Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa za Mwaka, 2023
This section names the bylaw as the Iringa Municipal Council Fees and Taxes By-law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa za Mwaka, 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section names the bylaw as the Iringa Municipal Council Fees and Taxes By-law, 2023. This by-law applies throughout the entire area of Iringa Municipal Council. This section defines key terms used in the by-law, including fees, permits, the council, markets, stations, charges, culture, motor vehicles, and agents. Halmashauri inapaswa kutoza ada na ushuru kwa vibali, leseni, na huduma zake, kwa viwango vilivyo kwenye Jedwali la Kwanza. Mtu anayestahili kulipa ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hii lazima alipe kwa viwango vilivyoainishwa humo.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa za Mwaka, 2023
Showing 45 of 45
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This section names the bylaw as the Iringa Municipal Council Fees and Taxes By-law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Iringa Municipal Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including fees, permits, the council, markets, stations, charges, culture, motor vehicles, and agents.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya vibali au leseni mbalimbali zitolewazo na Halmashauri; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Iringa; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa na Halmashauri; “madini ya ujenzi” maana yake ni tarazo, moramu, udongo, kifusi, kokoto, mawe, mchanga, chokaa na madini mengine yanayotumika katika ujenzi; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “soko” maana yake ni eneo lililotengwa na linalomilikiwa na Halmashauri kama soko; 1 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) “stendi” maana yake ni eneo maalumu lililotengwa au kujengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria au mizigo hii itajumuisha pia kituo cha kupaki malori na vituo vingine vidogo vidogo vya kupakia na kushusha abiria vya Halmashauri; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli au huduma mbalimbali zinazofanywa katika eneo la Halmashauri; “utamaduni” inajumuisha sanaa za maonyesho, sanaa za ufundi, muziki wa asili, ususi, michezo, disko, muziki wa dansi, picha mjongeo, muziki wa taarabu, maonyesho ya sinema, mazingaombwe, tiba za jadi na matumizi ya viwanja vya michezo; “vyombo vya moto” maana yake ni magari, mitambo na pikipiki za aina zote; na “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni iliyoteuliwa kukusanya ada na ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ada na ushuru kwa ajili ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inapaswa kutoza ada na ushuru kwa vibali, leseni, na huduma zake, kwa viwango vilivyo kwenye Jedwali la Kwanza.
4.-(1) Halmashauri itatoza ada na ushuru kwa ajili ya vibali, leseni na huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (2) Ada au ushuru unaotozwa chini ya Sheria Ndogo hii utalipwa kwa Halmashauri au wakala wa Halmashauri kama Halmashauri itakavyoelekeza. (3) Malipo ya ada au ushuru yatalipwa kabla au wakati wa kupokea huduma inayotozwa ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hii. Utozaji wa ada na ushuru Wajibu wa kulipa ada na ushuru - 5 Verify source ↗
Mtu yeyote anayestahili kulipa ada au ushuru kwa
AI-assisted research summary: Mtu anayestahili kulipa ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hii lazima alipe kwa viwango vilivyoainishwa humo.
5. Mtu yeyote anayestahili kulipa ada au ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii atatakiwa kulipa ada au ushuru huo kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. Muda wa kukusanya ada au ushuru - 6 Verify source ↗
(1) Muda wa kukusanya ada au ushuru utakuwa ni
AI-assisted research summary: Ada au ushuru hukusanywa kati ya saa 12:00 asubuhi na saa 12:00 jioni, na unaweza kukusanywa baada ya muda huo kwa kibali maalumu cha Mkurugenzi.
6.-(1) Muda wa kukusanya ada au ushuru utakuwa ni kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), Halmashauri au wakala kwa kibali maalumu kutoka kwa 2 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) Utoaji wa stakabadhi za malipo Ukusanyaji wa madeni Mkurugenzi, anaweza kukusanya ada au ushuru baada ya muda uliotajwa hapo juu. (3) Malipo ya ada au ushuru yatafanyika kila siku au kwa mwezi au kwa namna yeyote itakayokubalika kulingana na makubaliano yatakayowekwa kati ya Halmashauri na mlipa ada au ushuru. - 7 Verify source ↗
(1) Ada au ushuru utakaotozwa kwa mujibu wa
AI-assisted research summary: Ada au ushuru hulipwa kwa Halmashauri au wakala anayetoa stakabadhi ya kielektroniki, na mlipaji lazima aitake na aikague stakabadhi hiyo.
