Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
This section gives the short title of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law. This by-law applies throughout the entire area of Kyerwa District Council. This section defines key terms used in the by-law, including fee, council, permit, construction minerals, director, tax, and agent. Anayetaka kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi ndani ya Halmashauri lazima aombe kibali kwa Mkurugenzi kwa fomu maalumu. Mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi lazima iombe kibali kama kilivyoainishwa, ilipe ada ya shilingi laki tatu, izingatie masharti ya Sheria Ndogo na ya kibali, na ilipe ushuru na tozo nyingine za Halmashauri.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Kyerwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including fee, council, permit, construction minerals, director, tax, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni malipo yatakayolipwa na mtu yeyote kwa Halmashauri kwa ajili ya kupata kibali kinachotolewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “madini ya ujenzi” maana yake ni tarazo, moramu, udongo, kifusi, kokoto, mawe, mchanga, chokaa na madini mengine yanayotumika katika ujenzi; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa na atakayeteuliwa inajumuisha Afisa yeyote 1 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 890 (Linaendelea) kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; tozo “ushuru” maana yake ni inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli zinazohusu ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri; “wakala” maana yake mtu, taasisi, kikundi cha watu, kampuni au asasi iliyoteuliwa na Halmashauri kukusanya ushuru wa madini ya ujenzi kwa niaba yake. Maombi ya kibali - 4 Verify source ↗
(1) Mtu, taasisi au kampuni inayokusudia
AI-assisted research summary: Anayetaka kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi ndani ya Halmashauri lazima aombe kibali kwa Mkurugenzi kwa fomu maalumu.
4.-(1) Mtu, taasisi au kampuni inayokusudia kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri itatakiwa kuwasilisha kwa Mkurugenzi maombi ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi kupitia fomu maalumu itakayotolewa na Halmashauri. (2) Maombi ya kibali yataambatishwa na taarifa zifuatazo: (a) leseni ya uchimbaji wa madini iliyotolewa na mamlaka husika; (b) aina ya madini yanayokusudiwa kuchimbwa; (c) uthibitisho wa umiliki pamoja na ukubwa wa eneo linalokusudiwa kuchimbwa madini ya ujenzi; (d) mpango wa utunzaji wa mazingira katika eneo la machimbo; na (e) muhtasari wa mkutano wa kijiji ambacho uchimbaji wa madini ya ujenzi utafanyika ukionyesha kukubaliana na uchimbaji huo. (3) Ndani ya muda wa siku saba tangu kupokea maombi, Mkurugenzi atatakiwa kukagua eneo ambalo uchimbaji wa madini ya ujenzi unakusudiwa kufanyika ili kujiridhisha iwapo eneo hilo linafaa kwa shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi. tangu (4) Ndani ya muda wa siku saba kukamilika kwa ukaguzi wa eneo linaloombewa kibali, Mkurugenzi atatakiwa kukubali au kukataa maombi hayo na endapo atakataa atatakiwa kutoa sababu za kukataa maombi hayo. 2 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 890 (Linaendelea) Wajibu wa mpewa kibali - 5 Verify source ↗
Mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha
AI-assisted research summary: Mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi lazima iombe kibali kama kilivyoainishwa, ilipe ada ya shilingi laki tatu, izingatie masharti ya Sheria Ndogo na ya kibali, na ilipe ushuru na tozo nyingine za Halmashauri.
5. Mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi itatakiwa: (a) kuomba kibali kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii; (b) kulipa ada ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi ya kiasi cha shilingi laki tatu; (c) kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii na masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi; na (d) kulipa na ushuru tozo mbalimbali zitakazotozwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii au Sheria Ndogo nyingine iliyotungwa na Halmashauri. Muda wa uchimbaji na masharti ya usafirishaji
Part
Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii;
- 6 Verify source ↗
(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi
AI-assisted research summary: Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri lazima zifanyike kati ya saa 12 asubuhi na saa 12 jioni kila siku; Mkurugenzi anaweza kutoa kibali maalumu kwa shughuli hizo kufanyika nje ya muda huo, na mmiliki wa gari linalosafirisha madini hayo lazima ahakikishe gari limefunikwa wakati wa usafirishaji.
