Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za Mwaka 2023
Foreign exchange shops need the Bank’s license, must meet capital and filing requirements, and must follow rules on spot transactions, receipts, records, and remittance accounts.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This page preserves the statute’s identified version, provision structure, official source link, and stored legal text for reading and research.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za Mwaka 2023
Showing 1 of 1
- document Verify source ↗
Document text
AI-assisted research summary: Foreign exchange shops need the Bank’s license, must meet capital and filing requirements, and must follow rules on spot transactions, receipts, records, and remittance accounts.
Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) GOVERNMENT NOTICE No. 729 published on 6/10/2023 SHERIA YA FEDHA ZA KIGENI (SURA YA 271) ________ KANUNI ________ (Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 5(a) na 7) KANUNI ZA MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI ZA MWAKA 2023 MPANGILIO WA KANUNI Kanuni Jina SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI 1. Jina. 2. Matumizi. 3. Tafsiri. UTOAJI WA LESENI NA MATAKWA YA MTAJI SEHEMU YA PILI Jina la biashara. Idhini ya awali. 4. Katazo la kufanya biashara bila leseni. 5. Vigezo. 6. Maombi ya leseni. 7. 8. 9. Mapitio ya uamuzi wa Benki kukataa maombi. 10. Masharti baada ya idhini ya awali. 11. Ukaguzi kabla ya kuanza biashara. 12. Utoaji na uhalali wa leseni. 13. Ada ya mwaka. 14. Mabadiliko ya umiliki. 15. Matakwa ya mtaji. 16. Kufungua tawi. 17. Kuhamia duka la kubadilisha fedha Daraja A. 1 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) SEHEMU YA TATU MATAKWA YA UTOAJI WA LESENI YA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI LILILOANZISHWA NA HOTELI 18. Maombi ya leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni ya hoteli. SEHEMU YA NNE USIMAMIZI WA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI 19. Muundo wa uteuzi wa wajumbe wa bodi na wakurugenzi wakuu. 20. Majukumu ya Bodi. 21. Muundo na udhibiti wa ndani. SEHEMU YA TANO UENDESHAJI WA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI 22. Wigo wa uendeshaji. 23. Uhamisho wa biashara. 24. Kuonyesha viwango vya kubadilisha fedha, ada, tangazo, na leseni 25. Shughuli. 26. Amana ya dhamana. 27. Akaunti ya wateja. 28. Katazo la miamala isipokuwa ya papo kwa papo. 29. Kukataa kuuza. 30. Uuzaji wa fedha za kigeni kwa wasio wakazi. 31. Utumaji wa fedha kimataifa. 32. Taarifa za chanzo na madhumuni ya fedha za kigeni. 33. Ukusanyaji uwasilishaji na uhifadhi wa data. 34. Utambuzi na utoaji wa taarifa za miamala shuku. 35. Usiri wa miamala. SEHEMU YA SITA TAARIFA ZA FEDHA NA UKAGUZI 36. Taarifa za fedha. 37. Ukaguzi. SEHEMU YA SABA MASHARTI YA JUMLA 2 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) 38. Mafunzo 39. Kufunga biashara kwa hiari na kusalimisha leseni. 40. Adhabu za kiutawala. 41. Notisi ya kusitisha au kufuta leseni 42. Kufutwa. ________ JEDWALI ________ 3 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Jina Matumizi Tafsiri Sura ya 271 Sura ya 197 Sura ya 342 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI 1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za Mwaka 2023. 2. Kanuni hizi zitatumika kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni yaliyopatiwa leseni na Benki Kuu ya Tanzania kufanya biashara Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. 3.-(1) Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Sheria” maana yake ni Sheria ya Fedha za Kigeni; “Benki” maana yake ni Benki Kuu ya Tanzania iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania; “benki” itakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha; “Bodi” maana yake ni Bodi ya Wakurugenzi ya duka la kubadilisha fedha za kigeni; “tawi” maana yake ni eneo la biashara ya duka la kubadilisha fedha za kigeni tofauti na eneo kuu la biashara; “duka la kubadilisha fedha za kigeni” itakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria; “biashara ya duka la kubadilisha fedha za kigeni” maana yake ni biashara ya kubadilisha fedha za kigeni na biashara nyingine zozote zinazohusiana na fedha zilizoruhusiwa kwenye Sheria na Kanuni hizi; “duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A” maana yake ni duka la kubadilisha fedha za kigeni linalomilikiwa na wageni au wenyeji na limepewa leseni na Benki kufanya miamala ya fedha za kigeni ya papo kwa papo, kutuma fedha, na shughuli nyingine zozote za huduma za 4 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) kifedha; “duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja B” maana yake ni duka la kubadilisha fedha za kigeni lenye umiliki wa asilimia mia wa wanahisa wenyeji kufanya miamala ya papo kwa papo; “duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja C” maana yake ni duka la kubadilisha fedha za kigeni lililoanzishwa na hoteli kufanya miamala ya papo kwa papo kwa wateja wa hoteli tu; “taasisi ya fedha” itakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha; Sura ya 342 Sura ya 271 “akaunti ya fedha za kigeni” itakuwa na maana kama Sura ya 271 “fedha ya kigeni” itakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa ilivyotafsiriwa kwenye Sheria; kwenye Sheria; “hoteli” maana yake ni biashara inayotoa huduma za hoteli yenye hadhi ya nyota tatu au zaidi; “wakala wa kutuma fedha kimataifa” maana yake ni benki au taasisi ya fedha iliyoidhinishwa na Benki kufanya huduma za kutuma fedha kama wakala wa mtoa huduma za kutuma fedha kimataifa; “mtoa huduma ya fedha kwa njia ya simu” maana yake ni mtoa fedha za kielektroniki aliyepewa leseni na Benki ya kutoa huduma za fedha kwa kupitia mtandao wa simu; “mtaji wa wamiliki” maana yake ni kiasi cha fedha kinachomilikiwa na wamiliki wa duka la kubadilisha fedha za kigeni ikiwa ni tofauti kati ya mali na madeni; “eneo lililoainishwa” maana yake ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki au Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika; “mkazi” maana yake ni mtu ambaye anaishi, au ambaye kituo chake kikubwa cha maslahi ya kiuchumi kipo ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa kipindi cha miezi kumi na mbili mfululizo au zaidi; “muamala wa papo kwa papo” maana yake ni uuzaji au ununuzi wa fedha za kigeni ambao malipo hufanyika ndani ya siku hiyo hiyo kwa kutumia 5 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) pesa taslimu, benki, taasisi ya fedha, mtoa huduma wa fedha kwa njia ya simu au njia nyingine yoyote iliyoidhinishwa na Benki; (2) Katika Kanuni hizi, rejea ya kiasi chochote kwa Dola za Marekani, isipokuwa muktadha ukihitaji vinginevyo, itajumuisha rejea kwa kiasi sawa cha fedha yoyote ya kigeni au zote kwa pamoja. SEHEMU YA PILI UTOAJI WA LESENI NA MATAKWA YA MTAJI Katazo la kufanya biashara bila leseni 4.