Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020
This provision names the by-laws and says they apply throughout Mbeya City Council areas.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision names the by-laws and says they apply throughout Mbeya City Council areas. This section defines key terms used in the by-laws, including the authorized officer, conservation area, environmental conservation, permit, factory, council, director, livestock keeper, livestock, forests, and waste. Kila mfugaji lazima afuge idadi ya mifugo kama itakavyoamriwa na Halmashauri, aihifadhi au ailaze mahali pasipotumika kwa makazi ya binadamu, na awe na kadi ya mifugo inayoonyesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo. Mfugaji haruhusiwi kusafirisha, kuhamisha, kuingiza au kufuga mifugo kinyume cha kibali au utaratibu wa Halmashauri; pia lazima ahakikishe mifugo inafungiwa, inahudumiwa, na haiharibu mazingira. Halmashauri inakataza na kudhibiti kilimo, uchimbaji wa mchanga/mawe, na ufyatuaji wa matofali katika maeneo fulani bila vibali au kufuata taratibu.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020
Showing 30 of 30
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: This provision names the by-laws and says they apply throughout Mbeya City Council areas.
2. Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika maeneo yote ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa pale itakapoelekezwa
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-laws, including the authorized officer, conservation area, environmental conservation, permit, factory, council, director, livestock keeper, livestock, forests, and waste.
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa pale itakapoelekezwa vinginevyo; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “eneo la hifadhi” maana yake ni maeneo ya milima, mbuga za wanyama, maeneo ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu na maeneo mengine ambayo yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; “hifadhi ya mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi, mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji vinavyozingatia masharti na maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwidhiniwa chini ya Sheria 1 Sura 191 Sura 191 Sura 323 Sura 191 Sura 323 Sura 191 Sura 191 Sura 191 Sura 191 Sura 191 Sura 191 Sura 191 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ndogo hizi au Sheria nyingine yoyote itakayotamkwa na Halmashauri kuwa ni hifadhi ya mazingira; “kibali cha hifadhi ya Mazingira” maana yake ni kibali kinachotolewa na Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa; “kiwanda” maana yake ni jengo, majengo au eneo ambapo vitu au bidhaa zinatengenezwa au kuzalishwa. “maji” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya usimamizi wa Mazingira; “maji taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya usimamizi wa Mazingira; “mazao ya misitu” maana yake kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Misitu kifungu cha 2; “mazingira” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “Halmashauri “ maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “Mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anayejishughulisha na ufugaji mifugo katika eneo la Halmashauri; “Mifugo” maana yake ni mifugo yoyote inayofugwa na binadamu; “Misitu” maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia 10 ya miti, uoto wa asili au iliyopandwa, au asilimia 50 au zaidi, ya vichaka na miti na miti inayoota upya ambayo itajumuisha aina yote ya misitu 2 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya ya hifadhi ambayo itatangazwa chini ya Sheria ya Misitu na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri; “Taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka za viwandani” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “uchafu hatari” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika kifungu cha 133(5) cha Sheria ya usimamizi wa Mazingira; “uchafuzi wa mazingira” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “udongo”maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “vitu hatari” Maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; SEHEMU YA PILI: UFUGAJI NA HIFADHI YA MAZINGIRA Wajibu wa mfugaji
Part
SEHEMU YA PILI:
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Kila mfugaji lazima afuge idadi ya mifugo kama itakavyoamriwa na Halmashauri, aihifadhi au ailaze mahali pasipotumika kwa makazi ya binadamu, na awe na kadi ya mifugo inayoonyesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo.
4. Chini ya Sheria Ndogo hizi kila mfugaji; (a) atatakiwa kufuga idadi ya mifugo kama itakavyo amriwa na Halmashauri; (b) atahakikisha kuwa anatunza au kulaza mifugo katika nyumba au sehemu ya nyumba ambayo haitumiki kwa makazi ya binadamu; (c) atatakiwa kuwa na kadi ya mifugo itakayo onyesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo. Masharti kwa Mfugaji - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Mfugaji haruhusiwi kusafirisha, kuhamisha, kuingiza au kufuga mifugo kinyume cha kibali au utaratibu wa Halmashauri; pia lazima ahakikishe mifugo inafungiwa, inahudumiwa, na haiharibu mazingira.
