Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha za Mwaka 2020
This section gives the short title of the by-laws: the Siha District Council Markets and Fairs Tax By-laws, 2020.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha za Mwaka 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-laws: the Siha District Council Markets and Fairs Tax By-laws, 2020. These bylaws apply throughout the entire area of Siha District Council. Sehemu hii inafafanua istilahi zinazotumika katika Sheria Ndogo hizi. Halmashauri lazima kuanzisha, kuendesha na kusimamia masoko, pamoja na kusajili wafanyabiashara wote katika masoko yake. Halmashauri appoints a Market Officer to oversee market development and market operations, and may also hire an agent to run the market under agreed conditions.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha za Mwaka 2020
Showing 34 of 34
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-laws: the Siha District Council Markets and Fairs Tax By-laws, 2020.
1. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha za Mwaka 2020. Matumizi - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: These bylaws apply throughout the entire area of Siha District Council.
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Siha. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa
AI-assisted research summary: Sehemu hii inafafanua istilahi zinazotumika katika Sheria Ndogo hizi.
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo:- “dalali” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa za sokoni kwa njia ya mnada kwa niaba ya mwenye bidhaa kwa mujibu wa sheria na taratibu za soko; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Siha; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa mujibu Sheria Ndogo hizi; 1 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) “gazebo” maana yake ni kibanda chenye miguu ya chuma au plastiki au mbao ambacho juu yake kimefunikwa na paa la kitambaa au turubai au paa la aina yoyote; “gulio” maana yake ni soko la wazi linalofanyika kwa wakati maalumu kwa kibali maalumu cha Halmashauri; “kasha” maana yake ni kifaa maalumu cha kubebea au kuhifadhia bidhaa na mazao kama vile matenga, viroba, magunia, karatasi ngumu, masanduku na mbao; “soko” maana yake ni eneo maalumu la biashara lililotengwa na Halmashauri kwa matumizi ya kuuzia au kununulia bidhaa na ni pamoja na gulio; “meza au kizimba” maana yake ni kitu au kifaa kinachotumika kuweka bidhaa kwa ajili ya kuuza sokoni au gulioni; “mfanyabiashara” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa sokoni au gulioni kwa jumla au rejareja; “Mkuu wa Masoko” maana yake ni mtu yeyote aliyeteuliwa au aliyeajiriwa na Halmashauri kusimamia shughuli zote katika soko; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha; "mnada” maana yake soko la wazi ambalo mali au vitu mbalimbali vinauzwa kwa ushindani wa bei kwa kauli na kwa kibali maalumu cha Halmashauri; “wadau wa soko” maana yake ni mfanyabiashara binafsi, vikundi vilivyoandikishwa katika Kamati ya Wadau wa Soko au Gulio na kuwasilishwa kwa Mkuu wa Soko, au vyama vya ushirika vinavyofanya shughuli za biashara katika soko; “Wakala” maana yake ni mtu, kikundi, taasisi au 2 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) kampuni Halmashauri katika chanzo au vyanzo vya mapato; iliyopewa kazi ya kukusanya mapato ya “ushuru” maana yake ni tozo inayolipwa baada au kabla ya kupata huduma katika soko au gulio; “vikundi” maana yake ni vikundi vya ushirika vya vya wafanyabiashara wafanyabiashara vilivyosajiliwa au kuandikishwa na kuwasilishwa katika Kamati ya Soko au Gulio na kwa Mkuu wa Soko na kutambuliwa na Halmashauri; umoja wa vikundi au “zao” maana yake ni mavuno ya shambani au maliasili yanayoingizwa kwenye soko au ndani ya eneo la mamlaka ya Halmashauri. Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima kuanzisha, kuendesha na kusimamia masoko, pamoja na kusajili wafanyabiashara wote katika masoko yake.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa: (a) kuanzisha, kusimamia na kuendesha masoko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi; (b) kuendeleza masoko; (c) kusimamia usafi na usalama wa masoko; (d) kusimamia ufikishaji wa huduma za kijamii katika soko; (e) kugawa na kupangisha soko kwa vyumba, meza au vizimba; (f) kutenga maeneo kwa ajili ya magulio; na (g) kusajili wafanyabiashara wote katika masoko yote ya Halmashauri. Mkuu wa Masoko - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Halmashauri appoints a Market Officer to oversee market development and market operations, and may also hire an agent to run the market under agreed conditions.