7.-(1) Ada au ushuru utakaotozwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii utalipwa kwa Halmashauri au kwa wakala ambaye atatoa stakabadhi ya kielektroniki kama kielelezo cha malipo yaliyofanyika. (2) Mlipa ada au ushuru atakuwa na wajibu wa kudai na kuhakiki stakabadhi ya malipo kulingana na kiasi cha fedha alicholipa. (3) Utakuwa si utetezi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, mtu kudai kuwa amelipa ada au ushuru bila kupewa stakabadhi ya kielektroniki. - 8 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kukusanya ushuru kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuchukua hatua za kisheria kukusanya ushuru au ada ambazo hazijalipwa, ikijumuisha kukamata na kuuza mali kwa masharti fulani.
8.-(1) Halmashauri inaweza kukusanya ushuru kwa njia ya mahakama endapo mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni itakuwa imeshindwa kulipa ada au ushuru kwa muda uliokubaliwa. (2) Bila kuathiri masharti yaliyoainishwa katika aya ndogo ya (1), Halmashauri inaweza kukusanya madeni ya ushuru kwa njia ya kukamata au kushikilia mali zinazohamishika za wadaiwa zenye thamani sawa na deni la ushuru pamoja na gharama za kukamata. (3) Baada ya kipindi cha siku thelathini kupita tangu kukamatwa kwa mali za mdaiwa, Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuziuza kwa njia ya mnada baada ya kupata idhini ya mahakama. (4) Endapo mali zilizokamatwa zinaweza kuharibika kwa haraka, Halmashauri itakuwa na uwezo wa kuziuza kabla hazijaharibika baada ya kupata idhini ya mahakama. (5) Bila kuathiri masharti yaliyowekwa katika aya ndogo ya (3) na (4), kabla ya kuuza mali yoyote iliyokamatwa, Mkurugenzi atatoa taarifa ya siku saba kwa mdaiwa na umma juu ya kusudio la kuuza mali hizo. (6) Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote ile itakayotokea wakati wa kukusanya madeni au kwa mali itakayokamatwa na kushikiliwa na Halmashauri, isipokuwa 3 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) Ushuru wa nyumba za kulala wageni Uteuzi wa wakala kama hasara hiyo itakuwa imesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri au wakala. - 9 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni lazima alipe 10% ya mapato yanayolipwa na mgeni aliyesajiliwa, na awasilishe ushuru huo kwa Halmashauri kila mwezi ndani ya siku 7 baada ya mwisho wa mwezi wa malipo.
9.-(1) Kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni anapaswa kulipa asilimia kumi ya mapato yaliyolipwa na mgeni aliyesajiliwa. (2) Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni atawajibika kuwasilisha ushuru wa nyumba ya kulala wageni kila mwezi kwa Halmashauri ndani ya siku saba tangu kumalizika kwa mwezi wa malipo. - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kuteua wakala kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake, na wakala huyo lazima akusanye, apokee, na awasilishe makusanyo kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa.
10.-(1) Halmashauri inaweza kuteua wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kwa ajili ya kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa aya ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa- (a) kukusanya na kupokea ada au ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kukusanya ada au ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. Mamlaka ya afisa mwidhiniwa - 11 Verify source ↗
Bila kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo, jengo au chombo cha usafiri wakati wa saa za mchana kwa ajili ya kukusanya ada, ushuru, kufanya tathmini, au kushughulikia mambo ya leseni au kibali chini ya Sheria Ndogo hii.
11. Bila kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo hii, afisa mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo, jengo au chombo cha usafiri kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni kwa nia ya kukusanya ada au ushuru, kufanya tathmini au kufanya jambo lolote linalohusu ada, ushuru, leseni au kibali kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Ulipaji wa gharama za kuhifadhi mzigo au chombo kilichokamat wa - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza kiasi cha asilimia tano ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kutoza ada ya asilimia 5 kwa siku kwa mzigo uliokamatwa uliokuwa unasafirishwa bila kulipiwa, na inaweza kuuza kwa mnada mzigo au chombo kisicholipiwa ndani ya siku 7.
