Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya mwaka 2023
This section gives the short title of the by-law: Musoma District Council Guest House Tax By-Law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law: Musoma District Council Guest House Tax By-Law, 2023. This by-law applies throughout the entire area of Musoma District Council. This section defines key terms used in the by-laws for guest houses in Musoma District. Halmashauri inatoza na kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kutoka kwa kila mmiliki, kwa kiwango cha asilimia 10 ya mapato ya mwezi husika. Mlipa ushuru must keep guest records, register guests, maintain safety and hygiene, provide required amenities and receipts, pay guesthouse tax to the council within 15 days after the sales month ends, and allow inspections.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya mwaka 2023
Showing 24 of 24
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law: Musoma District Council Guest House Tax By-Law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Musoma District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-laws for guest houses in Musoma District.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “daftari la wageni” maana yake ni kitabu Maalumu kilichoandaliwa na Mmiliki au kilicho nunuliwa kwa lengo la kusajili na kutunza kumbukumbu za wageni wanaolala kwenye nyumba ya kulala wageni. lengo “gharama ya malazi” maana yake ni kiasi cha fedha kinachotozwa na mmiliki wa nyumba ya kulala wageni kwa mtu ambaye anapata huduma ya malazi. “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya 1 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) Musoma. “hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho wa mwezi zinazowasilishwa na mmiliki wa nyumba ya kulala wageni baada ya kipindi cha hesabu pamoja na nyaraka au maelezo yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. “kipindi cha hesabu” maana yake ni muda ambao mmiliki wa nyumba ya kulala wageni anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara yake; “marejesho” maana yake ni taarifa inayotaja jina la nyumba ya kulala wageni, aina ya vyumba, gharama ya kila aina vyumba ya ikiwa ni pamoja na ushuru vilivyopangishwa unaopaswa kulipwa kwa mwezi husika. chumba, jumla ya “mgeni” maana yake ni mtu yeyote ambaye hulipa pango la kukaa kwenye chumba cha kulala wageni aidha kwa siku nzima au sehemu ya siku nzima; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza kazi za Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni” maana yake ni mtu binafsi au kampuni inayomiliki nyumba ya kulala wageni inayopaswa kuwa na leseni ya kufanya biashara ya kutoa huduma ya malazi katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Musoma; “nyumba ya kulala wageni” maana yake ni jengo lililojengwa kwa ajili ya kuwapokea wasafiri au wageni kwa lengo ya kupata kipato au faida isipokuwa, mabweni, jengo la kupumzikia viongozi wa Serikali na jengo lililosajiliwa chini ya Sheria ya Utalii kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii; “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba yake. shirika ambalo 2 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) Utozaji wa ushuru wa hoteli au nyumba ya kulala wageni Wajibu wa mlipa ushuru - 4 Verify source ↗
Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: Halmashauri inatoza na kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kutoka kwa kila mmiliki, kwa kiwango cha asilimia 10 ya mapato ya mwezi husika.
4. Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kutoka kwa kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni kwa kiwango cha asilimia kumi ya mapato ya nyumba ya kulala wageni kwa mwezi husika. - 5 Verify source ↗
Mlipa ushuru atakuwa na wajibu ufuatao
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru must keep guest records, register guests, maintain safety and hygiene, provide required amenities and receipts, pay guesthouse tax to the council within 15 days after the sales month ends, and allow inspections.
