Sheria Ndogo ya Usafi, Afya na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ya Mwaka 2023
This by-law is named the Arusha District Council Sanitation, Health and Environmental Conservation By-Law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usafi, Afya na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This by-law is named the Arusha District Council Sanitation, Health and Environmental Conservation By-Law, 2023. This by-law applies throughout the entire area of Arusha District Council. This section defines key terms used in the by-law. Halmashauri ina mamlaka ya kuingia na kukagua maeneo na majengo yaliyotajwa, kisha kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Halmashauri must set aside a waste-disposal area and supervise cleanliness; people in the Council area must protect the environment and follow Council health guidelines.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usafi, Afya na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ya Mwaka 2023
Showing 43 of 43
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This by-law is named the Arusha District Council Sanitation, Health and Environmental Conservation By-Law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usafi, Afya na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ya Mwaka 2023. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Arusha District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Arusha. - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya vibali au leseni mbalimbali zitolewazo na Halmashauri; “afisa mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “biashara” maana yake ni aina yoyote ya shughuli halali lengo ya kiuchumi inayomuingizia mtu kipato; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa madawa au sumu; “choo bora” maana yake ni choo chenye shimo lililojengwa madhubuti kwa sakafu, na kujengewa banda lililoezekwa lenye milango na mifumo 1 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) inayosafirisha uchafu kwenda kwenye imara shimo; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Arusha; “huduma” maana yake ni huduma inayotolewa chini ya Sheria Ndogo hii; “jengo” maana yake ni nyumba, hema, kibanda, kontena na aina yoyote ya muundo wa jengo linalotumika au la Halmashauri; lililopo ndani ya eneo lisilotumika “kaya” maana yake ni familia yenye baba, mama na watoto au mtu yeyote aliyefikia umri wa miaka kumi na nane awe na mtoto au bila mtoto; “kero” maana yake ni kitu chochote kinachoweza kuleta kinyaa kwa mtu kwa kuona, kunusa, hewa chafu, madhara au kuhatarisha afya ya binadamu pamoja na viumbe wengine; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa na Halmashauri; “kituo cha taka” maana yake ni kituo kilichowekwa kwa madhumuni ya jamii inayoishi au inayofanya kazi, biashara jirani na kituo hicho kuweka taka ngumu kabla ya kusafirisha hadi kwenye dampo rasmi la taka ngumu; “kizimba” maana yake ni kituo kilichojengwa maalimu kwa ajili ya kukusanyia au kuhifadhia taka kwa muda ili zisafirishwe kutupwa kwenye dampo; “mabwawa ya maji taka” maana yake ni mabwawa yaliyojengwa kwa ajili ya kuhifadhia maji taka; “maji taka” maana yake ni maji machafu yanayozalishwa kutokana na shughuli za majumbani au viwandani; “mazalia ya wadudu” maana yake ni sehemu ambayo wadudu hufanya mazalia au kuishi kwa minajilia ya kufanya mzunguko wa maisha; “mifugo” maana yake ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku, 2 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) na wanyama wengine wafugwao na binafsi; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha; “mtandao wa maji taka” maana yake ni mfumo wa bomba kuu lililojengwa kwa madhumuni ya kupokea na kusafirisha maji taka toka kwenye Mifereji ya maji na kuyapeleka kwenye Mabwawa ya maji taka; “pipa la taka” maana yake ni chombo chochote chenye mfuniko kinachoweza kuhifadhi taka ngumu; “taka za bustani” maana yake ni taka zinazotokana na shughuli za kuandaa, kulima, kutengeneza au kupalilia bustani; “taka hatarishi” maana yake ni taka zozote zinazoweza kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu na viumbe hai wengine katika mazingira; “taka za nyumbani” maana yake ni taka zote zinazozalishwa kutokana na shughuli za kila siku za nyumbani; “taka ngumu” maana yake ni taka zote zisizo katika mfumo kimiminika; “taka za viwandani” maana yake ni taka zote zilizo katika mfumo yabisi, kimiminika au gesi zitokanazo na shughuli za viwandani; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa huduma mbalimbali au zinazofanywa katika eneo la Halmashauri; na shughuli “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi au iliyoteuliwa kukusanya ushuru kwa kampuni niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii. Ukaguzi wa mazingira - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuingia na
AI-assisted research summary: Halmashauri ina mamlaka ya kuingia na kukagua maeneo na majengo yaliyotajwa, kisha kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii.
4. Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuingia na kukagua nyumba, kiwanja, barabara, njia, uchochoro, mfereji au ardhi na kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. 3 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) Wajibu wa kutunza mazingira - 5 Verify source ↗
(1) Ni wajibu wa Halmashauri kutenga eneo
AI-assisted research summary: Halmashauri must set aside a waste-disposal area and supervise cleanliness; people in the Council area must protect the environment and follow Council health guidelines.
5.-(1) Ni wajibu wa Halmashauri kutenga eneo kwa ajili ya kutupa taka ngumu au laini na kusimamia kwa karibu usafi katika eneo lake. (2) Ni wajibu wa mtu yeyote anayeishi, anayetoa huduma, anayepata huduma au anayepita katika eneo lolote ndani ya Halmashauri kutunza mazingira. (3) Ni wajibu wa mtu yeyote anayeishi au kutoa huduma ndani ya Halmashauri kuzingatia miongozo, kanuni na taratibu za kiafya zilizoweka au zitakazowekwa na Halmashauri. Wajibu wa kujenga na kutumia choo bora - 6 Verify source ↗
(1) Ni wajibu wa kila mtu mwenye mamlaka ya
AI-assisted research summary: Wenye kusimamia majengo yanayotumiwa ndani ya Halmashauri lazima wahakikishe kuna choo bora, na kila mtu ndani ya Halmashauri lazima atumie choo.