5. Ni marufuku kwa mfugaji; (a) Kusafirisha mifugo kwa kuiswaga au kupitisha barabarani; (b) Kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo moja 3 Kudhibiti mifugo inayozurua hovyo Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya hadi lingine bila kibali kutoka Halmashauri; (c) Kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (d) Kufuga mifugo mingi Zaidi ya idadi ya mifugo iliyoainishwa katika kibali kilichotolewa na Halmashauri; na (e) Kuingiza mifugo ndani ya eneo la Halmashauri kwa lengo la kulisha, kunywesha au kufanya biashara bila kibali na bila kufuata utaratibu uliowekwa na Halmashauri. 6 (1) Itakuwa ni wajibu wa kila mfugaji kuhakikisha kwamba:- (a) mifugo yake inafungiwa na kuhudumiwa ndani ya eneo lake; (b) mifugo yake haiharibu mazingira; na (c) mifugo yake haizururi hovyo mitaani. (2) Halmashauri itakamata mifugo au mfugo wowote utakao onekana unazurura hovyo au kulishwa katika maeneo yasiyoruhusiwa katika eneo la Halmashauri (3) Mfugo wowote utakao kamatwa utalipiwa faini kama ilivyoainishwa kwenye jedwali la kwanza la Sheria Ndogo hizi (4) Endapo mwenye mifugo au mfugo hatatokea ndani tangu ya kipindi masaa ishirini na nne (24) kukamatwa kwa mifugo hiyo, Halmashauri itakuwa na uwezo wa kuuza kwa mnada mfugo au mifugo hiyo baada ya kupata idhini ya Mahakama (5) Halmashauri itafanya sensa ya mifugo pindi itakapoona kuna umuhimu wa kufanya hivyo na kutoa elimu juu ya ufugaji bora na endelevu usioharibu mazingira. 4 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya SEHEMU YA TATU: KILIMO NA UHIFADHI WA ARDHI Taratibu za Kilimo Sura ya 113 7(1) Mtu yeyote atakayetaka kufanya shughuli za kilimo katika Halmashauri atatakiwa kuzingatia taratibu za kilimo kwa kuzingatia Kalenda ya Kilimo ya Halmashauri na Sheria ya Ardhi na Sheria nyingine zozote. (2) Itakuwa halali kwa Halmashauri kuingia katika shamba lolote kwa madhumuni ya kufanya ukaguzi na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi 8 Itakuwa ni marufuku kwa mkulima au mtu yeyote; Masharti kwa Mkulima
Part
SEHEMU YA TATU:
- 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Halmashauri inakataza na kudhibiti kilimo, uchimbaji wa mchanga/mawe, na ufyatuaji wa matofali katika maeneo fulani bila vibali au kufuata taratibu.
9. Uchimbaji na Usafirishaj i wa Madini ya Ujenzi, Ufyatuaji na uchomaji wa tofali (a) Kufanya shughuli za kilimo cha mazao marefu ya zaidi ya futi tatu katika eneo lote la Halmashauri bila kibali cha Halmashauri. (b) Kulima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, Mabwawa na maziwa au kufanya jambo lolote litakalo haribu hifadhi ya mazingira bila kuzingatia ushauri wa Afisa Kilimo. (c) Kutumia kinyume ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kilimo kama ilivyopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri. (1) Mtu yeyote anayetaka kufanya shughuli za utafiti au uchimbaji wa mchanga, kokoto, mawe, kifusi, udongo, ufyatuaji na uchomaji wa tofali ndani ya eneo la Halmashauri atatakiwa kufuata taratibu kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010. (2) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga, kokoto, mawe, udongo, kifusi na au kufyatua tofali katika maeneo ndani ya Halmashauri au maeneo yasiyoruhusiwa kama vile maeneo ya makazi ya watu, miteremko, makorongo, maeneo ya hifadhi, kandokando ya mito au ndani ya mto, pembezoni mwa barabara, mabwawa na maeneo ya ardhi oevu isipokuwa kwa kibali maalumu cha Halmashauri. (3) Mtu yeyote anayefanya shughuli za ufyatuaji na 5 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya uchomaji matofali katika eneo la Halmashauri atatakiwa kwenye Halmashauri kama inavyoonesha kwenye Jedwali la pili la Sheria Ndogo hizi. ushuru kulipa ada au Kibali cha kuchoma moto - 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kusafisha shamba kwa kuchoma moto bila kibali cha Halmashauri, na uchomaji wa moto unaruhusiwa tu kati ya saa 12:00 asubuhi na saa 4:00 asubuhi.
