AI-assisted research summary: General and detailed plans for the area in the Schedule must be prepared and kept by the town planning director and the Buchosa District Council executive director.
3. Mipango ya jumla na ya kina kwenye eneo lililoainishwa katika Jedwali itaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa. 1 Tangazo la Serikali Na. 809(Linaendelea.) Amri ya Kupanga Eneo la Mji wa Nyehunge ________ JEDWALI ________ (Iimetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: ’Unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MPK1 yenye majira - nukta 420775.998MS, 9721952.443KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki katika uelekeo wa MS1200MS kwa umbali wa kilomita 1.8 kwa kukatisha barabara iendayo Kahunda hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MPK2 yenye majira - nukta 422635.087MS, 9722072426KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini-Mashariki katika uelekeo wa KS1300MS kwa umbali wa kilomita 0.6 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MPK3 yenye majira - nukta 423086.390MS, 9721608.029KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa KS1490MS kwa umbali wa kilomita 0.6 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MPK4 yenye majira - nukta 423227.871MS, 9721002.126KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS1130MG kwa umbali wa kilomita 0.9 kwa kukatisha barabara iendayo Sengerema hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MPK5 yenye majira - nukta 422438.378MS, 9720435.708KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa KS2340KS hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MPK6 yenye majira - nukta 422437.972MS, 9719589.453KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi katika uelekeo wa MG970MG kwa umbali wa kilomita 1.4 kwa kukatisha barabara itokayo Kayenze hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MPK7 yenye majira - nukta 421043.800MS, 9719503.595KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ1260MG kwa umbali wa kilomita 0.9 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MPK8 yenye majira - nukta 420479.056MS, 9720266.583KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini katika uelekeo wa KZ1420KZ kwa umbali wa kilomita 1.1 kwa kukatisha barabara itokayo Geita hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MPK9 yenye majira - nukta 420502.216MS, 9721386.848KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Mashariki katika uelekeo wa KZ1550MS kwa umbali wa kilomita 0.6 ulipoanzia. Dodoma, 19 Oktoba, 2023 JERRY WILLIAM SILAA, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2