5. Mlipa ushuru atakuwa na wajibu ufuatao: (a) kuwa na daftari la kumbukumbu kwa ajili ya kusajiri wageni wote wanaolala katika nyumba ya kulala wageni kutoka Halmashauri; (b) kuhakikisha kuwa kila mgeni anasajiliwa kwenye daftari la kulala wageni kwa kuingiza zote muhimu bila kujali muda taarifa aliokitumia chumba; (c) kuwa na ulinzi na usalama wa kutosha wa mgeni na mali zao; (d) kuhakikisha kuwa nyumba ya kulala wageni inakuwa safi muda wote na masharti mengine ya usafi yanafuatwa; (e) Kuwa na nyumba ya kulala wageni inayokidhi na kufuata maelekezo yote; (f) Kuendesha biashara hiyo kwa kuwa na leseni ya biashara hai; (g) Kuweka mahitaji yote ya msingi ambayo ni sabuni ya kuogea, mswaki, dawa ya meno, kondomu, maji ya moto au baridi, taulo, mashuka masafi, neti safi na isiyo na matobo na mahitaji mengine muhimu kwenye chumba cha kulala mgeni; (h) Kuhakikisha kuwa kila kitanda hakitumiki na watu wawili au zaidi wa jinsia moja; (i) kutoa stakabadhi halali kulingana na malipo aliyolipa mgeni; (j) kulipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni au nyumba ya kulala wageni kwa Halmashauri ndani ya siku 15 baada ya mwezi husika wa mauzo kuisha; 3 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) Taarifa ya hesabu za mwisho wa mwezi (k) kumruhusu Afisa Mwidhiniwa kufanya ukaguzi wa huduma kama inatolewa kwa mujibu wa Sheria; na (l) kumruhusu Afisa Mwidhiniwa kukagua daftari la malazi kama wageni wote wanasajiliwa na wamejaza taarifa zao na baada ya ukaguzi atasaini kitabu husika na kuweka muhuri kuthibitisha ukaguzi uliofanyika. - 6 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala
AI-assisted research summary: A guesthouse tax payer must keep a special guest register and submit accurate monthly guest and tax information to the Council using the prescribed forms.
6.-(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni anatakiwa kuwa na daftari maalum kwa ajili ya kuorodhesha wageni wanaoingia kupata huduma ya malazi. (2) Kila mlipa ushuru atatakiwa kuwasilisha Halmashauri taarifa sahihi ya idadi ya wageni kwa kila chumba kilichopangishwa pamoja na ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa kila mwisho wa mwezi kwa kutumia Fomu Na. H.L 1, H.L 2 na H.L 3 kama zilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. Endapo itabainika kuwa kuna mgeni au wageni ambao la wageni, hawajaorodheshwa katika daftari maalum Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kumtoza mmiliki huyo ushuru kwa kiwango cha idadi ya vyumba vyote vya nyumba hiyo ya kulala wageni. Uwezo wa kutaka taarifa - 7 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kutaka taarifa kimaandishi
AI-assisted research summary: The Director may require written information from any person or institution liable to pay the guest house tax under this bylaw.
7. Mkurugenzi anaweza kutaka taarifa kimaandishi kwa mtu yeyote au taasisi yoyote inayopaswa kulipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Uwezo wa kuingia kwenye jengo - 8 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye nyumba ya kulala wageni wakati wa kazi, na pia baada ya kazi, ili kukagua usahihi wa vitabu vya wageni na taarifa nyinginezo.
8.-(1) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye nyumba ya kulala wageni wakati wa muda wa kazi kwa lengo la kufanya ukaguzi na tathmini ya usahihi wa uandikishaji wageni katika vitabu vya wageni na taarifa nyinginezo. (2) Bila kuathiri aya ndogo ya (1), Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye nyumba ya kulala wageni baada ya muda wa kazi kwa lengo la kufanya 4 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) ulipaji wa ushuru na riba Uteuzi wa wakala Majukumu ya wakala ukaguzi na tathmini ya usahihi wa uandikishaji wageni katika vitabu vya wageni na taarifa nyinginezo kama atakavyoona inafaa kufanyiwa uchunguzi kwa ajili ya kupata na kujua idadi sahihi ya wageni na ushuru anaotakiwa kulipa ushuru. - 9 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni lazima alipe ushuru sawa na asilimia 10 ya mapato ya nyumba hiyo kila tarehe 1 ya mwezi unaofuata.
9.-(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni anapaswa kulipa ushuru katika kiwango cha asilimia kumi ya mapato ya nyumba ya kulala wageni kila tarehe mosi ya mwezi unaofuata. (2) Ushuru ambao hautalipwa kwa wakati utatozwa riba ya asilimia ishirini na tano ya ushuru uliopaswa kulipwa kwa mwezi husika. - 10 Verify source ↗
Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa niaba yake.
10. Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa niaba yake. - 11 Verify source ↗
Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri atakuwa na
AI-assisted research summary: A council-appointed agent must ensure guest-house owners use a special guest register and must submit collected tax on time during the period set by the contract.
11. Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuhakikisha kuwa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni wanatumia daftari maalum la kuandikishia wageni; na (b) kuwasilisha ushuru aliokusanya kwa wakati katika kipindi maalum kwa mujibu wa mkataba wake. Makosa - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: This section makes it an offence for any person to commit several guesthouse-related compliance failures or acts, including not filing required guesthouse tax/accounting information, not using the guest register, not showing records for audit, giving incorrect guest numbers, operating without a licence, failing health checks for providers/managers, making inaccurate guest books or records, or blocking the Director/authorized officer.
12. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo: atashindwa kuwasilisha ushuru wa nyumba ya kulala wageni na hesabu sahihi kulingana na idadi ya wageni waliopata huduma katika nyumba ya kulala wageni; (a) atashindwa kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa Halmashauri katika muda uliowekwa; (b) hatatumia daftari maalum la kuandikishia wageni; (c) atashindwa kuonyesha kumbukumbu yoyote au 5 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) nyaraka kwa ajili ya ukaguzi wa hesabu zake; (d) hatawasilisha taarifa sahihi kuhusu idadi ya wageni katika nyumba yake ya kulala wageni; (e) atafanya biashara ya nyumba ya kulala wageni bila leseni; (f) watoa huduma wake au wasimamizi wa nyumba ya kulala wageni hawatapima afya; (g) ataandaa au kutengeneza au kusababisha kuandaliwa au kutengenezwa kitabu cha wageni, mahesabu au kumbukumbu zozote za nyumba ya kulala wageni zisizo sahihi; na (h) atamzuia au atajaribu kumzuia Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Adhabu Kufifilisha Kosa - 13 Verify source ↗
Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa chini
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence under this subsidiary legislation must pay a fine, serve imprisonment, or both.
13. Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atatakiwa kulipa faini ya kiasi kisichopungua Shilingi laki mbili na kisichozidi Shilingi Milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. - 14 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji Shilingi laki mbili, ikiwa anakiri kosa, yuko tayari kujaza fomu maalum ya Jedwali la Pili, na kulipa ushuru anaodaiwa.
14. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ushuru anaodaiwa. 6 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) ________________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 6(2)) MAREJESHO YA KILA SIKU FOMU NA. H.L 1 Kwa Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. S.L.P 344, Musoma. Jina la nyumba ya kulala wageni Siku ya marejesho:..................................................... Aina ya chumba Jumla ya vyumba Vyumba vilivyopan gishwa Bei ya kila chumba (ukijumlisha gharama za Kifungua kinywa na chakula Jumla ya gharama Maoni Single Double Triple Suit Vinginevyo (Eleza) Jumla 7 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) MAREJESHO YA MWEZI FOMU NA. H.L 2 Kwa Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. S.L.P 344, Musoma.
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Marejesho kwa ajili ya mwezi wa……………. Mwaka 20……
AI-assisted research summary: A monthly return form for a guest house, asking for the establishment’s details, room types, rented rooms, and monthly guest-house tax total.
1. Marejesho kwa ajili ya mwezi wa……………. Mwaka 20…….. Kutoka: ………………………………………(Jina la nyumba ya kulala wageni). Anuani: ………………………..………………….. Namba ya Simu:…………………………………… Kijiji cha: ……..……………………………………. Kata ya: ……………………………………………. Aina ya chumba Jumla ya vyumba Vilivyopangishwa kwa mwezi Jumla ya tozo ya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa mwezi Maoni Single Double Triple Suite Vinginevyo (Eleza) Jumla - 2 Verify source ↗
Jumla ya ushuru kwa mwezi Shilingi: …………….…………………………
AI-assisted research summary: This section shows fields for monthly tax amount, applicable tax rate, and tax due.
2. Jumla ya ushuru kwa mwezi Shilingi: …………….………………………….. Kiwango cha ushuru kinachotumika Shilingi: ………………………………. Kiasi cha ushuru kinachodaiwa Shilingi: …………………………………….. - 3 Verify source ↗
Pamoja na marejesho hayo, tafadhali pokea kiasi cha pesa taslimu/Hundi Na………….. ya
AI-assisted research summary: Hii ni sehemu ya fomu ya kupokea marejesho ya ushuru wa nyumba ya kulala wageni na kuthibitisha maelezo yaliyotolewa.