-(1) Mtu hataruhusiwa kufanya biashara ya duka la kubadilisha fedha za kigeni bila kuwa na leseni halali iliyotolewa na Benki. (2) Mtu atakayekiuka sharti la kanuni hii atakuwa anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kupewa adhabu kama ilivyoainishwa chini ya Sheria. Vigezo 5.-(1) Mtu atakuwa na vigezo vya kuomba leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni isipokuwa kama, mtu huyo; (a) ni yenye kampuni hisa iliyosajiliwa chini ya sheria za Tanzania Bara au Tanzania Zanzibar; ukomo wa Maombi ya leseni (b) hoteli iliyosajiliwa chini ya sheria za Tanzania Bara au Tanzania Zanzibar. 6.-(1) Mtu anayekusudia kuendesha duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A au Daraja B atatakiwa kuomba leseni kwa kuandika barua Benki. (2) Maombi hayo yatasainiwa na mkurugenzi na pale ambapo ni kampuni, wakurugenzi wasiopungua wawili, au mtu aliyeidhinishwa na mwombaji na yataambatishwa na- (a) nakala iliyothibitishwa ya azimio la bodi linaloidhinisha maombi; (b) Fomu A iliyoainishwa katika Jedwali ikiwa imejazwa kikamilifu; (c) nakala iliyothibitishwa ya cheti cha usajili; (d) nakala iliyothibitishwa ya katiba na kanuni za 6 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) (i) (ii) (iii) kampuni; (e) ushahidi kutoka kwa Msajili wa Makampuni kwamba mtaji uliolipwa usiopungua - (i) Shilingi za Tanzania bilioni moja umesajiliwa kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A lenye hisa zaidi zinazomilikiwa na wageni; (ii) Shilingi za Tanzania milioni mia tano kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A lenye hisa zaidi zinazomilikiwa na wenyeji; au (iii) Shilingi za Tanzania milioni mia mbili kwa duka la kubadilisha fedha ya kigeni Daraja B; (f) barua kutoka kwa wadhamini wawili ambao si ndugu wa mdhaminiwa wakithibitisha maadili mema na tabia ya kila mwanahisa wa mwombaji, mkurugenzi na mtendaji mkuu anayependekezwa; (g) nakala iliyothibitishwa ya ukurasa wa pasipoti wenye taarifa binafsi, kitambulisho cha taifa au cheti cha kuzaliwa kama uthibitisho wa uraia kwa kila mwanahisa, mkurugenzi na mtendaji mkuu anayependekezwa; (h) nakala iliyothibitishwa ya kibali cha ukazi kwa mwanahisa au mkurugenzi wa mwombaji asio raia wa Tanzania; (i) Fomu C iliyoainishwa katika Jedwali ikiwa imejazwa kikamilifu; (j) nyaraka za uthibitisho wa chanzo cha mtaji wa biashara inayopendekezwa; (k) uthibitisho wa malipo ya ada isiyorejeshwa ya maombi ya leseni ya Shilingi za Tanzania milioni moja; (l) muundo wa kiutawala unaopendekezwa na mwombaji; (m) wasifu binafsi uliojitosheleza na picha moja ndogo ya pasipoti ya hivi karibuni; (n) uthibitisho kwamba kiasi cha mtaji 7 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) (i) (ii) (iii) kisichopungua - (i) Shilingi za Tanzania bilioni moja umetengwa kwa ajili ya duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A lenye hisa zaidi zinazomilikiwa na wageni; (ii) Shilingi za Tanzania milioni mia tano kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A lenye hisa zaidi zinazomilikiwa na wenyeji; au (iii) Shilingi za Tanzania milioni mia mbili kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja B; na (o) taarifa ya historia ya ukopaji kwa kila mwanahisa, mkurugenzi na afisa mtendaji mkuu anayependekezwa. Jina la biashara 7.-(1) Mtu anayekusudia kuendesha duka la kubadilisha fedha za kigeni atajumuisha katika jina la biashara maneno yafuatayo: “bureau de change”, “forex bureau” au “foreign exchange bureau”. (2) Mabadiliko yoyote ya la kubadilisha fedha za kigeni yatasajiliwa kwa Msajili wa Makampuni na uthibitisho wa mabadiliko hayo utawasilishwa Benki ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kusajiliwa. la duka jina Idhini ya awali (3) Taarifa ya mabadiliko ya jina la duka la kubadilisha fedha za kigeni itaambatishwa na uthibitisho wa malipo ya ada isiyorejeshwa ya Shilingi za Tanzania milioni moja. 8.-(1) Benki itatakiwa, ndani ya mwezi mmoja baada ya kupokea maombi ya leseni yaliyokamilika, kutoa idhini ya awali au kukataa maombi. (2) Endapo maombi hayo yamekataliwa, Benki itamjulisha mwombaji kwa maandishi sababu za kukataliwa kwa maombi hayo. (3) Idhini ya awali iliyotolewa chini ya kanuni hii haitamaanisha mwombaji amepewa leseni ya biashara ya duka ya kubadilisha fedha za kigeni. 8 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Mapitio ya uamuzi wa Benki kukataa maombi Masharti baada ya idhini ya awali 9.-(1) Mwombaji ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa Benki uliotolewa chini ya kanuni ya 8 anaweza kuiomba Benki kufanya mapitio ya uamuzi wake ndani ya siku ishirini na moja tangu tarehe ya kupokea taarifa ya uamuzi. (2) Benki itatakiwa, ndani ya siku thelathini baada ya kupokea maombi chini ya kanuni ndogo ya (1), kupitia uamuzi wake na kumjulisha mwombaji kwa maandishi juu ya uamuzi wake wa mwisho. 10.