Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mwaka 2023
This provision says the by-law is called the Kyerwa District Council Environmental Protection By-law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision says the by-law is called the Kyerwa District Council Environmental Protection By-law, 2023. This bylaw applies throughout all areas of Kyerwa District Council. Sehemu hii inaweka maana za istilahi mbalimbali zinazotumika katika Sheria Ndogo hii, ikiwemo Afisa Mwidhiniwa, Halmashauri, mfugaji, misitu, na maeneo ya hifadhi. The Council must set aside grazing areas, designate a special livestock route, conduct a livestock census, issue livestock cards, and provide improved livestock-keeping education to the community. Kila mfugaji katika Halmashauri ya Kyerwa anatakiwa kufuata masharti ya ufugaji, ikiwemo kutumia maeneo na njia zilizopangwa, kuwasilisha mifugo kwa huduma za majosho na chanjo, na kusajili mifugo.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mwaka 2023
Showing 32 of 32
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision says the by-law is called the Kyerwa District Council Environmental Protection By-law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika maeneo yote
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout all areas of Kyerwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika maeneo yote ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaweka maana za istilahi mbalimbali zinazotumika katika Sheria Ndogo hii, ikiwemo Afisa Mwidhiniwa, Halmashauri, mfugaji, misitu, na maeneo ya hifadhi.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “eneo la hifadhi” maana yake ni maeneo ya milima, maeneo ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu, ambayo miteremko yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; na maeneo mengine lengo “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa; “hifadhi ya mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi; mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji vinavyozingatia masharti na 1 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwidhiniwa chini ya Sheria ya Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote. “kiwanda” maana yake ni jengo au majengo au eneo ambapo vitu vinatengenezwa; “kuvuna misitu” maana yake ni pamoja na kufyeka, kukata au kung’oa misitu, visiki; “maeneo ya malisho” maana yake ni maeneo yaliyotemgwa kwa ajili ya malisho ya mifugo, pamoja na sehemu zote ambazo zimetengwa na Halmashauri kwa ajili ya malisho; Sura ya 191 “maji” kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Sura ya 191 “maji Mazingira; taka” kama Usimamizi wa Mazingira; ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Sura ya 323 “mazao ya misitu” maana yake kama ilivyotafsiriwa katika Sura ya 191 “mazingira” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Misitu; Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anaejishughulisha na ufugaji mifugo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “misitu” maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia 10 ya miti, uoto wa asili au iliyopandwa, au asilimia 50 au zaidi ya vichaka na miti inayoota upya ambayo itajumuisha aina yote ya misitu ya hifadhi ambayo itatangazwa chini ya Sheria ya Misitu na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri; Sura ya 191 “taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Sura ya 191 “taka ngumu” kama ilivyo katika Sheria ya Usimamizi wa Usimamizi wa Mazingira; 2 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) Mazingira; Sura ya 191 “taka za viwandani” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa Sura ya 191 “uchafu hatari” Kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; Sura ya 191 “uchafu wa mazingira” kama ilivyo katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; Sura ya 191 “udongo” kama ilivyo katika Sheria ya Usimamizi wa usimamizi wa Mazingira; Mazingira; Sura ya 191 “vitu hatari” Maana yake kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa. Wajibu wa Halmashaur i Wajibu wa mfugaji - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga
AI-assisted research summary: The Council must set aside grazing areas, designate a special livestock route, conduct a livestock census, issue livestock cards, and provide improved livestock-keeping education to the community.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za malisho ndani ya eneo la Halmashauri. (2) Halmashauri itatenga njia maalum ya kupitisha mifugo kwenda na kurudi malishoni au minadani. (3) Halmashauri itafanya sensa ya mifugo na kutoa kadi za mifugo na elimu ya ufugaji bora kwa jamii. - 5 Verify source ↗
Kila mfugaji katika Halmashauri ya Kyerwa
AI-assisted research summary: Kila mfugaji katika Halmashauri ya Kyerwa anatakiwa kufuata masharti ya ufugaji, ikiwemo kutumia maeneo na njia zilizopangwa, kuwasilisha mifugo kwa huduma za majosho na chanjo, na kusajili mifugo.