10. (1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kusafisha shamba kwa kuchoma moto isipokuwa kwa kibali cha Halmashauri. (2) Kibali kitakachotolewa chini ya Sheria Ndogo hizi kitakuwa cha maandishi na kitaonyesha jina la mwenye kibali, tarehe na eneo analotaka kuchoma moto. (3) Muda unaoruhusiwa kuchoma moto chini ya Sheria Ndogo hizi ni kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi. Uhifadhi wa Ardhi - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: Residents of the area must help restore damaged natural vegetation and environment by planting trees and not damaging the environment.
11. Itakuwa ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili kuwa au mazingira wanalirudisha katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti na kuendelea kutoharibu mazingira ili kuwezesha uoto urudi katika hali yake ya kawaida. yameharibiwa, kuhakikisha Ujenzi Holela - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kujenga nyumba au jengo lolote
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kujenga nyumba au jengo katika eneo ambalo Halmashauri imetangaza kuwa eneo la Hifadhi.
12. Mtu yeyote hataruhusiwa kujenga nyumba au jengo lolote katika eneo ambalo Halmashauri imetangaza kuwa eneo la Hifadhi. SEHEMU YA NNE: HIFADHI YA VYANZO VYA MAJI
Part
SEHEMU YA NNE:
- 13 Verify source ↗
Section 13
AI-assisted research summary: People within the Council must plant non-water-sucking trees as instructed by the authorized officer, and anyone is banned from damaging or using protected water-source areas in certain ways.
13. Wajibu wa Kulinda Vyanzo vya Maji (1) Itakuwa ni wajibu wa kila mtu ndani ya Halmashauri kupanda miti isiyonyonya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Mwidhiniwa. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote; (a) kuishi, kulima, kukata miti, kuchunga kufuga, au kunywesha mifugo, kufyatua tofali au kufanya jambo lolote linaloharibu kwa namna yoyote eneo lililotangazwa kuwa eneo la hifadhi au chanzo cha maji, au mto au kingo ya mto, kisima au bwawa; (b) kumiliki eneo la chanzo cha maji kilichopo 6 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya ndani ya Halmashauri, au (c) kupanda ndani ya mita sitini mmea au sehemu ya mmea uwe wa asili au usio wa asili ambao husababisha kukausha vyanzo vya maji.
Part
sehemu ya mmea uwe wa asili au usio wa
- 14 Verify source ↗
Section 14
AI-assisted research summary: Any person must not direct sewage pipes into rivers, ponds, wells, drains, springs, or any water source used by people, animals, or other living things.
14. Uchafuzi wa vyanzo vya maji Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hizi kwa mtu yeyote kuelekeza mabomba ya maji machafu kwenye mito, mabwawa, visima, mifereji, chemchem au sehemu yoyote ambayo ni chanzo cha maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama au viumbe vingine hai. SEHEMU YA TANO: UHIFADHI WA UOTO WA ASILI NA MISITU
Part
SEHEMU YA TANO:
- 15 Verify source ↗
Section 15
AI-assisted research summary: People living in the Halmashauri must protect natural vegetation and forest reserves; landowners and plot owners must plant or show at least five trees; the Halmashauri and institutions also have tree-planting and reporting duties.
