Kanuni za Vigezo na Masharti ya Kutoa Huduma Zinazodhibitiwa za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka, 2024
These regulations are titled the 2024 Regulated Transport Services Fees and Conditions Regulations of the Land Transport Regulatory Authority.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Vigezo na Masharti ya Kutoa Huduma Zinazodhibitiwa za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka, 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
These regulations are titled the 2024 Regulated Transport Services Fees and Conditions Regulations of the Land Transport Regulatory Authority. Kanuni hizi zinatumika kwa vyombo vya usafirishaji vinavyokusudiwa kutoa huduma za kibiashara Tanzania Bara. This section defines key terms used in the regulations. Mtoa huduma wa chombo cha usafiri kibiashara lazima ahakikishe chombo kinatimiza masharti ya usalama na matengenezo yaliyotajwa, vinginevyo anaweza kuadhibiwa. Mtoa huduma wa usafiri wa kibiashara anaweza kubadilisha chombo chake, lakini mabadiliko lazima yafuate vigezo vya mtengenezaji vilivyoidhinishwa na Shirika la Viwango au yafanyike kwenye karakana iliyothibitishwa. Basi la abiria haliruhusiwi kuundwa kwenye mwamba wa lori.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Vigezo na Masharti ya Kutoa Huduma Zinazodhibitiwa za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka, 2024
Showing 17 of 17
- 1 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: These regulations are titled the 2024 Regulated Transport Services Fees and Conditions Regulations of the Land Transport Regulatory Authority.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Vigezo na Masharti Ya Kutoa Huduma Zinazodhibitiwa za Mamlaka Ya Udhibiti Usafiri Ardhini za mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinatumika kwa vyombo vya usafirishaji vinavyokusudiwa kutoa huduma za kibiashara Tanzania Bara.
2. Kanuni hizi zitatumika kwa vyombo za usafirishaji vinavyokusudiwa kutoa huduma kibiashara Tanzania Bara. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Tafsiri
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the regulations.
3. Katika Kanuni hizi isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- Sura ya 413 “Sheria” maana yake ni Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini; “Mamlaka” maana yake ni Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini iliyoanzishwa chini ya Sheria; “Shirika la Viwango” maana yake ni Shirika la Viwango Tanzania lililoanzishwa chini cha Sheria ya Viwango; “Mkurugenzi Mkuu” maana yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka aliyeteuliwa kwa mujibu wa Sheria; “leseni” maana yake ni leseni za kutoa huduma za usafirishaji kwa njia ya barabara zinazotolewa na Mamlaka kwa ajili ya huduma inayodhibitiwa; “kelele” maana yake ni sauti zenye kadhia kwa binadamu ambazo zinaweza kusababisha madhara hasi kwa afya yake au mazingira; 3 Kanuni Za Vigezo Na Masharti ya Kutoa Huduma Zinazodhibitiwa Za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Tangazo la Serikali Na.27 (Lnaendelea.) “bidhaa za kukera” maana yake ni bidhaa zinazoweza kuleta karaha kama vile damu kavu, maiti, nyama ya mnyama aliyekufa, mifupa, samadi, nguo chafu ambazo uchafu wake hautokani na mafuta ya gari, mzoga, mboga zilizooza, mafuvu na viungo vingine vya binadamu; “mtoa huduma” maana yake ni mmiliki wa leseni ya uendeshaji wa chombo kinachotoa huduma ya usafiri kibiashara; Sura ya 297 “karakana iliyosajiliwa” maana yake ni karakana iliyokidhi viwango na kusajiliwa na Shirika la Viwango kwa ajili ya utengenezaji wa vyombo vinavyotoa huduma za usafiri kibiashara; "barabara" maana yake ni barabara kuu, barabara za kawaida, barabara za mitaa, daraja, kalvati, kivuko, maegesho ya magari, njia ya waenda kwa miguu au njia ya hatamu ambapo vyombo vya usafiri vinaweza kupita na umma unaweza ukafika endapo barabara hizo zimezuiwa au isipokuwa vinginevyo kwa masharti yoyote yale barabara gegedu kwenye maeneo ya makazi; na “chombo” maana yake ni chombo kinachoendeshwa kwa mitambo au umeme kilichokusudiwa kutoa huduma ya usafirishaji kibiashara; SEHEMU YA PILI VIWANGO VYA CHOMBO NA MAHITAJI YA USALAMA Mahitaji ya jumla ya usalama kwa vyombo vya kibiashara
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Mahitaji ya jumla ya usalama kwa chombo cha kibiashara
AI-assisted research summary: Mtoa huduma wa chombo cha usafiri kibiashara lazima ahakikishe chombo kinatimiza masharti ya usalama na matengenezo yaliyotajwa, vinginevyo anaweza kuadhibiwa.
