Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
This section gives the bylaw its short title.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the bylaw its short title. This by-law applies throughout the whole area of Kyerwa District Council. This section defines key terms used in the by-laws, including the Council, Director, authorized officer, service levy, and who counts as a service levy payer. Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma wa 0.3% ya mauzo kwa wafanyabiashara husika wanaowasilisha hesabu za mauzo kwa TRA, baada ya VAT na ushuru wa bidhaa kuondolewa. Service tax payers must pay the tax at the rate set in this bylaw, submit accurate monthly sales information in some cases, and pay within 14 days after filing the monthly sales report.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
Showing 10 of 10
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the bylaw its short title.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the whole area of Kyerwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-laws, including the Council, Director, authorized officer, service levy, and who counts as a service levy payer.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa; Sura ya 212 “kampuni” maana yake ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “kipindi maalum cha hesabu” maana yake ni muda ambao mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara kwa Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa au Afisa yeyote 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 887 (Linaenedelea) aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni kampuni, tawi la leseni la au mfanyabiashara mwenye zake shughuli katika eneo kampuni anayefanya Halmashauri; Sura ya 212 Ushuru wa huduma “tawi la kampuni” maana yake ni tawi la kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara yeyote mwenye leseni ya biashara ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne kutokana na huduma anazopata na kutumia miundombinu ya umma inayomuwezesha kufanya biashara katika eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri husika. shirika ambalo - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma wa 0.3% ya mauzo kwa wafanyabiashara husika wanaowasilisha hesabu za mauzo kwa TRA, baada ya VAT na ushuru wa bidhaa kuondolewa.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu (0.3%) ya mauzo baada ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Thamani na ushuru wa bidhaa kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara yeyote mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii kutoka kwa wafanyabiashara wenye leseni za biashara ambao hawawasilishi hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. Wajibu wa - 5 Verify source ↗
Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu
AI-assisted research summary: Service tax payers must pay the tax at the rate set in this bylaw, submit accurate monthly sales information in some cases, and pay within 14 days after filing the monthly sales report.
5. Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 887 (Linaenedelea) mlipa ushuru wa huduma wa: (a) kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila mwezi endapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Kila mlipa ushuru wa huduma atatakiwa kulipa ushuru wa huduma si zaidi ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kuwasilisha taarifa za mauzo ya kila mwezi. (3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (2), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru huo. - 6 Verify source ↗
(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtaka mlipa ushuru wa huduma au mfanyabiashara aliye chini ya Sheria Ndogo hii kuwasilisha taarifa kuhusu mauzo au taarifa nyingine zilizoandikwa.
6.-(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa kuwasilisha taarifa ya mauzo chini ya Sheria Ndogo hii atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo kwa wakati, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku thelathini kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi. (2) Mkurugenzi anaweza kumtaka kwa maandishi taarifa kuhusu mfanyabiashara mtu yeyote mwenye anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi. - 7 Verify source ↗
Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri must calculate the service levy for service taxpayers who submit sales information to the Tanzania Revenue Authority, using the information submitted during the relevant accounting period.
7. Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma kwa walipa ushuru wa huduma wanaowasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuzingatia taarifa zinazowasilishwa na walipa ushuru wa huduma katika kipindi maalum cha hesabu. - 8 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Any person who fails to file correct sales information, gives incorrect information, fails to pay service tax on time, persuades a taxpayer to avoid payment, or blocks council officials commits an offence.
8.-(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo: (a) atashindwa kuwasilisha kwa Halmashauri taarifa sahihi za mauzo katika muda ulioainishwa katika 3 Mamlaka ya Mkurugenzi Ukokotoaji wa ushuru wa huduma Makosa na adhabu Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 887 (Linaenedelea) Sheria Ndogo hii; (b) atawasilisha kwa Halmashauri taarifa zisizo sahihi; (c) atashindwa kulipa ushuru wa huduma katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (d) atamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru wa huduma; au (e) atamzuia Mkurugenzi, Afisa Mwidhiniwa au mtumishi yeyote wa Halmashauri kutekeleza masharti ya Sheria Ndogo hii. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) na kutiwa hatiani atatozwa faini isiyopungua Shilingi laki mbili na isiyozidi Shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. Kufifilisha kosa - 9 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote kiasi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote Shilingi laki mbili ikiwa mtu huyo anakiri kosa kwa kutumia fomu iliyotajwa na analipa kiasi hicho pamoja na ushuru unaodaiwa au anakubali kutimiza wajibu wake.
9. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote kiasi cha Shilingi laki mbili iwapo mtu huyo atakiri kosa kwa kujaza fomu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa kiasi hicho na kulipa Ushuru anaodaiwa au kukubali kutekeleza wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii. 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 887 (Linaenedelea) _________________ JEDWALI LA KWANZA _________________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 4(2)) USHURU WA HUDUMA Na KIWANGO CHA ADA YA LESENI YA BIASHARA KWA MWAKA MALIPO YA USHURU WA HUDUMA KWA MWAKA(SHILINGI)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: This provision shows a fee schedule for traditional alcohol club licences and a form for admitting an offence and agreeing to pay the owed fee/tax plus a fine instead of going to court.
8. 0 hadi 15,000 20,000 hadi 35,000 40,000 hadi 45,000 50,000 hadi 60,000 65,000 hadi 100,000 105,000 hadi 150,000 155,000 hadi 200,000 Malipo ya leseni za vilabu vya pombe za asili 5000 10,000 15,000 30,000 40,000 50,000 100,000 12,000 kwa miezi sita _____________ JEDWALI LA PILI ________________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 9) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi …………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Kifungu cha …… cha Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya mwaka, 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 887 (Linaenedelea) Leo tarehe………….ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina………………………………..Saini………………………...... MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………….... Saini………………………….…………………………..………… Wadhifa: …………………………………………………………… Tarehe……………………………………………………………… 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 887 (Linaenedelea) Lakiri ya Halmashuri ya Kerywa imegongwa kwenye sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katikak Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Kyerwa uliofanyika Tarehe …. Mwezi… Mwaka…. na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- SACF. JAMES MARCO Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa MH. BAHATI HENERICO Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 20 Novemba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, ( Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 7
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in