5. Kila mfugaji katika Halmashauri ya Kyerwa- (a) atatakiwa kufuga na kulisha mifugo katika na yaliyopangwa ya malisho maeneo Halmashauri; (b) atatakiwa kupitisha mifugo yake katika njia zilizopangwa na kutengwa na Halmashauri; (c) atatakiwa itakayoonesha aliyonayo; kuwa na ya mifugo idadi na aina ya mifugo kadi (d) atatakiwa kupeleka mifugo katika majosho kama atakavyoagizwa na Halmashauri; (e) atatakiwa kupeleka mifugo yake katika vituo vya na Halmashauri, na atalipia chanjo hiyo kama itakavyoamriwa chanjo kama 3 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) atatakiwa kufanya hivyo; (f) atatakiwa kuchangia gharama za ukarabati wa majosho kama sehemu ya mchango wake, pale itakapobidi kufanya hivyo, na kwa gharama itakayopendekezwa na Halmashauri; (g) atatakiwa kuchangia gharama za uboreshaji wa na ya malisho yaliyotengwa maeneo Halmashauri; (h) atatakiwa kuweka alama kwenye mifugo yake (branding, ear tags) na katika viungo vya mifugo vinavyopendekezwa ili kutoharibu zao la ngozi; (i) atatakiwa kuhudhuria mafunzo ya ufugaji kama atakavyohitajiwa na Halmashauri; (j) atatakiwa kutokata miti kwa lengo la kufukuza mbung’o; na (k) atatakiwa kusajili mifugo katika rejista ya kijiji na kuogesha mifugo katika majosho kama ratiba itakavyopangwa. - 6 Verify source ↗
Itakuwa marufuku kwa mfugaji yeyote
AI-assisted research summary: Mfugaji yeyote haruhusiwi kuchunga, kulisha, kunywesha, kusafirisha, kuhamisha, kuingiza, kuuza, kununua, au kupitisha mifugo kinyume na maeneo au vibali vilivyoidhinishwa.
6. Itakuwa marufuku kwa mfugaji yeyote- (a) kuchunga, kulisha au kunywesha maji mifugo katika maeneo yote ambayo hayakutengwa kwa ajili hiyo; (b) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani zaidi ya kilometa thelathini; Marufuku kwa mfugaji (c) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo kutoka lingine kibali bila moja hadi Halmashauri; (d) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali kitakachotolewa na Halmashauri; (e) kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa na Halmashauri; na (f) kupitisha mifugo katika maeneo ambayo hayakuidhinishwa na Halmashauri kupitisha 4 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) Kudhibiti mifugo inayozurura hovyo mifugo. - 7 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakamata mifugo au mfugo
AI-assisted research summary: Halmashauri must seize roaming livestock in prohibited grazing areas, and the owner must pay TZS 20,000 per animal if the animal is seized in the wrong place.
7.-(1) Halmashauri itakamata mifugo au mfugo wowote utakaoonekana unazurura hovyo katika eneo la Halmashauri ambapo hapajaruhusiwa kuchungia mifugo. (2) Mfugo wowote utakaokamatwa mahali pasipostahili utalipiwa faini ya Shilingi elfu ishirini kwa kila mfugo baada ya kulipia gharama hizo mfugaji atarudishiwa mifugo yake. (3) Endapo mwenye mifugo au mfugo hatatokea ndani ya siku saba (7) tangu kukamatwa kwa mifugo hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri atakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mfugo au mifugo hiyo baada ya kupata idhini ya Mahakama. (4) Baada ya mauzo, Mkurugenzi atakata fedha za faini, gharama za mnada na gharama za ulinzi na fedha zitakazobaki atapewa mwenye mifugo. (5) Endapo kwa mfugo kutatokea Halmashauri, haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama vifo hivyo vitakuwa vimesababishwa kwa uzembe wa Halmashauri. kufa Ukaguzi wa mifugo - 8 Verify source ↗
(1) Maafisa mifugo wa Halmashauri au Afisa
AI-assisted research summary: Livestock officers or an appointed officer may enter enclosures or buildings during working hours to inspect compliance with the bylaw.
