Notisi ya uanzishwaji wa Kamati za Shule za Serikali ya Mwaka 2023
This section says the notice will be known as the 2023 Government School Committees Establishment Notice.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Notice
- Citation
- Notisi ya uanzishwaji wa Kamati za Shule za Serikali ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section says the notice will be known as the 2023 Government School Committees Establishment Notice. Hii notisi inatumika kwa shule za awali na za msingi za Serikali. This provision defines key terms used in the Notice, including district education officer, director, law, and government schools. The school committee’s membership is set out, the head teacher is the secretary, gender balance must be considered when appointing members, and the committee may allow non-voting participants in some meetings. Kila mujumbe wa Kamati ya Shule atakuwa ofisini kwa miaka minne kuanzia tarehe ya uteuzi, isipokuwa nafasi yake itakuwa wazi kwa sababu zilizotajwa katika aya ya 10.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Notisi ya uanzishwaji wa Kamati za Shule za Serikali ya Mwaka 2023
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Notisi hii
AI-assisted research summary: This section says the notice will be known as the 2023 Government School Committees Establishment Notice.
1. Notisi hii itajulikana kama kama Notisi ya uanzishwaji wa Kamati za Shule za Serikali ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Notisi hii itatumika kwenye Shule za awali na
AI-assisted research summary: Hii notisi inatumika kwa shule za awali na za msingi za Serikali.
2. Notisi hii itatumika kwenye Shule za awali na msingi za Serikali. Tafsiri Sura ya 353 - 3 Verify source ↗
Katika Notisi hii, isipokuwa muktadha ukihitaji
AI-assisted research summary: This provision defines key terms used in the Notice, including district education officer, director, law, and government schools.
3. Katika Notisi hii, isipokuwa muktadha ukihitaji vinginevyo- “Afisa Elimu Wilaya” maana yake afisa elimu yeyote wa Serikali aliyeteuliwa kusimamia huduma za elimu katika wilaya na inajumuisha mtu yeyote ambaye amekaimishwa majukumu yake; “Mkurugenzi” kuhusiana na Halmashauri ya Wilaya maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya; kuhusiana na Mamlaka ya Mji, Mkurugenzi wa Mji; kuhusiana na Halmasauri ya Manispaa, Mkurugenzi wa Manispaa; na kuhusiana na Halmashauri ya Jiji, Mkurugenzi wa Jiji; “Sheria” maana yake Sheria ya Elimu; na “Shule za Serikali” maana yake shule inayoendeshwa na kusimamiwa moja kwa moja na Wizara au mamlaka ya serikali za mitaa. 1 Notisi ya Masharti ya Uanzishwaji wa Kamati Za Shule Za Serikali Tangazo La Serikali Na. 420 (Linaendedelea) Muundo wa Kamati za Shule - 4 Verify source ↗
(1) Kamati ya Shule ya Serikali inajumuisha
AI-assisted research summary: The school committee’s membership is set out, the head teacher is the secretary, gender balance must be considered when appointing members, and the committee may allow non-voting participants in some meetings.
4.-(1) Kamati ya Shule ya Serikali inajumuisha (c) wa mwalimu wa taaluma shuleni; wajumbe wafuatao: (a) (b) mjumbe mmoja kutoka miongoni mwa wafanyakazi shule wanataaluma aliyeteuliwa na wanataaluma wa shule na endapo shule ina Kitengo kinachohusiana na wanafunzi wenye mahitaji maalumu, mkuu wa Kitengo anakuwa mjumbe; wajumbe wawili walioteuliwa na wazazi wenyewe kutoka miongoni mwa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo katika mkutano wa wazazi ulioratibiwa na shule ambapo mmoja kati yao lazima awe ni mzazi wa mwanafunzi mwenye mahitaji maalum kama yupo; wajumbe wawili wanaowakilisha wanajamii wa eneo ambalo shule ipo ambao watateuliwa na mkuu wa shule; na Afisa Elimu Wilaya anayehusika na elimu ya awali na msingi ambapo shule ipo au mwakilishi wake. (d) (e) (2) Mkuu wa shule atakuwa katibu wa Kamati. (3) Watu wanaohusika na uteuzi wa wajumbe watazingatia usawa wa jinsia wakati wa uteuzi wa wajumbe. (4) Kamati inaweza kuruhusu katika kikao chake chochote mjumbe/ wajumbe washiriki, kutegemeana na hoja ambayo itakuwa inajadiliwa na ambayo inahitaji uwepo wa mtu/watu wenye ufahamu na ujuzi maalumu ili kusaidia Kamati kufanya maamuzi sahihi ila mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura. Muda wa ujumbe - 5 Verify source ↗
Kila mujumbe wa Kamati ya Shule atakuwa katika
AI-assisted research summary: Kila mujumbe wa Kamati ya Shule atakuwa ofisini kwa miaka minne kuanzia tarehe ya uteuzi, isipokuwa nafasi yake itakuwa wazi kwa sababu zilizotajwa katika aya ya 10.
