Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
This section states the short title of the by-law: the Kyerwa District Council Environmental Sanitation By-Law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the short title of the by-law: the Kyerwa District Council Environmental Sanitation By-Law, 2023. This bylaw applies throughout the Kyerwa District Council area. This section defines key terms used in the by-law and introduces a heading on environmental cleanliness duties. Residents who own a house, plot, or business area must keep the area clean, manage waste, build a proper toilet and refuse pit, and prevent mosquito, rat, and other harmful breeding sites. Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara lazima wawe na namna ya kuhifadhi maji taka, wayatoe pindi yanapojaa, na wasiyamwage barabarani au sehemu nyingine zisizoruhusiwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
Showing 21 of 21
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section states the short title of the by-law: the Kyerwa District Council Environmental Sanitation By-Law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the Kyerwa District Council area.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. Tafsiri Sura ya 331 - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law and introduces a heading on environmental cleanliness duties.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa dawa; “chanzo cha maji” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa au Afisa yeyote atakayeteuliwa ya Mkurugenzi; kutekeleza majukumu “kizimba cha taka” maana yake ni kizimba cha taka au 1 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 897 (Linaendelea) chombo maalumu kilichowekwa na Halmashauri kwa ajili ya jamii kuhifadhia taka ngumu kabla ya kusafirishwa kuu lililoidhinishwa; kwenda kwenye jalala “mkazi” maana yake ni mtu yeyote ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo lililoko chini ya mamlaka ya Halmashauri na ambaye ama ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “maji taka” maana yake ni kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka” maana yake ni kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; Sura ya 191 “taka ngumu” maana yake ni kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira. Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira - 4 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayemiliki eneo
AI-assisted research summary: Residents who own a house, plot, or business area must keep the area clean, manage waste, build a proper toilet and refuse pit, and prevent mosquito, rat, and other harmful breeding sites.
4. Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara kuhakikisha kwamba- (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; (b) taka zote zinakusanywa na kufukiwa au itakayoelekezwa na kuondolewa kwa njia Halmashauri; (c) anachimba shimo la kutupia taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi 3 na upana usiopungua futi 2; (d) anajenga choo imara cha kudumu kwa matofali na kuezekwa kwa bati, tembe, majani au vigae chenye mlango unaofunga na kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na kuwe na chombo cha maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; na (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi. 2 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 897 (Linaendelea) (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya aya ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Uhifadhi wa maji taka - 5 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara lazima wawe na namna ya kuhifadhi maji taka, wayatoe pindi yanapojaa, na wasiyamwage barabarani au sehemu nyingine zisizoruhusiwa.
5.-(1) Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara anatakiwa:- (a) kuhakikisha kuwa analo karo la kuhifadhi maji taka; (b) kunyonya maji taka pale karo linapojaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote isiyotengwa kuhifadhia maji taka. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya aya ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Utengenezaj i na uuzaji wa vyakula - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika,
AI-assisted research summary: Anyone who makes, burns, cooks, boils, or sells food in the Council area must follow health rules and have a permit from the Council Health Officer.
6. Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa- (a) kuzingatia masharti na kanuni za afya; na (b) kuwa na kibali kutoka kwa Afisa Afya wa Halmashauri. Upimaji wa afya Uwezo wa Afisa Mwidhiniwa - 7 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli,
AI-assisted research summary: Wafanyakazi na wahusika wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waoka mikate, na wauzaji wa vyakula vilivyopikwa lazima wapime afya zao kila baada ya miezi sita.
7. Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waoka mikate au watu wanaoshughulika na kuuza vyakula vilivyopikwa kuhakikisha kwamba wanapima afya zao kila baada ya miezi sita. - 8 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo kuingia
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia maeneo ya Halmashauri wakati wa kazi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo, na anaweza pia kushauri au kuelekeza watu wasikae katika jengo hatari kwa afya au maisha.
8.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo kuingia katika eneo lolote ndani ya Halmashauri wakati wa muda wa kazi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kushauri au kuelekeza watu au mtu kutokuishi katika jengo ambalo linahatarisha afya au maisha ya watu na viumbe hai. 3 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 897 (Linaendelea) Vifaa vya kuhifadhi taka ngumu Ada ya uzoaji taka Ukusanyaji wa taka ngumu - 9 Verify source ↗
(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji
AI-assisted research summary: Wamiliki, wapangaji na wafanyabiashara fulani lazima wawe na chombo cha taka chenye mfuniko na wakusanye taka katika maeneo yaliyotengwa; pia, katika ukanda wa kijani na maeneo ambayo hayajapimwa, mmiliki au mpangaji lazima awe na shimo kubwa la taka ngumu.