6.-(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri zitafanyika kuanzia Saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi Saa kumi na mbili jioni ya kila siku. (2) Bila kujali masharti ya aya ndogo ya (1), Mkurugenzi anaweza kutoa kibali maalumu kuruhusu shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi kufanyika nje ya muda ulioainishwa katika aya ndogo ya (1). (3) Kila mmiliki wa gari linalosafirisha madini ya ujenzi atatakiwa kuhakikisha kuwa gari hilo limefunikwa wakati wote wa usafirishaji wa madini ya ujenzi. Ushuru wa madini ya ujenzi - 7 Verify source ↗
Kutakuwa na ushuru wa madini ya ujenzi
AI-assisted research summary: Mnunuzi au msafirishaji wa madini ya ujenzi lazima alipe ushuru wa madini ya ujenzi kwa kiwango kilicho katika Jedwali la Pili.
7. Kutakuwa na ushuru wa madini ya ujenzi ambao utalipwa na mnunuzi au msafirishaji wa madini ya ujenzi kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. Vituo vya ukaguzi - 8 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo
AI-assisted research summary: Vigari au vyombo vinavyobeba madini ya ujenzi lazima visimame katika kituo cha ukaguzi na kuonyesha stakabadhi ya kielektroniki ya kulipa ushuru.
8.-(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo ya ushuru wa madini ya ujenzi katika njia zinazoingia au kutoka katika maeneo ya machimbo ya madini ya ujenzi. 3 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 890 (Linaendelea) Matumizi ya stakabadhi ya kielektroniki Kufutwa au kusimamishwa kwa kibali Wakala Makosa na adhabu (2) Kila dereva wa gari au chombo chochote cha usafiri kilichobeba madini ya ujenzi atatakiwa kusimama katika kituo cha ukaguzi wa malipo ya ushuru wa madini ya ujenzi na kuonesha stakabadhi ya kielektroniki kuthibitisha kulipwa kwa ushuru wa madini ya ujenzi yaliyo katika gari au chombo cha usafiri anachoendesha. - 9 Verify source ↗
Halmashauri itatakiwa kutoza ada au ushuru
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima kutoza ada au ushuru kwa kutumia mashine za kielektroniki.
9. Halmashauri itatakiwa kutoza ada au ushuru kwa kutumia mashine za kielektroniki. inaweza - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kufuta au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi ikiwa masharti yamekiukwa, lakini lazima itoe notisi ya siku 7 kabla na ibainishe sababu. Ikifutwa au ikisitishwa, mwenye kibali lazima aache uchimbaji.
10.-(1) Halmashauri au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi endapo itajiridhisha kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Sheria Ndogo hii au masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi. kufuta (2) Kabla ya kufuta au kusimamisha kibali, Halmashauri taasisi au itatakiwa kutoa kwa mtu, kampuni iliyopewa kibali notisi ya siku saba ya kusudio la kufuta au kusimamisha kibali. (3) Notisi itakayotolewa kwa mujibu wa aya ndogo ya (2) itaainisha sababu za kufuta au kusimamisha kibali husika. (4) Endapo kibali kitafutwa au kusimamishwa, mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi itakoma kuchimba madini hayo. - 11 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kuteua mtu, kikundi
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua mtu, kikundi cha watu, taasisi au kampuni kukusanya ushuru kwa niaba yake.
11. Halmashauri inaweza kuteua mtu, kikundi cha watu, taasisi au kampuni kukusanya ushuru kwa niaba yake. - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuanzisha, kusafirisha, au kuchimba madini ya ujenzi kinyume cha kibali, ushuru, muda ulioruhusiwa, au masharti ya usafirishaji; ukiukaji ni kosa la jinai.