12.-(1) Halmashauri itatoza kiasi cha asilimia tano ya thamani ya chombo kilichobeba mzigo kwa kila siku kwa mzigo ulioshikiliwa baada ya kukamatwa ukisafirishwa bila ya kulipa ada au ushuru. (2) Chombo au mzigo husika usipokuwa umelipiwa kwa muda wa siku saba Halmashauri itauza mzigo au chombo hicho kwa njia ya mnada ili kufidia gharama zake. 4 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) Fidia ya gharama za uendeshaji wa zoezi Makosa na adhabu - 13 Verify source ↗
Endapo mtu anayepaswa kulipa ada au ushuru
AI-assisted research summary: Mtu anayepaswa kulipa ada au ushuru akiepuka kulipa, mkosaji lazima alipe gharama zote ambazo Halmashauri ilitumia wakati wa kumkamata.
13. Endapo mtu anayepaswa kulipa ada au ushuru atakwepa kulipa gharama zote ambazo zitakuwa zimetumika na Halmashauri wakati wa kumkamata, mkosaji atawajibika kuzilipa. - 14 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Anyone who commits any of the listed acts relating to fees or taxes under the by-law commits an offence, and conviction can lead to a fine, imprisonment, or both.
14.-(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atashindwa kulipa ada au ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) atamshawishi mtu au kundi la watu kukwepa au kukataa kulipa ada au ushuru; (c) atamzuia Mkurugenzi, afisa mwidhiniwa au wakala kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (d) atatoa taarifa za uongo kwa Halmashauri au wakala kuhusu huduma zinazohitaji kulipiwa ada au ushuru; (e) atashindwa kuweka kumbukumbu, vitabu, hesabu, na yatakayohitajika yoyote au maelezo Halmashauri; (f) atashindwa, atadharau, atakaidi au kukataa kulipa ada au ushuru au kutekeleza agizo lolote alilopewa na Halmashauri kuhusiana na ulipaji wa ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hii; au (g) atatengeneza, ataidhinisha atatayarisha, kutengeneza au atatunza nyaraka za uongo kwa nia ya kujipatia manufaa yatokanayo na ukusanyaji wa ada au ushuru ndani ya Halmashauri. (2) Mtu atakayetiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hii atatakiwa kulipa faini ya kiasi kisichopungua shilingi laki mbili na kisichozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 15 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa na kumtoza mhalifu kiasi kisichozidi shilingi laki mbili, ikiwa mhalifu anakiri kosa na yuko tayari kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Pili.
15. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. 5 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) Kufutwa kwa Sheria Ndogo TS. Na. 220 la 2018 - 16 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii inafuta Sheria Ndogo ya Ada na
AI-assisted research summary: This section repeals the Iringa Municipal Council Fees and Charges By-law of 2018.
16. Sheria Ndogo hii inafuta Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ya Mwaka 2018. 6 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) __________ JEDWALI LA KWANZA __________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 4(1)) SEHEMU YA KWANZA Ushuru wa Madini ya Ujenzi Namba Aina ya madini
Part
SEHEMU YA KWANZA
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Hii ni orodha ya ada na ushuru kwa shughuli za madini ya ujenzi na baadhi ya vibali vinavyohusiana, pamoja na ada za kumbi na vifaa vya halmashauri.
3. Utozaji wa usombaji wa aina zote za madini ya ujenzi Utoaji wa kibali cha kuchimba madini ya ujenzi Utoaji wa kibali cha kufyatua tofari za udongo au kuchoma tanuru Kiwango cha Ada na Ushuru (Shilingi) 12,000/= kwa tripu 150,000/= kwa muda wa miezi sita 300,000/= kwa muda wa mwaka mmoja 20,000/= kwa mwaka 100,000/= kwa tanuru kwa mwaka SEHEMU YA PILI Ada ya Kumbi na Vifaa vya Halmashauri Namba Ukodishaji wa Kumbi na Thamani Kiwango cha Ada na Ushuru (Shilingi)
Part
SEHEMU YA PILI
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: This provision lists daily rental charges for Halmashauri halls and chairs in Kitanzani.
2. (ii) Ukodishaji wa kumbi za Halmashauri (Kitanzini) (a) Ukumbi mkubwa (b) Ukumbi mdogo viti vidogo (iii) viti vya chuma (a) 200,000/= kwa siku (b) 50,000/= kwa siku 300/= kimoja kwa siku 500/= kimoja kwa siku - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: The text lists two daily charge amounts: 500/= and 1,000/= for each item, under a section on meat inspection levy.
