Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya mwaka 2023
This provision states the short title of the by-law: the Mlimba District Council Service Levy By-law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision states the short title of the by-law: the Mlimba District Council Service Levy By-law, 2023. This provision says the by-law applies throughout the whole area of Mlimba District Council. This section defines key terms used in the By-Law, including the Council, Director, service levy, service levy payer, company, company branch, and authorized officer. Halmashauri must charge and collect service tax from business licence holders, using a 0.3% rate on sales after deducting VAT and excise duty when sales accounts are submitted to the Tanzania Revenue Authority; a different rate in the First Schedule applies when sales accounts are not submitted. Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe ushuru, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, atunze kumbukumbu, na atoee nyaraka kwa ukaguzi; pia kuna muda maalum wa malipo na uwasilishaji.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya mwaka 2023
Showing 13 of 13
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This provision states the short title of the by-law: the Mlimba District Council Service Levy By-law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This provision says the by-law applies throughout the whole area of Mlimba District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba. Tafsiri Sura ya 212 - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the By-Law, including the Council, Director, service levy, service levy payer, company, company branch, and authorized officer.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba; “hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho zinazowasilishwa na taasisi yoyote ya kibiashara baada ya kipindi cha hesabu pamoja na nyaraka au maelezo yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “kampuni” maana yake ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “kipindi maalumu cha hesabu” maana yake ni muda ambao mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu za 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 906 (Linaendelea) biashara kwa halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria; “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni taasisi, kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara mwenye leseni anayefanya shughuli zake katika eneo la Halmashauri; “tawi la kampuni” maana yake ni tawi la kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara yeyote mwenye leseni ya biashara ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne kutokana na huduma anazopata na kutumia miundombinu ya umma inayomuwezesha kufanya biashara katika eneo la Halmashauri; “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au shirika ambalo limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri husika. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge and collect service tax from business licence holders, using a 0.3% rate on sales after deducting VAT and excise duty when sales accounts are submitted to the Tanzania Revenue Authority; a different rate in the First Schedule applies when sales accounts are not submitted.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu ya mauzo baada ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Thamani na ushuru wa bidhaa kutoka kwa mtu yeyote mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza kutoka kwa wafanyabiashara wenye leseni za biashara ambao hawawasilishi hesabu za mauzo Mamlaka ya Mapato Tanzania. - 5 Verify source ↗
(1) Mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe ushuru, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, atunze kumbukumbu, na atoee nyaraka kwa ukaguzi; pia kuna muda maalum wa malipo na uwasilishaji.
5.-(1) Mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu wa- (a) kulipa ushuru wa huduma kiwango kwa 2 Sura ya 212; Ushuru wa Huduma Wajibu wa mlipa ushuru Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 906 (Linaendelea) kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila mwezi endapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania; (c) kuwasilisha hesabu sahihi na za kweli; (d) kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa kwa Halmashauri katika muda uliowekwa; (e) kutunza kumbukumbu za vitabu vya hesabu; na (f) kuonesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi. (2) Mlipa ushuru wa huduma atatakiwa kulipa ushuru wa huduma ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kuwasilisha taarifa za mauzo ya kila mwezi. (3) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (2), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru huo. (4) Mlipa ushuru atawasilisha kwa Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa kipindi cha hesabu. (5) Endapo mlipa ushuru hajawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha husika na ametakiwa kufanya hivyo kwa notisi ya siku thelathini, Mkurugenzi anaweza kwa kadri atakavyoona inafaa, kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (6) Ushuru uliotathminiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii utalipwa katika kipindi cha siku thelathini tangu tarehe ya kufanya tathmini. (7) Endapo mlipa ushuru hajawasilisha majumuisho ya hesabu zake kwa mwaka wowote wa mapato, na endapo Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa anafikiri kwamba mlipa ushuru huyo ana wajibu wa kulipa ushuru kwa mwaka huo, anaweza kwa kadri atakavyoona, kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo, isipokuwa tathmini hiyo haitaathiri wajibu wowote wa mlipa ushuru anayostahili kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kwa kushindwa kwake kuwasilisha hesabu hizo. 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 906 (Linaendelea) Mamlaka ya Mkurugenzi - 6 Verify source ↗
Mkurugenzi atakua na mamlaka yafuatayo
AI-assisted research summary: The Director has authority to require taxpayers and others to provide business records, information, and supporting documents for tax assessment and collection.
