Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023
Provision says this by-law is called the Mlimba District Council Markets and Fairs Tax By-law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Provision says this by-law is called the Mlimba District Council Markets and Fairs Tax By-law, 2023. This bylaw applies throughout the entire area of the Mlimba District Council. This section defines key terms used in the by-law on market and fair taxes. Halmashauri lazima ichukue hatua kadhaa kuhusu masoko, ikiwemo kukusanya ushuru au ada, kusimamia na kuendesha masoko, kusimamia usafi na usalama, na kusajili wafanyabiashara. Halmashauri lazima iunde Mkuu wa Soko, ambaye atasimamia uendeshaji wa soko na majukumu ya kila siku ya soko.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023
Showing 40 of 40
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Provision says this by-law is called the Mlimba District Council Markets and Fairs Tax By-law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the entire area of the Mlimba District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law on market and fair taxes.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “dalali” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa za sokoni kwa njia ya mnada kwa niaba ya mwenye bidhaa kwa mujibu wa sheria na taratibu za soko; “gulio” maana yake ni soko la wazi linalofanyika kwa wakati maalumu kwa kibali maalumu cha Halmashauri; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba; “kamati ya wadau wa soko” maana yake ni Kamati ya wafanyabiashara iliyoundwa kutokana na Wenyeviti na Makatibu wa vikundi vidogo vidogo vya 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) wafanyabiashara ndani ya soko; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa mujibu Sheria Ndogo hii; “kodi ya pango” maana yake ni kodi inayolipwa na mpangaji kwa Halmashauri kila mwezi au kila siku kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “kodi ya pango” maana yake ni kodi inayolipwa na mpangaji kwa Halmashauri kila mwezi au kila siku kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “makasha” maana yake ni vifaa maalum vya kubebea, kufungashia au kuhifadhia bidhaa au mazao na yatahusisha matenga, viroba, magunia, karatasi ngumu, masanduku ya mbao na mengine yenye asili hiyo; “meza au kizimba” maana yake ni kitu au kifaa kinachotumika kuweka bidhaa kwa ajili ya kuuza sokoni au gulioni; “mfanyabiashara” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa sokoni au gulioni kwa jumla au rejareja; “mkuu wa soko” maana yake ni mtu yeyote aliyeteuliwa au aliyeajiriwa na Halmashauri kusimamia shughuli zote katika soko; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri yeyote ya Mlimba ya kutekeleza au Afisa majukumu ya Wilaya atakayeteuliwa Mkurugenzi; "mnada” maana yake ni soko la wazi ambalo mali au vitu mbalimbali vinauzwa kwa ushindani wa bei kwa kauli na kwa kibali maalumu cha Halmashauri; “soko” maana yake ni eneo maalumu la biashara lililotengwa na Halmashauri kwa matumizi ya kuuzia au kununulia bidhaa pamoja na gulio; “ushuru” maana yake ni tozo inayolipwa baada au kabla ya kupata huduma katika soko au gulio; “vikundi” maana yake ni vikundi vya ushirika vya wafanyabiashara au umoja wa vikundi vya wafanyabiashara vilivyosajiliwa au kuandikishwa na 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) kuwasilishwa katika kamati ya soko au gulio na kwa mkuu wa soko na kutambuliwa na Halmashauri; “wadau wa soko” maana yake ni mfanyabiashara binafsi, vikundi vilivyoandikishwa katika kamati ya wadau wa soko au gulio na kuwasilishwa kwa mkuu wa soko, au vyama vya ushirika vinavyofanya shughuli za biashara katika soko; “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, shirika, taasisi au kampuni ambayo imeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri; na “mazao” maana yake ni mavuno ya shambani au maliasili yanayoingizwa kwenye soko au ndani ya eneo la mamlaka ya Halmashauri. Wajibu wa Halmashau ri - 4 Verify source ↗
Pamoja na wajibu mwingine, Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ichukue hatua kadhaa kuhusu masoko, ikiwemo kukusanya ushuru au ada, kusimamia na kuendesha masoko, kusimamia usafi na usalama, na kusajili wafanyabiashara.
