Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima za mwaka, 2020
This section names the by-law, applies it across the whole Itilima District Council area, and defines key terms used in it.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima za mwaka, 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section names the by-law, applies it across the whole Itilima District Council area, and defines key terms used in it. The Halmashauri must carry out a range of agricultural development duties, including farmer registration, input access, extension services, crop-market controls, and crop quality and pest management. Halmashauri must promote agriculture by encouraging farmer groups and cooperatives, establishing model farms, and creating training centers for draft animals and farm tools. Halmashauri ya Kijiji na uongozi wa kitongoji lazima waandae na wasimamie mipango ya matumizi bora ya ardhi na usimamizi wa mifugo. Afisa Mwidhiniwa lazima ahakikishe kila mkulima anaandaa shamba kwa wakati, anapanda mbegu kwa mstari, anazingatia nafasi sahihi kati ya mimea, na anaweka mbolea kwa viwango na kwa wakati.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima za mwaka, 2020
Showing 7 of 7
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: This section names the by-law, applies it across the whole Itilima District Council area, and defines key terms used in it.
3. SEHEMU YA KWANZA KILIMO CHA MAZAO Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima za mwaka, 2020. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Itilima. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo:- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri atakayeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “Afisa Ugani” maana yake ni mtaalamu wa kilimo, mifugo, Uvuvi au Nyuki wa Halmashauri; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Itilima. “kilimo” maana yake ni shughuli yoyote ya uzalishaji mali inayofanywa na binadamu na itajumuisha kilimo cha mazao, ufugaji wa wanyama, samaki na nyuki au uvuvi; “mazao” maana yake ni mazao yote ya chakula, biashara, maua, matunda na mbogamboga yanayolimwa 1 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) ndani ya eneo la Halmashauri; “mifugo” maana yake ni wanyama wote wafugwao na binadamu na itajumuisha nyuki, samaki, bata na kuku; “mfugaji” maana yeyote yake anayejishughulisha na ufugaji wa mifugo katika eneo la Halmashauri; ni mtu “mkulima” maana yake ni mtu yeyote yule anayejishiughulisha na kilimo; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja na Afisa yeyote wa umma atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “skimu ya umwagiliaji” maana yake ni miundo mbinu ya miradi ya maji ambayo imeanzishwa na Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, taasisi binafsi au taasisi za umma na kuwapa wananchi ili kuendeleza kilimo cha umwagiliaji; “uhawilishaji” maana yake ni kitendo cha uzalishaji wa wanyama kwa njia ya kisasa kwa kutumia mbegu za madume bora; “vyanzo vya maji” maana yake ni mito, vijito, visima, mabwawa, mifereji, maziwa, chemichemi, ardhi oevu au ardhi chepechepe; Wajibu wa Halmashau ri
Part
SEHEMU YA KWANZA
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: The Halmashauri must carry out a range of agricultural development duties, including farmer registration, input access, extension services, crop-market controls, and crop quality and pest management.
4. Katika kuhamasisha na kutekeleza azma ya Kilimo Kwanza, Halmashauri itakuwa na wajibu wa: (a) kuhakikisha viongozi wa Serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wanashiriki ipasavyo katika kuendeleza sekta ya kilimo katika Halmashauri; (b) kuhakikisha kuwa wakulima wanasajiliwa pamoja na mazao wanayolima na kiasi cha ekari ya mazao wanayolima; (c) kuhakikisha upatikanaji rahisi na kwa wakati wa pembejeo za kilimo; 2 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) (d) kutekeleza mipango ya msimu wa kilimo unaofuata mara baada ya mwisho wa msimu; (e) kuhakikisha upatikanaji wa maafisa ugani katika kila kijiji au mtaa au kata; (f) kuanzisha na kusimamia utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani; (g) kuainisha matumizi bora ya ardhi ili kubainisha na kutofautisha ardhi ya mifugo,kilimo na hifadhi; (h) kusimamia maadili, mwenendo na upatikanaji wa mawakala wa mbolea na pembejeo za kilimo; (i) kuhakikisha wanunuzi wanakuwa na vibali vya kununua mazao; wa mazao (j) kuhakikisha ubora wa mazao unazingatiwa na mkulima katika hatua zote za uzalishaji; (k) kuhakikisha visumbufu na magonjwa ya mazao yanadhibitiwa; (l) kuhakikisha kunakuwa na masoko rasmi ya mazao. Wajibu wa Halmashau ri kutekeleza majukumu ya kuendeleza mazao - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Halmashauri must promote agriculture by encouraging farmer groups and cooperatives, establishing model farms, and creating training centers for draft animals and farm tools.