8.-(1) Maafisa mifugo wa Halmashauri au Afisa Mwidhiniwa atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii ataweza kuingia katika maboma au jengo lolote wakati wa muda wa kazi kwa madhumuni ya kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Mtu yeyote atakayemzuia Afisa Mifugo au Afisa Mwidhiniwa katika kutekeleza wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa. Taratibu za ufugaji - 9 Verify source ↗
(1) Wafugaji wote watatakiwa kuzingatia
AI-assisted research summary: Wafugaji, na watu wanaoshughulika na mifugo, lazima wafuate masharti ya ufugaji; kuchinja hufanyika kwenye machinjio au sehemu iliyotengwa, na kuna marufuku ya biashara ya mifugo nje ya minada au magulio yaliyotengwa. Mbwa na nguruwe hawapaswi kuachiliwa wakizurura, na mbwa wanatakiwa kufungiwa kwa muda ulioelezwa.
9.-(1) Wafugaji wote watatakiwa kuzingatia masharti ya ufugaji kama yalivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (2) Kila mfugaji atatakiwa kuchinja mifugo yake 5 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) machinjioni au mahali palipotengwa kwa ajili ya huduma hiyo. (3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kununua, kuuza au kufanya biashara ya kubadilishana aina yoyote ya mifugo katika eneo lolote la Halmashauri isipokuwa kwenye minada au magulio yaliyotengwa kwa shughuli hiyo. (4) Itakuwa marufuku kwa mbwa na nguruwe kuachiliwa wakizurura. (5) Mbwa watatakiwa kufungiwa kuanzia Saa kumi na mbili kamili asubuhi na kuachiwa Saa nne kamili usiku. Taratibu za kilimo Marufuku - 10 Verify source ↗
(1) Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za
AI-assisted research summary: A person who wants to do farming in the Council area must follow agricultural procedures issued by the Council. The Agricultural Officer may enter any farm during working hours to inspect and ensure compliance with this by-law.
10.-(1) Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za kilimo katika Halmashauri atatakiwa kuzingatia taratibu za kilimo kama zitakavyotolewa na Halmashauri kwa kuzingatia ardhi na Sheria nyingine zitakazotungwa na Bunge. sheria za (2) Itakuwa halali kwa Afisa Kilimo kuingia katika shamba lolote wakati wa muda wa kazi kwa madhumuni ya kufanya ukaguzi na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. - 11 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima katika
AI-assisted research summary: People are prohibited from farming on slopes or near water bodies, using land against approved agricultural use, burning fields without a special council permit, and dumping pesticide waste into flowing water or rivers. The council must oversee farming and promote prevention of shifting cultivation and encourage crop rotation.
11.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, mabwawa na maziwa au kufanya jambo lolote litakalo haribu hifadhi ya mazingira. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kutumia ardhi kinyume na matumizi ya kilimo kama ilivyopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri. (3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kusafisha shamba kwa ajili ya kilimo kwa njia ya kuchoma moto isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa Halmashauri. (4) Kibali kitakachotolewa chini ya Sheria Ndogo hii kitakuwa cha maandishi na kitaonesha jina la mwenye kibali, tarehe na eneo analotaka kuchoma moto. (5) Muda unaotakiwa kuchoma moto chini ya Sheria Ndogo hii ni kuanzia Saa kumi na mbili kamili 6 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) asubuhi hadi Saa nne kamili asubuhi. (6) Ni wajibu wa Halmashauri kusimamia shughuli za kilimo na kuhakikisha kuwa wanazuia kilimo cha kuhamahama na kuhimiza kilimo cha mzunguko. (7) Ni marufuku kwa mtu yeyote kutupa mabaki ya vifungashio vya viuatilifu, kusafisha vipulizi au kumwaga mabaki ya viuatilifu katika vyanzo vya maji yanayotiririka au mito. Uhifadhi wa uoto wa asili - 12 Verify source ↗
Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa
AI-assisted research summary: Wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira yameharibiwa lazima warejeshe eneo hilo katika hali ya kawaida kwa kupanda miti.
12. Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira ya eneo husika yameharibiwa, kuhakikisha kuwa wanalirudisha katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti ili kutoendelea kuharibu mazingira na kurejesha uoto katika hali yake ya asili. Uchimbaji mchanga na kokoto Wajibu wa kulinda vyanzo vya maji - 13 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga, kifusi au kuchoma tofali katika maeneo yasiyoruhusiwa, na pia ni marufuku kujenga au kufanya shughuli za kiuchumi katika eneo la hifadhi.