4. Pamoja na wajibu mwingine, Halmashauri itakuwa na wajibu ufuatao: (a) kukusanya ushuru au ada mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wa masoko, minada na magulio; (b) kuanzisha, kusimamia na kuendesha masoko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (c) kuendeleza masoko; (d) kusimamia usafi na usalama wa masoko; (e) kusimamia ufikishaji wa huduma za kijamii katika soko; (f) kugawa na kupangisha soko kwa vyumba, meza au vizimba; (g) kutenga maeneo kwa ajili ya magulio; na (h) kusajili wafanyabiashara wote katika masoko yote ya Halmashauri. Mkuu wa Soko - 5 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mkuu wa Soko atakayeteuliwa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima iunde Mkuu wa Soko, ambaye atasimamia uendeshaji wa soko na majukumu ya kila siku ya soko.
5.-(1) Kutakuwa na Mkuu wa Soko atakayeteuliwa na Halmashauri kwa ajili ya kusimamia shughuli za uendeshaji wa soko. (2) Mkuu wa soko atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kusimamia ukusanyaji wa ushuru au ada 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) mbalimbali; (b) kusimamia usajili wa wadau wa soko kwa kushirikiana na kamati ya wadau wa soko; (c) kuimarisha huduma za ulinzi, maji na umeme katika masoko; (d) kusimamia usafi na uondoshaji wa taka katika soko; (e) kuhakikisha kuwa bidhaa haziuzwi kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kwa shughuli hiyo; (f) kuzuia ujenzi holela katika soko; na (g) kutekeleza majukumu mengine yatakayoagizwa na Halmashauri. yoyote (3) Bila kujali masharti ya aya ndogo ya (1), Halmashauri inaweza kuajiri wakala ambaye atawajibika kusimamia uendeshaji wa soko kwa niaba yake. (4) Wakala atakayeajiriwa chini ya aya ndogo ya (3) atasimamia shughuli za uendeshaji wa soko kwa kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika aya ndogo ya (1) na masharti ya mkataba wa uwakala kati yake na Halmashauri. - 6 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na kamati ya wadau wa soko
AI-assisted research summary: Market stakeholders must form a market stakeholders committee, and each cooperative group in the market must have one representative on it.
6.-(1) Kutakuwa na kamati ya wadau wa soko ambayo itaundwa na wadau wa soko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Kila kikundi cha ushirika katika soko kitakuwa na mwakilishi mmoja katika kamati ya wadau wa soko. (3) Kamati ya wadau wa soko itatakiwa kuweka utaratibu maalum wa kuwapata viongozi wake, kuwaondoa madarakani na uendeshaji wa shughuli zake na kuuwasilisha kwa Halmashauri. (4) Vikao vya Kamati ya wadau wa soko vitafanyika mara moja kila mwezi. (5) Mkuu wa Soko atakuwa Katibu katika vikao vyote vya Kamati ya wadau wa soko. (6) Muda wa wajumbe wa kamati ya wadau wa soko kuwa madarakani ni miaka mitatu. Kamati ya Soko Majukumu - 7 Verify source ↗
Kamati ya wadau wa soko itakuwa na majukumu
AI-assisted research summary: Kamati ya wadau wa soko ina majukumu ya kukagua biashara, kuboresha ustawi, kudumisha nidhamu, kuhakikisha ulipaji wa ushuru au ada, kusukuma usafi, na kuhakikisha ulinzi na usalama sokoni.
7. Kamati ya wadau wa soko itakuwa na majukumu 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) ya Kamati yafuatayo: (a) kuhakiki biashara zinazoendeshwa katika soko; (b) kuboresha ustawi wa wadau wa soko; (c) kuhakikisha uwepo wa nidhamu katika shughuli za soko; (d) kuhakikisha wadau wote wa soko na gulio wanalipa ushuru au ada kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (e) kukuza na kuendeleza mfumo wa biashara; (f) kuhakikisha kila eneo la mdau na soko kwa ujumla linakuwa safi muda wote; (g) kutekeleza kazi nyingine watakazoelekezwa na mkuu wa masoko kulingana na Sheria ndogo hii; na (h) kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo masokoni. Kamati ndogo - 8 Verify source ↗
(1) Kamati ya wadau wa soko itaunda kamati
AI-assisted research summary: Kamati ya wadau wa soko lazima itaunda kamati ndogo zenye wajumbe wanne, na inaweza pia kuunda kamati ndogo nyingine inapoona inafaa.
