Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023
This section states the short title of the by-law: the Mlimba District Council Environmental Conservation By-Law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the short title of the by-law: the Mlimba District Council Environmental Conservation By-Law, 2023. This section says the by-law applies throughout the entire area of the Mlimba District Council. This section defines key terms used in the by-law, including the Authorized Officer, protected area, Council, environmental protection, forest, grazing areas, and related environmental terms. Halmashauri must set aside grazing areas, create a special route for livestock, and carry out a livestock census, issue livestock cards, and provide animal husbandry education. Livestock keepers must follow the council’s grazing routes and areas, keep a livestock card, comply with dipping/vaccination instructions, contribute to related costs where required, mark animals, attend training when required, avoid cutting trees for tsetse control, register livestock, and dip animals on the scheduled timetable.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023
Showing 32 of 32
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itaijulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section states the short title of the by-law: the Mlimba District Council Environmental Conservation By-Law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itaijulikana kama Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This section says the by-law applies throughout the entire area of the Mlimba District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba. Tafasiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the Authorized Officer, protected area, Council, environmental protection, forest, grazing areas, and related environmental terms.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “afisa mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “eneo la hifadhi” maana yake ni maeneo ya milima, maeneo ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu, ambayo miteremko yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; na maeneo mengine lengo “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba; “hifadhi ya mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi; mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji vinavyozingatia masharti na 1 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwidhiniwa chini ya Sheria ya Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; “kiwanda” maana yake ni jengo au eneo ambapo vitu vinatengenezwa; “kuvuna misitu” inajumuisha kufyeka, kukata au kung’oa misitu au visiki; “maeneo ya malisho” maana yake ni maeneo yaliyotemgwa kwa ajili ya malisho ya mifugo, pamoja na sehemu zote ambazo zimetengwa na Halmashauri kwa ajili ya malisho; Sura ya 191 “maji” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; Sura ya 191 “maji taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; Sura ya 323 Sura ya 191 “mazao ya misitu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Misitu; “mazingira” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sura ya 323 Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anaejishughulisha na ufugaji wa mifugo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “misitu” maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia 10 ya miti, uoto wa asili au iliyopandwa, au asilimia 50 au zaidi ya vichaka na miti inayoota upya ambayo itajumuisha aina yote ya misitu ya hifadhi ambayo itatangazwa chini ya Sheria ya Misitu na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri; Sura ya 191 “taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika 2 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) Wajibu wa Halmashauri Sheria ya Usimamizi Mazingira; “udongo” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga
AI-assisted research summary: Halmashauri must set aside grazing areas, create a special route for livestock, and carry out a livestock census, issue livestock cards, and provide animal husbandry education.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli za malisho ndani ya eneo la Halmashauri. (2) Halmashauri itatenga njia maalum ya kupitisha mifugo kwenda na kurudi malishoni au minadani. (3) Halmashauri itafanya Sensa ya mifugo na kutoa kadi za mifugo na elimu ya ufugaji bora kwa jamii. Wajibu wa mfugaji - 5 Verify source ↗
Kila mfugaji chini ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: Livestock keepers must follow the council’s grazing routes and areas, keep a livestock card, comply with dipping/vaccination instructions, contribute to related costs where required, mark animals, attend training when required, avoid cutting trees for tsetse control, register livestock, and dip animals on the scheduled timetable.
