye nyumba ya kulala Wageni au Hoteli. “hoteli” maana yake ni nyumba lililojengwa kwa ajiri ya kupokea Wageni au Wasafiri kwa lengo la kujipatia faida na haitajumuisha nyumba yenye vyumba chini ya 6 pia halitajumuisha Mabweni na Nyumba za mapumziko za Serikali; 1 Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya “Mkurugenzi” maana yake” ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya au Afisa yeyote wa umma atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi. “mgeni” maana yake ni mtu yeyote ambaye hulipa pango la kukaa kwenye Chumba cha nyumba ya kulala wageni kwa siku nzima; “mmiliki” maana yake ni mtu yeyote anayemiliki na kuendesha biashara ya hoteli au nyumba ya kulala wageni mtunza Hoteli” maana yake ni mtu yeyote aliyeachiwa jukumu na Mmiliki la kusimamia shughuli za hoteli au nyumba ya kulala wageni za kila siku. “nyumba ya kulala wageni” maana yake ni Jengo lililo jengwa kwa ajili ya wasafiri na wageni kwa lengo la kupata faida ambayo itajumuisha jengo ambalo lina vyumba vya kulala Wageni chini ya 10 au jengo linaweza kutoa huduma ya Vyumba vya kulala. Tafsiri hii haita jumuisha nyumba za mapumziko za serikali; “siku” maana yake kipindi cha masaa ishirini na nne baada ya usiku wa manane na kumalizika usiku wa manane unao fuata; “ushuru wa nyumba ya kulala wageni” maana yake ni kiasi cha fedha kinacho takiwa kulipwa na mmiliki wa Hoteli au nyumba ya kulala wageni kwa Halmashauri; 2 Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya SEHEMU YA PILI UTOZAJI WA USHURU WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI / HOTELI Kiwango cha ushuru 4 Kila mtunza Hoteli au Mmiliki wa Nyumba ya kulala Wageni au Hoteli atalazimika kulipa Ushuru wa Nyumba za kulala Wageni kwa Halmashauri, ushuru ambao utakuwa sawa na asilimia kumi (10%) ya mauzo ya kila Chumba cha kulala wageni. Uwezo wa Afisa mwidhiniwa kukagua 5 (1) (2) (3) (4) (5) SEHEMU YA TATU UKAGUZI KWENYE NYUMBA ZA KULALA WAGENI Afisa Mwidhiniwa atakuwa na wajibu wa;- kukagua nyumba ya kulala wageni au hoteli kwa lengo la kutaka kujua kama wageni wote wameingizwa au wamesajiliwa kwenye daftari la wageni; kukagua kama Mmiliki au mtunza Hoteli ana vitabu halali vya kusajili wageni; kukagua kama nyumba ya kulala wageni ipo katika hali ya usafi takiwa; kukagua kama kwenye nyumba ya wageni kuna mahitaji yote yanayo takiwa kuwepo kwenye nyumba ya kulala wageni; kukagua kama taratibu za kulaza wageni kwenye nyumba ya kulala wageni zinafuatwa. SEHEMU YA NNE MASHARTI YA KULAZA WAGENI KWENYE NYUMBA YA KULALA WAGENI/ HOTELI Masharti ya kutunza hoteli 6 Kila Mmiliki au mtunza hoteli au nyumba ya kulala Wageni atahakikisha yafuatayo yanatekelezwa au yanafanyika:- 3 Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya (a) Kila mgeni anasajiliwa kwenye daftari la kulala wageni kwa kuingiza taarifa zote muhimu bila kujali muda aliokitumia chumba ; (b) Kulipa Ushuru wa Nyumba ya kulala Wageni kwa Halmashauri ndani ya siku 15 baada ya mwezi husika wa mauzo; (c) Kulipa ada ya leseni ya biashara ya nyumba ya kulala wageni ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa Sheria; (d) Kuhakikisha kuwa nyumba ya kulala Wageni inakuwa safi muda wote na masharti mengine ya usafi yanafuatwa. (e) Kuweka wazi vitabu vya kumbukumbu vya wageni na nyaraka zingine wakati wa ukaguzi; na (f) Kuhakikisha kuwa biashara ya nyumba za kulala Wageni inakuwa na leseni itakayowekwa wazi eneo la Biashara na kuzingatia masharti yote kama yalivyo fafanuliwa kwenye Sheria ya leseni na miongozo ya biashara. SEHEMU YA TANO ULINZI WA MALI ZA MGENI NA HUDUMA ZA LAZIMA KWA MGENI Wajibu wa mmiliki 7 Itakuwa ni jukumu la kila Mmiliki wa Nyumba ya kulala Wageni kuhakikisha kuwa: (a) Kunakuwa na ulinzi wa kutosha wa mgeni na mali zake na milango na madirisha imara; (b) Kwenye kila chumba cha kulala mgeni yanatolewa mahitaji yote ya msingi ambayo ni sabuni ya kuogea, mswaki, dawa ya meno, kondomu, maji ya moto, taulo, mashuka na mahitaji mengine mhimu kwa mgeni yanakuwa katika hali ya usafi; na (c) Kutoa stakabadhi kwa mgeni baada ya kupokea malipo. SEHEMU YA SITA ADHABU 4 Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya Adhabu 8 Mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili (200,000/= shilingi milioni moja (1,000,000/=) au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili (12) na kisichozidi miezi ishirini na nne (24) au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo isiyozidi na Kufililisha 9. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote faini isiyopungua shilingi laki mbili (200,000/=) na isiyozidi shilingi laki tano (500,000/=) iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari yake mwenyewe kwa maandishi na kukubali kutekeleza wajibu wake pamoja na kulipa faini anayodaiwa kama ilivyoekelezwa katika Jedwali la Sheria Ndogo hizi. JEDWALI (Limetungwa chini ya Kifungu cha 9) HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi …………………………………………………… ya …………………………………… ambaye ni Mkurugenzi, kwamba, mnamo tarehe ……. ya mwezi ……… mwaka ………… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Kifungu cha ………… cha Sheria Ndogo za (Ushuru wa nyumba za Kulala wageni) za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za mwaka 2020. nakiri mbele Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, kwa hiyari yangu niko tayari kulipa kiasi cha ushuru wa nyumba za Kulala wageni unaodaiwa pamoja na faini. Nathibitisha maelezo hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa kwa hiari yangu na ufahamu wangu. Leo tarehe …… ya mwezi …………… mwaka ………… Jina………………………..………………………… Saini…………… Mbele ya: Jina…………………………………………………. Cheo ……………………………………………….. Saini ……………… 5 Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya Muhuri wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya umebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa azimio la kikao cha Mkuatano wa baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 10/06/2020 na kubandikwa mbele ya; LS NAKUBALI DODOMA 05 Agosti, 2020 SAAD A. MTAMBULE Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya GIBSON J. MWAKALIBULE Mwenyekiti wa Mkutano Halmashauri ya Jiji la Mbeya SELEMANI S. JAFO WN OR-TAMISEMI DODOMA 6
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za mwaka 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in