AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kutoza shilingi 50,000 kwa mtu anayekiri kosa na kuwa tayari kutimiza wajibu wake; mtu huyo lazima ajaze fomu maalum ya Jedwali la Pili.
9. (1) Bila kujali masharti ya Sheria Ndogo hizi, Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kutoza kiasi cha shilingi elfu hamsini kwa mtu yeyote atakayekiri kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hizi na kuwa tayari kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi, (2) Mtu atakayekiri kosa chini ya kifungu kidogo cha (1) atatakiwa kujaza fomu maalum iliyoainishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. 4 Sheria Ndogo za Ushuru wa Huduma za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo Na 1007(Linaendelea) _______________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenezwa chini ya Kifungu cha 4(2)) Na. Kiasi cha Mapato halisi kwa Mwaka Kiasi(Tshs) cha malipo kwa mwaka (Tshs) 500,000/= hadi 1,999,999/= 2,000,000/= hadi 3,999,999/= 4,000,000/= hadi 5,999,999/= 6,000,000/= hadi 10,999,999/= 11,000,000/= hadi 20,999,999/= 21,000,000/= hadi 30,000,000/= 1 2 3 4 5 6 6,000/= 12,000/= 18,000/= 33,000/= 63,000/= 90,000/= _____________ JEDWALI LA PILI ______________ (Limetengenezwa chini ya Kifungu cha 9 (2)) FOMU YA KUFILILISHA KOSA Mimi…………………mwenye Na.…………………ninayefanya Simu biashara……………. katika eneo la ………….. lililopo katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, kwa hiari yangu mwenyewe nakiri kuwa Tarehe………Mwezi………… Mwaka…………. nilikiuka Kifungu cha………… cha Sheria Ndogo za Ushuru wa Huduma za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima za Mwaka 2020. Kwa hiyo, kwa hiari yangu mwenyewe na bila kushurutishwa na mtu yeyote nakubali kulipa kiasi cha shilingi ……………………………………. badala ya kushtakiwa Mahakamani na nipo tayari kutimiza wajibu wangu kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi iwapo Mkurugenzi ataamua kutekeleza madaraka yake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi. Jina……………………………………………………………………. Saini:…………………………Tarehe: ……………………………….. MBELE YANGU: Jina:…………………………………………………………………… Saini:…………………………………………………………………. Wadhifa:……………………………………………………………… 5 Sheria Ndogo za Ushuru wa Huduma za Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Tangazo Na 1007(Linaendelea) Tarehe:………………………………………………………………… Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima imebandikwa kwenye Sheria ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima uliofanyika tarehe 08-09 mwezi mei mwaka 2019 mbele ya:- ……………………………… Elizabeth M. Gumbo MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA ……………………………… Mh. Daudi M. Nyalamu MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA NAKUBALI ………………………………. Mhe. Selemani S. Jafo (Mb), WAZIRI WA NCHI – OR –TAMISEMI LS Dodoma Tarehe 28 Septemba, 2020 6