Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020
This section names the by-laws, says they apply in Mbeya City Council area, and defines key terms used in the market-management rules.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section names the by-laws, says they apply in Mbeya City Council area, and defines key terms used in the market-management rules. Halmashauri lazima isimamie na kuendesha masoko, na itekeleze majukumu mengine ya usimamizi wa masoko yaliyoorodheshwa hapa. Halmashauri must appoint a Market Officer to oversee market development activities, and the officer must carry out specified market-management tasks. Halmashauri may also hire an agent to run the market, and that agent must act under the listed conditions. Kamati ya Wadau wa Soko lazima iundwe, iwe na utaratibu maalum wa viongozi na uendeshaji, ikauwasilishe kwa Hlamashauri; kila kikundi cha ushirika kiwe na mwakilishi mmoja, na mikutano ifanyike kila mwezi. Kamati ya Wadau wa Soko lazima itekeleze majukumu yake ya kukagua biashara, kuboresha ustawi, kudumisha nidhamu, kuhakikisha malipo ya ushuru na ada, kukuza biashara, na kuhakikisha usafi wa maeneo ya soko; pia itafanya kazi nyingine itakazoelekezwa na Mkuu wa Masoko.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020
Showing 27 of 27
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: This section names the by-laws, says they apply in Mbeya City Council area, and defines key terms used in the market-management rules.
3. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo Halmashauri ya Jiji la Mbeya. lote la Katika Sheria Ndogo hizi vinginevyo isipokuwa itakapoelezwa “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “dalali” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa za sokoni kwa njia ya mnada kwa niaba ya mwenye bidhaa kwa mujibu wa sheria na taratibu za soko; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya; “kasha” maana yake ni kifaa maalumu cha kubebea au kuhifadhia bidhaa na mazao kama vile matenga, viroba, magunia, karatasi ngumu, masanduku na mbao; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa mujibu Sheria Ndogo hizi; “mfanyabiashara” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa sokoni au gulioni kwa jumla au rejareja; 1 Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya “Mkuu wa Masoko” maana yake ni mtu yeyote aliyeteuliwa au aliyeajiriwa na Halmashauri kusimamia shughuli zote katika soko; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya "mnada” maana yake soko la wazi ambalo mali au vitu mbalimbali vinauzwa kwa ushindani wa bei kwa kauli na kwa kibali maalumu cha Halmashauri; “soko” maana yake ni eneo maalumu la biashara lililotengwa na Halmashauri kwa matumizi ya kuuzia au kununulia bidhaa na ni pamoja na gulio; “Wakala” maana yake ni mtu, kikundi, taasisi au kampuni iliyopewa kazi ya kukusanya mapato ya Halmashauri katika chanzo au vyanzo vya mapato; “wadau wa soko” maana yake ni mfanyabiashara binafsi, vikundi vilivyoandikishwa katika Kamati ya Wadau wa Soko au Gulio na kuwasilishwa kwa Mkuu wa Soko, au vyama vya ushirika vinavyofanya shughuli za biashara katika soko; “ushuru” maana yake ni tozo inayolipwa baada au kabla ya kupata huduma katika soko au gulio; “vikundi” maana yake ni vikundi vya ushirika vya wafanyabiashara au umoja wa vikundi vya wafanyabiashara vilivyosajiliwa au kuandikishwa na kuwasilishwa katika kamati ya Soko au Gulio na kwa Mkuu wa Soko na kutambuliwa na Halmashauri; - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima isimamie na kuendesha masoko, na itekeleze majukumu mengine ya usimamizi wa masoko yaliyoorodheshwa hapa.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa: Wajibu wa Halmasha uri (a) kuanzisha, kusimamia na kuendesha masoko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi; (b) kuendeleza masoko; (c) kusimamia usafi na usalama wa masoko; 2 Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya (d) (e) (f) kusimamia ufikishaji wa huduma za kijamii katika soko; kugawa na kupangisha soko kwa vyumba, meza au vizimba; na kusajili wafanyabiashara wote katika masoko yote ya Halmashauri. Mkuu wa Masoko - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Halmashauri must appoint a Market Officer to oversee market development activities, and the officer must carry out specified market-management tasks. Halmashauri may also hire an agent to run the market, and that agent must act under the listed conditions.
