Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Mji wa Korogwe za Mwaka 2020
This provision gives the bylaw its title and begins the interpretation section.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Mji wa Korogwe za Mwaka 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the bylaw its title and begins the interpretation section. This section defines key terms used in the by-laws, including protected area, the Council, environmental protection, grazing areas, environment, livestock, and forests. Livestock keepers in the Council area must follow Council rules on grazing, movement, records, treatment, training, and contributions, and they must not do certain livestock activities without permission or in unauthorized places. Wakulima katika eneo la Halmashauri lazima wafuate masharti ya kilimo, wasilime maeneo yaliyokatazwa, wasitumie ardhi kinyume na mpango wa Halmashauri, na wasichome moto kusafisha shamba bila kibali maalumu na nje ya muda ulioruhusiwa. Kuchimba mchanga, kokoto, mawe, udongo au madini ya ujenzi kwa biashara karibu na maeneo ya makazi, hifadhi, mito, bwawa au ziwa hairuhusiwi bila kibali maalumu cha Halmashauri.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Mji wa Korogwe za Mwaka 2020
Showing 23 of 23
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za
AI-assisted research summary: This provision gives the bylaw its title and begins the interpretation section.
1. Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Mji wa Korogwe za Mwaka 2020. Tafsiri - 2 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi, isipokuwa pale
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-laws, including protected area, the Council, environmental protection, grazing areas, environment, livestock, and forests.
2. Katika Sheria Ndogo hizi, isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo- “eneo la hifadhi” maana yake ni maeneo ya milima, mbuga za wanyama, maeneo ya vyanzo vya maji, ambayo hifadhi ya misitu na maeneo mengine ya yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo hifadhi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Mji wa Korogwe; “hifadhi ya mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai wa ardhi, na vyanzo vya maji unaozingatia na maelekezo yatakayotolewa na Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hizi au Sheria nyingine “maeneo ya malisho” maana yake ni sehemu zote ambazo zimetengwa na Halmashauri au Kijiji kuwa maeneo ya malisho ya mifugo; “mazingira” maana yake ni kama ilivyo tafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mifugo” maana yake ni mifugo yoyote inayofugwa na binadamu; masharti yoyote; 1 Sura ya 191 Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) la ardhi ambalo “misitu” maana yake ni eneo asilimia kumi ya miti, limefunikwa angalau kwa uoto wa asili au iliyopandwa, au asilimia hamsini au zaidi, ya vichaka na miti na miti inayoota upya ambayo itajumuisha aina yote ya misitu ya imetangazwa chini ya Sheria ya hifadhi ambayo Misitu na mazao yote ya misitu majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri. ikijumuisha Sura ya 323 Masharti kuhusu ufugaji - 3 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayefuga katika eneo la
AI-assisted research summary: Livestock keepers in the Council area must follow Council rules on grazing, movement, records, treatment, training, and contributions, and they must not do certain livestock activities without permission or in unauthorized places.
3.-(1) Mtu yeyote anayefuga katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo: (a) kufuga na kulisha mifugo yake katika maeneo ya malisho yaliyopangwa na Halmashauri; (b) kupitisha mifugo yake katika njia zilizopangwa na kutengwa na Halmashauri; (c) kuwa na kadi ya mifugo itakayoonyesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; (d) kupeleka mifugo yake katika vituo vya na itakavyoamriwa kama chanjo Halmashauri; (e) kupeleka mifugo katika majosho kama atakavyoagizwa na Halmashauri; (f) kuchangia gharama za ukarabati wa majosho kama sehemu ya mchango wake, pale itakapobidi kufanya hivyo, na kwa gharama itakayopendekezwa na Halmashauri; (g) kuweka alama kwenye mifugo yake na katika mifugo vinavyopendekezwa ili kutoharibu zao la ngozi; viungo vya (h) kuchangia gharama za uboreshaji wa maeneo ya malisho yaliyotengwa na Halmashauri; (i) kuhudhuria mafunzo ya ufugaji kama atakavyohitajiwa na Halmashauri; na 2 Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) (j) kutokata miti kwa lengo la kufukuza mbung’o. (2) Itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kufanya yafuatayo: (a) kusafirisha barabarani; mifugo kwa kuiswaga (b) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo moja hadi lingine bila kibali kutoka kwa Halmashauri; (c) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (d) kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa na Halmashauri; (e) kufuga mifugo kwa zaidi ya idadi iliyoelekezwa na Halmashauri; au (f) kuchunga, kulisha au kunywesha maji ambayo mifugo hayakutengwa kwa shughuli hiyo. maeneo katika (3) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya katika maeneo kukamata mifugo yasiyoruhusiwa kuchunga, kulisha au kunywesha mifugo. inayokutwa (4) Endapo mmiliki wa mifugo iliyokamatwa kwa mujibu wa aya ya (c) ya kifungu kidogo cha (2) na kifungu kidogo cha (3) atashindwa kulipa faini kama ilivyoanishwa katika Sheria Ndogo hizi, Halmashauri inaweza, baada ya kupata amri ya Mahakama, kuuza kwa njia ya mnada wa hadhara mifugo hiyo na fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmiliki wa mifugo baada ya kutoa gharama za ukamataji, utunzaji wa mifugo na Mahakama. - 4 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayelima katika eneo la
AI-assisted research summary: Wakulima katika eneo la Halmashauri lazima wafuate masharti ya kilimo, wasilime maeneo yaliyokatazwa, wasitumie ardhi kinyume na mpango wa Halmashauri, na wasichome moto kusafisha shamba bila kibali maalumu na nje ya muda ulioruhusiwa.
