AI-assisted research summary: Halmashauri must cooperate with public and private institutions on address and postcode system tasks; section 8 makes several acts offences and section 9 allows the Director to impose a reduced penalty in some cases.
7. Katika kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria Ndogo hizi, Halmashauri itashirikiana na taasisi za umma na binafsi katika: (a) kutengeneza nguzo za alama za mitaa na vibao vya nambari za nyumba; (b) kuweka nguzo za majina ya barabara, mitaa na vibao vya nambari za nyumba; (c) kubandika au kuchora nambari za nyumba; (d) uchapishaji wa daftari la orodha ya Postikodi; (e) huduma za ushauri na usimamizi (f) kuhifadhi na Postikodi; kulinda miundombinu ya (g) kutoa vifaa kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa mfumo wa Anwani za Makazi; 3 Sheria Ndogo za Anwani za Makazi na Postikodi za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1003 (Linaendelea) (h) kutoa mafunzo na kushiriki shughuli za kuhamasisha utumiaji wa mfumo wa Anwani za Makazi; (i) uundaji wa hifadhi-data ya Anwani za Makazi na Postikodi; (j) usambazaji na ugawaji wa Anwani za Makazi na Postikodi; na (k) kuhusisha na kujumuisha mpango wa Anwani za Makazi katika mipango na miradi mingine kama vile ya ujenzi wa barabara, majengo, mazingira, usafi,na umeme. Makosa 8 . Endapo mtu yeyote- (a) atamshawishi mtu au kundi la watu kukataa au kukwepa kushiriki kutekeleza Mpango wa anwani za makazi na misimbo ya posta; (b) atatengeneza, ataidhinisha atatayarisha, utengenezaji, au atatunza miundo mbinu isiyo halali kwa nia ya kujipatia manufaa yatokanayo na kuweka, kutambua, na kufuta majina ya mitaa, barabara ndani ya Halmashauri; sehemu na (c) atatoa kwa makusudi huku akijua ni kosa taarifa za uongo kwa Halmashauri; (d) Atashindwa bila sababu za msingi kutoa taarifa zitakazohitajika na Halmashauri; (e) ataharibu kwa makusudi, ataziba, atang’oa au kufuta miundombinu ya Anwani za Makazi; na (g) atamzuia Afisa Mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu (300,000/=) au kutumikia kifungo kisichozidi miezi kumi na miwili (12) au adhabu zote mbili yaani faini na 4 Sheria Ndogo za Anwani za Makazi na Postikodi za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1003 (Linaendelea) kifungo. Kufililisha kosa 9 . Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote kiasi kisichozidi shilingi laki mbili tu (200,000/=) iwapo mkosaji atakiri kosa kwa maandishi na kukubali kulipa faini iliyoainishwa chini ya Sheria Ndogo hizi. ______ JEDWALI _______ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 9) HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA HATI Na. …….. Tarehe……………. FOMU YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA (Chini ya kifungu cha 9 cha Sheria Ndogo za Anwani za Makazi na Postikodi za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima za Mwaka 2020) Mimi ......………………….... nakiri mbele ya …………...……. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Itilima, kwamba mnamo tarehe ….. ya Mwezi .... Mwaka …...… nilitenda kosa la kukiuka maelekezo ya kifungu cha …… cha Sheria Ndogo za Anwani za Makazi na Postikodi za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima za Mwaka 2020 na kuwa 5 Sheria Ndogo za Anwani za Makazi na Postikodi za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1003 (Linaendelea) nipo tayari kulipa kiasi cha Sh………………na kutimiza wajibu wangu chini ya Sheria Ndogo ikiwa Mkurugenzi ataamua kutekeleza mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 9 cha Sheria Ndogo hii badala ya kushtakiwa Mahakamani. Nathibitisha kwamba maelezo niliyotoa ni ya kweli nimeyatoa kadri ya ufahamu wangu leo tarehe……….Saini………………. hapo AFISA MWIDHINIWA Nimepokea kiasi cha Sh……………………………… toka kwa mtajwa risiti nimemkatia namba………………………………………………….. Jina: …………………………………………… Cheo: …………………………………………. Saini: ………………………………………….. juu na 6 Sheria Ndogo za Anwani za Makazi na Postikodi za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1003 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima imebandikwa kwenye Sheria ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima uliofanyika tarehe 08-09 mwezi mei mwaka 2019 mbele ya:- ……………………………… ELIZABETH M. GUMBO MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA ……………………………… MH. DAUDI M. NYALAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA NAKUBALI ………………………………. MHE. SELEMANI S. JAFO (MB), WAZIRI WA NCHI – OR –TAMISEMI LS Dodoma Tarehe 28 Septemba, 2020 7