12. Mtu yeyote ambaye- (a) ataanzisha machimbo ya madini ya ujenzi bila kuwa na kibali kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hii; (b) atasafirisha madini ya ujenzi bila kulipa ushuru; 4 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 890 (Linaendelea) (c) atachimba madini ya ujenzi kabla au baada ya muda ulioruhusiwa kuchimba; (d) atasafirisha madini ya ujenzi katika gari ambalo halijafunikwa; au (e) atamshawishi mtu au kundi la watu kutolipa ushuru, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi laki mbili na isiyozidi Shilingi Milioni moja au kifungo kisichopungua mwaka mmoja na kisichozidi miaka miwili au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. - 13 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji Shilingi laki mbili, ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na kukubali kujaza fomu maalumu na kutimiza wajibu wake. Pia, kibali cha kuchimba madini ya ujenzi ni cha miezi kumi na mbili tu.
13. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi laki mbili iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii na kuwa tayari kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Kufifilisha kosa 5 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 890 (Linaendelea) ________________ JEDWALI LA KWANZA __________________ Limetengenezwa chini ya aya ya 5(a)) KIBALI CHA UCHIMBAJI WA MADINI YA UJENZI Kibali hiki kimetolewa kwa Bw/Bi ………………………………….……wa SLP………………,KYERWA. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ameridhia ndugu mtajwa hapo juu, aendeshe shughuli za Kuchimba madini ya Ujenzi katika eneo la …………………………kijiji cha …………………………….kata ya …………………………… baada ya kufanya ukaguzi katika eneo husika ili kutathimini athari za Mazingira. Kutokana na uzingatiaji wa athari za Mazingira Mchimbaji anaruhusiwa kuchimba madini ya ujenzi katika eneo hilo kwa muda wa miezi kumi na mbili tu. Mwombaji analazimika kuomba tena kibali baada ya muda huo kuisha na ukaguzi utafanyika tena. TAMKO LA MWOMBAJI; MIMI…………………………………………………………Nipo tayari kufuata masharti ya kibali hiki cha Uchimbaji wa Madini ya Ujenzi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa lengo la kutunza na kuhifadhi mazingira. Nathibitisha kwa hiari yangu nimeelewa vema kibali hiki. Jina: ……………………………… Saini …………Tarehe ………………… KWA MATUMIZI YA OFISI; Mwombaji amelipia Shilingi …………………….tarehe…………….mwezi………….mwaka………….. (Ambatanisha stakabadhi ya malipo na fomu hii) Jina la Afisa aliyetoa kibali ……………………… Saini …………… Tarehe ………………. 6 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 890 (Linaendelea) __________ JEDWALI LA PILI ______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 7) USHURU WA MADINI YA UJENZI Aina ya Madini Na.
Part
JEDWALI LA PILI
- 5 Verify source ↗
Mawe, Moramu,
AI-assisted research summary: This provision shows fee amounts for mawe, moramu, mchanga na kokoto by trip or volume, and includes a confession form for admitting a violation and paying the owed fee or tax plus a fine.
5. Mawe, Moramu, Mchanga na Kokoto Ujazo /Tani Tani 3 –Tani 7 Tani 3 –Tani 7 Tani 3 –Tani 7 Tani 3 –Tani 7 Zaidi ya Tani 7 Kiwango cha Ada (Shilingi) 3,000 kwa tripu 2,000 kwa tripu 2,000 kwa tripu 5,000 kwa tripu 3% ya bei ya madini husika _______________ JEDWALI LA TATU _______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 13) HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi;………………………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka;…….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya….. ya Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023. ya;………………………………………..…….ambaye Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe:…....... ya Mwezi:………… Mwaka:………….. Jina:…………………………………..……………………. Saini:…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jina:…………………………….………..…………………… 7 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 890 (Linaendelea) Cheo:…………………………………………………..……. Saini:………………………………………………………… Tarehe:………………………………………………………. 8 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 890 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Kerywa imegongwa kwenye sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Kerywa uliofanyika Tarehe …. Mwezi… Mwaka…. na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- SACF. JAMES MARCO JOHN Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa MH. BAHATI HENERICO Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 20 Novemba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, ( Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in