4.-(1) Mtoa huduma wa chombo cha usafiri kibiashara anapaswa kuhakikisha kuwa- (a) sakafu ya chombo cha usafiri isiwe ya kuteleza, kushika kutu na chombo kiwe kimetengenezwa katika hali ya kumkinga abiria dhidi ya vumbi, mvuke, mafusho, kelele, hitilafu ya umeme, dutu hatarishi, kuvuja kwa mafuta na vilainishi vingine hatari; (b) milango na madirisha ya chombo kinachotoa huduma lazima ifunguke na kufunga kwa urahisi na isiruhusu vumbi au maji kuingia sehemu anapoketi abiria; (c) usukani wa chombo uwe mbele upande wa kulia; 4 Kanuni Za Vigezo Na Masharti ya Kutoa Huduma Zinazodhibitiwa Za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Tangazo la Serikali Na.27 (Lnaendelea.) (d) mwamba wa chombo, mineso, ekseli na rimu za vyombo vya usafiri kwa umma viwe vimefungwa madhubuti na havijapasuka wala kuungwa kwa umeme; (e) chombo hakitaruhusiwa kuendeshwa, kutoa huduma au kuegeshwa barabarani au mahali pengine kama hakijafanyiwa matengenezo pamoja na vifaa vyake; (f) chombo kisiwe kimeungwa minyororo, vyuma, vifaa, gurudumu au vifaa vingine ndani au nje ya chombo na kuhatarisha maisha ya dereva, wahudumu, abiria na watumiaji wengine wa barabara; na, (g) chombo kinaendeshwa kwa ajili ya lengo lililokusudiwa. (2) Mtoa huduma atakayekiuka masharti ya kanuni hii atakuwa ametenda kosa na atakapopatikana na hatia atalipa faini isiyopungua Shilingi laki mbili na isiyozidi Shilingi laki tano au kifungo kisichopungua mwezi mmoja na kisichozidi miezi mitatu jela au vyote. Mabadiliko ya chombo - 5 Verify source ↗
Mabadiliko ya chombo
AI-assisted research summary: Mtoa huduma wa usafiri wa kibiashara anaweza kubadilisha chombo chake, lakini mabadiliko lazima yafuate vigezo vya mtengenezaji vilivyoidhinishwa na Shirika la Viwango au yafanyike kwenye karakana iliyothibitishwa. Basi la abiria haliruhusiwi kuundwa kwenye mwamba wa lori.
5.-(1) Mtoa huduma wa chombo kinachotoa huduma ya usafiri kibiashara anaweza kubadilisha chombo chake isipokuwa mabadiliko hayo yanapaswa kufanyika- (a) kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa na mtengenezaji na kuidhinishwa na Shirika la Viwango; au (b) katika karakana iliyothibitishwa na Shirika la Viwango. (2) Bila kuathiri masharti yaliyoainishwa katika kanuni ndogo ya (1), chombo cha abiria aina ya basi hakitaruhusiwa kuundwa kwenye mwamba wa lori. 5 Kanuni Za Vigezo Na Masharti ya Kutoa Huduma Zinazodhibitiwa Za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Tangazo la Serikali Na.27 (Lnaendelea.) SEHEMU YA TATU VIWANGO MAALUMU NA MAHITAJI YA USALAMA Viwango na mahitaji ya usalama kwa vyombo vya usafiri wa umma Viwango na mahitaji ya usalama kwa vyombo vya kusafirisha mizigo Viwango na mahitaji ya usalama kwa vyombo vya Huduma ya usafiri wa kukodi
Part
SEHEMU YA TATU
- 6 Verify source ↗
Viwango na mahitaji ya usalama kwa chombo cha usafiri wa umma
AI-assisted research summary: Mtoa huduma wa chombo cha usafiri wa umma lazima ahakikishe chombo kina nafasi ya kuhudumia abiria wenye mahitaji maalum.