5. Katika kuhamasisha kilimo Halmashauri itakuwa na wajibu wa: cha mazao bora, (a) kuhamasisha uundaji wa vikundi vya kiuchumi vinavyohamasisha kilimo cha kisasa; (b) kuanzisha mashamba darasa ya mfano; (c) kuhamasisha uanzishwaji wa vyama vya wakulima vya kuweka na kukopa kwa lengo la kujipatia mikopo ya benki; (d) kuanzisha vituo vya kukuzia na kufundishia wanyama kazi; (e) kuanzisha vituo maalum kwa ajili ya kutolea mafunzo ya utumiaji na utunzaji wa zana bora 3 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) za kilimo; - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Halmashauri ya Kijiji na uongozi wa kitongoji lazima waandae na wasimamie mipango ya matumizi bora ya ardhi na usimamizi wa mifugo.
6. Wajibu wa Halmashau ri ya Kijiji kutekeleza majukumu ya usimamizi (f) kuhamasisha matumizi ya wanyama kazi katika maeneo ambayo wafugaji hujishughulisha pia na kilimo cha mazao; (g) kushindanisha maafisa ugani wote katika mitaa, vijiji na kata ili kumpata afisa ugani bora katika ngazi za vijiji, mitaa, kata na Halmashauri; (h) kuanzisha benki ya ardhi ya Halmashauri; na (i) kuhakikisha inashirikiana na vituo na tasisi za utafiti katika utafiti wa mazao. Halmashauri ya Kijiji kwa kushirikiana na uongozi wa kitongoji itakuwa na wajibu ufuatao: (a) kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi; (b) kuhakikisha kila mfugaji anapata ardhi ya kutosha ya malisho ya mifugo; (c) kusimamia na kulinda mipaka ya ardhi ya kilimo na mifugo iliyobainishwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi; (d) kutoa au kutaja idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji ataruhusiwa kuwa nayo kwa mujibu wa sheria; (e) kusimamia uanzishwaji wa majosho ya mifugo kwa ushirikiano na wafugaji; (f) kuhamasisha wafugaji kuvuna mifugo yao mara kwa mara ili kubakisha idadi ya mifugo yenye kuleta tija; (g) kuhakikisha wataalamu wa ugani waliopo katika kijiji wanatoa elimu ya ufugaji wa kisasa ili kupata mifugo bora na mazao bora ya mifugo; na (h) kuandaa njia maalum za kupitishia mifugo. Wajibu wa Afisa Mwidhini wa - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa lazima ahakikishe kila mkulima anaandaa shamba kwa wakati, anapanda mbegu kwa mstari, anazingatia nafasi sahihi kati ya mimea, na anaweka mbolea kwa viwango na kwa wakati.
7. (1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba kila mkulima: (a) anaandaa shamba kwa wakati; (b) anapanda mbegu kwa mstari; (c) anazingatia nafasi kati ya mmea na mmea inayotakiwa kitaalam; (d) anaweka mbolea kwa viwango na kwa wakati; 4 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) na Hifadhi ya mazao - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Mkulima lazima avune mazao yanapokomaa au kukauka na kuyahifadhi kwa usafi na usalama; kila kaya lazima iwe na ghala salama la chakula; afisa mwidhiniwa anaweza kuingia na kukagua shamba wakati wa saa za kazi.
8. (e) anapalilia kwa wakati palizi mbili au zaidi; (2) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia na kukagua shamba lolote wakati wa saa za kazi ili kujionea kama mkulima amezingatia maelezo ya kitaalam kama yalivyotolewa na wataalam wa kilimo. (1) Kila mkulima atakayelima shamba katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuvuna mazao yake pindi yakikomaa au kukauka na kuyahifadhi katika hali ya usafi na usalama ili kutunza ubora wake. (2) Kila kaya itatakiwa kluwa na ghala la kuhifadhia chakula ambalo litapaswa kuwa katika hali ya usalama na lisiloruhusu wadudu kama dumizi, panya au wadudu wengine kusababisha uharibifu wa chakula hicho. Wajibu wa kulima - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaweka wajibu kwa wakulima, wafugaji na wafugaji wa nyuki, na pia wajibu wa Halmashauri na maafisa wake katika kusimamia kilimo, ufugaji, umwagiliaji, samaki na nyuki.