9.-(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji wa jengo la makazi au mtu yeyote anayefanyia biashara katika eneo lolote ndani ya Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhia taka chenye mfuniko na atawajibika kukusanya taka hizo kwenye vizimba vya kuzolea taka katika maeneo yaliyoainishwa. (2) Kila mmiliki wa jengo au mpangaji wa nyumba iliyoko katika ukanda wa kijani, katika maeneo ambayo hayajapimwa atalazimika kuwa na shimo kubwa la kukusanyia taka ngumu katika eneo lake. - 10 Verify source ↗
Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu
AI-assisted research summary: Halmashauri must collect solid waste from designated waste bins in each ward, and waste generators must pay the waste collection fee or levy at the rate set in the First Schedule.
10. Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu kutoka katika vizimba vya taka vilivyoainishwa katika kila kata, na wazalishaji taka watalipia ada au ushuru wa ukusanyaji wa taka kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii.
Part
Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii.
- 11 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kuweka uchafu wenye asili ya
AI-assisted research summary: Ni marufuku kuweka uchafu au maji maji kwenye pipa linaloweza kulipuka; taka ngumu pia haziruhusiwi kuchomwa au kufukiwa bila kibali cha Halmashauri.
11.-(1) Ni marufuku kuweka uchafu wenye asili ya taka au kitu chochote maji maji kwenye pipa kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara. la (2) Taka ngumu zote zitakazokusanywa kwenye mapipa ya taka zitabaki kuwa mali ya mkazi au mmliki wa eneo lile mpaka zitakapokuwa zimefikishwa kwenye kizimba cha taka au zitakapokuwa zimetolewa na wakala kutoka katika eneo lake. (3) Hairuhusiwi mtu yeyote kuchoma au kufukia taka ngumu bila kibali cha Halmashauri. Eneo la kutupa taka - 12 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupia taka, iweke vyombo maalumu vya kuhifadhia taka, na itoe huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka kwenda dampo.
12. Halmashauri itakuwa na wajibu wa: (a) kutenga eneo maalumu kwa ajili ya kutupia taka; (b) kuweka vyombo maalumu vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. Siku ya usafi - 13 Verify source ↗
(1) Kila Alhamisi ya wiki na Jumamosi ya
AI-assisted research summary: Wakazi wa kijiji na kitongoji lazima washiriki usafi wa mazingira siku itakayopangwa na Halmashauri, na kila mtu ahakikishe maeneo yake na maeneo yaliyo karibu yake yanakuwa safi.
13.-(1) Kila Alhamisi ya wiki na Jumamosi ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku maalumu ya kufanya 4 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 897 (Linaendelea) usafi wa mazingira katika maeneo ya makazi na umma. (2) Itakuwa ni wajibu na lazima kwa kila mkazi katika kijiji na kitongoji kushiriki usafi wa mazingira kwa siku iliyopangwa na Halmashauri katika maeneo yao na maeneo ya umma. (3) Kila mtu atahakikisha eneo la makazi yake na vichochoro vilivyomzunguka, eneo analofanyia biashara, eneo la wazi lililo karibu naye kwa umbali wa mita kumi na eneo la mazingira ya Ofisi ni safi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Vikundi vya usafi - 14 Verify source ↗
Halmashauri itahamasisha uundaji wa Vikundi
AI-assisted research summary: Halmashauri inapaswa kuhamasisha uundaji na utambuzi wa Vikundi Jamii ili viweze kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu na usafi wa mazingira katika mitaa, baada ya kuingia mkataba na Halmashauri.
14. Halmashauri itahamasisha uundaji wa Vikundi Jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika mitaa baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Marufuku - 15 Verify source ↗
Ni marufuku
AI-assisted research summary: Section 15 prohibits several sanitation and environmental acts, including operating pest-control business without recognized professional certification and a license, dumping waste, letting livestock roam, and blocking or polluting water and wastewater flows.
