Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa za Mwaka 2023
This section gives the by-law’s title: the Kyerwa District Council Markets and Fairs Tax By-Law of 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa za Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the by-law’s title: the Kyerwa District Council Markets and Fairs Tax By-Law of 2023. This by-law applies throughout the whole area of Kyerwa District Council. This section defines key terms used in the by-law, including officials, market actors, permits, markets, auctions, fees, groups, and produce. Halmashauri must run, manage, develop, clean, secure, allocate, and register market activities and traders. Halmashauri must appoint a Market Officer to oversee market development activities; it may also hire an agent to run the market, and that agent must follow the stated conditions and the agency contract.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa za Mwaka 2023
Showing 29 of 29
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the by-law’s title: the Kyerwa District Council Markets and Fairs Tax By-Law of 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa za Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the whole area of Kyerwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including officials, market actors, permits, markets, auctions, fees, groups, and produce.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “dalali” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa za sokoni kwa njia ya mnada kwa niaba ya mwenye bidhaa kwa mujibu wa sheria na taratibu za soko; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa mujibu Sheria Ndogo hii; “gulio” maana yake ni soko la wazi linalofanyika kwa cha wakati maalumu kwa kibali maalumu Halmashauri; “soko” maana yake ni eneo maalumu la biashara 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) lililotengwa na Halmashauri kwa matumizi ya kuuzia au kununulia bidhaa na inajumuisha gulio; “meza au kizimba” maana yake ni kitu au kifaa kinachotumika kuweka bidhaa kwa ajili ya kuuza sokoni au gulioni; “mfanyabiashara” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa sokoni au gulioni kwa jumla au rejareja; “Mkuu wa Soko” maana yake ni mtu yeyote aliyeteuliwa au aliyeajiriwa na Halmashauri kusimamia shughuli zote katika soko; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa na inajumuisha Afisa yeyote ya atakayeteuliwa Mkurugenzi; majukumu kutekeleza “mnada” maana yake soko la wazi ambalo mali au vitu mbalimbali vinauzwa kwa ushindani wa bei kwa kauli na kwa kibali maalumu cha Halmashauri; “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri; shirika ambalo “wadau wa soko” maana yake ni mfanyabiashara binafsi, vikundi vilivyoandikishwa katika kamati ya wadau wa soko au gulio na kuwasilishwa kwa mkuu wa soko, au vyama vya ushirika vinavyofanya shughuli za biashara katika soko; “ushuru” maana yake ni tozo inayolipwa baada au kabla ya kupata huduma katika soko au gulio; “vikundi” maana yake ni vikundi vya ushirika vya wafanyabiashara au umoja wa vikundi vya wafanyabiashara vilivyosajiliwa au kuandikishwa na kuwasilishwa katika kamati ya soko au gulio na kwa mkuu wa soko na kutambuliwa na Halmashauri; “zao” maana yake ni mavuno ya shambani au maliasili yanayoingizwa kwenye soko au ndani ya eneo la mamlaka ya Halmashauri. 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must run, manage, develop, clean, secure, allocate, and register market activities and traders.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kuanzisha, kusimamia na kuendesha masoko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) kuendeleza masoko; (c) kusimamia usafi na usalama wa masoko; (d) kusimamia ufikishaji wa huduma za kijamii katika soko; (e) kugawa na kupangisha soko kwa vyumba, meza au vizimba; (f) kutenga maeneo kwa ajili ya magulio; na (g) kusajili wafanyabiashara wote katika masoko yote ya Halmashauri. Mkuu wa Soko - 5 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mkuu wa Soko atakayeteuliwa
AI-assisted research summary: Halmashauri must appoint a Market Officer to oversee market development activities; it may also hire an agent to run the market, and that agent must follow the stated conditions and the agency contract.
5.-(1) Kutakuwa na Mkuu wa Soko atakayeteuliwa na Halmashauri kwa ajili ya kusimamia shughuli za uendelezaji wa Masoko pamoja na- (a) kusimamia ukusanyaji wa ushuru na ada mbalimbali; (b) kusimamia usajili wa wadau wa soko kwa kushirikiana na kamati ya wadau wa soko; (c) kuimarisha huduma za ulinzi, maji na umeme katika masoko; (d) kusimamia usafi na uondoshaji wa taka katika soko; (e) kuhakikisha kuwa bidhaa haziuzwi kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kwa shughuli hiyo; (f) kuzuia ujenzi holela katika soko; na (g) kutekeleza majukumu mengine yatakayoagizwa na Halmashauri. yoyote (2) Bila kujali masharti ya aya ndogo ya (1), Halmashauri inaweza kuajiri wakala ambaye atawajibika kusimamia uendeshaji wa soko kwa niaba yake. (3) Wakala atakayeajiriwa chini ya aya ndogo ya (2) atasimamia shughuli za uendeshaji wa soko kwa kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika aya ndogo ya (1) na masharti ya mkataba wa uwakala kati yake na Halmashauri. 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) Kamati ya Soko - 6 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na kamati ya wadau wa soko
AI-assisted research summary: The market stakeholders committee must be set up, each market cooperative group gets one representative, meetings happen monthly, the Market Chief serves as secretary, and the committee lasts three years.