6.-(1) Ni wajibu wa kila mtu mwenye mamlaka ya usimamizi wa jengo linalotumiwa na mtu au watu ndani ya Halmashauri kuhakikisha kwamba kunakuwa na choo bora. (2) Ni wajibu wa kila mtu ndani ya Halmashauri kuhakikisha kuwa anatumia choo. Choo sehemu ya kazi - 7 Verify source ↗
Kila mmiliki au msimamizi wa jengo lolote
AI-assisted research summary: Mmiliki au msimamizi wa jengo linalotumika kwa biashara lazima ajenge choo ndani ya jengo hilo.
7. Kila mmiliki au msimamizi wa jengo lolote lonalotumika kwa biashara atapaswa kujenga choo katika jengo hilo. Choo cha watu wenye mahitaji maalumu - 8 Verify source ↗
Mtu yeyote anaetaka kujenga choo cha watu
AI-assisted research summary: Mtu anayetaka kujenga choo cha watu wenye mahitaji maalumu lazima azingatie masharti atakayopewa na Halmashauri.
8. Mtu yeyote anaetaka kujenga choo cha watu wenye mahitaji maalumu atatakiwa kuzingatia masharti atakayopewa na Halmashauri. Choo cha muda - 9 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayetaka kujenga au kuweka
AI-assisted research summary: Anayetaka kujenga au kuweka choo cha muda katika maeneo ya ujenzi, sherehe, kambi au mkusanyiko wa muda lazima apate idhini na usimamizi wa Halmashauri.
9.-(1) Mtu yeyote anayetaka kujenga au kuweka choo cha muda sehemu ya ujenzi, sherehe, kambi au sehemu yoyote ambayo inakutanisha watu kwa muda ni lazima ajenge au aweke choo kwa idhini na usimamizi wa Halmashauri. (2) Choo cha muda kitahamishwa au kuvunjwa na kufukiwa baada ya kazi au kusudio kumalizika. 4 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) Umbali wa kujenga choo kutoka kwenye chanzo cha maji. Wajibu wa kutupa taka katika maeneo maalumu Ushuru wa taka ngumu
Part
sehemu yoyote ambayo inakutanisha watu kwa muda ni
- 10 Verify source ↗
Mtu yeyote atatakiwa kujenga choo umbali wa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatakiwa kujenga choo umbali wa zaidi ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji.
10. Mtu yeyote atatakiwa kujenga choo umbali wa zaidi ya mita sitini kutoka kwenye chanzo cha maji. - 11 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima iweke utaratibu wa ukusanyaji na usafirishaji wa taka; kila mtu anatakiwa kutupa taka kwenye kituo au kizimba, kila kaya iwe na chombo chenye mfuniko kwa taka ngumu, na wazalishaji wa taka hatarishi wafuate taratibu maalumu za kuzitupa au kuziteketeza.
11.-(1) Halmashauri itaweka utaratibu wa taka kutoka majumbani, kukusanya na kusafirisha kwenye vituo vya taka au vizimba hadi kwenye dampo kwa ratiba ambayo kila mtu atalazimika kuifuata. (2) Kila mtu ana wajibu wa kutupa taka katika kituo cha taka au kizimba. (3) Kila kaya inapaswa kuwa na chombo maalumu chenye mfuniko kitakachotumika kutupia taka ngumu na kuzimwaga katika kituo cha taka au kizimba au kwenye gari la taka kadiri ya ratiba ilivyo katika kata, kijiji au kitongoji. (4) Mtu yeyote anayezalisha taka hatarishi atalazimika kuzitupa au kuteketeza kwa kuzingatia taratibu za utupaji wa taka hatarishi. - 12 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atawajibika kulipa ushuru wa
AI-assisted research summary: Anyone must pay the solid waste levy at the rates set out in the First and Second Schedules, monthly, by the fifth day of the following month.
12.-(1) Mtu yeyote atawajibika kulipa ushuru wa taka ngumu kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza na la Pili. (2) Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru wa taka. (3) Ushuru wa taka utalipwa kila mwezi na mwisho wa kulipa utakuwa tarehe tano ya kila mwezi unaofuata. (4) Mtu yeyote anayezalisha taka nyingi zinazoilazimu Halmashauri au wakala kuzoa kwa ratiba tofauti na ratiba iliyowekwa atalazimika kulipa gharama za kuzoa na kusafirisha taka hizo. Taratibu za kutupa maji taka - 13 Verify source ↗
(1) Mtu anayezalisha maji taka anawajibu
AI-assisted research summary: Wastewater producers must ensure wastewater goes into a wastewater system or an approved pit, and factory owners must direct industrial wastewater into an official disposal system or an approved pit or pond.
13.-(1) Mtu anayezalisha maji taka anawajibu kuwa na karo au kuhakikisha anayaelekeza katika mfumo wa maji taka au shimo rasmi lililoandaliwa kwa ajili ya 5 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) Wajibu wa kudhibiti na kuondoa mazalia ya mbu na wadudu wengine Utaratibu wa kuchinja na kusafirisha nyama kusafirisha au kupokea au kuhifadhi maji taka. (2) Wamiliki i wa viwanda wana wajibu wa kuelekeza maji taka ya viwandani katika mfumo rasmi wa kusafirisha maji taka au kuelekeza kwenye shimo au bwawa lililoandaliwa rasmi kwa ajili ya kutakasa au kuhifadhi maji ya viwanda. - 14 Verify source ↗
Kila mtu ana wajibu wa kudhibiti na kuondoa
AI-assisted research summary: Everyone has a duty to control and remove mosquito and other insect breeding sites.
