Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ya Mwaka 2023
This provision gives the short title of the bylaw: the Liwale District Council Livestock Management and Control By-law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the bylaw: the Liwale District Council Livestock Management and Control By-law, 2023. This bylaw applies throughout the entire area of Liwale District Council. This section defines key terms used in the by-law, including the Council, Director, livestock, household, permit, and authorized officer. Halmashauri inapaswa kufanya shughuli kadhaa za usimamizi wa ardhi na ufugaji, ikiwemo kupanga matumizi bora ya ardhi, kutenga maeneo ya ufugaji, kujenga majosho, kutoa elimu, kufanya sensa na kutoa chanjo ya mifugo, na kudhibiti uzururaji holela. Kila mfugaji lazima azingatie masharti ya ufugaji, ikiwemo uogeshaji wa mifugo, chanjo, alama maalumu, idadi iliyoidhinishwa, vibali vinavyohitajika, mafunzo, na uuzaji katika maeneo yaliyoidhinishwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ya Mwaka 2023
Showing 16 of 16
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the bylaw: the Liwale District Council Livestock Management and Control By-law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the entire area of Liwale District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the Council, Director, livestock, household, permit, and authorized officer.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote la lengo aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Liwale; “kaya” maana yake ni familia ya watu akiwemo baba, mama, mtoto au watoto na mtu mwingine yeyote anayeishi na familia hiyo, au watu wanaokaa katika nyumba moja na kuishi kama familia au mtu yeyote anayeishi peke yake katika chumba au nyumba; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa 1 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Tangazo La Serikali Na. 917 (Linaendelea) na Halmashauri kwa ajili ya kufanya shughuli iliyokusudiwa chini ya Sheria Ndogo hii; “mfugo” maana yake ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku na wanyama wengine wafugwao na binafsi; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “ufugaji wa ndani” maana yake ni ufugaji na ulishaji wa mifugo ndani ya jengo lililoruhusiwa; “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi, shirika, au kampuni iliyoteuliwa kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa kufanya
AI-assisted research summary: Halmashauri inapaswa kufanya shughuli kadhaa za usimamizi wa ardhi na ufugaji, ikiwemo kupanga matumizi bora ya ardhi, kutenga maeneo ya ufugaji, kujenga majosho, kutoa elimu, kufanya sensa na kutoa chanjo ya mifugo, na kudhibiti uzururaji holela.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa kufanya mambo yafuatayo: (a) kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi; (b) kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli ya ufugaji kwa mujibu wa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi; (c) kujenga majosho ya mifugo kwa kushirikiana na wananchi; (d) kutoa elimu ya ufugaji bora kwa jamii ili kuongeza tija; (e) kufanya sensa ya mifugo, kuweka alama na kutoa kadi za mifugo; (f) kutoa chanjo kwa kushirikiana na wafugaji ya mifugo yanayoambukiza kudhibiti magonjwa na ili yasiyoambukiza binadamu; na (g) kudhibiti uzururaji holela wa mifugo na wanyama katika Halmashauri. Wajibu wa mfugaji - 5 Verify source ↗
Kila mfugaji atahakikisha kuwa
AI-assisted research summary: Kila mfugaji lazima azingatie masharti ya ufugaji, ikiwemo uogeshaji wa mifugo, chanjo, alama maalumu, idadi iliyoidhinishwa, vibali vinavyohitajika, mafunzo, na uuzaji katika maeneo yaliyoidhinishwa.
5. Kila mfugaji atahakikisha kuwa- (a) anaogesha mifugo yake ili kudhibiti 2 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Tangazo La Serikali Na. 917 (Linaendelea) magonjwa ya atakavyoelekezwa na Halmashauri; wanyama kama kama itakavyoamriwa (b) anapeleka mifugo yake katika vituo vya na chanjo Halmashauri na atalipia chanjo hiyo kama atatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa viwango vitakavyoainishwa na mamlaka husika; (c) mifugo yake inawekwa alama maalumu zinazotolewa kwa mujibu wa sheria na miongozo; (d) anafuga mifugo kwa idadi iliyoidhinishwa kulingana na maelekezo ya sheria na miongozo; (e) hakaribishi wafugaji wengine bila kibali cha Halmashauri; (f) anawapa mifugo malisho na maji ya kutosha kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji; (g) ana kibali cha kusafirisha mifugo na mazao yake; (h) kabla ya kuingiza mifugo katika Halmashauri anapaswa kuwa na kibali cha maandishi cha kukubaliwa kuingiza mifugo hiyo; (i) anafuga kwa kuzingatia mipango ya matumizi bora ya ardhi; (j) anahudhuria mafunzo ya ufugaji kama atakavyohitajika na Halmashauri; (k) anauza mifugo yake katika masoko na minada iliyoidhinishwa au eneo lingine kwa taarifa maalumu. Kibali cha kufuga wanyama - 6 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakayetaka kufuga mifugo
AI-assisted research summary: Mtu anayetaka kufuga mifugo lazima apate kibali cha kufuga kutoka kwa Halmashauri.