5.- (1) Kutakuwa na Mkuu wa Masoko atakayeteuliwa na Halmashauri kwa ajili ya kusimamia shughuli za uendelezaji wa Masoko pamoja na: 3 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) (a) (b) (c) (d) (e) (f) (g) kukusanya ushuru na ada mbalimbali; kusimamia usajili wa wadau wa soko kwa kushirikiana na Kamati ya Wadau wa Soko; kuimarisha huduma za ulinzi, maji na umeme katika masoko; kusimamia usafi na uondoshaji wa taka katika soko; kuhakikisha kuwa bidhaa haziuzwi kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kwa shughuli hiyo; kuzuia ujenzi holela katika soko; na kutekeleza majukumu mengine yeyote atakayoagizwa na Halmashauri. (2) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo cha (1), inaweza kuajiri Wakala ambaye Halmashauri atawajibika kusimamia uendeshaji wa soko kwa niaba ya Halmashauri. (3) Wakala atakayeajiriwa chini ya kifungu kidogo cha (2) atasimamia shughuli za uendeshaji wa soko kwa kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika kifungu kidogo cha (1) na masharti ya mkataba wa uwakala kati yake na Halmashauri. Kamati ya Soko - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Kamati ya Wadau wa Soko itaundwa, kila kikundi cha ushirika kitakuwa na mwakilishi mmoja, na kamati itafanya vikao vya kila mwezi.
6.- (1) Kutakuwa na Kamati ya Wadau wa Soko ambayo itaundwa na wadau wa soko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi. (2) Kila kikundi cha ushirika katika soko kitakuwa na mwakilishi mmoja katika Kamati ya Wadau wa Soko. (3) Kamati ya Wadau wa Soko itatakiwa kuweka 4 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) utaratibu maalum wa kuwapata viongozi wake, kuwaondoa madarakani na uendeshaji wa shughuli zake na kuuwasilisha kwa Hlamashauri. (4) Vikao vya Kamati ya Wadau wa Soko vitafanyika mara moja kila mwezi. (5) Mkuu wa Masoko atakuwa Katibu katika vikao vyote vya Kamati ya Wadau wa Soko. Majukumu ya Kamati - 7 Verify source ↗
Kamati ya Wadau wa Soko itakuwa na majukumu
AI-assisted research summary: The Market Stakeholders Committee must carry out the listed duties for market operations.
7. Kamati ya Wadau wa Soko itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuhakiki biashara zinazoendeshwa katika soko; (b) kuboresha ustawi wa wadau wa soko; (c) kuhakikisha uwepo wa nidhamu katika shughuli za soko; (d) kuhakikisha wadau wote wa soko na gulio wanalipa ushuru na ada kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi; (e) kukuza na kuendeleza mfumo wa biashara; (f) kuhakikisha kila eneo la mdau na soko kwa ujumla linakuwa safi muda wote; na (g) kutekeleza kazi nyingine watakazoelekezwa na Mkuu wa Masoko kulingana na Sheria ndogo hizi. Kamati Ndogo - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Kamati ya Wadau wa Soko lazima iunde kamati ndogo zenye wajumbe wanne kutoka miongoni mwa wajumbe wake.
8.- (1) Kamati ya Wadau wa Soko itaunda kamati ndogo zenye wajumbe wanne kutoka miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Wadau wa Soko ambazo ni: (a) Kamati Ndogo ya Miundombinu na Usafi; (b) Kamati Ndogo ya Utawala na Biashara; na 5 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) Usajili wa wadau - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Wanataka kufanya biashara sokoni lazima wasajiliwe; baada ya usajili, mfanyabiashara hupata kibali cha biashara kutoka Mkuu wa Masoko na kibali hicho hutolewa baada ya kulipa ada na hudumu mwaka mmoja.
