Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023
This provision states the short title of the by-law: the Kibondo District Council Environmental Sanitation By-Law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision states the short title of the by-law: the Kibondo District Council Environmental Sanitation By-Law, 2023. This by-law applies throughout the entire area of the Kibondo District Council authority. This section defines key terms used in the By-Law. Mkazi anayemiliki nyumba, kiwanja au biashara lazima aweke eneo lake safi na ashughulikie taka, shimo la taka, choo, na udhibiti wa wadudu; pia hapaswi kutupa taka wazi. Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara lazima wawe na njia ya kuhifadhi maji taka, waondoe maji taka panapojaa, na wasiyatoe maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabara, vichochoroni, mito, vyanzo vya maji, maeneo ya wazi au mifereji isiyotengwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023
Showing 28 of 28
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision states the short title of the by-law: the Kibondo District Council Environmental Sanitation By-Law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of the Kibondo District Council authority.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the By-Law.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote kusimamia na Mkurugenzi atakayeteuliwa utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa dawa; “chanzo cha maji” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji; “dampo” au “Jalala” maana yake ni eneo maalum lililotangazwa kuwa limetengwa na kuhifadhiwa na Halmashauri kama eneo maalum nje ya makazi ya watu kwa ajili ya kumwaga au kutupa taka taka za aina yoyote; 1 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo; “kizimba cha taka” maana yake ni kizimba au chombo maalumu kilichowekwa na Halmashauri kwa ajili ya jamii kuhifadhia taka ngumu kabla ya kusafirishwa hadi kwenye jalala kuu lililoidhinishwa; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara au afisa yeyote atakayeteuliwa ya Mkurugenzi; kutekeleza majukumu “mkazi” maana yake ni mtu yeyote ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo lililoko chini ya mamlaka ya Halmashauri na ambaye ama ana kaya au anaishi katika kaya au la Halmashauri; iliyopo katika eneo taasisi “maji taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “uchafu hatarishi” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “uchafu wa mazingira” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri husika. shirika ambalo - 4 Verify source ↗
Kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba au
AI-assisted research summary: Mkazi anayemiliki nyumba, kiwanja au biashara lazima aweke eneo lake safi na ashughulikie taka, shimo la taka, choo, na udhibiti wa wadudu; pia hapaswi kutupa taka wazi.
4. Kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba au kiwanja au biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba- (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; (b) taka zote zinakusanywa, kufukiwa au 2 Sura ya 331 Sura ya 191 Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) kuondolewa kwa njia Halmashauri; itakayoelekezwa na (c) anachimba shimo la kutupa taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi 3 na upana usiopungua futi 2; (d) anajenga choo imara cha kudumu kilichojengwa kwa matofali na kuezekwa kwa bati, tembe, majani au vigae chenye mlango unaofunga na kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na kuna chombo cha maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya au wadudu wengine hatarishi; na (f) hatupi taka katika maeneo ya wazi, mitaani au barabarani. Uhifadhi wa maji taka - 5 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba au kiwanda au eneo la
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara lazima wawe na njia ya kuhifadhi maji taka, waondoe maji taka panapojaa, na wasiyatoe maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabara, vichochoroni, mito, vyanzo vya maji, maeneo ya wazi au mifereji isiyotengwa.
5. Kila mmiliki wa nyumba au kiwanda au eneo la biashara anatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa ana karo la kuhifadhi maji taka; (b) kunyonya maji taka endapo karo litajaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni au kwenye vyanzo vya maji au maeneo ya wazi au kwenye mfereji wa maji isiyotengwa ya mvua au kuhifadhia maji taka. sehemu yoyote Utengenezaj i na uuzaji wa vyakula
Part
sehemu yoyote
- 6 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetengeneza matunda, kuchoma,
AI-assisted research summary: Watu wanaotengeneza au kuuza chakula katika eneo la Halmashauri lazima wafuate masharti ya afya na wawe na kibali cha afisa afya wa Halmashauri.
6. Mtu yeyote anayetengeneza matunda, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa- (a) kutimiza masharti na kanuni za afya; na (b) kuwa na kibali kutoka kwa afisa afya wa Halmashauri. Upimaji wa afya - 7 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli,
AI-assisted research summary: Wahudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waokaji mikate, na wauzaji wa vyakula vilivyopikwa lazima wapime afya zao kila baada ya miezi sita.
7. Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli, mgahawa, baa, nyumba ya kulala wageni au bucha au 3 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) waoka mikate au watu wanaoshughulika na kuuza vyakula vilivyopikwa kuhakikisha kwamba wanapima afya zao kila baada ya miezi sita. Mamlaka ya afisa mwidhiniwa - 8 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo lolote ndani ya Halmashauri wakati wa saa za mchana maalum na anaweza pia kuashauri au kumuamuru mtu asikae katika jengo linalohatarisha afya au maisha.
8.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika eneo lolote ndani ya Halmashauri kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Vifaa vya kuhifadhi taka ngumu Ukusanyaji taka ngumu (2) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kushauri au kumuelekeza mtu kutokuishi katika jengo ambalo linahatarisha afya yake au maisha ya watu na viumbe hai. - 9 Verify source ↗
(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji
AI-assisted research summary: Certain residential occupants, businesses, and vehicles within the Council area must keep a covered waste container and collect waste in designated collection cages; owners or tenants in green belt, unsurveyed areas must also have a large pit for solid waste on their premises.
9.-(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji wa jengo la makazi au mtu yeyote anayefanya biashara katika eneo lolote au chombo cha usafiri ndani ya Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhia taka chenye mfuniko na atawajibika kukusanya taka hizo kwenye vizimba vya kuzolea taka katika maeneo yaliyoainishwa. (2) Kila mmiliki wa jengo au mpangaji wa nyumba iliyo katika ukanda wa kijani, katika maeneo ambayo hayajapimwa atalazimika kuwa na shimo kubwa la kukusanyia taka ngumu katika eneo lake. - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri itawajibika kukusanya taka
AI-assisted research summary: Halmashauri must collect solid waste from designated waste sheds in each ward.
10.-(1) Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu kutoka katika vizimba vya taka vilivyotengwa katika kila kata. (2) Taka ngumu zote zitakazokusanywa kwenye mapipa ya taka zitabaki kuwa mali ya mkazi au mmliki wa eneo husika mpaka zitakapokuwa zimefikishwa kwenye kizimba cha taka au zitakapokuwa zimetolewa na Wakala kutoka katika eneo lake. 4 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) Ada ya uzoaji taka Eneo la kutupa taka Siku ya usafi Uteuzi wa wakala - 11 Verify source ↗
Mtu yeyote anayezalisha taka atalipia ada au
AI-assisted research summary: A person who generates waste must pay the waste collection fee or levy at the rate set in the First Schedule.
11. Mtu yeyote anayezalisha taka atalipia ada au ushuru wa ukusanyaji wa taka kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. - 12 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: The council must designate a waste disposal area, place special waste containers in council areas, and provide waste collection services for a fee.
12. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kutenga eneo maalumu kwa ajili ya kutupa taka; (b) kuweka vyombo maalumu vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. - 13 Verify source ↗
(1) Kila alhamisi ya wiki na jumamosi ya
AI-assisted research summary: Kila Alhamisi na Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku maalumu ya usafi; wakazi na watu wote wanapaswa kushiriki na kuhakikisha maeneo yao yanabaki safi.
13.-(1) Kila alhamisi ya wiki na jumamosi ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku maalamu ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya makazi na umma. (2) Kila mkazi katika kijiji na kitongoji atapaswa kushiriki usafi wa mazingira kwa siku iliyopangwa na Halmashauri katika maeneo yao na maeneo ya umma. (3) Kila mtu atahakikisha eneo la makazi yake na vichochoro vilivyomzunguka, eneo analofanyia biashara, eneo la wazi lililo karibu naye kwa umbali wa mita kumi na eneo la mazingira ya ofisi ni safi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (4) Halmashuri inaweza kuelekeza kikundi au taasisi yoyote kufanya usafi katika eneo lolote la Halmshauri. - 14 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kumteua wakala kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumteua wakala wa kufanya usafishaji na ukusanyaji taka kwa niaba yake.
14.-(1) Halmashauri inaweza kumteua wakala kwa ajili ya kutoa huduma ya usafishaji na ukusanyaji taka kwa niaba yake. (2) Wakala atakayeteuliwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa- (a) ameingia mkataba na Halmashauri kwa ajili ya kutoa huduma ya usafi wa mazingira; (b) anakusanya na kutupa taka hizo kwenye dampo kuu la Halmashauri. 5 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) Vikundi vya usafi - 15 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri must promote and recognize community groups for waste control and sanitation, and involved groups have reporting and fee-related limits.
