Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi Wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ya Mwaka, 2024
This provision gives the by-law’s short title: the Iringa Municipal Council Health, Sanitation and Environmental Management By-law of 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi Wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ya Mwaka, 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the by-law’s short title: the Iringa Municipal Council Health, Sanitation and Environmental Management By-law of 2023. This by-law applies throughout the area of Iringa Municipal Council. This section defines terms used in the by-law, including officer, food, water source, council, cleanliness certificate, business building, household, nuisance, permit, epidemic diseases, wastewater, livestock, resident, director, waste, solid waste, and agent. Halmashauri lazima isimamie usafi, afya na mazingira, ielimishe wananchi, na ifanye ukaguzi. Pia ina mamlaka ya kuteua wengine kutekeleza shughuli hizi, kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka, na kuingia mikataba ya utekelezaji. Wamiliki wa nyumba au maeneo ya biashara lazima waweke mazingira yao safi, wadhibiti taka na maji taka, na wafanye matengenezo ya jengo; wafanyabiashara wa matunda au miwa lazima wawe na chombo cha kuhifadhia mabaki; kutupa au kuacha taka sehemu zisizoruhusiwa ni kosa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi Wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ya Mwaka, 2024
Showing 47 of 47
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision gives the by-law’s short title: the Iringa Municipal Council Health, Sanitation and Environmental Management By-law of 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the area of Iringa Municipal Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines terms used in the by-law, including officer, food, water source, council, cleanliness certificate, business building, household, nuisance, permit, epidemic diseases, wastewater, livestock, resident, director, waste, solid waste, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa na binadamu na inajumuisha maji na dawa; “chanzo cha maji” maana yake ni eneo lolote ambalo limetengwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha maji kwa matumizi ya ikiwemo visima, mito, chemchemi, vijito na maeneo yote ambayo maji hupatikana; jamii “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Iringa; “hati ya usafi” maana yake ni hati inayotolewa na Afisa kwa Mwidhiniwa inayothibitisha maeneo yote yaliyotajwa katika Sheria Ndogo hii na sheria husika za afya kwa umma; kukaguliwa “jengo la biashara” maana yake ni jengo lolote lililojengwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kufanya biashara iliyokusudiwa; Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) “kaya” maana yake ni familia inayojumuisha baba, mama, mtoto au watoto na mtu mwingine yeyote anayeishi na familia hiyo au watu wanaokaa katika nyumba moja na kuishi kama familia au mtu yeyote anayeishi peke yake katika chumba au nyumba kwenye eneo la Halmashauri; “kero” maana yake ni kitu chochote ambacho kipo katika kimewekwa, hali kimejengwa au ni kichafu kiasi cha kusababisha- (a) hatari kwa viumbe na maisha ya kinatumika, yoyote iwe binadamu; (b) harufu mbaya au harufu ya kuudhi au kuleta kinyaa; (c) kuzaliana kwa wadudu hatari kama vile inzi, mende, sisimizi, panya, nyoka, nyuki, kunguni au viumbe wengine hatari; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “magonjwa ya mlipuko” maana yake ni magonjwa yanayotokea kwa muda mfupi ya kuambukiza na kuenea kwa haraka na kuathiri watu wengi ndani ya muda mfupi yanayoweza kutolewa amri ya taadhari, ikijumuisha kupooza, kipindupindu, kuhara, surua na homa ya matumbo; “maji taka” maana yake ni maji yenye mchanganyiko wa kinyesi, mkojo, na maji kutoka katika masinki ya kuogea, kutema mate na kunawia mikono, pamoja na maji yenye mchanganyiko wa vitu vingine vyenye asili ya kemikali au visivyo na kemikali; “mifugo” maana yake ni ng’ombe, punda, nguruwe, mbuzi, mbwa, kondoo au kuku na wanyama wengine wote wafugwao majumbani; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote anayeishi katika eneo la Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; Sura ya 191 “taka” ina maana iliyotolewa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni kitu chochote, tofauti na Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) kimiminika, ambacho baada ya kutumika kimepoteza thamani yake kwa jamii husika, na ambacho uwepo wake katika eneo husika unaweza kusababisha madhara au kuhatarisha afya ya jamii; na “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni iliyoteuliwa kukusanya ada na ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii. Wajibu na mamlaka ya Halmashauri - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima isimamie usafi, afya na mazingira, ielimishe wananchi, na ifanye ukaguzi. Pia ina mamlaka ya kuteua wengine kutekeleza shughuli hizi, kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka, na kuingia mikataba ya utekelezaji.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kusimamia utekelezaji wa shughuli za usafi, afya na mazingira; (b) kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kufuata kanuni za afya, usafi na kutunza mazingira; na (c) kufanya ukaguzi ili kuhakikisha uzingatiaji wa kanuni za afya, usafi na utunzaji wa mazingira ndani ya eneo la Halmashauri. (2) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya- (a) kuteua mtu yeyote, wakala, kikundi au taasisi kutekeleza shughuli za usimamizi wa afya, usafi na mazingira kwa niaba ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote anayekiuka Sheria Ndogo hii au sheria nyingine inayohusiana na afya, usafi na usimamizi wa mazingira; na (c) kuingia mkataba na mtu yeyote, taasisi au kampuni kutelekeza shughuli za usimamizi wa afya, usafi na mazingira kwa niaba ya Halmshauri katika eneo ndani ya Halmashauri. Wajibu wa kila mkazi au mfanyabiashara - 5 Verify source ↗
(1) Kila mkazi au mfanyabiashara anayemiliki
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba au maeneo ya biashara lazima waweke mazingira yao safi, wadhibiti taka na maji taka, na wafanye matengenezo ya jengo; wafanyabiashara wa matunda au miwa lazima wawe na chombo cha kuhifadhia mabaki; kutupa au kuacha taka sehemu zisizoruhusiwa ni kosa.
5.-(1) Kila mkazi au mfanyabiashara anayemiliki jengo au eneo la biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba- (a) majani yanayozunguka jengo lake au makazi yanakatwa au kupaliliwa na kuondolewa katika eneo lake; (b) taka ngumu zote ikijumuisha mifuko ya plastiki zinakusanywa na kuhifadhiwa katika eneo lililoruhusiwa na Halmashauri; (c) maji taka yanaelekezwa ndani ya mfumo wa maji taka; Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) (d) anaboresha na kupaka rangi jengo lake kila linapochakaa; (e) anakuwa na choo kilicho bora na kisafi wakati wote; (f) anashiriki siku ya usafi ya Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi au katika siku itakayopangwa na Halmashauri; (g) anaondoa uchafu ikiwemo mchanga, majani, nyasi au vitu vingine vinavyofanana na hivyo katika mifereji ya maji ya mvua inayomzunguka au kupita kando ya nyumba, eneo la biashara au kiwanja chake na kuhakikisha mifereji hiyo inakuwa safi wakati wote; (h) taa yenye mwanga inawekwa nje ya jengo analoishi au analolitumia kwa shughuli yoyote na atatakiwa kuiwasha wakati wa usiku; (i) hakuna mkusanyiko wa taka, maji taka au taka ngumu ambazo zinaweza kuathiri upitishaji wa maji ya mvua na hivyo kuruhusu uwepo wa mazalia ya mbu au wadudu wengine wenye madhara kwa afya ya binadamu na mazingira kwa ujumla; (j) anafanya uchambuzi wa taka kulingana na aina ya taka husika. (2) Kila mfanyabiashara wa matunda au miwa anapaswa kuhakikisha kuwa ana chombo maalumu cha kuhifadhia maganda au mabaki ya matunda. (3) Mtu yeyote anayetupa taka au uchafu wowote au kuacha taka au uchafu kwenye nyumba, kiwanja, mfereji wa maji ya mvua, barabara au eneo linalopakana na nyumba au ardhi yoyote au karibu na maeneo ya nyumba au mahali popote pasipotengwa kwa shughuli hiyo anatenda kosa. Kibali cha matengenezo ya vyombo vya moto - 6 Verify source ↗
(1) Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo
AI-assisted research summary: Vehicle, motorcycle, and machinery repairs must be done in approved workshops, garages, or other permitted places, and only after formal permission from the Council.