9.- (c) Kamati Ndogo ya Ulinzi na Usalama. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Kamati ya Wadau wa Soko inaweza kuunda kamati ndogo yoyote kwa kadri itakavyoona inafaa. (1) Mtu yeyote anayetaka kufanya biashara biashara katika eneo la soko atatakiwa kusajiliwa na Mkuu wa Masoko akishirikiana na Kamati ya Wadau wa Soko kwa lengo la kumtambua na kumworodhesha katika rejesta ya wadau wa soko. (2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1), kila mfanyabiashara atakayesajiliwa atapewa kibali cha kufanya biashara katika soko husika kutoka kama kwa Mkuu wa Masoko kilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi. (3) Kibali kitatatolewa kwa mfanyabiashara baada ya kulipa ada na kitadumu kwa muda wa mwaka mmoja tangu siku ya kutolewa na endapo atataka kuendelea na biashara katika soko atatakiwa kuomba kibali kingine kwa Mkuu wa Masoko. Utolewaji wa kibali kwa biashara ambazo hazikuwepo - 10 Verify source ↗
Mtu au mfanyabiashara yeyote ambaye anataka kufanya
AI-assisted research summary: Mtu au mfanyabiashara anayetaka kufanya biashara mpya au biashara isiyo na eneo ndani ya soko lazima aombe kibali kwa Halmashauri.
10. Mtu au mfanyabiashara yeyote ambaye anataka kufanya biashara ambayo awali haikuwepo au haikuwa na eneo ndani ya soko ataomba kibali kwa Halmashauri na masharti ya kifungu cha 9 yatatumika. Kufuta kibali - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: The Market Officer may cancel a permit after 30 days’ notice if stated grounds exist. A dissatisfied trader may object within 14 days, and the Director must decide the objection within 7 days.
11. - (1) Mkuu wa Masoko anaweza kufuta kibali kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hizi, baada ya kutoa notisi ya siku thelathini, endapo mwenye 6 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) kibali hicho: (a) (b) (c) (d) (e) atakuwa na malimbikizo ya ada au ushuru; atakuwa amesimamisha shughuli zake kwa miezi mitatu bila taarifa; atakuwa na mwenendo unaokiuka masharti ya Sheria Ndogo hizi; atawashawishi wafanyabiashara wengine kutofuata Sheria Ndogo hizi au kusababisha uvunjaji wa amani; au atatumia chumba, kibanda, meza au kizimba alichopanga kinyume na madhumuni ya kufanyia biashara kama yalivyoainishwa kwenye mkataba wa upangishaji au maelekezo yatakayotolewa na Halmashauri. (2) Mfanyabiashara ambaye hatoridhika na uamuzi wa kufutiwa kibali anaweza kiuwasilisha pingamizi lake kwa Mkurugenzi katika kipindi cha siku kumi na nne tangu tarehe ya kufutiwa kibali. (3) Baada ya kupokea pingamizi, Mkurugenzi atatakiwa kutoa uamuzi wa pingamizi ndani ya siku saba tangu tarehe ya kupokea pingamizi husika. Wajibu wa mfanyabisha ra - 12 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara katika eneo la soko atakuwa na
AI-assisted research summary: Every market trader in the market area must register with the Market Officer, keep the market infrastructure safe, trade only in allowed areas, keep their area clean, pay taxes and fees on time, and follow the council’s layout conditions and instructions from the Council, Market Officer, and Market Stakeholders Committee.
12. Kila mfanyabiashara katika eneo la soko atakuwa na wajibu wa (a) kusajiliwa na Mkuu wa Masoko katika rejesta ya wadau wa soko; (b) kulinda na kuhifadhi miundombinu ya soko; (c) kufanya biashara katika maeneo yanayoruhusiwa; (d) kufanya usafi katika eneo lake la biashara; 7 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) (e) kulipa ushuru na ada kwa wakati; (f) kutobandika au kutobandua tangazo bila idhini ya Mkuu wa Masoko; (g) kutotumia lugha ya matusi, kuudhi au kashfa katika eneo la soko; (h) kushiriki usafi wa jumla wa soko; (i) kutoweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la soko; (j) kutofanya shughuli za kisiasa katika eneo la soko; (k) kutotupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; (l) (m ) kutowasha moto maeneo yasiyohusika ndani ya soko; na kuheshimu masharti ya upangaji aliyopewa na Halmashauri na maelekezo atakayopewa na Halmashauri, Mkuu wa Masoko na Kamati ya Wadau wa Soko. Muda wa biashara - 13 Verify source ↗
Section 13
AI-assisted research summary: The market must stay open every day from 12:00 a.m. to 12:00 p.m. The market chief may close it for maintenance or other emergencies, but maintenance closure needs seven days’ notice to market stakeholders unless there is another emergency reason.