4.-(1) Mtu yeyote anayelima katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo: (a) taratibu za kilimo kwa kuzingatia kalenda ya 3 Masharti kuhusu kilimo Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) kilimo ya Halmashauri na kwa kuzingatia Sheria zinazosimamia masuala ya ardhi na mazingira; (b) kutolima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, mabwawa au maziwa au kufanya jambo lolote litakaloharibu hifadhi ya mazingira; (c) kutotumia ardhi kinyume na matumizi kama na kuidhinishwa na ilivyopangwa Halmashauri; na (d) kutosafisha shamba kwa njia ya kuchoma moto, isipokuwa kwa kibali maalumu cha Halmashauri. (2) Kibali cha kusafisha shamba kwa njia ya kuchoma moto kitakuwa cha maandishi na kitaonyesha jina la mwenye kibali, tarehe na eneo analotaka kuchoma moto. (3) Muda unaoruhusiwa kuchoma moto chini ya Sheria Ndogo hii ni kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne kamili asubuhi na saa kumi na mbili jioni hadi saa moja kamili usiku. (4) Itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kufanya yafuatayo: (a) kutozingatia Halmashauri; kalenda ya kilimo ya (b) kulima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, milima, mabwana au maziwa au kufanya jambo lolote litakaloharibu hifadhi ya mazingira; (c) Kutumia ardhi kinyume na matumizi kama na kuidhinishwa na ilivyopangwa Halmashauri; au (d) kusafisha shamba kwa njia ya kuchoma moto bila ya kuwa na kibali au nje ya muda ulioruhusiwa chini ya Sheria Ndogo hizi. 4 Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) Uchimbaji wa madini ya ujenzi - 5 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuchimba
AI-assisted research summary: Kuchimba mchanga, kokoto, mawe, udongo au madini ya ujenzi kwa biashara karibu na maeneo ya makazi, hifadhi, mito, bwawa au ziwa hairuhusiwi bila kibali maalumu cha Halmashauri.
5.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuchimba mchanga, kokoto, mawe, udongo au madini yoyote ya ujenzi kwa madhumuni ya kibiashara karibu na makazi ya watu, maeneo ya hifadhi, kandokando ya mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa isipokuwa kwa kibali maalumu cha Halmashauri. (2) Mtu atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. (3) Mtu yeyote anayetaka kuchimba mchanga, kokoto au mawe katika eneo la Halmashauri atatuma maombi yake kwa njia ya maandishi na kulipia ada ya maombi hayo kwa viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo za Halmashauri zilizotungwa mahsusi kwa ajili ya kuainisha ada na ushuru unaotozwa na Halmashauri. Uhifadhi wa vyanzo vya maji - 6 Verify source ↗
(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri
AI-assisted research summary: Kila mtu katika eneo la Halmashauri lazima afuate masharti ya kulinda maeneo ya hifadhi na vyanzo vya maji, ikiwemo kupanda miti isiyonyonya maji na kuepuka vitendo vinavyoharibu maeneo hayo.