6.-(1) Mtu yeyote atakayetaka kufuga mifugo atalazimika kupata kibali cha kufuga kutoka kwa Halmashauri kama ilivyoainishwa katika Jedwali la 3 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Tangazo La Serikali Na. 917 (Linaendelea) Kwanza la Sheria Ndogo hii. (2) Bila kuathiri aya ndogo ya (1), mtu yeyote atakayekiuka taratibu za ufugaji chini ya Sheria Ndogo hii, atafutiwa kibali na atalazimika kuhamisha mifugo yake yote. Masharti kwa mfugaji - 7 Verify source ↗
(1) Kila mfugaji hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Kila mfugaji haruhusiwi kufanya shughuli fulani za mifugo bila kibali au katika maeneo yasiyoruhusiwa, na pia anatakiwa kuboresha eneo alilopewa na Halmashauri.
7.-(1) Kila mfugaji hataruhusiwa- (a) kuchunga, kulisha au kunywesha maji ambayo mifugo hayakutengwa kwa shughuli hiyo; maeneo katika (b) kutumia wanafunzi kuchunga au kuhudumia mifugo muda ambao wanatakiwa kuwa shule; (c) kusafirisha, kuswaga au kuhamisha mifugo kutoka eneo moja hadi lingine bila kibali kutoka Halmashauri; (d) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (e) kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo si mnada, masoko au magulio ya kibali mifugo maalumu cha Halmashauri; yaliyoaidhinishwa bila (f) kulisha mifugo kwenye maeneo ya kilimo au wakulima kukaribisha mifugo kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo; (g) kununua, kuuza au kufanya biashara ya kubadilishana aina yoyote ya mfugo au mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali maalum isipokuwa kwenye minada au magulio yaliyotengwa kwa shughuli hiyo na Halmashauri. (2) Kila mfugaji atapaswa kuboresha eneo alilopewa na Halmashauri ikiwa ni pamoja na kuchimba virambo na visima (Msomera) na kupanda nyasi ili kuepuka changamoto za kuhamahama mara kwa mara 4 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Tangazo La Serikali Na. 917 (Linaendelea) kutafuta malisho. Kibali cha kusafirisha mifugo Kudhibiti mifugo inayozurura ovyo ambaye - 8 Verify source ↗
(1) Mtu
AI-assisted research summary: Anyone transporting livestock or livestock products into or out of the council area must have a special permit.
8.-(1) Mtu anakusudia yeyote kusafirisha mfugo au mifugo na mazao yake kutoka au kuingia katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuwa na kibali maalumu kilichoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. (2) Halmashauri itatoa kibali cha kusafirisha mifugo kwa utaratibu ufuatao: (a) mfugaji atatoa au kuonesha uthibitisho wa kumiliki mfugo au mifugo kutoka kwa Afisa Mwidhiniwa; na (b) Halmashauri itakagua kibali cha kusafirisha mfugo au mifugo. (3) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kukamata na kutoza faini na adhabu kwa mfugo au mifugo yoyote inayosafirishwa kinyume na Sheria Ndogo hii. - 9 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakamata mfugo au mifugo
AI-assisted research summary: Halmashauri must seize livestock found wandering in its area, charge storage costs, and may auction uncollected livestock after 7 days with court permission.