13. - (1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. (2) Mkuu wa Masoko, kwa kushauriana na Mkurugenzi, anaweza kufunga soko kwa ajili ya matengenezo au sababu nyingine yoyote ya dharura pale itakapoonekana inafaa. (3) Isipokuwa kwa sababu nyingine za dharura, Mkuu wa Soko hatakuwa na mamlaka ya kufunga soko kwa sababu za matengenezo isipokuwa tu baada ya kutoa notisi ya siku saba kwa wadau wa soko kuhusu kusudio la kufunga soko kwa ajili ya matengenezo. 8 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) Ushuru wa soko au gulio - 14 Verify source ↗
Section 14
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itozeshe ushuru wa soko au gulio kwa wafanyabiashara waliosajiliwa, na pia ushuru pamoja na ada ya kibali kwa baadhi ya miundombinu ya biashara iliyo nje ya soko.
14. - (1) Halmashauri itatoza ushuru wa soko au ushuru wa gulio kutoka kwa kila mfanyabiashara aliyesajiliwa kufanya biashara katika eneo la soko au gulio kwa kadri itakavyokuwa. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Halmashauri itatoza ushuru na ada ya kibali cha kuweka kioski, kibanda, gazebo, konteina au genge la biashara lilio nje ya eneo la soko. Ushuru wa kupakua na kubeba mizigo - 15 Verify source ↗
Section 15
AI-assisted research summary: Magari yanayoingia eneo la soko au barabara za soko kwa ajili ya kupakua au kubeba mizigo yatazuiwa/kutozwa ushuru, na magari yanaruhusiwa kuingia kwa shughuli hizo kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.
15. - (1) Kutakuwa na ushuru utakaotozwa kwa kila gari litakaloingia ndani ya eneo la soko au barabara za soko kwa ajili ya kupakua au kubeba mizigo. (2) Magari yataruhusiwa kuingia katika eneo la soko kwa lengo la kupakua au kubeba mizigo kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. Ada ya pango - 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: Halmashauri inatoza ada ya pango kwa mfanyabiashara aliyesajiliwa katika eneo la soko, na inaweza kwa makubaliano maalum kuruhusu mtu kujenga banda la biashara huko.
16. - (1) Halmashauri itatoza ada ya pango la eneo la ambayo biashara katika italipwa na soko mfanyabiashara yeyote aliyesajiliwa kufanya biashara katika eneo la soko. (2) Halmashauri inaweza, kwa makubaliano maalum, kumruhusu mtu yeyote kujenga banda la biashara katika eneo la soko. Kibali cha minada na magulio - 17 Verify source ↗
Section 17
AI-assisted research summary: Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine inaweza kufanyika sokoni tu kwa kibali maalum cha Halmashauri; Halmashauri pia inaweza kutoa kibali cha magulio kufanyika katika maeneo itakayoyatenga.
17. - (1) Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine itaruhusiwa kufanyika kwenye masoko kwa kibali maalum cha Halmashauri. (2) Halmashauri inaweza kutoa kibali maalum cha katika maeneo kwa magulio kufanyika yatakayotengwa na Halmashauri. 9 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) Viwango vya ada na ushuru na muda wa kulipa - 18 Verify source ↗
Section 18
AI-assisted research summary: Halmashauri inatoza ada na ushuru kwa viwango vilivyo kwenye Jedwali la Pili; ada hulipwa kabla ya huduma kutolewa, ushuru hulipwa kabla au wakati wa kupata huduma, na Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru kuhusu namna ya kulipa.
18. - (1) Viwango vya ada na ushuru vitakavyotozwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi vitakuwa kama vilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. (2) Ada itakayotozwa chini ya Sheria Ndogo hizi italipwa kabla ya huduma kutolewa. (3) Ushuru unaotozwa chini ya Sheria Ndogo hizi utalipwa kabla au wakati wa kupata huduma. (4) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (3) cha Sheria Ndogo hizi, Halamashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru kuhusu utaratibu wa kulipa ushuru. Usafi wa soko - 19 Verify source ↗
Section 19
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wa soko lazima waweke eneo lao katika usafi wakati wote na wazingatie kanuni za afya.
19. - (1) Kila mfanyabiashara anayefanya biashara katika eneo la soko atawajibika kuweka eneo lake katika hali ya usafi wakati wote. (2) Mkuu wa Masoko kwa kushirikiana na Kamati ya Wadau wa Soko atasimamia usafi wa jumla wa soko siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi. (3) Kila mfanyabiashara atatakiwa kuzingatia kanuni za afya. Huduma ndani ya soko - 20 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara katika soko atatakiwa kugharamia
AI-assisted research summary: Kila mfanyabiashara katika soko lazima alipe gharama za ulinzi, usafi, maji na umeme kulingana na matumizi yake ya kila mwezi.
