Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
Sheria Ndogo hii inaitwa Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Sheria Ndogo hii inaitwa Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023. This by-law applies throughout the entire area of Kyerwa District Council. This section defines key terms used in the by-law, including fee, council, permit, building minerals, the Director, levy, and agent. Anayetaka kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri lazima aombe kibali kwa Mkurugenzi na aambatishe nyaraka zinazotakiwa. Aliyepewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi lazima aombe kibali, alipe ada ya shilingi 300,000, azingatie masharti husika, na alipe ushuru na tozo zinazotozwa na Halmashauri.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama
AI-assisted research summary: Sheria Ndogo hii inaitwa Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Kyerwa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including fee, council, permit, building minerals, the Director, levy, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni malipo yatakayolipwa na mtu yeyote kwa Halmashauri kwa ajili ya kupata kibali kinachotolewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “madini ya ujenzi” maana yake ni tarazo, moramu, udongo, kifusi, kokoto, mawe, 1 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 900 (Linaendelea) mchanga, chokaa na madini mengine yanayotumika katika ujenzi; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa na inajumuisha Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli zinazohusu ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri; “wakala” maana yake mtu, taasisi, kikundi cha watu, kampuni au asasi iliyoteuliwa na Halmashauri kukusanya ushuru wa madini ya ujenzi kwa niaba yake. Maombi ya kibali au taasisi - 4 Verify source ↗
(1) Mtu,
AI-assisted research summary: Anayetaka kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri lazima aombe kibali kwa Mkurugenzi na aambatishe nyaraka zinazotakiwa.
4.-(1) Mtu, kampuni inayokusudia kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri itatakiwa kuwasilisha kwa Mkurugenzi maombi ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi kupitia fomu maalumu itakayotolewa na Halmashauri. (2) Maombi ya kibali yataambatishwa na taarifa zifuatazo: (a) leseni ya uchimbaji wa madini iliyotolewa na mamlaka husika; (b) aina ya madini yanayokusudiwa kuchimbwa; (c) uthibitisho wa umiliki pamoja na linalokusudiwa ukubwa wa eneo kuchimbwa madini ya ujenzi; (d) mpango wa utunzaji wa mazingira katika eneo la machimbo; na (e) muhtasari wa mkutano wa kijiji ambacho uchimbaji wa madini ya ukionyesha utafanyika ujenzi kukubaliana na uchimbaji huo. (3) Ndani ya muda wa siku saba tangu 2 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 900 (Linaendelea) kupokea maombi, Mkurugenzi atatakiwa kukagua eneo ambalo uchimbaji wa madini ya ujenzi unakusudiwa kufanyika ili kujiridhisha iwapo eneo hilo linafaa kwa shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi. (4) Ndani ya muda wa siku saba tangu kukamilika kwa ukaguzi wa eneo linaloombewa kibali, Mkurugenzi atatakiwa kukubali au kukataa maombi hayo na endapo atakataa atatakiwa kutoa sababu za kukataa maombi hayo. Wajibu wa mpewa kibali - 5 Verify source ↗
Mtu, taasisi au kampuni iliyopewa
AI-assisted research summary: Aliyepewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi lazima aombe kibali, alipe ada ya shilingi 300,000, azingatie masharti husika, na alipe ushuru na tozo zinazotozwa na Halmashauri.
5. Mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi itatakiwa: (a) kuomba kibali kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii; (b) kulipa ada ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi ya kiasi cha shilingi laki tatu; (c) kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii na masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi; na (d) kulipa ushuru na tozo mbalimbali zitakazotozwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii au Sheria Ndogo nyingine iliyotungwa na Halmashauri. Muda wa uchimbaji na masharti ya usafirishaji - 6 Verify source ↗
(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji na
AI-assisted research summary: Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri hufanyika kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni; Mkurugenzi anaweza kutoa kibali maalumu kwa shughuli hizi kufanyika nje ya muda huo; na mmiliki wa gari linalosafirisha madini ya ujenzi lazima ahakikishe gari limefunikwa wakati wa usafirishaji.