4. Meza ndogo Meza kubwa 500/= kila moja kwa siku 1,000/= kila moja kwa siku SEHEMU YA TATU Ushuru wa Ukaguzi wa Nyama Namba Aina ya mnyama Kiasi cha Ushuru (Shilingi)
Part
SEHEMU YA TATU
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: This provision lists local charges for livestock and poultry, including amounts for cattle, goats/sheep, pigs, and chickens.
4. Ng’ombe Mbuzi au kondoo Nguruwe Kuku 10,000/= kwa kila Ng’ombe 3,000/= kwa kila Mbuzi au Kondoo 3,000/= kwa kila Nguruwe 200/= kwa kila kuku SEHEMU YA NNE 7 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) Ada ya Kuanika Ngozi Namba Aina ya mnyama Idadi ya vipande vya ngozi Kiasi cha Ushuru (Shilingi)
Part
SEHEMU YA NNE
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: This section sets daily meat storage charges for cattle and for goats/sheep, with different amounts depending on the number of animals.
4. Ng’ombe Ng’ombe Mbuzi na Kondoo Mbuzi na Kondoo kuanzia 1 hadi 1000 kuanzia 1000 na kuendelea kuanzia 1 hadi 1000 kuanzia 1000 na kuendelea 50,000/= 100,000/= 25,000/= 50,000/= SEHEMU YA TANO Ushuru wa Kuhifadhi Nyama Namba Aina ya Mnyama Kipimo Kiasi cha ushuru kwa siku (Shilingi).
Part
SEHEMU YA TANO
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: The text shows a fee schedule for transporting livestock outside the council area.
2. Ng’ombe Mbuzi au Kondoo 5,000/= kilo 50 kwa Mbuzi au kondoo 1,000/= SEHEMU YA SITA Ushuru wa Kusafirisha Mifugo nje ya Halmashauri Namba Aina ya mnyama Kiasi cha ushuru kwa siku (Shilingi)
Part
SEHEMU YA SITA
- 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Egg trays are free for 1 to 100 trays; from tray 101 onward, a charge applies per tray.
9. Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Mbwa Paka Punda/Farasi Mayai trei 1 hadi 100 ni bure ila kuanzia trei 101 na kuendelea kila trei Kuku ndani na nje ya Halmashauri 2,500/= 1,000/= 1,000/= 1,500/= 1,000/= 1,000/= 2,500/= 200/= kwa trei 200/=kwa kuku SEHEMU YA SABA Ushuru wa Utumiaji wa Masoko Namba Aina ya bidhaa
Part
SEHEMU YA SABA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: A daily fee of Shilingi 500 is stated for table use.
1. Ushuru wa Meza Kiwango cha Ushuru (Shilingi) 500/= kwa siku SEHEMU YA NANE Ushuru kwa matumizi ya Minada, Bidhaa na Magulio Mengine Namba Aina ya Bidhaa Kiwango cha Ada na Ushuru kwa siku (Shilingi) 8 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.)
Part
SEHEMU YA NANE
- 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: Kifungu kinaorodhesha bidhaa na shughuli mbalimbali pamoja na ada ya Sh 500 kwa kila moja, na kinaanza sehemu ya ada ya ukodishaji mitambo.
16. Bidhaa zinazotengenezwa viwandani na karakana Wauza mitumba Wauza bia na vinywaji baridi Wauza nafaka Mfugo aina ya ndege Pombe za asili Wauza madawa ya asili Wauza vipuri vya baiskeli, pikipiki, magari Wauza dagaa Wauza samaki Wauza chumvi, nyama, na mboga za majani Wauza vyungu Wauza vyombo vya nyumbani Wauza viatu Wauza nguo mpya Fundi baiskeli 500/= 500/= 500/= 500/= kwa kila gunia la kilo 100 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= 500/= SEHEMU YA TISA Ada ya Ukodishaji Mitambo Namba Aina ya kifaa Kiwango cha Ada na Ushuru kwa siku (Shilingi)
Part
SEHEMU YA TISA
- 17 Verify source ↗
Section 17
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaorodhesha aina za vibali vya ujenzi na ada zao kwa shilingi.