6. Mtoa huduma wa chombo cha usafiri wa umma anapaswa kuhakikisha kuwa chombo kinakuwa na nafasi kwa ajili ya kuhudumia abiria wenye mahitaji maalum. - 7 Verify source ↗
Viwango na mahitaji ya usalama kwa chombo cha kusafirisha
AI-assisted research summary: Mtoa huduma wa chombo cha kusafirisha mizigo lazima ahakikishe sehemu ya dereva imetenganishwa na sehemu ya mizigo, na mizigo ifunikwe.
7. Mtoa huduma wa chombo cha kusafirisha mizigo anapaswa kuhakikisha kuwa- (a) chombo cha kusafirisha mizigo kimetenganisha sehemu ya dereva na sehemu ya mizigo ili kuzuia mwingiliano baina ya mizigo na dereva; na (b) mizigo iliyobebwa iwe imefunikwa ili kuzuia kudondosha kwa chembechembe, vumbi, unyevu, kuvuja au moshi.
Part
sehemu ya dereva na sehemu ya mizigo ili kuzuia
- 8 Verify source ↗
Viwango na mahitaji ya usalama kwa chombo cha huduma ya usafiri
AI-assisted research summary: Mtoa huduma wa chombo cha usafiri wa kukodi lazima ahakikishe usalama na uwepo wa nafasi kwa abiria wenye mahitaji maalum, na asibebe abiria wakati wa matengenezo au kujaza mafuta, wala kubeba wanyama hai au bidhaa hatarishi/zinaokera.
8.-(1) Mtoa huduma wa chombo cha usafiri wa kukodi anapaswa kuhakikisha kwamba - (a) chombo kinakuwa na nafasi kwa ajili ya kuhudumia abiria wenye mahitaji maalum; (b) abiria hawakai ndani ya chombo wakati chombo kikifanyiwa matengenezo au kujazwa mafuta; (c) chombo cha usafiri wa kukodi hakibebi wanyama hai, bidhaa hatarishi au zinazokera; (2) Mtoa huduma atakayekiuka masharti ya kanuni hii atakuwa ametenda kosa na atakapokutwa na hatia- (a) ikiwa ni pikipiki ya magurudumu mawili au matatu, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu thelathini lakini isiyozidi shilingi elfu hamsini au kifungo cha muda usiozidi miezi mitatu jela au vyote; (b) ikiwa ni teksi ya kukodi, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu thelathini lakini isiyozidi shilingi elfu hamsini au kifungo cha muda usiozidi miezi mitatu jela au vyote; 6 Kanuni Za Vigezo Na Masharti ya Kutoa Huduma Zinazodhibitiwa Za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Tangazo la Serikali Na.27 (Lnaendelea.) (c) ikiwa ni mtoa huduma wa teksi mtandao, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini lakini isiyozidi shilingi laki moja au kifungo cha muda usiozidi miezi mitatu jela au vyote; au (d) ikiwa ni mtoa huduma wa teksi mtandao wa kushirikiana, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki tano lakini isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo cha muda usiozidi miezi mitatu jela au vyote. SEHEMU YA NNE VIWANGO VYA UBORA WA HUDUMA
Part
SEHEMU YA NNE
- 9 Verify source ↗
Mahitaji ya huduma
AI-assisted research summary: Mtoa huduma lazima ahakikishe chombo cha huduma ya biashara kinatii mahitaji ya kanuni husika za leseni za usafirishaji.
9. Mtoa huduma atahakikisha kuwa chombo cha huduma ya biashara kinakidhi mahitaji yaliyoainishwa chini ya Kanuni za leseni za Usafirishaji za Vyombo vya Huduma za Usafiri wa Umma, Kanuni za leseni za Usafirishaji za Vyombo vya Huduma za Usafirishaji wa Mizigo, na Kanuni za leseni za Usafirishaji za Vyombo vya Huduma za Usafiri wa Kukodi. - 10 Verify source ↗
Muda wa basi kusimama kituo cha njiani
AI-assisted research summary: Mtoa huduma lazima ahakikishe chombo cha biashara hakisimami kituo cha njiani zaidi ya dakika tatu.
10. Mtoa huduma atahakikisha chombo cha biashara hakisimami kituo cha njiani kwa zaidi ya muda wa dakika tatu. - 11 Verify source ↗
Mahitaji ya kuwa na wataalam
AI-assisted research summary: Mtoa huduma wa usafiri lazima awe na wataalam fulani kulingana na idadi ya vyombo alivyonavyo, na pia aajiri dereva aliyethibitishwa na mhudumu aliyesajiliwa na Mamlaka.