-(1) Mwombaji wa la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A au Daraja B atatakiwa, ndani ya miezi sita baada ya kupewa idhini ya awali, kuwasilisha Benki yafuatayo- leseni ya duka (a) taarifa ya akaunti ya benki yenye jina la duka la kubadilisha fedha za kigeni inayothibitisha uwepo wa kiasi kilichotengwa kama mtaji uliolipwa kwa Shilingi ya Tanzania au kwa fedha ya kigeni; (b) uthibitisho wa malipo ya ada ya maombi ya leseni isiyorejeshwa ya Shilingi ya Tanzania milioni moja; (c) nakala iliyothibitishwa ya mkataba wa upangishaji au hati miliki yenye jina la mwombaji; la eneo kwamba (d) ushahidi biashara limewekwa kamera za usalama (CCTV) katika maeneo yote ya kimkakati, ikiwa ni pamoja na kaunta au vizimba vya kutolea huduma na sehemu za kupumzikia wateja; (e) taratibu za kimaandishi zinazoainisha namna ya kugundua na kutoa taarifa za matukio ya utakatishaji fedha kwa kuzingatia sheria na kanuni za kuzuia utakatishaji wa fedha haramu na upambanaji wa ufadhili wa ugaidi; na (f) sera za uendeshaji zitakazojumuisha masuala ya ya fedha, mawasiliano ya habari na kuzuia utakatishaji teknolojia hesabu za 9 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) wa fedha haramu na upambanaji wa ufadhili wa ugaidi. (2) Mwombaji wa leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A anayekusudia kutoa huduma ya kutuma fedha atatakiwa, pamoja na taarifa zinazohitajika chini ya kanuni ndogo ya (1), kuwasilisha Benki yafuatayo- (a) ushahidi akaunti kwamba maalum itakayotumika mahsusi kwa lengo la kuweka fedha ya mteja ikisubiri kutumwa au kupokelewa, imefunguliwa katika benki au taasisi ya fedha; (b) ushahidi kwamba amana isiyozaa riba ya Dola za Marekani laki moja imewekwa Benki kwa ajili ya duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A lenye umiliki wa hisa zaidi zinazomilikiwa na wageni na Dola za Marekani elfu hamsini kwa ajili ya duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A lenye umiliki wa hisa zaidi zinazomilikiwa na wenyeji; na (c) nakala iliyothibitishwa ya makubaliano husika baina ya duka la kubadilisha fedha za kigeni na mtoa huduma wa fedha kwa njia ya simu, benki, taasisi ya fedha au wakala wa kutuma fedha kimataifa, kadiri itakavyoweza kuwa. Ukaguzi kabla ya kuanza biashara 11. Duka fedha za kigeni la kubadilisha halitatakiwa kuanza biashara mpaka pale, eneo la biashara, mitambo ya usalama, mitambo ya mawasiliano, vifaa vya uchakataji, na mifumo ya hesabu za fedha iwe imewekwa, imekaguliwa, imepitiwa na kuidhinishwa na Benki. Utoaji na uhalali wa leseni 12.-(1) Benki inaweza kutoa leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni pale ambapo mwombaji atakidhi matakwa ya Kanuni hizi. (2) Leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni isipokuwa pale itabaki kuwa halali itakapotolewa, 10 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Ada ya mwaka Mabadiliko ya umiliki ambapo itasitishwa au kufutwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria na Kanuni hizi. 13. Duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A na Daraja B litalipa ada ya mwaka ya Shilingi ya Tanzania laki tano kwa kila tawi linaloendesha biashara. 14.-(1) Mabadiliko yoyote ya umiliki wa duka la kubadilisha fedha za kigeni yatahitaji kupata idhini ya Benki kabla ya kufanyika. (2) Duka fedha za kigeni la kubadilisha litatakiwa, baada ya kupata idhini ya Benki kuhusiana na mabadiliko ya umiliki, kusajili mabadiliko hayo kwa Msajili wa Makampuni na kuwasilisha ushahidi wa usajili Benki ndani ya siku saba za usajili. Matakwa ya mtaji 15.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni litatakiwa kuanza biashara na mtaji uliolipwa na kuhakikisha muda wote, mtaji wa wamiliki haupungui- (a) shilingi ya Tanzania bilioni moja kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A lenye hisa zaidi zinazomilikiwa na wageni; (b) shilingi ya Tanzania milioni mia tano kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A lenye hisa zaidi zinazomilikiwa na wenyeji; au (c) shilingi ya Tanzania milioni mia mbili kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja B. (2) Duka la kubadilisha fedha za kigeni litatakiwa kusajili mtaji ulioongezeka kwa Msajili wa Makampuni na kuwasilisha ushahidi wa usajili huo Benki ndani ya siku saba za usajili; Isipokuwa kwamba, duka la kubadilisha fedha za kigeni halitatakiwa kuongeza mtaji bila kuitaarifu Benki. (3) Bila ya kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1), duka la kubadilisha fedha za kigeni litatakiwa, muda wote, kuwa na mtaji wa biashara au kiasi sawa na mtaji wa wamiliki usiopungua asilimia sabini. (4) Kwa madhumuni ya kanuni hii, mtaji wa biashara utajumuisha fedha taslimu, hisa za fedha ya 11 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Kufungua tawi kigeni, dhamana za hazina zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na bakaa kwenye benki na taasisi ya fedha ikiwemo bakaa kwenye akaunti ya hundi, akaunti ya muda maalum (call account) na akaunti ya ukomo wa muda. 16.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A linaweza, kwa idhini ya Benki, kufungua tawi popote ndani ya Jamuhuri ya Muungano. (2) Maombi ya kufungua tawi yataambatishwa na- (a) Fomu D iliyoanishwa katika Jedwali ikiwa imejazwa kikamilifu; (b) uthibitisho wa malipo ya ada isiyorejeshwa ya maombi ya Shilingi za Tanzania milioni moja; (c) makadirio ya matumizi ya mtaji kwa ajili ya ufunguzi wa tawi; (d) wasifu binafsi wa mkuu wa tawi anayependekezwa; na (e) barua kutoka kwa wadhamini wawili ambao si ndugu wa mdhaminiwa wakithibitisha maadili mema na tabia ya mkuu wa tawi anayependekezwa. (3) Katika kupitia maombi hayo, Benki itajiridhisha kwamba- (a) duka la kubadilisha fedha za kigeni lina uwezo thabiti wa kifedha; (b) mkuu wa tawi anayependekezwa amefuzu tathmini iliyofanywa na benki kubaini sifa, maadili na uzoefu wa mtu anayefaa; (c) duka la kubadilishia fedha za kigeni lina mfumo jumuishi wa kuchakata taarifa za matawi yake yote, kuziunganisha na kuaanda marejesho yalioanishwa kwa mujibu wa sheria pamoja na taarifa za fedha za kila mwaka; na (d) duka la kubadilisha fedha za kigeni lina rekodi ya kufuata sheria na kanuni zinazosimamia biashara ya maduka ya 12 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) kubadilisha fedha za kigeni. Kuhamia duka la kubadilisha fedha Daraja A 17.