17. Isuzu tipa ya tani 10 Isuzu tipa ya tani 7 Lori la mizigo tani 3.5 na kreni Mashine ya kuchanganyia saruji Mashine ya kutoa hewa kwenye sakafu Mashine ya kukata sehemu ngumu ya sakafu au lami iliyoharibika Mashine ya kusafisha barabara Mashine ya kuzalisha hewa Mashine ya mkono ya kushindilia barabara Mashine ya kushindilia barabara Mashine ya kushindilia kifusi Gari la kubeba maji Mtambo wa kumimina lami Mtambo wa kumimina lami kwa mkono Mashine ya kusambaza kukoto kwenye barabara Kijiko Greda 200,000/= 150,000/= 120,000/= 80,000/= 50,000/= 100,000/= 100,000/= 200,000/= 100,000/= 250,000/= 70,000/= 150,000/= 150,000/= 200,000/= 200,000/= 600,000/= 800,000/= SEHEMU YA KUMI Vibali vya Ujenzi Namba Aina ya kibali cha ujenzi Kiwango cha Ada na Ushuru (Shilingi)
Part
SEHEMU YA KUMI
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This section sets fees for residential plots based on land size and adds a fee for each additional house built.
1. Viwanja vya makazi (i) mita za mraba 0 hadi 600 35,000/= 9 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) (ii) mita za mraba 601 hadi 1200 (iii) mita za mraba 1200 na 45,000/= 55,000/= kuendelea (iv) ujenzi wa nyumba zaidi ya 20,000/= kwa kila nyumba itayoongezeka - 15 Verify source ↗
Section 15
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaorodhesha ada/ushuru unaohusiana na vibali vya ujenzi na pia inaanza jedwali la ada na ushuru wa maegesho.
15. moja (shule, vyuo, Taasisi mbalimbali nyumba za ibada, ofisi mbalimbali, kumbi) ambazo sio ghorofa Viwanda vikubwa Viwanda vya uzalishaji Viwanda vidogo Vituo vya mafuta ukarabati Uzio au fensi (nyumba,taasisi) Hifadhi ndogo, uwanja wa michezo, hoteli za utalii ambazo sio ghorofa Ghorofa Ghorofa 1 hadi 3 Ghorofa 4 hadi 6 Ghorofa 6 na kuendelea Kuhuisha kibali cha ujenzi wa ghorofa Kusimika minara ya mawasiliano Kuhuisha kibali cha ujenzi usio wa ghorofa 200,000/= 300,000/= 200,000/= 100,000/= 200,000/= 35,000/= 100,000/= 200,000/= 175,000/= na kwa 200,000/= 200,000/= inayoongezeka ni 75,000/= 200,000/= 500,000/= Ada ni kama ilivyo kwa kibali cha awali. kila ghorofa SEHEMU YA KUMI NA MOJA Ada na Ushuru wa Maegesho Namba Aina ya Gari Kiwango cha Ada na Ushuru kwa siku (Shilingi)
Part
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
- 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaorodhesha ada za kulaza/kutunza magari na pikipiki zilizokamatwa au kuzuiliwa, pamoja na ada ya kulaza magari kwenye vituo binafsi.
9. Gari lenye uwezo wa kubeba uzito chini ya tani 10 Lori lenye uwezo wa kubeba uzito zaidi ya tani 10 Gari dogo Pikipiki ya magurudumu mawili Pikipiki ya magurudumu matatu Gari dogo la mizigo Ada ya kutunza gari lililokamatwa au kuzuiliwa Ada ya kutunza pikipiki iliyokamatwa au kuzuiliwa Ada ya kulaza magari kwenye vituo binafsi 2,500/ = 3,000/= 1,000/= 500/= 500/= 1,500/= 20,000/= kwa siku 10,000/= kwa siku 100,000/= kwa mwaka SEHEMU YA KUMI NA MBILI Ada ya Kulaza Magari Maeneo yanayomilikiwa na Halmashauri Namba Aina ya Gari
Part
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Section 2 lists daily fees/charges for a large bus and a small bus.
2. Basi kubwa Basi dogo Ada na Ushuru kwa siku (Shilingi) 3,000/= 2,000/= 10 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaonyesha ada/ushuru kwa magari madogo ya abiria na ya mizigo, ikiwa ni 1,000/= na 1,500/=.