14. Kila mtu ana wajibu wa kudhibiti na kuondoa mazalia ya mbu na wadudu wengine. - 15 Verify source ↗
(1) Kila mfugaji atatakiwa kupeleka mfugo au
AI-assisted research summary: Wafugaji lazima wapeleke mifugo machinjioni; kuchinja nje ya machinjio ni marufuku isipokuwa baada ya kumjulisha Afisa Mwidhiniwa. Duka la nyama lazima litimize masharti ya usafi, na wauzaji wa nyama lazima wafuate ukaguzi, sare, vipimo vya afya, na kanuni za usafirishaji.
15.-(1) Kila mfugaji atatakiwa kupeleka mfugo au mifugo yake machinjioni au mahali huduma hiyo inapopatikana na itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchinja mfugo au mifugo mahali pengine popote ambapo si machinjio isipokuwa kwa kutoa taarifa kwa Afisa Mwidhiniwa na atalazimika kulipia gharama za machinjio kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. (2) Duka la nyama linatakiwa kuwa na- (a) mwanga wa kutosha, kusakafiwa kwa marumaru nyeupe kwa urefu wa futi sita kutoka usawa wa ardhi; (b) gogo la kukatia nyama au misumeno maalumu ya kukatia nyama; (c) maji safi, meza, visu, mzani wa kawaida au wa kielektroniki na vyuma vya kuning’inizia nyama; (d) wavu wa kuzuia inzi na wadudu wengine kwenye milango na madirisha; na (e) pipa la kuhifadhia taka ngumu na laini. (3) Nyama inayouzwa itakaguliwa na mkaguzi aliyeidhinishwa na kugongwa muhuri na muuzaji atahakikisha kuwa nyama inauzwa ndani ya jengo 6 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) (4) Muuzaji atahakikisha anavaa sare maalum na anapima afya yake kila baada ya miezi sita na kuhakikisha anakuwa na cheti cha upimaji; (5) Mfanyabiashara wa atatakiwa kusafirisha nyama kutoka machinjioni kwa kutumia gari maalumu lililosajiliwa na kupewa cheti maalumu na endapo atatumia usafiri wa pikipiki au baiskeli atatakiwa kubeba nyama kwa kutumia chombo maalumu kilichoidhinishwa na Halmashauri. nyama (6) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia kwenye machinjio au duka la nyama kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hii ikibainika kuna jambo au mazingira yoyote ambayo ni hatarishi kwa afya ya binadamu ataamuru machinjio au bucha hilo kufungwa au kutekeleza maelekezo atakayoyatoa au kulipa faini kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (7) Mmiliki wa bucha au Muuzaji wa nyama atalazimika kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakaguzi mara atakapotakiwa kufanya hivyo wakati wote wa ukaguzi. - 16 Verify source ↗
(1) Mtu anatakiwa kuchukua
AI-assisted research summary: People must take reasonable precautions to prevent disease and fire, and certain persons or bodies in congregated areas must accept vaccination when directed by the Ministry of Health.
16.-(1) Mtu anatakiwa kuchukua tahadhari zinazokubalika kwa mujibu wa Sheria za nchi ili kuzuia kutokea kwa magonjwa yote ya kuambukiza au yasiyoambukiza na kuchukua tahadhari dhidi ya moto kwa kuweka vifaa vya tahadhari ya moto katika eneo lake ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri. (2) Mtu au taasisi au uongozi wa eneo lolote lenye mkusanyiko wa watu atawajibika kukubali kupatiwa chanjo ya kuzuia au kutibu ugonjwa wowote kama itakavyoelekezwa na Wizara ya Afya katika nyakati tofauti. Udhibiti na uzuiaji wa magonjwa ya mlipuko na tahadhari ya moto Usafi na utengenezaji wa vyakula, - 17 Verify source ↗
(1) Mtu au mmiliki wa maduka, hoteli au
AI-assisted research summary: Watu au wamiliki wa maduka, hoteli au migahawa wanaouza au kutangaza chakula na vinywaji katika maeneo fulani lazima wapate kibali na usajili kutoka Halmashauri kupitia Afisa Mwidhiniwa.
17.-(1) Mtu au mmiliki wa maduka, hoteli au migahawa atakayetengeneza au kuonesha kwa kuuza 7 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) maji na vinywaji vingine chakula au kutangaza ili kufanya biashara ya kuuza chakula mahali popote, mtaani, kichochoroni au katika nyumba yoyote atalazimika kupata kibali na usajili kutoka kwa Halmashauri kupitia kwa Afisa Mwidhiniwa. (2) Mtu hataruhusiwa kuuza au kutangaza vyakula au vinywaji katika eneo la wazi lisilojengwa na vifaa vya isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kudumu Halmashauri. (3) Halmashauri itakuwa na uwezo wa kuzuia upishi au utengenezaji wa pombe na vyakula katika mazingira yasiyoridhisha kiafya. (4) Kila mfanyabiashara wa bidhaa za mboga mboga na matunda atalazimika kuuza bidhaa hizo juu ya kichanja. Unyunyiziaji na upuliziaji wa viuatilifu - 18 Verify source ↗
Mtu anayeendesha biashara ya unyunyiziaji au
AI-assisted research summary: Mtu anayeendesha biashara ya kunyunyizia au kupulizia viuatilifu vya kuua wanyama au wadudu waharibifu lazima apate kibali cha Halmashauri.
18. Mtu anayeendesha biashara ya unyunyiziaji au upuliziaji wa viuatilifu vya kuua wanyama au wadudu waharibifu atalazimika kupata kibali cha Halmashauri. Usalama wa afya na tahadhari katika viwanda, nyumba na maeneo ya wazi - 19 Verify source ↗
(1) Mtu, taasisi au kampuni inayozalisha au
AI-assisted research summary: Wazalishaji wa taka zenye madhara lazima waandae utaratibu salama wa kuzihifadhi, na msimamizi wa familia au biashara lazima ahakikishe nyumba au mahali pa biashara ni safi na salama.
