NOTISI YA KUBADILI ORODHA YA VIONGOZI WA UMMA KATIKA SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA YA MWAKA 2023
This notice is titled the Notice on Changing the List of Public Leaders, and it is to be read together with the Public Leaders Ethics Act.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Notice
- Citation
- NOTISI YA KUBADILI ORODHA YA VIONGOZI WA UMMA KATIKA SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA YA MWAKA 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This notice is titled the Notice on Changing the List of Public Leaders, and it is to be read together with the Public Leaders Ethics Act. Provision hii inabadilisha orodha ya nyadhifa za umma iliyo chini ya kifungu cha 4 kwa kufuta orodha ya zamani na kuweka orodha mpya. Hii inafuta notisi mbili zilizotajwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of NOTISI YA KUBADILI ORODHA YA VIONGOZI WA UMMA KATIKA SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA YA MWAKA 2023
Showing 3 of 3
- 1 Verify source ↗
Notisi hii itajulikana kama Notisi ya Kubadili
AI-assisted research summary: This notice is titled the Notice on Changing the List of Public Leaders, and it is to be read together with the Public Leaders Ethics Act.
1. Notisi hii itajulikana kama Notisi ya Kubadili Orodha ya Viongozi wa Umma katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 2023 na itasomwa pamoja na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambayo hapa itarejewa kama “Sheria”. - 2 Verify source ↗
Orodha ya nyadhifa za umma iliyoainishwa
AI-assisted research summary: Provision hii inabadilisha orodha ya nyadhifa za umma iliyo chini ya kifungu cha 4 kwa kufuta orodha ya zamani na kuweka orodha mpya.
2. Orodha ya nyadhifa za umma iliyoainishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria, katika tafsiri ya neno “kiongozi wa umma”, inabadilishwa kwa kufutwa na badala yake kuwekwa orodha ifuatayo: “ (i) Rais wa Jamhuri ya Muungano; (ii) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano; (iii) Rais wa Zanzibar; (iv) Waziri Mkuu; (v) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar; (vi) Spika, Naibu Spika na Mbunge; (vii) Jaji Mkuu, Jaji wa Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu na Hakimu; (viii) Waziri, Naibu Waziri, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya; (ix) Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali; (x) Balozi Mwakilishi wa Tanzania nchi za Nje; 1 Notisi ya Kubadili Orodha ya Viongozi wa Umma Katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Tangazo La Serikali Na. 857 (Linaendelea)) (xi) Katibu Mkuu Kiongozi, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Katibu Tawala wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa Msaidizi na Katibu Tawala wa Wilaya; (xii) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Nje; (xiii) Katibu wa Bunge; (xiv) Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi; (xv) Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi; (xvi) Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa; (xvii) Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza; (xviii) Kamishna Jenerali wa Uhamiaji; (xix) Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji; (xx) Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya; (xxi) Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa; (xxii) Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na na Rushwa; Mkuu wa na Mkuu wa Kupambana TAKUKURU Mkoa TAKUKURU Wilaya; (xxiii) Afisa katika Jeshi la Ulinzi kuanzia cheo cha Kanali; (xxiv) Afisa katika Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto na Uokoaji kuanzia cheo cha Kamishna Msaidizi; (xxv) Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Upelelezi Mkoa, Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa, Mkuu wa Polisi Wilaya, Mkuu wa Upelelezi Wilaya na Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya; (xxvi) Mkuu wa Magereza Mkoa na Mkuu wa Gereza; (xxvii) Gavana na Naibu Gavana; 2 Notisi ya Kubadili Orodha ya Viongozi wa Umma Katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Tangazo La Serikali Na. 857 (Linaendelea)) (xxviii) Mtendaji Mkuu na Naibu Mtendaji Mkuu katika Taasisi, Idara, Mamlaka, Wakala wa Serikali, Shirika na Kampuni ya Umma; (xxix) Mwakilishi wa Serikali katika Shirika au Kampuni ambayo Serikali ina Maslahi; (xxx) Meya, Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani; (xxxi) Mkurugenzi, Naibu