6.-(1) Kutakuwa na kamati ya wadau wa soko ambayo itaundwa na wadau wa soko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Kila kikundi cha ushirika katika soko kitakuwa na mwakilishi mmoja katika kamati ya wadau wa soko. (3) Kamati ya wadau wa soko itatakiwa kuweka utaratibu maalumu wa kuwapata viongozi wake, kuwaondoa madarakani na uendeshaji wa shughuli zake na kuuwasilisha kwa Halmashauri. (4) Vikao vya kamati ya wadau wa soko vitafanyika mara moja kila mwezi. (5) Mkuu wa Soko atakuwa katibu katika vikao vyote vya kamati ya wadau wa soko. (6) Muda wa kamati ya soko kuwa madarakani ni miaka mitatu. Majukumu ya Kamati - 7 Verify source ↗
Kamati ya wadau wa soko itakuwa na majukumu
AI-assisted research summary: The market stakeholders committee must carry out the listed market-management duties, including checking businesses, improving welfare, ensuring discipline, collecting taxes and fees, keeping markets clean, and helping with security.
7. Kamati ya wadau wa soko itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuhakiki biashara zinazoendeshwa katika soko; (b) kuboresha ustawi wa wadau wa soko; (c) kuhakikisha uwepo wa nidhamu katika shughuli za soko; (d) kuhakikisha wadau wote wa soko na gulio wanalipa ushuru na ada kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (e) kukuza na kuendeleza mfumo wa biashara; (f) kuhakikisha kila eneo la mdau na soko kwa ujumla linakuwa safi muda wote; (g) kutekeleza kazi nyingine watakazoelekezwa na Mkuu wa Soko kwa mujibu wa Sheria ndogo hii; na (h) kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo masokoni. Kamati ndogo - 8 Verify source ↗
(1) Kamati ya wadau wa soko itaunda kamati
AI-assisted research summary: Kamati ya wadau wa soko must form subcommittees with four members from among its members, and it may form other subcommittees if it considers them appropriate.
8.-(1) Kamati ya wadau wa soko itaunda kamati ndogo zenye wajumbe wanne kutoka miongoni mwa wajumbe wa kamati ya wadau wa soko ambazo ni: 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) (a) kamati ndogo ya miundombinu na usafi; (b) kamati ndogo ya utawala na biashara; na (c) kamati ndogo ya ulinzi na usalama. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), kamati ya wadau wa soko inaweza kuunda kamati ndogo nyingine yoyote kwa kadri itakavyoona inafaa. Usajili wa wadau - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetaka kufanya biashara katika
AI-assisted research summary: Anyone who wants to do business in a market area must be registered by the Market Head working with the market stakeholders committee.
9. Mtu yeyote anayetaka kufanya biashara katika eneo la soko atatakiwa kusajiliwa na Mkuu wa Soko akishirikiana na kamati ya wadau wa soko kwa lengo la kumtambua na kumuorodhesha katika rejesta ya wadau wa soko. Utolewaji wa kibali kwa biashara ambazo hazikuwepo - 10 Verify source ↗
Mtu au mfanyabiashara yeyote ambaye anataka
AI-assisted research summary: Mtu au mfanyabiashara anayetaka kuanzisha biashara mpya au biashara isiyo na eneo ndani ya soko lazima aombe kibali kwa Halmashauri.
10. Mtu au mfanyabiashara yeyote ambaye anataka kufanya biashara ambayo awali haikuwepo au haikuwa na eneo ndani ya soko ataomba kibali kwa Halmashauri na masharti ya aya ya 9 yatatumika. Kufuta kibali - 11 Verify source ↗
Mkuu wa Soko anaweza kufuta kibali
AI-assisted research summary: The Market Officer may revoke a permit after 30 days’ notice if the permit holder meets specified grounds; a dissatisfied trader may object to the Director within 14 days, and the Director must decide within 7 days.
