Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ya Mwaka 2023
This by-law is called the Ngara District Council Environmental Sanitation By-law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This by-law is called the Ngara District Council Environmental Sanitation By-law, 2023. This by-law applies throughout the area of Ngara District Council. This section defines key terms used in the by-law, including council, resident, waste, food, wastewater, and authorized persons. Kila mkazi anayemiliki nyumba, kiwanja au biashara lazima ahakikishe eneo lake ni safi, taka zinashughulikiwa ipasavyo, na vifaa au miundombinu ya usafi wa mazingira iko mahali panapohitajika. Owners of houses, factories, or business premises must have a sewage pit, empty sewage when it fills up, and not direct wastewater into streets, drains, rivers, water sources, open areas, or any place not meant for sewage storage.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ya Mwaka 2023
Showing 22 of 22
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This by-law is called the Ngara District Council Environmental Sanitation By-law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the area of Ngara District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Ngara. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including council, resident, waste, food, wastewater, and authorized persons.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote kusimamia na Mkurugenzi atakayeteuliwa utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa dawa; “chanzo cha maji” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Ngara; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara au Afisa yeyote atakayeteuliwa ya Mkurugenzi; kutekeleza majukumu 1 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) “kizimba cha taka” maana yake ni kizimba cha taka au chombo maalum kilichowekwa na Halmashauri kwa ajili ya jamii kuhifadhia taka ngumu kabla ya kusafirishwa kuu lililoidhinishwa; kwenye jalala hadi “mkazi” maana yake ni mtu yeyote ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo lililoko chini ya mamlaka ya Halmashauri na ambaye ama ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “maji taka” maana yake ni ile iliyoanishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka” maana yake ni ile iliyoanishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; Sura ya 191 “taka ngumu” Maana yake ni ile iliyoainishwa katika Sura ya 331 Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. shirika ambalo Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira - 4 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayemiliki
AI-assisted research summary: Kila mkazi anayemiliki nyumba, kiwanja au biashara lazima ahakikishe eneo lake ni safi, taka zinashughulikiwa ipasavyo, na vifaa au miundombinu ya usafi wa mazingira iko mahali panapohitajika.
4.-(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara kuhakikisha kwamba- (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; (b) taka zote zinakusanywa na kufukiwa au itakayoelekezwa na kuondolewa kwa njia Halmashauri; (c) anachimba shimo la kutupia taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi tatu na upana usiopungua futi mbili; (d) anajenga choo imara cha kudumu kilichojengwa kwa matofali na kuezekwa kwa bati, tembe, majani, vigae chenye mlango unaofunga na kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na kuwe na chombo cha 2 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi; (f) anaweka wavu maalumu kwenye gari lake ili taka au kuzuia kumwagika kwa mchanga, mbolea katika barabara au eneo lolote katika Halmashauri; (g) anaweka chombo cha kuhifadhia taka ndani ya gari la abiria. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya aya ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Uhifadhi wa maji taka - 5 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la
AI-assisted research summary: Owners of houses, factories, or business premises must have a sewage pit, empty sewage when it fills up, and not direct wastewater into streets, drains, rivers, water sources, open areas, or any place not meant for sewage storage.
5.-(1) Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara anatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa analo karo la kuhifadhi maji taka; (b) kunyonya maji taka pale karo linapojaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote isiyotengwa kuhifadhia maji taka. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya aya ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Utengenezaji na uuzaji wa vyakula - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetengeneza matunda, kuchoma,
AI-assisted research summary: Anyone making, cooking, boiling, grilling, or selling food in the council area must follow the bylaw and have a permit from the council’s health officer.
6. Mtu yeyote anayetengeneza matunda, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa- (a) kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii; na (b) kuwa na kibali kutoka kwa afisa afya wa Halmashauri. Upimaji wa afya - 7 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli,
AI-assisted research summary: Wahudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waoka mikate, na wauzaji wa vyakula vilivyopikwa lazima wahakikishe wanapima afya zao kila baada ya miezi sita.
7. Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waoka mikate, au watu wanaoshughulika na kuuza vyakula 3 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) Uwezo wa afisa mwidhiniwa Vifaa vya kuhifadhi taka ngumu Ada ya uzoaji taka Ukusanyaji taka ngumu vilivyopikwa kuhakikisha kwamba wanapima afya zao kila baada ya miezi sita. - 8 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia eneo lolote ndani ya Halmashauri wakati wa kazi ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii, na anaweza kushauri au kuelekeza watu wasiishi katika jengo linalohatarisha afya au maisha.
8.- (1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo kuingia katika eneo lolote ndani ya Halmashauri wakati wa muda wa kazi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kushauri au kuelekeza watu au mtu kutokuishi katika jengo ambalo linahatarisha afya au maisha ya watu na viumbe hai. - 9 Verify source ↗
(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji
AI-assisted research summary: Wamiliki na wapangaji fulani lazima wawe na chombo cha taka chenye mfuniko na kukusanya taka mahali palipoainishwa; katika ukanda wa kijani usiopimwa lazima pia kuwe na shimo kubwa la taka ngumu.
9.-(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji wa jengo la makazi au mtu yeyote anayefanya biashara katika eneo lolote au chombo cha usafiri ndani ya Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhia taka chenye mfuniko na atawajibika kukusanya taka hizo kwenye vizimba vya kuzolea taka katika maeneo yaliyoainishwa. (2) Kila mmiliki wa jengo au mpangaji wa nyumba iliyoko katika ukanda wa kijani, katika maeneo ambayo hayajapimwa atalazimika kuwa na shimo kubwa la kukusanyia taka ngumu katika eneo lake. - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri itawajibika kukusanya taka
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikusanye taka ngumu kutoka vizimba vya taka vilivyoainishwa katika kila kata, na wazalishaji taka lazima walipe ada au ushuru wa ukusanyaji wa taka kama ulivyo katika Jedwali la Kwanza.
10.-(1) Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu kutoka katika vizimba vya taka vilivyoainishwa katika kila kata, na wazalishaji taka watalipia ada au ushuru wa ukusanyaji wa taka kama ilivyooneshwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. - 11 Verify source ↗
(1) Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma au kufukia taka ngumu bila kibali cha Halmashauri.
11.- (1) Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya taka au kitu chochote maji maji kwenye pipa kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara. la (2) Taka ngumu zote zitakazokusanywa kwenye mapipa ya taka zitabaki kuwa mali ya mkazi au mmliki wa eneo lile mpaka zitakapokuwa zimefikishwa kwenye kizimba cha taka au zitakapokuwa zimetolewa na wakala 4 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) kutoka katika eneo lake. (3) Hairuhusiwi mtu yeyote kuchoma au kufukia taka ngumu bila kibali cha Halmashauri. Eneo la kutupa taka - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupia taka, iweke vyombo vya kuhifadhia taka, na itoe huduma ya kuzoa taka kwa malipo. Pia, mtu yeyote haruhusiwi kuweka au kutupa taka, mchanga au uchafu unaosababisha chukizo na uharibifu wa mazingira.
12.- (1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupia taka; (b) kuweka vyombo maalum vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. (2) Hairuhusiwi kwa mtu yeyote kuweka au kutupa taka, mchanga au uchafu wowote utakaoleta chukizo na uharibifu wa mazingira - 13 Verify source ↗
(1) Kila alhamisi ya wiki na jumamosi ya
AI-assisted research summary: Residents must join scheduled sanitation cleanups, and everyone must keep specified residential, business, public, and office-adjacent areas clean. The council may direct certain areas to be cleaned by local groups or institutions.
