Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama za Mwaka, 2020
This section gives the title of the by-laws and defines key terms used in them, including protected areas, the Council, environmental conservation, grazing areas, livestock, and forests.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama za Mwaka, 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the title of the by-laws and defines key terms used in them, including protected areas, the Council, environmental conservation, grazing areas, livestock, and forests. Mwenye kufuga katika eneo la Halmashauri lazima azingatie masharti ya ufugaji na usafirishaji wa mifugo, na baadhi ya vitendo vya mifugo ni makosa. Wakulima katika eneo la Halmashauri lazima wafuate kalenda ya kilimo na masharti ya ardhi na mazingira, na hawaruhusiwi kulima au kuchoma shamba kinyume na vikwazo vilivyoelezwa. People in the Council area must follow several environmental protection rules, including planting water-absorbing trees as directed by the Council and avoiding protected areas and water sources. People in the council area must not cut trees or burn forests without permission, and charcoal burning requires a special council permit in designated areas.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama za Mwaka, 2020
Showing 9 of 9
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: This section gives the title of the by-laws and defines key terms used in them, including protected areas, the Council, environmental conservation, grazing areas, livestock, and forests.
2. Sura ya 191 SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama za Mwaka, 2020. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa pale itakavyoelezwa vinginevyo: “eneo la hifadhi” maana yake ni maeneo ya milima, mbuga za wanyama, maeneo ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu na maeneo mengine ambayo yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama; “hifadhi ya mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi, mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji na maelekezo yatakayotolewa na Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hizi au Sheria nyingine yoyote; “maeneo ya malisho” maana yake ni sehemu zote ambazo zimetengwa na Halmashauri au Kijiji kuwa maeneo ya malisho ya mifugo; “mazingira” maana yake ni kama ilivyo tafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mifugo” maana yake ni mifugo yoyote inayofugwa na unaozingatia masharti 1 Sheria Ndogo Za Hifadhi Ya Mazingira Za Halmashauri Ya Wilaya Ya Mkalama Tangazo la Serikali Na.911 (Linaendelea.) Sura ya 323 binadamu; “misitu” maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia kumi na miti, uoto wa asili au iliyopandwa, au asilimia hamsini au zaidi, ya vichaka na miti na miti inayoota upya ambayo itajumuisha aina yote ya misitu ya hifadhi ambayo imetangazwa chini ya Sheria ya Misitu na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri; Masharti ufugaji kuhusu
Part
SEHEMU YA KWANZA
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Mwenye kufuga katika eneo la Halmashauri lazima azingatie masharti ya ufugaji na usafirishaji wa mifugo, na baadhi ya vitendo vya mifugo ni makosa.
3.- (1) Mtu yeyote anayefuga katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo- (a) kufuga na kulisha mifugo yake katika maeneo ya malisho yaliyopangwa na Halmashauri; (b) kupitisha mifugo yake katika njia na zilizopangwa Halmashauri; kuwa na kadi ya mifugo itakayoonyesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; kutengwa (c) na (d) kupeleka mifugo yake katika vituo vya chanjo (e) (f) kama itakavyoamriwa na Halmashauri; kupeleka mifugo katika majosho atakavyoagizwa na Halmashauri; kuchangia gharama za ukarabati wa majosho kama sehemu ya mchango wake, pale itakapobidi kufanya hivyo, na kwa gharama itakayopendekezwa na Halmashauri; kama (g) kuweka alama kwenye mifugo yake na katika mifugo vinavyopendekezwa ili kutoharibu zao la ngozi; viungo vya (h) kuchangia gharama za uboreshaji wa maeneo ya malisho yaliyotengwa na Halmashauri; kuhudhuria mafunzo ya ufugaji kama atakavyohitajiwa na Halmashauri; kutokata miti kwa lengo la kufukuza mbung’o (j) (i) (2) Itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kufanya yafuatayo: (a) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani; (b) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo 2 Sheria Ndogo Za Hifadhi Ya Mazingira Za Halmashauri Ya Wilaya Ya Mkalama Tangazo la Serikali Na.911 (Linaendelea.) lingine bila kibali kutoka kwa moja hadi Halmashauri; kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (c) (e) (d) kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa na Halmashauri; kufuga mifugo kwa zaidi ya idadi iliyoelekezwa na Halmashauri; au kuchunga, kulisha au kunywesha maji mifugo katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hiyo. (f) (3) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kukamata mifugo inayokutwa katika maeneo yasiyoruhusiwa kuchunga, kulisha au kunywesha mifugo. (4) Endapo mmiliki wa mifugo iliyokamatwa kwa mujibu wa aya ya (c) kanuni ndogo ya (2) na kanuni ndogo ya (3) atashindwa kulipa faini iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi, Halmashauri inaweza, baada ya kupata amri ya Mahakama, kuuza kwa njia ya mnada wa hadhara mifugo hiyo na fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmiliki wa mifugo baada ya kutoa gharama za ukamataji, utunzaji wa mifugo na Mahakama. Masharti kilimo kuhusu
Part
Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi, Halmashauri
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Wakulima katika eneo la Halmashauri lazima wafuate kalenda ya kilimo na masharti ya ardhi na mazingira, na hawaruhusiwi kulima au kuchoma shamba kinyume na vikwazo vilivyoelezwa.
