Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya Mwaka 2023
This bylaw is named the Musoma District Council Environmental Health and Sanitation By-Law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This bylaw is named the Musoma District Council Environmental Health and Sanitation By-Law, 2023. This by-law applies throughout the entire area of Musoma District Council. Sehemu hii inaweka maana ya maneno na istilahi mbalimbali zinazotumika katika Sheria Ndogo hii. Wakazi au wamiliki wa nyumba, viwanja au biashara lazima waweke eneo lao safi na kutekeleza masharti ya usafi wa mazingira yaliyoorodheshwa. Property owners of houses, factories, or business premises must provide a wastewater pit, empty it when full, and not discharge wastewater onto roads, alleys, rivers, water sources, open areas, storm drains, or other undesignated places.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya Mwaka 2023
Showing 25 of 25
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This bylaw is named the Musoma District Council Environmental Health and Sanitation By-Law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Musoma District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaweka maana ya maneno na istilahi mbalimbali zinazotumika katika Sheria Ndogo hii.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa madawa; “chanzo cha maji” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Musoma; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma au Afisa yeyote ya atakayeteuliwa Mkurugenzi; majukumu kutekeleza 1 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) “kitakasa mikono” maana yake ni sabuni au kemikali ambayo inatumika kuangamiza vidudu na virusi wa aina mbalimbali katika mikono. “kizimba cha taka” maana yake ni kizimba cha taka au chombo maalum kilichowekwa na Halmashauri kwa ajili ya jamii kuhifadhia taka ngumu kabla ya kuzisafirishwa kuu lililoidhinishwa na Halmashauri; kwenye jalala hadi Sura ya 331 “maji taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo lililoko ndani ya Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “mtoa huduma” ni mfanyakazi kwenye sehemu za biashara zinazotoa huduma ya chakula, malazi au vinywaji mbalimbali; “taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; Sura ya 191 “taka ngumu” Maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “wakala “maana yake ni, kampuni, taasisi, kikundi au mtu binafsi aliyeteuliwa na halmashauri kwa ajili ya kutoa huduma ya kuzoa taka; Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira - 4 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayeishi,
AI-assisted research summary: Wakazi au wamiliki wa nyumba, viwanja au biashara lazima waweke eneo lao safi na kutekeleza masharti ya usafi wa mazingira yaliyoorodheshwa.
4. Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayeishi, la nyumba, kiwanja au biashara anayemiliki eneo kuhakikisha kwamba: (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; (b) taka zote zinakusanywa na kuondolewa kwa njia itakayoelekezwa na Halmashauri; (c) anachimba shimo la kutupia taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi tatu (3) na upana usiopungua futi mbili (2); (d) anajenga choo imara cha kudumu kwa matofali 2 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) na kuezeka kwa bati, tembe, majani, vigae chenye mlango unaofunga na kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na kuwe na chombo cha maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi; (f) maji yote yanayotumika kwa kunywa ni safi na salama bila kujali yametoka kwenye chanzo gani cha maji; na (g) kuwa na chombo chenye maji tiririka pamoja na kitakasa mikono mbele ya sehemu ya biashara na kuhakikisha kuwa kila muhitaji huduma ananawa au kujitakasa mikono kabla ya kupata huduma. Uhifadhi wa maji taka - 5 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la
AI-assisted research summary: Property owners of houses, factories, or business premises must provide a wastewater pit, empty it when full, and not discharge wastewater onto roads, alleys, rivers, water sources, open areas, storm drains, or other undesignated places.
5. Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara anatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa anakaro la kuhifadhia maji taka; (b) kunyonya maji taka kila wakati karo linapojaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote ambayo haijatenmgwa kwa ajili ya kuhifadhia maji taka. Utengenezaji na uuzaji wa vyakula - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika,
AI-assisted research summary: Watu wanaotengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula katika eneo la Halmashauri lazima wafuate masharti ya afya na wawe na kibali kutoka kwa Afisa Afya wa Halmashauri.
6. Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa- (a) kutimiza masharti na kanuni za afya; na (b) kuwa na kibali kutoka kwa Afisa Afya wa Halmashauri. Upimaji wa afya - 7 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabiashara au mmiliki au mhudumu
AI-assisted research summary: Certain food and hospitality businesses must get health checks every six months and pay the inspection fee; the council must keep a list of examined service providers.