9. (1) Kila mkulima anayemiliki au atakayemilikishwa shamba kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi atawajibika kulilima, kulitunza na kuendeleza shamba hilo kwa mujibu wa maelezo ya kitaalamu atakayopewa na Afisa Ugani. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), kila mkulima atakuwa na wajibu wa:- isipokuwa kama (a) kupalilia shamba kabla ya wakati wa itaelezwa mavuno vinginevyo; (b) kuweka mbolea; (c) kutoa taarifa kwa mamlaka za kijiji, mtaa, kata au Halmashauri au Afisa Ugani yoyote kwa njia yoyote atakayoona inafaa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa mazao au kuwepo kwa wadudu waharibifu; (d) kutumia pembejeo kwa kuzingatia maelezo ya kitaalamu kila mwaka isipokuwa itaelekezwa kama vinginevyo na Afisa Ugani; (e) kuchukua hatua za kuangamiza wadudu waharibifu au kutibu magonjwa kama atakavyokuwa ameelekezwa na Afisa Ugani; na (f) kuzuia moto kuharibu usiweze 5 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) mazingira. Wajibu wa Afisa Ugani 10 . Ukaguzi 11 . Kila Afisa Ugani atawajibika kutoa programu ya kilimo ya mwaka kulingana na hali ya hewa ambayo itazingatia mambo yafuatayo; (a) aina ya mazao ya msimu; (b) aina ya mbegu kwa msimu husika; (c) namna na wakati wa kupanda; (d) namna na wakati gani wa kuvuna; (e) namna ya kuhifadhi mazao baada ya kuvunwa. Afisa mwidhiniwa au Afisa Ugani atatakiwa:- (a) wakati wa saa za kazi kuingia kwenye eneo la madhumuni ya kusimamia kilimo kwa utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; na (b) wakati wa saa za kazi kuingia katika kaya yoyote ili kukagua ghala la chakula kuona kama taratibu za kuhifadhi chakula zinazingatiwa. (2) Kwa madhumuni ya ukaguzi Afisa Mwidhiniwa atatakiwa:- (a) kuwa na daftari linaloonyesha idadi kamili ya wakazi na idadi ya ekari za mazao ya kilimo; na (b) ratiba ya kutembelea mashamba ya wakazi ili kujionea kama wanatekeleza wajibu wa kulima na kutunza mashamba kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi. Makosa 12 Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hizi kwa mtu 6 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) . yeyote: 13 . Wajibu wa Halmashau ri katika kuendeleza ufugaji (a) anayemiliki ardhi ya kilimo kushindwa, kukataa au kakataza ardhi hiyo kutumika kwa kilimo; (b) bila sababu za msingi kutotunza shamba; (c) bila sababu za msingi kutovuna kwa wakati mazao yaliyoko shambani ambayo yamefikia wakati wa kuvunwa; na (d) kumzuia Afisa Mwidhiniwa au Afisa Ugavi kutekeleza majukumu yake. SEHEMU YA PILI UFUGAJI Katika kuendeleza ufugaji bora na wa kisasa, Halmashauri itakuwa na wajibu ufuatao: (a) kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kutenga maeneo ya wakulima, wafugaji na maeneo ya hifadhi; (b) kuhakikisha upatikanaji wa maafisa ugani; (c) kuhakikisha upatikanaji wa madawa ya mifugo na chanjo za mifugo; (d) kuhakikisha uwepo wa majosho kwa kushirikisha nguvu za wananchi; (e) kuanzisha kamati za majosho kwenye kila vijiji ambapo majosho hayo yameanzishwa; (f) kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya mifugo hai na wanyama; (g) kuanzisha minada na magulio ya mifugo ndani ya maeneo ya Halmashauri na kuhimiza ili kuvuna na wafugaji kutumia minada kupunguza idadi ya mifugo; (h) kuhamasisha wananchi kuanzisha vyama vya ushirika wa wafugaji na vyama vya kuweka na kukopa; (i) kusaidia kuanzisha vituo vya uhawilishaji wa mifugo; (j) kushindanisha maafisa ugani wote katika vijiji ili kumpata afisa ugani bora katika ngazi za Vijiji na Halmashauri; (k) kuandaa vigezo vya kuwapata maafisa ugani bora wa mifugo katika vijiji; (l) kutoa zawadi kwa mfugaji bora kwa mwaka kwa kila kijiji na Halmashauri; 7 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) (m) kutoa zawadi