5. Kila mujumbe wa Kamati ya Shule atakuwa katika ofisi kwa kipindi cha miaka minne kutoka tarehe ya uteuzi isipokuwa pale ujumbe wake kwenye Kamati utakuwa wazi kwa sababu zilizoanishwa kwenye aya ya 10. sifa za uteuzi na uidhinishwaji - 6 Verify source ↗
Mtu atastahili kuteuliwa na kuidhinishwa kama
AI-assisted research summary: A person is eligible to be appointed and approved as a school committee member only if they meet the listed conditions.
6. Mtu atastahili kuteuliwa na kuidhinishwa kama mjumbe wa Kamati ya Shule kama- 2 Notisi ya Masharti ya Uanzishwaji wa Kamati Za Shule Za Serikali Tangazo La Serikali Na. 420 (Linaendedelea) taratibu ya uidhinishwaji wa wajumbe (a) ana angalau Cheti cha Elimu ya Sekondari; (b) ana kipato kinachotokana na shughuli halali; (c) sio Diwani, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji wa Kijiji au Mtaa ndani ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa; na (d) sio mdhibiti ubora aliye katika utumishi. - 7 Verify source ↗
(1) Mkuu wa Shule atakusanya majina na sifa za
AI-assisted research summary: Mkuu wa Shule lazima akusanye na kuwasilisha majina na sifa za wajumbe wa kamati ya shule kwa Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa kwa ajili ya kuidhinishwa. Mkurugenzi anaweza kukataa uteuzi usiozingatia Notisi hii au kuagiza uteuzi upya.
7.- (1) Mkuu wa Shule atakusanya majina na sifa za wajumbe wote wa kamati ya shule walioteuliwa katika namna iliyoainishwa na kuwasilisha kwa ajili ya kuidhinishwa kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambako shule ipo. (2) Mkurugenzi baada ya kupokea majina yaliyoteuliwa na sifa zao atakuwa na mamlaka ya- (a) kukataa uteuzi wa mjumbe ambaye hajafikia mahitaji ya Notisi hii; na (b) kuagiza kuteuliwa upya kwa wajumbe kama uteuzi wao uko kinyume na masharti ya Notisi hii. Utolewaji wa barua ya uteuzi - 8 Verify source ↗
Mkuu wa Shule baada ya kupokea barua ya
AI-assisted research summary: Mkuu wa Shule lazima atoe barua ya uteuzi kwa wajumbe walioidhinishwa baada ya kupokea barua ya kuidhinisha majina kutoka kwa Mkurugenzi.
8. Mkuu wa Shule baada ya kupokea barua ya kuidhinisha majina yaliyoteuliwa toka kwa Mkurugenzi, atatoa barua ya uteuzi kwa wajumbe walioidhinishwa. Mwenyekiti wa Kamati - 9 Verify source ↗
(1) Kamati ya Shule, katika kikao cha kwanza
AI-assisted research summary: Kamati ya Shule lazima ichague Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti katika kikao cha kwanza.
9.-(1) Kamati ya Shule, katika kikao cha kwanza itachagua Mwenyekiti na makamu Mwenyekiti wa Kamati. (2) Endapo Mwenyekiti hatokuwepo, Makamu Mwenyekiti ataongoza vikao vyote vya Kamati, na endapo wote wawili hawapo, wajumbe waliopo wanaweza kuchagua kutoka miongoni mwao Mwenyekiti kwa madhumuni ya kikao hicho. (3).Mwenyekiti Mwenyekiti waliochaguliwa hawatakiwi kuwa walimu wanaofundisha katika shule husika. Makamu na kusitisha ujumbe - 10 Verify source ↗
(1) Ujumbe katika Kamati ya Shule utasitishwa
AI-assisted research summary: Ujumbe wa Kamati ya Shule huisha pale mjumbe anapojiuzulu, kuacha mamlaka ya uteuzi, kuondolewa na mamlaka hiyo, kufariki, kupata ulemavu wa kudumu, au baada ya miaka minne tangu uteuzi.