6.-(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atakuwa na wajibu wa- (a) kupanda miti isiyonyonya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Halmashauri; (b) kutoishi katika eneo la hifadhi au chanzo cha maji; (c) kutolima, kutokata miti, kutochunga mifugo au kutofanya jambo lolote linaloharibu kwa namna yoyote eneo lililotangazwa kuwa eneo la hifadhi au chanzo cha maji; (d) kutoelekeza mabomba ya maji machafu au kujisaidia kwenye mito, mabwawa, maziwa, visima, mifereji, chemchem au sehemu yoyote ambayo ni chanzo cha maji; au (e) kujimilikisha eneo ambalo ni chanzo cha maji cha umma. (2) Mtu atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. 5 Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) Uhifadhi misitu wa - 7 Verify source ↗
(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri
AI-assisted research summary: Watu wote ndani ya eneo la Halmashauri hawaruhusiwi kukata miti au kuchoma misitu, na uvunaji wa miti unahitaji kibali maalumu cha Halmashauri katika hali zilizoelezwa.
7.-(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atakuwa na wajibu wa: (a) kutokata miti katika maeneo ya misitu iliyohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya aina kutoka kupata bila yoyote Halmashauri; kibali (b) kutochoma moto misitu kwa namna yoyote ile katika eneo la Halmashauri; (c) kutovuna miti isipokuwa kwa kibali maalumu cha Halmashauri; au katika msitu (d) kutovuna miti ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe malumu. (2) Uchomaji wa mkaa utafanyika kwa kibali maalumu cha Halmashauri katika maeneo yaliyotengwa mahsusi kwa ajili hiyo. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) na (2) atakuwa ametenda kosa. Utupaji wa taka - 8 Verify source ↗
(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri
AI-assisted research summary: Watu wote katika eneo la Halmashauri lazima wawe na njia ya kuhifadhi taka na choo safi na salama; Halmashauri lazima itenge eneo la kutupa taka na kulisimamia; vikundi vya ukusanyaji taka lazima vikusanye ada zilizowekwa.
8.-(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atakiwa kufanya yafuatayo: (a) kuwa na shimo au chombo maalumu cha kuhifadhi taka ngumu na laini na gharama za utupaji wa taka hizo kwenye jaa la taka ni kama la Kwanza la Sheria Ndogo hizi; ilivyoainishwa katika Jedwali (b) kuwa na choo safi na salama. (2) Halmashauri itatakiwa kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupa taka ngumu na laini na kusimamia kwa karibu usafi katika eneo hilo. (3) Vikundi vya kijamii vitakavyokuwa vimeundwa kwaajili ya kukusanya taka ngumu na kuzipeleka kwenye dampo vitakusanya ada za uzoaji wa taka ngumu kama zilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. 6 Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) Uendeshaji wa viwanda Wajibu jumla wa (4) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. - 9 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hatoruhusiwa kuendesha
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuendesha kiwanda, karakana, au shughuli inayotoa uchafu unaoathiri watu katika maeneo ya makazi bila kufuata taratibu za ujenzi; pia hairuhusiwi kufanya matengenezo ya magari, pikipiki au mitambo nje ya maeneo yaliyoruhusiwa bila sababu za msingi, kibali, na ada kwa Halmashauri.
9.-(1) Mtu yeyote hatoruhusiwa kuendesha shughuli za kiwanda au karakana au shughuli yoyote inayozalisha uchafu ambao unaleta athari kwa binadamu na viumbe wengine katika maeneo ya makazi ya watu bila kuzingatia taratibu za ujenzi. (2) Mtu yeyote hatoruhusiwa, bila sababu za msingi, kufanya matengenezo ya magari, pikipiki au mitambo katika eneo lolote isipokuwa katika karakana, gereji au maeneo yaliyoruhusiwa baada ya kupata kibali na kulipa ada kwa Halmashauri kama ilivyoainishwa katika Sheria Ndogo mahsusi kwa ajili ya ada na ushuru unaotozwa na Halmashauri. (3) Mtu yeyote atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) na (2) atakuwa ametenda kosa. - 10 Verify source ↗
(1) Wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au
AI-assisted research summary: Wakazi wa maeneo yaliyoharibiwa na mazingira au yenye moto hatarishi lazima wahusike katika urejeshaji au kuzima moto, kwa maelekezo ya Halmashauri.
