Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba
This provision gives the short title of the by-law: the Mlimba District Council Building Minerals Fees and Levies By-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the by-law: the Mlimba District Council Building Minerals Fees and Levies By-law. This by-law applies throughout the area of Mlimba District Council. This section defines key terms used in the by-law, including fees, authorized officers, the council, permits, building minerals, the director, levy, and agents. An applicant for a construction-mining permit in the council area must file the application with the Director and include the listed supporting documents; the Director must inspect the site within seven days and then approve or reject the application, giving reasons for any rejection. Holders of a construction-mining permit must pay a permit fee of TZS 300,000 and comply with the bylaw, the permit conditions, and any fee or levy charged by the Council under the bylaw.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba
Showing 17 of 17
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the by-law: the Mlimba District Council Building Minerals Fees and Levies By-law.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the area of Mlimba District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including fees, authorized officers, the council, permits, building minerals, the director, levy, and agents.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya vibali au leseni mbalimbali zitolewazo na Halmashauri; “afisa mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi lengo inayotolewa na Halmashauri; “madini ya ujenzi” maana yake ni tarazo, moramu, udongo, kifusi, kokoto, mawe, mchanga, 1 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 909 (Linaendelea)) Maombi ya kibali chokaa na madini mengine yanayotumika katika ujenzi; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; shughuli “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa huduma mbalimbali au zinazotolewa katika eneo la Halmashauri; na “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi, kampuni au asasi na Halmashauri kukusanya ushuru au ada kwa niaba ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. - 4 Verify source ↗
(1) Mtu anayekusudia kuanzisha machimbo ya
AI-assisted research summary: An applicant for a construction-mining permit in the council area must file the application with the Director and include the listed supporting documents; the Director must inspect the site within seven days and then approve or reject the application, giving reasons for any rejection.
4.-(1) Mtu anayekusudia kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuwasilisha kwa Mkurugenzi maombi ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Maombi ya kibali yatatakiwa kuambatishwa na taarifa zifuatazo: (a) leseni ya uchimbaji wa madini iliyotolewa na Mamlaka husika; (b) aina ya madini yanayokusudiwa kuchimbwa; (c) umiliki pamoja na ukubwa wa eneo linalokusudiwa kuchimbwa madini ya ujenzi; (d) mpango wa utunzaji wa mazingira katika eneo la machimbo; na (e) muhtasari wa Mkutano wa Kijiji ambacho uchimbaji wa madini ya ujenzi utafanyika ukionesha kukubaliana na uchimbaji huo. (3) Ndani ya muda wa siku saba tangu kupokea maombi, Mkurugenzi atatakiwa kukagua eneo ambalo uchimbaji wa madini ya ujenzi unakusudiwa kufanyika ili kujiridhisha iwapo eneo hilo linafaa kwa shughuli za 2 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 909 (Linaendelea)) uchimbaji. (4) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa eneo linaloombewa kibali, Mkurugenzi atatakiwa kukubali au kukataa maombi na endapo atakataa atatoa sababu za kukataliwa kwa maombi hayo. Wajibu wa mpewa kibali - 5 Verify source ↗
Mtu yeyote aliyepewa kibali cha uchimbaji wa
AI-assisted research summary: Holders of a construction-mining permit must pay a permit fee of TZS 300,000 and comply with the bylaw, the permit conditions, and any fee or levy charged by the Council under the bylaw.
5. Mtu yeyote aliyepewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi atatakiwa: (a) kulipa ada ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi ya kiasi cha shilingi laki tatu; (b) kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii na masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi; na (c) kulipa ada au ushuru utakaotozwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. - 6 Verify source ↗
(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi
AI-assisted research summary: Mining, selling, and buying construction minerals in the Council area must occur only during the stated daily hours, unless the Director gives a special permit. Vehicle owners transporting construction minerals must keep the vehicle covered throughout transport.
6.-(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri zitafanyika kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kila siku. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), Mkurugenzi anaweza kutoa kibali maalumu kuruhusu shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi kufanyika nje ya muda ulioainishwa. (3) Kila mmiliki wa gari linalosafirisha madini ya ujenzi atatakiwa kuhakikisha kuwa gari hilo limefunikwa wakati wote wa usafirishaji wa madini ya ujenzi. - 7 Verify source ↗
Bila kuathiri masharti yaliyowekwa na Sheria
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye maeneo ya uchimbaji wa madini ya ujenzi kati ya saa 12 asubuhi na saa 12 jioni kwa ajili ya ukaguzi na ushauri.