kwa afisa ugani bora kwa mwaka wa Halmashauri, kijiji na kata; (n) kutoa zawadi kwa shamba darasa la mifugo kwa mwaka; (o) kuhakikisha upatikanaji wa mabwawa ya maji ya kunyweshea mifugo; (p) kuhakikisha upatikanaji rahisi wa soko la ngozi na mifugo, mazao ya mifugo kama mikanda, pochi, mapambo yatokanayo na ngozi za wanyama na usindikaji wa maziwa, siagi, jibini na mtindi; (q) kuanzisha klabu za wanywaji maziwa katika Halmashauri; (r) kufanya uperembaji wa mara kwa mara juu ya ufugaji wa kisasa kwa madhumuni ya kujadili mafanikio na changamoto katika utekelezaji ili kuimarisha kasoro zilizojitokeza; kurekebisha au (s) kuhamasisha wafugaji kuanzisha mashamba ya mazao ya kilimo ili wanufaike na upatikanaji rahisi wa mbolea ya mboji; (t) kuhamasisha wafugaji kufanya uvunaji wa mara kwa mara wa mifugo ili kubakisha idadi ndogo ya mifugo yenye kuleta tija na urahisi wa kuihudumia; (u) kuanzisha machinjio ya wanyama ya kisasa na salama ili kurahisisha uvunaji wa mifugo kwa njia ya uchinjaji; (v) kuhakikisha udhibiti wa ufugaji wa kuhamahama ili kuhifadhi mazingira; (w) kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi ili kudumisha amani, utulivu na maelewano katika jamii za wakulima na wafugaji. Wajibu wa Halmashau ri ya Kijiji 14 . Halmashauri ya kijiji itakuwa na wajibu wa: (a) kuandaa mpango wa matumizi bora wa ardhi; (b) kuhakikisha kila mfugaji anapata ardhi ya kutosha ya malisho ya mifugo; (c) kusimamia na kulinda mipaka ya ardhi ya kilimo na mifugo iliyobainishwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi; (d) kusimamia uanzishwaji wa majosho ya mifugo kwa ushirikiano wa wafugaji; (e) kuhamasisha wafugaji kuvuna mifugo yao mara 8 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) 15 . Wajibu wa Afisa Mwidhini wa katika kuboresha ufugaji Wajibu wa Mfugaji 16 . kwa mara ili kubakisha idadi ya mifugo yenye kuleta tija; (f) kuhakikisha wataalamu wa ugani waliopo katika kijiji wanatoa elimu ya ufugaji wa kisasa ili kupata mifugo bora na mazao bora ya mifugo; na (g) kuandaa njia maalum za kupitisha mifugo. Afisa Mwidhiniwa au Afisa Ugani atatakiwa: (a) kuwa na daftari linaloonyesha idadi kamili ya mifugo kwa kila mfugaji; (b) kufanya ukaguzi wakati wa saa za kazi katika kaya yoyote ili kukagua idadi ya mifugo; (c) kuhakikisha kuwa mfugaji anachanja na kuogesha mifugo yake mara kwa mara ili kuepuka magonjwa ya mifugo; taarifa (e) kutoa (d) kuhakikisha kuwa mfugaji mwenye mifugo iliyozidi idadi ya kibali chake kwa mujibu wa sheria anavuna mifugo yake kwa njia endelevu; kwa Halmashauri mara anapogundua kuna mlipuko wa magonjwa ambayo yanahitaji msaada kutoka ngazi za juu; (f) kumchukulia hatua za kisheria mfugaji yeyote anayekwenda kinyume na masharti ya ufugaji yaliyoainishwa chini ya sheria ndogo hizi au sheria yoyote iliyoandikwa; na (g) kuhamasisha wafugaji kutumia njia za kisasa za kuitambua mifugo badala ya kutumia njia za kizamani ambazo zinaharibu ubora wa ngozi. Kila mfugaji atawajibika: (a) atahakikisha anafuga idadi ya wanyama ambayo haitasababisha usumbufu kwa wadau wengine wa kilimo kama ilivyoidhinishwa kwenye kibali cha Halmashauri; (b) atalazimika kuchanja mifugo yake kila mara ili kuzuia magonjwa ya mifugo na magonjwa ya mlipuko; (c) atalazimika kuogesha mifugo yake ili kujihami dhidi ya magonjwa, kupe na mbung’o; (d) atalazimika kujiunga na vyama vya wafugaji wajasiriamali; (e) atalazimika kutoa taarifa yoyote juu ya kutokea kwa magonjwa ya mifugo akiyaona au kuhisi 9 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) au kuyatambua dhidi ya mifugo yake; (f) atalazimika kuchungia mifugo yake katika maeneo yaliyotengwa katika mpango wa matumizi bora ya ardhi au kufuga mifugo yake ndani ya banda kwa idadi ambayo Halmashauri