Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini kwa Jamii za mwaka 2023
This provision names the rules as the 2023 regulations on the duties of mineral licence holders to communities.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini kwa Jamii za mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision names the rules as the 2023 regulations on the duties of mineral licence holders to communities. These regulations apply to holders of mining licences specified in Part Four of the Act. This section defines key terms used in the regulations. Mmiliki wa leseni ya madini lazima aandae mpango wa wajibu kwa jamii kwa kushirikisha halmashauri ya kijiji au mtaa husika. Every district, town, municipal, or city council where mining activities take place must establish an expert committee.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini kwa Jamii za mwaka 2023
Showing 21 of 21
- 1 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: This provision names the rules as the 2023 regulations on the duties of mineral licence holders to communities.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini kwa Jamii za mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: These regulations apply to holders of mining licences specified in Part Four of the Act.
2. Kanuni hizi zitatumika kwa wamiliki wa leseni za madini zilizoainishwa katika Sehemu ya Nne ya Sheria. Tafsiri Sura ya 287 Sura ya 288 - 3 Verify source ↗
Tafsiri
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the regulations.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Kamati ya Wataalamu” maana yake ni Kamati ya Wataalamu kuhusu Wajibu wa Mmiliki wa Leseni ya Madini kwa Jamii itakayoanzishwa kwa mujibu wa kanuni ya 5; “Mamlaka ya Serikali ya Mtaa” maana yake ni: (a) halmashauri ya kijiji, halmashauri ya mji mdogo, kitongoji, halmashauri ya wilaya au mamlaka nyingine yoyote ya serikali za mitaa zilizoanzishwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya); au (b) kata, mtaa, halmashauri ya mji, halmashauri ya manispaa au halmashauri ya jiji iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji); Sura ya 123 “Sheria” maana yake ni Sheria ya Madini; 3 Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini Kwa Jamii Tangazo La Serikali Na. 409 (Linaendelea) “Tume” maana yake ni Tume ya Madini ambayo imeanzishwa chini ya Sheria; na “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya masula ya madini. SEHEMU YA PILI MPANGO WA WAJIBU WA MMILIKI WA LESENI YA MADINI KWA JAMII Uandaaji wa mpango
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Uandaaji wa mpango
AI-assisted research summary: Mmiliki wa leseni ya madini lazima aandae mpango wa wajibu kwa jamii kwa kushirikisha halmashauri ya kijiji au mtaa husika.
4.-(1) Mmiliki wa leseni ya madini atawajibika kuandaa mpango madhubuti wa wajibu wake kwa jamii kwa kushirikisha halmashauri ya kijiji au mtaa uliopo katika eneo lenye shughuli za madini kupitia halmashauri husika. (2) Mmiliki wa leseni ya madini atakuwa na wajibu wa kushirikisha halmashauri ya kijiji au mtaa uliopo eneo lenye shughuli za madini katika kuainisha vipaumbele vya jamii zilizopo au zinazozunguka eneo hilo kwenye zoezi la uandaaji wa mpango wa wajibu wake kwa jamii. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), miradi itakayoibuliwa na halmashauri ya kijiji au mtaa itapaswa kujadiliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata kwa kumshirikisha mmliki wa leseni ya madini na kisha kuwasilishwa kwenye halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji husika kwa ajili ya uchambuzi na uhakiki ifikapo mwezi Oktoba kila mwaka. (4) Kwa madhumuni ya kifungu cha 105(5) cha Sheria, lenye jamii zilizopo au zinazozunguka eneo shughuli za madini zitanufaika na mpango wa wajibu kwa jamii kwa utaratibu ufuatao: (a) kiasi cha asilimia 40 kitatengwa kwa ajili ya miradi ya kijiji au mtaa ambapo shughuli za madini zinafanyika; na (b) kiasi cha asilimia 60 kitatengwa kwa ajili ya miradi ya halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji husika ambako shughuli za madini zinafanyika. 4 Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini Kwa Jamii Tangazo La Serikali Na. 409 (Linaendelea) Kamati ya Wataalamu Muundo wa Kamati ya Wataalamu - 5 Verify source ↗
Kamati ya Wataalamu
AI-assisted research summary: Every district, town, municipal, or city council where mining activities take place must establish an expert committee.