7. Bila kuathiri masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hii, Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo lolote yanapochimbwa madini ya ujenzi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kwa nia ya kufanya ukaguzi na kutoa ushauri wa uendeshaji wa shughuli za uchimbaji. 3 Muda wa uchimbaji na masharti ya usafirishaji Mamlaka ya afisa mwidhiniwa Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 909 (Linaendelea)) Ushuru wa madini ya ujenzi Vituo vya ukaguzi Utoaji wa stakabadhi za malipo - 8 Verify source ↗
(1) Kila mnunuzi au msafirishaji wa madini ya
AI-assisted research summary: Wachuuzi na wasafirishaji wa madini ya ujenzi lazima walipie ushuru kwa viwango vya Jedwali la Pili.
8.-(1) Kila mnunuzi au msafirishaji wa madini ya ujenzi atatakiwa kulipia ushuru wa madini ya ujenzi kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. (2) Ushuru wa madini ya ujenzi utatozwa katika eneo la machimbo, barabara zinazoelekea au kutoka maeneo ya machimbo au eneo lolote lililo chini ya mamlaka ya Halmashauri. (3) Mnunuzi yeyote atakayeshindwa kulipa ushuru anaotakiwa kulipa atatakiwa kupakua madini ya ujenzi kutoka katika chombo au kutochukua madini hayo mpaka hapo atakapolipa ushuru anaodaiwa. - 9 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo
AI-assisted research summary: Vehicles carrying construction minerals must stop at a checkpoint and show an electronic receipt proving the tax has been paid. If a seized vehicle’s driver or owner flees, the vehicle cannot leave until the fines and taxes due are paid.
9.-(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo ya ushuru wa madini ya ujenzi katika njia zinazoingia au kutoka katika maeneo ya machimbo. (2) Kila dereva wa chombo cha usafiri kilichobeba madini ya ujenzi atatakiwa kusimama katika kituo cha ukaguzi na kuonesha stakabadhi ya kielektroniki ili kuthibitisha kulipwa kwa ushuru wa madini ya ujenzi yaliyo katika chombo cha usafiri. (3) Chombo cha usafiri kitakachokamatwa kwenye eneo la machimbo na dereva au mmiliki wake akakimbia au kutoroka, chombo hicho hakitaruhusiwa kutoka mpaka kitakapolipiwa faini na ushuru unaodaiwa. - 10 Verify source ↗
(1) Ada au ushuru utakaotozwa kwa mujibu
AI-assisted research summary: Ada au ushuru uliotozwa chini ya sheria ndogo hii hulipwa kwa Halmashauri au wakala, na malipo lazima yathibitishwe kwa stakabadhi ya kielektroniki.
10.-(1) Ada au ushuru utakaotozwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii utalipwa kwa Halmashauri au wakala ambaye atatoa stakabadhi ya kielektroniki kama kielelezo cha malipo yaliyofanyika. (2) Utakuwa ni wajibu wa kila mlipa ada au ushuru kudai na kuhakiki stakabadhi ya malipo kulingana na kiasi cha fedha alicholipa. (3) Utakuwa sio utetezi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, mtu kudai kuwa amelipa ada au ushuru lakini hakupewa stakabadhi ya kielektroniki. 4 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 909 (Linaendelea)) Kufutwa au kusimamishwa kwa kibali inaweza - 11 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kufuta au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi ikiwa kuna ukiukwaji wa masharti, lakini lazima itoe notisi ya siku saba na kueleza sababu kabla ya kufanya hivyo.
11.-(1) Halmashauri au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi endapo itajiridhisha kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Sheria Ndogo hii au masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi. kufuta (2) Kwa kuzingatia masharti ya aya ndogo ya (1), kabla ya kufuta au kusimamisha kibali, Halmashauri itatakiwa kutoa notisi ya siku saba ya kusudio la kufuta au kusimamisha kibali kwa mtu yeyote aliyepewa kibali cha uchimbaji. (3) Notisi itakayotolewa kwa mujibu wa aya ndogo ya (2) itaainisha sababu za kufuta au kusimamisha kibali husika. (4) Endapo kibali kitafutwa au kusimamishwa, mtu yeyote aliyepewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi atasimama kuchimba madini hayo. Uteuzi wa wakala - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake, na wakala huyo lazima akusanye na kuwasilisha makusanyo kwa mujibu wa masharti ya Sheria Ndogo na mkataba wa uwakala.
12.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kwa ajili ya kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa aya ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa: (a) kukusanya na kupokea ada au ushuru kwa niaba eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; ya Halmashauri katika (b) kukusanya ada au ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroni na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashuri. Halmashauri kutowajibika kwa hasara - 13 Verify source ↗
Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote
AI-assisted research summary: Halmashauri haitawajibika kwa hasara ya mnunuzi au msafirishaji wa madini ya ujenzi wakati wa kukusanya ushuru, isipokuwa hasara hiyo imesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri au wakala.
13. Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote atakayopata mnunuzi au msafirishaji wa madini ya ujenzi wakati wa kukusanya ushuru isipokuwa kama hasara 5 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 909 (Linaendelea)) itasababishwa na uzembe wa watumishi wa hiyo Halmashauri au wakala. Makosa - 14 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Anyone commits an offence if they do any of the listed acts about construction minerals, permits, tax payment, transport, mining location, inspection orders, or rehabilitation.
14. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) ataanzisha machimbo ya madini ya ujenzi bila kuwa na kibali kilichotolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) atasafirisha madini ya ujenzi bila kulipa ushuru; (c) atachimba madini ya ujenzi kabla au baada ya muda ulioruhusiwa kuchimba; (d) atasafirisha madini ya ujenzi katika gari ambalo halijafunikwa; (e) atamshawishi mtu au kundi la watu kutolipa ushuru; (f) atakataa kutii agizo lolote atakalopewa na afisa mwidhiniwa wakati wa utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (g) atakataa kulipa ushuru au kumzuia afisa mwidhiniwa au wakala kutekeleza wajibu wake; (h) atakwepa kulipa ushuru kwa kupita njia tofauti na kituo cha ukaguzi; (i) atachimba madini katika maeneo yasiyoidhinishwa; (j) atachimba shimo kubwa kwa ajili ya madini na kuliacha bila kupanda miti au mimea mara baada ya madini hayo kumalizika; au (k) atachimba madini bila kuwa na kibali cha uchimbaji. Adhabu - 15 Verify source ↗
Mtu atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: A person who violates this by-law commits an offence and may be fined or imprisoned, or both.
15. Mtu atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi 6 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 909 (Linaendelea)) Kufifilisha Kosa kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. - 16 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtenda kosa hadi shilingi 200,000 ikiwa anakiri kwa hiari, yuko tayari kujaza fomu maalumu, na analipa ada au ushuru unaodaiwa.
16. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. _______________ JEDWALI LA KWANZA ___________________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 4(1)) KIBALI CHA UCHIMBAJI WA MADINI YA UJENZI Kibali hiki kimetolewa kwa Bw/Bi: ……………………………………………….……wa S.L.P………………, Mlimba. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ameridhia Ndugu mtajwa hapo juu, aendeshe shughuli za kuchimba madini ya ujenzi katika eneo la …………………………Kijiji cha………………………. kata ya …………………………… baada ya kufanya ukaguzi katika eneo husika ili kutathimini athari za mazingira. Kutokana na uzingatiaji wa athari za Mazingira mchimbaji anaruhusiwa kuchimba madini ya ujenzi katika eneo hilo kwa muda wa miezi kumi na mbili tu. Mwombaji analazimika kuomba tena kibali baada ya muda huo kuisha na ukaguzi utafanyika tena. TAMKO LA MWOMBAJI: MIMI…………………………………………………………nipo tayari kufuata masharti ya kibali hiki cha Uchimbaji wa Madini ya Ujenzi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kwa lengo la kutunza na kuhifadhi mazingira. Nathibitisha kwa hiari yangu nimeelewa vema masharti ya kibali hiki. Jina: ……………………………………… Saini ………………….. Tarehe ………………… KWA MATUMIZI YA OFISITU: Mwombaji amelipia Shilingi ……………. tarehe……….mwezi………….Mwaka………….. (Ambatanisha stakabadhi ya malipo na fomu hii) 7 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 909 (Linaendelea)) Jina la Afisa aliyetoa kibali……………………… Saini …………… Tarehe ………………. Muhuri: ……………………………………………. ___________ JEDWALI LA PILI ____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 8(1)) USHURU WA MADINI YA UJENZI Namba Aina ya Madini Ujazo au Tani Kiwango cha Ushuru (Shilingi)
Part
JEDWALI LA PILI
- 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: This section shows fee amounts for certain construction materials and provides a form for admitting an offence and agreeing to pay the amount owed plus a fine.
5. Mawe Moramu Mchanga Kokoto Tani 3 –Tani 7 3,000/= kwa tripu Tani 3 –Tani 7 2,000/= kwa tripu Tani 3 –Tani 7 2,000/= kwa tripu Tani 3 –Tani 7 5,000/= kwa tripu Mawe au Moramu au Zaidi ya Tani 7 3% ya Bei ya Madini husika Mchanga au Kokoto __________ JEDWALI LA TATU __________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 16) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi; ……………………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya; ………………………………………..……. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka; …….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya…….. ya Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. 8 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 909 (Linaendelea)) NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe;…....... ya Mwezi;………… Mwaka;………….. Jina;…………………………………..……………………. Saini;…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jina;…………………………….………..…………………… Wadhifa;…………………………………………………..… Saini;………………………………………………………… Tarehe;………………………………………………………. 9 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Tangazo La Serikali Na. 909 (Linaendelea)) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya Mlimba imegongwa kwenye sheria Ndogo hii kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Mlimba uliofanyika Tarehe 27 Mwezi Oktoba Mwaka 2021 na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- ENG. STEPHANO B. KALIWA Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba INNOCENT SIMON MWANGASA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 10
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in