11. Mkuu wa Soko anaweza kufuta kibali kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hii, baada ya kutoa notisi ya siku thelathini, endapo mwenye kibali hicho- (a) atakuwa na malimbikizo ya ada au ushuru; (b) atakuwa amesimamisha shughuli zake kwa miezi mitatu bila taarifa; (c) atakuwa na mwenendo unaokiuka masharti ya Sheria Ndogo hii; (d) atawashawishi wengine kutozingatia Sheria Ndogo hii au kusababisha uvunjaji wa amani; au wafanyabiashara (e) atatumia chumba, kibanda, meza au kizimba alichopanga kinyume na madhumuni ya kufanyia biashara kama yalivyoainishwa kwenye mkataba wa upangishaji au maelekezo yatakayotolewa na Halmashauri. (2) Mfanyabiashara ambaye hataridhika na uamuzi wa kufutiwa kibali anaweza kuwasilisha pingamizi lake kwa Mkurugenzi katika kipindi cha siku kumi na nne tangu 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) tarehe ya kufutiwa kibali. (3) Baada ya kupokea pingamizi, Mkurugenzi atatakiwa kutoa uamuzi wa pingamizi ndani ya siku saba tangu tarehe ya kupokea pingamizi husika. Wajibu wa mfanyabisha ra - 12 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara katika eneo
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wote katika eneo la soko lazima wajiandikishe kwa Mkuu wa Soko na wazingatie sheria za usafi, matumizi ya maeneo, malipo ya ushuru na ada, na marufuku mbalimbali za tabia na shughuli ndani ya soko.
12. Kila mfanyabiashara katika eneo la soko atakuwa na wajibu wa- (a) kusajiliwa na Mkuu wa Soko katika rejesta ya wadau wa soko; (b) kulinda na kuhifadhi miundombinu ya soko; (c) kufanya biashara katika maeneo yanayoruhusiwa; (d) kufanya usafi katika eneo lake la biashara; (e) kulipa ushuru na ada kwa wakati; (f) kutobandika au kutobandua tangazo bila idhini ya Mkuu wa Soko; (g) kutotumia lugha ya matusi, kuudhi au kashfa katika eneo la soko; (h) kushiriki usafi wa jumla wa soko; (i) kutoweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la soko; (j) kutofanya shughuli za kisiasa katika eneo la soko; (k) kutotupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; (l) kutowasha moto maeneo yasiyohusika ndani ya soko; na (m) kuheshimu masharti ya upangaji aliyopewa na Halmashauri na maelekezo atakayopewa na Halmashauri, Mkuu wa Soko na kamati ya wadau wa soko. Muda wa biashara - 13 Verify source ↗
(1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa
AI-assisted research summary: The market must stay open every day during the stated hours, and the Market Master may close it for repairs or other emergencies.
13.-(1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. (2) Mkuu wa Soko, kwa kushauriana na soko kwa ajili ya Mkurugenzi, anaweza kufunga matengenezo au sababu nyingine yoyote ya dharura pale 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) Ushuru wa soko au gulio Kodi ya upangishwaj i Usimamizi wa magari itakapoonekana inafaa. (3) Isipokuwa kwa sababu nyingine za dharura, Mkuu wa Soko hatakuwa na mamlaka ya kufunga soko kwa sababu za matengenezo isipokuwa tu baada ya kutoa notisi ya siku saba kwa wadau wa soko kuhusu kusudio la kufunga soko kwa ajili ya matengenezo. - 14 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa soko kutoka
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ichukue ushuru wa soko kutoka kwa wafanyabiashara waliosajiliwa katika eneo la soko, na kila mfanyabiashara lazima alipe ushuru wa bidhaa za jumla katika magulio na minada kwa viwango vilivyo kwenye ratiba za sheria ndogo.
14.-(1) Halmashauri itatoza ushuru wa soko kutoka kwa kila mfanyabiashara aliyesajiliwa kufanya biashara katika eneo la soko kwa kadri itakavyoelekezwa. (2) Kila mfanyabiashara atawajibika kulipa ushuru wa bidhaa za jumla katika magulio na minada katika Halmashauri kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza na la Pili la Sheria Ndogo hii. - 15 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabishara katika soko atalipa kodi
AI-assisted research summary: Market traders must pay the rent tax for a kiosk or stall under the rental contract, and the council may allow a business stall to be built in the market area under a special agreement.