20. Kila mfanyabiashara katika soko atatakiwa kugharamia huduma ya ulinzi, usafi, maji na umeme kulingana na matumizi yake ya kila mwezi. Uingizaji wa bidhaa - 21 Verify source ↗
Section 21
AI-assisted research summary: Wakulima, wafanyabiashara, madalali na watu wengine hawaruhusiwi kuingiza sokoni bidhaa zilizofungwa kwa majani au zilizo haribika.
21. - (1) Bidhaa zote soko zitakazoingizwa zitatakiwa kuhifadhiwa kwenye makasha maalumu ya kusafirishia bidhaa. katika 10 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) (2) Ni marufuku kwa mkulima, mfanyabiashara, dalali au mtu mwingine yeyote kuingiza sokoni bidhaa zilizofungwa kwa majani au bidhaa zilizoharibika. Mifugo kutoingizwa sokoni - 22 Verify source ↗
Mtu yeyote hatoruhusiwa kuingiza mifugo katika eneo la
AI-assisted research summary: Hatutakiwi kuingiza mifugo katika eneo la soko, isipokuwa ndege na wanyama wadogo kama sungura wanaoletwa kwa ajili ya kuuzwa.
22. Mtu yeyote hatoruhusiwa kuingiza mifugo katika eneo la soko isipokuwa mifugo ya jamii ya ndege na wanyama wadogo kama sungura watakaoletwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa. Tahadhari ya moto - 23 Verify source ↗
Mtu yeyote hatoruhusiwa kufanya shughuli yoyote
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kufanya shughuli yoyote inayohusisha matumizi ya moto bila idhini ya maandishi ya Halmashauri.
23. Mtu yeyote hatoruhusiwa kufanya shughuli yoyote inayohusisha matumizi ya moto isipokuwa kwa idhini ya maandishi ya Halmashauri. Makosa na adhabu Kufililisha kosa - 24 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka au kwenda kinyume na kifungu
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayekiuka au kwenda kinyume na kifungu chochote cha Sheria Ndogo hizi anatenda kosa.
24. Mtu yeyote atakayekiuka au kwenda kinyume na kifungu chochote cha Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi laki mbili na isiyozidi Shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote faini na kifungo kwa pamoja. - 25 Verify source ↗
Bila kujali masharti ya kifungu cha 24, Mkurugenzi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote shilingi 200,000 ikiwa mtu huyo anakiri kosa kwa kujaza fomu ya Jedwali la Tatu.
25. Bila kujali masharti ya kifungu cha 24, Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote kiasi cha shilingi laki mbili endapo mtu huyo atakiri kosa kwa kujaza fomu iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hizi na kulipa kiasi hicho pamoja na ada au ushuru anaodaiwa iwapo kosa linahusisha kudaiwa ushuru au ada. _______________ 11 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) JEDWALI LA KWANZA _______ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 9 (2)) KIBALI CHA KUTUMIA SOKO/GULIO
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: The form asks for the applicant’s name.
1. Jina la Mwombaji ……………………………………………………………….. - 2 Verify source ↗
Anuani ya mwombaji ……………………………………………………………
AI-assisted research summary: This section refers to the applicant’s address.
2. Anuani ya mwombaji …………………………………………………………… - 3 Verify source ↗
Kibali cha ……………………………………………………………………………
AI-assisted research summary: 3. Kibali cha ……………………………………………………………………………
3. Kibali cha …………………………………………………………………………… - 4 Verify source ↗
Eneo ambalo kibali hicho kitatumika ………………………………………
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaonyesha eneo ambako kibali hicho kitatumika.
4. Eneo ambalo kibali hicho kitatumika ……………………………………….. - 5 Verify source ↗
Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe……………………hadi tarehe……………
AI-assisted research summary: Kibali kinaanza tarehe iliyowekwa na kinaisha tarehe iliyowekwa.
5. Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe……………………hadi tarehe…………… - 6 Verify source ↗
Masharti ya kutumia kibali hicho……………………………………………
AI-assisted research summary: Section 6 sets out the conditions for using the permit, but the text shown is incomplete.
6. Masharti ya kutumia kibali hicho…………………………………………….. (a) ……………………………………………… (b) ……………………………………………… (c) ……………………………………………… (d) ……………………………………………… (e) ……………………………………………… - 7 Verify source ↗
Tarehe ya kikao kilichoidhinisha kibali……………………………………………
AI-assisted research summary: This section is a heading about the date of the meeting that approved a permit.