-(1) Miliki wa leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja B anaweza kubadilika kuwa Daraja A baada ya kutuma maombi Benki na kukidhi vigezo vilivyoainishwa katika Kanuni hizi. (2) Mmiliki wa leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja B linalokusudia kubadilika kuwa Daraja A atalazimika kufanya yafuatayo: (a) kukidhi matakwa ya kufungua duka la fedha za kigeni Daraja A kubadilisha yaliyoainishwa chini ya Kanuni hizi; na (b) kuwasilisha azimio la bodi linaloidhinisha mabadiliko hayo. SEHEMU YA TATU MATAKWA YA UTOAJI WA LESENI YA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI LILILOANZISHWA NA HOTELI Maombi ya leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni ya hoteli 18.-(1) Hoteli inayokusudia kutoa huduma za kubadilisha fedha za kigeni itatakiwa kuomba leseni ya Daraja C Benki kwa njia ya maandishi. (2) Maombi hayo yataambatana na yafuatayo: (a) Fomu B iliyoainishwa katika Jedwali ikiwa imejazwa kikamilifu; (b) nakala iliyothibitishwa ya cheti cha usajili wa jina la biashara au cheti cha usajili wa kampuni; (c) nakala iliyothibitishwa ya leseni ya kufanya biashara ya hoteli; na (d) ushahidi wa hoteli kuwa na hadhi ya nyota tatu au zaidi uliyotolewa na mamlaka husika. (3) Duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja C litaweka taratibu za kimaandishi za kugundua na kutoa taarifa za matukio ya utakatishaji fedha haramu kwa kuzingatia sheria na kanuni za kuzuia utakatishaji wa fedha haramu na upambanaji wa ufadhili wa ugaidi. (4) Kumbukumbu za miamala ya kubadilisha fedha za kigeni kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni 13 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Daraja C zitawekwa tofauti na shughuli zingine na zitawasilishwa Benki katika mpangilio na kwa kadiri ya muda uliowekwa na Benki. SEHEMU YA NNE USIMAMIZI WA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI Muundo na uteuzi wa wajumbe wa Bodi na viongozi 19.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A au Daraja B litahakikisha - (a) lina Bodi inayoundwa na wajumbe wasiopungua wawili; (b) halitateua mtu yeyote kama mjumbe wa Bodi bila kupata idhini ya Benki; (c) halimtamteua mtu yeyote kwa nafasi ya afisa mkuu mtendanji au mkuu wa tawi bila kupata idhini ya Benki. (2) Afisa mtendaji mkuu au mkuu wa tawi wa duka la kubadilisha fedha za kigeni atatakiwa kuwa na ujuzi na uzoefu wa kutosha wa biashara ya kubadilisha fedha za kigeni. (3) Endapo afisa mtendaji mkuu au mkuu wa tawi ataacha kushika nafasi hiyo, duka la kubadilisha fedha za kigeni litatakiwa, ndani ya siku saba za nafasi hiyo kuwa wazi, kuitaarifu Benki kwa maandishi na kutoa sababu za nafasi hiyo kuachwa wazi. Majukumu ya Bodi 20. Bodi ya duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A au Daraja B itahakikisha- (a) ina uelewa wa jumla wa shughuli za kubadilisha fedha za kigeni; (b) inatoa uangalizi thabiti wa masuala ya kubadilisha fedha za kigeni; (c) kuwa inazingatia sheria na kanuni na maelekezo yanayotolewa na Benki; (d) inapitia na kuidhinisha sera za ndani na taratibu za uendeshaji; na (e) kuwa nyakati zote, duka la kubadilisha fedha za kigeni lina mfumo madhubuti wa udhibiti wa ndani. 14 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Muundo na udhibiti wa ndani 21.-(1) Muundo wa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A utatakiwa, angalau, kuhusisha shughuli za kifedha na taratibu za uzingatiaji wa sheria. (2) Bila kujali sharti la kanuni hii, duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A litatakiwa kuwa na mkaguzi wa hesabu wa ndani, ambaye anaweza kuchukuliwa kutoka nje ya duka. SEHEMU YA TANO UENDESHAJI WA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI Wigo wa uendeshaji 22.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni litafanya miamala ya papo kwa papo. (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (1), malipo ya ununuzi na uuzaji wa fedha za kigeni yanaweza kufanywa kupitia- (a) fedha taslimu; (b) benki, taasisi ya fedha au mtoa huduma wa fedha kwa njia ya simu; au (c) chombo kingine cha malipo kama itavyoidhinishwa na Benki. (3) Duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A linaweza kutoa huduma ya kutuma fedha kama wakala mdogo wa wakala wa kutuma fedha kimataifa au watoa huduma wa fedha kwa njia ya simu. (4) Kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika Kanuni hizi, duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A linaweza kutuma fedha kupitia benki au taasisi ya fedha, mtoa huduma wa fedha kwa njia ya simu au wakala wa kutuma fedha kimataifa au watoa huduma wa fedha kwa njia ya simu pekee. (5) Duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A au Daraja B linaweza kufanya biashara kama wakala wa benki, taasisi ya fedha, kampuni ya bima, mtoa huduma wa fedha kwa njia ya simu, au huduma nyingine zozote za kifedha kama itakavyoidhinishwa na Benki. (6) Duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A linalotoa huduma ya kutuma fedha litatakiwa kuweka fedha kwenye akaunti maalum iliyofunguliwa mahsusi fedha, na pesa zote kwa huduma ya kutuma 15 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) zinazopokelewa kutoka kwa wateja wake kwa madhumuni ya kuzituma si zaidi ya siku ya biashara ya benki inayofuata baada ya siku ambayo pesa hizo zilipokelewa. (7) Duka la kubadilisha fedha za kigeni linapokusudia kufunga biashara yake, litatakiwa kuhakikisha kuwa pesa zote zilizowekwa kwenye akaunti maalum zinatumwa kwa wanufaika stahiki na kuwasilisha tamko la kimaandishi Benki kuthibitisha hilo. (8) Duka la kubadilisha fedha za kigeni linaweza kuuza fedha za kigeni kwa dhumuni lolote na kwa kiasi chochote ikiwa kama muamala huo utaambatishwa na nyaraka zifuatazo: (a) ushahidi wa nyaraka za ukazi na nyaraka halali za kusafiria kwa ajili ya safari; (b) ombi rasmi kutoka kwa mnufaika kwa njia ya barua, barua pepe, au faksi, kwa ajili ya posho ya kujikimu kwa kiasi kisichozidi Dola za Marekani elfu kumi au kiasi sawa kwa kila muamala; (c) ankara husika, kwa uagizaji bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi au gharama nyingine zinazolipwa kwa fedha za kigeni; (d) barua au ankara kutoka kwa taasisi husika za elimu au afya, kwa ajili ya gharama za matibabu, elimu, au mafunzo; au (e) risiti halisi, kwa miamala kati ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni, au benki. 23.