5.- (1) Kutakuwa na Mkuu wa Masoko atakayeteuliwa na Halmashauri kwa ajili ya kusimamia shughuli za uendelezaji wa Masoko pamoja na: (a) kukusanya ushuru na ada mbalimbali; (b) kusimamia usajili wa wadau wa soko kwa kushirikiana na Kamati ya Wadau wa Soko; (c) kuimarisha huduma za ulinzi, maji na umeme katika masoko; (d) kusimamia usafi na uondoshaji wa taka katika soko; (e) kuhakikisha kuwa bidhaa haziuzwi kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kwa shughuli hiyo; (f) kuzuia ujenzi holela katika soko; na (g) kutekeleza majukumu mengine atakayoagizwa na Halmashauri. yeyote (2) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo cha (1), Halmashauri ambaye atawajibika kusimamia uendeshaji wa soko kwa niaba ya Halmashauri. inaweza kuajiri Wakala (3) Wakala atakayeajiriwa chini ya kifungu kidogo cha (2) atasimamia shughuli za uendeshaji wa soko kwa kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika kifungu kidogo cha (1) na masharti ya mkataba wa uwakala kati yake na Halmashauri. Kamati ya Soko - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Kamati ya Wadau wa Soko lazima iundwe, iwe na utaratibu maalum wa viongozi na uendeshaji, ikauwasilishe kwa Hlamashauri; kila kikundi cha ushirika kiwe na mwakilishi mmoja, na mikutano ifanyike kila mwezi.
6.- (1) Kutakuwa na Kamati ya Wadau wa Soko ambayo itaundwa na wadau wa soko kwa mujibu wa Sheria 3 Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ndogo hizi. (2) Kila kikundi cha ushirika katika soko kitakuwa na mwakilishi mmoja katika Kamati ya Wadau wa Soko. (3) Kamati ya Wadau wa Soko itatakiwa kuweka utaratibu maalum wa kuwapata viongozi wake, kuwaondoa madarakani na uendeshaji wa shughuli zake na kuuwasilisha kwa Hlamashauri. (4) Vikao vya Kamati ya Wadau wa Soko vitafanyika mara moja kila mwezi. (5) Mkuu wa Masoko atakuwa Katibu katika vikao vyote vya Kamati ya Wadau wa Soko. Majukumu ya Kamati - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Kamati ya Wadau wa Soko lazima itekeleze majukumu yake ya kukagua biashara, kuboresha ustawi, kudumisha nidhamu, kuhakikisha malipo ya ushuru na ada, kukuza biashara, na kuhakikisha usafi wa maeneo ya soko; pia itafanya kazi nyingine itakazoelekezwa na Mkuu wa Masoko.
7. Kamati ya Wadau wa Soko itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuhakiki biashara zinazoendeshwa katika soko; (b) kuboresha ustawi wa wadau wa soko; (c) (d) kuhakikisha uwepo wa nidhamu katika shughuli za soko; kuhakikisha wadau wote wa soko na gulio wanalipa ushuru na ada kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi; (e) kukuza na kuendeleza mfumo wa biashara; (f) (g) kuhakikisha kila eneo la mdau na soko kwa ujumla linakuwa safi muda wote; na kutekeleza kazi nyingine watakazoelekezwa na Mkuu wa Masoko kulingana na Sheria Ndogo hizi. Kamati Ndogo - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Kamati ya Wadau wa Soko lazima iunde kamati ndogo zenye wajumbe wanne kutoka miongoni mwa wajumbe wake, na inaweza pia kuunda kamati ndogo nyingine inapoona inafaa.
8.- (1) Kamati ya Wadau wa Soko itaunda Kamati Ndogo zenye wajumbe wanne kutoka miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Wadau wa Soko ambazo ni: (a) Kamati Ndogo ya Miundombinu na Usafi; (b) Kamati Ndogo ya Utawala na Biashara; na (c) Kamati Ndogo ya Ulinzi na Usalama. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), 4 Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya Kamati ya Wadau wa Soko inaweza kuunda Kamati Ndogo yoyote kwa kadri itakavyoona inafaa. Usajili wa wadau - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Anyone who wants to trade in a market must be registered, then receive a market trading permit from the Market Commissioner, and pay the fee before the permit is issued.
9.- (1) Mtu yeyote anayetaka kufanya biashara katika eneo la soko atatakiwa kusajiliwa na Mkuu wa Masoko akishirikiana na Kamati ya Wadau wa Soko kwa lengo la kumtambua na kumworodhesha katika rejesta ya wadau wa soko. (2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1), kila mfanyabiashara atakayesajiliwa atapewa kibali cha kufanya biashara katika soko husika kutoka kwa Mkuu wa Masoko kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi. (3) Kibali kitatolewa kwa mfanyabiashara baada ya kulipa ada na kitadumu kwa muda wa mwaka mmoja tangu siku ya kutolewa na endapo atataka kuendelea na biashara katika soko atatakiwa kuomba kibali kingine kwa Mkuu wa Masoko. kibali Utolewaji wa kwa biashara ambazo hazikuwepo
Part
Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi.
