Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga ya mwaka 2023
This provision gives the bylaw its short title.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga ya mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the bylaw its short title. This bylaw applies throughout the whole area of Mkinga District Council. This section defines key terms used in the by-law, including authorized officer, Council, service levy, taxpayer, revenue year, and agent. Halmashauri lazima itozе na kukusanya ushuru wa huduma kwa 0.3% ya mauzo baada ya VAT na ushuru wa bidhaa kwa wafanyabiashara wenye leseni wanaowasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, na kiwango cha Jedwali la Kwanza kwa wale wasiowasilisha. Mlipa ushuru wa huduma lazima kuwasilisha taarifa ya mauzo kwa wakati; akishindwa, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka alete taarifa hiyo ndani ya siku 30.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga ya mwaka 2023
Showing 16 of 16
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This provision gives the bylaw its short title.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga ya mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the whole area of Mkinga District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including authorized officer, Council, service levy, taxpayer, revenue year, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa muidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga; “kipindi maalumu cha hesabu” maana yake ni muda ambao mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara kwa Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga au afisa yeyote 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Tangazo La Serikali Na. 901(Linaendelea) aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria; “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni taasisi, kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara mwenye leseni anayefanya shughuli zake katika eneo la Halmashauri; “mwaka wa mapato” maana yake ni kipindi cha mwaka wa fedha wa Serikali; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara yeyote mwenye leseni ya biashara ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne kutokana na huduma anazopata na kutumia miundombinu ya umma inayomuwezesha kufanya biashara katika eneo la Halmashauri; “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au shirika ambalo limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itozе na kukusanya ushuru wa huduma kwa 0.3% ya mauzo baada ya VAT na ushuru wa bidhaa kwa wafanyabiashara wenye leseni wanaowasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, na kiwango cha Jedwali la Kwanza kwa wale wasiowasilisha.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu (0.3) ya mauzo baada ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Thamani na ushuru wa bidhaa kutoka kwa mtu yeyote mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza kutoka kwa wafanyabiashara wenye leseni za biashara ambao hawawasilishi hesabu za mauzo Mamlaka ya Mapato Tanzania. Ushuru wa huduma Mamlaka ya - 5 Verify source ↗
(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma lazima kuwasilisha taarifa ya mauzo kwa wakati; akishindwa, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka alete taarifa hiyo ndani ya siku 30.
5.-(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Tangazo La Serikali Na. 901(Linaendelea) Mkurugenzi Wajibu wa mlipa ushuru kuwasilisha taarifa ya mauzo chini ya Sheria Ndogo hii atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo kwa wakati, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku thelathini kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi. - 6 Verify source ↗
(1) Mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, atunze kumbukumbu, na azionyeshe kwa uchunguzi kwa muda uliowekwa.
6.-(1) Mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu wa- (a) kulipa kwa kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hii; ushuru wa huduma kiwango (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila mwezi endapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania; (c) kuwasilisha hesabu sahihi na za kweli; (d) kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa kwa Halmashauri katika muda uliowekwa; (e) kutunza kumbukumbu za vitabu vya hesabu; na (f) kuonesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi. (2) Mlipa ushuru atawasilisha kwa Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa kipindi cha hesabu. (3) Mlipa ushuru wa huduma atatakiwa kulipa ushuru wa huduma ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kuwasilisha taarifa za mauzo ya kila mwezi. (4) Endapo mlipa ushuru hajawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha husika, Mkurugenzi atatoa notisi ya kumtaka kuwasilisha hesabu hizo ndani ya siku thelathini tangu siku ya kutolewa kwa notisi hiyo. (5) Endapo mlipa ushuru hajawasilisha majumuisho ya hesabu zake kwa mwaka wowote wa mapato, Mkurugenzi au afisa mwidhiniwa anaweza kwa kadri atakavyoona inafaa, 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Tangazo La Serikali Na. 901(Linaendelea) kukadiria kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo, isipokuwa makadirio hayo hayataathiri wajibu wowote wa mlipa ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kwa kushindwa kwake kuwasilisha hesabu hizo. (6) Ushuru unaotakiwa kulipwa kwa mujibu wa makadirio katika aya ndogo ya (5), utalipwa katika kipindi cha siku thelathini tangu tarehe ya makadirio hayo. (7) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (3), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru huo. Mamlaka ya Mkurugenzi - 7 Verify source ↗
Mkurugenzi atakua na mamlaka yafuatayo
AI-assisted research summary: The Director may require taxpayers and other persons with relevant information to provide records, accounts, and information for service levy assessment and collection.
7. Mkurugenzi atakua na mamlaka yafuatayo: (a) kumtaka mlipa ushuru yeyote kuwasilisha hesabu zenye taarifa kamili za shughuli za kibiashara zikionesha thamani ya kiasi na ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, kutolewa, kusambazwa au kuuzwa kibiashara na taarifa ya fedha katika kipindi maalumu kisichozidi siku thelathini tangu tarehe ya taarifa hiyo; (b) kwa taarifa ya maandishi ya siku saba anaweza kumtaka mlipa ushuru kuwasilisha kumbukumbu za kibiashara na vitabu vya hesabu kwa nia ya kupata taarifa kwa ajili ya kufanyiwa tathmini au kukusanya ushuru wa huduma; (c) kumtaka kwa maandishi mtu yeyote mwenye taarifa kuhusu mfanyabiashara anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi; (d) kumteua Kamishna wa kodi ya forodha au kodi ya mapato kwa ajili ya kutathmini na kukusanya ushuru wa huduma na kuwasilisha kwa Halmashauri kwa 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Tangazo La Serikali Na. 901(Linaendelea) lengo la kupata ushuru wa huduma pamoja na madeni yake; (e) kumwagiza kwa maandishi Afisa Mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la taasisi ya kibiashara au la mlipa ushuru yeyote kwa nia ya kufanya uchunguzi na tathmini ya kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa kwa ajili ya kupata na kujua kiwango sahihi cha ushuru anachotakiwa kulipa. Ukokotoaji wa ushuru wa huduma - 8 Verify source ↗
Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikokotoe ushuru wa huduma kwa walipa ushuru wa huduma wanaowasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, ikizingatia taarifa za kipindi maalumu cha hesabu.
8. Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma kwa walipa ushuru wa huduma wanaowasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuzingatia taarifa zinazowasilishwa na walipa ushuru wa huduma katika kipindi maalumu cha hesabu. Uteuzi wa wakala Mamlaka ya afisa mwidhiniwa - 9 Verify source ↗
Bila ya kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri, na wakala huyo lazima awasilishe majumuisho ya makusanyo na ushuru aliokusanya.
9. Bila ya kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo hii, Mkurugenzi anaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri na wakala huyo atakuwa na majukumu ya- (a) kuwasilisha majumuisho ya makusanyo ya ushuru kwa Mkurugenzi au afisa mwidhiniwa; na (b) kuwasilisha ushuru aliokusanya kwa mujibu wa mkataba. - 10 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa anaweza
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kupokea, kukubali na kutathmini hesabu za mlipa ushuru, na pia kukataa hesabu za mwisho na kufanya tathmini nyingine akiwa na sababu za msingi za kuamini hesabu si sahihi.
10. Afisa Mwidhiniwa anaweza- (a) kupokea na kukubali hesabu za mlipa ushuru na kuzifanyia kutathmini; (b) kufanya tathmini kuhusu kiwango cha hesabu cha mlipa ushuru endapo hesabu hizo zitakuwa si sahihi; au (c) kukataa hesabu za mwisho na kufanya tathmini 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Tangazo La Serikali Na. 901(Linaendelea) Makosa kuhusu hesabu hizo iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hesabu hizo siyo sahihi. - 11 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akishindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo, kulipa ushuru wa huduma kwa wakati, kutoa taarifa zisizo sahihi, kuzuia maafisa kutekeleza majukumu yao, au kutunza kumbukumbu na nyaraka zinazoombwa kwa ajili ya ukaguzi.
11.-(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atashindwa kuwasilisha kwa Halmashauri taarifa sahihi za mauzo katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) atawasilisha kwa Halmashauri taarifa zisizo sahihi; (c) atashindwa kulipa ushuru wa huduma katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (d) atamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru; (e) atamzuia au atajaribu kumzuia afisa mwidhiniwa au wakala kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria Ndogo hii; (f) atafanya hesabu za uongo kwa kupunguza au kutoa hesabu zisizokuwa sahihi kwa Halmashauri au wakala; (g) atatoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu jambo lolote la mtu lake au jukumu linaloweza kuathiri mwingine la kulipa ushuru; au (h) ataandaa atatengeneza atasababisha kuandaliwa au kutengenezwa kwa vitabu vya uongo vya hesabu au kumbukumbu; au (i) atashindwa kulipa ushuru wa huduma ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; au (j) atashindwa kutunza kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya ukaguzi. Adhabu - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetenda kosa chini ya Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Anyone convicted of an offence under this by-law may be fined, imprisoned for 12 to 24 months, or receive both penalties.
12. Mtu yeyote atakayetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii na akatiwa hatiani atatozwa faini isiyopungua shilingi laki shilingi milioni moja au kifungo mbili na isiyozidi 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Tangazo La Serikali Na. 901(Linaendelea) kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote mbili kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 13 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtenda kosa hadi shilingi 200,000 ikiwa mkosaji anakiri, anajaza fomu maalumu, na analipa ada au ushuru unaodaiwa.
13. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. ______________ JEDWALI LA KWANZA _______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 4(2)) _____________ VIWANGO VYA USHURU WA HUDUMA KWA WAFANYABIASHARA WADOGO Namba Kiwango cha Leseni kwa Mwaka Tsh. 0- 20,000 Ushuru wa Huduma anayopaswa kulipa (Shilingi) 10,000.0 kwa mwaka
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wanaotumia mashine za EFD wanatakiwa kulipa 0.3% ya mapato yao kwa mwaka.
8. Tsh. 21,000-50,000 15,000.00 kwa mwaka Tsh. 51,000-100,000 20,000.00 kwa mwaka Tsh. 101,000- 30,000.00 kwa mwaka Wafanyabiashara wanaotumia mashine za EFD 0.3% ya mapato yao kwa mwaka Mnara wa simu na redio - 0 Verify source ↗
3% kwa kila robo mwaka
AI-assisted research summary: The text mentions 0.3% per quarter for salt mines.
0.3% kwa kila robo mwaka Migodi ya chumvi - 0 Verify source ↗
3% ya mauzo kwa mwezi
AI-assisted research summary: Inaonyesha ushuru wa 0.3% ya mauzo kwa mwezi na kiasi cha 5,000/= kwa mwaka kwa wafanyabiashara wadogo wasio na leseni wala kitambulisho cha Mjasiliamali.
0.3% ya mauzo kwa mwezi Wafanyabiashara wadogo wasio na leseni wala kitambulisho cha Mjasiliamali 5,000/= kwa mwaka 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Tangazo La Serikali Na. 901(Linaendelea) _____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 12) _____________ FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi………………………………………………………nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, niko tayari kulipa kiasi cha Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe………….ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina………………………………..Saini……………………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Tangazo La Serikali Na. 901(Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Mkinga imegongwa kwenye sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Mkinga uliofanyika Tarehe 29 Mwezi 11 Mwaka. 2022 na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- ZAHARA A. MSANGI Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga AMANI J. KASINYA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais,( Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga ya mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in