itatoa kibali; (g) atalazimika kuheshimu mipaka iliyotenganisha ardhi ya kilimo, mifugo, hifadhi za taifa, makazi maeneo ya taasisi na maeneo mengine ya wadau wa kilimo kama mazao ya wakulima, wafugaji wa nyuki, samaki na skimu za umwagiliaji; (h) atashirikiana na maafisa mifugo na maafisa ugani wakati wa chanjo, wakati wa magonjwa ya mlipuko na karantini na kampeni zozote za kitaifa za kudhibiti magonjwa na vifo vya nifugo; (i) atashirikiana na maafisa ugani kuanzisha mashamba darasa na mashamba ya kulishia mifugo; (j) ataheshimu masharti ya karantini wakati wa magonjwa ya mlipuko; (k) atatakiwa kupitisha mifugo yake katika njia zilizotengwa na Halmashauri; na (l) ataweka alama za utambuzi wa mifugo yake katika kama za atakavyoelekezwa na wataalam ili kutoharibu ubora wa thamani ya ngozi. wanyama sehemu Uvunaji wa mifugo 17 . (1) Kila mfugaji atawajibika kuvuna mifugo yake kila atakapobaini kuwa imevuka idadi iliyoko kwenye kibali kilichotolewa na Halmashauri. Kabla ya kuvuna mfugaji atashirikiana na Afisa Muidhiniwa ili kujiridhisha kwamba mifugo yake haina maradhi au magonjwa ya kuambukiza. (2) (3) Wakati wa uvunaji wa mifugo, mfugaji anaweza kuuza wanyama hai au kwa kuchinja na kuuza nyama. Makosa 18 . Mtu atakuwa ametenda kosa endapo:- (a) bila sababu za msingi atashindwa au kukataa kuchanja mifugo yake ili kuzuia magonjwa; 10 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) (b) bila sababu za msingi atazembea au kushindwa kutoa taarifa juu ya ugonjwa wa mifugo au; (c) atamzuia Afisa Muidhiniwa au Afisa Ugani kutekeleza majukumu yake. SEHEMU YA TATU SKIMU ZA UMWAGILIAJI 19 . Wajibu wa Halmashur i katika Skimu za umwagiliaj i Katika Halmashauri itakuwa na wajibu wa: kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, (a) kuanzisha skimu za umwagiliaji katika maeneo ya Vijiji ambayo upatikanaji wa maji siyo wa shida ili kuchochea kilimo cha umwagiliaji; (b) kugawa skimu za umwagiliaji zilizoanzishwa na Halmashauri kwa wananchi watakaoomba na kuahidi kutunza skimu hizo ili ziwe endelevu; (c) kutoa utaalam wa ugani na matumizi bora ya ili kuzifanya ziwe skimu za umwagiliaji endelevu; (d) kufanya ukarabati wa miundombinu katika skimu isipokuwa ukarabati utakaosababishwa na uharibifu wa makusudi, uzembe au matumizi mabaya ya skimu; (e) kumfutia kibali mtu yeyote ambaye atathibitika kutumia vibaya skimu na ambaye ataharibu au kukodisha kwa mtu mwingine bila ridhaa ya Halmashauri; (f) kushindanisha watumiaji wa kumpata za umwagiliaji mshindi atakayejulikana kama “mtunzaji na mtumiaji bora wa skimu” ambaye atapewa zawadi na Halmashauri; na skimu ili Maombi ya Kibali 20 . (g) kutoa, kufuta, kubatilisha au kusimamisha kibali cha utumiaji wa skimu. Kabla ya kupewa kibali cha utumiaji wa skimu ya umwagiliaji, mwombaji atalizimika kulipa ada ya utunzaji wa skimu itakayopangwa na Halmashauri ambayo italipwa kila mwaka kama ilivyoanishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi. Ukaguzi 21 (1) Afisa mwidhiniwa, Afisa Ugani au Afisa yoyote wa 11 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) . Halmashauri anaweza kuingia kwenye skimu muda wowote wakati wa saa za kazi ili kufanya ukaguzi. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Afisa Mwidhiniwa. Afisa Ugani au afisa yeyote wa Halmashauri anaweza kufanya ukaguzi baada ya saa za kazi na baada ya kupata kibali cha maandishi cha Mkurugenzi. 