AI-assisted research summary: This provision lists technical requirements for a water well and says a commercial/community well registration certificate is valid for 12 months unless cancelled or extended.
3. Je muombaji amekidhi matakwa ya usajili wa kutoa huduma ya maji kwa jamii? Ndio Hapana Tarehe ya Kupokea: ………………………………... Imepokelewa na: ……………………… 16 Kanuni Za Maji Na Usafi wa Mazingira Za Visima vya Kibiashara Na Kijamii Tangazo la Serikali Na. 429 (Linaendelea.) Nambari ya Mwombaji: ………………………………… Saini: …………………………… Muhuri wa Ofisi ___________ JEDWALI LA PILI ___________ (Imetayarishwa chini ya Kanuni ya 4(b)(a) (Weka logo ya Mwenye leseni) Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira CHETI CHA USAJILI WA KISIMA CHA KIBIASHARA NA CHA KIJAMII CHETI NAMBARI ………………. Cheti cha usajili wa Kisima cha Kibiashara/kijamii kimetolewa kwa ……………………… wa sanduku la posta ………………… kutumia/kuendesha kisima namba ………………. Barabara ……………………… Wilaya …. Kwa ajili ya kutoa huduma za maji kuzingatia vigezo na matakwa yaliyopo kwenye kiambatisho. Cheti hiki kitaanza kutumika kuanzia …. Siku ya …………..,20 … na kitaendelea kutumika kwa kipindi cha miezi kumi na mbili (12), labda kifutwe au kuongezewa muda kama inavyoelekezwa katika Kanuni za maji na Usafi wa Mazingira (Kanuni za Huduma ya Maji Kutoka Visima Binafsi vya Maji), 2021 Tarehe ya kutolewa ………………. ……………………. Mkurugenzi Mtendaji _____________ JEDWALI LA TATU _____________ (Limetayarishwa chini ya Kanuni ya 7(h)) Mahitaji ya Kiufundi ya Kisima cha Maji Kisima cha maji kinatakiwa kiwe: (a) Kiwe mahali ambapo ni rahisi kufikika kwa aili ya kufanya ukaguzi, matengenezo, maboresho ya mitambo, kusafisha maji na kupima ubora wa maji. (b) Kisiwe ndani ya mzunguko wa mita 50 kutoka majosho ya ng’ombe, vyoo, mashimo ya maji machafu na sehemu nyingine hatari. Uchafu kutoka kwenye mashimo utupwe upande wa chini wa kisima ili kuzuia uchafuzi wa maji. (c) Kiwe na kina cha mita kumi na tano (d) Kichinbwe kwenye maeneo ambayo hakuna mafuriko wakati wa mvua au uchafuzi wa maji yanayotiririka na kijengwe kuepuka kuchafuliwa na mafuriko (e) Kijengwe sehemu yenye mwinuko kuepuka uchafuzi wa maji. 17 Kanuni Za Maji Na Usafi wa Mazingira Za Visima vya Kibiashara Na Kijamii Tangazo la Serikali Na. 429 (Linaendelea.) (f) Kiwe kimezungushiwa zege yenye upana wa centimita 15 na upana wa kisima uwe angalau sentimita sitini (60) pande zote za kisima kutoka katikati ya mfuniko. (g) Mfuniko wa kisima uwe angalau sentimita thelasini juu ya zege na chini la kisima (h) Kama pampu ya kutumbukiza majini itatumika, mfuniko wa kisima lazima uzibwe kikamilifu ili usiruhusu maji kuingia na ustahilimi mitikisiko au misukosuko ya ‘conductors or cables’ (i) Kuwe na mfumo wa mabomba ya kutolea maji: (i) Ulio na mabomba ya kufunga na kufungua (check valve, shutoff valve, pressure gauge) na mita ya maji ya kupima mwenendo au mtiririko wa maji; na (ii) Wenye ‘raw meter sampling tap’ kabla ya bomba la kutolea maji kutoka kwenye kisima; na (iii) Iwe imeunganishwa na sehemu ya kuhifandhia maji. Dodoma, ........................., 2023 JAMES A. MWAINYEKULE, Mkurugenzi Mkuu 18