7.-(1) Kila mfanyabiashara au mmiliki au mhudumu 3 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waoka mikate, au watu wanaoshughulika na kuuza vyakula vilivyopikwa atahakikisha kwamba anapima afya kila baada ya miezi sita na kulipa ada ya upimaji kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (2) Halmashauri itahifadhi orodha ya majina ya watoa huduma wote ambao wamepimwa afya zao ili kurahisisha uhakiki wa afya za watumiaji hata kama mtoa huduma au mfanyakazi amehama kwenda sehemu nyingine ndani ya Halmashauri aweze kutambulika kwa urahisi. - 8 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: The Health Officer is empowered to enter areas within the council during specified daytime hours and to give advice, direct people not to live in dangerous buildings, stop activities during disease outbreaks, seize harmful equipment, and close uninspected or non-compliant businesses or buildings.
8.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika eneo lolote ndani ya Halmashauri wakati wa kuanzia Saa moja na nusu asubuhi hadi Saa tisa na nusu alasiri kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kushauri au kuelekeza watu au mtu kutokuishi katika jengo ambalo linahatarisha afya au maisha ya watu na viumbe hai. (3) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuzuia shughuli mbalimbali wakati wa mlipuko wa magonjwa ikiwa pamoja na kukamata vyombo au vifaa vingine vinavyotumika na ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa wakazi wa Halmashari. (4) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kufunga au kuagiza kufungwa kwa biashara yoyote au jengo ambalo halijakaguliwa au lililokaguliwa na kukutwa limekiuka kanuni na masharti ya afya. - 9 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila mfanyabiashara ana wajibu unaohusiana na kukaguliwa na Afisa jengo kabla ya kuanza biashara.
9. Kila mfanyabiashara atakuwa na wajibu wa linakaguliwa na Afisa jengo kuhakikisha Mwidhiniwa kabla ya kuanzisha biashara la biashara - 10 Verify source ↗
(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji
AI-assisted research summary: Certain residential owners, tenants, and business operators must keep a covered waste container and collect waste in designated places; some households must also have a pit for solid waste, and passenger vehicle owners/drivers must carry and dispose of waste properly.
10.-(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji wa jengo la makazi au mtu yeyote anayefanyia biashara katika eneo lolote ndani ya Halmashauri atatakiwa kuwa na 4 Uwezo wa Afisa Mwidhiniwa Ukaguzi wa jengo la biashara Vifaa vya kuhifadhia taka ngumu Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) chombo cha kuhifadhia takataka chenye mfuniko na atawajibika kukusanya takataka hizo kwenye vizimba vya kuzolea takataka katika maeneo yaliyoainishwa. (2) Kila mmiliki wa jengo au mpangaji wa nyumba iliyoko katika ukanda wa kijani, katika maeneo ambayo la hayajapimwa atalazimika kuwa na shimo kubwa kukusanyia taka ngumu katika eneo lake. (3) Mtu yeyote anaemiliki au dereva wa chombo cha kusafirisha abiria atahakikisha kwamba anaweka chombo cha kuhifadhia taka zitakazozalishwa ndani ya chombo cha usafiri na kuzitupa katika sehemu maalum iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili hiyo. Taratibu za kubomoa jengo - 11 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mtu anayebomoa jengo au sehemu yake lazima apate kibali cha Halmashauri.
11.-(1) Mtu yeyote au kusababisha kubomoka jengo au sehemu ya jengo anatakiwa kuwa na kibali cha Halmashauri. anaetaka kubomoa (2) Mtu yeyote atakayeomba na kupata kibali cha kubomoa jengo au sehemu ya jengo atahakikisha anazuia uchafuzi wa hali ya hewa, anaondoa na kutupa mabaki ya jengo alilobomoa mahali alipoelekezwa kwa mujibu wa kibali. Ada ya uzoaji taka - 12 Verify source ↗
Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu
AI-assisted research summary: Halmashauri must collect solid waste from specified bins in each ward, and waste producers must pay the collection fee or levy at the rate set in the Second Schedule.
12. Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu kutoka katika vizimba vya takataka vilivyoainishwa katika kila kata, na wazalishaji takataka watalipia ada au ushuru wa ukusanyaji wa takataka kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. Ukusanyaji taka ngumu
Part
Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii.
- 13 Verify source ↗
(1) Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya
AI-assisted research summary: Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye chombo cha taka ngumu, na mtu yeyote lazima awe na kibali cha Halmashauri ili kuchoma au kufukia taka ngumu.