19.-(1) Mtu, taasisi au kampuni inayozalisha au kwa asili ya kazi wanazozifanya zinawapelekea kuzalisha uchafu, takataka, vumbi ama kitu kingine kama hicho chenye madhara kwa afya ya binadamu au viumbe wengine atalazimika kuandaa utaratibu wa kuhifadhi taka hizo katika hali isiyoweza kudhuru afya ya binadamu na viumbe wengine. (2) Mtu ambaye ni msimamizi wa familia au biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa nyumba au mahali anapoishi au kufanya biashara panakuwa safi na salama kwa maisha ya binadamu. Upandaji na utunzaji wa miti - 20 Verify source ↗
(1) Bila kuathiri matakwa ya kijiografia na
AI-assisted research summary: Wamiliki wa ardhi ndani ya Halmashauri lazima wapande miti, wakazi washiriki katika upandaji miti wa pamoja, na mtu anayetaka kuvuna miti apate kibali kutoka Halmashauri na alipe ada.
20.-(1) Bila kuathiri matakwa ya kijiografia na kitaalamu ya upandaji na ukuzaji wa mazao mengine kila mmiliki wa ardhi katika eneo la Halmashauri atapanda angalau miti mitano katika eneo la kiwanja cha kawaida 8 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) cha makazi na kupanda angalau miti kumi kila mwaka kwa mashamba yenye ukubwa wa kuanzia hekari tatu. (2) Mkazi wa Halmashauri atakuwa wajibu wa kushiriki katika zoezi la upandaji miti la pamoja litakaloandaliwa na Halmashauri kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa. (3) Mtu anayetaka kuvuna mti au miti katika eneo lolote ndani ya Halmashauri atalazimika kupata kibali kutoka Halmashauri kwa kulipia ada ya kibali. - 21 Verify source ↗
(1) Serikali ya Kijiji na Kamati ya Maendeleo
AI-assisted research summary: Village government bodies and residents must help identify, protect, and care for water sources, and people planning construction or economic activity must get a council certificate first.
21.-(1) Serikali ya Kijiji na Kamati ya Maendeleo ya Kata itabainisha na kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji vyanzo vyote vya maji vinavyopatikana katika eneo lao ikiwa ni pamoja na kuleta mapendekezo yaliyopitishwa na wananchi kupitia Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi, kuhusu namna ya kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji katika maeneo yao. (2) Kila mtu atatunza vyanzo vya maji vilivyoko katika Kijiji au Kitongoji anachoishi ikiwa ni pamoja na kushiriki zoezi la kufanya usafi na kupanda miti kwenye vyanzo vya maji kulingana na ratiba itakayowekwa. (3) Mtu yeyote anayetaka kujenga nyumba au kufanya shughuli yoyote ya kiuchumi atalazimika kupata cheti maalumu kutoka Halmashauri kitakacho thibitisha kwamba jengo linalojengwa au mradi haupo ndani ya Mita Sitini kutoka kwenye chanzo cha maji na kwamba mradi husika hautakuwa na athari kwenye vyanzo vya maji. - 22 Verify source ↗
Mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mtu anayependekeza au kuendesha mradi fulani, au kujenga jengo la huduma kama shule, hoteli, kanisa au kiwanda, lazima afanyiwe ukaguzi wa mazingira na apate cheti kinachotajwa na Halmashauri.
22. Mtu yeyote anayeendesha mradi au anayekusudia kuanzisha mradi mdogo au mkubwa au kufanya ujenzi wa jengo lolote la kutolea huduma kama shule, hoteli, kanisa au kiwanda atalazimika kufanyiwa ukaguzi wa mazingira na kupata cheti kutoka ada ya ukaguzi kama Halmashauri na kulipa 9 Utunzaji wa vyanzo vya maji Ukaguzi wa mazingira Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. Wajibu wa kushiriki usafi wa pamoja kila mwezi - 23 Verify source ↗
Kila mtu atakuwa na wajibu wa kushiriki
AI-assisted research summary: Everyone must take part in the cleaning exercise on the last Saturday of every month.
23. Kila mtu atakuwa na wajibu wa kushiriki zoezi la usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi katika maeneo yatakayokuwa yamepangwa na kwa muda uliopangwa. Utunzaji wa maeneo yasiyotumika Utaratibu wa ufugaji - 24 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa jengo, kontena, gari,
AI-assisted research summary: Wamiliki wa majengo, magari, kontena, viwanja, mashamba na vitu vingine vilivyo katika mazingira lazima wakitunze na kukiweka safi ili kisilete kero, makazi ya viumbe wanaoweza kudhuru, maficho ya wahalifu, au sehemu ya kutupia taka.
24.-(1) Kila mmiliki wa jengo, kontena, gari, kiwanja, shamba na kitu kingine chochote kilichopo kwenye mazingira atawajibika kukitunza kwa kufanya usafi na kukiweka katika hali ambayo hakiwezi kusababisha kero kwa watu au kufanyika makazi ya viumbe wanaoweza kumuathiri mtu au kiumbe chochote au kuwa maficho ya wahalifu au sehemu ya kutupia taka. (2) Halmashauri itakuwa na jukumu la kutunza jengo, eneo au kitu kingine chochote kilichotelekezwa ambacho mmiliki wake hajulikani na ambacho kinaleta kero katika mazingira na kitatangazwa katika maeneo ya wazi na kwenye vyombo vya habari kwa muda wa siku tisini, endapo mmiliki huyo hatajitokeza Halmashauri itafanya utaratibu wa kutwaa, na endapo mmiliki atajitokeza baadaye au wakati utaratibu wa kutwaa eneo au kitu hicho unafanyika atalazimika kulipa faini na gharama zote zilizotumika kusafisha na kutunza eneo, jengo au kitu hicho. - 25 Verify source ↗
(1) Mtu anayefanya shughuli za ufugaji katika
AI-assisted research summary: Livestock keepers in the Ngaramtoni Small Town Authority wards and urban areas must keep livestock indoors, and anyone starting a livestock project must have the council’s environmental inspection certificate.