8.-(1) Kamati ya wadau wa soko itaunda kamati ndogo zenye wajumbe wanne kutoka miongoni mwa wajumbe wa kamati ya wadau wa soko ambazo ni: (a) Kamati Ndogo ya Miundombinu na Usafi; (b) Kamati Ndogo ya Utawala na Biashara; na (c) Kamati Ndogo ya Ulinzi na Usalama. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), kamati ya wadau wa soko inaweza kuunda kamati ndogo yoyote kwa kadri itakavyoona inafaa. Vikao vya Kamati ya wadau wa soko - 9 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na kikao cha kamati ya wadau wa
AI-assisted research summary: The market stakeholders committee must meet once every month, and its chairperson must be chosen from among the committee members.
9.-(1) Kutakuwa na kikao cha kamati ya wadau wa soko kitakachofanyika mara moja kila mwezi ambapo Mwenyekiti atachaguliwa miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo. (2) Kamati ya wadau inaweza kukutana kwa jinsi itakavyoona inafaa nje ya kikao cha kisheria kwa ajili ya kutekeleza maazimio yaliyoainishwa katika kikao cha kamati ya wadau wa soko. Ushuru wa kupakua na - 10 Verify source ↗
Kutakuwa na ushuru utakaotozwa kwa kila
AI-assisted research summary: Ushuru unatozwa kwa kila chombo cha usafiri kinachoingia eneo la soko au barabara za soko ili kupakua au kupakia bidhaa.
10. Kutakuwa na ushuru utakaotozwa kwa kila 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) kupakia mizigo Usajili wa wadau Utolewaji wa kibali kwa biashara ambazo hazikuwep o Uteuzi wa wakala chombo cha usafiri kitakachoingia ndani ya eneo la soko au barabara za soko kwa ajili ya kupakua au kupakia bidhaa kwa kuzingatia viwango viilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. - 11 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekusudia kufanya biashara
AI-assisted research summary: Anyone who intends to do business in the market area must be registered by the Market Master working with the market stakeholders committee.
11. Mtu yeyote anayekusudia kufanya biashara katika eneo la soko atatakiwa kusajiliwa na Mkuu wa Soko akishirikiana na kamati ya wadau wa soko kwa lengo la kumtambua na kumworodhesha katika rejesta ya wadau wa soko. - 12 Verify source ↗
Mtu au mfanyabiashara yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu au mfanyabiashara anayetaka kuanza biashara mpya au biashara isiyo na eneo sokoni lazima aombe kibali kwa Halmashauri na azingatie masharti ya aya ya 11.
12. Mtu au mfanyabiashara yeyote ambaye anakusudia kufanya biashara ambayo awali haikuwepo au haikuwa na eneo ndani ya soko ataomba kibali kwa Halmashauri na atapaswa kuzingatia masharti ya aya ya 11. - 13 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kumteua mtu yeyote au
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumteua wakala kukusanya ushuru, na wakala huyo lazima akusanye, apokee, na awasilishe makusanyo kwa masharti yaliyotajwa.
13.-(1) Halmashauri inaweza kumteua mtu yeyote au kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria kuwa wakala ambaye atawajibika kukusanye ushuru kwa niaba ya Halmashauri. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa aya ndogo ya (1) atakuwa na wajibu ufuatao: (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. Kufuta kibali - 14 Verify source ↗
(1) Mkuu wa soko anaweza kufuta kibali
AI-assisted research summary: Mkuu wa soko anaweza kufuta kibali baada ya kutoa notisi ya siku 30 ikiwa mwenye kibali ana hali fulani za uvunjaji au matumizi mabaya; mfanyabiashara anaweza kupinga uamuzi huo kwa Mkurugenzi ndani ya siku 14, na Mkurugenzi lazima ajibu ndani ya siku 7.