15. Wajibu wa kupanda miti, kuhifadhi na kulinda uoto wa asili na hifadhi ya misitu. (1) Kila mtu anayeishi ndani ya Halmashauri ana wajibu wa kutunza, kulinda na kutoharibu uoto wa asili na hifadhi za misitu. (2) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa ardhi kupanda na kuhifadhi miti isiyopungua mitano (5) kulingana na mazingira ya eneo lake. (3) Mmiliki yeyote wa kiwanja sharti aoneshe kuwa katika ramani yake ya kiwanja kuna miti isiyopungua mitano wakati anaomba kibali cha ujenzi. (4) Halmashauri itapanga siku moja au zaidi kwa kila mwaka kwa ajili ya kupanda miti, na wakazi wote wa Halmashauri watahamasishwa kushiriki katika zoezi hilo. (5) Kila asasi na taasisi zilizomo ndani ya Halmashauri zitahakikisha kwamba: (a) zinapanda na kutunza miti katika maeneo yaliyo chini ya uangalizi wao; (b) zinashiriki vema katika shughuli za kupanda pale mazingira miti watakapotakiwa kufanya hivyo; kuhifadhi na (c) zinashirikiana na Halmashauri katika kukuza weledi, kuhamasisha na kuwezesha wananchi juu ya njia bora za usimamizi na utunzaji wa uoto wa asili, misitu na mazingira; (d) zinatoa taarifa mara moja kwa Halmashauri pale 7 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya inapobainika kuwa kuna uharibifu wowote wa uoto wa asili, misitu na mazingira kwa ujumla katika eneo lolote ndani ya Halmashauri. - 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma moto msitu, uoto wa asili au nyika ndani ya eneo la Halmashauri ya Jiji bila idhini ya Afisa Mwidhiniwa.
16. Kuchoma au kusababish a moto. (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma moto msitu, uoto wa asili au nyika kwa namna yoyote ile ndani ya eneo la Halmashauri ya Jiji bila idhini ya Afisa Mwidhiniwa. jukumu la Afisa Mtendaji wa Kata na au Mwenyekiti wa Mtaa kuhamasisha au kutoa amri kwa wakazi wa eneo hilo kwenda kuzima moto huo. (2) Ni - 17 Verify source ↗
Section 17
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kukata au kuvuna mti, sehemu ya mti au miti ndani ya eneo la Halmashauri bila idhini ya Halmashauri.
17. Kukata mti au miti. Ni marufuku kwa mtu yeyote kukata au kuvuna mti, sehemu ya mti au miti kwa ajili ya matumizi yoyote ndani ya eneo la Halmashauri ya bila idhini ya Halmashauri. SEHEMU YA SITA: TAKA NGUMU NA MIMINIKA
Part
SEHEMU YA SITA:
- 19 Verify source ↗
Section 19
AI-assisted research summary: Section title on solid waste disposal and maintenance of rainwater drainage channels.
19. Utupaji wa taka ngumu Utunzaji wa mifereji ya maji ya mvua - 20 Verify source ↗
Section 20
AI-assisted research summary: Watu ndani ya eneo la Halmashauri lazima wawe na chombo cha takataka chenye mshikio na mfuniko cha angalau lita 20, na watu walio karibu na mifereji ya maji ya mvua lazima wasafishe eneo hilo. Pia, shughuli fulani za uchafuzi zimepigwa marufuku katika maeneo ya makazi bila kibali cha mazingira.
20. Uendeshaji wa viwanda Ni wajibu wa kila Mtu ndani ya eneo la Halmashauri kuwa na chombo chenye mshikio na mfuniko chenye ukubwa usiopungua lita 20 kwa ajili ya kuhifadhia takataka. (1) Mifereji ya maji ya mvua daima inapaswa kuwa safi muda wote kwa madhumuni yaliyoifanya ijengwe na hivyo ni wajibu wa mmiliki, msimamizi, mtumiaji au mpangaji wa eneo lililo karibu na mfereji wa maji ya mvua kufanyia usafi eneo hilo. (2) Itakuwa ni wajibu wa mmiliki, msimamizi, mtumiaji au mpangaji wa eneo lililo karibu na mfereji wa maji ya mvua kufanyia usafi eneo hilo. Itakuwa ni marufuku kuendesha shughuli za karakana, mashine ya kusaga, kuranda mbao, kukamua maji ya matunda, kuchomelea vyuma au kuendesha shughuli yoyote inayozalisha uchafu ambao unaleta athari kwa binadamu na viumbe wengine katika maeneo ya makazi ya watu bila kuwa na kibali cha mazingira Kamati au - 21 Verify source ↗
Section 21
AI-assisted research summary: The council must form environmental committees or groups in each ward and street. These groups, working with the council’s askari mgambo, inspect cleanliness and may issue immediate fines of up to 300,000 shillings for each violation; refusal to pay leads to court prosecution.