25.-(1) Mtu anayefanya shughuli za ufugaji katika kata zote zilizopo chini ya Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni na maeneo ya miji atalazimika kufanya ufugaji wa ndani. (2) Mtu anayekusudia kuanzisha mradi wa ufugaji atalazimika kuwa na cheti cha ukaguzi wa mazingira cha Halmashauri. (3) Halmashauri itakamata mfugo au mifugo yoyote itakayoonekana inazurura hovyo katika eneo la 10 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) Halmashauri. (4) Mfugo utakaokamatwa chini ya aya ndogo ya (3) utalipiwa faini ya Shilingi elfu kumi kwa kila siku. (5) Endapo mfugo uliokamatwa hautachukuliwa na mmiliki ndani ya kipindi cha siku saba tangu kukamatwa, Halmashauri itakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mfugo huo baada ya kupata idhini ya Mahakama, na fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmliki wa mfugo huo baada ya kutoa faini inayodaiwa, gharama za kuhifadhi mfugo, gharama ya Mahakama na gharama ya mnada. (6) Bila kuathiri aya ndogo ya (5), Halmashauri kabla ya kuuza mfugo huo kwa mnada itamjulisha mmliki na umma juu ya kusudio hilo. na (7) Endapo kutatokea kufa kwa mifugo au mfugo kutokana ile, Halmashauri yoyote haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama vifo hivyo vitakuwa vimesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri sababu Udhibiti wa sauti na mitetemo Udhibiti wa uchafuzi wa hewa - 26 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mtu anayetaka kufanya matangazo, mkutano, tamasha, au mkusanyiko wa nje lazima apate kibali kutoka kwa Halmashauri. Pia, kumbi za muziki, baa, vilabu, na nyumba za ibada zinazofanya mikesha lazima zizuie sauti kuwasumbua majirani au ziwe na vifaa vya kuzuia sauti kutoka nje.
26.-(1) Mtu yeyote anayekusudia kufanya matangazo au mkutano au tamasha au mkusanyiko wowote wa nje atahakikisha anapata kibali kutoka kwa Halmashauri. (2) Kumbi zote za muziki au baa au kilabu au nyumba za ibada zenye kufanya mikesha zitalazimika kuweka sauti isiyoleta kero kwa majirani au kuwa na vifaa maalumu vya kuzuia sauti kutoka nje - 27 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuchoma taka hatarishi isipokuwa kwa utaratibu na kanuni maalumu; wazalishaji wa taka hizo lazima wawe na kichomea taka kilichoandaliwa kitaalamu, na wenye viwanda, mashamba au miradi inayotumia au kuzalisha kemikali lazima wasiiweke katika eneo la makazi na wawe na cheti cha ukaguzi wa mazingira.
27.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma taka hatarishi zinazoruhusiwa isipokuwa kwa taka kuteketezwa kwa utaratibu na kanuni maalumu. (2) Mtu yeyote anayezalisha taka hatarishi atalazimika kuwa na kichomea taka kilichoandaliwa kitaalamu kwa ajili ya kuchomea taka hizo. 11 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) Usalama katika mazingira ya migodi na ukaguzi (3) Mtu yeyote mwenye kiwanda, shamba au mradi wowote unaotumia au kuzalisha kemikali hataweka kiwanda, shamba au mradi huo katika eneo la makazi na atalazimika kuwa na cheti cha ukaguzi wa mazingira kwa mujibu Sheria Ndogo hii. - 28 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anaemiliki mgodi uliorasmi na
AI-assisted research summary: Wamiliki wa migodi ndani ya eneo la Halmashauri lazima wajisajili na watambuliwe, migodi ichunguzwe na kupatiwa cheti cha mazingira, na migodi isiyo rasmi iliyokaguliwa ifuate utaratibu wa kurasimishwa na kupata leseni ndani ya miezi sita.
28.-(1) Mtu yeyote anaemiliki mgodi uliorasmi na usio rasmi ndani ya eneo la Halmashauri atalazimika kusajiliwa na kutambuliwa na Halmashauri ndani ya siku tisini tangu tarehe ya kuanza kutumika kwa Sheria Ndogo hii, na atawajibika kulipa ada ya urejeshaji mazingira (2) Migodi yote rasmi na isiyo rasmi itapaswa kukaguliwa na kupata cheti cha ukaguzi wa mazingira kutoka Halmashari. (3) Mgodi wowote usio rasmi uliokaguliwa na kupatiwa cheti na Halmashauri utalazimika kufuata utaratibu wa kurasimisha machimbo hayo na kupata leseni ndani ya miezi sita tangu tarehe ya kukaguliwa na kupewa cheti cha Halmashauri, na yeyote atakayeshindwa kutimiza masharti hayo atafungiwa mgodi na kulipa faini ya shilingi laki tatu. (4) Afisa Mtendaji wa Kijiji atakuwa na wajibu wa kuorodhesha migodi yote iliyopo katika eneo lake na kuwasilisha kwa Mkurugenzi. (5) Mtu yeyote anayetaka kuanzisha mgodi mpya atalazimika kupata kibali pamoja na cheti cha ukaguzi wa Mazingira cha Halmashauri sambamba na kufuata taratibu zote za kisheria za kuanzisha na kimiliki migodi. (6) Kwa madhumuni ya aya hii “mgodi” unamaanisha machimbo ya aina yoyote ya madini ikiwemo udongo, moramu, kokoto na vifusi. Shughuli za kilimo - 29 Verify source ↗
(1) Mtu anayefanya shughuli za kilimo ndani
AI-assisted research summary: Wakulima ndani ya Halmashauri lazima wazingatie kilimo rafiki kwa mazingira na baadhi ya shughuli, kama kuchoma shamba au miradi ya umwagiliaji, zinahitaji kibali cha Halmashauri.
