Sheria Ndogo za (Anwani ya Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa za mwaka 2020
This section states the name of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za (Anwani ya Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa za mwaka 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the name of the by-law. These by-laws apply throughout the area under the Ludewa District Council authority. Halmashauri lazima itenge maeneo ya mitaa au barabara, iweke na ihifadhi/ibadilishe majina ya mitaa, sehemu na barabara, na iweke na ikague nambari za nyumba, barabara na mitaa inapohitajika. Halmashauri lazima iunde Kamati ya Wataalam ndani ya miezi sita, na kamati hiyo isimamie alama za majina ya barabara na nambari za nyumba pamoja na utekelezaji wa mwongozo wa anwani. Kamati ya Wataalam lazima itoe notisi za ukiukwaji, itunze kumbukumbu za anwani na ramani, ikabidhi kumbukumbu hizo kwa mamlaka husika inapohitajika, ipendekeze mabadiliko ya anwani, na ifanye kazi nyingine zinazoelekezwa na Halmashauri.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za (Anwani ya Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa za mwaka 2020
Showing 11 of 11
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za
AI-assisted research summary: This section states the name of the by-law.
1. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Anwani ya Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa za mwaka 2020. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi itatumika katika eneo lote lililo chini ya
AI-assisted research summary: These by-laws apply throughout the area under the Ludewa District Council authority.
2. Sheria Ndogo hizi itatumika katika eneo lote lililo chini ya Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge maeneo ya mitaa au barabara, iweke na ihifadhi/ibadilishe majina ya mitaa, sehemu na barabara, na iweke na ikague nambari za nyumba, barabara na mitaa inapohitajika.
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa na kuidhinishwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “anwani” maana yake ni mbinu ya msingi ya kutambua kitu kwa mahali kilipo; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa; “hadhi ya barabara au mtaa” maana yake ni umuhimu au hadhi katika mtandao wa barabara kulingana na ukubwa wa matumizi; “barabara” maana yake ni pamoja na barabara kuu, barabra ya kawaida, njia, barabara funge, kichochoro, mzunguko na njia 1 Sheria Ndogo za (Anwani za Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa TANGAZO NAMBA 842 (Linaendelea) za miguu ambazo hutumika kutoa anwani za makazi; “hifadhi-data za anwani” maana yake ni mkusanyiko wa taarifa za anwani uliohifadhiwa kwa mpango maalum kwenye kompyuta na ambao unaweza kupatikana kwa watumiaji walioidhinishwa; “Kamati ya wataalam” maana yake ni kamati ya utoaji wa majina ya barabara na nambari za nyumba katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa; Sura 288 “Kata” maana yake ni sehemu ya mgawanyo wa Wilaya iliyo chini ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa; “Kijiji” maana yake ni Kijiji kilichosajiliwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya); “kitengo cha usimamizi wa anwani” maana yake ni kitengo kilichopo Posta Tanzania Shirika kinachoshughulikia utunzaji wa taarifa za anwani; chini ya la “Kitongoji” maana yake ni sehemu ya Kijiji na inayojumuisha sehemu au eneo la mji lililopo katika eneo lililo chini ya Halmashauri ya Wilaya; “kitu maarufu” maana yake ni kitu au mahali maarufu (dhahiri au dhahania) ambapo hutambulika kutokana na umaarufu huo; “Mamlaka” maana yake ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa; “misimboposta” (Postikodi) maana yake ni kibainishi cha eneo au maeneo ya usambazaji wa huduma za posta, kinachoundwa na mfuatano wa tarakimu pekee au tarakimu na herufi; “mtaa” Kwa maana ya anwani za makazi ni njia ya umma katika makazi mahususi yenye nyumba, maduka na mambo mengine katika upande mmoja au pande zote mbili za barabara; “Mtaa” ni sehemu au mgawanyo wa Kata unaojumuisha sehemu au mgawanyo wa mji ulio chini ya usimamizi wa 2 Sheria Ndogo za (Anwani za Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa TANGAZO NAMBA 842 (Linaendelea) kisheria wa Mamlaka ya Mji kama ilivyobainishwa kwenye Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji); “mwongozo” maana yake ni waraka unaoelekeza kuhusu mchkato na hatua zinazopaswa kufuatwa katika kuanzisha, kugawa anwani na kusimamia hifadhi-data za anwani; “sekratarieti ya Taifa ya anwani za makazi” maana yake ni Sekretarieti ya Taifa ya Anwani za Makazi iliyo chini ya Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa na Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Afisa yeyote wa umma atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “wadau wa umma” maana yake ni Taasisi, Kampuni, Wakala na Mashirika ya umma; “wakala” maana yake ni mtu, taasisi, kampuni au asasi yoyote iliyoteuliwa kisheria na Halmashauri kutekeleza majukumu kwa niaba ya Halmashauri; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa. SEHEMU YA PILI ANWANI ZA MAKAZI NA MISIMBO YA POSTA Katika kuhamsisha na kutekeleza mpango wa anwani za makazi na misimbo ya posta, Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kutenga maeneo kwa ajili ya mitaa au barabara; (b) kuweka, kutambua na kufuta majina ya mitaa, sehemu na barabara; (c) kuweka, kurekebisha, kutambua na kufuta nambari za nyumba, barabara na mitaa mara kwa mara kwa kadri itakavyohitajika; 3
Part
sehemu na barabara;
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima iunde Kamati ya Wataalam ndani ya miezi sita, na kamati hiyo isimamie alama za majina ya barabara na nambari za nyumba pamoja na utekelezaji wa mwongozo wa anwani.