5. Kila mfugaji chini ya Sheria Ndogo hii atatakiwa- (a) kufuga na kulisha mifugo katika maeneo ya malisho yaliyopangwa na Halmashauri; (b) kupitisha mifugo yake katika njia zilizopangwa na kutengwa na Halmashauri; (c) kuwa na kadi ya mifugo itakayoonesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; (d) akupeleka mifugo katika josho kama atakavyoagizwa na Halmashauri; (e) kupeleka mifugo yake katika vituo vya chanjo kama itakavyoamriwa na Halmashauri, na atalipia chanjo hiyo kama atatakiwa kufanya hivyo; (f) kuchangia gharama za ukarabati wa josho kama sehemu ya mchango wake, pale itakapobidi kufanya gharama na itakayopendekezwa na Halmashauri; hivyo, kwa (g) kuchangia gharama za uboreshaji wa maeneo ya malisho yaliyotengwa na Halmashauri; (h) kuweka alama kwenye mifugo yake na katika viungo vya mifugo vinavyopendekezwa ili kutoharibu zao la ngozi; (i) kuhudhuria mafunzo ufugaji kama ya 3 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) Marufuku kwa mfugaji Kudhibiti mifugo inayozurura ovyo atakavyohitajiwa na Halmashauri; (j) kutokata miti kwa lengo la kufukuza mbung’o; na (k) kusajili mifugo katika rejista ya Kijiji nakuogesha mifugo katika majosho kama ratiba itakavyopangwa.
Part
sehemu ya mchango wake, pale itakapobidi
- 6 Verify source ↗
Itakuwa marufuku kwa mfugaji yeyote
AI-assisted research summary: Mfugaji yeyote haruhusiwi kuchunga, kulisha, kunywesha, kusafirisha, kuhamisha, kuingiza, kuuza, kununua au kupitisha mifugo kinyume na maeneo na vibali vilivyoidhinishwa na Halmashauri.
6. Itakuwa marufuku kwa mfugaji yeyote- (a) kuchunga, kulisha au kunywesha maji mifugo katika maeneo yote ambayo hayakutengwa kwa ajili hiyo; (b) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani zaidi ya kilometa thelathini; (c) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo kutoka lingine kibali bila hadi moja Halmashauri; (d) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali kitakachotolewa na Halmashauri; (e) kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, soko au gulio la mifugo lililoidhinishwa na Halmashauri; na (f) kupitisha mifugo katika maeneo ambayo hayakuidhinishwa na Halmashauri. - 7 Verify source ↗
(1)
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kukamata mifugo inayozurura sehemu zisizoruhusiwa, kutoza faini ya shilingi 20,000 kwa kila mfugo, na inaweza kuuza mnadani mfugo ambao haujachukuliwa ndani ya siku 7 kwa idhini ya Mahakama.
7.-(1) mifugo itakayoonekana inazurura ovyo katika eneo la Halmashauri ambalo halijaruhusiwa kuchungia mifugo. Halmashauri itakamata (2) Mfugo wowote utakaokamatwa mahali pasipostahili utalipiwa faini ya shilingi elfu ishirini kwa kila mfugo na baada ya kulipia gharama hizo mfugaji atarudishiwa mfugo wake. (3) Endapo mfugo uliokamatwa hautachukuliwa na mmiliki ndani ya kipindi cha siku saba tangu kukamatwa, Halmashauri itakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mfugo huo baada ya kupata idhini ya Mahakama, na fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmiliki wa mfugo huo 4 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) Ukaguzi wa mifugo Taratibu za ufugaji baada ya kutoa faini inayodaiwa, gharama za kuhifadhi mfugo, gharama ya Mahakama na gharama ya mnada. (4) Bila kuathiri aya ndogo ya (3), kabla ya kuuza mfugo huo kwa mnada, Halmashauri itamjulisha mmliki na umma juu ya kusudio hilo. (5) Endapo kutatokea kufa kwa mifugo kutokana na sababu yoyote, Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama vifo hivyo vitakuwa vimesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri au wakala. - 8 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye boma au jengo kati ya saa 12 asubuhi na saa 12 jioni ili kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; mtu yeyote anayemzuia hufanya kosa.
8.-(1) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika boma au jengo lolote kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni Kwa dhumuni la kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Mtu yeyote atakayemzuia Afisa Mwidhiniwa katika kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa. - 9 Verify source ↗
(1) Wafugaji wote watatakiwa kuzingatia
AI-assisted research summary: Wafugaji lazima wazingatie masharti ya kufuga, wapeleke mifugo machinjioni au mahali huduma hiyo ilipo, na wafuate sheria za kuuza, kuchinja, na kufunga mbwa.