13.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga, kifusi au kuchoma tofali katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri kama vile katika maeneo ya makazi ya watu, maeneo yaliyohifadhiwa, kando ya mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa isipokuwa kwa ruhusa maalumu ya Halmashauri. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kujenga nyumba au jengo lolote au kufanya shughuli zozote za kiuchumi katika eneo la hifadhi. - 14 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima isimamie na kulinda vyanzo vya maji, ichukue hatua za kisheria dhidi ya waharibifu, na Halmashauri pamoja na jamii husika wapande miti isiyonyonya maji; mtu yeyote haruhusiwi kumiliki eneo la chanzo cha maji isipokuwa Halmashauri.
14.-(1) Halmashauri kusimamia na kulinda vyanzo vya maji. itawajibika kuanzisha, (2) Halmashauri itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayeharibu chanzo cha maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji bila sababu ya msingi. (3) Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri na jamii husika kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo vya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu. (4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kumiliki eneo la chanzo cha maji isipokuwa Halmashauri. 7 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) Kulinda eneo la hifadhi Uchafuzi wa vyanzo vya maji Kuchoma au kusababisha moto - 15 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima,
AI-assisted research summary: Watu wote wanapigwa marufuku kulima, kukata miti, kuchunga mifugo au kuharibu chanzo cha maji ndani ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji; Halmashauri pia ina wajibu wa kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo hivyo kwa kufuata maelekezo ya Afisa Misitu.
15.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima, kukata miti, kuchunga mifugo katika umbali wa mita sitini kutoka vyanzo vya maji au kufanya lolote linaloharibu kwa namna yoyote chanzo cha maji na hifadhi ya mazingira. jambo (2) Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo vya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu. (3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kumiliki eneo la chanzo cha maji isipokuwa Halmashauri. - 16 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote, kiwanda,
AI-assisted research summary: Ni marufuku kumwaga maji machafu kwenye vyanzo vya maji au kuweka kitu chenye sumu ndani ya maji yanayotumiwa na binadamu au viumbe hai.
16.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote, kiwanda, taasisi au shirika kuelekeza mabomba ya maji machafu kwenye mito, mabwawa, ziwa, visima, mifereji, chemchemi au sehemu yoyote ambayo ni chanzo cha maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama au viumbe vingine vilivyo hai. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuweka kitu chochote chenye sumu ndani ya maji ambayo yanatumiwa na binadamu au kiumbe chochote hai. - 17 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuchoma au
AI-assisted research summary: No one may burn or cause fire in the forest council area, and people in the area must extinguish dangerous fires and help with fire-extinguishing when required.
17.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuchoma au la iliyoko eneo kusababisha moto katika misitu Halmashauri. (2) Ni wajibu wa kila mwananchi kuzima moto ambao utaonekana kuwaka katika eneo la Halmashauri yenye kuleta viashiria vya hatari. (3) Kila mkazi wa eneo hilo atawajibika kushiriki katika zoezi la kuzima moto endapo atatakiwa kufanya hivyo, kama (4) Mtu ambaye atashindwa kushiriki katika kuzima moto bila sababu ya msingi atakuwa ametenda kosa. Kibali cha kuchoma - 18 Verify source ↗
Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto
AI-assisted research summary: A person who has a permit to burn fire must notify nearby neighbors two days before burning and must take steps to stop the fire spreading.
18. Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto atalazimika kutoa taarifa siku mbili kabla ya kuchoma 8 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) moto moto kwa majirani walioko katika eneo analotaka kuchoma na ataweka njia za kuzuia moto kusambaa maeneo mengine. Ukataji miti Wajibu wa kupanda miti Wajibu wa Halmashaur i ya Kijiji - 19 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kukata miti
AI-assisted research summary: Kukata miti bila kibali cha Halmashauri ni marufuku, na kuvuna miti katika msitu uliohifadhiwa pia ni marufuku. Wavunaji wa miti kwa ajili ya mkaa lazima wawe na eneo maalumu lililoidhinishwa na Halmashauri.
19.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kukata miti kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali kutoka Halmashauri. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuvuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe hai maalumu ambao ni rasilimali kwa Taifa. (3) Watu wanaovuna miti kwa ajili ya kuchoma mkaa watatakiwa kuwa na eneo maalumu lililoidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kuchoma mkaa. - 20 Verify source ↗
Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika
AI-assisted research summary: Kila mkazi wa Halmashauri lazima apande na kutunza miti katika eneo lake, makazi yake, na mashamba anayomiliki.