15.-(1) Kila mfanyabishara katika soko atalipa kodi ya upangishwaji kizimba au kibanda kwa mujibu wa mkataba wa upangishwaji. (2) Halmashauri inaweza, kwa makubaliano maalum, kumruhusu mtu yeyote kujenga banda la biashara katika eneo la soko. - 16 Verify source ↗
(1) Magari yote yanayotumika kusafirisha
AI-assisted research summary: Vehicles carrying produce or goods for the market must unload only in designated areas. The Market Manager may control how many vehicles may unload and may remove vehicles from the designated area when necessary.
16.-(1) Magari yote yanayotumika kusafirisha mazao au bidhaa kwa ajili ya soko yatashusha bidhaa katika maeneo yaliyoainishwa kwa shughuli hiyo. (2) Mkuu wa Soko atakuwa na mamlaka ya kupanga na kusimamia idadi ya magari yatakayoruhusiwa kushusha bidhaa au mazao sokoni. (3) Mkuu wa Soko anaweza kuondoa gari lolote kutoka katika sehemu iliyotengwa endapo itabidi kufanya hivyo. Kibali cha minada na magulio - 17 Verify source ↗
(1) Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine
AI-assisted research summary: Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine inaweza kufanyika katika masoko ikiwa kuna kibali maalumu cha Halmashauri.
17.-(1) Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine itaruhusiwa kufanyika kwenye masoko kwa kibali maalumu cha Halmashauri. (2) Halmashauri inaweza kutoa kibali maalumu cha kufanyika kwa magulio katika maeneo yatakayotengwa na 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) Halmashauri. Usafi wa soko - 18 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabiashara anayefanya biashara
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara katika eneo la soko lazima waweke sehemu zao katika hali ya usafi wakati wote na wazingatie kanuni za afya.
18.-(1) Kila mfanyabiashara anayefanya biashara katika eneo la soko atawajibika kuweka eneo lake katika hali ya usafi wakati wote. (2) Mkuu wa Soko, kwa kushirikiana na kamati ya wadau wa soko, atasimamia usafi wa jumla wa soko siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi. (3) Kila mfanyabiashara atatakiwa kuzingatia kanuni za afya. Mbwa - 19 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kuingiza au kuruhusu
AI-assisted research summary: Anyone is prohibited from bringing dogs into the market or allowing them to be brought in.
19. Mtu yeyote hataruhusiwa kuingiza au kuruhusu kuingiza mbwa ndani ya soko. Mifugo kutoingizwa sokoni - 20 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kuingiza mifugo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuingiza mifugo ndani ya soko, magulio au minada, isipokuwa katika sehemu maalumu iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya biashara ya mifugo.
20. Mtu yeyote hataruhusiwa kuingiza mifugo sehemu yoyote ndani ya soko, magulio au minada isipokuwa sehemu maalumu iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya biashara ya mifugo. Minada Biashara ya kutembeza Tahadhari ya moto
Part
sehemu yoyote ndani ya soko, magulio au minada
- 21 Verify source ↗
(1) Mazao yatakayoletwa sokoni kwa ajili ya
AI-assisted research summary: Mazao yanayoletwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa kwa mnada lazima yapokelewe na dalali aliyechaguliwa na wafanyabiashara kwa makubaliano na kamati ya soko, kisha yauzwe kwa mnada katika eneo lililotengwa na Halmashauri.
21.-(1) Mazao yatakayoletwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa kwa mnada yatapokelewa na dalali atakayeteuliwa na wafanyabiashara na kukubaliana na kamati ya soko. (2) Dalali aliyeteuliwa atauza mazao hayo kwa mnada katika eneo lililotengwa na Halmashauri kwa shughuli hiyo. - 22 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kutembeza bidhaa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kutembeza bidhaa ndani ya soko bila kibali cha Halmashauri.
22. Mtu yeyote hataruhusiwa kutembeza bidhaa ndani ya soko bila kibali cha Halmashauri. - 23 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya shughuli
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kufanya shughuli yoyote inayohusisha matumizi ya moto bila idhini ya maandishi ya Halmashauri.
23. Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya shughuli yoyote inayohusisha matumizi ya moto isipokuwa kwa idhini ya maandishi ya Halmashauri. Uuzaji wa pombe - 24 Verify source ↗
Mfanyabiashara yeyote hataruhusiwa kuuza
AI-assisted research summary: A trader may not sell alcohol in a market, fair, or auction without a permit and liquor licence from the Council.
24. Mfanyabiashara yeyote hataruhusiwa kuuza pombe ndani ya soko, gulio, mnada bila kibali na leseni ya vileo iliyotolewa na Halmashauri. 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) Makosa na adhabu Kufifilisha kosa - 25 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti yoyote Sheria
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii anatenda kosa na anaweza kupewa faini, kifungo, au vyote kwa pamoja.