9.-(1) Wafugaji wote watatakiwa kuzingatia masharti ya kufuga kama yalivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. (2) Kila mfugaji atatakiwa kupeleka mifugo yake machinjioni au mahali huduma hiyo inapopatikana na itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchinja mifugo mahali pengine popote ambapo sio machinjio isipokuwa kwa kutoa taarifa kwa Afisa Mwidhiniwa na atalazimika kulipia gharama za machinjio kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. (3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kununua, kuuza au kufanya biashara ya kubadilishana aina yoyote ya mifugo katika eneo lolote la Halmashauri isipokuwa kwenye minada au magulio yaliyotengwa kwa shughuli hiyo. (4) Mfugaji atawajibika kumfungia mbwa wake wakati wote wa mchana na atamfungulia kuanzia saa nne 5 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) Taratibu za Kilimo Marufuku kamili usiku na kumfungia saa kumi na mbili kamili. - 10 Verify source ↗
(1) Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za
AI-assisted research summary: A person who wants to carry on agricultural activities in the Halmashauri must follow the agricultural procedures issued by the Halmashauri, and an authorized officer may enter any farm between 6:00 a.m. and 6:00 p.m. to inspect compliance.
10.-(1) Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za kilimo katika Halmashauri atatakiwa kuzingatia taratibu za kilimo kama zitakavyotolewa na Halmashauri kwa kuzingatia Sheria husika za ardhi. (2) Afisa mwidhiniwa anaweza kuingia katika shamba lolote kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. kwa dhumuni la kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. - 11 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: This section bans several farming and waste-disposal practices and requires the Council to oversee agriculture and promote rotational farming.
11.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote- (a) kulima katika miteremko, au karibu na vyanzo vya maji au kandokando ya mito au mabwawa na maziwa au kufanya jambo lolote litakalo haribu hifadhi ya mazingira; (b) kutumia ardhi kinyume na matumizi ya kilimo ilivyopangwa na kuidhinishwa na kama Halmashauri.; (c) kusafisha shamba kwa ajili ya kilimo kwa njia isipokuwa kwa kibali ya kuchoma moto maalum kutoka Halmashauri; au (d) kutupa mabaki ya vifungashio vya viuatilifu au kusafisha vipulizi au kumwaga mabaki ya viuatilifu katika chanzo cha maji au mto. (2) Kibali kitakachotolewa chini ya Sheria Ndogo hii kitakuwa cha maandishi na kitaonesha jina la mwenye kibali, tarehe na eneo analotaka kuchoma moto. (3) Muda unaotakiwa kuchoma moto chini ya Sheria Ndogo hii ni kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa nne kamili asubuhi. (4) Ni wajibu wa Halmashauri kusimamia shughuli za kilimo na kuzuia kilimo cha kuhamahama na kuhimiza kilimo cha mzunguko. Uhifadhi wa uoto wa asili - 12 Verify source ↗
Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa
AI-assisted research summary: Wakazi wa eneo husika wana wajibu wa kulinda mazingira yaliyoharibiwa na kuyarejesha katika hali ya kawaida kwa kupanda miti.
12. Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa 6 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) Uchimbaji mchanga na kokoto Wajibu wa kulinda vyanzo vya maji Kulinda eneo la Hifadhi asili au mazingira ya eneo husika yameharibiwa, kuhakikisha kua wanalirudisha katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti ili kutoendelea kuharibu mazingira. - 13 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga au kifusi, kuchoma tofali, kujenga nyumba/jengo, au kufanya shughuli za kiuchumi katika maeneo fulani bila ruhusa maalumu ya Halmashauri.
13.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga au kifusi au kuchoma tofali katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri kama vile katika maeneo ya makazi ya watu, maeneo yaliyohifadhiwa, kando kando ya mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa isipokuwa kwa ruhusa maalumu ya Halmashauri. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kujenga nyumba au jengo lolote au kufanya shughuli zozote za kiuchumi katika eneo la hifadhi. - 14 Verify source ↗
(1) Halmashauri itawajibika kusimamia na
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima isimamie na kulinda vyanzo vya maji, ichukue hatua za kisheria dhidi ya waharibifu au wanaoshindwa kushiriki uhifadhi bila sababu ya msingi, na Halmashauri pamoja na jamii husika zipande miti isiyonyonya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu. Ni marufuku kumiliki eneo la chanzo cha maji.