13.- (1) Kila alhamisi ya wiki na jumamosi ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku maalamu ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya makazi na umma. (2) kila mkazi katika kijiji na kitongoji anapaswa kushiriki kufanya usafi wa mazingira kwa siku iliyopangwa na Halmashauri katika maeneo yao na maeneo ya umma. (3) Kila mtu atahakikisha eneo la makazi yake na vichochoro vilivyomzunguka, eneo analofanyia biashara, eneo la wazi lililokaribu naye kwa umbali wa mita kumi na eneo la mazingira ya ofisi ni safi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (4) Halmashuri itaelekeza eneo fulani kufanyiwa usafi na kikundi, makundi au taasisi yotote iliyoko katika eneo la Halmshauri. - 14 Verify source ↗
Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ihamasishe na itambue uundaji wa vikundi vya jamii ili viweze kufanya udhibiti wa taka ngumu na usafi wa mazingira katika mitaa, baada ya mkataba na Halmashauri.
14. Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika mitaa baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. - 15 Verify source ↗
Wamiliki wote wa magari yanayovuka mipaka
AI-assisted research summary: Wamiliki wa magari yanayovuka mipaka lazima wakague magari yao, wayapangilie kuwa katika hali nzuri, wafunge mabomba imara ya moshi, wafunike mizigo ya ujenzi au taka za ujenzi, wasiandike taka ovyo ndani ya Halmashauri, na waegeshe kwenye eneo lililotengwa.
15. Wamiliki wote wa magari yanayovuka mipaka watahakikisha kuwa- 5 Siku ya usafi Vikundi vya kufanya usafi Wajibu wa wamiliki wa magari Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) (a) wanakagua magari yao mara kwa mara ili yanapopita ndani ya Halmashauri yawe katika hali njema; (b) wanafunga mabomba imara ya kutolea moshi na chafu ili yasipitishe hewa chafu hewa itakayoharibu mazingira; Marufuku (c) magari yote yabebayo vifaa vya ujenzi au taka zitokanazo na mabaki ya ujenzi yanafunikwa; (d) kutotupa taka ovyo muda wote wanapokuwa ndani ya Halmashauri; na (e) wanaegesha magari sehemu maalum iliyotengwa na Halmashauri. - 16 Verify source ↗
Ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinapiga marufuku vitendo kadhaa vinavyohusu usafi wa mazingira, taka, maji, ujenzi, biashara fulani, mifugo, na mikusanyiko wakati wa milipuko ya magonjwa isipokuwa kwa ruhusa au kibali kinachotajwa.
16. Ni marufuku kwa mtu yeyote: (a) kuendesha biashara ya upulizaji dawa au biashara ya kuua wadudu au wanyama waharibifu katika nyumba yoyote au mahali popote bila cheti cha taaluma kinachotambuliwa na Serikali na leseni kutoka Halmashauri; (b) mfanyabiashara kupanga bidhaa nje ya jengo lake la biashara, barabarani, vichochoroni au katika eneo lolote ambalo halikuidhinishwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (c) mfugaji kuruhusu mifugo kuzurura ovyo mitaani au barabarani; (d) kutupa taka za aina yoyote barabarani au eneo lolote la wazi, kwenye vichochoro au kwenye chanzo chochote cha maji au katika eneo lolote ambalo halikutengwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (e) aliye ndani ya gari kudondosha taka ngumu nje ya gari likiwa ndani au nje ya kituo cha magari na sehemu yoyote ile ambapo gari hilo linapita; (f) kuanzisha shughuli za kiwanda au mradi wowote unaoweza kuathiri mazingira bila kufanya utafiti wa mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; (g) kuzuia maji kupitia njia yake ya asili kwa 6 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) kujenga au kulima au kuweka kitu chochote kwenye maji kitakachoingilia mtiririko wa asili wa maji katika chanzo cha maji; (h) kuweka kitu chochote kwenye maji taka ambacho kinaweza kuathiri mtu yeyote au kuharibu mfumo wa tiba ya maji taka au kinachoweza kusababisha kuzuia mtiririko wa maji taka; (i) kulima kilimo cha matuta yanayosababisha maji kutuama ndani ya eneo la katikati ya mji; (j) kuchimba mchanga, kokoto au mawe katika vyanzo vya maji, mito barabarani; (k) kujenga kisima cha maji bila idhini ya maandishi ya