5. Kila halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji ambako shughuli za madini zinafanyika itaunda kamati ya wataalamu itakayoitwa Kamati ya Wataalamu kuhusu Wajibu wa Mmiliki wa Leseni ya Madini kwa Jamii. - 6 Verify source ↗
Muundo wa Kamati ya Wataalamu
AI-assisted research summary: Kamati ya Wataalamu itaundwa kwa wajumbe waliotajwa katika kifungu hiki.
6. Kamati ya Wataalamu itaundwa na wajumbe wafuatao: (a) Mkurugenzi Mtendaji ambaye atakuwa Mwenyekiti; (b) Afisa Mipango ambaye atakuwa Katibu; (c) Afisa wa Tume wa eneo husika; (d) wawakilishi wawili wa mmiliki wa leseni ya madini; (e) mhandisi; (f) Wakili wa Serikali; (g) Afisa Mazingira; (h) Afisa Maendeleo; na (i) afisa kutoka katika mradi mahsusi Majukumu ya Kamati unaotekelezwa na mpango husika. - 7 Verify source ↗
Majukumu ya Kamati
AI-assisted research summary: Kamati lazima ichunguze, ifuatilie, isimamie na kuripoti utekelezaji wa miradi, kisha iwasilishe taarifa kwa halmashauri husika.
7.-(1) Kamati itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kupitia mipango, michoro, ratiba ya utekelezaji na masuala mengine yanayohusiana na wajibu wa mmiliki wa leseni kwa jamii na kuwasilisha kwa halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji; (b) kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa na wamiliki wa leseni inazingatia thamani ya fedha; (c) kusimamia ubora wa vifaa na miundombinu pamoja na ufanisi katika utekelezaji wa miradi; (d) kufuatilia na kuhakikisha miradi iliyoidhinishwa chini ya mipango inatekelezwa kwa wakati; (e) kufuatilia uzingatiaji katika utekelezaji wa sera ya mmiliki wa leseni kuhusu wajibu wake kwa jamii; ufanisi na (f) kutoa ushauri wa kitaalamu kwa watekelezaji wa miradi; na (g) kuandaa taarifa ya utekelezaji wa miradi na 5 Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini Kwa Jamii Tangazo La Serikali Na. 409 (Linaendelea) kuiwasilisha kwa halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji. (2) Kamati ya Wataalamu ya halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji husika itachambua na kuhakiki mpango uliowasilishwa chini ya kanuni ndogo ya (1) ndani ya muda wa siku kumi na nne tangu ulipopokelewa na kuuwasilisha katika halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji husika ukiwa pamoja na ushauri wa Kamati hiyo. - 8 Verify source ↗
Kuwasilisha mpango kwa halmashauri husika
AI-assisted research summary: Halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji lazima ichunguze na kupitisha mpango uliowasilishwa ndani ya siku saba; inaweza kuuleta pingamizi na kuurudisha kwa maboresho, na mmiliki wa leseni ya madini lazima autengeneze upya na kuuwasilisha tena.
