Sheria Ndogoya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023
This provision gives the short title of the bylaw.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogoya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the bylaw. This bylaw applies throughout the entire area of Kibondo District Council. This section defines key terms used in the by-law, including officer, council, farmer, trader, crops, fungi, aflatoxin, storage, drying, processing, harvesting, crop-damage indicators, and pesticides. Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na inaweza kukagua mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, kiwanda, na maeneo ya usindikaji. A person intending to cultivate must follow proper farm-preparation practices, prepare the farm on time, and not burn during land preparation.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogoya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023
Showing 17 of 17
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogoya Kuzuia
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the bylaw.
1. Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogoya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the entire area of Kibondo District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including officer, council, farmer, trader, crops, fungi, aflatoxin, storage, drying, processing, harvesting, crop-damage indicators, and pesticides.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo; “kanuni bora za kilimo” maana yake ni uandaaji wa shamba kwa usahihi, upandaji mbegu bora kwa wakati na kwa nafasi sahihi, upaliliaji, utumiaji mbolea kwa usahihi, udhibiti wa wadudu na wanyama waharibifu, uvunaji na hifadhi sahihi ya mazao; “kilimo” maana yake ni shughuli ya uzalishaji wa mazao; “mkulima” maana yake ni mtu, taasisi, kampuni au kikundi cha watu anayejihusisha na shughuli za kilimo; 1 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Serikali Na. 919 (Linaendelea) “mfanyabiashara’’ maana yake ni taasisi, kampuni, kikundi cha watu au mtu binafsi anayejihusisha na shughuli za kuuza au kununua mazao ya kilimo; “Mkurugenzi” Maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mazao’’ maana yake ni punje zinazotokana na mmea wa mhindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi na mazao ya mizizi yatokanayo na mihogo na viazi; “kuvu’’ maana yake ni ukungu unaoota kwenye mazao; “sumukuvu” maana yake ni sumu zinazozalishwa na kuvu wanao ota kwenye mazao; “uhifadhi” maana yake ni utaratibu wa kutunza mazao katika sehemu ambayo haisababishi mazingira ya uotaji wa kuvu; “ukaushaji” maana yake ni taratibu sahihi za kupunguza unyevu kwenye mazao kwa ajili ya matumizi au uhifadhi; “usindikaji” maana yake ni hatua ya uchakataji wa zao kwa lengo la kuongeza thamani; “uvunaji” maana yake ni uondoaji wa mazao kutoka kwenye mmea baada ya kukomaa au kukauka; “viashiria vya sumukuvu” maana yake ni dalili zinazoonyesha uwepo wa sumukuvu kwenye mazao ya mahindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi zilizovunjika, na mazao ambayo hayajauka vizuri; “viuatilifu” maana yake ni sumu ya kuua au kuzuia wadudu waharibifu wa mazao.
Part
sehemu ambayo haisababishi mazingira ya uotaji wa
- 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuratibu
AI-assisted research summary: Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na inaweza kukagua mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, kiwanda, na maeneo ya usindikaji.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuratibu la na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo Halmashauri kwa lengo la kuzuia na kudhibiti sumukuvu. 2 Uratibu na usimamizi wa shughuli za kilimo na udhibiti wa sumukuvu Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Serikali Na. 919 (Linaendelea) (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufanya ukaguzi katika mashamba,vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, kiwanda na eneo la usindikaji kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Uandaaji wa shamba - 5 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekusudia kulima, atapaswa
AI-assisted research summary: A person intending to cultivate must follow proper farm-preparation practices, prepare the farm on time, and not burn during land preparation.
5. Mtu yeyote anayekusudia kulima, atapaswa kuzingatia misingi ifuatayo: (a) kufuata njia sahihi za uandaaji wa shamba; (b) kutayarisha shamba kwa wakati; na (c) kutochoma moto wakati wa uandaaji wa shamba. Upandaji wa mazao - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone who plants crops must use proper planting methods, including good seeds, planting when planting rains begin, and using correct spacing.
6. Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa kuzingatia njia sahihi za upandaji kama ifuatavyo: (a) kutumia mbegu bora; (b) kupanda mara tu mvua za kupandia zinapoanza kunyesha; na (c) kupanda kwa nafasi sahihi. Utunzaji wa mazao shambani - 7 Verify source ↗
Mtu yeyote aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza
AI-assisted research summary: Anyone who has planted crops must care for them properly.