4. Gari dogo la abiria Gari dogo la mizigo 1,000/= 1,500/= SEHEMU YA KUMI NA TATU Ushuru wa Kuingiza Vyombo vya Moto Stendi Namba Aina ya Gari
Part
SEHEMU YA KUMI NA TATU
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: This section lists daily fees and one entry charge for different vehicle types and passengers entering the stand.
8. Basi kubwa Basi ya kati Gari dogo la abiria Gari dogo Gari la mizigo -tani 1 hadi 3 -tani 4 hadi 10 Pikipiki ya magurudumu matatu Pikipiki ya magurudumu mawili Abiria atakayeingia Stendi Kiwango cha Ada na Ushuru kwa siku (Shilingi) 2,500/= 2,000/= 1,500/= 1,000/= 1,000/= 2,500/= 500/= 300/= 200/= kila anapoingia SEHEMU YA KUMI NA NNE Ada ya Huduma za Usafi Namba Taasisi Kiwango cha ushuru kwa Mwaka (Shilingi) Kiwango cha Ushuru kwa Mwezi (Shilingi)
Part
SEHEMU YA KUMI NA NNE
- 23 Verify source ↗
Section 23
AI-assisted research summary: This section lists fees/charges for different types of institutions, businesses, and premises.
23. Taasisi zote na mashirika Hospitali ya rufaa Viwanda vikubwa Viwanda vya kuoka mikate Hoteli za kitalii Migahawa Useremala Wauza mbao Mashine ndogo za kusaga na kukoboa Duka la jumla Duka la rejareja Ghala Viwanda vidogo vya kukamua mafuta Bucha za samaki au nyama Machinjio Baa na mgahawa Mini super market Vilabu vya pombe za kienyeji Nyumba ya kuishi kwa kila kaya Saluni za wanaume na wanawake Grosari Nyumba za kulala wageni Vituo vya afya na zahanati 360,000/= 600,000/= 600,000/= 360,000/= 300,000/= 60,000/= 50,400/= 60,000/= 36,000/= 60,000/= 25,000/= 300,000/= 50,000/= 30,000/= 300,000/= 60,000/= 60,000/= 30,000/= 24,000/= 36,000/= 36,000/= 600,000/= 60,000/= 11 30,000/= 50,000/= 50,000/= 30,000/= 25,000/= 5,000/= 4,200/= 5,000/= 3000/= 5,000/= 2,000/= 25,000/= 5,000/= 2,500/= 25,000/= 5,000/= 5,000/= 2,500/= 2,000/= 3000/= 3000/= 5,000/= 5,000/= Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) - 37 Verify source ↗
Section 37
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaorodhesha viwango vya ushuru wa soko kwa aina mbalimbali za maduka na bidhaa.
37. 60,000/= Vituo vya mafuta 60,000/= Maduka ya vifaa vya ujenzi 36,000/= Maduka ya nguo na viatu 60,000/= Maduka ya dawa (Famasi) 36,000/= Maduka ya dawa muhimu 25,000/= Maduka ya mikate na vitafunwa Maduka ya vyombo 25,000/= Maduka ya kuuza magodoro na samani 30,000/= 60,000/= Maduka ya kuuza spea za magari, pikipiki na baiskeli Maduka ya kuuza shajala na kudurufu Maduka ya kuuza vipodozi Maduka ya kuuza simu au saa Mama na Baba Lishe Mgahawa 60,000/= 36,000/= 36,000/= 30,000/= 60,000/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 5,000/= 3,000/= 2,000/= 2,000/= 2,500/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 3,000/= 2,500/= 5,000/= SEHEMU YA KUMI NA TANO Ushuru wa Soko kwa Mazao au Bidhaa zitokanazo na Mazao Namba Aina ya Bidhaa
Part
SEHEMU YA KUMI NA TANO
- 19 Verify source ↗
Section 19
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaorodhesha ada na ushuru kwa bidhaa na huduma mbalimbali, zikiwemo viwango tofauti kwa gunia, tenga, au tani.