8.-(1) Kila halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji itapitia na kupitisha mpango uliowasilishwa ndani ya siku saba tangu ulipowasilishwa na Kamati ya Wataalamu, na iwapo haitaridhika na maudhui ya mpango huo, inaweza, kwa kuzingatia kanuni ya 10, kuukataa na kuelekeza mpango huo urejeshwe kwa mmiliki wa leseni ya madini kwa ajili ya maboresho. (2) Endapo halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji itaukataa mpango na kuurejesha kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) itapaswa kuwasilisha kwa mmiliki wa leseni sababu za kuukataa mpango huo. (3) Mmiliki wa leseni ya madini atawajibika kuboresha mpango kulingana na maelekezo ya halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji na kwa mujibu wa masharti ya Sheria na kuwasilisha tena kwenye halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji husika. (4) Endapo kutakuwa na mkwamo wowote katika kuafikiana kati ya halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji husika na mmiliki wa leseni ya madini kuhusu uandaaji na upitishaji wa mpango, mkwamo huo utatatuliwa na Mkuu wa Mkoa katika halmashauri husika. - 9 Verify source ↗
Kuwasilisha mpango kwa Mawaziri
AI-assisted research summary: Section 9 sets a review-and-forwarding process for a community obligation plan, with deadlines for the council, ministers, and the license holder.
9.-(1) Endapo halmashauri husika itaridhika na maudhui ya mpango wa wajibu kwa jamii uliowasilishwa na mmiliki wa leseni ya madini, halmashauri hiyo itauwasilisha mpango huo kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya serikali za mitaa na Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha ndani ya siku thelathini tangu kupokelewa kutoka kwa mmiliki wa leseni ya madini. 6 Kuwasilisha mpango kwa halmashauri husika Kuwasilisha mpango kwa Mawaziri Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini Kwa Jamii Tangazo La Serikali Na. 409 (Linaendelea) (2) Waziri mwenye dhamana ya masuala ya serikali za mitaa kwa kushirikiana na Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha wataunda Kamati ya Pamoja ambayo jukumu lake litakuwa ni kuwashauri Mawaziri husika kuhusu mipango ya wajibu wa wamiliki wa leseni kwa jamii inayowasilishwa kwa ajili ya idhini. (3) Kamati ya Pamoja kuiwasilisha kwa Mawaziri, na iwapo Mawaziri- itaandaa taarifa na (a) wataridhika na maudhui ya mpango huo kulingana na Sera za Serikali za Mitaa na Sera za Fedha watawasilisha mpango huo kwenye halmashauri ndani ya kipindi cha siku kumi na nne tangu tarehe ya kuupokea mpango huo kutoka kwenye halmashauri; au (b) hawataridhika na maudhui ya mpango huo kulingana na Sera za Serikali za Mitaa na Sera za Fedha, wataurejesha mpango huo kwenye halmashauri ndani ya kipindi cha siku kumi na nne tangu tarehe ya kuupokea mpango huo ukiwa na maelekezo mahususi. (4) Bila kuathiri utaratibu ulioainishwa chini ya kanuni ndogo ya (1), (2) na (3) endapo utapita muda wa siku ishirini na moja bila halmashauri husika kupokea majibu tangu tarehe ambayo Mawaziri walipokea mpango huo, itahesabika kuwa mpango umeridhiwa na halmashauri itamjulisha mmiliki wa leseni kuendelea na utekelezaji kwa kuzingatia muda uliokubaliwa kwenye mpango. (5) Halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji itawasilisha mpango ulioridhiwa kwa mmiliki wa leseni ndani ya siku saba baada ya kuupokea kutoka kwa Mawaziri na mmiliki huyo atauwasilisha mpango huo kwenye Tume ndani ya siku saba tangu alipoupokea kutoka halmashauri husika. Vipaumbele vya jamii zilizopo katika eneo lenye - 10 Verify source ↗
Vipaumbele vya jamii zilizopo katika eneo lenye shughuli za madini
AI-assisted research summary: Mmiliki wa leseni ya madini na halmashauri husika lazima wahakikishe miradi chini ya mpango uliokubaliwa kwa pamoja inazingatia mazingira, jamii, uchumi, utamaduni, na vipaumbele vya jamii.