29.-(1) Mtu anayefanya shughuli za kilimo ndani ya Halmashauri atalazimika kuzingatia kilimo rafiki kwa mazingira. 12 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) (2) Mtu anayeandaa shamba kwa kuchoma moto atalazimika kupata kibali cha Halmashauri. (3) Mtu anayelima kwenye mteremko analazimika kuzingatia kanuni za kilimo kwenye miteremko au miinuko. (4) Mtu anaelima karibu na vyanzo vya maji atalazimika kuwa nje ya mita sitini na atatunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti na mimea inayokubalika katika maeneo hayo. (5) Mtu yeyote anayefanya mradi wa kilimo cha umwagiliaji atalazimika kupata kibali cha Halmashauri. Shughuli za usafirishaji na utunzajia wa barabara Maeneo ya kuoshea magari - 30 Verify source ↗
(1) Mmiliki wa
AI-assisted research summary: Wamiliki wa vyombo vya usafiri lazima wahakikishe mizigo yao ni ya uzito unaoruhusiwa kwenye barabara husika, watu lazima wapitishe mifugo kwenye barabara rasmi zilizotengwa kwa mifugo tu, na wamiliki au wapangaji lazima waweke mifereji au kalavati za maji ya mvua zilizo mbele ya nyumba zao zikiwa safi muda wote.
30.-(1) Mmiliki wa cha usafiri atahakikisha kuwa chombo chake cha usafiri kinabeba mzigo wenye uzito unaokubalika katika barabara husika ili kuepusha uharibifu wa barabara za Halmashauri. chombo (2) Mtu atatakiwa kupitisha mifugo katika barabara rasmi zilizotengwa kwa ajili ya kupitisha mifugo tu. (3) Mmiliki wa nyumba au kiwanja au mpangaji atahakikisha mtaro au kalavati ya kutiririsha maji ya mvua iliyo kando ya barabara mbele ya nyumba yake inakuwa safi muda wote. - 31 Verify source ↗
Mtu anayekusudia kuanzisha biashara ya
AI-assisted research summary: Mtu anayetaka kuanzisha biashara ya kuosha magari lazima aombe kibali kutoka Halmashauri; pia ukaguzi wa mazingira utafanyika, na afisa mwidhiniwa atatoa cheti cha ukaguzi baada ya kuridhika na baada ya ada iliyotajwa kulipwa.
31. Mtu anayekusudia kuanzisha biashara ya kuosha magari atalazimika kuomba kibali kutoka Halmashauri, na ukaguzi wa mazingira utafanyika na afisa mwidhiniwa akiridhika atampatia cheti cha ukaguzi wa mazingira baada ya kulipa ada kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. Matangazo na mikutano - 32 Verify source ↗
Mtu anayekusudia kufanya matangazo au
AI-assisted research summary: A person planning advertisements or a public meeting must apply to the Council for a permit and pay the fees listed in Schedule Three.
32. Mtu anayekusudia kufanya matangazo au mkutano wa hadhara atatakiwa kuomba kibali kwa Halmashauri na kulipa ada kama zilivyoanishwa katika Jedwali la Tatu. 13 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) Biashara ya kuupulizia na kuua wadudu
Part
Jedwali la Tatu.
- 33 Verify source ↗
Mtu anayekusudia kuanzisha biashara ya
AI-assisted research summary: Mtu anayetaka kuanzisha biashara ya kupulizia dawa ya kuuwa wadudu waenezao magonjwa kwa binadamu lazima aombe kibali kutoka halmashauri; pia afisa mwidhiniwa hufanya ukaguzi wa mazingira na, akiridhika, hutoa cheti baada ya kulipwa ada iliyotajwa katika Jedwali la Nne.
33. Mtu anayekusudia kuanzisha biashara ya kupulizia dawa ya kuuwa wadudu waenezao magonjwa kwa binadamu atalazimika kuomba kibali kutoka halmashauri, na ukaguzi wa mazingira utafanyika na afisa mwidhiniwa akiridhika atampatia cheti cha ukaguzi wa mazingira baada ya kulipa ada kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Nne. Uteuzi wa wakala - 34 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba yake.
34.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kukusanya ushuru kwa niaba yake. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa aya ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa: Makosa (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 35 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akifanya mojawapo ya vitendo vilivyokatazwa kuhusu usafi, taka, maji taka, vibali, kilimo, mifugo na mazingira.
35. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo:- (a) atamzuia Mkurugenzi, Afisa Mwidhiniwa au wakala kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) atajisaidia haja kubwa au ndogo mahali ambapo sio chooni; (c) hatajenga choo katika jengo au eneo lake; (d) atachimba shimo la maji taka bila kibali cha Halmashauri; (e) atasababisha shimo la maji taka au bwawa la maji taka au chemba ya choo kupasuka au kuziba kwa bomba la maji taka na kutiririsha 14 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) maji taka; (f) atatupa taka katika eneo ambalo halikutengwa kwa ajili ya kutupia taka; (g) atasafirisha taka bila kuzifunika; (h) atatupa taka hatarishi katika mazingira yoyote bila kuchukuwa tahadhari au kufuata taratibu; (i) atakusanya ushuru wa taka bila kibali cha Halmashauri au kuchelewa kulipa ada ya taka kwa muda ulioainishwa; (j) atatiririsha au kumwaga maji taka barabarani, uchochoroni, kwenye mifereji, mtoni, kwenye vyanzo vya maji au sehemu nyingine yoyote isiyotengwa kwa ajili ya kuhifadhia au kusafirisha maji taka; (k) atatupa kemikali yabisi, kimiminika au kemikali za gesi katika maeneo yasiyo rasmi; (l) atahifadhi au kuweka viuatilifu kwenye chumba au ghala au stoo au eneo linalofanana na hilo bila idhini ya Halmashauri; (m) ataruhusu mazalia ya mbu au wadudu wengine; (n) atatelekeza eneo au kitu chochote anachomiliki kiasi cha kuleta kero au kusababisha madhara kwa wengine; (o) ataanzisha au kuendesha biashara ya kuosha magari bila kibali cha Halmashauri; (p) ataelekeza mtaro wa maji ya mvua au maji taka au kutupa takataka barabarani; (q) atasafirisha mzigo uliozidi uzito, au kupitisha mfugo au mifugo au kuelekeza maji machafu au kutupa takataka barabarani; (r) ataacha mitaro ya maji ya mvua iliyopo mbele ya nyumba kuwa michafu; (s) atafanya shughuli za kilimo kinyume na shughuli za Sheria Ndogo hii; 15 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) (t) atamiliki au kuanzisha mradi wa kufuga nguruwe bila ya kuwa na cheti cha ukaguzi wa mazingira; (u) ataizurulisha au kupitishwa katika barabara za Halmashauri ambazo si rasmi kwa ajili ya mifugo; (v) atauza au kutaka kuuza kwenye halaiki ama hadharani kwenye kundi la watu ama kwa mtu mmoja pombe, maji ama chakula bila kupata idhini ya Halmashauri; (w) atauza mboga mboga au matunda kwa kuweka ardhini; na (x) atauza au kutumia au kutoa kama msaada kwa mtu bidhaa yoyote ambayo imekwisha muda wa matumizi; (y) ataweka nembo yoyote juu ya kifungashio cha bidhaa ya chakula ambayo haina uhalisia wa kile kilichopo ndani; (z) atauza vipodozi vyenye viambata sumu kwa mujibu wa Sheria na kanuni zinazo simamia uuzaji na utengeneza jiwa vipodozi; (aa) atakata mti bila kibali, au kuacha eneo la ardhi analolimiliki bila kupanda miti, au atakayekaidi kushiriki zoezi la pamoja la upandaji miti; (bb) atajenga ndani ya mita sitini kutoka kwenye chanzo cha maji, kufanya shughuli yoyote ya kiuchumi inayoharibu chanzo, kuelekeza maji taka ya nyumbani au viwandani au kufua nguo, kuosha vyombo au kuoga kwenye chanzo cha maji; (cc) ataanzisha mgodi kwenye eneo la makazi ya watu, kando kando ya miundombinu ya barabara, shule na maeneo mengine ya huduma za jamii, au kuchimba na kuacha 16 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) mashimo yanayohatarisha maisha ya watu katika mazingira; au (dd) ataweka au kutaka kuweka kitu chochote chenye kutoa sauti au mitetemo inayoweza kuleta madhara ya kiafya au ambayo ni kero na kwa jamii inayozunguka eneo hilo. Adhabu - 36 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii anatenda kosa na akihukumiwa anaweza kutozwa faini, kifungo cha hadi miezi 12 jela, au vyote viwili.
36. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini ya kiasi kisichopungua Shilingi elfu hamsini na kisichozidi Shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. Kufifilisha kosa - 37 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza faini mtu
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza faini mtu aliyekosa chini ya Sheria Ndogo hii, ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa fomu maalumu ya Jedwali la Tano.
37. Mkurugenzi anaweza kumtoza faini mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii, kiasi cha Shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa fomu maalumu hiari iliyoambatanishwa kwenye Jedwali la Tano la Sheria Ndogo hii. kujaza tayari kuwa na _____ JEDWALI LA KWANZA _____ (Limetengenezwa chini ya aya ya 12(1)) USHURU WA UZOAJI NA UTUPAJI TAKA NGUMU Namba. Aina ya Jengo
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: The provision lists monthly fee amounts for different business types.
6. Duka la jumla Duka la rejareja au nafaka au Steshenari au stoo ya vinywaji Taka za nyumbani Fundi au msafisha viatu Kibanda cha matunda au genge Bucha Kiwango cha Ushuru kwa Mwezi (Shilingi) 10,000/= 5,000/= 3,000/=- 2000/= 2000/= 5000/= 17 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) - 49 Verify source ↗
Section 49
AI-assisted research summary: This section lists fees for many businesses, services, and waste-related activities.
49. Mama au Baba lishe Mashine ya kusaga na kukoboa Duka la dawa muhimu Duka la vipuri Saluni ya kiume au kike Studio Fundi cherehani Gereji ya kuchomelea Baa Duka la vinywaji baridi na pombe Duka la vifaa vya ujenzi Karakana Gereji Mgahawa Sehemu ya kutengeneza matofali Mashine ya kuchana mbao Mini Supermarket Kituo cha mafuta Fundi seremala Kiwanda kikubwa Kiwanda cha kati Kiwanda kidogo Hoteli kubwa Hoteli ya kati Nyumba ya kulala wageni Hospitali Kituo cha afya na Zahanati Ofisi Mkandarasi wa majengo Duka la vifaa vya magari Ofisi ya Wakili Ofisi ya mtaalamu wa kuuwa wadudu Ghala kubwa Ghala la kati Ghala dogo Ofisi ya Mhasibu au Mkaguzi na huduma za kompyuta Taka za bustani Jumba la sinema karakana Ada ya kutupa taka kutoka kwenye mkokoteni ndani ya kizimba Huduma ya kufua na kunyoosha Uwanja wa maonesho Kiwanja cha michezo 18 5000/= 5000/= 5000/= 5000/= 5000/= 3000/= 5000/= 5000/= 12000/= 10,000/= 10,000/= 10,000/= 20,000/= 10,000/= 20000/= 20000/= 10000/= 50000/= 5000/= 10,000/= 60,000/= 30,000/= 100,000/= 45,000/= 25,000/= 50,000/= 30,000/= 30,000/= 50,000/= 15,000/= 10,000/= 10,000/= 50,000/= 30,000/= 20,000/= 20,000/= 180,000/= kwa safari moja 20,000/= 20,000/= 5,000.00/= 10,000.00/= 10,000.00/= 20,000.00/= Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea)
Part
Sehemu ya kutengeneza matofali
- 62 Verify source ↗
Section 62
AI-assisted research summary: Hii ni jedwali la ada za usajili na ukaguzi wa mazingira kwa aina mbalimbali za shughuli, kila shughuli ikiwa na kiasi tofauti cha ada.