-(1) Eneo la biashara ya duka la kubadilisha fedha za kigeni litatakiwa kufikika na umma. (2) Duka fedha za kigeni la kubadilisha halitatakiwa kuhamisha biashara yake bila idhini ya Benki. (3) Maombi ya idhini ya uhamisho wa biashara yataambatishwa na uthibitisho wa malipo ya ada ya uhamisho ya Shilingi za Tanzania milioni moja. (4) Duka fedha za kigeni la kubadilisha linapokusudia kufunga ofisi yake kuu au tawi kwa muda 16 Uhamisho wa biashara Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) au moja kwa moja, litatakikwa, ndani ya siku tatu tokea tarehe ya kufunga, kuitaarifu/kuijulisha Benki kwa maandishi na kutoa sababu za kufunga: Isipokuwa kwamba, ufungaji wa muda hautozidi miezi sita. (5) Duka fedha za kigeni la kubadilisha halitatakiwa kupangisha, au kumruhusu mtu mwingine yeyote kufanya biashara ingine yoyote, au kutoa huduma au bidhaa nyingine yoyote katika eneo lake la biashara bila idhini ya Benki. Kuonyesha viwango vya kubadilisha fedha, ada, tangazo, na leseni 24. Duka fedha za kigeni la kubadilisha litatakiwa kuonyesha kwenye sehemu inayoonekana katika kila eneo la biashara yake- (a) viwango vya kununua na kuuza fedha za kigeni na ada nyingine zozote; (b) tangazo linaloarifu wateja kuwa wanastahiki kupewa risiti ya kielektroniki kwa ajili ya ununuzi au uuzaji wa fedha za kigeni au huduma yoyote nyingine inayotolewa; (c) nakala halali ya leseni ya biashara. Shughuli 25.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni litatakiwa- (a) kutoa risiti ya kielektroniki kwa kila ununuzi au uuzaji wa fedha za kigeni kwa kuonyesha kiasi kilichouzwa au kununuliwa, madhumuni ya mauzo au chanzo cha fedha za kigeni, viwango vya ubadilishaji vilivyotumika, tarehe na muda; (b) kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A linalofanya biashara ya kutuma fedha kutoa risiti ya kielektroniki kwa kila muamala, angalau, kwa kuonyesha maelezo ya mtumaji, lengo, mpokeaji, kiasi na gharama; (c) kuhifadhi nakala halali za vitambulisho na nyaraka zinazothibitisha kila mauzo ya fedha za kigeni kinachozidi zaidi ya kiasi cha Dola za Marekani elfu tano; 17 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) (d) kutogawanya miamala katika viwango vidogo vidogo kwa lengo la kuepuka matakwa ya utoaji taarifa, na uhifadhi wa nyaraka za miamala; (e) kufungua na kuendesha akaunti za fedha za ndani na za kigeni na benki au taasisi ya fedha kwa jina la duka la kubadilisha fedha za kigeni kwa shughuli za duka la kubadilisha fedha za kigeni tu; (f) kuwa na taarifa ya miamala ya kila siku iliyoainishwa kwenye sera yake ya uendeshaji kama msingi wa ambayo kubainisha mahitaji ya kila siku ya pesa taslimu; na itatumika (g) kuhitahifadhi fedha taslimu zaidi ya kiwango kinachohitajika kwa siku tatu zinazofuata kwa kuzingatia taarifa ya miamala ya kila siku iliyoainishwa chini ya kanuni ndogo ya (f). (2) Duka la kubadilisha fedha za kigeni linaweza- (a) kununua au kuuza fedha za kigeni kati yao na kubadilishana risiti za miamala husika; au (b) kununua fedha za kigeni kutoka kwa benki au taasisi ya fedha kwa lengo la kuuza tena ili kukidhi mahitaji yake ya kawaida ya kila siku kupitia akaunti zake za benki. Amana ya dhamana 26.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni linalotoa huduma ya kutuma fedha litaweka Benki amana isiyozaa riba kama dhamana ya kutoa huduma ya kutuma fedha kama ifuatavyo: (a) Dola za Marekani laki moja kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraja A lenye hisa zaidi zinazomilikiwa na wageni; au (b) Dola za Marekani elfu hamsini kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni Daraia A lenye hisa zaidi zinazomilikiwa na wenyeji. (2) Endapo duka la kubadilisha fedha za kigeni litaacha kutoa huduma ya kutuma fedha, Benki inaweza kutumia amana ya dhamana kulipa madai yoyote ya 18 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Akaunti ya wateja wateja dhidi ya duka la kubadilisha fedha za kigeni yatokanayo na fedha ambazo hazikutumwa. (3) Endapo duka la kubadilisha fedha za kigeni litakuwa halina fedha ambazo hazikutumwa au lina madai ya fedha ambazo hazikutumwa chini ya kiasi cha amana ya dhamana, Benki itarejesha kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni kiasi kamili kilichowekwa kama amana ya dhamana au kiasi kilichobaki baada ya kulipwa kwa fedha ambazo hazikutumwa kwa, wateja husika kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (2). 27.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni linalotoa huduma ya kutuma fedha litatunza akaunti ya fedha za kigeni na ya shilingi za Tanzania kwa jina la duka la kubadilisha fedha za kigeni kwenye benki au taasisi ya fedha ndani ya Jamhuri ya Muungano ikijumuisha maneno “akaunti za wateja” kwenye jina la akaunti. (2) Akaunti za wateja zilizoainishwa katika kanuni ndogo ya (1) zitatumika mahsusi kwa ajili ya miamala ya kutuma fedha. Katazo la miamala isipokuwa ya papo kwa papo 28.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni litafanya miamala ya kununua au kuuza fedha za kigeni papo kwa papo. (2) Duka la kubadilisha fedha za kigeni halitaruhusiwa- (a) kuweka au kupokea Shilingi za Tanzania kwa nia ya kupata au kutoa kiasi sawa na fedha za kigeni, aidha kiasi chote au sehemu ya kiasi cha fedha hizo katika siku za mbele; au (b) kuweka au kupokea fedha za kigeni kwa nia ya kupata au kutoa kiasi sawa na shilingi za Tanzania, aidha kiasi chote au sehemu ya kiasi cha fedha hizo katika siku za mbele. Kukataa kuuza 29. Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni hizi, duka la kubadilisha fedha za kigeni halitakataa kuuza fedha za kigeni kwa mteja, isipokuwa pale ambapo fedha za kigeni hazipatikani. 19 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Uuzaji wa fedha za kigeni kwa wasio wakazi 30.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni halitauza fedha za kigeni kwa mtu asiye mkaazi. (2) Bila kujali masharti ya kanuni hii duka la kubadirisha fedha za kigeni litauza fedha za kigeni kwa mtu asiye mkazi pale ambapo mtu huyo atathibitisha kwamba Shilingi za Tanzania zilipatikana ndani ya Jamhuri ya Muungano kutokana na mauzo ya fedha za kigeni; au shughuli nyingine halali zenye utambulisho sahihi na uhifadhi wa kumbukumbu ya muamala. Utumaji wa fedha kimataifa 31.