11.-(1) Mtoa huduma anayemiliki vyombo vya usafiri visivyozidi sita anawajibika kuwa na angalau mtaalam mmoja mwenye stashahada ya masuala ya usimamizi wa logistiki na uchukuzi kutoka katika Chuo kinachotambulika. (2) Mtoa huduma anayemiliki idadi ya vyombo vya usafiri sita au zaidi anawajibika kuwa na angalau mtaalam mmoja mwenye stashahada ya masuala ya usimamizi wa logistiki na uchukuzi na mwajiriwa wa kudumu mwenye stashahada ya ufundi wa magari kutoka katika Chuo kinachotambulika. 7 Mahitaji ya huduma T.S Na. 76 la 2020 T.S Na. 77 la 2020 T.S Na. 78 la 2020 Muda wa basi kusimama kituo cha njiani Takwa la kuwa na wataalamu Kanuni Za Vigezo Na Masharti ya Kutoa Huduma Zinazodhibitiwa Za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Tangazo la Serikali Na.27 (Lnaendelea.) (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1) na (2), mtoa huduma anapaswa kuajiri dereva aliyethibitishwa na mhudumu aliyesajiliwa na Mamlaka. - 12 Verify source ↗
Matakwa ya kutoa huduma kupitia kampuni au ushirika
AI-assisted research summary: Mtoa huduma anayetoa huduma kwenye njia za zaidi ya kilomita 600 lazima awe na angalau vyombo vinne vya usafiri na atoe huduma kupitia kampuni au ushirika.
12.Mtoa huduma anayehitaji kutoa huduma kwenye njia zenye umbali wa zaidi ya kilomita mia sita anapaswa- (a) kumiliki vyombo vya usafiri visivyopungua vinne; na (b) kutoa huduma kupitia kampuni au ushirika. SEHEMU YA TANO MASHARTI YA UJUMLA
Part
SEHEMU YA TANO
- 13 Verify source ↗
Adhabu ya jumla
AI-assisted research summary: Mtu anayekiuka masharti ya Kanuni hizi anatenda kosa, na akitiwa hatiani anaweza kupewa faini, kifungo, au vyote pamoja.
13. Mtu atakayekiuka masharti ya Kanuni hizi atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani pale ambapo hakuna adhabu maalum iliyotolewa, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili lakini isiyozidi shilingi laki tano au kifungo cha muda usiopungua miezi mitatu lakini usiozidi mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. - 14 Verify source ↗
Kumzuia Afisa
AI-assisted research summary: A person commits an offence if they obstruct an Authority Officer or a Police Officer from carrying out their duties under these Regulations.
14. Mtu anayezuia Afisa wa Mamlaka au Afisa wa Polisi kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi anatenda kosa. - 15 Verify source ↗
Notisi ya kujiondoa kutoa huduma
AI-assisted research summary: A commercial transport service provider intending to stop services must give the Authority one month’s written notice before withdrawing.
15. Mtoa huduma anayekusudia kuacha kutoa huduma za usafirishaji kibiashara atatakiwa kutoa notisi ya maandishi ya mwezi mmoja kwa Mamlaka kabla ya kujiondoa. - 16 Verify source ↗
Mapitio
AI-assisted research summary: A person dissatisfied with the Authority’s decision must submit a review application.
16. Mtu ambaye hataridhishwa na maamuzi ya Mamlaka atatakiwa kuwasilisha maombi ya mapitio kwa mujibu wa Kanuni za Utaratibu wa Mapitio za Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini. - 17 Verify source ↗
Kufutwa
AI-assisted research summary: Kanuni za Vigezo na Masharti ya Kutoa huduma za SUMATRA zinafutwa.
17.Kanuni za Vigezo na Masharti ya Kutoa huduma za SUMATRA zinafutwa. Matakwa ya kutoa huduma kupitia kampuni au ushirika Adhabu ya jumla Kumzuia Afisa Notisi ya kujiondoa kutoa huduma Mapitio TS. Na. 73 la 2020 Kufutwa T.S. Na. 412 la 2014 Dodoma, 2 Disemba, 2023 AHMED MOHAMED AME, Mwenyekiti wa Bodi 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Vigezo na Masharti ya Kutoa Huduma Zinazodhibitiwa za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka, 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in