9.-(1) Halmashauri itakamata mfugo au mifugo yoyote itakayoonekana inazurura ovyo katika eneo la Halmashauri na kila mfugo utalipiwa gharama ya kuhifadhiwa kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Tatu. (2) Endapo mfugo uliokamatwa hautachukuliwa na mmiliki ndani ya kipindi cha siku saba (7) tangu kukamatwa, Halmashauri itakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mfugo huo baada ya kupata idhini ya Mahakama, na fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmliki wa mfugo huo baada ya kutoa faini inayodaiwa, gharama za kuhifadhi mfugo, gharama ya Mahakama na gharama ya mnada. (3) Bila kuathiri aya ndogo ya (2), kabla ya kuuza mfugo kwa mnada, Halmashauri itamjulisha mmliki na umma juu ya kusudio hilo. 5 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Tangazo La Serikali Na. 917 (Linaendelea) Ukaguzi wa mifugo na bidhaa za mifugo Taratibu za biashara ya mifugo na mazao yake (4) Endapo kutatokea kufa kwa mifugo au mfugo kutokana na sababu yoyote ile, Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama vifo hivyo vitakuwa vimesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri.
Part
Jedwali la Tatu.
- 10 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kukataa mifugo au bidhaa kuingia au kuuzwa ndani ya eneo la Halmashauri ikiwa zinaweza kuhatarisha afya au usalama, na anaweza pia kuingia nyumba au jengo kwa ajili ya kukagua uzingatiaji wa Sheria Ndogo hii ndani ya muda uliotajwa.
10.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kukataa aina yoyote ya mifugo au bidhaa kuingia au kuuzwa ndani ya eneo la Halmashauri, iwapo mifugo hiyo au bidhaa hizo zinaweza kuhatarisha afya au usalama wa mifugo mingine au watumiaji. (2) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika nyumba au jengo lolote kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kwa lengo la kukagua uzingatiaji wa Sheria Ndogo hii. - 11 Verify source ↗
(1) Mfanyabiashara anatakiwa kuwa na
AI-assisted research summary: Mfanyabiashara wa mifugo lazima awe na leseni na vibali vinavyohusika, awasilishe vibali kwa Halmashauri, na afuate masharti ya kibali na maeneo/masoko yanayotambulika.
11.-(1) Mfanyabiashara anatakiwa kuwa na leseni na vibali kutoka Mamlaka husika vinavyohusu kuuza na kununua mifugo na mazao ya mifugo na anatakiwa kuwasilisha vibali vyake Halmashauri kwa ajili ya uhakiki. (2) Mfanyabiashara wa mifugo inayopelekwa au kutoka mnadani au machinjioni atatakiwa kuwa na kibali maalumu kutoka Halmashauri. (3) Mfanyabiashara atakayesafirisha mifugo kutoka nje ya Halmashauri atatakiwa kuwa na kibali kutoka katika Halmashauiri ambayo mifugo hiyo inatoka. (4) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (2) na (3), mfanyabiashara wa mifugo anapaswa kusafirisha mifugo katika vyombo vya usafiri vinavyokubalika kwa mujibu wa Sheria. (5) Mifugo yote itauzwa au kununuliwa katika minada na masoko yanayotambulika kwa mujibu wa Sheria. 6 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Tangazo La Serikali Na. 917 (Linaendelea) (6) Minada yote ya mifugo au magulio ya cha mifugo yatafanyika kwa kibali maalumu Halmashauri na kwenye maeneo yaliyoruhusiwa. Makosa - 12 Verify source ↗
Mfugaji yeyote atakuwa ametenda kosa
AI-assisted research summary: A livestock keeper commits an offence if they do any of the listed acts, including failing to vaccinate or wash livestock, feeding them in prohibited places, letting them roam freely, moving livestock into the Halmashauri without following the rules, lacking a livestock permit, failing to report disease or sudden death, not cooperating with marking, making livestock feed without expertise, or obstructing an Authorized Officer.
12. Mfugaji yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo- (a) atashindwa au kuchanja mfugo au mifugo yake ili kuzuia magonjwa; atakataa kuogesha au (b) atalisha mfugo au mifugo kwenye maeneo yasiyoruhusiwa; (c) ataruhusu mfugo au mifugo yake kuzurura hovyo; (d) atamshawishi mtu au kundi la watu kuingiza mifugo ndani ya Halmashauri bila kufuata sheria, kanuni na taratibu; (e) hatokuwa na kibali cha ufugaji; (f) atashindwa kutoa taarifa juu ya uwepo wa au dalili za ugonjwa au kifo cha ghafla cha mfugo au mifugo katika banda lake; (g) atashindwa kutoa ushirikiano wa uwekaji wa alama kwa mfugo au mifugo yake; (h) atajihusisha na utengenezaji wa vyakula vya mifugo huku akijua hana utaalamu huo; au (i) atamzuia Afisa Mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake. Adhabu - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria
AI-assisted research summary: Anyone who violates the bylaw commits an offence and may be fined, imprisoned, or both.
13. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini ya kiasi kisichopungua Shilingi elfu hamsini na kisichozidi Shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. Kufifilisha kosa - 14 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza faini mtu
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza faini mtu aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii, hadi shilingi 50,000, ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Nne.
14. Mkurugenzi anaweza kumtoza faini mtu 7 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Tangazo La Serikali Na. 917 (Linaendelea) yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii, kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Nne. _________________ JEDWALI LA KWANZA __________________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 6(1)) KIBALI CHA KUFUGA MFUGO Jina la Mfugaji:……………………………………………………….. Anuani:………………………………………………………… Kata:…………………………………… Mtaa ………………… Namba Nyumba:…………………………………… Namba Kitalu:…………… Ameruhusiwa kufuga Mifugo ifuatao katika eneo la…………... Na Aina ya Mfugo Koo Idadi ya Mifugo Dume Jike Jumla Ng’ombe Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura 1 2 Mbuzi 3 4 5 6 7 8 9 10 Mbwa 11 Kuku au Bata 12 Wanyama wengine Kibali hiki kimetolewa kwa Ndugu……………………………………kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) kwa Mfugo au mifugo kuanzia tarehe……………...hadi tarehe…………... Kimetolewa na: Jina la Afisa Mwidhiniwa…………………………………..Saini……....................… Wadhifa:………………………………………………………......................……….. Tarehe:………………….............................................................................................. Muhuri:……………………………………………..................................................... 8 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Tangazo La Serikali Na. 917 (Linaendelea) ______________ JEDWALI LA PILI ______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 8(1)) KIBALI CHA KUSAFIRISHA MIFUGO Jina:……………………………………………. Anuani:………………………………………… Ameruhusiwa kusafirisha Mifugo ifuatayo kutoka ………………kupitia njia za……………………..hadi…………..….. Idadi ya Mifugo Aina ya Mfugo Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura Namba
Part
JEDWALI LA PILI
- 12 Verify source ↗
Mifugo wengine
AI-assisted research summary: This section says the permit for other livestock, chickens, or ducks is valid for a stated number of days between the dates shown.
12. Mifugo wengine Kuku au Bata Kibali hiki kitakuwa cha muda wa siku…........ kuanzia tarehe…....hadi tarehe………. Kimetolewa na : Jina la Afisa Mwidhiniwa:………………………………………. Saini:…………………………………………………………….. Wadhifa:…………………………………………………………….. Tarehe:………………………………………………………….... Muhuri:……………………………………… 9 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Tangazo La Serikali Na. 917 (Linaendelea) ____________ JEDWALI LA TATU _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 9) VIWANGO VYA MALIPO YA KUHIFADHI MIFUGO ILIYOKAMATWA NA HALMASHAURI KWA KILA MFUGO Jina la Mfugo Na
Part
JEDWALI LA TATU
- 5 Verify source ↗
Mbwa/Paka
AI-assisted research summary: This is a form for admitting an offence and agreeing to pay a fine instead of being taken to court, before the Director of Liwale District Council.
5. Mbwa/Paka Kiasi 2500 1500 1500 2500 1000 Siku 1 1 1 1 1 ____________ JEDWALI LA NNE _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 14) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, kwamba mnamo tarehe …… ya Mwezi ………. Mwaka ……….…… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …… ya Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Niko tayari kulipa kiasi cha faini badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. MBELE YANGU: Jina:……………………………………..………………….....… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa………………………………………………...………… Tarehe………………………………………………………….... Saini………………………........ 10 Sheria Ndogo ya Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Tangazo La Serikali Na. 917 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya Liwale imegongwa kwenye sheria Ndogo hii kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano mkuu wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Liwale uliofanyika Tarehe ……. mwezi …… Mwaka……. na kushuhudiwa lakari hiyo ikigongwa mbele ya TINA SEKAMBO Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Halmashauri ya Wilaya ya Liwale MOHAMED RASHID MTESA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Liwale NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in