7. Mtu yeyote aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza kwa kuzingatia njia sahihi za utunzaji wa mazao kama ifuatavyo: (a) kutumia mbolea; (b) kupalilia kwa wakati; na (c) kudhibiti magonjwa, wadudu waharibifu. na wanyama Uvunaji wa mazao - 8 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa kuvuna
AI-assisted research summary: Anyone harvesting crops must do so using good harvesting practices.
8. Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa kuvuna kwa kuzingatia kanuni bora za uvunaji kama ifuatavyo: (a) kuvuna mara baada ya mazao kukomaa au kukauka; (b) kusafirisha na kuhifadhi mazao vizuri; na (c) kusafisha shamba baada ya kuvuna. Ukaushaji wa mazao - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Anyone who harvests crops must dry them properly immediately after harvesting.
9. Mtu yeyote atakayevuna mazao anapaswa kuyakausha kwa kutumia njia sahihi mara tu baada ya 3 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Serikali Na. 919 (Linaendelea) kuvuna kama ifuatavyo: (a) kutumia njia za asili zisizoruhusu kuvu kuota; (b) kutumia maturubai, mikeka na vichanja vinavyozuia uchafuzi wa mazao; na (c) kukausha kwa njia yoyote sahihi itakayoelekezwa na wataalamu. Uhifadhi wa mazao - 10 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atawajibika kuhifadhi mazao kwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote lazima ahifadhi mazao kwa njia sahihi za asili au za kisasa zinazozuia kuota kwa kuvu.
10.-(1) Mtu yeyote atawajibika kuhifadhi mazao kwa kutumia njia sahihi za asili au za kisasa ambazo zitazuia kuota kwa kuvu. (2) Njia sahihi zinazopaswa kutumika kuhifadhi mazao ni pamoja na: (a) mifuko isiyopitisha hewa; (b) magunia ya kawaida kwa ajili ya mazao yaliyowekwa viuatilifu; (c) kihenge na kichanja bora cha asili; (d) silo au pipa maalumu; (e) ghala bora lililo safi; (f) kutumia viuatilifu kwenye mazao kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu; au (g) njia nyingine kadri wataalamu. itakavyoshauriwa na Wajibu wa Halmashaur i - 11 Verify source ↗
(1) Katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: Halmashauri must carry out several support duties for crop production, storage, records, training, and market facilities under this by-law.
11.-(1) Katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hii, Halmashauri itakuwa na wajibu wa: (a) kuhamasisha na kutoa elimu ya uzalishaji na usimamizi wa mazao; (b) kuhamasisha uhifadhi wa mazao katika eneo au uchafuzi wa ili kuepuka mahala salama sumukuvu; (c) kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo; (d) kutunza kumbukumbu za mashamba yote ya mazao ya kilimo katika Kata na Vijiji ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (e) kuanzisha, kuendeleza mashamba darasa na vituo 4 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Serikali Na. 919 (Linaendelea) maalumu kwa ajili ya kutolea mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu; (f) kuanzisha na kuhamasisha wakulima na wadau wengine kujenga sehemu za kuhifadhia mazao; au (g) kuandaa vituo maalumu vya kuuza na kununua mazao. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), kumteua Afisa Mwidhiniwa Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. inaweza Wajibu wa mkulima - 12 Verify source ↗
Kila Mkulima atakuwa na wajibu ufuatao
AI-assisted research summary: Kila mkulima lazima afanye kilimo kwa kanuni bora, aripoti dalili za kuvu kwa Halmashauri, na ahudhurie mafunzo ya Halmashauri na kuyatumia ujuzi huo.
12. Kila Mkulima atakuwa na wajibu ufuatao: (a) kufanya shughuli za kilimo kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na usimamizi wa mazao kabla na baada ya kuvuna; (b) kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusu uwepo wa dalili za kuvu katika mazao; na (c) kushiriki mafunzo ya na Halmashauri na kudhibiti kutekeleza ujuzi uliopatikana kwenye mafunzo hayo. yaliyoandaliwa sumukuvu Wajibu wa msafirishaji - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote anayesafirisha mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Mtu anayesafirisha mazao lazima ahakikishe vifungashio na vifaa vinakuwa vikavu au haviruhusu maji, unyevu, na vumbi kuingia ndani.