25. Mtu yeyote atakayekiuka masharti yoyote Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi laki mbili na isiyozidi Shilingi Milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote faini na kifungo kwa pamoja. - 26 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii Shilingi 200,000 ikiwa mkosaji anakiri kwa hiari na kukubali kujaza fomu ya Jedwali la Tatu na kutimiza wajibu wake.
26. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi laki mbili iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii na kuwa tayari kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. _______________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 14(2)) USHURU WA BIDHAA MINADANI NA KATIKA MAGULIO Namba Aina ya Bidhaa Kiwango cha Ada kwa Siku (Shilingi)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 14 Verify source ↗
Section 14
AI-assisted research summary: Wauza mitumba na baadhi ya wauzaji waliotajwa wanatozwa ada/ushuru kulingana na eneo na kundi la bidhaa lililotajwa.
14. Wauza mitumba katika eneo lisilozidi ukubwa wa mita nne (4) za mraba kila eneo linalozidi mita hizo 4 za mraba italipiwa Wauza vinywaji (bia, maji na soda Wauza nafaka Wauza madawa ya asili Wauza vipuri vya baiskeli, pikipiki, magari Wauza dagaaa Wauza samaki Wauza chumvi, nyama na mboga za majani Wauza vyungu Wauza vyombo vya nyumbani Wauza viatu Wauza nguo mpya Mafundi baiskeli Bidhaa nyingine ambazo hazikutajwa 500/= 200/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 9 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) - 18 Verify source ↗
Section 18
AI-assisted research summary: Mnunuzi hulipa ushuru kwa kila mnyama anayeuzwa mnadani, kwa viwango tofauti kulingana na aina ya mnyama.
18. Punda atakayeuzwa mnadani mnunuzi atalipa kwa kila punda atakayemnunua Mbuzi, nguruwe au kondoo atakayeuzwa mnadani – mnunuzi atalipa kwa kila mbuzi, nguruwe au kondoo atakayeuzwa mnadani, mnunuzi atalipa ushuru kwa kila mfugo Ng’ombe atakayeuzwa mnadani-mnunuzi atalipa kwa kila Ng’ombe Mifugo mingine ambayo haikutajwa- mnunuzi atalipa ushuru kwa mfugo 1,500/= 1,500/= 5000/= 500/= ______________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 14(2)) USHURU WA BIDHAA ZA JUMLA KATIKA MASOKO Namba Aina ya Bidhaa
Part
JEDWALI LA PILI
- 13 Verify source ↗
Section 13
AI-assisted research summary: The section lists market goods and vehicle categories with daily fee amounts in shillings.
13. Gunia la Mahindi lenye uzito wa kg. 100 Gunia la Maharage lenye uzito wa kg100 Gunia la Viazi vitamu lenye uzito wa kg. 100 Gunia la Viazi Ulaya lenye uzito wa kg. 100 Gunia la Vitunguu lenye uzito wa kg. 100 Gunia la Nazi lenye uzito wa kg. 100 Gunia la Parachichi lenye uzito wa kg. 100 Gunia la Vitunguu Swaumu lenye uzito wa kg. 100 Gunia la Matunda lenye uzito wa kg. 100 Tenga la Mazao ya Mbogamboga kama Nyanya, Matole, Kabeji, Pilipili Hoho, Karoti, Malimao na mazao mengineyo Gari la Matunda Tani 1-3 Gari la Matunda Tani 4 - 8 Gari la Matunda zaidi ya Tani 8 Kiwango cha Ada kwa Siku (Shilingi) 1000/= 1000/= 1000/= 1000/= 1000/= 1000/= 1000/= 1000/= 1000/= 2000/= 10,000/= 15,000/= 20,000/= 10 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) ________________ JEDWALI LA TATU ________________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 26) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi; ……………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya; ………………………………………..……. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka; …….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ….. ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe:…....... ya Mwezi:………… Mwaka:………….. Jina:…………………………………..……………………. Saini:…………………………..…………………………… MBELE YANGU: Jina:…………………………….………..…………………. Wadhifa: …………………………………………………… Saini: ……………………………………………………….. Tarehe: ……………………………………………………… 11 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 889 (Linaendelea) Lakiri la Halmashsuri ya Kyerwa imegongwa kwenye sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katikak Mkutano wa Baraza la Madiwani Halamshauri ya Wilaya ya Kyerwa uliofanyika Tarehe ..…. Mwezi…… Mwaka…… na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- SACF. JAMES MARCO JOHN Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa MH. BAHATI HENERICO Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 20 Novemba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 12
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa za Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in