- 10 Verify source ↗
Mtu au mfanyabiashara yeyote ambaye anataka kufanya
AI-assisted research summary: Mtu au mfanyabiashara anayetarajia biashara mpya au isiyo na eneo sokoni lazima aombe kibali kwa Halmashauri.
10. Mtu au mfanyabiashara yeyote ambaye anataka kufanya biashara ambayo awali haikuwepo au haikuwa na eneo ndani ya soko ataomba kibali kwa Halmashauri na masharti ya kifungu cha 9 yatatumika. Kufuta kibali - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: Mkuu wa Masoko anaweza kufuta kibali kwa notisi ya siku 30 ikiwa mwenye kibali ana mojawapo ya sababu zilizoorodheshwa; mfanyabiashara anaweza kupinga ndani ya siku 14, na Mkurugenzi lazima aamue ndani ya siku 7.
11. - (1) Mkuu wa Masoko anaweza kufuta kibali kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hizi, baada ya kutoa notisi ya siku thelathini, endapo mwenye kibali hicho: (a) atakuwa na malimbikizo ya ada au ushuru; (b) atakuwa amesimamisha shughuli zake kwa miezi mitatu bila taarifa; (c) atakuwa na mwenendo unaokiuka masharti ya Sheria Ndogo hizi; (d) atawashawishi wengine kutofuata Sheria Ndogo hizi au kusababisha wafanyabiashara 5 Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya uvunjaji wa amani; au (e) atatumia chumba, kibanda, meza au kizimba alichopanga kinyume na madhumuni ya kufanyia biashara kama yalivyoainishwa kwenye mkataba wa upangishaji au maelekezo yatakayotolewa na Halmashauri. (2) Mfanyabiashara ambaye hatoridhika na uamuzi wa kufutiwa kibali anaweza kuwasilisha pingamizi lake kwa Mkurugenzi katika kipindi cha siku kumi na nne tangu tarehe ya kufutiwa kibali. (3) Baada ya kupokea pingamizi, Mkurugenzi atatakiwa kutoa uamuzi wa pingamizi ndani ya siku saba tangu tarehe ya kupokea pingamizi husika. (4) Mkurugenzi asipotoa uamuzi ndani ya siku saba, itachukuliwa kuwa pingamizi hilo limeshinda na mfanyabiashara huyo ataendelea na biashara yake kama kawaida. Wajibu wa mfanyabis hara - 12 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara katika eneo la soko atakuwa na wajibu
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wote wa soko lazima wajisajili, wahifadhi miundombinu ya soko, wafanye biashara kwenye maeneo yanayoruhusiwa, waweke usafi, walipe ushuru na ada kwa wakati, na wazingatie masharti na maelekezo ya mamlaka za soko.
12. Kila mfanyabiashara katika eneo la soko atakuwa na wajibu wa (a) kusajiliwa na Mkuu wa Masoko katika rejesta ya wadau wa soko; (b) kulinda na kuhifadhi miundombinu ya soko; (c) kufanya biashara katika maeneo yanayoruhusiwa; (d) kufanya usafi katika eneo lake la biashara; (e) kulipa ushuru na ada kwa wakati; (f) kutobandika au kutobandua tangazo bila idhini ya Mkuu wa Masoko; (g) kushiriki usafi wa jumla wa soko; (h) (i) (j) kutoweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la soko; kutofanya shughuli za kisiasa katika eneo la soko; kutotupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; 6 Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya (k) kutowasha moto ndani ya soko; na (l) kuheshimu masharti ya upangaji aliyopewa na Halmashauri na Halmashauri, Mkuu wa Masoko na Kamati ya Wadau wa Soko. na maelekezo atakayopewa Muda wa biashara - 13 Verify source ↗
Section 13
AI-assisted research summary: The market must stay open every day from 12:00 a.m. to 12:00 p.m. The Head of Market may close it for maintenance or an emergency after consulting the Director, but maintenance closure needs seven days’ notice to market stakeholders unless another emergency applies.