10.-(1) Ujumbe katika Kamati ya Shule utasitishwa- (a) ambapo mjumbe atajiuzulu kwa hiari kwa kutoa angalau notisi ya siku kumi na nne kwa maandishi 3 Notisi ya Masharti ya Uanzishwaji wa Kamati Za Shule Za Serikali Tangazo La Serikali Na. 420 (Linaendedelea) inayoelekezwa kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa wa eneo husika; (b) kama mjumbe atakoma kuwa kwenye mamlaka ya uteuzi; (c) kama uteuzi wa mjumbe utaondolewa na mamlaka ya uteuzi; (d) kama mjumbe amekufa au kupata la kudumu kiasi cha kuondoa uwezo wake wa kutekeleza majukumu kama mjumbe; na tatizo majukumu ya Kamati ya Shule Sura ya 353 (e) katika kipindi cha kuisha miaka minne kutoka tarehe ya uteuzi. (2) Hata hivyo, mjumbe ambaye kipindi chake cha ujumbe kimefikia mwisho kutokana na ukomo wa muda anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine. (3) Kama nafasi yoyote itatokea katika ujumbe wa Kamati, Mkuu wa Shule ataratibu mchakato wa uteuzi wa mjumbe mpya kulingana na masharti yaliyoainishwa katika la aliyeteuliwa Notisi hii na baada ya kupokea atawasilisha kwa Mkurugenzi ili kuidhinishwa na mjumbe huyo mpya atakuwa mjumbe kwa kipindi kilichobaki baada ya kuondoka kwa mjumbe ambaye kwa nafasi yake ameteuliwa kuhudumu. jina - 11 Verify source ↗
Kwa mujibu wa kifungu cha 40(4) na (5) cha
AI-assisted research summary: Kamati ya Shule ina majukumu ya kusimamia masuala ya shule, ikiwemo nidhamu ya wanafunzi, maendeleo ya shule, fedha, miundombinu, usalama, usajili na mahudhurio, pamoja na vikao na taarifa zake.
11. Kwa mujibu wa kifungu cha 40(4) na (5) cha Sheria, Kamati ya Shule itakuwa na majukumu yafuatayo- (a) kuamua kuhusu kesi za nidhamu za wanafunzi; (b) kushauri kuhusu mpango wa maendeleo ya shule na mikakati ya utekelezaji; (c) kuwezesha uundwaji wa jukwaa la walimu na wazazi; (d) kuitisha vikao vya walimu na wazazi na kutoa taarifa ya masuala yanayohusiana na maendeleo ya shule; (e) kuidhinisha matumizi ya fedha na kusimamia matumizi ya fedha kwa maendeleo yenye ufanisi ya shule; (f) kusimamia ujenzi na ukarabati wa madarasa na miundombinu mingine ya shule; 4 Notisi ya Masharti ya Uanzishwaji wa Kamati Za Shule Za Serikali Tangazo La Serikali Na. 420 (Linaendedelea) (g) kuhakikisha shule ina miundombinu ya kujitosheleza ikijumuisha madarasa, ofisi, vyoo, maji safi, madawati, ardhi kwa ajili ya michezo na shughuli nyingine za Shule; (h) kuhakikisha kwamba eneo la shule limewekewa mipaka ya kutosha ikiwezekana kujumuisha na hati miliki; (i) kuhakikisha usalama na ulinzi wa wanafunzi, majengo ya shule na mali zake; (j) kuhakikisha matengenezo ya majengo ya shule na samani; (k) kuhakikisha kwamba wazazi na wanajamii wengine wanashiriki kwenye maendeleo ya shule; ya shule na (l) kuidhinisha bajeti ya mwaka matumizi ya fedha zote za shule; (m) kukusanya fedha na michango kwa ustawi wa shule; (n) kushauri kwenye Serikali ya Kijiji michango katika kila moja au kwa aina ya kufanywa na wanajamii ikijumuisha kwa njia ya kujisaidia mwenyewe; (o) kuhimiza usafi wa mazingira ya shule na usafi binafsi wa wanafunzi; (p) kusimamia ufundishaji na ujifunzaji fanisi katika shule; (q) kusimamia usajili wa wanafunzi na mahudhurio shuleni; (r) kuhakikisha kwamba shule ina huduma ya kwanza na kuhimiza elimu ya afya; na (s) kuhakikisha kwamba shule inatoa mwongozo na huduma za ushauri nasaha kwa wanafunzi. Vikao 12-(1) Kamati ya Shule itakutana kawaida mara nne kwa mwaka kwa ajili ya kutekeleza kazi zake katika muda na sehemu itakayotegemea kalenda ya Shule iliyoidhinishwa na Kamati kutokana na mapendekezo ya Shule yenyewe (2) Bila kujali masharti ya aya ndogo ya (1) Mwenyekiti anaweza kuitisha mkutano maalumu- 5 Notisi ya Masharti ya Uanzishwaji wa Kamati Za Shule Za Serikali Tangazo La Serikali Na. 420 (Linaendedelea) (a) baada ya kupokea ombi kwa maandishi kwa niaba hiyo ya wajumbe wasiopungua sita wa Kamati ya Shule wakieleza kwa kiundani lengo la