-(1) Kabla ya kutuma fedha kimataifa, duka la kubadilisha fedha za kigeni linalotoa huduma ya kutuma fedha, litatakiwa kumtaka mwombaji kuwasilisha, angalau, nyaraka zifuatazo- (a) ankara husika kwa uagizaji bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi; (b) barua au ankara kutoka kwa taasisi husika ya elimu au tiba, kama suala linahusu gharama za elimu au matibabu; (c) nakala iliyothibitishwa ya kibali halali cha kazi na mkataba wa ajira kama fedha ni za mtaalamu kutoka nje ya nchi; (d) nakala iliyothibitishwa ya barua ya tuzo ya pensheni na mkataba wa ajira kama ni mafao ya kustaafu; (e) nyaraka za mkataba, ankara au hati ya malipo ya ada na nyaraka za uthibitisho wa ulipaji wa kodi kama ni suala la ushauri na mirabaha; (f) ikiwa ni suala la gawio na faida kwa wanahisa wa kigeni, fedha taarifa za zilizokaguliwa zinazoonyesha gawio au faida iliyotangazwa inayotarajiwa kutumwa nje ya nchi na nyaraka zinazothibitisha malipo ya kodi zote husika; au (g) nyaraka nyingine zozote husika kutegemea aina ya maombi. (2) Duka fedha za kigeni la kubadilisha halitatuma fedha kwa madhumuni ya uwekezaji nje ya eneo lililoainishwa. 20 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Taarifa za chanzo na madhumuni ya fedha za kigeni Ukusanyaji, uwasilishaji na uhifadhi wa data. Utambuzi na utoaji wa taarifa za miamala shuku 32.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni litaomba taarifa kutoka kwa mteja kuhusu chanzo na madhumuni ya fedha za kigeni. (2)endapo mteja taarifa zilizoombwa kwa mujibu wa kanuni hii bila ya sababu za msingi duka la kubadilisha fedha za kigeni halitotoa huduma inayohusiana na muamala huo. atakataa kutoa 33. Duka la kubadilisha fedha za kigeni litatakiwa- (a) kuwa na mfumo madhubuti wa taarifa ambao utawezesha ukusanyaji na uchakataji wa taarifa na data za kitakwimu wenye uwezo wa taarifa ya kilichofanyika kwenye kutoa mfumo na kimefanywa na nani ili kuwezesha ukaguzi kufanyika kwa matumizi yake yenyewe, wakaguzi wa ndani na nje na Benki; (b) kutunza kumbukumbu za miamala yote iliyofanyika na kuzihifadhi kwa muda usiopungua miaka kumi tangu tarehe ya muamala husika; biashara katika yake (c) kuwasilisha taarifa Benki kwa namna na nyakati zitakazoainishwa na Benki; na (d) kuhakikisha kuwa matukio ndani ya eneo la biashara yanarekodiwa wakati huohuo na kuhakikisha kuwa picha za kamera za usalama (CCTV) za kila siku zinahifadhiwa kwa usalama kwa muda usiopungua miezi sita. 34.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni litatakiwa- (a) kuweka taratibu za utambuzi wa mteja kwa kuzingatia masharti ya sheria na kanuni za na kuzuia kupambana na ufadhili wa ugaidi kwa madhumuni ya kutambua na kutoa taarifa za miamala shuku yoyote ya utakatishaji fedha utakatishaji haramu fedha 21 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) au ufadhili wa ugaidi; na (b) kuweka utaratibu na vidhibiti vya ndani kwa ajili ya kutambua na kutoa taarifa ya miamala shuku kwa kuzingatia masharti ya sheria na kanuni za kuzuia utakatishaji fedha haramu na kupambana na ufadhili wa ugaidi. Usiri wa miamala 35. Duka la kubadilisha fedha za kigeni litafanya miamala ya fedha za kigeni na kuhifadhi taarifa za miamala hiyo kwa usiri wa hali ya juu. SEHEMU YA SITA TAARIFA ZA FEDHA NA UKAGUZI Taarifa za fedha 36.-(1) Duka la kubadilisha fedha za kigeni la Daraja A au Daraja B litatakiwa- (a) kuwasilisha Benki nakala ya taarifa za fedha zilizokaguliwa ndani ya miezi mitatu baada ya kuisha kwa mwaka wa fedha; (b) kuwasilisha Benki taarifa za fedha za kila robo mwaka ndani ya siku kumi na nne baada ya mwisho wa robo husika ya mwaka kwa utaratibu ulioanishwa na Benki; na (c) kuwa na mkaguzi wa nje aliyesajiliwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi. (2) Kwa madhumuni ya kanuni hii, mwaka wa fedha maana yake ni mwaka wa kalenda. 37.-(1) Benki inaweza kufanya ukaguzi wa duka la kubadilisha fedha za kigeni kwa kutoa notisi au bila kutoa notisi. (2) Duka fedha za kigeni la kubadilisha litatakiwa, ndani ya kipindi kitakachoainishwa wakati wa ukaguzi, kutoa nyaraka na taarifa zozote zitakazoombwa na Benki. (3) Benki itatakiwa, baada ya kufanya ukaguzi, kulipatia duka la kubadilisha fedha za kigeni, muhtasari 22 Ukaguzi Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) wa matokeo ya ukaguzi na kulitaka duka la kubadilisha fedha za kigeni kurekebisha mapungufu yaliyobainishwa ndani ya kipindi kitakachoainishwa na Benki. SEHEMU YA SABA MASHARTI YA JUMLA Mafunzo 38. Duka fedha za kigeni la kubadilisha litahakikisha wafanyakazi wake wanapewa mafunzo ya kutosha kuhusu uendeshaji wa biashara, sheria husika na matakwa ya usimamizi. Kufunga biashara kwa hiari na kusalimisha leseni Adhabu za kiutawala 39.-(1) Endapo duka la kubadilisha fedha za kigeni linakusudia kufunga biashara kwa hiari, litatakiwa kutoa notisi ya maandishi kwa Benki ya kusudio lake la kufunga biashara kwa hiari. (2) Duka la kubadilisha fedha za kigeni litatakiwa kusalimisha leseni yake Benki ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya taarifa hiyo ya kufunga biashara. 40.-(1) Bila kuathiri adhabu za kiutawala na hatua zilizoainishwa chini ya Sheria, pale ambapo Benki imejiridhisha kwamba duka la kubadilisha fedha za kigeni limekiuka masharti ya Sheria, Kanuni hizi au maelekezo yoyote yaliyotolewa na Benki, Benki inaweza- (a) kusitisha shughuli za duka la kubadilisha fedha za kigeni kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja; (b) kutoza faini sawa na kiwango kisichozidi Dola za Marekani elfu tatu; au (c) kufuta leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni. (2) Bila kujali sharti la kanuni ndogo ya (1)(c), Benki inaweza kufuta leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni iwapo duka hilo au afisa wake yeyote- (a) amepata fedha za kigeni isivyo halali; (b) ametiwa hatiani na mahakama kwa ulaghai au makosa yanayohusiana na kukosa uaminifu; au (c) amewasilisha taarifa za uongo wakati au 23 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Notisi ya kusitisha au kufuta leseni baada ya mchakato wa maombi ya leseni. 41.