13.-(1) Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye pipa au chombo chochote cha taka ngumu au kitu chochote kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara. (2) Taka ngumu zote zitakazokusanywa kwenye pipa au chombo cha taka zitabaki kuwa mali ya mkazi au mmliki wa eneo lile mpaka zitakapokuwa zimefikishwa kwenye kizimba cha taka au zitakapokuwa zimetolewa na wakala 5 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) Eneo la kutupa taka Usafi katika kaya kutoka katika eneo lake. (3) Mtu yeyote atatakiwa kuwa na kibali cha Halmashauri ili kuchoma au kufukia taka ngumu. - 14 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupia taka, iweke vyombo maalum vya kuhifadhia taka, na itoe huduma ya kuchukua taka kwa malipo. Serikali ya Kijiji pia lazima itenge eneo la dampo kwa ajili ya taka ngumu.
14.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa: (a) kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupia taka; (b) kuweka vyombo maalum vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji takataka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa takataka hadi kwenye dampo. (2) Serikali ya Kijiji itawajibika kutenga eneo la dampo kwa ajili ya utupaji wa taka ngumu. - 15 Verify source ↗
(1) kila mkazi mwenye nyumba, mpangaji,
AI-assisted research summary: Wakazi wa nyumba, wapangaji, wamiliki, na wamiliki wa biashara lazima wahifadhi usafi na kuweka vifaa vya usafi vilivyotajwa.
15.-(1) kila mkazi mwenye nyumba, mpangaji, mmiliki atalazimika kuwa na choo na kupalilia majani na kufagia kila mara na kutunza mazingira safi kwa umbali wa futi kumi kutoka ukuta wa jengo kama ilivyo katika vipimo vilivyowekwa na kukubalika na Halmashauri. (2) kila mkazi mwenye nyumba au mmiliki atapaswa kuweka jengo lake madirisha makubwa yasiyopungua 1/8 ya eneo la sakafu ya chumba au vipimo vilivyowekwa na kukubaliwa na Halmashauri. (3) Kila mkazi mwenye nyumba au mmiliki atalazimika kuwa na shimo la taka au pipa la taka pembeni mwa nyumba yake na kuhakikisha taka hizo zinaondolewa au kuteketezwa mara pipa linapojaa; na (4) kila mmiliki wa biashara ni lazima kuwa na ndoo ya kunawia maji tiririka ikiwa pamoja na sabuni au kuwa na kitakasa mikono kwa ajili ya wateja wake. Udhibiti wa taka maji - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote, kaya, taasisi, kampuni, kiwanda,
AI-assisted research summary: Watu na places listed must keep their premises clean and provide acceptable toilets, empty septic/latrine facilities at their own expense when full, and have a rack for drying washed utensils.
16. Mtu yeyote, kaya, taasisi, kampuni, kiwanda, ofisi , hoteli na mgahawa majengo yoyote wanapokusanyika watu kama vile soko, minada, magulio, makanisa, misikiti, sharti itunze maeneo yake ikiwa ni pamoja na kufanya yafuatayo: 6 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) Wajibu wa mmiliki wa duka la kuuza nyama Siku yau (a) kuwa na choo chenye hadhi inayokubalika kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi na kitahesabika kujaa kukisalia futi tatu (3) kufikia usawa wa sakafu ya karo; (b) kunyonya choo kikijaa kwa gharama zake mwenyewe; na (c) kuwa na kichanja kwa ajili ya kuanika vyombo baada ya kuoshwa. - 17 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa duka la
AI-assisted research summary: Kila mmiliki wa duka la kuuzia nyama lazima ahakikishe duka lina masharti fulani ya usafi na vifaa, na wahudumu wazingatie mavazi na uchunguzi wa afya.
17. Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa duka la kuuzia nyama kuhakikisha kwamba: (a) ana jengo la kudumu lililosakafiwa na kuwekwa marumaru nyeupe kwenye sakafu na kuta kwa urefu wa futi 6 kutoka usawa wa sakafu; (b) jengo lina maji safi, gogo na misumeno ya kukatia nyama; (c) kuna pipa la kuhifadhia takataka; (d) muhudumu ana koti jeupe pamoja na viatu vyeupe aina ya buti; (e) muhudumu anapima afya kila baada ya miezi sita. - 18 Verify source ↗
(1) Kila jumamosi ya wiki ya pili na jumamosi
AI-assisted research summary: Kila jumamosi ya wiki ya pili na ya mwisho wa mwezi ni siku maalumu ya usafi; wakazi wa Kijiji na Kitongoji lazima washiriki, na kila mtu ahakikishe maeneo yake na ya jirani yako safi.