62. Shule ya kutwa Kituo cha kutunza watoto Stendi kubwa ya Basi Stendi ndogo ya Basi Ukarabati wa vifaa vya umeme Kizimba cha soko Kutupa taka kwenye dampo Hoteli yenye baa au kumbi za starehe na sherehe Benki tawi kubwa Benki tawi dogo Mikutano ya hadhara au dini au semina au kongamano Shule ya bweni Biashara yoyote ambayo haijaainishwa 20,000.00/= 10,000.00/= 80,000.00/= 40,000.00/= 10,000.00/= 300/= kwa siku 50,000/= kwa safari moja 200,000/= 100,000/= 60,000/= 20,000/= kwa siku 50,000/= 10,000/= __________ JEDWALI LA PILI ___________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 12 na 22) ADA ZA UKAGUZI WA MAZINGIRA USAJILI NA VIBALI Namba. Aina ya Shughuli Ada ya Usajili.
Part
JEDWALI LA PILI
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Watu au kampuni wanaoomba kibali cha kupulizia dawa wanalipa ada ya Sh. 100,000, na kibali cha kufanya matangazo au mikutano ya hadhara kina ada ya Sh. 50,000 kwa siku.
8. Migodi ya madini ya ujenzi Eneo la kuoshea magari Minara ya simu Ujenzi wa jengo hadi ghorofa moja. Ujenzi wa ghorofa 2 hadi 5 Ujenzi wa ghorofa 6 na kuendelea Mradi wa kilimo Kibali cha kupakua maji taka 20,000/= 10,000/= 20,000/= ____________ JEDWALI LA TATU ____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 32) Ada ya Ukaguzi wa Mazingira na Kibali kwa Mwaka. 50,000/= 20,000/= 50,000/= 50,000/= 100,000/= 300,000/= 50,000/= 50,000/= Namba. Aina ya Kibali Kibali cha kufanya Matangazo au Mikutano ya Hadhara Kiwango cha ada (Shilingi) 50,000/= kwa siku 19 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) ___________ JEDWALI LA NNE ____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 33) VIWANGO VYA MALIPO YA UKAGUZI, USAJILI, KUPIMA AFYA NA KUPULIZIA DAWA YA KUUWA WADUDU WAENEZAO MAGONJWA KWA BINADAMU Namba. AINA YA BIASHARA UKAGUZI KUPILIZIA DAWA Mtu au kampuni itakayoomba kibali cha kupulizia dawa italipa ada ya kibali Sh. 100,000/= KIPIMA AFYA 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 30,000 30,000 20,000 10,000 10,000 10,000 100,000 10,000 20,000 100,000 20,000 20,000 20,000 10,000 20,000 20,000 10,000 20,000 10,000 10,000 50,000 100,000 100,000
Part
JEDWALI LA NNE
- 32 Verify source ↗
Section 32
AI-assisted research summary: Section 32 lists retail and related business types and shows associated amounts for them, but the text is ambiguous about the exact rule.
32. Maduka ya Rejareja. Bucha Nyumba za Wageni Maduka ya Jumla Migahawa Mashine ya Kusaga Mifigo/kilimo Hoteli Vipodozi Dawa za binadamu Chuo Stoo ya Vinywaji Garage Vifaa vya Ujenzi Mwafrika Bar Restaurant/on bar Maduka ya nafaka Stationary Spareparts kinyozi Saloon za kike Ghala/Godown Viwanda Shule za Binafsi zenye wanafunzi zaidi ya 700 Shule Binafsi zenye wanafunzi wasiozidi 700 Timberyard/sawmil Matofali Petrostation Karakana Minisupermarket Shamba la Maua Pub/grocery 20 70,000 10,000 50,000 50,000 100,000 20,000 20,000 100,000 20,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) - 44 Verify source ↗
Section 44
AI-assisted research summary: Hii ni fomu ya kukiri kosa na kukubali kulipa ada au ushuru pamoja na faini mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
44. Wachoma nyama Fundi cherehani Bustani za maua Viwanda vya ushonaji Machimbo ya mawe/moram na madini mengine. Day care Safari &campsite Kambi za muda bakery Magari ya kubeba vyakula Depot 10,000 10,000 10,000 20,000 100,000 20,000 100,000 50,000 20,000 30,000 100,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 10,000 __________ JEDWALI LA TANO __________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 37) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ........................................................................nakiri KWA HIARI YANGU MIMI MWENYEWE mbele ya........................................................... ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kwamba Tarehe ..........ya Mwezi .................. Mwaka................ nilitenda kosa kwa kukiuka masharti ya aya ya ……..ya Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ya Mwaka 2023. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Niko tayari kulipa kiasi cha ada au ushuru na faini ninayodaiwa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo Tarehe ......................ya Mwezi ................................Mwaka …… Jina: ..................................................... Saini: .................................................... MBELE YA: Jina……............................................... Wadhifa: .............................................. Saini: .................................................... Tarehe: ............................................... 21 Sheria Ndogo ya Usafi, Afya Na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Tangazo La Serikali Na. 921 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya Arusha imegongwa kwenye sheria Ndogo hii kufutia azimio lililopitishwa kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika mnamoTarehe 10 mwezi Mei 2023 mbele ya:- SELEMAN HAMISI MSUMI Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Arusha OJUNG’U SALEKWA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Arusha NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 22
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usafi, Afya na Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in