19. Mahindi Maharage Muhogo Mtama Mpunga Dagaa Samaki Vitunguu Alizeti Kabeji, machungwa, miwa, nanasi, ndizi, parachichi Viazi Hoho Karanga Njegere maganda Pumba za mpunga Mashudu ya Alizeti Nyanya Mchele Unga Kiwango cha Ada na Ushuru (Shilingi) 1,000/= kwa kila gunia. 1,500/= kwa kila gunia 500/= kwa kila gunia 1,500/=kwa kila gunia 1,500/=kwa kila gunia 1,500/=kwa kila gunia 3,000/= kwa tenga kubwa na 1,500 /= kwa tenga dogo 1,500/= kwa kila gunia 1,000/= kwa kila gunia 7,000/= kwa kila tani moja 1,500/= kwa kila gunia 500/= kwa kila gunia 2,500/= kwa kila gunia 1,000/= kwa kila gunia 500/= kwa kila gunia 1,000/= kwa kila gunia 500/= kwa kila tenga 1,000/= kwa kila gunia au kilo mia moja 500/= kwa kila gunia au kila roba au kilo mia moja 12 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) SEHEMU YA KUMI NA SITA Ada ya Shughuli za Burudani, Utamaduni, Sanaa na Matangazo Namba Aina ya Huduma
Part
SEHEMU YA KUMI NA SITA
- 22 Verify source ↗
Section 22
AI-assisted research summary: This section lists fees for various events, advertisements, performances, and related activities, including amounts based on venue size and time period.
22. Washereheshaji Wapambaji wa kumbi za burudani, harusi, sherehe za jikoni, sherehe za kuanga binti na nyinginezo Mpiga muziki (D.J) Wamiliki wa kumbi mbalimbali kuuza bidhaa Matangazo ya barabarani ya sherehe Wapishi wa vyakula Picha jongevu na mnato Matangazo ya zinazopungua bei Maombi ya kibali cha kufanya tiba za jadi Matamasha Fete na bahati nasibu Mnada Kupiga muziki ukumbi mkubwa Kupiga muziki ukumbi mdogo Matangazo ya biashara kwa kutumia vipaza sauti au vipeperushi na au fani za sanaa Udhamini wa vipindi, tamthilia Taarifa ya Habari Maandishi kupita sauti Picha Picha Mahojiano Matangazo ya makampuni mbalimbali asubuhi,mchana na jioni filamu na Kiwango cha Ada au Ushuru (Shilingi) 50,000/= kwa tukio 50,000/= kwa tukio 50,000/=kwa tukio Ukumbi unaochukua watu 100-200 shilingi 20,000 /=, ukumbi unaochukua watu 300-500 ni shs. 40,000/= kwa kila siku 50,000/= kwa moja kwa siku 50,000/= kwa tukio na kwa mpishi moja 30,000/= kwa tukio moja kwa moja 40,000/= kwa tangazo 20,000/= kwa siku 100,000/= kwa tamasha 20,000/= kwa siku 40,000/= kwa mnada 100,000/= kwa siku 40,000/= kwa siku 30,000/= kwa siku 755,000/= kwa dakika 30 hadi 35 2,500,000/= kwa siku 30 10,000/= kwa sekunde 60 300,000/= kwa sekunde 60 1,000,000/= kwa siku 7 250,000/= kwa dakika 30 3,000,000/= kwa sekunde 60 SEHEMU YA KUMI NA SABA Ada za Ukataji Barabara Namba Aina ya ukataji Barabara Ukubwa Gharama (Shilingi)
Part
SEHEMU YA KUMI NA SABA
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: The text shows fee amounts, including an annual-style fence fee payable every three months, and a registration-fee table for transport/taxi-related items.
4. Barabara ya lami Barabara ya changarawe Barabara ya vumbi Ada ya uzio[inalipwa kila baada ya miezi mitatu] Mita moja Mita moja Mita moja Mita moja ya mraba 200,000/= 80,000/= 30,000/= 3,000/= 13 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) SEHEMU YA KUMI NA NANE Ada za Usajili wa Teksi Namba Aina ya Chombo cha Usafiri Ada (Shilingi) Muda
Part
SEHEMU YA KUMI NA NANE
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: A yearly amount of TZS 100,000 is stated for forest produce tax.
1. Teksi 100,000/= Kwa kila mwaka SEHEMU YA KUMI NA TISA Ushuru wa Mazao ya Misitu Namba
Part
SEHEMU YA KUMI NA TISA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Ushuru kwa mazao ya misitu ni asilimia 5 ya bei ya kununulia.