14.-(1) Mkuu wa soko anaweza kufuta kibali kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hii, baada ya kutoa notisi ya siku thelathini, endapo mwenye kibali hicho- (a) atakuwa na malimbikizo ya ushuru; (b) atakuwa amesimamisha shughuli zake kwa miezi 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) mitatu bila taarifa; (c) atakuwa na mwenendo unaokiuka masharti ya Sheria Ndogo hii; (d) atawashawishi wengine kutofuata Sheria Ndogo hii au kusababisha uvunjaji wa amani; au wafanyabiashara (e) atatumia chumba, kibanda, meza au kizimba alichopanga kinyume na madhumuni ya kufanyia biashara kama yalivyoainishwa kwenye mkataba wa upangishaji au maelekezo yatakayotolewa na Halmashauri. (2) Mfanyabiashara ambaye hataridhika na uamuzi wa kufutiwa kibali anaweza kuwasilisha pingamizi lake kwa Mkurugenzi katika kipindi cha siku kumi na nne tangu tarehe ya kufutiwa kibali. (3) Baada ya kupokea pingamizi, Mkurugenzi atatakiwa kutoa uamuzi wa pingamizi ndani ya siku saba tangu tarehe ya kupokea pingamizi husika. Wajibu wa mfanyabish ara - 15 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara katika eneo
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wote katika eneo la soko lazima wajisajili, walinde usafi na miundombinu, walipe ushuru kwa wakati, na wafuate masharti ya soko; pia kuna marufuku juu ya matangazo bila idhini, lugha chafu, siasa, taka, moto, na bendera za vyama.
15. Kila mfanyabiashara katika eneo la soko atakuwa na wajibu ufuatao: (a) kusajiliwa na Mkuu wa soko katika rejesta ya wadau wa soko; (b) kulinda na kuhifadhi miundombinu ya soko; (c) kufanya biashara katika maeneo yanayoruhusiwa; (d) kufanya usafi katika eneo lake la biashara; (e) kulipa ushuru kwa wakati; (f) kutobandika au kutobandua tangazo bila idhini ya Mkuu wa soko; (g) kutotumia lugha ya matusi, kuudhi au kashfa katika eneo la soko; (h) kushiriki usafi wa jumla wa soko; (i) kutoweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la soko; (j) kutofanya shughuli za kisiasa katika eneo la soko; 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) Ujenzi na ukarabati Muda wa biashara Kodi ya upangishw aji (k) kutotupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; (l) kutowasha moto maeneo yasiyohusika ndani ya soko; na (m) kuheshimu masharti ya upangaji aliyopewa na Halmashauri na maelekezo atakayopewa na Halmashauri, Mkuu wa soko na kamati ya wadau wa soko. - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya ujenzi,
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kujenga, kukarabati au kufanya marekebisho ya chumba, kibanda, meza au kizimba bila idhini ya maandishi ya Halmashauri.
16. Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya ujenzi, ukarabati au marekebisho ya chumba, kibanda, meza au kizimba pasipo idhini ya maandishi ya Halmashauri. - 17 Verify source ↗
(1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa
AI-assisted research summary: The market must stay open every day from 6:00 a.m. to 6:00 p.m. The market manager may close it for maintenance or an emergency, after consulting the Director.
17.-(1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. (2) Mkuu wa Soko, kwa kushauriana na Mkurugenzi, anaweza kufunga soko kwa ajili ya matengenezo au sababu nyingine yoyote ya dharura pale itakapoonekana inafaa. (3) Isipokuwa kwa sababu nyingine za dharura, Mkuu wa soko hatakuwa na mamlaka ya kufunga soko kwa sababu za matengenezo isipokuwa tu baada ya kutoa notisi ya siku saba kwa wadau wa soko kuhusu kusudio la kufunga soko kwa ajili ya matengenezo. - 18 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabishara katika soko atalipa kodi
AI-assisted research summary: Market traders must pay stall or kiosk rental tax under the rental agreement, and payment goes to the council or its agent at rates set in the Second Schedule.