4. Wajibu wa Halmashau ri Sheria Ndogo za (Anwani za Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa TANGAZO NAMBA 842 (Linaendelea) (d) kutunza na kulinda miundombinu yote ya anwani za makazi na misimbo ya posta; (e) kuzuia na kudhibiti matumizi ya barabara na mitaa katika maeneo husika; (f) kutunza kumbukumbu za majina, nambari za mitaa, barabara, nyumba na ramani, kuhakikisha kuwa kumbukumbu hizo zinapatikana kwa urahisi; (g) kutoa adhabu dhidi ya uhalifu katika miundombinu ya mfumo wa anwani za makazi, nambari za mitaa na majina ya mitaa na barabara zilizotengenezwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi; (h) kushirikisha sekta binafsi, kulingana na mazingira katika kutekeleza mpango wa anwani za makazi na misimbo ya posta. Halmashauri itakuwa na wajibu wa kuunda ndani ya miezi sita tangu kuanza kwa Sheria Ndogo hizi, Kamati ya Wataalam wa kushughulikia masuala ya anwani za makazi ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao- a) mkuu wa idara inayohusika na Mipango Miji na Mazingira ambaye atakuwa Mwenyekiti; b) mkuu wa idara inayohusika na Ujenzi ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti) c) afisa ardhi; d) mpima ardhi; e) mwanasheria ambaye atakuwa Katibu; f) msanifu wa ramani; g) afisa wa posta ambaye atakuwa mjumbe mwalikwa wa kudumu; h) afisa maendeleo ya Jamii au afisa ustawi wa jamii; na i) mtaalam mmoja na yeyote Mkurugenzi. atakayeteuliwa Kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi za chini katika Halmashauri Kamati ya Wataalamu itakuwa na wajibu wa- a) kusimamia uwekaji wa vibao vya majina ya barabara na nambari za nyumba katika eneo lililo chini ya mamlaka yake ya kisheria; b) kusahihisha, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa vipengele vyote vya Mwongozo wa Mfumo wa Anwani ambavyo hasa havipo katika mamlaka ya 4 Kamati ya Wataalam - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Kamati ya Wataalam lazima itoe notisi za ukiukwaji, itunze kumbukumbu za anwani na ramani, ikabidhi kumbukumbu hizo kwa mamlaka husika inapohitajika, ipendekeze mabadiliko ya anwani, na ifanye kazi nyingine zinazoelekezwa na Halmashauri.
5. 6 Majukumu ya Kamati ya Wataalam Sheria Ndogo za (Anwani za Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa TANGAZO NAMBA 842 (Linaendelea) Halmashauri; c) kutoa notisi za ukiukwaji wa hatua nyingine yoyote inayofaa kuchukuliwa kulingana na Sheria Ndogo hizi; d) Kutunza kumbukumbu za anwani zote kwa kila milki katika ramani kwenye sehemu zinazotunzwa na Halmashauri; e) Kutoa kumbukumbu na ramani hizo zitapopaswa kutolewa kwa mamlaka zote za Serikali, Wakala wa utekelezaji wa Sheria na mawakala wa huduma za dharura kwa ajili ya matumizi yao katika utendaji wa majukumu yao kama ilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hizi; f) Kupendekeza mabadiliko ya anwani; na g) Kufanya kazi nyingine zitakazoelekezwa na Halmashauri kufuatana na Sheria Ndogo hizi. SEHEMU YA TATU USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI Wadau watakao husishwa taasisi za Kifedha;
Part
SEHEMU YA TATU
- 7 Verify source ↗
Katika kutekeleza mpango wa anwani za makazi na misimbo
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima iwahusishe wadau mbalimbali wakati wa kutekeleza mpango wa anwani za makazi na misimbo ya Posta.