14.-(1) Halmashauri itawajibika kusimamia na kulinda vyanzo vya maji. (2) Halmashauri itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayeharibu chanzo cha maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji bila sababu ya msingi. (3) Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri na jamii husika kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo vya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu. (4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kumiliki eneo la chanzo cha maji. - 15 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima au
AI-assisted research summary: People may not cultivate, cut trees, graze livestock, or otherwise damage a water source within 60 metres of it. The council must plant non-water-absorbing trees at protected water sources under the Forest Officer’s directions.
15.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima au kukata miti au kuchunga mifugo katika umbali wa mita 60 kutoka chanzo cha maji au kufanya lolote linaloharibu kwa namna yoyote chanzo cha maji na hifadhi ya mazingira. jambo (2) Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo vya majivilivyo katika maeneo ya hifadhi kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu. 7 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) Uchafuzi wa vyanzo vya maji Kuchoma au kusababisha moto Kibali cha kuchoma moto Ukataji miti - 16 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuelekeza
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kuelekeza maji machafu kwenye vyanzo vya maji au kuweka vitu vyenye sumu kwenye maji yanayotumiwa na watu au viumbe hai.
16.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuelekeza mabomba ya maji machafu kwenye mito, mabwawa, ziwa, visima, mifereji, chemchemi au sehemu yoyote ambayo ni chanzo cha maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama au viumbe vingine vilivyo hai. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuweka kitu chochote chenye sumu ndani ya maji ambayo yanatumiwa na binadamu au kiumbe chochote hai. - 17 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuchoma au
AI-assisted research summary: People are prohibited from burning in ways that could cause fires in the council forests area, and residents/citizens must help extinguish fires when needed.
17.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuchoma au la iliyoko eneo kusababisha moto katika misitu Halmashauri. (2) Ni wajibu wa kila mwananchi kuzima moto ambao utaonekana kuwaka katika eneo la Halmashauri wenye viashiria vya kuleta hatari. (3) Kila mkazi wa eneo hilo atawajibika kushiriki katika zoezi la kuzima moto endapo atatakiwa kufanya hivyo na endapoatashindwa kushiriki katika zoezi la kuzima moto bila sababu ya msingi atakuwa ametenda kosa. - 18 Verify source ↗
Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto
AI-assisted research summary: Mtu aliyepewa kibali cha kuchoma moto lazima atoe taarifa ya siku mbili kabla kwa majirani na achukue hatua za kuzuia moto kusambaa.
18. Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto atalazimika kutoa taarifa ya siku mbili kabla ya kuchoma moto kwa majirani walioko katika eneo analotaka kuchoma na ataweka njia za kuzuia moto kusambaa maeneo mengine. - 19 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kukata miti bila kibali cha Halmashauri, au kuvuna miti katika msitu uliohifadhiwa kwa viumbe hai maalum. Wanaovuna miti kwa ajili ya mkaa lazima wawe na eneo maalumu lililoidhinishwa na Halmashauri.
19.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote- (a) kukata miti kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali kutoka Halmashauri; au (b) kuvuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe hai maalum ambao ni rasilimali kwa Taifa. (2) Watu wanaovuna miti kwa ajili ya kuchoma mkaa wanatakiwa kuwa na eneo maalumu lililoidhinishwa 8 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) na Halmashauri kwa ajili ya kuchoma mkaa. Wajibu wa kupanda miti Wajibu wa Halmashauri ya Kijiji - 20 Verify source ↗
Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika
AI-assisted research summary: Kila mkazi wa Halmashauri anawajibika kupanda na kutunza miti katika eneo lake, makazi yake, na mashamba anayomiliki.
20. Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika: (a) kupanda na kutunza miti katika eneo lake; (b) kupanda na kutunza miti katika makazi yake; na (c) kupanda na kutunza miti katika shamba au mashamba anayomiliki. - 21 Verify source ↗
Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kila Kijiji
AI-assisted research summary: Kila Kijiji lazima lichukue hatua za kuhifadhi miti na maeneo ya asili, kupanda miti kila mwaka, na kusimamia matumizi ya ardhi na miti.
21. Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kila Kijiji- (a) kitawajibika kutenga eneo la hifadhi ya Msitu wa asili kwa ajili ya matumizi ya baadaye; (b) kinatunza miti yote inayopandwa katika eneo la Kijiji; (c) kitasimamia kila Kaya kupanda miti katika maeneo yao kila Mwaka; (d) kinapanda na kumiliki shamba la miti lenye ukubwa wa ekari mbili kila mwaka na kulitunza; (e) kila Taasisii ndani ya Halmashauri itapaswa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka majengo yake na kuwa na shamba lisilopungua miti hekta mbili; (f) kinatunza na kuhifadhi miti na nyasi kwenye milima, makorongo na vyanzo vya maji ili kuzuia mmomonyoko wa udongo; (g) kitahakikisha kuwa kila anayeandaa shamba kwa ajili ya kilimo hatumii moto bila kibali na anapanda miti kwenye mipaka ya shamba lake kama kinga upepo; (h) kitahakikisha kuwa kila Mwenyekiti wa Kitongoji, Mtendaji wa Kijiji, Mkuu wa Taasisi yoyote Wilayani ana msitu wa hifadhi ya miti ya kupandwa au ya asili kwa madhumuni ya kuhifadhi ardhi na mazingira; (i) kitahakikisha kuwa maeneo yote ya vilima na yenye vipara ambayo yanamilikiwa na watu 9 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) Utupaji wa taka ngumu na laini Uendeshaji wa viwanda, vituo vya mafuta na huduma za ujenzi Makosa yanayohusu mifugo binafsi au Serikali ya Kijiji yanapandwa miti. - 22 Verify source ↗
(1) Ni wajibu wa Halmashauri kutenga eneo
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupa taka ngumu au laini na isimamie usafi katika eneo lake. Mtu yeyote akitupa taka ovyo au kujisaidia kwenye kingo za mabwawa au vyanzo vya maji ndani ya Halmashauri anatenda kosa.
22.-(1) Ni wajibu wa Halmashauri kutenga eneo kwa ajili ya kutupa taka ngumu au laini na kusimamia kwa karibu usafi katika eneo lake. (2) Mtu yeyote atakayetupa ovyo taka ngumu au laini, au kujisaidia katika kingo za mabwawa au kwenye vyanzo vya maji vilivyoko katika Halmashauri atakuwa ametenda kosa. - 23 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayeendesha shughuli za
AI-assisted research summary: People operating workshops, mills, wood planers, juice extractors, welding activities, factories, fuel stations, or construction service centers must follow the bylaw’s conditions and consider environmental impacts.
23.-(1) Mtu yeyote anayeendesha shughuli za karakana, mashine ya kusaga, kuranda mbao, kukamua maji ya matunda, kuchomelea vyuma au kuendesha shughuli yoyote inayozalisha uchafu ambao unaleta athari kwa binadamu na viumbe wengine hai katika maeneo ya makazi ya watu atatakiwa kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii. (2) Endapo mtu yeyote anataka kuendesha shughuli za kiwanda, kituo cha mafuta, kituo cha huduma mbalimbali za ujenzi atatakiwa kuzingatia tahadhari ya athari za mazingira. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya aya ya (1) na (2) atakuwa ametenda kosa. - 24 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anafanya kosa akileta, kusafirisha, au kulisha mifugo bila kibali katika maeneo yaliyokatazwa, au akivua samaki kwa sumu au nyavu zenye matundu madogo.
24. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa- (a) ataingiza mfugo au mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (b) atasafirisha mfugo au mifugo bila kuwa na kibali; (c) atalisha mfugo au mifugo katika maeneo yasiyoruhusiwa; (d) atavua samaki kwa kutumia sumu au nyavu zenye matundu madogo (kokoro). Makosa yanayohusu kilimo - 25 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti kuhusu
AI-assisted research summary: Anyone who violates the agricultural conditions set out in this bylaw commits an offence.