10. Mmiliki wa leseni ya madini na halmashauri husika watahakikisha kuwa miradi yote itakayotekelezwa chini ya mpango uliokubaliwa kwa pamoja- (a) inazingatia masuala ya kimazingira, kijamii, 7 Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini Kwa Jamii Tangazo La Serikali Na. 409 (Linaendelea) shughuli za madini Fedha za mpango Hesabu na ukaguzi wa fedha kiuchumi kitamaduni na vipaumbele vya jamii husika; kulingana na (b) inaweza kupimika kwa vigezo vya manufaa na mafanikio; (c) inatekelezeka; na (d) inakamilika ndani ya muda ulioafikiwa. SEHEMU YA TATU MASHARTI YA FEDHA
Part
SEHEMU YA TATU
- 11 Verify source ↗
Fedha za mpango
AI-assisted research summary: Mmiliki wa leseni ya madini lazima atenge fedha, agharamie miradi ya mpango wa wajibu kwa jamii, na atoe taarifa ya maandishi kwa halmashauri husika kuhusu malipo yaliyofanywa.
11. Mmiliki wa leseni ya madini atawajibika- (a) kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa wajibu kwa jamii zilizopo eneo lenye shughuli za madini kwa kila mwaka; (b) kugharamia miradi yote iliyo chini ya mpango wa wajibu kwa jamii kulingana na mpango uliokubaliwa; na na Tume (c) kutoa taarifa ya maandishi kwa halmashauri husika yote yaliyofanywa kwa wakandarasi, wakandarasi wadogo au washirika wengine waliotekeleza miradi. kuhusu malipo - 12 Verify source ↗
Hesabu na ukaguzi wa fedha
AI-assisted research summary: Tume inapaswa kukagua fedha za miradi ya wajibu kwa jamii, na mmiliki wa leseni ya madini lazima aripoti na kueleza sababu kwa halmashauri na Tume ikiwa fedha zilizotengwa hazikutumika.
12.-(1) Fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi chini ya mpango wa wajibu kwa jamii zitakaguliwa na Tume kulingana na viwango vya ukaguzi. (2) Endapo fedha zilizotengwa hazitatumika kwa namna yoyote ile, mmiliki wa leseni ya madini atakuwa na wajibu wa kutoa taarifa na sababu kwa halmashauri husika na Tume kuhusu fedha zilizotengwa kutokutumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi au miradi katika mwaka wa fedha husika. (3) Fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi au miradi iliyoafikiwa na mmiliki wa leseni na halmashauri ya wilaya, mji, manispaa au jiji kwa kila mwaka wa fedha, zitatolewa na kutumika ndani ya mwaka wa fedha husika, na endapo fedha iliyotengwa haikutumika 8 Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini Kwa Jamii Tangazo La Serikali Na. 409 (Linaendelea) katika mwaka wa fedha husika, fedha hiyo itatumika katika mwaka wa fedha unaofuata na haitaathiri miradi mingine iliyopangwa kutekelezwa katika mpango wa mwaka huo. Fedha za ziada - 13 Verify source ↗
Fedha za ziada
AI-assisted research summary: If project money remains after the work is completed, it must be used for other agreed projects. If the allocated funds are not enough to finish existing work, the license holder must reflect that amount in the next year’s plan.
13.-(1) Iwapo kutakuwa na kiasi cha fedha kitakachobaki baada ya kutekeleza mradi husika, kiasi hicho cha fedha kitatumika kugharamia miradi mingine inayokusudiwa kutekelezwa baada ya pande zote kufikia muafaka. (2) Endapo ambazo kutakuwa hazijakamilika katika utekelezaji wa mradi uliopo kwenye mpango kutokana na kiwango cha fedha kilichotengwa kutokutosheleza, mmiliki wa leseni atazingatia kiwango hicho cha fedha katika mpango wa mwaka unaofuata. kazi na Taarifa ya fedha na miradi - 14 Verify source ↗
Taarifa ya fedha na miradi
AI-assisted research summary: Mmiliki wa leseni ya madini lazima apeleke kwa Tume taarifa kuhusu fedha zilizotumika na miradi iliyotekelezwa kila robo mwaka na pia taarifa ya mwaka.