18.-(1) Kila mfanyabishara katika soko atalipa kodi ya upangishwaji kizimba au kibanda kwa mujibu wa mkataba wa upangishwaji. (2) Kodi ya upangishwaji italipwa kwa Halmashauri au wakala kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. (3) Halmashauri inaweza, kwa makubaliano maalum, kumruhusu mtu yeyote kujenga banda la biashara katika eneo la soko. Usimamizi wa magari
Part
Jedwali la Pili.
- 19 Verify source ↗
(1) Magari yote yanayotumika kusafirisha mazao
AI-assisted research summary: Vehicles carrying produce or goods for the market must unload in designated areas, and the market master can control how many vehicles are allowed to unload at the market.
19.-(1) Magari yote yanayotumika kusafirisha mazao au bidhaa kwa ajili ya soko yatashusha bidhaa katika maeneo yaliyoainishwa kwa shughuli hiyo. 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) (2) Mkuu wa soko atakuwa na mamlaka ya kupanga na kusimamia idadi ya magari yatakayoruhusiwa kushusha bidhaa au mazao sokoni. lolote (3) Gari sehemu iliyotengwa endapo itabidi kufanya hivyo na Mkuu wa soko. litaondolewa kutoka Kibali cha minada na magulio Usafi wa soko - 20 Verify source ↗
(1) Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine
AI-assisted research summary: Certain market trading is allowed only with a special permit from the Council, and the Council may issue special permits for magulio in designated areas.
20.-(1) Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyingine itaruhusiwa kufanyika kwenye masoko kwa kibali maalum cha Halmashauri. (2) Halmashauri inaweza kutoa kibali maalum cha kufanyika kwa magulio katika maeneo yatakayotengwa na Halmashauri na kitakuwa kama kinavyoonekana kwenye Jedwali la Tatu.
Part
Jedwali la Tatu.
- 21 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabiashara anayefanya biashara
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wa sokoni lazima waweke maeneo yao safi wakati wote, na waheshimu kanuni za afya. Mkuu wa soko, pamoja na kamati ya wadau wa soko, husimamia usafi wa jumla wa soko kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
21.-(1) Kila mfanyabiashara anayefanya biashara katika eneo la soko atawajibika kuweka eneo lake katika hali ya usafi wakati wote. (2) Mkuu wa soko kwa kushirikiana na kamati ya wadau wa soko atasimamia usafi wa jumla wa soko siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi. (3) Kila mfanyabiashara atatakiwa kuzingatia kanuni za afya. Uingizaji wa bidhaa sokoni au gulioni - 22 Verify source ↗
(1) Bidhaa zote zitakazoingizwa katika soko au
AI-assisted research summary: Goods brought into the market or auction must be kept in special carrying containers, and damaged goods must not be brought into the market or auction.
22.-(1) Bidhaa zote zitakazoingizwa katika soko au gulio zitatakiwa kuhifadhiwa kwenye makasha maalumu ya kusafirishia bidhaa. (2) Ni marufuku kwa mkulima, mfanyabiashara, dalali au mtu mwingine yeyote kuingiza sokoni au gulioni bidhaa zilizoharibika. (3) Mtu yeyote atakayeingiza sokoni bidhaa zilizofungwa kwa majani atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Mifugo kutoingizw a sokoni - 23 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kuingiza mifugo
AI-assisted research summary: Hakuna mtu anayeruhusiwa kuingiza mifugo ndani ya soko, magulio au minada isipokuwa eneo maalum lililotengwa na Halmashauri kwa biashara ya mifugo.
23. Mtu yeyote hataruhusiwa kuingiza mifugo sehemu yoyote ndani ya soko, magulio au minada isipokuwa sehemu maalum iliyotengwa na Halmashauri 9 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) kwa ajili ya biashara ya mifugo. Minada Biashara ya kutembeza Tahadhari ya moto Uuzaji wa pombe Marufuku Makosa na adhabu
Part
sehemu yoyote ndani ya soko, magulio au minada
- 24 Verify source ↗
(1) Mazao yatakayoletwa sokoni kwa ajili ya
AI-assisted research summary: Mazao yanayoletwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa kwa mnada yanapokelewa na dalali aliyechaguliwa na wafanyabiashara kwa makubaliano ya kamati ya soko, kisha dalali huyo anauza mazao hayo kwa mnada katika eneo lililotengwa na Halmashauri.