13. Mtu yeyote anayesafirisha mazao anapaswa kuhakikisha vifungashio na vifaa anavyotumia kusafirisha mazao ni vikavu au visivyoruhusu maji au unyevu na vumbi kuingia ndani ili kuepusha kuvu kuota kwenye mazao. Wajibu wa mfanyabias hara - 14 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara wa mazao atakuwa na
AI-assisted research summary: Kila mfanyabiashara wa mazao lazima ahakikishe ananunua, anahifadhi, anasafirisha, au anauza mazao yasiyo na viashiria vya sumukuvu vilivyoorodheshwa kwenye Jedwali la Kwanza.
14. Kila mfanyabiashara wa mazao atakuwa na wajibu wa kuhakikisha ananunua au anahifadhi au anasafirisha au kuuza mazao ambayo hayana viashiria vya sumukuvu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. Wajibu wa msindikaji - 15 Verify source ↗
Kila msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika
AI-assisted research summary: Kila msindikaji lazima asindike mazao ambayo hayana viashiria vya sumukuvu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza.
15. Kila msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika mazao ambayo hayana viashiria vya sumukuvu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo 5 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Serikali Na. 919 (Linaendelea) hii. Makosa na adhabu - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayefanya vitendo vilivyoorodheshwa kuhusu utunzaji, uvunaji, ulishaji, usafirishaji, au matumizi ya mazao yenye sumukuvu au vihatarishi vingine anakosa chini ya kifungu hiki.
16. Mtu yeyote ambaye: (a) atashindwa kuandaa, kupanda, kutunza shamba na mazao kwa usahihi; (b) atashindwa kuvuna kwa wakati mara baada ya mazao kukomaa; (c) atashindwa kuondoa kwa wakati mazao shambani baada ya kuvuna; (d) ataanika mazao kwenye udongo, vumbi au mchanga; (e) atakausha mazao katika mazingira yanayoweza kusababisha sumukuvu; (f) atatumia viuatilifu vilivyozuiliwa kutumika kwenye mazao; (g) atauza mazao yenye viashiria vya sumukuvu; (h) atasafirisha mazao kwa njia zitakazosababisha mazingira ya kuvu kuota; (i) atatumia mazao yenye viashiria vya sumukuvu wakati wa usindikaji; au (j) atatenda jambo lolote linalokiuka masharti ya Sheria Ndogo hii, atakuwa ametenda kosa na endapo atapatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kutumikia kifungo kisichozidi miezi kumi na miwili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kutoza mtu aliyekiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu kiasi kisichozidi shilingi 50,000.
17. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. 6 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Serikali Na. 919 (Linaendelea) ______________ JEDWALI LA KWANZA ______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 14 na 15) VIASHIRIA VYA SUMUKUVU MWONEKANO WA PUNJE Punje kuwa na ukungu au kuvu - rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo Punje kuwa na ukungu au kuvu – rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo Na. AINA YA MAZAO Mahindi HALI YA UNYEVU AU KUVU Punje kuwa na unyevu 1 2 Karanga Punje kuwa na unyevu 7 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Serikali Na. 919 (Linaendelea) ____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 17) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi ………………………………. Nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya…………………………………….…ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwamba mnamo tarehe…………ya Mwezi….......... Mwaka …………….. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ………. ya Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Niko tayari kulipa kiasi cha Shilingi…………… kwa ajili ya kufifilisha Kosa nililotenda chini ya Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe………..ya Mwezi……………………Mwaka………………….. Jina………………………………..…………….Saini………………………. MBELE YANGU: Jina……………………………………………….….. Wadhifa………………………..…………………….….. Saini…………………………………………………… Tarehe…………………………………………………. 8 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Serikali Na. 919 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya Kibondo imebandikwa kwenye sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmshauri ya Wilaya ya Kibondo uliofanyika Tarehe 31 mwezi 01 Mwaka 2023 DIOCLES M. RUTEMA Mkurugenzi Mtendaji (W) Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo HABILI C. MASEKE Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogoya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in