13. - (1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. (2) Mkuu wa Masoko, kwa kushauriana na Mkurugenzi, anaweza kufunga soko kwa ajili ya matengenezo au pale yoyote sababu itakapoonekana inafaa. nyingine dharura ya (3) Isipokuwa kwa sababu nyingine za dharura, Mkuu wa Soko hatakuwa na mamlaka ya kufunga soko kwa sababu za matengenezo isipokuwa tu baada ya kutoa notisi ya siku saba kwa wadau wa soko kuhusu kusudio la kufunga soko kwa ajili ya matengenezo. ya Ada pango - 14 Verify source ↗
Section 14
AI-assisted research summary: Halmashauri inaingia mikataba ya ada ya pango na wafanyabiashara wa soko, na mfanyabiashara aliyesajiliwa katika eneo la soko lazima alipe ada kwa mujibu wa mkataba wake. Halmashauri pia inaweza, kwa makubaliano maalum, kumruhusu mtu yeyote kujenga banda la biashara katika eneo la soko.
14. - (1) Halmashauri itaingia mikataba ya ada ya pango na wafanyabiashara katika soko ambapo mfanyabiashara yeyote aliyesajiliwa kufanya biashara katika eneo la soko atawajibika kulipa ada kwa mujibu wa mkataba wake. (2) Halmashauri inaweza, kwa makubaliano maalum, kumruhusu mtu yeyote kujenga banda la biashara katika eneo la soko. Kibali cha minada - 15 Verify source ↗
Section 15
AI-assisted research summary: Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine inaweza kufanyika katika masoko tu kwa kibali maalum cha Halmashauri.
15. - (1) Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine itaruhusiwa kufanyika kwenye masoko kwa kibali maalum cha Halmashauri. (2) Halmashauri inaweza kutoa kibali maalum cha kufanyika minada katika maeneo yatakayotengwa na Halmashauri. 7 Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya Usafi wa soko - 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wa soko lazima waweke maeneo yao safi wakati wote na wazingatie kanuni za afya. Mkuu wa Masoko na Kamati ya Wadau wa Soko husimamia usafi wa jumla wa soko mwishoni mwa kila mwezi.
16. - (1) Kila mfanyabiashara anayefanya biashara katika eneo la soko atawajibika kuweka eneo lake katika hali ya usafi wakati wote. (2) Mkuu wa Masoko kwa kushirikiana na Kamati ya Wadau wa Soko atasimamia usafi wa jumla wa soko siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi. (3) Kila mfanyabiashara atatakiwa kuzingatia kanuni za afya. Huduma ndani soko ya - 17 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara katika soko atatakiwa kugharamia
AI-assisted research summary: Kila mfanyabiashara sokoni anatakiwa kulipia huduma za ulinzi, usafi, maji na umeme kulingana na matumizi yake ya kila mwezi.
17. Kila mfanyabiashara katika soko atatakiwa kugharamia huduma ya ulinzi, usafi, maji na umeme kulingana na matumizi yake ya kila mwezi. Uingizaji wa bidhaa - 18 Verify source ↗
Section 18
AI-assisted research summary: Bidhaa zinazoingizwa sokoni zinapaswa kuwa kwenye makasha maalumu ya kusafirishia, na ni marufuku kwa mkulima, mfanyabiashara, dalali au mtu mwingine yeyote kuingiza sokoni bidhaa zilizofungwa kwa majani au zilizo haribika.
18. - (1) Bidhaa zote zitakazoingizwa katika soko zitatakiwa ya kwenye makasha maalumu kuhifadhiwa kusafirishia bidhaa. (2) Ni marufuku kwa mkulima, mfanyabiashara, dalali au mtu mwingine yeyote kuingiza sokoni bidhaa zilizofungwa kwa majani au bidhaa zilizoharibika. Mifugo kutoingiz wa sokoni - 19 Verify source ↗
Mtu yeyote hatoruhusiwa kuingiza mifugo katika eneo la
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuingiza mifugo katika eneo la soko, isipokuwa ndege na wanyama wadogo kama sungura wanaoletwa kwa ajili ya kuuzwa.
19. Mtu yeyote hatoruhusiwa kuingiza mifugo katika eneo la soko isipokuwa mifugo ya jamii ya ndege na wanyama wadogo kama sungura watakaoletwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa. Tahadhari ya moto - 20 Verify source ↗
Mtu yeyote hatoruhusiwa kufanya
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kufanya shughuli zinazohusisha matumizi ya moto bila idhini ya maandishi ya Halmashauri.
20. Mtu yeyote hatoruhusiwa kufanya shughuli yoyote inayohusisha matumizi ya moto isipokuwa kwa idhini ya maandishi ya Halmashauri. Makosa na adhabu - 21 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka au kwenda kinyume na kifungu
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayekiuka au kwenda kinyume na kifungu chochote cha Sheria Ndogo hizi anafanya kosa na, akipatikana na hatia, anaweza kutozwa faini ya hadi Shilingi laki tatu, kifungo cha hadi miezi 12, au vyote pamoja.