6.-(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri zitafanyika kuanzia Saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi Saa kumi na mbili jioni ya kila siku. (2) Bila kujali masharti ya aya ndogo ya (1), Mkurugenzi anaweza kutoa kibali maalumu 3 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 900 (Linaendelea) kuruhusu shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi kufanyika nje ya muda ulioainishwa katika aya ndogo ya (1). (3) Kila mmiliki wa gari linalosafirisha madini ya ujenzi atatakiwa kuhakikisha kuwa limefunikwa wakati wote wa gari hilo usafirishaji wa madini ya ujenzi. - 7 Verify source ↗
Kutakuwa na ushuru wa madini ya
AI-assisted research summary: Mnunuzi au msafirishaji wa madini ya ujenzi anatakiwa kulipa ushuru wa madini hayo.
7. Kutakuwa na ushuru wa madini ya ujenzi ambao utalipwa na mnunuzi au msafirishaji wa madini ya ujenzi kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. - 8 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi
AI-assisted research summary: Madereva wanaobeba madini ya ujenzi lazima wasimame katika kituo cha ukaguzi na kuonyesha stakabadhi ya kielektroni kuthibitisha malipo ya ushuru.
8.-(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo ya ushuru wa madini ya ujenzi katika njia zinazoingia au kutoka katika maeneo ya machimbo ya madini ya ujenzi. (2) Kila dereva wa gari au chombo chochote cha usafiri kilichobeba madini ya ujenzi atatakiwa kusimama katika kituo cha ukaguzi wa malipo ya ushuru wa madini ya ujenzi na kuonesha stakabadhi ya kielektroniki kuthibitisha kulipwa kwa ushuru wa madini ya ujenzi yaliyo katika gari au chombo cha usafiri anachoendesha. - 9 Verify source ↗
Halmashauri itatakiwa kutoza ada au
AI-assisted research summary: Halmashauri must collect fees or taxes using electronic machines.
9. Halmashauri itatakiwa kutoza ada au ushuru kwa kutumia mashine za kielektroniki. - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kufuta au
AI-assisted research summary: The Council may revoke or suspend a construction-mining permit if it finds a breach of the by-law or permit conditions.
10.-(1) Halmashauri inaweza kufuta au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi endapo itajiridhisha kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Sheria Ndogo hii au masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi. (2) Kabla ya kufuta au kusimamisha 4 Ushuru wa madini ya ujenzi Vituo vya ukaguzi Matumizi ya stakabadhi ya kielektroniki Kufutwa au kusimamishwa kwa kibali Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 900 (Linaendelea) kibali, Halmashauri itatakiwa kutoa kwa mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali notisi ya siku saba ya kusudio la kufuta au kusimamisha kibali. (3) Notisi itakayotolewa kwa mujibu wa aya ndogo ya (2) itaainisha sababu za kufuta au kusimamisha kibali husika. (4) Endapo kitafutwa au kusimamishwa, mtu, au kampuni iliyopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi itakoma kuchimba madini hayo. kibali taasisi Wakala Makosa na adhabu - 11 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kuteua mtu,
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua mtu, kikundi cha watu, taasisi au kampuni kukusanya ushuru kwa niaba yake.
11. Halmashauri inaweza kuteua mtu, kikundi cha watu, taasisi au kampuni kukusanya ushuru kwa niaba yake. - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayechimba au kusafirisha madini ya ujenzi bila kibali au bila kulipa ushuru, au anayevunja masharti ya usafirishaji na muda wa uchimbaji, anatenda kosa na anaweza kuadhibiwa kwa faini, kifungo, au vyote viwili.