21. (1) Halmashauri itaunda kamati au vikundi vya 8 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya vikundi vya Mazingira Utupaji wa maji taka na taka miminika katika eneo zilipozalis hwa. kwenye na Mtaa mazingira itakayojihusisha na usimamizi wa mazingira kwenye kila Kata na Mtaa husika. kila Kata (2) Kamati au vikundi vilivyoundwa katika kifungu kidogo cha 21(1) zitashirikiana na Askari mgambo wa Halmashauri kupita na kukagua usafi wa nyumba kwa nyumba na maeneo yote ya Halmashauri na ikibaini ukiukwaji wa Sheria Ndogo hizi kamati zitakuwa na mamlaka ya kutoza faini za papo kwa papo ya kiasi kisichozidi laki tatu kwa kila kosa, iwapo mkosaji atakataa kuilipa faini atashitakiwa mahakamani. (3) Mapato yatakayo kusanywa katika kifungu kidogo cha (2) cha Sheria Ndogo hizi yatagawanywa kama ifuatavyo; - 22 Verify source ↗
Section 22
AI-assisted research summary: The provision splits the amount into 20% as allowance for the involved askari mgambo, 50% for the Ward or Street Office, and 30% for the Council account.
22. (a) Asilimia 20% itakuwa ni posho ya Askari mgambo waliohusika; (b) Asilimia 50% itabaki kwa matumizi ya Ofisi ya Kata au Mtaa; na (c) Asilimia 30% itaingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri - 23 Verify source ↗
Section 23
AI-assisted research summary: Hii inakataza kumwaga maji taka mahali pasipoidhinishwa na inaweka wajibu wa kuunganisha, kutibu, na kudhibiti maji taka; pia inakataza kuosha au kutengeneza magari kwenye maeneo fulani.
23. Wajibu wa kuunganis ha mfumo wa Maji taka (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kutiririsha maji taka toka nyumbani, kiwandani au sehemu nyingine na kuyaelekeza ardhini, mtoni, barabarani, au kwenye mifereji ya kutiririshia maji ya mvua. (2) Kila mmiliki wa nyumba ya kuishi au eneo la biashara, nyumba ya burudani au kiongozi wa Ofisi ya Taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali atahakikisha kuwa anakuwa na mfumo bora wa kuhifadhi taka miminika ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa anachimba na kujengea mfumo wa kutunzia maji taka au taka miminika au kuunganisha kwenye mfumo wa maji taka. (3) Mtu yoyote au taasisi ambayo haijaunganisha maji taka kwenye mfumo wa maji taka itatakiwa kukodi magari ya kunyonya maji taka na kulipa ushuru kama inavyoonesha kwenye Jedwali la tatu la Sheria ndogo hizi. (1) Kwa maeneo ambayo mfumo wa maji taka umepita 9 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya ni wajibu wa kila mkazi, taasisi au kiwanda kuunganisha maji taka kwenye mtandao wa maji taka. (2) Endapo mtu yeyote, taasisi au kiwanda kabla ya kutiririsha maji taka kwenye mfumo wa maji taka wa umma (public sewer) watatakiwa kuwa na mitambo ya kusafisha na kutakasa maji taka hayo kabla ya kuyatiririsha katika mtandao kwa kuzingatia viwango vilivyokubalika kwa mujibu wa kanuni za ubora wa maji. (3) Itakuwa ni kosa kuhujumu mfumo wa maji taka kwa kuiba, kuvunja au kuharibu kwa namna yoyote ile miundombinu ya mfumo wa maji taka. (1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kutengeneza au kuosha magari, bajaj, pikipiki (bodaboda) katika maeneo ya vituo vya mabasi, barabarani, kando ya mito na maeneo au katika hifadhi mazingira cha Halmashauri. (2) Mtu atakayepewa kibali cha hifadhi ya mazingira 24 Utengenez aji na uoshaji wa vyombo vya moto atatakiwa kuhakikisha mambo yafuatayo: (a) kutumia maji safi ya bomba au kisima; (b) kusakafia eneo lote litakalotumika kwa Udhibiti wa taka hatari mahali zinapozalis hwa Sura 191 shughuli za kuoshea magari; (c) kuwa na mfumo bora wa maji taka ikiwa ni pamoja na mifereji iliyojengewa kupitisha maji taka hadi kwenye shimo sanifu la maji taka au kuunganisha kwenye mfumo wa maji taka; (d) kuwa na mfumo bora wa kutenganisha vilainishi au girisi na maji taka mengine; (e) kuwa na chombo bora cha kuhifadhia taka
Part
sehemu nyingine na
- 25 Verify source ↗
Section 25
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara ambako taka hatari huzalishwa lazima wahakikishe uingizaji hewa wa kutosha, kufunga mitambo inayotoa gesi taka hatari, kufuata viwango vya sheria ya mazingira, kuzuia utupaji wa taka hatari, na kuwa na kutumia choo bora.