14. Mmiliki wa leseni ya madini atawajibika kuwasilisha kwa Tume taarifa kuhusu fedha zilizotumika na miradi iliyotekelezwa ndani ya siku kumi na nne kila baada ya robo ya mwaka wa kalenda na taarifa ya mwaka ndani ya siku sitini baada ya tarehe 31 Desemba. SEHEMU YA NNE UTEKELEZAJI WA MPANGO WA WAJIBU WA MMILIKI WA LESENI YA MADINI KWA JAMII Utekelezaji wa mpango
Part
SEHEMU YA NNE
- 15 Verify source ↗
Utekelezaji wa mpango
AI-assisted research summary: Mmiliki wa leseni ya madini lazima atekeleze mpango wa wajibu kwa jamii kwa kufuata taratibu za ununuzi, anaweza kuajiri mkandarasi au mtu mwingine, na lazima atoe taarifa ya utekelezaji kila robo mwaka kwa halmashauri husika na Tume.
15.-(1) Mmiliki wa leseni ya madini atawajibika kutekeleza mpango wa wajibu wake kwa jamii kwa kuzingatia taratibu za ununuzi na anaweza kumwajiri mkandarasi au mtu mwingine yeyote katika utekelezaji wa miradi iliyopo kwenye mpango. (2) Katika utekelezaji wa mpango mmiliki wa leseni ya madini atawasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango ya kila robo mwaka kwenye halmashauri husika na Tume. Usimamizi na ukaguzi wa utekelezaji wa mpango - 16 Verify source ↗
Usimamizi na ukaguzi wa utekelezaji wa mpango
AI-assisted research summary: Halmashauri na Tume lazima zisimamie na zifuatilie utekelezaji wa mpango; Halmashauri pia inaweza kukagua nyaraka na kupokea taarifa za msingi, na baadhi ya miradi hukaguliwa kila robo mwaka na taarifa kupelekwa kwa Tume.
16.-(1) Halmashauri itawajibika kusimamia utekelezaji wa mpango na itakuwa na haki zifuatazo: (a) kukagua mikataba yoyote, makadirio ya kiasi (BOQ) au nyaraka nyingine zinazohusiana na 9 Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini Kwa Jamii Tangazo La Serikali Na. 409 (Linaendelea) utekelezaji wa mpango; na (b) kupewa taarifa za msingi zinazohusiana na mpango kutoka kwa mmiliki wa leseni ya madini au mtu au kampuni inayohusika na utekelezaji wa mpango. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa wajibu kwa jamii itakaguliwa na halmashauri husika kila robo mwaka wa fedha na taarifa ya ukaguzi itawasilishwa kwa Tume. (3) Tume itawajibika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa mpango wa wajibu wa mmiliki wa leseni ya madini kwa jamii kwa mujibu wa Sheria. (4) Katika kutekeleza kanuni ndogo ya (1) na (2), ukaguzi kuhusiana na utekelezaji wa mpango utafanywa kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha na kazi iliyofanyika, na katika kuthibitisha na kupima kama mradi husika umejengwa kwa thamani fulani, vigezo vya bei na ubora vitatumika. (5) Mmiliki wa leseni ya madini na halmashauri husika wanapaswa kutunza taarifa za fedha zilizotolewa katika mpango wa wajibu wa wamiliki wa leseni kwa jamii na na kutekelezwa iliyotekelezwa kwa kipindi cha angalau miaka mitano. kwenye miradi inayoendelea Utatuzi wa migogoro - 17 Verify source ↗
Utatuzi wa migogoro
AI-assisted research summary: Migogoro kati ya mmiliki wa leseni ya madini na halmashauri husika itatuliwa kwa mazungumzo ya amani; ikishindikana, mgogoro hupelekwa kwa Tume ndani ya siku 7, Tume uamue ndani ya siku 14, na upande usioridhika unaweza kukata rufaa kwa Waziri ndani ya siku 7.