Halmashauri; (l) kuchafua, kuoga, kufulia au kuvuruga maji yanayotumika kwa ajili ya matumizi ya binadamu au wanyama; (m) kuuza mchanga, kokoto na mawe kandokando mwa barabara; (n) kukata mti uliokwisha pandwa au ulioota wenyewe bila kupata kibali cha Halmashauri ambacho kitatolewa kwa masharti maalum; (o) kuegesha au kufanya matengenezo ya gari, pikipiki au baiskeli kwenye maeneo ya makazi, bakaa za barabara maeneo ya wazi; (p) kufanya biashara ya pombe ya aina yoyote katika nyumba, au kwenye maeneo ya akiba za barabara, mitaani; (q) kuuza matunda au bidhaa nyingine za vyakula barabarani au kuanzisha masoko au magenge ya kuuzia matunda, vyakula au biashara nyingine ndogo bila ruhusa ya Halmashauri; (r) kuunganisha bomba la taka vimiminika katika mifereji ya maji ya mvua; (s) kufungulia au kutiririsha maji ya choo au taka vimiminika katika mkondo asili wa maji ya mvua au barabara au mfereji wa barabara wa 7 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) maji ya mvua; (t) kujisaidia haja ndogo au haja kubwa barabarani au mitaani au sehemu yoyote isiyokusudiwa kwa madhumuni hayo; (u) kubomoa jengo lolote kwa njia yeyote ile bila kupata kibali cha Halmashauri; (v) kuhakikisha mifugo haizururi ovyo, na kinyesi au uchafu wowote unaotokana na wanyama wafugwao unatupwa ovyo na kuleta kero kwa jamii; (w) mzalishaji, mfanyabiashara au mchuuzi wa mazao au vitu vinavyoharibika kuingiza sokoni vitu hivyo vikiwa vimefungwa au kufunikwa kwa majani ya miti au aina yeyote ile ya sehemu ya mimea; (x) kufanya mikusanyiko ya kidini, kiutamaduni au kijamii wakati wa milipuko ya magonjwa ya kuambukiza, isipokuwa kwa ruhusa maalum ya Halmashauri na usimamizi wa Afisa Afya; na (y) kuchoma moto za majumbani, takataka makaratasi, majani, michongoma au takataka za aina yeyote katika maeneo ya makazi ya watu na kusababisha moshi kwa wakazi na kuchafua hewa kwa moshi na mazingira kwa ujumla. Makosa - 17 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa ikiwa anafanya mojawapo ya vitendo vilivyotajwa, kama kujenga choo karibu sana na chanzo cha maji, kumwaga uchafu kwenye maeneo ya umma, au kushindwa kuwa na vifaa au miundombinu ya usafi inayohitajika.
17. Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa mtu yeyote- kujenga choo chini ya umbali wa mita sitini kutoka kisimani, bwawani, mtoni, au chanzo kingine cha maji yanayotumika, kwa matumizi ya binadamu; kutoa kinyesi au kusababisha kinyesi, mkojo, maji machafu, yenye kinyesi kutoka kwenye choo chake au bafu lake au karo la kuoshea vyombo au nguo au kutoka kwenye bomba lolote linalochukua maji machafu na kuyatitirisha kwenye barabara, mitaa, au kwenye mifereji ya maji ya mvua, au mfereji wowote uliowazi; 8 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) (a) kutupa taka au kusababisha mtu mwingine atupe na pasiporuhusiwa popote taka mahali Halmashauri; (b) kuuza chakula nje ya eneo ambalo halijasajiliwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (c) kuzika maiti katika eneo ambalo halikuainishwa kwa shughuli hiyo; (d) kutolipa ada ya mfululizo; taka kwa miezi miwili (e) kutembeza vyakula mitaani bila kibali cha Halmashauri; (f) kuchezesha michezo au kuonyesha michezo au burudani katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri; (g) kuegesha gari bovu na kuliacha kando ya barabara au kichochoro au eneo la wazi ambalo halijaidhinishwa kwa shughuli za gereji na kuliacha zaidi ya siku moja; (h) kulima ndani ya vyanzo vya maji; (i) kutokuwa na pipa la taka lenye mfuniko katika eneo la biashara; (j) kutokuwa na choo au kukutwa na choo kibovu au kilichojaa; (k) kukutwa na shimo la maji taka lililojaa au ambalo halina mfuniko; (l) kuziba kichochoro; na (m) kutokuwa na chombo maalum cha kukusanyia taka ndani ya gari la abiria na mizigo. Adhabu - 18 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria
AI-assisted research summary: Anyone who violates the by-law commits an offence and, if convicted, may be fined, imprisoned for up to 12 months, or both.
18. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na endapo akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi elfu hamsini na isiyozidi Shilingi laki tatu au kutumikia kifungo kisichozidi miezi kumi na miwili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja faini na kifungo. 9 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) Kufifilisha kosa - 19 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii faini ya Shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalum ya Jedwali la Pili.
19. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. ______________ JEDWALI LA KWANZA ______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya (10)) A: ADA ZA UZOAJI TAKA Na Aina ya biashara Viwango 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 Maduka ya madawa na pembejeo za kilimo na mifugo Duka dogo la rejareja 10,000/= Kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi Karakana za ufundi wa aina mbalimbali 5,000/= Kwa mwezi Baa/Duka la vinywaji baridi 5,000/= Kwa mwezi Nyumba ya kulala wageni. 10,000/= Kwa mwezi Saluni za nywele za kike na kiume 5,000/= Kwa mwezi Kituo cha kuuza mafuta 30,000/= Kwa mwezi Klabu cha kuuza pombe za asili 5,000/= Kwa mwezi Usafi wa soko kwa kila mfanyabiashara aliyeleta bidhaa. Nyama ya kuchoma Zahanati 12 Washona viatu na nguo 13 14 15 16 17 Shughuli nyingine yeyote ambayo haijatajwa hapa Maegesho ya magari mapya yanayosafirishwa kwenda nje ya mipaka ya Tanzania pamoja na maegesho ya kuuzia magari mapya Mgahawa mdogo Mgahawa mkubwa Zahanati (taka zisizohatari) 10 200/=Kwa siku 5,000/= Kwa mwezi 10,000/= Kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 30,000/=kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 10,000/= Kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 46 37 38 39 30 41 42 43 44 45 46 47 48 49 50 51 52 53 54 55 56 57 58 59 60 Kituo cha afya (taka zisizohatari) Hospitali ya Rufaa (taka zisizohatari) Hospitali ya Wilaya/Mkoa (taka zisizohatari) Kiwanda cha mbao Fundi Seremala (mdogo) Fundi chuma Karakana nyinginezo (magari na pikipiki) Kiwanda kidogo Kiwanda kikubwa Duka la jumla Duka la rejareja/huduma Shule ya Msingi ya Bweni Shule ya Sekondari ya Bweni Kituo cha kulelea watoto Kituo cha kutunzia watu wenye mahitaji maalum Duka dogo la chakula Duka kubwa la chakula Baa kubwa Klabu ya usiku Kumbi za Sherehe Duka la kuuza nyama na samaki Nyama choma/chipsi inayojitegemea Duka la Dawa (Jumla na Rejareja) Duka la Dawa (DLDM - Rejareja) Kiwanda kidogo Dobi mdogo Dobi mkubwa Fundi wa vifaa vya umeme Fundi kushona(ofisi) kwa kila cherehani Duka la kuuza spea Stoo za kuhifadhia mizigo Ghala Hoteli Taasisi Klabu ya pombe ya asili Dahalia Kituo cha michezo Uwanja wa michezo Ofisi za wauza viatu na nguo za mitumba Stoo za mkaa Mama lishe/Baba lishe Duka la kuuza Magari 10,000/= kwa mwezi 50,000/= kwa mwezi 50,000/= kwa mwezi 30,000/= kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 15,000/= kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 50,000/= kwa mwezi 200,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 15,000/= kwa mwezi 30,000/= kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi Bure 5,000/= Kwa mwezi 30,000/= kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 40,000/= kwa mwezi 25,000/= kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 25,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 50,000/= kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 30,000/= kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 100,000/= kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 5,000/= Kwa mwezi 30,000/= kwa mwezi Sehemu za kuoshea vyombo vya usafiri 30,000/= kwa mwezi 11 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) B: ADA YA UNYONYAJI WA MAJI MACHAFU KWA KUTUMIA MAGARI YA HALMASHAURI i. Maeneo ya biashara……………...