Mkurugenzi, Mkurugenzi Msaidizi, Katibu, Naibu Katibu, Katibu Msaidizi na Meneja katika Wizara, Taasisi ya Umma, Idara ya Serikali, Mamlaka ya Serikali, Wakala wa Serikali, Shirika la Umma, Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa; (xxxii) Mkuu wa Idara au Kitengo katika Wizara, Idara ya Serikali, Taasisi ya Umma, Mamlaka ya Serikali, Wakala wa Serikali, Shirika la Umma, Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa; (xxxiii) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mjumbe au Kamishna katika Tume; (xxxiv) Msajili, Mrajisi, Naibu Msajili, Naibu Mrajisi, Msajili Msaidizi, Mrajisi Msaidizi katika Wizara, Idara ya Serikali, Taasisi ya Umma, Mamlaka ya Serikali, Wakala wa Serikali, Shirika la Umma, Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa; (xxxv) Kamishna na Kamishna Msaidizi katika Wizara, Idara ya Serikali, Taasisi ya Umma, Shirika la Umma, Mamlaka ya Serikali na Wakala wa Serikali; (xxxvi) Katibu Binafsi na Naibu Katibu au Katibu Msaidizi Binafsi wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu; (xxxvii) Mshauri wa Rais; (xxxviii) Msaidizi wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu; 3 Notisi ya Kubadili Orodha ya Viongozi wa Umma Katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Tangazo La Serikali Na. 857 (Linaendelea)) (xxxix) Mwandishi wa Habari, Mwandishi wa Habari Msaidizi na Mpiga Picha wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu; (xl) Mratibu, Mratibu Msaidizi katika Wizara, Idara ya Serikali, Taasisi ya Umma, Shirika la Umma, Mamlaka na Wakala wa Serikali; (xli) Mratibu wa Mradi katika Wizara, Idara ya Serikali, Taasisi ya Umma, Shirika la Umma, Mamlaka ya Serikali, Wakala wa Serikali, Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa; (xlii) Mnikulu na Naibu Mnikulu; (xliii) Karani na Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri; (xliv) Msaidizi wa Katibu na Katibu Msaidizi wa Baraza la Mawaziri; (xlv) Mganga Mkuu na Mfamasia Mkuu wa Serikali, Mganga Mkuu wa Mkoa, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kanda, Mkoa na Wilaya; (xlvi) Mhasibu Mkuu wa Serikali, Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi na Mkuu wa Hazina Ndogo na Mhakikimali wa Mkoa na Wilaya. (xlvii) Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi; (xlviii) Msajili Mkuu, Msajili na Naibu Msajili wa Mahakama; (xlix) Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Mtendaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu; (l) Mwandishi Mkuu wa Sheria; (li) Msajili wa Hazina; (lii) Mhasibu Mkuu na Mkaguzi wa Ndani Mkuu katika Wizara, Idara ya Serikali, Taasisi ya la Umma, Mamlaka ya Umma, Shirika Serikali, Wakala wa Serikali, Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; 4 Notisi ya Kubadili Orodha ya Viongozi wa Umma Katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Tangazo La Serikali Na. 857 (Linaendelea)) (liii) Makamu Mkuu wa Chuo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mkuu wa Kampasi, Mkuu wa Ndaki, Mkuu wa Kitivo na Mkuu wa Shule katika Chuo Kikuu cha Umma; (liv) Mkuu wa Chuo, Naibu Mkuu wa Chuo, Mkuu wa Kampasi, Mkuu wa Ndaki na Mkuu wa Kitivo katika Taasisi ya Elimu; (lv) Mthamini Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Wilaya; (lvi) Afisa Usalama Mkoa na Wilaya; (lvii) Mkurugenzi wa Mashtaka, Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Mkuu wa Mashtaka Mkoa na Mwendesha Mashtaka Wilaya; (lviii) Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali; (lix) Kabidhi Wasii Mkuu na Naibu Kabidhi Wasii Mkuu; (lx) Msuluhishi na Muamuzi katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi; (lxi) Afisa Madini Mkazi; na (lxii) Mwenyekiti na Mjumbe wa Bodi katika Bodi ya Wakurugenzi na Bodi ya Wadhamini katika Taasisi ya Umma.”. Kufuta TS. Na. 209 la 2005 260 la 2013 - 3 Verify source ↗
Notisi ya Mabadiliko ya Orodha ya Viongozi wa
AI-assisted research summary: Hii inafuta notisi mbili zilizotajwa.
3. Notisi ya Mabadiliko ya Orodha ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 2005 na Notisi ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Nyongeza ya Orodha ya Viongozi wa Umma) Taarifa, 2013 zinafutwa. Dodoma, 28 Agosti, 2023 SAMIA SULUHU HASSAN Rais 5
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
NOTISI YA KUBADILI ORODHA YA VIONGOZI WA UMMA KATIKA SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA YA MWAKA 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in