10.-(1) Wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira yameharibiwa watakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa wanalirudisha katika hali yake ya kawaida eneo hilo kwa kupanda miti na kuendelea kutoharibu mazingira ili kuwezesha uoto au mazingira yarudi katika hali yake ya kawaida kwa kadri watakavyoelekezwa na Halmashauri. (2) Wakazi wa eneo ambalo moto umetokea unaotishia maisha ya watu, mali au mazingira watakuwa na wajibu wa kushiriki kuzima moto huo kwa kadri watakavyoelekezwa na Halmashauri. (3) Kila Halmashauri ya Serikali ya Kijiji itatakiwa kutenga eneo la hifadhi ya misitu, kusimamia kila mwanakijiji anapanda miti isiyopungua kumi katika eneo la makazi na miti hamsini katika eneo la shamba, kila shule au taasisi ya umma inapanda miti ya kukinga upepo kuzunga majengo. 7 Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) (4) Mtu yeyote atakayeshindwa, bila sababu za msingi, kutekeleza maelekezo ya Halmashauri chini ya kifungu kidogo cha (1), (2) na cha (3) atakuwa ametenda kosa. - 11 Verify source ↗
Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa atakua na
AI-assisted research summary: Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa ana uwezo wa kuingia eneo lolote wakati wa kazi ili kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi, na ada ya ukaguzi hulipwa mara moja kwa mwaka kama ilivyo kwenye Jedwali la Tatu.
11. Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa atakua na uwezo wa kuingia katika muda wa kazi, katika eneo lolote kwa madhumuni ya kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi, na ada ya ukaguzi italipwa mara moja kwa mwaka kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hizi. - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote aliyehukumiwa kwa kosa chini ya Sheria Ndogo hizi anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu, kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili, au vyote viwili.
12. Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hizi atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote faini na kifungo kwa pamoja. Ukaguzi Adhabu Kufililisha kosa - 13 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufililisha kosa endapo
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuchukua hatua ya kufililisha kosa na kumtoza mtu shilingi 30,000 ikiwa mtu huyo anakiri kosa chini ya Sheria Ndogo hizi na amejaza fomu maalumu ya Jedwali la Nne.
13. Mkurugenzi anaweza kufililisha kosa endapo mtu atakiri kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hizi kwa kumtoza kiasi cha shilingi elfu thelathini baada ya kujaza fomu maalumu iliyoambatishwa katika Jedwali la Nne la Sheria Ndogo hizi. 8 Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA KWANZA ___________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 8(1) (a)) GHARAMA ZA UTUPAJI TAKA KWENYE JAA LA TAKA Na. Kiasi cha taka
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: This provision shows a fee table for waste collection, including charges for vehicles under five tons per trip and for vehicles of five tons or more per extra ton, and it lists business/residential premises categories.
2. Gari chini ya tani tano kwa safari Gari la tani tano na zaidi kwa kila tani moja inayoongezeka Kiwango 40,000/= 10,000/= _________ JEDWALI LA PILI _________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 8 (3)) GHARAMA ZA UKUSANYAJI TAKA KATIKA MAJENGO YA BIASHARA NA MAKAZI NA. AINA YA BIASHARA Nyumba ya kulala wageni 1 Makazi au kaya 2 Mgahawa mkubwa 3 4 Zahanati (Taka zisizo hatari)
Part
JEDWALI LA PILI
- 5 Verify source ↗
Kituo cha afya (taka zisizo hatari)
AI-assisted research summary: This provision lists a health facility category for non-hazardous waste and mentions hospitals.
5. Kituo cha afya (taka zisizo hatari) 6 Hospitali 7 - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: This section lists categories of premises or businesses, including carpentry, metalwork, timber sales, workshops, small factories, and large factories.
9. Fundi seremala Fundi chuma Kiwanda cha kuuza mbao 10 Karakana 11 Kiwanda kidogo 12 Kiwanda kikubwa - 17 Verify source ↗
Shule ya sekondari ya kutwa (binafsi)
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaeleza shule ya sekondari ya kutwa ya binafsi.
17. Shule ya sekondari ya kutwa (binafsi) - 18 Verify source ↗
Shule ya sekondari ya bweni (binafsi)
AI-assisted research summary: Section 18 concerns private boarding secondary schools.
18. Shule ya sekondari ya bweni (binafsi) - 19 Verify source ↗
Duka dogo la chakula (min
AI-assisted research summary: Section title: Duka dogo la chakula (min supermarket).