21. Mtu yeyote atakayekiuka au kwenda kinyume na kifungu chochote cha Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi Shilingi laki tatu au kutumikia kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote faini na kifungo kwa pamoja. 8 Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya Kufililisha kosa - 22 Verify source ↗
Bila kujali masharti ya kifungu cha 21, Mkurugenzi anaweza
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote shilingi laki mbili ikiwa mtu huyo anakiri kosa kwa kujaza fomu ya Jedwali la Tatu na kulipa kiasi hicho; ikiwa kosa linahusu ushuru au ada, kiasi hicho hulipwa pamoja na ushuru au ada inayodaiwa.
22. Bila kujali masharti ya kifungu cha 21, Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote kiasi cha shilingi laki mbili endapo mtu huyo atakiri kosa kwa kujaza fomu iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Kanuni hizi na kulipa kiasi hicho pamoja na ada au ushuru anaodaiwa iwapo kosa linahusisha kudaiwa ushuru au ada.
Part
Jedwali la Tatu la Kanuni hizi na kulipa kiasi hicho pamoja
- 23 Verify source ↗
Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko za Halmashauri ya Jiji
AI-assisted research summary: The market by-laws for Mbeya City Council, 2011 have been repealed.
23. Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya, 2011 zimefutwa. Kufutwa kwa tangazo la Serikali Na. 375 la mwaka 2011 JEDWALI LA KWANZA (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 9 (2)) KIBALI CHA KUTUMIA SOKO
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Jina la Mwombaji ………………………………………………
AI-assisted research summary: This section is labeled for the applicant’s name.
1. Jina la Mwombaji ……………………………………………….. - 4 Verify source ↗
Eneo ambalo kibali hicho kitatumika …………………………
AI-assisted research summary: This section states the area where the permit applies.
4. Eneo ambalo kibali hicho kitatumika ………………………….. - 5 Verify source ↗
Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe………hadi tarehe……………
AI-assisted research summary: Muda wa kibali ni kuanzia tarehe fulani hadi tarehe fulani.
5. Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe………hadi tarehe…………… - 6 Verify source ↗
Masharti ya kutumia kibali hicho………………………………
AI-assisted research summary: This section sets out conditions for using the permit, but the listed conditions are blank in the source text.
6. Masharti ya kutumia kibali hicho……………………………….. a) ……………………………………………… b) ……………………………………………… c) ……………………………………………… d) ……………………………………………… e) ……………………………………………… - 7 Verify source ↗
Tarehe ya kikao kilichoidhinisha kibali………………………………
AI-assisted research summary: This provision is a heading for the date of the meeting that approved the permit.
7. Tarehe ya kikao kilichoidhinisha kibali……………………………….. Muhtasari Na.…………… - 8 Verify source ↗
Imesajiliwa na
AI-assisted research summary: This section contains a form for admitting an offence and agreeing to pay shilingi 200,000 instead of being taken to court, if the Director exercises the relevant powers.
8. Imesajiliwa na: 9 Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya Jina ……………………………………… Saini…………………………………….. Mkuu wa Soko Saini ya Mwombaji Tarehe ………………………. Tarehe ………………………….. Mhuri………………………… JEDWALI LA PILI (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 22) HATI YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA la Mimi …………………… wa S.L.P. ………. nakiri kutenda kosa ikiwa ni kinyume na kifungu cha …………………………………….. ……………… cha Sheria ya Ndogo za (Usimamizi wa Masoko) za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020. Kwa hiari yangu mwenyewe pasipo kushawishiwa na mtu yeyote nakubali kulipa kiasi cha shilingi laki mbili badala ya kushtakiwa Mahakamani iwapo Mkurugenzi atatekeleza madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha………………………………. cha Sheria Ndogo hizi. Saini: ………………………………………………... Tarehe …………………………………………………… Mbele yangu:- Jina: …………………………………………….….. Saini: …………………………………………….….. Wadhifa: ………………………………………………... Tarehe …………………………………………………… 10 Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya Muhuri wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Umebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa azimio la kikao cha Mkuatano wa baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 10/06/2020 na kubandikwa mbele ya; LS NAKUBALI DODOMA 05 Agosti, 2020 SAAD A. MTAMBULE Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya GIBSON J. MWAKALIBULE Mwenyekiti wa Mkutano Halmashauri ya Jiji la Mbeya SELEMANI S. JAFO WN OR-TAMISEMI DODOMA 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za Usimamizi wa Masoko za Halmashauri ya Jiji la Mbeya za Mwaka 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in