AI-assisted research summary: Mwombaji must build the gas pipeline under the listed safety, technical, environmental, and route-control conditions.
3. Kibali cha Ujenzi kimetolewa kwa Mwombaji kujenga bomba la kusambaza gesi asilia lenye urefu wa 1 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji wa Gesi Asilia Kwa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania Maeneo ya Mwenge-Mbezi Beach Mkoa wa Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 343 (linaendelea) Ujenzi kilomita 12.4 na kipenyo cha milimita 63-250 lenyekiwango cha HDPE na vifaavyake kwa ajili ya kupeleka gesi asilia kwa wateja wa mahoteli na viwanda maeneo ya Mbezi Beach wilaya ya Kinondoni kwa vigezo na masharti ya fuatayo: (a) kuzingatia michoro, viwango vya kiufundi, na taratibu zilizoidhinishwa (usimikaji, ujenzi, uchomeleaji na upimaji) haki ya kutumia njia zilizotengwa au sheria nyingine zinazohusika; (b) kuhakikisha kuwa bomba la gesi asilia na vifaa vyake vinajengwa kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Taifa au sheria husika; (c) kuhakikisha kuwa ukaguzi wa bomba na vifaa vyake wakati wa ujenzi unafanyika kadri inavyohitajika ili kuhakikisha kuwa ujenzi, vifaa, uchomeleaji, maunganisho na ujaribuji wa bomba baada ya kukamilika unafanyika kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Taifa; (d) kuhakikisha kuwa bomba pamoja na vifaa vyake vinajengwa kwa kufuata mikuza iliyoidhinishwa kwa madhumuni ya kuepusha au kupunguza uwezekano wa hatari za mbeleni zitakazosababishwa na maendeleo ya viwanda au miji, kupanuliwa kwa njia na kutoharibu mazingira au sehemu za kihistoria; (e) kuhakikisha kuwa hakuna au kupunguza usumbufu kwa wakazi walio karibu na eneo la ujenzi na usalama kwa umma upewe kipaumbele. Endapo ulipuzi utafanyika, ufanywe kwa kuzingatia taratibu za kisheria zilizopo na kufanywa na mtu mwenye sifa za kazi ya ulipuzi kwa kuzingatia usalama kwa umma, mifugo, wanyama, majengo, 2 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji wa Gesi Asilia Kwa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania Maeneo ya Mwenge-Mbezi Beach Mkoa wa Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 343 (linaendelea) miundombinu ya simu, umeme, miundombinu ya chini ya ardhi na mali nyingine zilizo karibu na eneo kunakofanyika ulipuzi; (f) kuhakikisha kuwa zinakuwepo juhudi za kupunguza uharibifu kwenye ardhi na kuzuia mazingira yatakayosababisha kuziba kwa mifereji ya kupitisha maji na mmomonyoko wa udongo. Baada ya ujenzi, ardhi itapaswa kurudishwa katika hali iliyokuwepo kwa kadri itakavyowezekana; (g) kuhakikisha kuwa, ujenzi wa bomba linalokatisha reli, barabara, vijito, maziwa, mito na alama za usalama kama vile taa hauathiri vitu hivi kwa usalama wa umma. Kukatisha kwa bomba kwenye vitu hivi kutazingatia sheria zilizopo na makatazo ya wadhibiti kwenye eneo hili. Kabla ya ujenzi wa bomba unaokatisha maeneo tajwa, ni lazima uwepo utaratibu baina ya Mwombaji na wamiliki wa maeneo au miundombinu linakopita bomba; savei kuainishwa (h) kuhakikisha kuwa njia na linakopita bomba na imefanyiwa kuwekewa alama ambazo zitaendelea kuwepo wakati wote wa ujenzi kwa mujibu wa kibali kilichotolewa na mmiliki wa njia; (i) bomba litafuata mkuza ulioanishwa; (j) kuhakikisha kuwa urefu wa mfereji wa bomba ni sahihi kwa kuzingatia eneo, matumizi ya uso wa ardhi, hali ya ardhi na uzito utokanao na barabara na reli. Upana wa mfereji ni lazima uruhusu kuwekwa kwa bomba bila kuharibu rangi yake na kuwezesha kazi ya kupaka rangi na ufungaji wa bomba kufanyika ndani ya mfereji; 3 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji wa Gesi Asilia Kwa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania Maeneo ya Mwenge-Mbezi Beach Mkoa wa Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 343 (linaendelea) (k) kuchukua hatua zote stahiki ili kulilinda bomba na vifaa vyake dhidi ya mafuriko, udongo dhaifu, tetemeko la ardhi na hatari nyingine zinazoweza kusababisha bomba kuhama au kupata uzito wa ziada; (l) kuhakikisha kuwa bomba linalazwa umbali wa nchi 12 (milimita 300) kutoka kwenye miundombinu mingine iliyo chini ya ardhi ambayo haihusiani na gesi asilia. Endapo haitawezekana kupata umbali huu, bomba lilindwe dhidi ya uharibifu unaoweza kujitokeza kwa kuwa karibu na miundombinu mingine. Ni lazima uwepo umbali wa kutosha kutoka kwenye bomba na miundombinu mingine ya chini ya ardhi ili kuwezesha bomba kufanyiwa matengenezo na kulilinda dhidi ya uharibifu unaoweza kujitokeza kwa kuwa karibu na miundombinu mingine; (m) kuhakikisha kuwa vifaa vinavyotumika kwa ajili ya uchomeleaji ni vya ukubwa na aina sahihi kwa kazi hiyo vitakavyohakikisha uchomeleaji mzuri utakaowezesha bomba kuendelea kutumika na usalama wa watu; (n) kuzingatia viwango vya mazingira, afya na usalama vilivyoainishwa na sheria. Afya na usalama wa watu na vifaa vitapaswa kuzingatiwa na kuhakikisha matumizi ya vifaa vya usalama (PPE) wakati wote kama vile kofia ngumu, miwani na viatu vya usalama na matumizi ya kizima moto; (o) kuhakikisha kuwa miundombinu yote ya utoaji huduma kwa umma bila kujali kuwa inadhibitiwa na Mamlaka ama la inalindwa dhidi ya uharibifu na kuwaarifu wamiliki wake wawepo eneo la ujenzi wakati wa 4 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji wa Gesi Asilia Kwa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania Maeneo ya Mwenge-Mbezi Beach Mkoa wa Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na. 343 (linaendelea) kujenga; (p) kuhakikisha la kuwa limezungushiwa utepe wa tahadhari; eneo ujenzi (q) kuweka mifumo ya ulinzi na ufuatiliaji wa bomba ikiwemo mifumo ya kuzuia kutu, valvu za kuondoa mgandamizo, valvu za kujifunga, kipimo cha mgandamizo, mfumo wa kugundua uvujaji wa gesi, mfumo wa kusafisha na kufuatilia unene wa bomba na mifumo ya mawasiliano; (s) kuhakikisha (r) kuhakikisha alama mbalimbali kama vile za kuanisha mkuza, bomba na mapumulio zimewekwa eneo lote la bomba; na kuwa zilizowekwa zinakuwa na alama za onyo, taarifa ya tahadhari na namba za simu za dharula. Herufi kwenye taarifa ya tahadhari itaandikwa kwa rangi nyeusi kwa maneno “Onyo au rangi Tahadhari” kwenye ubao wenye nyekundu. alama Ukomo wa kibali