19. Duka dogo la chakula (min supermarket) - 25 Verify source ↗
Duka la dawa (jumla na Rejareja)
AI-assisted research summary: Section 25 lists monthly fee amounts for “Duka la dawa (jumla na Rejareja)” and related entries.
25. Duka la dawa (jumla na Rejareja) 9 VIWANGO 5000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 15,000/= kwa mwezi 30,000/= kwa mwaezi 30,000/=kwa mwezi 5000/= kwa mwezi 5000/=kwa mwezi 20,000/=Kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 20,000/=kwa mwezi 20,000/=kwa mwezi 3000/= kwa mwezi 20,000/=kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 15,000/=kwa mwezi 30,000/=kwa mwezi 5000/=kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 30,000/=kwa mwezi 10,000/=kwa mwezi 10,000/=kwa mwezi Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) - 27 Verify source ↗
Kiwanda kidogo kwa trip zisizozidi 4
AI-assisted research summary: Kichwa cha kifungu kuhusu kiwanda kidogo na trip zisizozidi 4 kwa mwezi.
27. Kiwanda kidogo kwa trip zisizozidi 4 kwa mwezi - 47 Verify source ↗
Aina nyingine ya biashara au huduma
AI-assisted research summary: This section appears to list monthly fees for “other business or service” and inspection costs for an area or building.
47. Aina nyingine ya biashara au huduma 5,000/=kwa mwezi 50,000/=kwa mwezi 1,000/=kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 5,000/=kwa mwezi 1,000/=kwa mwezi 5,000/=kwa mwezi 50,000/=kwa mwezi 5,000/=kwa mwezi 30,000/=kwa mwezi 100,000/=kwa mwezi 50,000/=kwa mwezi 100,000/=kwa mwezi 10,000/=kwa mwezi 5,000/=kwa mwezi 10,000/=kwa mwezi 20,000/=kwa mwezi 10,000/=kwa mwezi 1,000/=kwa mwezi 50,000/=kwa mwezi 20,000/=kwa mwezi 10,000/=kwa mwezi _______ JEDWALI LA TATU __________ ( Limetengenezwa chini ya kifungu cha 11) GHARAMA ZA UKAGUZI ENEO AU JENGO NA.
Part
JEDWALI LA TATU
- 15 Verify source ↗
Magari yanayotembeza biashara
AI-assisted research summary: This section lists annual charges for business-moving vehicles.
15. Magari yanayotembeza biashara KIWANGO 180,000/=kwa mwaka 60,000/=kwa mwaka 180,000/= kwa mwaka 120,000/=kwa mwaka 60,000/=kwa mwaka 60,000/=kwa mwaka 120,000/=kwa mwaka 60,000/= kwa mwaka 120,000/=kwa mwaka 60,000/=kwa mwaka 60,000/=kwa mwaka 120,000/=kwa mwaka 120,000/=kwa mwaka 120,000/= kwa mwaka 60,000/=kwa mwaka 10 Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) _________ JEDWALI LA NNE _________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 13) HATI YA KUFILILISHA KOSA ........................................................................ Mimi nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya........................................................... ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwamba Tarehe ..........ya Mwezi ................... Mwaka................. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha …….. cha Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Mji wa Korogwe za Mwaka 2020. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri niko tayari kulipa kiasi cha shilingi elfu thelathini badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe ......................ya Mwezi ................................Mwaka …… Jina: ..................................................... Saini: .................................................... Mbele ya: Jina……............................................... Cheo: .................................................. Saini: .................................................. Tarehe: .............................................. 11 Sheria Ndogo Za Hifadhi ya Mazingira Za Halmashauri ya Mji Wa Korogwe Tangazo la Serikali Na. 933 (Linaendelea.) Muhuri wa Halmashauri ya mji Korogwe ulibandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 31/10/2019 Muhuri uliobandikwa mbele ya:- NICODEMUS J. BEI, Mkurugenzi wa Mji, Halmashauri ya Mji, Korogwe MHE. HILLARY H. NGONYANI, Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji, Korogwe L.S NAKUBALI, Dodoma, SELEMANI S. JAFO (MB.) 28 Septemba, 2020 WN-OR-TAMISEMI 12
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za Hifadhi ya Mazingira za Halmashauri ya Mji wa Korogwe za Mwaka 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in