………Shilingi. 300,000/= kwa kila safari moja. ii. Maeneo ya makazi………………………Shilingi. 200,000/= kwa kila safari iii. moja. Nje ya Halmashauri…………………….Shilingi. 500,000/= kwa kila moja. safari C: ADA ZINAZOHUSIANA NA MIZIGO NA KUTUPA TAKA
Part
Sehemu za kuoshea vyombo vya usafiri
- 1 Verify source ↗
Kutupa taka kwenye eneo lililotengwa na Halmashauri Shilingi. 5,000/= kwa
AI-assisted research summary: Kutupa taka kwenye eneo lililotengwa na Halmashauri kunahusishwa na faini ya Shilingi 5,000 kwa safari moja.
1. Kutupa taka kwenye eneo lililotengwa na Halmashauri Shilingi. 5,000/= kwa safari moja - 2 Verify source ↗
Kila gari litakaposhusha au kupakia mzigo litalipa kiasi cha Shilingi 10,000/=
AI-assisted research summary: Kila gari linaloshusha au kupakia mzigo lazima lilipie Shilingi 10,000/=
2. Kila gari litakaposhusha au kupakia mzigo litalipa kiasi cha Shilingi 10,000/= - 3 Verify source ↗
Kufaulisha mizigo kwenye Maegesho ya Rusumo na Kabanga
AI-assisted research summary: Hii aya inaweka ada za magari kwenye Maegesho ya Rusumo na Kabanga, na ada ya kila siku kwa magari katika Kabanga, Benaco na Kahaza.
3. Kufaulisha mizigo kwenye Maegesho ya Rusumo na Kabanga : Gari chini ya Tani 10 Gari chini ya Tani 25 Gari zaidi ya Tani 26 Shilingi. 50,000/= Shilingi. 75,000/= Shilingi. 100,000/= i. ii. iii. - - - D:ADA KWA AJILI YA MAEGESHO YA KABANGA, BENACO NA KAHAZA AINA YA GARI Magari makubwa Magari madogo KIWANGO Shilingi 3,000/= kwa siku Shilingi 3,000/= kwa siku _______________ JEDWALI LA PILI ________________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 19) KUFIFILISHA KOSA Mimi ………………………………. Nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya…………………………………….…ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya tarehe…………ya Mwezi….......... Mwaka Wilaya ya Ngara kwamba mnamo …………….. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ………. ya Sheria Ndogo za Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Ngara za Mwaka 2023. 12 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Niko tayari kulipa kiasi cha Shilingi…………… kwa ajili ya kufifilisha Kosa nililotendachini ya Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ninaodaiwapamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe………..ya Mwezi……………………Mwaka………………….. Jina………………………………..…………….Saini………………………. MBELE YA: Jina……………………………………………….….. Wadhifa………………………..…………………….….. Saini…………………………………………………… Tarehe…………………………………………………. 13 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Tangazo La Serikali Na. 924 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya Ngara imegongwa kwenye sheria Ndogo hii kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ngara uliofanyika Tarehe 27 Mwezi Oktoba Mwaka 2021 na Kushudiwa na Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya :- SOLOMON. O KIMILIKE Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngara WILBARD. J. BAMBARA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Ngara NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARI MCHENGERWA (MB) 31 Oktoba, 2023 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 14
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in