25. ngumu; (f) Kuwa na choo bora na kukitumia; Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda, eneo la biashara au eneo au sehemu yoyote ambapo taka hatari huzalishwa anatakiwa kuhakikisha mambo yafuatayo: (a) Kuna kuwa na hewa ya kutosha na mitambo inayotoa gesi taka hatari inafungwa kuzuia uchafuzi 10 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya wa hewa na kuhakikisha vifaa hivyo vinakidhi viwango vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; Kuzuia umwagaji wa taka hatari, kemikali, mafuta n.k - 26 Verify source ↗
Section 26
AI-assisted research summary: Section 26 concerns control of devices that produce loud noise.
26. Udhibiti wa vyombo vitoavyo kelele kubwa - 27 Verify source ↗
Section 27
AI-assisted research summary: Marufuku kumwaga taka hatari, kemikali, mafuta au mchanganyiko wenye mafuta bila kibali maalumu cha Halmashauri; pia baadhi ya shughuli za biashara kwa vipaza sauti zinahitaji kibali na ada.
27. (b) kuhakikisha kuwa taka hatari miminika zinatakaswa kabla ya kupelekwa kwenye mfumo wa maji taka au kuhifadhiwa na Halmashauri; iliyothibitishwa sehemu (c) kuwa na kifaa maalumu cha kuhifadhia taka hatari na kuhakikisha zinatenganishwa na aina nyingine ya taka zisizo hatari kabla ya kutupwa kwa utaratibu atakaopewa na Halmashauri; na (d) kuhakikisha kuwa watu wote wanaohusika na taka hatari kuhifadhi, kutumia au kusafirisha wanavaa vifaa kinga. (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote, taasisi, kampuni au kiwanda kumwaga taka hatari, kemikali, mafuta au mchanganyiko wenye mafuta kwenye eneo lake au eneo lolote la ardhi au maji au sehemu yoyote ya mazingira isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka Halmashauri (2) Mtu yeyote aliyepewa kibali cha kutupa taka hatari, mafuta au mchanganyiko wa mafuta kwenye sehemu yoyote atatakiwa kuhakikisha kuwa anatakasa taka hatari kabla ya kumwaga kwenye eneo lililoruhusiwa. (3) Mbali na adhabu ya jumla inayotolewa chini ya Sheria Ndogo hii mtu atakayetiwa hatiani kwa kosa chini ya kifungu hiki anaweza kuamrishwa na Mahakama: (a) Kulipa gharama za kuondosha takataka pamoja na gharama zozote ambazo Serikali au Wakala wa Serikali wamegharamia katika urejeshwaji wa hali ya mazingira yaliyoharibika kutokana na umwagaji; na (b) Kulipa gharama za walioathiriwa kwa njia ya umwagaji, ukarabati, urejeshaji katika hali ya awali au fidia kama itakavyoamriwa na mahakama. 11 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya SEHEMU YA SABA KELELE NA MITETEMO (1) Itakuwa ni marufuku kupitisha vyombo vya usafiri wa barabara vitoavyo sauti kubwa katika maeneo maalumu na yanayohitaji utulivu ambayo ni hospitali, mashuleni, na Ofisi za Taasisi mbalimbali. (2) Mtu yeyote atakayeendesha shughuli za kibiashara kama vile muziki, mihadhara, minada na matangazo yoyote ya kibiashara kwa kutumia vipaza sauti atatakiwa kupata kibali cha Halmashauri na kulipa ada ya Tsh. 50,000 kwa siku na Tsh.300,000 kwa mwezi. atatakiwa kufanya matangazo (3) Mtu yeyote aliyepewa kibali cha matangazo na au mikutano mikutano hiyo kuanzia saa 12.00 asubuhi hadi saa
Part
SEHEMU YA SABA
- 12 Verify source ↗
00 jioni kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa
AI-assisted research summary: Wamiliki, wasimamizi au wapangaji wa kumbi za starehe lazima wahakikishe kumbi zina kidhibiti sauti (sound proof).