25. Mtu yeyote atakayekiuka masharti kuhusu kilimo yaliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii atakuwa 10 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) Makosa yanayohusu hifadhi ya ardhi Makosa yanayohusu vyanzo vya maji Makosa yanayohusu mazao ya misitu ametenda kosa. - 26 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti kuhusu
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayekiuka masharti ya kuhifadhi ardhi yaliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii anatenda kosa.
26. Mtu yeyote atakayekiuka masharti kuhusu kuhifadhi ardhi yaliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa. - 27 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakayeharibu chanzo cha maji
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayeharibu chanzo cha maji, kushindwa kushiriki katika kuhifadhi vyanzo vya maji, au kuweka sumu inayoathiri maisha ya binadamu na viumbe hai anatenda kosa.
27.-(1) Mtu yeyote atakayeharibu chanzo cha maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji atakuwa ametenda kosa. (2) Mtu yeyote atakayeweka sumu ya aina yoyote ambayo inaathiri maisha ya binadamu na viumbe hai atakuwa ametenda kosa. - 28 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akifanya vitendo fulani vya misitu bila kibali au kinyume cha masharti yaliyotajwa.
28. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa- (a) atachoma au kusababisha moto katika misitu bila kibali; (b) atashindwa kushiriki katika kuzima moto; (c) atavuna mazao ya misitu katika misitu iliyohifadhiwa na isiyohifadhiwa bila kibali; (d) atachoma mkaa na kukata kuni bila kibali; (e) atafyeka nyasi, kung’oa vichaka na kung’oa visiki kwenye misitu bila kibali; kwenye (f) atachunga mifugo lolote lililopandwa miti, iliyohifadhiwa kama bustani ya miti, msitu ya asili au iliyopandwa kwa ajili ya hifadhi; eneo (g) atakata miti au kuchungia mifugo kwenye miti iliyopandwa kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko wa udongo au kinga upepo; (h) atabandua magome ya miti kwa ajili ya kutengeneza vilindo, mzinga na vitu vingine bila ya kuwa na kibali; na (i) atalima au kukata miti katika vyanzo vya maji, milima, kando ya njia, makorongo na sehemu nyingine zozote zinazohifadhiwa ili kupunguza mmomonyoko wa udongo. 11 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) Makosa yanayohusu taka ngumu na laini Makosa yanayohusu taka za majimaji Adhabu Kufifilisha kosa - 29 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetupa ovyo taka ngumu au
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kutupa ovyo taka ngumu au laini katika maeneo yasiyoruhusiwa na Sheria Ndogo hii; kufanya hivyo ni kosa.
29. Mtu yeyote atakayetupa ovyo taka ngumu au laini katika maeneo yoyote yasiyoruhusiwa na Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa. - 30 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetiririsha maji machafu
AI-assisted research summary: Anyone who discharges harmful wastewater commits an offence.
30. Mtu yeyote atakayetiririsha maji machafu yanayoleta madhara kwa binadamu na viumbe hai wengine atakuwa ametenda kosa. - 31 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa na
AI-assisted research summary: Mtu yeyote akitenda kosa anaweza kupewa faini, kifungo cha hadi miezi 12 jela, au vyote pamoja.
31. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. - 32 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: The Director may compound an offence by charging the offender up to TZS 50,000, if the offender admits the offence and is willing to complete the specified form.
32. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Sheria Ndogo hii. 12 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) _______ JEDWALI _______ (Limetengenezwa chini ya aya ya 32) FOMU YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …..… ya Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. Jina……………………………….. Saini……………………… ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 13 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 907 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya Mlimba imegongwa kwenye sheria Ndogo hii kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Mlimba uliofanyika Tarehe 27 Mwezi Oktoba Mwaka 2021 na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- ENG. STEPHANO B. KALIWA Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba INNOCENT SIMON MWANGASA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 14
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in