15.-(1) Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika mitaa baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. (2) Kwa kuzingatia idadi ya watu, kiwango cha taka kinachozalishwa na utendaji kazi wa kikundi cha kijamii taka, katika eneo ambamo kinakusanya na kuzoa Halmashauri inaweza- (a) kukijengea uwezo kikundi kwa kuruhusu kutoza ada kwa kila kaya au jengo lililopo katika eneo ambalo kikundi hicho kimepewa mkataba wa kukusanya na kuzoa taka kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kukipa vitendea kazi na motisha nyinginezo kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa kikundi. (3) Endapo kikundi cha kijamii kitaomba kushirikishwa katika shughuli za kuzoa na kukusanya taka katika eneo lolote la Kata- (a) shughuli za kikundi hicho zitaratibiwa na Afisa Mwidhinishwa pamoja na afisa mtendaji wa kata husika na taarifa zote za utendaji wa kikundi zitawasilishwa na kujadiliwa katika kamati ya maendeleo ya kata husika; (b) hakitatoza viwango vya tofauti na vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale ambapo wamepewa kibali na Halmashauri; ada (c) kitawasilisha taarifa ya utekelezaji na makusanyo ya ada kutoka kila kaya au mmiliki wa jengo au familia pamoja na changamoto kilizokumbana nazo kwa Halmashauri na kamati ya maendeleo ya kata; na (d) kitawasilisha makusanyayo yote ya fedha ya kila siku kwa Afisa Mtendaji wa Kata ambaye 6 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) Marufuku atawasilisha makusanyanyo hayo kila wiki kwa Mkurugenzi. - 16 Verify source ↗
Ni marufuku kwa
AI-assisted research summary: Section 16 says many activities are prohibited unless the required approval, licence, permit, or written consent is obtained.
16. Ni marufuku kwa- (a) mtu yeyote kuendesha biashara ya upulizaji dawa au biashara ya kuua wadudu au wanyama waharibifu katika nyumba yoyote au mahali popote bila cheti cha taaluma kinachotambuliwa na Serikali na leseni kutoka Halmashauri; lake (b) mfanyabiashara yeyote kupanga bidhaa nje ya la biashara au barabarani au lolote ambalo jengo vichochoroni au katika eneo halikuidhinishwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (c) mfugaji kuruhusu mifugo kuzurura ovyo mitaani Sura ya 191 au barabarani; (d) mtu yeyote kutupa taka za aina yoyote barabarani au eneo lolote la wazi au kwenye vichochoro au kwenye chanzo chochote cha maji au katika eneo lolote ambalo halikutengwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (e) mtu yeyote aliye ndani ya gari kudondosha taka ngumu nje ya gari likiwa ndani au nje ya kituo cha magari na sehemu yoyote ile ambapo gari hilo linapita; (f) mtu yeyote kuanzisha shughuli za kiwanda au mradi wowote unaoweza kuathiri mazingira bila kufanya tathmini ya athari kwa mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; (g) mtu yeyote kuzuia maji kupitia njia yake ya asili kwa kujenga, kulima au kuweka kitu chochote kwenye maji kitakachoingilia mtiririko wa asili wa maji katika chanzo cha maji; (h) mtu yeyote kuweka kitu chochote kwenye maji taka ambacho kinaweza kuathiri mtu yeyote au kuharibu mfumo wa tiba ya maji taka au kinachoweza kusababisha kuzuia mtiririko wa 7 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) maji taka; (i) mtu yeyote kulima kilimo cha matuta yanayosababisha maji kutuama ndani ya eneo la katikati ya mji; (j) kuchimba mchanga, kokoto au mawe katika vyanzo vya maji au mito barabarani; (k) kujenga kisima cha maji bila idhini ya maandishi ya Halmashauri; (l) kuchafua, kuoga, kufulia au kuvuruga maji yanayotumika kwa ajili ya matumizi ya binadamu au wanyama; (m) kuuza mchanga au kokoto na mawe kandokando mwa barabara; (n) kukata mti uliokwisha pandwa au ulioota wenyewe bila kupata kibali cha Halmashauri ambacho kitatolewa kwa masharti maalumu; (o) kuegesha au kufanya matengenezo ya gari, pikipiki au baiskeli kwenye maeneo ya makazi, bakaa za barabara au maeneo ya wazi; (p) kufanya biashara ya pombe ya aina yoyote katika nyumba au kwenye maeneo ya akiba za barabara au mitaani; (q) kuuza matunda au bidhaa nyingine za vyakula barabarani au kuanzisha masoko au magenge ya kuuzia matunda au vyakula au biashara nyingine ndogo bila ruhusa ya