3. Pamoja na marejesho hayo, tafadhali pokea kiasi cha pesa taslimu/Hundi Na………….. ya kiasi cha Shilingi. ………..…………….. Nathibitisha kwamba maelezo haya ni ya kweli na kiasi cha Ushuru wa nyumba ya kulala wageni unaodaiwa kimekokotolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo ya Ushuru wa nyumba za kulala wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Tarehe: ………………………Saini: ……………………………. Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni 8 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) KWA MATUMIZI YA OFISI TU Tarehe iliyopokelewa : ……………… Marejesho yamekaguliwa na: Ndg… …………………………………….… Wadhifa: …………………………………… Maoni: ……………………………………… Exchequer Receipt Voucher:…………………….. Tarehe:…………………………………………… No. ………………… Saini:……………………………….. TAARIFA ZA HOTELI FOMU NA. H.L 3 Kwa Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. S.L.P 344, Musoma. (Iwasilishwe kwa nakala tatu) - 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Hii ni fomu inayotaka kujazwa jina la nyumba ya kulala wageni, anuani, na namba ya simu.
1. Jina la nyumba ya kulala wageni:……………………………… Anuani: …………………… Simu Na: ………………………………… - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: The form asks the filer to mark the type of ownership: private, partnership, company, or other.
2. Aina ya Umiliki: Weka alama √ Binafsi Ubia Kampuni Aina nyingineyo (Eleza) - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: This section is a form asking for details about a guest house’s number of rooms, number of beds, and the services provided.
4. Idadi ya Vyumba …………… Idadi ya Vitanda ………………… Huduma zinazotolewa kwenye nyumba ya kulala wageni: Jaza neno Ndiyo au Hapana Kifungua kinywa Chakula Vinywaji 9 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) Huduma nyinginezo (Eleza): ……..………………………………………………… - 5 Verify source ↗
Nyaraka na Vitabu vya hesabu vinatunzwa katika nyumba ya kulala wageni:Weka
AI-assisted research summary: The text refers to documents and accounting books being kept in the lodging house.
5. Nyaraka na Vitabu vya hesabu vinatunzwa katika nyumba ya kulala wageni:Weka alama √ Ndiyo Hapana - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Inaomba taarifa za mmiliki wa nyumba ya kulala wageni, zikiwemo jina, wadhfa, anuani, idadi ya waajiriwa, na saini.
7. Taarifa za Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni: Jina: ………………………………………………………………… Wadhfa: …………………………………………………………….. Anuani: ……………………………………………………………… Idadi ya Waajiriwa: ...…………………………………………………… Saini: …………………………………….. - 8 Verify source ↗
Malipo ya kawaida kwa malazi kwa siku
AI-assisted research summary: The section is a form for listing daily accommodation rates by room type in shillings.
8. Malipo ya kawaida kwa malazi kwa siku. Maelezo………………………Idadi ya vyumba………….....… Maoni………………………………………………………..…. Single Shilingi: ………………………………….……………… Double. Shilingi: . ……………….………………………...…… Suite. Shilingi: ………………….……………………………… Vyumba vinginevyo: …………..……………………………… - 9 Verify source ↗
Tamko
AI-assisted research summary: The declarant must say the information given is true and complete and must report any changes immediately.
9. Tamko: Mimi/Sisi: ………………………………………………………………ninatamka/tunatamka kwamba taarifa nilizotoa/ tulizotoa ni sahihi na zimekamilika na kwamba nitakutaarifu/tutakutaarifu mara moja iwapo kutatokea mabadiliko yeyote. Tarehe:............................Mhuri wa Ofisi na Sahihi:.............................................. Kiwango kinachotumika kwa nyumba ya kulala wageni: ……………………… Tarehe: ………........................…………Sahihi.................................................... KWA MATUMIZI YA OFISI TU 10 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) ____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 14) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi; ………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya; ………………………………………..…….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka; …….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ….. ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe;…....... ya Mwezi;………… Mwaka;………….. Jina;…………………………………..……………………. Saini;…………………………..…………………………… MBELE YANGU: Jina;…………………………….………..…………………… Wadhifa; …………………………………………………..…. Saini ;………………………………………………………… Tarehe; ………………………………………………………. 11 Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni) ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 894 (Linaendelea) Lakari ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Musoma uliofanyika mnamo tarehe 16/03/2022 mbele ya :- MSONGELA N. PALELA Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma MH. CHARLES M. NYAMBITA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Musoma NAKUBALI Dodoma MOHAMED OMARI MCHENGELWA (MB) 20 Novemba, 2023 Waaziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikao Na Serikali za Mitaa 12
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in