7. Katika kutekeleza mpango wa anwani za makazi na misimbo ya Posta, Halmashauri itawahusisha wadau wafuatao- a) makampuni binafsi; b) taasisi na Mashirika ya Umma; c) d) asasi za Kijamii; e) taasisi za Kidini; f) mashirika yasiyo ya Kiserikali; g) washirika wa Maendeleo; h) watu binafsi; na i) wadau wengine ambao Halmashauri itaona wanafaa. Shughuli zitakazohu sisha wadau - 8 Verify source ↗
Halmashauri itashirikisha wadau wengine kama mashirika
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ishirikishe wadau wengine, ikiwemo mashirika ya serikali na binafsi, katika shughuli za anwani za makazi na misimbo ya posta zilizoainishwa.
8. Halmashauri itashirikisha wadau wengine kama mashirika ya Serikali na binafsi katika- a) kutengeneza nguzo za alama za mitaa na vibao vya nambari za nyumba; b) kuweka nguzo za majina ya barabara, mitaa na vibao vya nambari za nyumba; c) kubandika au kuchora nambari za nyumba; d) uchapishaji wa daftari la orodha ya misimbo ya posta; 5 Sheria Ndogo za (Anwani za Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa TANGAZO NAMBA 842 (Linaendelea) e) huduma ya ushauri na usimamizi; f) kuhifadhi na kulinda miundombinu ya misimbo ya posta; g) kutoa vifaa na “software” kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Mfumo wa anwani za makazi; na h) utoaji wa mafunzo na shughuli za kuhamasisha utumiaji wa mfumo wa anwani za makazi. Shughuli zitakazoshi kirikisha wadau wa Umma tu - 9 Verify source ↗
Halmashauri itashirikisha shughuli zifuatazo kwa wadau wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must involve only public stakeholders when carrying out the listed activities.
9. Halmashauri itashirikisha shughuli zifuatazo kwa wadau wa umma tu:- (a) uundaji wa hifadhi-data ya anwani za makazi na misimbo ya posta; (b) usambazaji na ugawaji wa anwani za makazi na misimbo ya posta; (c) utengenezaji na uchapishaji wa misimbo ya posta na ramani; (d) shughuli nyingine yoyote idhaniwayo kuwa ni nyeti kwa maslahi ya Taifa; Utaratibu wa kushirikish a wadau 1 - 0 Verify source ↗
Section 0
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ishirkishe wadau katika kutekeleza mpango wa anwani za makazi na misimbo ya posta.
0. 1) Katika kutekeleza mpango, Halmashauri itawashirikisha wadau katika:- a) uchangiaji wa moja kwa moja kwa njia ya fedha au misaada kwa ajili ya Mpango; b) kushiriki katika utekelezaji wa shughuli yoyote iliyotajwa chini ya kifungu cha 7 cha Sheria Ndogo hizi; c) kushirikiana katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Anwani za Makazi; d) kuhusisha na kujumuisha Mpango wa anwani za makazi katika Mpango na miradi mingine kama vile ujenzi wa barabara, majengo, mazingira, usafi, umeme; na e) kuingia katika ubia maalum kutegemeana na Mamlaka inayohusika. 2) Njia zitakazotumiwa na Halmashauri wakati wa kuwahusisha wadau katika utekelezaji wa mpango mpya wa anwani za makazi na misimbo ya posta ni- a) kuainisha wadau katika eneo husika kwa ajili ya kuwashirikisha kutekeleza mpango wa anwani na misimbo ya posta; b) kufuatilia wadau watakao ainishwa kwa mujibu wa 6 Sheria Ndogo za (Anwani za Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa TANGAZO NAMBA 842 (Linaendelea) kifungu cha 9(2) (a), kila Halmashauri itaamua maeneo na namna ya kuwahusisha wadau hao; c) katika kutekeleza kifungu cha 9(2)(b) cha Sheria Ndogo hizi, Halmashauri inaweza kushauriwa lakini haitazuiliwa na maeneo na wadau waliotajwa katika kifungu cha 6 na 7 cha Sheria Ndogo hizi; d) kutangaza au kuweka wazi juu ya uwepo wa utekelezaji wa mpango wa anwani na misimbo ya posta ili kukaribisha na kuvutia wadau mbalimbali katika maeneo yaliyoainishwa katika Sheria Ndogo hizi; e) kuwataka wadau wote wenye nia na wanaotaka huu kutekeleza mpango kushiriki kuwasiliana na Halmashauri itaona inafaa; na katika Makosa na adhabu 1 - 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayekiuka maagizo ya Halmashauri kuhusu mpango wa anwani za makazi na misimbo ya posta, kutoa taarifa za uongo, kuharibu miundombinu, au kuzuia Afisa Mwidhiniwa anaweza kuwa ametenda kosa.