24.-(1) Mazao yatakayoletwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa kwa mnada yatapokelewa na dalali atakayeteuliwa na wafanyabiashara na kukubaliana na kamati ya soko. (2) Dalali aliyeteuliwa atauza mazao hayo kwa mnada katika eneo lililotengwa na Halmashauri kwa shughuli hiyo. - 25 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kutembeza bidhaa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kutembeza bidhaa ndani ya soko bila kibali cha Halmashauri.
25. Mtu yeyote hataruhusiwa kutembeza bidhaa ndani ya soko bila kibali cha Halmashauri. - 26 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya shughuli
AI-assisted research summary: Anyone may not carry out any activity involving fire unless the Council gives written permission.
26. Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya shughuli yoyote inayohusisha matumizi ya moto isipokuwa kwa idhini ya maandishi ya Halmashauri. - 27 Verify source ↗
Mfanyabiashara yeyote hataruhusiwa kuuza
AI-assisted research summary: Mfanyabiashara yeyote haruhusiwi kuuza pombe ndani ya soko, gulio, au mnada bila kibali na leseni ya vileo kutoka Halmashauri.
27. Mfanyabiashara yeyote hataruhusiwa kuuza pombe ndani ya soko, gulio, mnada bila kibali na leseni ya vileo iliyotolewa na Halmashauri. - 28 Verify source ↗
Ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kufanya vitendo kadhaa ndani ya soko, ikiwemo kubandika au kubandua matangazo bila idhini ya Mkuu wa Soko.
28. Ni marufuku kwa mtu yeyote: (a) kubandika au kubandua tangazo lolote bila ya idhini ya Mkuu wa Soko; (b) kuweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la soko; (c) kufanya shughuli za siasa ndani ya soko; (d) kuharibu miundombinu ya soko; (e) kutumia lugha ya matusi ndani ya soko; (f) kufanya shughuli yeyote kwenye eneo ambalo haliruhusiwi au halijatengwa kwa shughuli hiyo; (g) kutupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; (h) kuwasha moto maeneo yasiyohusika ndani ya soko; na (i) kufunga chumba cha biashara kwa madai ya kukitumia kama stoo au matumizi mengine yasiyoainishwa katika mkataba au leseni; - 29 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka au kwenda kinyume na
AI-assisted research summary: Anyone who violates or acts contrary to any provision of this by-law commits an offence and may be fined, imprisoned, or both.
29. Mtu yeyote atakayekiuka au kwenda kinyume na 10 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) kifungu chochote cha Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi laki mbili na isiyozidi Shilingi Milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote kwa pamoja. Kufifilisha Kosa - 30 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mkosaji kiasi kisichozidi shilingi laki mbili ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari, anajaza fomu maalum ya Jedwali la Nne, na yuko tayari kutimiza wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii.
30. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Nne la Sheria Ndogo hii na kuwa tayari kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. ________________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 10) A: USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO SOKONI Nam ba Aina ya chombo cha usafiri Ada kwa siku (Shilingi) 1 Chombo cha usafiri chenye uwezo wa kubeba - kilogram 500 2 Chombo cha usafiri chenye uwezo wa kubeba Tani 1 3 Chombo cha usafiri chenye uwezo wa kubeba Tani - 5000
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1
AI-assisted research summary: The text lists market parking fees by vehicle capacity and gives daily charges in Tanzanian shillings.
1.5 4 Chombo cha usafiri chenye uwezo wa kubeba Tani 2 5 Chombo cha usafiri chenye uwezo wa kubeba Tani 3 6 Chombo cha usafiri chenye uwezo wa kubeba Tani 4 7 Chombo cha usafiri chenye uwezo wa kubeba Tani 5 8 Chombo cha usafiri chenye uwezo wa kubeba Tani 7 9 Chombo cha usafiri chenye uwezo wa kubeba Tani 8 hadi 10 Chombo cha usafiri chenye uwezo wa kubeba Zaidi ya tani 10 1 0 10,000 12,000 15,000 16,000 18,000 20,000 25,000 11 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) B: USHURU WA MAEGESHO SOKONI Namba Aina ya Chombo cha Usafiri Kiwango cha Ushuru kwa siku (shilingi) 1 - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: This provision lists fee amounts for different vehicle types and for different kinds of market premises or businesses.