1. Aina zote za mazao ya misitu Aina zote za mazao ya misitu Kiwango cha ushuru Asilimia tano (5%) ya bei ya kununulia SEHEMU YA ISHIRINI Ushuru wa Mazao ya Uvuvi Namba Aina Uzito Kiasi cha ushuru kwa siku (Shilingi)
Part
SEHEMU YA ISHIRINI
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Inaonyesha ushuru wa siku kwa samaki kilo 1 kuwa Shilingi 15.
1. Samaki Kilo 1 15/= SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA Ushuru wa Kupakia na Kushusha Mazao Namba Aina Uzito Kiasi cha ushuru kwa siku (Shilingi)
Part
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This section appears to be a fee schedule for mobile towers, with annual fees stated in shillings.
1. Mazao Tani 1 3,000/= SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI Ada ya Minara ya Simu Namba Aina ya Ada Kiasi cha Ada kwa Mwaka (Shilingi)
Part
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaonyesha kiasi cha ushuru/ada kwa mmiliki wa mnara wa simu na kwa bango la tangazo lililowekwa kwenye eneo la Halmashauri, kisha inaanza sehemu ya ushuru kwenye vivutio vya utalii.
2. Mmiliki wa mnara wa simu Mmiliki lilikosimikwa bango la Tangazo kwenye eneo la Halmashauri 100,000/= 10,000/= kwa mita moja ya mraba SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU Ushuru kwenye Vivutio vya Utalii Namba Aina ya ushuru Kiasi cha ushuru kwa siku (shilingi)
Part
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaonyesha ada za vivutio vya utalii, zikiwemo viwango tofauti kwa mtoto na mtu mzima.
4. Vivutio vya utalii vya ndani Vivutio vya utalii wa ndani Vivutio vya utalii kwa raia wa kigeni Vivutio vya kitalii kwa raia wa kigeni 500/= kwa Mtoto 1,000/= kwa Mkubwa 1,500/= kwa Mtoto 3,000/= kwa Mkubwa 14 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE Ada ya Ujenzi wa Vituo vya Kuoshea Vyombo vya Moto na Viwanda vya Kufyatua Tofali Namba Sehemu husika Ada kwa Mwezi (Shilingi)
Part
Sehemu husika
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: The text appears to list local fees, including amounts for large and small brick-making factories and a container entry fee for a council area.
4. Maeneo ya katikati ya Manispaa Nje ya maeneo ya katikati ya Manispaa Viwanda vikubwa vya kufyatua tofali Viwanda vidogo vya kufyatua tofali 100,000/= 50,000/= 100,000/= 50,000/= SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO Ada ya kuingiza kontena kwenye eneo la Halmashauri Namba Ukubwa wa kontena
Part
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: The text shows a fee schedule by tonnage and a form for admitting an offence and agreeing to pay the owed fee or tax plus a fine.
4. Tani 3 hadi 10 Tani 11 hadi 20 Tani 21 hadi 30 Tani 30 na kuendelea Kiasi kwa tani (Shilingi) 50,000/= 100,000/= 150,000/= 300,000/= 15 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) ______________ JEDWALI LA PILI _______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 15) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA ........................................................................ nakiri KWA HIARI YANGU MIMI Mimi MWENYEWE mbele ya........................................................... ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwamba Tarehe ..........ya Mwezi .................. Mwaka................ nilitenda kosa kwa kukiuka masharti ya aya ya ……..ya Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ya Mwaka 2023. Hivyo, kwa kuzingatia masharti ya sheria husika, nipo tayari kulipa kiasi cha ada au ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe …………………..ya Mwezi …………… Mwaka ………………… Jina: …………………………………………. Saini: ……………………………. MBELE YA: Jina: …………………………………… Wadhifa: ………………………………. Saini: ……………………………….. Tarehe: …………………………… 16 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.29 (Linaendelea.) Nembo na Chapa ya Halmashauri yaManispaa ya Iringa imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa na Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ulioitishwa na kufanyika tarehe 28 Januari, 2022 na ulibandikwa mbele ya:- KASTORI G. MSIGALA, Mkurugenzi, Halmashauri ya Manispaa Iringa IBRAHIM A. NGWADA, Meya Halmashauri ya Manispaa Iringa L.S NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (Mb.), 30 Novemba, 2023 Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, 17
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa za Mwaka, 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in