6. Mkurugenzi atakua na mamlaka yafuatayo: (a) kumtaka mlipa ushuru yeyote kuwasilisha hesabu zenye taarifa kamili za shughuli za kibiashara zikionyesha thamani ya kiasi na ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, kutolewa kusambazwa au kuuzwa kibiashara na taarifa ya fedha katika kipindi maalum kisichozidi siku thelathini tangu tarehe ya taarifa hiyo; (b) kwa taarifa ya maandishi ya siku saba anaweza kumtaka mlipa ushuru kuwasilisha kumbukumbu za kibiashara na vitabu vya hesabu kwa nia ya kupata taarifa kwa ajili ya kufanyiwa tathmini au kukusanya ushuru wa huduma; (c) kumtaka kwa maandishi mtu yeyote mwenye taarifa kuhusu mfanyabiashara anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi; (d) kumteua Kamishna wa kodi ya forodha au kodi ya mapato kwa ajili ya kutathmini na kukusanya ushuru wa huduma na kuwasilisha kwa Halmashauri kwa lengo la kupata ushuru wa huduma pamoja na madeni yake; (e) kumwagiza kwa maandishi Afisa Mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la taasisi ya kibiashara au la mlipa ushuru yeyote kwa nia ya kufanya uchunguzi na tathmini ya kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa kwa ajili ya kupata na kujua kiwango sahihi cha ushuru anachotakiwa kulipa. Uteuzi wa wakala - 7 Verify source ↗
Bila ya kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri, na wakala huyo lazima akusanye na kupokea ushuru katika eneo alilopangiwa kwa viwango vilivyoidhinishwa.
7. Bila ya kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo hii, Mkurugenzi anaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa aya ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa: 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 906 (Linaendelea) (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 8 Verify source ↗
Afisa mwidhiniwa anaweza
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa anaweza kupokea, kukubali, au kukataa hesabu za mlipa ushuru na kufanya tathmini ikiwa ana sababu za kuamini hesabu hizo si sahihi.
8. Afisa mwidhiniwa anaweza- (a) kupokea na kukubali hesabu za mlipa ushuru na kuzifanyia kutathmini kuhusu kiwango cha hesabu cha mlipa ushuru endapo hesabu hizo zitakuwa si sahihi; au (b) kukataa hesabu za mwisho na kufanya tathmini kuhusu hesabu hizo iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hesabu hizo si sahihi. Mamlaka ya afisa mwidhiniwa Ukokotoaji wa ushuru wa huduma - 9 Verify source ↗
Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa mlipa
AI-assisted research summary: Halmashauri must calculate the service levy for a taxpayer who submits sales information to the Tanzania Revenue Authority.
9. Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa mlipa ushuru anaewasilisha taarifa za mauzo Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuzingatia taarifa zinazowasilishwa na mlipa ushuru wa huduma katika kipindi maalumu cha hesabu. Makosa - 10 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Anyone commits an offence if they fail to file correct sales returns, submit incorrect information, fail to pay the service levy on time, interfere with a service levy payer, block an authorized officer or agent, keep false accounts, or give false information that could affect another person’s levy obligation.
10.-(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atashindwa kuwasilisha kwa Halmashauri taarifa sahihi za mauzo katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) atawasilisha kwa Halmashauri taarifa zisizo sahihi; (c) atashindwa kulipa ushuru wa huduma katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (d) atamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru; (e) atamzuia au atajaribu kumzuia afisa muidhiniwa au wakala kutekeleza majukumu yake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (f) atafanya hesabu za uongo kwa kupunguza au kutoa hesabu zisizokuwa sahihi kwa Halmashauri au 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 906 (Linaendelea) wakala; au (g) atatoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu jambo lolote la mtu lake au jukumu linaloweza kuathiri mwingine la kulipa ushuru. Adhabu Kufifilisha kosa - 11 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetenda kosa chini ya Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence under this by-law is liable to a fine, imprisonment, or both.
11. Mtu yeyote atakayetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii na akatiwa hatiani atatozwa faini isiyopungua shilingi laki shilingi milioni moja au kifungo mbili na kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote mbili kwa pamoja. isiyozidi - 12 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji hadi shilingi laki mbili, ikiwa mkosaji anakiri kosa, anakubali kujaza fomu maalumu, na analipa ada au ushuru unaodaiwa.
12. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 906 (Linaendelea) _____________ JEDWALI LA KWANZA _______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 4(2)) _____________ USHURU WA HUDUMA Namba Aina ya malipo Leseni ya biashara
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: This section lists fee amounts for local alcohol club licences and annual service levy amounts, and includes a form for admitting an offence and agreeing to pay the debt and fine.
8. 0 hadi 15,000/= 20,000/= hadi 35,000/= 40,000/= hadi 45,000/= 50,000/= hadi 60,000/= 65,000/= hadi 100,000/= 105,000/= hadi 150,000/= 155,000/= hadi 200,000/= Malipo ya leseni za vilabu vya pombe za asili _____________ Kiasi cha malipo ya Ushuru wa Huduma kwa Mwaka (Shilingi) 5000/= 10,000/= 15,000/= 30,000/= 40,000/= 50,000/= 100,000/= 12,000/= kwa miezi sita(6) JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 12) _____________ FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi………………………………………………………nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, niko tayari kulipa kiasi cha Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe………….ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina………………………………..Saini……………………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 906 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya Mlimba imegongwa kwenye sheria Ndogo hii kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Mlimba uliofanyika Tarehe 27 Mwezi Oktoba Mwaka 2021 na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- ENG. STEPHANO B. KALIWA Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba INNOCENT SIMON MWANGASA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) . 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in