20.Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika- (a) kupanda na kutunza miti katika eneo lake; (b) kupanda na kutunza miti katika makazi yake; na (c) kupanda na kutunza miti katika shamba au mashamba anayomiliki. - 21 Verify source ↗
Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kila kijiji
AI-assisted research summary: Vijiji, kaya na taasisi zinatakiwa kulinda na kupanda miti, kutenga maeneo ya hifadhi ya msitu, na kuzuia matumizi ya moto bila kibali wakati wa kuandaa mashamba.
21. Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kila kijiji- kitawajibika kutenga eneo la hifadhi ya msitu wa asili kwa ajili ya matumizi ya baadaye; kitatunza miti yote inayopandwa katika eneo la Kijiji; (a) (b) (c) kwa kila Kaya, inatakiwa kupanda miti katika maeneo yake kila mwaka; (d) kitapanda na kumiliki shamba la 9 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) miti lenye ukubwa wa ekari 2 kila mwaka na kulitunza; (e) kitahakikisha kuwa kila Taasisii ndani ya Halmashauri itapaswa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka majengo yake na lisilopungua kuwa na shamba miti hekta mbili; (f) kitatunza na kuhifadhi miti na nyasi kwenye milima, makorongo na vyanzo vya maji ili kuzuia mmomonyoko wa udongo; (g) kitahakikisha kuwa kila anayeandaa shamba kwa ajili ya kilimo hatumii moto bila kibali na anapanda miti kwenye mipaka ya shamba lake kama kinga upepo; (h) kila Mwenyekiti wa Kitongoji, Mtendaji wa Kijiji, Mkuu wa Taasisi yoyote Wilayani ana msitu wa hifadhi ya miti ya kupandwa au ya asili kwa madhumuni ya kuhifadhi ardhi na mazingira; (i) kitahakikisha kuwa maeneo yote ya vilima na yenye vipara ambayo yanamilikiwa na watu binafsi na au Serikali ya Kijiji yanapandwa miti. - 22 Verify source ↗
(1)
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupia taka ngumu na laini na isimamie usafi kwa karibu katika eneo lake.
22.- (1) Utupaji wa taka ngumu na laini Ni wajibu wa Halmashauri kutenga eneo kwa ajili ya kutupa taka ngumu na laini na kusimamia kwa karibu usafi katika eneo lake. 10 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) (2) - 23 Verify source ↗
(1)
AI-assisted research summary: This section forbids dumping waste or relieving oneself near dam banks or water sources in the council area, and requires certain noisy/polluting activities and planned industrial/fuel/service activities to follow building and environmental precaution rules.
23.- (1) Uendesh aji wa viwanda, vituo vya mafuta, huduma za ujenzi Mtu yeyote atakayetupa hovyo taka ngumu au laini au kujisaidia katika kingo za mabwawa au kwenye vyanzo vya maji vilivyoko katika Halmashauri atakuwa ametenda kosa. Mtu yeyote anayeendesha shughuli za karakana, mashine ya kusaga, kuranda mbao, kukamua maji ya matunda, kuchomelea vyuma au kuendesha inayozalisha uchafu ambao shughuli yoyote unaleta athari kwa binadamu na viumbe wengine katika maeneo ya makazi ya watu atatakiwa kuzingatia taratibu za ujenzi. (2) (3) Endapo mtu yeyote atataka kuendesha shughuli za viwanda, vituo vya mafuta, vituo vya huduma mbalimbali za kuzingatia atatakiwa tahadhari ya athari za mazingira. ujenzi Mtu yeyote atakayekiuka aya ndogo ya (1) na (2) atakuwa ametenda kosa. Makosa yanayoh usu mifugo - 24 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akipeleka au kusafirisha mifugo bila kibali, akilisha mifugo mahali pasiporuhusiwa, au akivua samaki kwa sumu au nyavu zenye matundu madogo.
24. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa- (a) ataingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (b) atasafirisha mifugo bila kuwa na kibali; (c) atalisha mifugo katika maeneo yasiyoruhusiwa; (d) atavua samaki kwa kutumia sumu au nyavu zenye matundu madogo (kokoro). Makosa yanayoh usu kilimo - 25 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kilimo,
AI-assisted research summary: Anyone who breaks the agricultural rules or digs sand, gravel, or minerals in areas not allowed by the Council commits an offence.
25. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kilimo, kuchimba mchanga, kokoto, madini katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri atakuwa ametenda kosa. 11 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) Makosa yanayoh usu hifadhi ya ardhi Makosa yanayoh usu vyanzo vya maji Makosa yanayoh usu kuvuna, kuuza, kusafiris ha na kuhifadh i Mazao ya Misitu - 26 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kuhifadhi ardhi
AI-assisted research summary: A person who violates land conservation conditions commits an offence.
26. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kuhifadhi ardhi atakuwa ametenda kosa. - 27 Verify source ↗
(1)
AI-assisted research summary: Anyone who destroys water sources, fails to take part in conserving them, or places poison that affects human or other living things commits an offence.
27.- (1) (2) Mtu yeyote atakayeharibu vyanzo vya maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji atakuwa ametenda kosa. Mtu yeyote atakayebainika kuwa ameweka sumu ya aina yoyote kwa inaathiri namna yoyote maisha ya binadamu na viumbe wengine ambao ni rasilimali ya Taifa atakuwa ametenda kosa. ambayo - 28 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa
AI-assisted research summary: Any person commits an offence if they do any of the listed forest and land-use activities without permission, or fail to help extinguish a fire.
28. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa- (a) atachoma au kusababisha moto katika misitu bila kibali; (b) atashindwa kushiriki katika kuzima moto; (c) atavuna mazao ya misitu katika misitu iliyohifadhiwa na isiyohifadhiwa bila kibali; (d) atachoma mkaa na kukata kuni bila kibali; (e) atafyeka nyasi, kung’oa vichaka na kung’oa visiki kwenye misitu bila kibali; kwenye (f) atachunga mifugo lolote lililopandwa miti, iliyohifadhiwa kama bustani ya miti, msitu ya asili au iliyopandwa kwa ajili ya hifadhi; eneo (g) atakata miti au kuchungia mifugo kwenye miti iliyopandwa kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko wa udongo au kukinga upepo; (h) atabandua magome ya miti kwa ajili ya kutengeneza vilindo, mzinga na vitu vingine bila 12 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) Makosa yanayoh usu taka ngumu na laini Makosa yanayoh usu taka za majimaji Adhabu ya kuwa na kibali; au (i) atalima au kukata miti katika vyanzo vya maji, milima, kando ya njia, makorongo na sehemu nyingine zozote zinazohifadhiwa ili kupunguza mmomonyoko wa udongo. - 29 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetupa hovyo taka ngumu au laini
AI-assisted research summary: Anyone must not dump solid or liquid waste in places that are not allowed.
29. Mtu yeyote atakayetupa hovyo taka ngumu au laini katika maeneo yoyote yasiyoruhusiwa na Sheria Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa ametenda kosa. - 30 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetiririsha maji machafu yanayoleta
AI-assisted research summary: Anyone who discharges wastewater that harms humans or other living creatures commits an offence.
30. Mtu yeyote atakayetiririsha maji machafu yanayoleta madhara kwa binadamu na viumbe vingine hai atakuwa ametenda kosa. - 31 Verify source ↗
Section 31
AI-assisted research summary: Anyone who breaches the by-law commits an offence and may be fined, imprisoned for up to 12 months, or both.
31.- (1) (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti yaliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi elfu hamsini na isiyozidi Shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. Pamoja na adhabu iliyotolewa chini ya aya ndogo ya (1), mkosaji anaweza Halmashauri kuamriwa gharama uharibifu wowote aliosababisha kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. kuilipa za Kufifilis ha kosa - 32 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji Shilingi elfu hamsini ikiwa anakiri kosa na yuko tayari kujaza fomu maalumu.
32. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari 13 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Sheria Ndogo hii. ___ ___ ___ _ JEDWALI __________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 32) HATI YA UFILILISHAJI WA MAKOSA mbele MWENYEWE Mimi …………………………………………nakiri KWA HIARI YANGU ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …… ya Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya mwaka, 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 14 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 898 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Kyerwa imegongwa kwenye sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Kyerwa uliofanyika Tarehe …. Mwezi… Mwaka…. na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- SACF. JAMES MARCO JOHN Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa MH. BAHATI HENERICO Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 20 Novemba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 15
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in