Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2023
This section states the short title of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the short title of the by-law. This by-law applies throughout the entire area of Korogwe District Council. Kifungu hiki kinafafanua istilahi zinazotumika kwenye Sheria Ndogo hii. Halmashauri lazima itozeshe na kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kutoka kwa kila mmiliki kwa kiwango cha asilimia 10 ya mapato ya mwezi husika. Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni anatakiwa kulipa ushuru kwa Halmashauri kwa wakati, kuzingatia usafi, kuweka na kutumia rejista ya wageni, kutoa stakabadhi ya kieletroniki, kulipa ada ya leseni kwa muda, kuonyesha nyaraka wakati wa ukaguzi, kusajili wageni, na kuhakikisha kitanda hakitumiwi na wageni wawili au zaidi wa jinsia moja.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2023
Showing 15 of 15
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section states the short title of the by-law.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Korogwe District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinafafanua istilahi zinazotumika kwenye Sheria Ndogo hii.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “daftari la wageni” maana yake ni kitabu Maalumu kilichoandaliwa na Mmiliki au kilicho nunuliwa kwa lengo la kusajili na kutunza kumbukumbu za wageni wanaolala kwenye nyumba ya kulala wageni; “gharama ya malazi” maana yake ni kiasi cha fedha kinachotozwa na mmiliki wa nyumba ya kulala wageni kwa mtu ambaye anapata huduma ya malazi; 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 915 (Linaendelea) “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe; “hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho wa mwezi zinazowasilishwa na mmiliki wa nyumba ya kulala wageni baada ya kipindi cha hesabu pamoja na nyaraka au maelezo yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheriahii; “kipindi cha hesabu” maana yake ni muda ambao mmiliki wa nyumba ya kulala wageni anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara yake; “marejesho” maana yake ni taarifa inayotaja jina la nyumba ya kulala wageni, aina ya vyumba, gharama ya kila aina ya chumba, jumla ya vyumba vilivyopangishwa ikiwa ni pamoja na ushuru unaopaswa kulipwa kwa mwezi husika. “mgeni” maana yake ni mtu yeyote ambaye hulipa pango la kukaa kwenye chumba cha kulala wageni aidha kwa siku nzima au sehemu ya siku nzima; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza kazi za Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “mkusanya ushuru” maana yake ni afisa yeyote wa Halmashauri au Wakala ambaye ameteuliwa na Halmashauri kufanya kazi ya kukusanya ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “mlipa ushuru” maana yake ni mtu binafsi au kampuni inayomiliki nyumba ya kulala wageni inayopaswa kuwa na leseni ya kufanya biashara ya kutoa huduma ya malazi katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe; “mmiliki” maana yake ni mtu yeyote aliyepewa jukumu la kusimamia nyumba ya kulala wageni au hoteli au 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 915 (Linaendelea) mwajiriwa au mtu yeyote anayehusika kukusanya gharama za pango toka kwa mgeni kutokana na kulala kwenye nyumba ya kulala wageni; Sura ya 65 Kiwango cha ushuru Wajibu wa mmiliki wa nyumba ya kulala wageni “nyumba ya kulala wageni” maana yake ni jengo lililojengwa kwa ajili ya kuwapokea wasafiri au wageni kwa lengo ya kupata kipato au faida isipokuwa, mabweni, jengo la kupumzikia viongozi wa Serikali na jengo lililosajiliwa chini ya Sheria ya Utalii kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii; “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba yake. shirika ambalo - 4 Verify source ↗
Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itozeshe na kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kutoka kwa kila mmiliki kwa kiwango cha asilimia 10 ya mapato ya mwezi husika.
4. Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kutoka kwa kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni kwa kiwango cha asilimia kumi ya mapato ya nyumba ya kulala wageni kwa mwezi husika. - 5 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni anatakiwa kulipa ushuru kwa Halmashauri kwa wakati, kuzingatia usafi, kuweka na kutumia rejista ya wageni, kutoa stakabadhi ya kieletroniki, kulipa ada ya leseni kwa muda, kuonyesha nyaraka wakati wa ukaguzi, kusajili wageni, na kuhakikisha kitanda hakitumiwi na wageni wawili au zaidi wa jinsia moja.
5. Kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni anatakiwa kuhakikisha kuwa: (a) analipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa Halmashauri kila ifikapo tarehe moja na si zaidi ya tarehe tano ya kila mwezi; (b) nyumba ya kulala wageni inakuwa safi muda wote na masharti mengine ya usafi yanafuatwa; (c) ana kitabu alichopata kutoka Halmashauri kwa ajili ya kuandika orodha ya wageni na kukitumia kuorodhesha wageni wote wanaoingia na kulala kila siku; (d) anatoa stakabadhi ya kieletroniki yenye nembo ya Halmashauri baada ya kupokea malipo; 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 915 (Linaendelea) (e) analipa ada ya leseni ya biashara ya nyumba ya kulala wageni ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa sheria; (f) anaweka wazi vitabu vya kumbukumbu vya wageni na nyaraka zingine wakati wa ukaguzi; (g) kila mgeni anasajiliwa kwenye daftari la kulala wageni kwa kuingiza taarifa zote muhimu bila kujali muda aliokitumia chumba; na (h) kila kitanda hakitaruhusiwa kutumika na wageni wawili au zaidi wa jinsia moja. - 6 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni lazima awe na daftari maalum la kuorodhesha wageni na awasilishe taarifa sahihi za idadi ya wageni kwa Halmashauri.
6.-(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni anatakiwa kuwa na daftari maalum kwa ajili ya kuorodhesha wageni wanaoingia kupata huduma ya malazi. (2) Kila mlipa ushuru atatakiwa kuwasilisha Halmashauri taarifa sahihi ya idadi ya wageni kwa kila chumba kilichopangishwa. (3) Endapo itabainika kuwa kuna mgeni au wageni ambao hawajaorodheshwa katika daftari maalum la wageni, Halmashauri itakuwa na mamlaka kisheria ya kumtoza mmiliki huyo ushuru kwa kiwango cha idadi ya vyumba vyote vya hoteli hiyo. Mlipa Ushuru kuwasilisha taarifa ya Hesabu za mwisho wa Mwezi Utoaji wa leseni - 7 Verify source ↗
Leseni ya kuendesha biashara ya nyumba ya
AI-assisted research summary: Leseni ya kuendesha biashara ya nyumba ya kulala wageni hutolewa tu baada ya Halmashauri kujiridhisha kuwa jengo linatimiza masharti fulani ya usafi, vifaa, na usalama.
7. Leseni ya kuendesha biashara ya nyumba ya kulala wageni, itatolewa baada ya Halmashauri kujiridhisha kuwa katika jengo hilo kuna: (a) mwanga na hewa ya kutosha; (b) nafasi na vifaa (samani) vya kutosha; (c) usafi wa jumla wa jengo na vifaa vyake; (d) mfumo wa uondoshaji wa maji taka na taka 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 915 (Linaendelea) ngumu wa kuaminika; (e) vyoo na mabafu kwa jinsia zote; (f) vifaa vya zima moto; (g) tanki la kuhifadhia maji safi; (h) vyoo na bafu vilivyosakafiwa vema kwa vigae au marumaru na kuta zake ziwe zimewekwa vigae kiasi cha futi sita kutoka usawa wa sakafu; (i) kuwa na jozi zaidi ya mbili za mashuka, foronya za mito na magodoro kwa kila kitanda na ziwe na rangi isiyoficha uchafu; (j) kuwepo na sehemu maalumu ya kufulia na kuanikia nguo; na (k) stoo na chumba cha kubadilishia nguo kwa ajili ya wafanyakazi. Uwezo wa kutaka taarifa Uteuzi wa wakala Majukumu ya wakala - 8 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kutaka taarifa kimaandishi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuwataka kwa maandishi taarifa kutoka kwa mtu au taasisi inayopaswa kulipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni.
8. Mkurugenzi anaweza kutaka taarifa kimaandishi kwa mtu yeyote au taasisi yoyote inayopaswa kulipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. - 9 Verify source ↗
Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa niaba yake.
9. Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa niaba yake. - 10 Verify source ↗
Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri atakuwa na
AI-assisted research summary: Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri lazima ahakikishe wamiliki wa nyumba za kulala wageni wanatumia daftari maalum la kuandikishia wageni, na lazima awasilishe ushuru aliokusanya kwa wakati katika kipindi kilichopangwa.
10. Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuhakikisha kuwa wamiliki wa nyumba ya kulala la daftari maalum wageni wanatumia kuandikishia wageni; na (b) kuwasilisha ushuru aliokusanya kwa wakati katika kipindi maalum kwa mujibu wa mkataba 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 915 (Linaendelea) wake. Uwezo wa kuingia kufanya ukaguzi au tathmini - 11 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika nyumba ya kulala wageni ili kukagua taarifa za wageni, kumbukumbu za ushuru, na kufuatilia taratibu za kulaza wageni.
11.-(1) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye nyumba ya kulala wageni kwa lengo la kufanya ukaguzi na tathmini ya usahihi wa uandikishaji wageni katika vitabu vya wageni, kumbukumbu za malipo ya ushuru, na taarifa nyinginezo zinazohusu ushuru wa nyumba za kulala wageni. (2) kukagua kama taratibu za kulaza wageni kwenye nyumba ya kulala wageni zinafuatwa. (3) kukagua kama mmiliki wa nyumba ya kulala wageni ana vitabu vya orodha ya kulala wageni vilivyoidhinishwa na Halmashauri. Ulipaji wa ushuru na riba - 12 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala
AI-assisted research summary: The hotel-lodging taxpayer must pay tax at 10% of the lodging income; late unpaid tax attracts 25% interest for the relevant month.
12.-(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni anapaswa kulipa ushuru katika kiwango cha asilimia kumi ya mapato ya nyumba ya kulala wageni. (2) Ushuru ambao hautalipwa kwa wakati utatozwa riba ya asilimia ishirini na tano ya ushuru uliopaswa kulipwa kwa mwezi husika. Makosa - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: A person commits an offence if they fail to submit required guest-house tax, records, information, or guest registers, keep correct records, or obstruct an authorized officer.
13. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo endapo: (a) atashindwa kuwasilisha ushuru wa nyumba ya kulala wageni na hesabu sahihi kulingana na idadi ya wageni waliopata huduma katika nyumba ya kulala wageni; (b) atashindwa kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa Halmashauri katika muda uliowekwa; (c) atashindwa kuonyesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya ukaguzi wa hesabu zake; (d) atashindwa au kusababisha kuandaliwa au kutengenezwa kitabu kutengeneza kuandaa au 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 915 (Linaendelea) cha wageni, mahesabu au kumbukumbu zozote za nyumba za kulala wageni zisizo sahihi; (e) atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi kuhusu idadi ya wageni katika nyumba yake ya kulala wageni; (f) atashindwa daftari maalum la kutumia kuandikishia wageni; (g) atashindwa kuandaa na kutunza kumbukumbu sahihi kwenye kitabu au daftari alilopewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. atajaribu kumzuia Afisa Mwidhiniwa yake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa. kutekeleza majukumu (h) atamzuia au Adhabu - 14 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti yaliyowekwa
AI-assisted research summary: Anyone who violates the conditions set by this bylaw commits an offence and may be fined, imprisoned, or both if convicted.
14. Mtu yeyote atakayekiuka masharti yaliyowekwa kwenye Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi laki mbili na isiyozidi Shilingi Milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. Kufifilisha kosa - 15 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote kiasi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote Shilingi 200,000 ikiwa mtu huyo atakiri kosa kwa kutumia fomu iliyotajwa na kulipa kiasi hicho pamoja na ushuru unaodaiwa au kukubali kutimiza wajibu wake chini ya sheria ndogo hii.
15. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote kiasi cha Shilingi laki mbili iwapo mtu huyo atakiri kosa kwa kujaza fomu iliyoainishwa katika Jedwali la Sheria Ndogo hii na kulipa kiasi hicho na kulipa ushuru anaodaiwa au kukubali kutekeleza wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii. 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 915 (Linaendelea) _______ JEDWALI _______ (Limetengenezwa chini ya aya ya 15) KUFIFILISHA KOSA Mimi…………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwamba mnamo tarehe……………ya mwezi……………..mwaka ……………………….nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ………… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2023. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninayodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA WANGU Leo tarehe…………… ya Mwezi……………Mwaka………..…. Jina………………………….…………………..….. Saini…………………………..………………..…. MBELE YA: Jina……………………………………….. Cheo……………………………………… Saini……..……………………………….. Tarehe: ………………………… 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 915 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya Korogwe imegongwa kwenye sheria Ndogo hii kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe uliofanyika Tarehe 5/11/2021 na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- GOODLUCK A. MWANGOMANGO Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe KALLAGHE S. YUSUPH Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in