22 . Wajibu wa watumiaji skimu za umwagiliaj i Mtumiaji wa skimu za umwagiliaji atakuwa na wajibu wa:- (a) kutunza, kulinda, kuhifadhi na kuheshimu za iliyoko katika skimu miundombinu umwagiliaji; (b) kutoa taarifa za uharibifu wa miundombinu ya skimu kila inapotokea; (c) kulipia kibali na ada za skimu kila mwaka kwa kadri itakavyopangwa na Halmashauri; (d) kujiunga na umoja wa skimu au chama cha watumiaji wa skimu katika skimu ambayo yeye ni watumiaji; (e) kufanya ukarabati wa skimu kwa uharibifu ambao umesababishwa na uzembe au matumizi mabaya ya miundombinu ya skimu; (f) kulipa fidia ya gharama kwa Halmashauri endapo Halmashauri ukarabati uharibifu uliosababishwa na uzembe na matumizi mabaya; itafanyia (g) kuwaruhusu maafisa wa Halmashauri na kuwapa ushirikiano wakati wowote wanapotaka kuingia au kukagua miundombinu ya skimu; (h) kushirikiana na Halmashauri au kijiji wakati wowote kunapotokea haja ya kuboresha miundombinu ya skimu ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwenye skimu (i) kulinda vyanzo vya maji ambavyo vinaingiza maji katika skimu za umwagiliaji;- (j) kutochepusha maji kwa sababu yoyote au kwa namna yoyote bila ruhusa ya Halmashauri;na 12 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) Makosa 23 . (k) kutopanda miti au mimea yoyote ambayo inaweza kusababisha hasara au uharibifu au kuhatarisha miundombinu ya au kupunguza kina cha maji katika skimu. skimu Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo;- (a) ataharibu miundombinu iliyopo kwenye skimu za umwagiliaji; (b) bila sababu za msingi atashindwa kukarabati skimu kwa uharibifu miundombinu ya uliotokana na uzembe au matumizi mabaya ya miundombinu hiyo; (c) atashindwa au atakataa kulipia leseni na ada ya skimu; (d) atachepusha maji kutoka kwenye vyanzo vya maji bila kibali cha Halmashauri; au (e) atapanda miti inayoweza kusababisha hasara, kuhatarisha au kuharibu miundombinu ya skimu. au mimea SEHEMU YA NNE UFUGAJI WA SAMAKI Ufugaji wa samaki 24 . Halmashauri kulingana na jiografia yake, sayansi yake ya udongo, upatikanaji wa maji na mvua itakua na wajibu wa kuhamasisha Serikali za Vijiji na wananchi kwa ujumla kuanzisha ufugaji wa samaki wa kisasa katika eneo lake. Wajibu wa Halmashau ri 25 . Halmashauri itakuwa na wajibu wa kwamba: kuhakikisha (a) inaanzisha mabwawa ya mfano ya samaki katika kila kata; (b) inawezesha upatikanaji wa maafisa ugani wa uvuvi kwenye kata na vijiji; (c) vifaranga ili samaki kupandikizwa katika mabwawa ya wananchi, vinapatikana vya 13 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) kata, vijiji, na vitongoji. Wajibu wa Halmashau ri ya Kijiji 26 . Katika kutekeleza azma na dhamira ya kuhamasisha ufugaji wa samaki, Halmashauri ya kijiji itahakikisha: (a) inatenga ardhi ya kuanzishia mabwawa ya mfano au mashamba darasa ya ufugaji wa samaki; (b) inashirikiana na Halmashauri kuanzisha mafunzo ya nadharia na vitendo kuhusiana na ufugaji bora wa samaki; (c) inatunga Sheria Ndogo ya Kijiji kuhimiza ufugaji na uvuvi bora wa samaki; (d) inaanzisha vikosi vya kulinda na kuhifadhi rasilimali za fukwe za ziwa na mabwawa. Wajibu wa Afisa uvuvi 27 . Kila Afisa uvuvi wa kata au kijiji atakuwa na jukumu la; (a) kuanzisha rejesta ya orodha ya wafugaji wote wa samaki katika kata au kijiji; (b) kupanga ratiba ya kuwatembelea wafugaji wa samaki katika kata au kijiji; (c) kuanzisha orodha na idadi ya mabwawa ya samaki na aina ya samaki katika kila bwawa katika kata au kijiji; (d) kuanzisha mashamba darasa au mabwawa ya mfano kwa ajili ya kutolea mafunzo ya nadharia na vitendo; (e) kuhakikisha upatikanaji wa vifaranga na mbegu bora ya samaki; (f) kuanzisha programu ya kuvuna au kuvua samaki wakubwa wanaowala samaki wadogo 14 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) katika mabwawa; (g) kuanzisha programu ya kuangamiza magugu maji katika mabwawa; (h) kuandaa programu ya uendelezaji na ukuzaji wa kilimo cha ufugaji wa samaki katika kata au kijiji; (i) kuhakikisha wafugaji wa samaki wanatumia nyavu sahihi wakati wa kuvuna katika ili kutoharibu mazalia na mabwawa yao kutovuna samaki wadogo; (j) kudhibiti uvuvi haramu na uvuvi holela katika eneo lake. Makosa 28 . Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo;- (a) atatumia nyavu zisizo sahihi zinazoharibu mazalia ya samaki; na (b) kuvuna samaki wadogo ambao hawajafikia Ufugaji wa Nyuki 29 . umri wa kuvunwa. SEHEMU YA TANO UFUGAJI WA NYUKI Katika kukuza na kuendeleza ufugaji bora na wa kisasa wa nyuki Halmashauri itakuwa na wajibu ufuatao; (a) kuhakikisha kunakuwepo mtaalamu wa nyuki katika kila kata au kijiji; (b) kutoa elimu ya ufugaji wa nyuki; (c) kuhamasisha na kuanzisha vikundi vya wafugaji wa nyuki katika kata na vijiji; (d) kutoa elimu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira; (e) kurahisisha upatikanaji wa miche bora ya miti ya asili au ya kisasa itakayotoa maua mengi ambayo nyuki watatumia kutengeneza asali; (f) kusambaza bure au kwa bei rahisi miche ya miti kwa wakulima; (g) kuhakikisha upatikanaji wa dawa baridi za kurinia asali ambazo haziui nyuki wala kuharibu mazalia au masega yao; 15 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) (h) kutengeneza mizinga bora ya mfano kwa ajili ya ufugaji wa nyuki na kufundishia; (i) kuwezesha upatikanaji rahisi wa zana na vifaa vya kisasa vya kuvunia asali; (j) kuwatafutia wafugaji soko la uhakika la asali; (k) kuwasaidia wakulima walioko katika vikundi kuanzisha vituo vya kukusanyia na kuuza asali; (l) kuanzisha mashamba darasa ya ufugaji wa nyuki na hifadhi ya mazingira; (m) kuzihamasisha shule za Sekondari na za Msingi kuanzisha miradi ya ufugaji wa nyuki; (n) kufanya tathmini ya kila mwaka ya ukuaji wa sekta ya ufugaji wa nyuki; (o) kuwapatia maofisa ugani vyombo vya usafiri ili kuwapa unafuu wa kuwatembelea wafugaji; (p) kuwezesha vikundi vya wafugaji wa nyuki kuhudhuria maonesho ya siku ya wakulima nane nane ili kuonesha bidhaa ya maonesho katika kanda husika; (q) kuwashawishi wananchi kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa ili kukuza mitaji; (r) kutenga maeneo maalum ya ardhi kwa ajili ya wafugaji wa nyuki; (s) kuhakikisha upatikanaji wa zihusianazo na ufugaji wa nyuki; pembejeo Wajibu wa Halmashau ri ya Kijiji 30 . Kila Halmashauri ya Kijiji ambayo wananchi wake wanafuga nyuki itakuwa na wajibu wa: (a) kutenga maeneo maalumu ya ufugaji wa nyuki; (b) kuanzisha daftari litakalokuwa na orodha ya wafugaji wa nyuki kijijini; (c) kuanzisha vikundi na vyama vya kuhifadhi mazingira vitakavyokua na jukumu la:- (i) kuhimiza upandaji miti, (ii) kuzima moto au kupambana na wachoma moto; (iii) kupambana na kuzuia uvunaji au urinaji wa asali wa kutumia moto. (d) kutunga Sheria Ndogo za Kijiji kuhamasisha hifadhi ya mazingira na ufugaji bora wa nyuki. Wajibu wa Afisa 31 Kila Afisa Nyuki wa kata au kijiji atatakiwa kufanya yafuatayo:- 16 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) Nyuki . (a) atakuwa ndiye Afisa Mwidhiniwa wa masuala ya nyuki katika kata au kijiji; (b) atatunza orodha ya wafugaji wote wa nyuki katika Kata au kijiji; (c) atatunza orodha ya vikundi vyote vya wafugaji wa nyuki katika kata au kijiji; (d) atatoa mafunzo elekezi ya ufugaji bora wa nyuki katika kata au kijiji; (e) ataanzisha mashamba darasa ya ufugaji wa nyuki katika kata au kila kijiji; (f) atahakikisha upatikanaji wa pembejeo zote zihusianazo na ufugaji wa nyuki; (g) ataandaa ratiba ya kuwatembelea wafugaji wa nyuki waliomo katika kata yake au kijiji chake; (h) atahamasisha upandaji wa miti ili kurahisisha upatikanaji wa maua yanayotumiwa na nyuki kutengeneza asali. Wajibu wa Mfugaji wa Nyuki 32 . Kila mfugaji wa nyuki atakuwa na wajibu ufuatao:- (a) kutumia mizinga ya kisasa ya kufugia nyuki; (b) kulima asali kwa katumia njia za kisasa badala ya kutumia moshi au moto; (c) kuhifadhi mazingira kwa kutochoma