12. Mtu yeyote ambaye- (a) ataanzisha machimbo ya madini ya ujenzi kibali kuwa kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hii; bila na (b) atasafirisha madini ya ujenzi bila kulipa ushuru; (c) atachimba madini ya ujenzi kabla au ulioruhusiwa ya muda baada kuchimba; (d) atasafirisha madini ya ujenzi katika gari ambalo halijafunikwa; au (e) atamshawishi mtu au kundi la watu kutolipa ushuru, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi laki mbili na isiyozidi Shilingi Milioni moja au kifungo kisichopungua mwaka mmoja na kisichozidi miaka miwili au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. 5 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 900 (Linaendelea) Kufifilisha kosa - 13 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa na kumtoza mkosaji Shilingi laki mbili ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari, anatumia fomu maalumu, na yuko tayari kutimiza wajibu wake.
13. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi laki mbili iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari fomu maalumu na kuwa iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii na kuwa tayari kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. tayari kujaza 6 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 900 (Linaendelea) ________________ JEDWALI LA KWANZA __________________ Limetengenezwa chini ya aya ya 5(a)) KIBALI CHA UCHIMBAJI WA MADINI YA UJENZI kwa kimetolewa Bw/Bi Kibali hiki ………………………………….……wa SLP………………,KYERWA. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ameridhia ndugu mtajwa hapo juu, aendeshe shughuli za Kuchimba madini ya Ujenzi katika eneo la …………………………kijiji cha …………………………….kata ya …………………………… baada ya kufanya ukaguzi katika eneo husika ili kutathimini athari za Mazingira. Kutokana na uzingatiaji wa athari za Mazingira Mchimbaji anaruhusiwa kuchimba madini ya ujenzi katika eneo hilo kwa muda wa miezi kumi na mbili tu. Mwombaji analazimika kuomba tena kibali baada ya muda huo kuisha na ukaguzi utafanyika tena. TAMKO LA MWOMBAJI; MIMI…………………………………………………………Nipo tayari kufuata masharti ya kibali hiki cha Uchimbaji wa Madini ya Ujenzi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa lengo la kutunza na kuhifadhi mazingira. Nathibitisha kwa hiari yangu nimeelewa vema kibali hiki. Jina: ……………………………… Saini …………Tarehe ………………… KWA MATUMIZI YA OFISI; Mwombaji amelipia Shilingi …………………….tarehe…………….mwezi………….mwaka………….. (Ambatanisha stakabadhi ya malipo na fomu hii) Jina la Afisa aliyetoa kibali ……………………… Saini …………… Tarehe ………………. 7 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 900 (Linaendelea) __________ JEDWALI LA PILI ______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 7) USHURU WA MADINI YA UJENZI Aina ya Madini Na.
Part
JEDWALI LA PILI
- 5 Verify source ↗
Mawe, Moramu,
AI-assisted research summary: The provision lists fees for construction stones, sand, and gravel by quantity band, including fixed per-trip charges and a 3% charge for quantities above 7 tons.
5. Mawe, Moramu, Mchanga na Kokoto Ujazo /Tani Tani 3 –Tani 7 Tani 3 –Tani 7 Tani 3 –Tani 7 Tani 3 –Tani 7 Zaidi ya Tani 7 Kiwango cha Ada (Shilingi) 3,000 kwa tripu 2,000 kwa tripu 2,000 kwa tripu 5,000 kwa tripu 3% ya bei ya madini husika 8 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 900 (Linaendelea) _______________ JEDWALI LA TATU _______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 13) HATI YA KUFIFILISHA KOSA YANGU Mimi;………………………………………………………. nakiri KWA HIARI mbele ni Mkurugenzi ya;………………………………………..…….ambaye Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka;…….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya….. ya Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023. MWENYEWE Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe:…....... ya Mwezi:………… Mwaka:………….. Jina:…………………………………..……………………. Saini:…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jina:…………………………….………..…………………… Cheo:…………………………………………………..……. Saini:………………………………………………………… Tarehe:………………………………………………………. 9 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Tangazo La Serikali Na. 900 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Kerywa imegongwa kwenye sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Kyerwa uliofanyika Tarehe …. Mwezi… Mwaka…. na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- SACF. JAMES MARCO Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa MH. BAHATI HENERICO Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 20 Novemba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 10
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in