4. Lori kubwa lenye uwezo wa kubeba tani 5 na kuendelea Lori la kati lenye uwezo wa kubeba tani 5 Gari dogo Pikipiki 1,000/= 600/= 500/= 500/= __________ JEDWALI LA PILI ___________ ( Limetengenezwa chini ya aya ya 18(2)) ADA YA KUPANGISHA ENEO Namb a 1 2 3 4 5 6 Aina ya eneo au chanzo Ada kwa mwezi (Shilingi) Kizimba Banda vya kuku Mama au Baba lishe Vioski au mabanda ya Mitumba na Bucha Duka Stoo 10,000 10,000 10,000 30,000 50,000 150,000 JEDWALI LA TATU (Limetengenezwa chini ya aya ya 20(1)) KIBALI CHA KUTUMIA SOKO
Part
JEDWALI LA TATU
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This is a form field for the applicant’s name.
1. Jina la Mwombaji ………………………………………………………… - 2 Verify source ↗
Anuani ya mwombaji ………………………………………………………
AI-assisted research summary: Section heading: applicant’s address.
2. Anuani ya mwombaji ……………………………………………………… - 3 Verify source ↗
Kibali cha ……………………………………………………………………
AI-assisted research summary: 3. Kibali cha …………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………
3. Kibali cha …………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………… - 4 Verify source ↗
Eneo ambalo kibali hicho kitatumika ………………………………………
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaonyesha eneo ambalo kibali hicho kitakuwa na matumizi.
4. Eneo ambalo kibali hicho kitatumika ……………………………………….. ……………………………………………………………………………… - 5 Verify source ↗
Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe……………………hadi tarehe…………
AI-assisted research summary: The permit period starts on one date and ends on another date, but the dates are left blank here.
5. Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe……………………hadi tarehe………… - 6 Verify source ↗
Masharti ya kutumia kibali hicho……………………………………………
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaonyesha masharti ya kutumia kibali hicho, lakini maandishi yaliyoonekana yanaorodhesha tu vipengele (a) hadi (e) bila maelezo ya masharti yenyewe.
6. Masharti ya kutumia kibali hicho…………………………………………….. a) ……………………………………………… b) ……………………………………………… 12 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) c) ……………………………………………… d) ……………………………………………… e) ……………………………………………… - 7 Verify source ↗
Tarehe ya kikao iliyoidhinisha kibali…………………………………………
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaonyesha tarehe ya kikao kilichoidhinisha kibali.
7. Tarehe ya kikao iliyoidhinisha kibali………………………………………… Muhtasari Na.…………… - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: This is a form for admitting an offense under the market and fair fees bylaw and stating readiness to pay the fee or levy owed plus any fine.
8. Imesajiliwa na: Jina ……………………………………… Saini…………………………………….. ……………………………… Mkuu wa Soko Saini ya Mwombaji Tarehe …………………………………. Tarehe …………………… Mhuri…………………………………… ___________ JEDWALI LA TATU ___________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 30) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi………………………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya………………………………………..……. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, kwamba mnamo tarehe: …… ya Mwezi:….…. Mwaka: …….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ….. ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlim ba ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe:…....... ya Mwezi:………… Mwaka:………….. Jina:…………………………………..……………………. Saini:…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jina: …………………………….………..…………………… Cheo: …………………………………………………..……. Saini: ………………………………………………………… Tarehe: ………………………………………………………. 13 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 908 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya Mlimba imegongwa kwenye sheria Ndogo hii kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Mlimba uliofanyika Tarehe 27 Mwezi Oktoba Mwaka 2021 na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- ENG. STEPHANO B. KALIWA Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba INNOCENT SIMON MWANGASA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 14
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in