12.00 jioni kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa kwenye kanuni za udhibiti wa kelele na mitetemo za mwaka 2011. (4) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki, msimamizi au mpangaji wa kumbi za starehe kuhakikisha kwamba kumbi la Halmashauri lazima ziwe na kidhibiti sauti (sound proof) zinazojengwa katika eneo zote SEHEMU YA NANE: MAKOSA NA ADHABU Makosa
Part
SEHEMU YA NANE:
- 28 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akifanya vitendo vilivyotajwa, ikiwemo kuingiza au kusafirisha mifugo bila kibali, kutupa taka au kumwaga maji machafu katika maeneo yasiyoruhusiwa, au kuendesha shughuli fulani katika makazi bila kuzingatia taratibu za mipango miji.
28. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo; (a) ataingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (b) atasafirisha mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (c) ataingiza mifugo katika maeneo yasiyoruhusiwa; (d) atafuga mifugo zaidi ya idadi iliyoruhusiwa; (e) atalima mazao marefu ya zaidi ya futi tatu katika maeneo ya Halmashauri 12 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya (f) atakiuka masharti ya kilimo, kuchimba mchanga, kokoto, madini na udongo katika maeneo yasiyoruhusiwa; (g) atakiuka masharti ya kuhifadhi ardhi; (h) ataharibu vyanzo vya maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji; (i) atabainika kuwa ameweka sumu ya aina yoyote kwa inaathiri maisha ya namna yoyote ambayo binadamu na viumbe wengine; (j) atatupa hovyo taka ngumu au laini katika maeneo yoyote yasiyoruhusiwa; (k) ataosha magari katika maeneo yasiyoruhusiwa; (l) atatiririsha maji machafu yanayoleta madhara kwa binadamu na viumbe vingine hai; (m) atafuga mifugo bila kufuata kibali na kanuni bora za ufugaji; (n) kuacha mifugo inazurula hovyo; (o) ataendesha shughuli za kiwanda au viwanda vidogo, karakana, mashine za kusaga na kukoboa nafaka mashine za kuranda mbao katika makazi ya watu bila kuzingatia taratibu za mipango miji. Adhabu - 29 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya Sheria
AI-assisted research summary: A person who acts contrary to these by-laws commits an offence and, if convicted, may be fined up to 300,000 shillings, imprisoned for up to 12 months, or both.
29. Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu (300,000) au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja yaani faini na kifungo. Kufililisha kosa - 30 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote faini isiyozidi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote faini isiyozidi shilingi laki mbili, ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa maandishi kwa hiari na anakubali kutekeleza wajibu wake pamoja na kulipa anayodaiwa kama ilivyoelekezwa.
30. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote faini isiyozidi shilingi laki mbili iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari yake mwenyewe kwa maandishi na kukubali kutekeleza wajibu wake pamoja na kulipa anayodaiwa kama ilivyoelekezwa katika Jedwali na Nne la Sheria Ndogo hizi. faini JEDWALI LA KWANZA (Limetungwa chini ya Kifungu cha 6(3)) 13 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya VIWANGO VYA FAINI KWA MIFUGO ILIYOKAMATWA NA AINA YA MIFUGO IDADI YA MIFUGO ILIYOKAMATWA
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Section 6 lists fines for each impounded animal and a table of fees/taxes for brick-making activities.