Halmashauri; (r) kuunganisha bomba la taka vimiminika katika mifereji ya maji ya mvua; (s) kufungulia au kutiririsha maji ya choo au taka vimiminika katika mkondo asili wa maji ya mvua au barabara au mfereji wa barabara wa maji ya mvua; (t) kujisaidia haja ndogo au haja kubwa barabarani, mitaani au sehemu yoyote isiyokusudiwa kwa madhumuni hayo; 8 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) (u) kubomoa jengo lolote kwa njia yeyote ile bila kupata kibali cha Halmashauri; (v) kufanya mikusanyiko ya kidini au kiutamaduni au kijamii wakati wa milipuko ya magonjwa ya kuambukiza, isipokuwa kwa ruhusa maalumu ya Halmashauri na usimamizi wa Afisa Afya; na (w) kuchoma moto taka za majumbani, makaratasi, majani, michongoma au takataka za aina yeyote katika maeneo ya makazi ya watu na kusababisha moshi kwa wakazi na kuchafua hewa kwa moshi na mazingira kwa ujumla; na (x) kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye pipa la taka au kitu chochote kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara. Makosa - 17 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinakataza mtu yeyote kutekeleza vitendo kadhaa vya usafi, taka, maji machafu, biashara ya chakula, maziko, matumizi ya vyoo, na matumizi ya maeneo/barabara bila ruhusa au kwa njia iliyopigwa marufuku.
17. Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa mtu yeyote: (a) kujenga choo chini ya umbali wa mita 60 kutoka kisimani, bwawani, mtoni, au chanzo kingine cha maji yanayotumika, kwa matumizi ya binadamu; (b) kutoa kinyesi au kusababisha kinyesi au mkojo au maji machafu yenye kinyesi kutoka kwenye choo chake au bafu lake au karo la kuoshea vyombo au nguo au kutoka kwenye bomba lolote linalochukua maji machafu na kuyatitirisha kwenye barabara au mitaani au kwenye mifereji ya maji ya mvua au mfereji wowote uliowazi; (c) kutupa taka au kusababisha mtu mwingine atupe na pasiporuhusiwa popote taka mahali Halmashauri; (d) kuuza chakula nje ya eneo ambalo halijasajiliwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (e) kuzika maiti katika eneo ambalo halikuainishwa kwa shughuli hiyo; (f) kutolipa ada ya taka kwa miezi miwili mfululizo; (g) kutembeza vyakula mitaani bila kibali cha 9 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) Halmashauri; (h) kuchezesha michezo au kuonyesha michezo au burudani katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri; (i) kuegesha gari bovu na kuliacha kando ya barabara au kichochoro au eneo la wazi ambalo halijaidhinishwa kwa shughuli za gereji na kuliacha zaidi ya siku moja; (j) kulima ndani ya vyanzo vya maji; (k) kutokuwa na pipa la taka lenye mfuniko katika eneo la biashara; (l) kutokuwa na choo au kukutwa na choo kibovu au kilichojaa; (m) kukutwa na shimo la maji taka lililojaa au ambalo halina mfuniko; (n) kuziba kichochoro; na (o) kutokuwa na chombo maalum cha kukusanyia taka ndani ya gari la abiria. Adhabu - 18 Verify source ↗
Mtu yeyote atakaye kiuka masharti ya Sheria
AI-assisted research summary: Anyone who violates the by-laws commits an offence and, if convicted, may be fined, imprisoned for up to 12 months, or receive both penalties.
18. Mtu yeyote atakaye kiuka masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na endapo akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kutumikia kifungo kisichozidi miezi kumi na miwili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja faini na kifungo. Kufifilisha kosa - 19 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii hadi shilingi 50,000, ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalum ya Jedwali la Pili.
19. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. 10 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) __________ JEDWALI KWANZA __________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 11) A. Ada ya Huduma ya Ukusanyaji na Uzoaji wa taka Namba. Aina ya Biashara au mchangiaji Kiwango cha Ada kwa Mwezi (Shilingi) Mgahawa mdogo au kibanda cha kuuzia chai au chakula. Kioski na glosari. Nyumba ya kulala wageni Zahanati (Taka zisizo hatari). Kituo cha Afya (Taka zisizo hatari). Fundi seremala. Fundi chuma. Karakana au gereji za magari. Karakana nyinginezo.