15. Ni marufuku: (a) mtu yeyote kuendesha biashara ya upulizaji dawa au biashara ya kuua wadudu au wanyama waharibifu katika nyumba yoyote au mahali popote bila cheti cha taaluma kinachotambuliwa na Serikali na leseni kutoka Halmashauri; (b) mfanyabiashara yeyote kupanga bidhaa nje ya jengo lake la biashara, barabarani, vichochoroni au katika eneo lolote ambalo halikuidhinishwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (c) mfugaji kuruhusu mifugo kuzurura hovyo mitaani au barabarani; (d) mtu yeyote kutupa taka za aina yoyote barabarani au eneo lolote la wazi, kwenye vichochoro au kwenye chanzo chochote cha maji au katika eneo lolote ambalo halikutengwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (e) mtu yeyote aliye ndani ya gari kudondosha taka ngumu nje ya gari likiwa ndani au nje ya kituo cha magari na sehemu yoyote ile ambapo gari hilo linapita; 5 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 897 (Linaendelea) (f) mtu yeyote kuanzisha shughuli za kiwanda au mradi wowote unaoweza kuathiri mazingira bila kufanya tathmini ya athari kwa mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; (g) mtu yeyote kuzuia maji kupita njia yake ya asili kwa kujenga au kulima au kuweka kitu chochote kwenye maji kitakachoingilia mtiririko wa asili wa maji katika chanzo cha maji; (h) mtu yeyote kuweka kitu chochote kwenye maji taka ambacho kinaweza kuathiri mtu yeyote au kuharibu mfumo wa tiba ya maji taka au kinachoweza kusababisha kuzuia mtiririko wa maji taka; na (i) mtu yeyote kulima kilimo cha matuta yanayosababisha maji kutuama ndani ya eneo la katikati ya mji. Makosa - 16 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinakataza mtu yeyote kufanya vitendo kadhaa vya usafi wa mazingira na matumizi ya maeneo bila kibali.
16. Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa mtu yeyote- (a) kujenga choo chini ya umbali wa mita sitini kutoka kisimani, bwawani, mtoni au chanzo kingine cha maji yanayotumika kwa matumizi ya binadamu; (b) kutoa kinyesi au kusababisha kinyesi, mkojo, maji machafu au yenye kinyesi kutoka kwenye choo chake, bafu lake au karo la kuoshea vyombo au nguo au kutoka kwenye bomba lolote linalochukua maji machafu na kuyatitirisha kwenye barabara, mitaa, kwenye mifereji ya maji ya mvua au mfereji wowote ulio wazi; (c) kutupa taka au kusababisha mtu mwingine atupe na pasiporuhusiwa popote taka mahali Halmashauri; (d) kuuza chakula katika eneo ambalo halijasajiliwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (e) kuzika maiti katika eneo ambalo halikuainishwa kwa shughuli hiyo; 6 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 897 (Linaendelea) (f) kutolipa ada ya taka kwa miezi miwili mfululizo; (g) kutembeza chakula mitaani bila kibali cha Halmashauri; (h) kuchezesha michezo au kuonyesha michezo au burudani katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri; (i) kuegesha gari bovu na kuliacha kando ya barabara au kichochoro au eneo la wazi ambalo halijaidhinishwa kwa shughuli za gereji na kuliacha zaidi ya siku moja; (j) kulima ndani ya vyanzo vya maji; (k) kutokuwa na pipa la taka lenye mfuniko katika eneo la biashara; (l) kutokuwa na choo au kukutwa na choo kibovu au kilichojaa; (m) kukutwa na shimo la maji taka lililojaa au ambalo halina mfuniko; (n) kuziba kichochoro; na (o) kutokuwa na chombo maalumu cha kukusanyia taka ndani ya gari la abiria. Adhabu - 17 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria
AI-assisted research summary: Anyone who violates these by-laws commits an offence and may be fined, jailed for up to 12 months, or both.
17. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na endapo akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi elfu hamsini na isiyozidi Shilingi laki tatu au kutumikia kifungo kisichozidi miezi kumi na miwili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja faini na kifungo. Kufifilisha kosa - 18 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii Shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalumu.
18. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. 7 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 897 (Linaendelea) _____________ JEDWALI LA KWANZA ______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 10) ADA YA KUZOA TAKA NA AINA YA BIASHARA/MAENEO YA UZALISHAJI TAKA MIJI YA KIBIASHARA (NKWENDA, MABIRA, ISINGIRO, MURONGO, RUBWERA- RWENKORO NGOADA KWA MWEZI (SHILINGI) 1,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 5,000 MAKAO MAKUU YA KATA TOFAUTI NA MIJI YA KIBIASHAR A ADA KWA MWEZI (SHILINGI) 800 8,000 1,000 5,000 5,000 5000 5,000 1,000 3,000 3,000 3,000 4,000 5,000 5,000 MAKAO MAKUU YA VIJIJI TOFAUTI NA MAKAO MAKUU YA KATA, ADA KWA MWEZI (SHILINGI) 500 5,000 5,00 3000 3000 3000 2,000 500 1,500 1,500 1,500 2,000 2,000 2,000 Ofisi (Ya Umma na Binafsi) 2,000 1 2 3 4 Makazi ya Familia Nyumba ya kulala wageni Taasisi za Kifedha Benki za kibiashara Duka la kubadilishia pesa 5 VYAKULA NA VINYWAJI Hotel Mgahawa Café (vitafunwa na vinywaji baridi) 8,000 Duka la vyakula na vinywaji Grocery Bar (Pombe, vinywaji baridi na vikali) Bar na Mgahawa Bar na Nyumba ya Kulala Wageni 8,000 8,000 10,000 10,000 10,000 8 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 897 (Linaendelea) Bar Nyumba ya Kulala wageni na Ukumbi wa Starehe Bar na ukumbi wa Starehe 10,000 5,000 Bar na klabu ya usiku
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: This section lists fee amounts for different business types and services.