-(1) Benki itatakiwa kutoa notisi ya maandishi kwa duka la kubadilisha fedha za kigeni kuhusu kusudio lake la kusitisha au kufuta leseni. (2) Duka la kubadilisha fedha za kigeni linaweza, ndani ya siku ishirini na moja baada ya kupokea notisi, kuiomba Benki kufanya mapitio ya kusudio lake la kusitisha au kufuta na kueleza sababu za kusudio hilo. (3) Benki itatakiwa, ndani ya siku arobaini na tano baada ya kupokea maombi, kufanya marejeo ya kusudio lake la kusitisha au kufuta leseni na kulijulisha duka la kubadilisha fedha za kigeni kwa maandishi uamuzi uliofikiwa. (4) Benki inaweza kusitisha au kufuta leseni endapo- (a) duka la kubadilisha fedha za kigeni limeshindwa kujibu taarifa iliyotolewa; au (b) Benki haijaridhishwa na maelezo yaliyotolewa; na italijulisha duka la kubadilisha fedha za kigeni kwa maandishi uamuzi uliofikiwa. (5) Endapo duka la kubadilisha fedha za kigeni litafutiwa leseni, litatakiwa kusalimisha leseni Benki ndani ya siku kumi na nne, tangu tarehe ya kufutwa. Kufutwa TS Na. 450 la 2019 42. Kanuni za Fedha za Kigeni (Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni), 2019 zimefutwa. 24 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) __________ JEDWALI __________ (Limetungwa chini ya kanuni ya 6, 16 na 18) FOMU – A (Imetungwa chini ya kanuni ya 6(2)(b)) MAOMBI YA LESENI YA DARAJA A AU DARAJA B YA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI TAFADHALI TUMIA HERUFI KUBWA 1. JINA LA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI: …………………………………………………………………………… 2. DARAJA LA LESENI INAYOOMBWA: …………………………… 3. ANUANI YA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI: A. MKOA………………………………………………………… B. WILAYA……………………………………………………… C. MTAA…………………………………………………………… D. NAMBA YA KIWANJA……………………………………………………. E. NAMBA YA JENGO ……………………………………... F. S.L.P.…………………………………………………………… G. NAMBA YA SIMU…………………………………………………………. H. BARUA PEPE……………………………………………… 25 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) 4. TAARIFA ZA WANAHISA NA. JINA URAIA NAMBA ZA SIMU NA BARUA PEPE KAZI ASILIM IA YA HISA 1. 2. 3. 4. 5. TAARIFA ZA WAJUMBE WA BODI NA. JINA URAIA NAMBA ZA SIMU NA BARUA PEPE KAZI 1. 2. 3. 4. 6. TAARIFA ZA OFISA MTENDAJI MKUU NA MAMENEJA KWA KUZINGATIA VYEO NA. JINA URAIA CHEO SIFA ZA ELIMU 1. 2. 3. 6. TAMKO (la Wanahisa): Mimi/Sisi, tuliosaini hapa chini, tunatamka: 26 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) (a) KWAMBA, taarifa zilizotolewa kwenye fomu hii ni za kweli na sahihi kwa kadiri ya ufahamu na imani yangu/yetu; (b) KWAMBA, mimi/sisi hatujawahi kufilisiwa wala kuhukumiwa kwa ulaghai au kwa kukosa uaminifu; (c) KWAMBA, kama tutapata leseni, Mimi/Sisi tutafanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kwa kufuata masharti yaliyomo kwenye Sheria ya Kubadilisha Fedha za Kigeni, Sura ya 271 na Kanuni, Miongozo au Maagizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania kadiri yatakavyotolewa. Tarehe ………………………………………………. Jina ……………………………………. ………Saini………….…………..………….. Jina ……………………………………………. Saini………………………..……….… Jina ……………………………………………...Saini………………..………………… Jina ……………………………………………....Saini ……………..……………….… Jina ……………………………………………….Saini…………………………….……. MBELE YANGU: JINA ………………………………………………………………………….. SAINI ……………………………………………………………………….. TAREHE: ……………………………………………………………………... ANWANI……………………………………………………………………… MTHIBITISHAJI NYARAKA/KAMISHNA WA VIAPO ________________________________________________________________________ _____ ZINGATIA: TAFADHALI AMBATISHA NYARAKA ZIFUATAZO: 1. Barua ya maombi; na 2. Nyaraka zote zilizoorodheshwa chini ya kanuni ya 6 ya Kanuni hizi. 27 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) FOMU-B (Imetungwa chini ya kanuni ya 18(2)(a)) MAOMBI YA LESENI YA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI DARAJA C TAFADHALI TUMIA HERUFI KUBWA 1. JINA LA HOTELI: ……………………………………………………………………… 2. ANWANI YA HOTELI: A. MKOA………………………………………………………………… …….. B. WILAYA……………………………………………………………… ……. C. MTAA…………………………………………………………………… ….. D. NAMBA YA KIWANJA……………………………………………………. E. NAMBA YA JENGO……………………………………………………….. F. S.L.P.……………………………………………………………………. ...... G. NAMBA YA SIMU…………………………………………………………. H. BARUA PEPE………………………………………………………………. 3. TAARIFA ZA WAMILIKI NA. JINA URAIA NAMBA ZA SIMU BARUA PEPE 1. 2. 3. 28 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) 4. 4. TAARIFA ZA MUENDESHAJI /WAENDESHAJI WA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI URAIA NA JINA NAMBA YA SIMU BARUA PEPE 1 2 5. TAMKO (la mtu aliyeidhinishwa) Mimi niliesaini hapa chini, ninatamka: a) KWAMBA, taarifa zilizotolewa kwenye fomu hii ni za kweli na sahihi kwa kadri ya ufahamu na imani yangu; b) KWAMBA, kama nitapata leseni, nitafanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kwa kufuata masharti yaliyomo kwenye Sheria ya Kubadilisha Fedha za Kigeni, Sura ya 271, Kanuni, Miongozo au Maagizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania kadiri yatakavyotolewa. Tarehe ………………………………………………. Jina ……………………………………. ………Saini………….…………..………….. MBELE YANGU: JINA ………………………………………………………………………….. SAINI ……………………………………………………………………….. TAREHE: ……………………………………………………………………... ANWANI……………………………………………………………………… MTHIBITISHAJI NYARAKA/KAMISHNA WA VIAPO 29 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) ________________________________________________________________________ ZINGATIA: TAFADHALI AMBATISHA NYARAKA ZIFUATAZO: 1. Barua ya maombi; na 2. Nyaraka zote zilizoorodheshwa chini ya kanuni ya 18 ya Kanuni hizi. 30 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) FOMU - C (Imetungwa chini ya kanuni ya 6(2)(i)) FOMU YA VIGEZO VYA SIFA, MAADILI NA UZOEFU WA MTU (IJAZWE NA WANAHISA, WAJUMBE WA BODI, AFISA MTENDAJI MKUU NA MKUU WA TAWI WA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI) 1. TAARIFA BINAFSI (a) Jina Kamili (Bw/ Bi.)…………………………………………………………… (b) Majina ya zamani (kama yapo)………………................................................................... (c) Mwaka na mahali pa kuzaliwa: ………………………………………………………… (d) Uraia:…………………………………………………………………………………….. (e) Kitambulisho / namba ya Pasipoti, …………………… tarehe ya kutolewa……………………… mahali ilipotolewa:………………………… (f) Anwani ya posta:…………………………………………………………………………. (g) Anwani ya Makazi: ……………………………………………………………………… (h) Namba ya simu: ………………………………………………………………………….. (i) Barua Pepe:…………………………………………………………………............................. (j) Sifa za Elimu:……………………………………………………………………………............ (k) Sifa za Taaluma:…………………………………………………………………………………. (l) Namba ya Kibali cha Ukazi (inapohitajika) ……………………………………………………… (m) Namba ya Kibali cha Kazi (inapohitajika) ………………………………………………………… 2. TAARIFA ZA AJIRA/BIASHARA Kipindi Jina la Mwajiri/Biashara na anwani Nafasi zilizoshikiliwa na tarehe Majukumu Sababu za kuondoka (inapohusu) 3. HISA KATIKA MAKAMPUNI MENGINE (ZINAZOMILIKIWA MOJA KWA MOJA AU KUPITIA WASIMAMIZI) 31 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) Jina la Kampuni Tarehe ya Usajili Asilimia (%) ya Umiliki 4. VYANZO VYA FEDHA Tafadhali toa maelezo ya chanzo/vyanzo halisi vya fedha ambavyo wewe, kama mwanahisa, ungependa kuwekeza au kutumia katika biashara inayopendekezwa, ukiambatisha nyaraka zinazothibitisha vyanzo hivyo. (a) ……………………………………………………………………………… (b) ……………………………………………………………………………… (c) ………………………………………………………………………………. 5. HATI YA UTHIBITISHO WA ULIPAJI KODI Wasilisha Hati ya uthibitisho wa ulipaji kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania ya sasa na chanzo chochote cha fedha ambacho hutozwa kodi. 6. TAARIFA NYINGINE 6.1. Je, wewe au taasisi yoyote ambayo unahusiana nayo kama mwanahisa au mkurugenzi imewahi kuwa na leseni au kuomba leseni ya kuendesha biashara ya kigeni ?………………………………………………………………………………… kubadilisha fedha za ………………………………………………………………………………… 6.2. Je, umewahi kwa wakati wowote kutiwa hatiani kwa kosa la jinai mahali popote? Kama ndiyo, toa maelezo ya mahakama iliyokutia hatiani, kosa na adhabu uliyopewa na tarehe uliyotiwa hatiani. ………………………………………………………………………… ……… ………………………………………………………………………… ……… 6.3. Je, umewahi kufukuzwa kazi katika ofisi au ajira yoyote, kukabiliwa na mashtaka ya kinidhamu na mwajiri wako au kuzuiwa kujihusisha katika taaluma au kazi yoyote? Ikiwa ndivyo, toa maelezo. ………………………………………………………………………… ……… ………………………………………………………………………… …… 6.4. Je, umewahi kutangazwa na mahakama kuwa umefilisika, au kupokea taarifa zozote kuhusu shauri la kisheria kuhusiana na masuala hayo? Kama ndivyo, eleza hatua iliyopo. ………………………………………………………………………… ……… 32 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) ………………………………………………………………………… 6.5. Je, umewahi kuhukumiwa na mahakama kwa kosa la ulaghai au mwenendo wowote mbaya? Ikiwa ndivyo, toa maelezo. ………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………… 6.6. Je, kuna maelezo yoyote ya ziada ambayo unaona yanafaa kuzingatiwa katika maombi yako ya leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni? Kama yapo toa maelezo ………………………………………………………………………… …………………………………………………………… _____________________________________________________________________ ZINGATIA: Taarifa zilizotolewa kwa kujibu dodoso hili zitahifadhiwa kwa siri na Benki, isipokuwa zitakapohitajika kisheria. Ambatisha nakala husika chini ya hitaji no. 1(l) na (m) 7. TAMKO Ninafahamu kuwa ni kosa kutoa taarifa yoyote ambayo ni ya uongo au ya kupotosha kuhusiana na maombi ya leseni ya duka la kubadilisha fedha za kigeni kwa kujua au kwa uzembe. Ninathibitisha kwamba taarifa zilizotolewa hapo juu ni za kweli kwa kadiri ya ufahamu wangu na kwamba hakuna taarifa nyingine zinazohusiana na maombi haya ambazo Benki Kuu ya Tanzania inapaswa kufahamu. Niko tayari kuifahamisha Benki Kuu ya Tanzania kuhusiana na mabadiliko yoyote muhimu yanayohusiana na maombi haya yatakayojitokeza wakati maombi yanashughulikiwa. Jina:…………………………………………………………………………….. Tarehe:…………………………………………………………………………. MBELE YANGU: JINA:………………………………………………………………………... SAINI:………………………………………………………………… TAREHE:…………………………………………………………………………. ANWANI:…………………………………………………………………… MTHIBITISHAJI NYARAKA/KAMISHNA WA VIAPO 33 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) FOMU - D (Imetungwa chini ya kanuni namba 16(2)(a)) MAOMBI YA KUFUNGUA TAWI LA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI TAFADHALI TUMIA HERUFI KUBWA 1. JINA LA DUKA LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI: ………………………………………………….. 2. TAARIFA ZA MATAWI YALIYOPO: NA JINA ANUANI YA ENEO ANUANI YA POSTA TAREHE YA KUANZISHWA: 1. 2. 3. 4. 3. JINA LA TAWI JIPYA: …………………………………………………… A. MKOA ………………………………………………………………………….. B. WILAYA: ………………………………………………………………………. C. MTAA………………………………………………………………………………. D. NAMBA YA KIWANJA ………………………………………………………… E. NAMBA YA JENGO……………………………………………………………… F. S.L.P ………………………………………………………………………………… G. NAMBA YA SIMU …………………………………………………………………. H. BARUA PEPE ………………………………………………………………………. 34 Kanuni Za Maduka ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni Tangazo la Serikali Na. 729 (Linaendelea.) 4. TAMKO (la Wanahisa) Mimi/Sisi, tuliosaini hapa chini, tunatamka: (a) KWAMBA, taarifa zilizotolewa kwenye fomu hii ni za kweli na sahihi kwa kadiri ya ufahamu na imani yangu; (b) KWAMBA, mimi/sisi hatujawahi kufilisiwa wala kutiwa hatiani kwa ulaghai au kukosa uaminifu; (c) KWAMBA, kama tutapata leseni, Mimi/Sisi tutafanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kwa kufuata masharti yaliyomo kwenye Sheria ya Kubadilisha Fedha za Kigeni ya Sura ya 271 na Kanuni, Miongozo au Maagizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania kadiri yatakavyotolewa. Tarehe …………………………………………………. Jina………………………………………………….. Saini …………………… Jina ………………………………………………… Saini………………… Jina ………………………………………………… Saini…………………. Jina …………………………………………………. Saini ………………..... Jina ………………………………………………… Saini …………………. MBELE YANGU: JINA: …………………………………………………………………………. SAINI: ………………………………………………………………………. TAREHE: ……………………………………………………………………… ANWANI ……………………………………………………………………….. MTHIBITISHAJI NYARAKA/KAMISHNA WA VIAPO _________________________________ ZINGATIA: TAFADHALI AMBATISHA NYARAKA ZIFUATAZO: 1. Barua ya maombi 2.Nyaraka zote zilizoorodheshwa chini ya kanuni namba 16 ya Kanuni hizi. Dodoma, …………….., 2023 EMMANUEL M. TUTUBA, Gavana 35
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in