kikao hicho na nakala ya notisi pamoja na dondoo itapelekwa pia kwa Katibu angalau siku tano kabla ya kikao hicho maalumu; na (b) baada ya kupokea notisi ya maandishi kutoka kwa Katibu wa Kamati ya Shule, kuhusu jambo lolote linalohitaji kuwasilishwa kwa haraka na kutolewa maamuzi na Kamati. (3) Katibu wa Kamati ya Shule,baada ya kushauriana na Mwenyekiti, ataitisha vikao vyote vya Kamati ya Shule, isipokuwa vile ambavyo vinaitishwa na Mwenyekiti kwa mujibu wa Notisi hii, kwa notisi ambayo itabainisha ajenda, mahali, tarehe na muda wa kikao, na notisi hiyo itatumwa kila mjumbe katika anuani yake ya kawaida kwa njia yoyote ikijumuisha njia ya kielectroniki angalau siku saba kabla ya tarehe ya kikao. (4) Akidi ya kikao cha Kamati ya Shule itakuwa zaidi ya nusu ya wajumbe wanaopiga kura pasipo kujumuisha Katibu. (5) Isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo, maamuzi ya wajumbe wengi wa Kamati ya Shule waliopo na waliokutana kikamilifu yatakuwa maamuzi ya kamati ya Shule. (6) Shule itagharamia gharama za uendeshaji wa vikao vyote vya Kamati ya Shule na gharama hizo zitakuwa ni sehemu ya bajeti itakayoidhinishwa na Kamati ya Shule baada ya kupokea mapendekezo kutoka kwenye Shule yenyewe. (7) Katibu ataweka na kutunza taarifa ya mienendo ya Kamati ya Shule, na kuzisambaza kwa wajumbe wake na Afisa Elimu Wilaya anayehusika. (8) Kwa kuzingatia vifungu vya Notisi hii, kamati ya inaweza kusimamia uendeshaji wa vikao vyake Shule yenyewe. (9) Isipokuwa pale ametangaza kuwa na maslahi, Mjumbe wa Kamati ya Shule hatashiriki katika majadiliano katika kikao au kufanya au kufanya maamuzi kuhusu masuala 6 Notisi ya Masharti ya Uanzishwaji wa Kamati Za Shule Za Serikali Tangazo La Serikali Na. 420 (Linaendedelea) yaliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Shule ambayo mwenza wake, ndugu wa damu, mbia au mwajiri, tofauti na serikali, au mbia au mwajiri wa mweza wake au ndugu wa damu au vinginevyo ana maslahi ya moja kwa moja au sio ya moja ya moja kwa moja. Kamati ndogo
Part
sehemu itakayotegemea kalenda ya Shule iliyoidhinishwa na
- 13 Verify source ↗
Kamati za Shule, katika kutekeleza kwa ufanisi
AI-assisted research summary: School committees must set up subcommittees, and the District Commissioner has authority to suspend or dissolve the School Committee.
13. Kamati za Shule, katika kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake, itaanzisha Kamati ndogo zifuatazo- (a) Kamati ndogo ya Taaluma, Unasihi, Ushauri na Ulinzi wa wanafunzi (b) Kamati ndogo ya Fedha, Mipango na Maendeleo ya Miundombinu; (c) Kamati ndogo ya Nidhamu, Ulinzi, Mazingira, Afya na Chakula; na (d) Kamati ndogo yoyote ili itakavyoonekana ni muhimu kutokana na mapendekezo ya Shule. Mamlaka ya Mkuu wa Wilaya kusimamisha au kuvunja Kamati ya Shule Kufutwa kwa T.S Na. 288 la mwaka 2002 - 14 Verify source ↗
Mkuu wa Wilaya anaweza, kama kwa maoni
AI-assisted research summary: Mkuu wa Wilaya anaweza, ikiwa anaona maslahi ya umma yanahitaji, kusimamisha Kamati ya Shule au kuagiza wajumbe wote au baadhi yao wajiudhuru na waliobaki wateuliwe mbadala.
14.- Mkuu wa Wilaya anaweza, kama kwa maoni yake maslahi ya umma yanahitaji- (a) kusimamisha Kamati ya Shule katika kutekeleza jukumu lake lolote au yote; au (b) Kuagiza kujiudhuru kwa wajumbe wote au mjumbe yeyote na kuagiza kuteuliwa mbadala wake au wao ili kujaza nafasi iliyobaki wazi kwa mujibu wa masharti ya Notisi hii. - 15 Verify source ↗
Notisi ya Uanzishwaji wa Kamati za Shule ya
AI-assisted research summary: Notisi ya Uanzishwaji wa Kamati za Shule ya mwaka, 2002 imefutwa.
15. Notisi ya Uanzishwaji wa Kamati za Shule ya mwaka, 2002 inafutwa. Dodoma, 8 Juni, 2023 ADOLF F. MKENDA Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia 7
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Notisi ya uanzishwaji wa Kamati za Shule za Serikali ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in