6. 7 Bucha ya Nyama na Samaki wabichi DUKA JUMLA NA REJA REJA 10,000 10,000/= Vyakula na bidhaa Mchanganyiko Nguo Vifaa vya umeme Vifaa vya ujenzi Vitabu, shajara na zawadi Sonara na vipodozi Vinywaji na pombe Kali Vipuri Vifaa chakavu KARAKANA NA VIWANDA Fundi selemala na mashine ya mbao Karakana ya chuma (fitting and turning, welding etc) Karakana ya Magari Sonara na uhunzi wa vito Shughuli za vioo Mchapishaji Viwanda vikubwa kwa tani moja ya taka Viwanda vidogo kwa tani moja ya taka BIASHARA NDOGO NDOGO Fundi cherehani Fundi viatu Saluni ya nywele (kike na kiume) Dobi na dry cleaner Genge/Meza ya biashara Watengeneza juice/barafu na bisi Wachoma chipsi na nyama choma Waosha magari, pikipiki na bajaji Mashine ya kusaga na/au kukoboa nafaka Waziba pancha mitaani Wauza mitumba ndani ya soko Wauza mitumba nje ya soko Mama lishe HUDUMA ZA AFYA Duka la dawa baridi za binadamu Maabara binafsi ya vipimo 8000 8000 5,000 8,000 8000 8,000 8,000 8,000 8,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 20,000 10,000 10,000 500 2,000 2,000 1,000 5,000 2,000 5,000 1,000 500 3000 2000 10,000 10,000 9 - 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: The provision lists fee amounts for several categories of premises and activities.
10. 5,000 3,000 5,000 5,000/= 3,000 3,000 2,000 3,000 3,000 3,000 3,000 3,000 3,000 5,000 5,000 5,000 5,000 5,000 5,000 10,000 5,000 5,000 - 1,000 1,000 500 3,000 1,000 3,000 500 - 2,000 1,000 5,000 5,000 1,500 2,000 1,000 3,000 1,000 1,000 500 1,000 1,000 1,000 1,000 1,000 1,000 2,000 2,000 2,000 2,000 2,000 2,000 5,000 3,000 2,000 - 500 500 - 2,000 500 2,000 - - 1,000 500 3,000 3,000 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 897 (Linaendelea) Zahanati binafsi Hospitali binafsi Kituo cha Afya binafsi Madawa asilia TAASISI ZA MAFUNZO Shule Binafsi Chuo binafsi VITUO VYA MAFUTA Kituo kikubwa Kituo kidogo Kituo cha mafuta ya taa Kituo cha kuuzia gesi Kibanda cha kuuzia mkaa Duka la simu, kampuni ya simu na mnara wa simu Taka za uvunjaji nyumba kwa tani 10,000 20,000 15,000 10,000 20,000 30,000 50,000 30,000 10,000 10,000 10,000 10,000 20,000 11 - 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: Hii ni fomu ya kukiri kosa na kuonyesha nia ya kulipa ada/ushuru unaodaiwa pamoja na faini mbele ya Mkurugenzi Mtendaji.
12. 13 14 5,000 10,000 8,000 5,000 10,000 15,000 30,000 15,000 5,000 5,000 5,000 5,000 3,000 5,000 5,000 3,000 5,000 8,000 15,000 8,000 3,000 3,000 3,000 3,000 10,000 5,000 ___________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 18) HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi; ………………………………………nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya; ………………………………………..……. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka; …….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ….. ya Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe:…....... ya Mwezi:………… Mwaka:………….. Jina:…………………………………..……………………. Saini:…………………………..…………………………… MBELE YANGU: Jina:…………………………….………..…………………… 10 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 897 (Linaendelea) Wadhifa: …………………………………………………..… Saini: ………………………………………………………… Tarehe: ………………………………………………………. Lakiri ya Halmashauri ya Kyerwa imegongwa kwenye sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Kyerwa uliofanyika Tarehe …. Mwezi… Mwaka…. na Kushuhudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- SACF. JAMES MARCO JOHN Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa MH. BAHATI HENERICO Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 20 Novemba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in