4.- (1) Mtu yeyote anayelima katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo: (a) taratibu za kilimo kwa kuzingatia kalenda ya kilimo ya Halmashauri na kwa kuzingatia Sheria zinazosimamia masuala ya ardhi na mazingira; (b) kutolima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, mabwawa au maziwa au kufanya jambo lolote litakaloharibu hifadhi ya mazingira; kutotumia ardhi kinyume na matumizi kama ilivyopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri; na (c) (d) kutosafisha shamba kwa njia ya kuchoma moto, cha kibali maalumu kwa isipokuwa Halmashauri. 3 Sheria Ndogo Za Hifadhi Ya Mazingira Za Halmashauri Ya Wilaya Ya Mkalama Tangazo la Serikali Na.911 (Linaendelea.) (2) Kibali cha kusafisha shamba kwa njia ya kuchoma moto kitakuwa cha maandishi na kitaonyesha jina la mwenye kibali, tarehe na eneo analotaka kuchoma moto. (4) (3) Muda unaoruhusiwa kuchoma moto chini ya Sheria Ndogo hizi ni kuanzia kumi na mbili asubuhi hadi saa nne kamili asubuhi na saa kumi na mbili jioni hadi saa moja kamili usiku. Itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kufanya yafuatayo: (a) kutozingatia kalenda ya kilimo ya Halmashauri; (b) kulima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, milima, mabwana au maziwa au kufanya jambo lolote litakaloharibu hifadhi ya mazingira; (c) Kutumia ardhi kinyume na matumizi kama ilivyopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri; au (d) kusafisha shamba kwa njia ya kuchoma moto bila ya kuwa na kibali au nje ya muda ulioruhusiwa chini ya Sheria Ndogo hizi. (1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuchimba mchanga, kokoto, mawe, udongo au madini yoyote ya ujenzi kwa madhumuni ya kibiashara karibu na makazi ya watu, maeneo ya hifadhi, kandokando ya mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa isipokuwa kwa kibali maalumu cha Halmashauri. (2) Mtu atakayekiuka masharti ya kanuni ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Uchimbaji madini ya ujenzi wa - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: People in the Council area must follow several environmental protection rules, including planting water-absorbing trees as directed by the Council and avoiding protected areas and water sources.
6.- (1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atakuwa na wajibu wa: (a) kupanda miti isiyonyonya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Halmashauri; (b) kutoishi katika eneo la hifadhi au chanzo cha maji; (c) kutolima, kutokata miti, kutochunga mifugo au kutofanya jambo lolote linaloharibu kwa namna yoyote eneo lililotangazwa kuwa eneo la hifadhi au chanzo cha maji; au (d) kutoelekeza mabomba ya maji machafu au 4 Sheria Ndogo Za Hifadhi Ya Mazingira Za Halmashauri Ya Wilaya Ya Mkalama Tangazo la Serikali Na.911 (Linaendelea.) kujisaidia kwenye mito, mabwawa, maziwa, visima, mifereji, chemchem au sehemu yoyote ambayo ni chanzo cha maji; (e) kujimilikisha eneo ambalo ni chanzo cha maji cha umma. (2) Mtu atakayekiuka masharti ya kanuni ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Uhifadhi misitu wa - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: People in the council area must not cut trees or burn forests without permission, and charcoal burning requires a special council permit in designated areas.
7.- (1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atakuwa na wajibu wa: (a) kutokata miti katika maeneo ya misitu iliyohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali kutoka Halmashauri; (b) kutochoma moto misitu kwa namna yoyote ile (c) katika eneo la Halmashauri; kutovuna miti isipokuwa kwa kibali maalum cha Halmashauri; au (d) kutovuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe malum. (2) Uchomaji wa mkaa utafanyika kwa kibali maalum cha Halmashauri katika maeneo yaliyotengwa mahsusi kwa ajili hiyo. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kanuni ndogo ya (1) na (2) atakuwa ametenda kosa. Utupaji wa taka - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Watu wote katika eneo la Halmashauri lazima wawe na njia ya kuhifadhi taka ngumu na laini na choo safi na salama; Halmashauri lazima itenge eneo la kutupia taka na isimamie usafi.
8.- (1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atatakiwa kufanya yafuatayo: (a) kuwa na shimo au chombo maalum cha kuhifadhi taka ngumu na laini; na (b) kuwa na choo safi na salama. (2) Halmashauri itatakiwa kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupa taka ngumu na laini na kusimamia kwa karibu usafi katika eneo hilo. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kanuni ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Wajibu wa jumla - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Residents in affected areas must restore damaged natural vegetation or environment and help extinguish dangerous fires when directed by the Council; Village Government Councils must set aside forest reserve land and oversee tree planting duties.