moto misitu; (d) kujiunga katika vikundi vya uhifadhi wa mazingira; (e) atajiunga na vyama vya kuweka na kukopa vya wafugaji wa nyuki; (f) kutumia dawa isiyoua nyuki wala kuharibu ubora wa asali wakati wa urinaji; (g) kutumia vyombo au vifaa vilivyo safi na salama kwa ajili ya kurinia na kuhifadhia asali; katika (h) kuhudhuria mafunzo yatolewayo mashamba darasa ya ufugaji wa nyuki; Makosa 33 . Mtu yeyote atakua ametenda kosa endapo: (a) atalima asali kwa kutumia moto au moshi; (b) atauza asali iliyorinwa kwa moto au moshi; 17 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) (c) atachanganya au amechanganya asali na vitu vingine ambavyo siyo asali; (d) atachoma moto msitu au eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya wafugaji wa nyuki; (e) atakata miti bila kuwa na kibali kutoka Halmashauri; (f) atang’oa miti iliyopandwa kwa ajili ya kuhifadhi mazingira; (g) atatenda jambo lolote ambalo linadhuru au linahatarisha maendeleo na ukuaji wa kilimo cha nyuki; (h) atatenda kitendo chochote kinachohatarisha upatikanaji wa asali yenye ubora na salama; (i) atahujumu miundombinu ya ufugaji wa nyuki ya shule, kikundi, kijiji, kata, taasisi na mtu binafsi; SEHEMU YA SITA MASUALA MENGINEYO Halmashauri itakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba barabara za Halmashauri zinapitika wakati wote ili kuwezesha usafirishaji na usambazaji wa pembejeo na mazao. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hizi atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi sita kumi na mbili au vyote kwa pamoja yaani faini na kifungo. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi kiasi cha shillingi laki mbili endapo atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. ______________ JEDWALI LA KWANZA ________________ ADA YA UTUNZAJI SKIMU (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 20) 18 Wajibu wa kuimarisha miundombi nu Adhabu Kufililisha kosa 34 . 35 . 36 . Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) Na 1 2 3 Aina ya Mtumiaji Skimu Ada kwa Mwaka Mkulima ekari chini ya Tano Mkulima ekari zaidi ya Tano na zisizozidi ekari ishirini Mashamba ya Taasisi binafsi Tshs 60,000/- Tshs 120,000/- Tshs 240,000/- _____________ JEDWALI LA PILI ____________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 36) HATI YA KUFILILISHA KOSA Mimi ………………………..nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………….ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, kwamba tarehe……ya mwezi …mwaka……nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha ………..cha Sheria Ndogo za Kilimo na Usalama wa Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima za Mwaka 2020. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri, niko tayari kulipa kiasi cha shillingi laki mbili na kutimiza wajibu wangu badala ya kushitakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWAHIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi………Mwaka ……… Jina…………………………………….. Saini……………………………………. Mbele ya:…………………………. Cheo: …………………………… Saini: …………………………… Tarehe………………………….. 19 Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo namba 1006 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima uliofonyika tarehe 08-09 mwezi Mei mwaka 2019 mbele ya:- ……………………………… ELIZABETH M. GUMBO MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA ……………………………… MH. DAUDI M. NYALAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA NAKUBALI ………………………………. MHE. SELEMANI S. JAFO (MB), WAZIRI WA NCHI – OR –TAMISEMI Dodoma Tarehe 28 Septemba, 2020 20
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za Kilimo na Hifadhi ya Chakula za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima za mwaka, 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in