Part
JEDWALI KWANZA
- 16 Verify source ↗
Duka la kuuza samaki au nyama (bucha ya samaki au nyama)
AI-assisted research summary: Section 16 is titled “Duka la kuuza samaki au nyama (bucha ya samaki au nyama)”.
16. Duka la kuuza samaki au nyama (bucha ya samaki au nyama) - 17 Verify source ↗
Kibanda au kituo cha nyama choma au chipsi
AI-assisted research summary: This section is about an independent kibanda, or a nyama choma or chipsi stall.
17. Kibanda au kituo cha nyama choma au chipsi kinachojitegemea - 23 Verify source ↗
Kibanda au mwamvuli wa kuuza vocha za simu eneo la
AI-assisted research summary: This section concerns kiosks or umbrellas used to sell phone vouchers in the district council land reserve area.
23. Kibanda au mwamvuli wa kuuza vocha za simu eneo la Hifadhi la ardhi la Halmashauri ya Wilaya. - 33 Verify source ↗
Kila kaya
AI-assisted research summary: This section lists amounts associated with "kila kaya" (every household).
33. Kila kaya 11 3,000/= 3,000/= 5, 000/= 10, 000/= 15, 000/= 3,000/= 2, 000/= 5,000/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 2, 000/= 3,000/= 3,000/= 10,000/= 3,000/= 2,000/= 2,000/= 2,000/= 10, 000/= 2,000/= 3,000/= 2,000/= 10,000/= 2,000/= 2,000/= 2,000/= 2,000/= 5,000/= 5,000/= 2,000/= 3,000/= 500/= Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) - 35 Verify source ↗
Ofisi za Taasisi kama benki au posta na tasisi nyingine za
AI-assisted research summary: The excerpt mentions offices of institutions such as banks, post offices, and other financial institutions, and lists amounts of 2,000/= and 10,000/=, but it does not state the full rule here.
35. Ofisi za Taasisi kama benki au posta na tasisi nyingine za 2,000/= 10,000/= kifedha. - 36 Verify source ↗
Steshenari au maduka ya kuuza vitabu
AI-assisted research summary: Section 36 concerns stationers or shops that sell books.
36. Steshenari au maduka ya kuuza vitabu - 37 Verify source ↗
Duka la dawa muhimu za binadam au duka la dawa za mifugo
AI-assisted research summary: The provision lists amounts of 5,000/= and 3,000/= for a human essential medicines pharmacy or a veterinary pharmacy, and mentions agricultural inputs.
37. Duka la dawa muhimu za binadam au duka la dawa za mifugo 5,000/= 3,000/= au pembejeo za kilimo - 38 Verify source ↗
Hospitali au vituo vya Afya au zahanati za watu binafsi
AI-assisted research summary: Section title: private hospitals, health centers, or clinics.
38. Hospitali au vituo vya Afya au zahanati za watu binafsi - 39 Verify source ↗
Vyuma chakavu tani moja
AI-assisted research summary: Section 39 sets monthly waste-disposal fees for municipal dump use, with different amounts depending on whether waste volume is under one ton or one ton.
39. Vyuma chakavu tani moja 10,000/= 12,000/= B. Gharama za Utupaji Taka kwenye Jalala (jaa) la Taka la Halmashauri Na. 1 2 Kiasi cha Taka Taka za aina yoyote kwa kiwango cha ujazo chini ya tani moja. Taka za aina yoyote kwa kiwango cha ujazo tani moja. Ada kwa Mwezi (Shilingi) 30,000/= 50,000/= _____________ JEDWALI LA PILI ______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 19) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi ………………………………. Nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya…………………………………….…ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwamba mnamo tarehe ………… ya Mwezi….......... Mwaka …………….. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ………. ya Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Niko tayari kulipa kiasi cha Shilingi …………… kwa ajili ya kufifilisha Kosa nililotenda chini ya Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe ………..ya Mwezi…………………… Mwaka………………….. Jina ………………………………..……………. Saini……………………… MBELE YA: Jina ……………………………………………….…. Wadhifa ………………………..……………………. Saini …………………………………………………. Tarehe ………………………………………………. 12 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Tangazo La Seikali Na. 920 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya Kibondo imebandikwa kwenye sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo uliofanyika Tarehe 31 mwezi 01 Mwaka 2023 DIOCLES M. RUTEMA Mkurugenzi Mtendaji (W) Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo HABILI C. MASEKE Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 13
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in