9.- (1) Wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira yameharibiwa watakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa wanalirudisha katika hali yake ya kawaida eneo hilo kwa kupanda miti na kuendelea kutoharibu 5 Sheria Ndogo Za Hifadhi Ya Mazingira Za Halmashauri Ya Wilaya Ya Mkalama Tangazo la Serikali Na.911 (Linaendelea.) mazingira ili kuwezesha uoto au mazingira yarudi katika kadri yake watakavyoelekezwa na Halmashauri. kawaida kwa hali ya (2) Wakazi wa eneo ambalo moto umetokea unaotishia maisha ya watu, mali au mazingira watakuwa na wajibu wa kushiriki kuzima moto huo kwa kadri watakavyoelekezwa na Halmashauri. (3) Kila Halmashauri ya Serikali ya Kijiji itatakiwa kutenga eneo la hifadhi ya misitu, kusimamia kila mwanakijiji anapanda miti isiyopungua kumi katika eneo la makazi na miti hamsini katika eneo la shamba, kila shule au taasisi ya umma inapanda miti ya kukinga upepo kuzunga majengo. (4) Mtu yeyote atakayeshindwa, bila sababu za msingi, kutekeleza maelekezo ya Halmashauri chini ya kanuni ndogo ya (1), (2) na (3) atakuwa ametenda kosa. Adhabu Kufililisha Kosa - 10 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya
AI-assisted research summary: A person convicted of any offence under these subsidiary laws may be fined up to TZS 300,000, jailed for up to 12 months, or given both penalties.
10. Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hizi atahukumiwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na miwili au adhabu zote mbili kwa pamoja. - 11 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufililisha kosa endapo mtu atakiri
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufililisha kosa ikiwa mtu anakiri kosa chini ya Sheria Ndogo hizi na kulipa kiasi kilichotajwa baada ya kujaza fomu maalum ya Jedwali la Pili.
11. Mkurugenzi anaweza kufililisha kosa endapo mtu atakiri kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa kumtoza kiasi cha shilingi laki tatu baada ya kujaza fomu maalum iliyoambatishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. JEDWALI LA KWANZA (Limetengenezwa chini ya kanuni ndogo ya 3(4)) SEHEMU YA KWANZA VIWANGO VYA FAINI KWA MFUGO AU MIFUGO INAYOZURURA NDANI YA ENEO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA Na 1 2 AINA YA MFUGO NG’OMBE MBUZI KIWANGO CHA FAINI (TSHS) 2000/= 1000/= 6 Sheria Ndogo Za Hifadhi Ya Mazingira Za Halmashauri Ya Wilaya Ya Mkalama Tangazo la Serikali Na.911 (Linaendelea.) 3 4 5 6 7 KONDOO PUNDA PAKA AU MBWA NGURUWE KUKU AU BATA 1000/= 2000/= 10000/= 10000/= 5000/= SEHEMU YA PILI VIWANGO VYA FAINI KWA MFUGO AU MIFUGO ILIYOKAMATWA NA KUTUNZWA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA Na AINA YA MFUGO 1 2 3 4 5 6 7 NG’OMBE MBUZI KONDOO PUNDA PAKA AU MBWA NGURUWE KUKU AU BATA USHURU WA MATUNZO KWA SIKU (TSHS) 2000/= 1000/= 1000/= 2000/= 10000/= 10000/= 5000/= ____________________ JEDWALI LA PILI __________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ndogo ya 11) HATI YA KUFILILISHA KOSA 7 Sheria Ndogo Za Hifadhi Ya Mazingira Za Halmashauri Ya Wilaya Ya Mkalama Tangazo la Serikali Na.911 (Linaendelea.) ya........................................................... Mimi ........................................................................ nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwamba tarehe ..........ya Mwezi ................... Mwaka................. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha …….. cha Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama za Mwaka 2020. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri niko tayari kulipa kiasi cha shilingi elfu thelathini badala ya kushtakiwa Mahakamani. ambaye NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe ......................ya Mwezi ................................Mwaka ……............... Jina: ..................................................... Saini: .................................................... Mbele ya: Jina……............................................... Cheo: .................................................. Saini: .................................................. Tarehe: .............................................. 8 Sheria Ndogo Za Hifadhi Ya Mazingira Za Halmashauri Ya Wilaya Ya Mkalama Tangazo la Serikali Na.911 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa baraza la Madiwani wa Halmashauri uliopitisha na kufanyika tarehe 24/02/2017 na kubandikwa mbele ya; ENG. GODFREY T. SANGA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA JAMES J. MKWEGA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA SELEMANI S. JAFO WN OR-TAMISEMI 9 NAKUBALI DODOMA 01/09/2020
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama za Mwaka, 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in