7. Tarehe ya kikao kilichoidhinisha kibali…………………………………………….. Muhtasari Na.…………… - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: This schedule lists market-related fees and charges in Tanzanian shillings for different goods, stalls, loading/unloading vehicles, and market rents.
8. Imesajiliwa na: Jina ……………………………………… Saini…………………………………….. …………………………………… Mkuu wa Soko Saini ya Mwombaji Tarehe …………………………………. Tarehe ………………………….. Mhuri…………………………………… 12 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 18 (1)) Na. Aina ya ushuru Kiwango cha Ushuru (Tshs.) A. USHURU WA SOKO KWA KUTWA 1 3 4 7 8 9 10 11 Vizimba Baba/Mama Lishe Mitumba B. USHURU WA BIDHAA ZILETWAZO SOKONI KWA SIKU Kuanzia Kilo 50 Hadi 100 Dagaa Vitunguu Viazi mbatata Karanga Nazi Ushuru Wa Matenga/Boksi 12 Maembe 13 14 15 16 Papai Nyanya Ndizi Samaki wakavu 17 Mabungo 18 Samaki wabichi Ushuru Wa Viroba (Kg 50) 13 500 500 500 500 500 500 500 500 1000 500 500 500 1000 1000 1000 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) 19 20 Nyanya chungu Pilipili 21 Karoti 22 Matango 23 24 25 26 27 28 Ndimu Limau Pensheni Parachichi Peasi Embe 29 Machungwa 30 Viazi vitamu 31 Mihogo 32 33 34 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 Kunde Njegere Hoho C. USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIAMIZIGO SOKONI Chombo cha 1/2 tani (500kgs) Tani 1 Tani 1.5 Tani 2 Tani 3 Tani 4 Tani 15 Tani 7 Tani 8 – 10 Zaidi ya tani10 14 500 500 500 500 500 500 500 500 500 500 500 500 500 500 500 500 4,000 6,000 7,500 12,000 14,000 16,000 18,000 20,000 25,000 30,000 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) D. VIWANGO VYA KODI ZA PANGO SOKONI) 43 44 Vizimba Vibandavya kuku 45 Mama/Baba lishe 46 Viosk/Mabanda ya Mitumba Bucha n.k. 47 Maduka 48 49 Stoo Cold room 10,000 15,000 20,000 50,000 75,000 300,000 350,000 USHURU WA MAEGESHO SOKONI
Part
JEDWALI LA PILI
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Section 4 lists daily market fees for different vehicle types and mentions a shilingi 200,000 payment option instead of prosecution if the Director exercises the stated power.
4. Magari mkubwa Tani 7 na kuendelea 2000/= kwa siku Magari ya kati Magari madogo Pikipiki Tani 2-7 - Aina zote 1000/= kwa siku 500/= kwa siku 500/= kwa siku 15 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) _________ JEDWALI LA TATU (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 25) HATI YA KUFILILISHA KOSA ……………………………..…………………………… S.L.P. Mimi ……………………………………………. la ………………………………………………………………….. ikiwa ni kinyume na kifungu cha ……………… cha Sheria ya Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha za Mwaka 2020. kutenda nakiri kosa wa Kwa hiari yangu mwenyewe pasipo kushawishiwa na mtu yeyote nakubali kulipa kiasi cha shilingi laki mbili badala ya kushtakiwa Mahakamani iwapo Mkurugenzi atatekeleza madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha………………………………. cha Sheria Ndogo hizi. Saini: ………………………………………………... Tarehe …………………………………………………… Mbele yangu:- Jina: …………………………………………….….. Saini: …………………………………………….….. Wadhifa: ………………………………………………... Tarehe …………………………………………………… 16 Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha Tangazo la Serikali Na. 1044 (Linaendelea.) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Siha kilichofanyika tarehe 06 ya mwezi 3 mwaka 2019. NDAKI S. MHULI Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya SIHA GODSON J. NGOMUO Halmashauri ya Wilaya SIHA L.S NAKUBALI, Dodoma, SELEMANI S. JAFO (MB.) 2 Novemba, 2020 WN-OR-TAMISEMI 17
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za Ushuru wa Masoko na Magulio za Halmashauri ya Wilaya ya Siha za Mwaka 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in