18.-(1) Kila jumamosi ya wiki ya pili na jumamosi ya wiki ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku maalamu ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yote ya Halmashauri. (2) Itakuwa ni wajibu na lazima kwa kila mkazi katika Kijiji na Kitongoji kushiriki usafi wa mazingira kwa siku iliyopangwa na Halmashauri katika maeneo yao na maeneo ya umma. (3) Kila mtu atahakikisha eneo lake la makazi na linalomzunguka, eneo analofanyia biashara, eneo la wazi lililokaribu naye kwa umbali wa mita kumi na eneo la mazingira ya ofisi ni safi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Vikundi vya usafi - 19 Verify source ↗
Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi
AI-assisted research summary: Halmashauri must encourage and recognize community groups so they can carry out solid waste control and environmental sanitation in villages and hamlets, after signing a contract with the council.
19. Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi 7 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika Vijiji na Vitongoji baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Marufuku - 20 Verify source ↗
Ni marufuku
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinakataza shughuli na vitendo kadhaa vinavyohusiana na usafi, mazingira, mifugo, matengenezo ya magari, na uuzaji wa nyama katika maeneo yasiyoruhusiwa.
20. Ni marufuku: (a) mtu yeyote kuendesha biashara ya upulizaji dawa au biashara ya kuua wadudu au wanyama waharibifu katika nyumba yoyote au mahali popote bila cheti cha taaluma kinachotambuliwa na Serikali na leseni kutoka Halmashauri; (b) mfanyabiashara yeyote kupanga bidhaa nje ya jengo lake la biashara, barabarani, vichochoroni au katika eneo lolote ambalo halikuidhinishwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (c) mfugaji kuruhusu mfugo au mifugo kuzurura ovyo mitaani au barabarani; (d) mtu yeyote kutupa takataka za aina yoyote barabarani au eneo lolote la wazi, kwenye vichochoro au kwenye chanzo chochote cha maji au katika eneo lolote ambalo halijatengwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (e) mtu yeyote aliye ndani ya gari kudondosha taka ngumu nje ya gari likiwa ndani au nje ya kituo cha magari na sehemu yoyote ile ambapo gari hilo linapita; (f) mtu yeyote kuanzisha shughuli za kiwanda au mradi wowote unaoweza kuathiri mazingira bila kufanya utafiti wa mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira; (g) mtu yeyote kuzuia maji kupitia njia yake ya asili kwa kujenga au kulima au kuweka kitu chochote kwenye njia ya maji kitakachoingilia mtiririko wa asili wa maji katika chanzo cha maji; (h) mtu yeyote kuweka kitu chochote kwenye maji taka ambacho kinaweza kuathiri mtu yeyote au 8 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) kuharibu mfumo wa tiba ya maji taka au kusababisha kuzuia mtiririko wa maji taka; (i) mtu yeyote kulima kilimo cha matuta yanayosababisha maji kutuama ndani ya eneo la katikati ya mji; (j) mtu yeyote kufanya matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo kwenye maeneo ya Halmashauri bila kibali; (k) mtu yeyote kuegesha gari bovu kwenye njia ya miguu, mtaa, uchochoro, mtaro, maeneo ya wazi, barabarani na kusababidha adha kwa wakazi au watumiaji wa njia hiyo; na (l) mtu yeyote kuchinja au kuuza nyama ya aina yoyote katika maeneo yasiyokuwa machinjio au maduka ya kuuza nyama au katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri. Makosa - 21 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa
AI-assisted research summary: Anyone commits an offence under this bylaw by doing any of the listed sanitation, food-handling, waste, water-source, or public-space acts.
21. Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa mtu yeyote: (a) kujenga choo umbali usiozidi mita 60 kutoka kisimani, bwawani, mtoni, au chanzo cha maji yanayotumika, kwa matumizi ya binadamu; (b) kutoa kinyesi au kusababisha kinyesi, mkojo, taka maji, yenye kinyesi kutoka kwenye choo chake au bafu lake au karo la kuoshea vyombo au nguo au kutoka kwenye bomba lolote linalochukua taka maji na kuyatitirisha kwenye barabara, mitaa, au kwenye mifereji ya maji ya mvua, au mfereji wowote uliowazi; (c) kutupa taka au kusababisha mtu mwingine atupe na pasiporuhusiwa popote taka mahali Halmashauri; (d) kutiririsha maji taka barabarani, ziwani, mashambani, mitaani au katika eneo la nyumba ya jirani, mitaro ya barabara au eneo la wazi; (e) kuendesha mashine ya kusaga na kukoboa katika 9 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) jengo ambalo halijatekeleza masharti ya afya; (f) kuuza nyama iliyotundikwa chini ya mti, kuuza nyama ya mnyama aliyechinjwa bila kibali cha Afisa Mwidhiniwa au kwenye bucha ambalo sio safi na halijatekeleza masharti kama yalivyo katika Sheria Ndogo hizi; (g) kuuza chakula katika eneo ambalo halijatengwa au kusajiliwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (h) kuzika maiti katika eneo ambalo halikuainishwa kwa shughuli hiyo bila taarifa maalum kwa Afisa Mwidhiniwa; (i) kutolipa ushuru taka; (j) kufanya biashara ya kuuza vyakula vya aina yoyote barabarani , mitaani na nje ya majengo bila kuweka ndani ya chombo safi chenye mfuniko; (k) kuchezesha michezo au kuonesha michezo au burudani katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri; (l) kuegesha gari bovu na kuliacha kando ya barabara au kichochoroni au eneo la wazi ambalo halijaidhinishwa kwa shughuli za gereji na kuliacha zaidi ya siku moja; (m) kulima kandokando au ndani ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji; (n) kutokuwa na pipa au chombo cha takataka chenye mfuniko katika eneo la biashara; (o) kutokuwa na choo au kukutwa na choo kibovu au kilichojaa; (p) kukutwa na shimo la taka maji lililojaa au ambalo halina mfuniko; (q) kusafirisha nyama bila kutumia gari ya kusafirishia nyama ambayo imekaguliwa na kupewa kibali cha kusafirisha nyama kwa ajili ya matumizi ya binadamu; (r) kutoshiriki katika zoezi la usafi kiwilaya kila 10 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) siku ya alhamisi ya kila mwisho wa mwezi kulingana na mwongozo wa kitaifa wa zoezi hilo; (s) kuziba kichochoro; na (t) kutokuwa na chombo maalumu cha kukusanyia takataka ndani ya gari la abiria. Adhabu Kufifilisha kosa - 22 Verify source ↗
Mtu yeyote atakaekuwa ametenda kosa na
AI-assisted research summary: A person who commits an offence and is found guilty may be fined between 50,000 and 300,000 shillings, imprisoned for up to 12 months, or both.
22. Mtu yeyote atakaekuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi elfu hamsini na isiyozidi Shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. - 23 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji Shilingi 50,000 ikiwa anakiri kosa na yuko tayari kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Tatu.
23. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii. __________________ JEDWALI LA KWANZA _________________ ADA YA UPIMAJI WA AFYA (Limetengenezwa chini ya aya ya 7) Namba
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: The provision lists business fee amounts and waste collection charges for certain business types.
9. Aina ya Biashara Nyumba ya starehe (baa, vilabu vya pombe za kienyeji na nyumba ya kulala wageni Duka la bidhaa Nyumba ya kutengeneza na kuuzia vyakula na au nyama choma. Duka la nyama Viwanda vya kati Viwanda vidogo vya vyakula Mhudumu wa chakula Kiwango cha Ada kwa Shilingi 5,000/= kwa kila mfanyakazi/Mhudumu 3,000/= kwa kila mfanyakazi/Mhudumu 5,000/= kila mfanyakazi/Mhudumu 5,000/= kwa kila mfanyakazi/Mhudumu 3,000/=Kwa kila mfanyakazi/Mhudumu 5,000/= kwa kila mfanyakazi/Mhudumu 5,000/= kila mfanyakazi/Mhudumu 11 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) ____________ JEDWALI LA PILI ____________ USHURU WA UZOAJI TAKA (Limetengenezwa chini ya aya ya 12) Namba Maeneo ya Uzalishaji Taka Kiwango cha Ushuru kwa Shilingi Senta za Vijiji vya Busekela, Bukima, Kome, Rusoli, Murangi, Masinono, Saragana, Suguti, Kusenyi, Kwikuba, Mugango, Bwai Kumusoma, Busekela, Rukuba na Etaro Duka la rejareja Duka la jumla Biashara ya huduma 500/= 1,000/= 2,000/=
Part
JEDWALI LA PILI
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: This section is a confession form where a person admits violating a bylaw and says they are willing to pay any owed fees or taxes and a fine.
3. ____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 23) KUFIFILISHA KOSA Mimi; ………………………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya; ………………………………………..……. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya MUSOMA, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka; …….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ………….. ya Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe;…....... ya mwezi;………… mwaka;………….. Jina:…………………………………..……………………. 12 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) Saini:…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jina: …………………………….………..……………….. Wadhifa: ………………………………………………….. Saini: ……………………………………………………… Tarehe: ……………………………………………………. 13 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Tangazo La Serikali Na. 895 (Linaendelea) Lakari ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutilia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Musoma uliofanyika mnamo tarehe 16/03/2022 mbele ya :- MSONGELA N. PALELA Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Musoma MH. CHARLES M. NYAMBITA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Musoma NAKUBALI Dodoma MOHAMED OMARI MCHENGELWA (MB) 20 Juni, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikao Na Serikali za Mitaa 14
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in