17.-(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, endapo kutakuwa na mgogoro kati ya mmiliki wa leseni ya madini na halmashauri husika katika utekelezaji wa mpango, mgogoro huo utatatuliwa kwa njia ya mazungumzo ya amani. (2) Endapo pande zote zitashindwa kutatua mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo ya amani, upande usioridhika utawasilisha mgogoro huo kwa Tume ndani ya siku saba tangu waliposhindwa kuafikiana, na Tume itatoa uamuzi ndani ya siku kumi na nne. (3) Endapo kuna upande ambao hautaridhika na uamuzi wa Tume, upande huo utakuwa na haki ya kukata rufaa kwa Waziri ndani ya siku saba tangu tarehe ya uamuzi wa Tume, na Waziri atatoa uamuzi wake ndani ya siku 10 Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini Kwa Jamii Tangazo La Serikali Na. 409 (Linaendelea) thelathini. Elimu kuhusu wajibu wa mmiliki wa leseni Ukomo wa muda wa kutekeleza majukumu SEHEMU YA TANO MASHARTI YA JUMLA
Part
SEHEMU YA TANO
- 18 Verify source ↗
Elimu kuhusu wajibu wa mmiliki wa leseni
AI-assisted research summary: Halmashauri na mmiliki wa leseni ya madini, pamoja na wizara husika, lazima waelimishe umma kuhusu wajibu wa wamiliki wa leseni za madini kwa jamii angalau mara mbili kwa mwaka.
18. Kila halmashauri na mmiliki wa leseni ya madini kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya masuala ya madini watatoa elimu kwa umma angalau mara mbili kwa mwaka kuhusu wajibu wa wamiliki wa leseni za madini kwa jamii. - 19 Verify source ↗
Ukomo wa muda wa kutekeleza majukumu
AI-assisted research summary: Mmiliki wa leseni au halmashauri akichelewa kutekeleza jukumu kwa muda uliowekwa, anaweza kuomba nyongeza kwa Waziri na kutoa sababu; Waziri anaweza kuongeza hadi siku 30 au kukataa kwa sababu.
19.-(1) Endapo yeyote kati ya mmiliki wa leseni au halmashauri atashindwa kutekeleza majukumu ndani ya muda ulioainishwa chini ya Kanuni hizi, anaweza kuomba nyongeza ya muda kwa Waziri na kubainisha sababu za msingi za maombi ya nyongeza hiyo. (2) Waziri anaweza kuongeza muda ambao hautazidi siku thelathini au kukataa ombi hilo na atatoa sababu. (3) Endapo Waziri atakubali maombi ya kuongeza muda, mmiliki wa leseni au halmashauri atatakiwa kutekeleza jukumu hilo ndani ya muda utakaobainishwa na Waziri bila nyongeza nyingine. Miongozo au sheria ndogo za serikali za mitaa - 20 Verify source ↗
Miongozo au sheria ndogo za serikali za mitaa
AI-assisted research summary: Local governments must ensure any guidelines or subsidiary bylaws made under section 105 of the Act comply with these Regulations.
20. Miongozo au sheria ndogo zitakazoandaliwa na serikali za mitaa kwa mujibu wa kifungu cha 105 cha Sheria zitapaswa kuzingatia masharti ya Kanuni hizi. Makosa - 21 Verify source ↗
Makosa
AI-assisted research summary: A mining licence holder who fails to comply with the conditions set out under these Regulations commits an offence and is subject to action under section 63 of the Act.
21. Mmiliki wa leseni ya madini atakayeshindwa kutekeleza masharti yaliyoainishwa chini ya Kanuni hizi atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria na atachukuliwa hatua kwa mujibu wa kifungu cha 63 cha Sheria. Dodoma, 15th June, 2023 DOTO MASHAKA BITEKO Waziri wa Madini 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini kwa Jamii za mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in