1. f) kuwashirikisha Wadau katika kuchangia na kutoa taarifa ya michango itakayotolewa katika vikao vya Halmashauri kwa ajili ya uwazi na uwajibikaji. SEHEMU YA NNE MAKOSA NA ADHABU Iwapo mtu yeyote- a) atadharau au atakaidi kutekeleza agizo lolote alilopewa na Halmashauri kuhusiana na Mpango wa anwani za makazi na misimbo ya posta chini ya Sheria Ndogo hizi; b) atamshawishi mtu au kundi la watu kukataa au kukwepa kushiriki kutekeleza mpango wa anwani za makazi na misimbo ya posta; c) atatengeneza, atatayarisha, ataidhinisha utengenezaji, au atatunza miundo mbinu isiyo halali kwa njia ya kujipatia manufaa yatokanayo na kuweka, kutambua na kufuta majina ya mitaa, sehemu na barabara ndani ya Halmashauri; d) atatoa kwa makusudi huku akijua ni kosa taarifa za uongo kwa Halmashauri; e) atashindwa kutoa taarifa zitakazohitajika na Halmashauri; f) ataharibu kwa makusudi, ataziba, atang’oa au kufuta miundombinu ya anwani za makazi; au g) atamzuia Afisa Mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake, 7 Sheria Ndogo za (Anwani za Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa TANGAZO NAMBA 842 (Linaendelea) atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili (200,000/=) na isiyozidi shilingi milioni moja (1,000,000/=) au adhabu ya kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili (miezi 12) jela na kisischozidi miezi ishirini na nne jela au adhabu zote mbili. Kufililisha kosa 1
Part
SEHEMU YA NNE
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kutoza faini isiyozidi shilingi 100,000 kwa mtu anayekiri kosa kwa maandishi na kukubali kulipa faini hiyo kama ilivyo kwenye Jedwali la Sheria Ndogo.
2. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote fasini isiyozidi shilingi laki moja iwapo mkosaji atakiri kosa kwa maandishi na kukubali kulipa faini kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Sheria Ndogo hizi. 8 Sheria Ndogo za (Anwani za Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa TANGAZO NAMBA 842 (Linaendelea) JEDWALI (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 12) HATI YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA Mimi………………………………… wa S.L.P. …………………………., nakiri kutenda kosa la ……………………………………………………. ikiwa ni kinyume na kifungu cha ……………… cha Sheria Ndogo za Anwani za Makazi za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa za Mwaka 2020. Kwa hiari yangu mwenyewe pasipo kushawishiwa na mtu yeyote nakubali kulipa kiasi cha shilingi laki moja badala ya kushtakiwa Mahakamani iwapo Mkurugenzi atatekeleza madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha………………………………. cha Sheria Ndogo hizi. Saini: ………………………………………………... Tarehe …………………………………………………… Mbele yangu: Jina: …………………………………………….….. Saini: …………………………………………….….. Wadhifa: ………………………………………………... Tarehe …………………………………………………… 9 Sheria Ndogo za (Anwani za Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa TANGAZO NAMBA 842 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio la Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri tarehe 27 ya mwezi Julai, 2019 mbele ya:- SUNDAY NDORI DEOGRATIUS, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa EDWARD LESLIE HAULE, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa NAKUBALI, DODOMA, Tarehe 01 Septemba 2020 …………………………………….…… SELEMANI S. JAFO Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI) 10
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za (Anwani ya Makazi na Misimbo ya Posta) za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa za mwaka 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in