6. Ng’ombe Punda/farasi Mbuzi Kondoo Nguruwe Paka/ mbwa Kwa kila Ng’ombe aliyekamatwa Kwa kila Punda aliyekamatwa Kwa kila Mbuzi aliyekamatwa Kwa kila Kondoo aliyekamatwa Kwa kila Nguruwe aliyekamatwa Kwa kila mnyama aliyekamatwa VIWANGO VYA FAINI KWA KILA MFUGO ULIOKAMAT WA VYA ZAMANI VIWANGO VYA FAINI KWA KILA MFUGO ULIOKAMAT WA VYA SASA 30,000/= 50,000/= 20,000/= 40,000/= 20,000/= 30,000/= 20,000/= 30,000/= 20,000/= 20,000/= 20,000/= 30,000/= JEDWALI LA PILI (Chini ya Kifungu cha 9(3)) ADA NA USHURU KWA SHUGHULI ZA UFYATUAJI MATOFALI SHUGHULI ADA/USHURU
Part
JEDWALI LA PILI
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: The text appears to set charges for brick making and firing for ordinary use, with amounts linked to brick quantities.
1. Ufyatuaji na uchomaji matofali kwa matumizi ya kawaida 30,000 kwa tofali zisizozidi 10000 50,000 kwa tofali zisizozidi 14 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya 30000 100,000 kwa tofali zisizozidi 50,000 - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: The text lists a yearly charge of 300,000 for commercial brick making and burning.
2. Ufyatuaji na uchomaji matofali kibiashara 300,000 kwa mwaka JEDWALI LA TATU (Limetungwa chini ya Kifungu cha 22 (3)) GHARAMA ZA KUNYONYA MAJI TAKA KWA KUTUMIA MAGARI YA HALMASHAURI NA.
Part
JEDWALI LA TATU
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaweka mada ya huduma kuhusu kuzibua mtandao wa maji taka majumbani, na kinaonyesha kuwa si katika shughuli binafsi.
1. AINA YA HUDUMA KIWANGO Kuzibua mtandao wa maji taka majumbani (si katika shughuli binafsi) a) b) c) d) - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: The text contains a local environmental by-law schedule and a confession form for a director admitting a violation and agreeing to pay the amount owed and any fine.
2. Uondoaji maji taka shimoni Maeneo ya viwanda Maeneo ya biashara Maeneo ya makazi Taasisi 20,000 15,000 10,000 15,000 Maeneo ya viwanda kwa safari 130,000 (a) a) b) c) d) Maeneo ya biashara kwa safari Maeneo ya makazi kwa safari Taasisi kwa safari Ada za umbali nje ya mipaka ya Jiji kwa kilomita kwenda na kurudi 120,000 100,000 120,000 6,000 15 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya JEDWALI LA NNE (Limetungwa chini ya kifungu cha 30) HATI YA KUKIRI KOSA ………………………………………… Mimi ya ……………………………………… ambaye ni Mkurugenzi, kwamba, mnamo tarehe ……. ya mwezi ……… mwaka ………… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Kifungu cha ………… cha Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za mwaka 2020. mbele nakiri Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, kwa hiyari yangu niko tayari kulipa kiasi ninachodaiwa pamoja na faini. Nathibitisha maelezo hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa kwa hiari yangu na ufahamu wangu. Leo tarehe …… ya mwezi …………… mwaka ………… Jina………………………..………………………… Saini…………… Mbele ya: Jina…………………………………………………. Cheo ……………………………………………….. Saini ……………… Muhuri wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Umebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa azimio la kikao cha Mkuatano wa baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 10/06/2020 na kubandikwa mbele ya; SAAD A. MTAMBULE Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya LS 16 Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya NAKUBALI DODOMA 05 Agosti, 2020 GIBSON J. MWAKALIBULE Mwenyekiti wa Mkutano Halmashauri ya Jiji la Mbeya SELEMANI S. JAFO WN OR-TAMISEMI DODOMA 17
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in