6.-(1) Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yatatakiwa kufanyika kwenye karakana, gereji au maeneo yaliyoruhusiwa baada ya kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri. (2) Mtu yeyote ambaye- (a) anatengeneza gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo halikutengwa kwa shughuli hiyo; (b) anaegesha magari mabovu kwenye njia ya miguu, Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) mtaa, uchochoro, mitaro, maeneo ya wazi au barabarani na kusababisha adha kwa wakazi au watumiaji wa njia hiyo; (c) anamwaga ovyo au kutiririsha mafuta, mafuta machafu na grisi katika maeneo yasiyoruhusiwa; au (d) anafanya biashara ya kuosha gari, pikipiki au ambalo mtambo wowote halikutengwa kwa shughuli hiyo au kuruhusu eneo lake kutumika kwa shughuli za kuosha vyombo vya moto katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hizo, katika eneo bila kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri, anatenda kosa. Udhibiti wa kelele kwa shughuli mbalimbali za kijamii - 7 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kusababisha kelele,
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kusababisha kelele bila kibali cha Halmashauri.
7. Mtu yeyote hataruhusiwa kusababisha kelele, ikijumuisha kufungulia muziki kwa sauti ya juu kupita kiasi na kelele za kiwanda, jenereta au kitu kingine chochote, bila kupata kibali cha Halmashauri. Wajibu wa Halmashauri kusimamia vyanzo vya maji Makosa yanayohusiana na vyanzo vya maji - 8 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: The council must protect water sources, take legal action in specified cases, and plant suitable non-water-absorbing trees in water-source areas according to expert guidance.
8. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kusimamia na kulinda vyanzo vya maji; (b) kuchukuwa hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote cha maji, kuchafua chanzo cha maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji bila sababu ya msingi; na atakayeharibu chanzo (c) kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo vya maji kwa kuzingatia maelekezo ya kitaalamu. - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kufanya vitendo vinavyohusisha chanzo cha maji au ndani ya mita 60 zake, na kufanya hivyo ni kosa.
9. Mtu yeyote ambaye- (a) ananawa, kuoga, kufulia nguo au kunywesha mifugo karibu au kwenye chanzo cha maji; (b) anafuga au kujenga boma la mifugo karibu, au kuruhusu mkojo ya mifugo au maji machafu kuelekea karibu, na chanzo cha maji; (c) anafanya shughuli yoyote ikiwemo, kujenga, kulima, kukata miti, kuchunga mifugo au jambo lingine lolote, ndani ya umbali wa mita sitini toka vyanzo vya maji au maeneo yanayohifadhiwa, zinazoweza kuharibu kwa namna yoyote chanzo cha maji au hifadhi ya mazingira; Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) (d) anamiliki eneo la chanzo cha maji asili; (e) anaelekeza mabomba ya maji machafu kwenye chanzo cha maji; (f) anaunganisha maji ya mvua na maji taka au kutapisha choo na kutiririsha vinyesi vya mifugo au binadamu kwenye chanzo cha maji au mfereji wa maji ya mvua; au (g) anaweka kitu chochote chenye sumu kwenye chanzo cha maji, anatenda kosa. - 10 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa kutiririsha au kumwaga au
AI-assisted research summary: No one may dump wastewater in public places or water areas not designated for wastewater storage, and factories and homeowners have storage and handling duties.
10.-(1) Mtu hataruhusiwa kutiririsha au kumwaga au kuruhusu au kusababisha kutiririsha au kumwaga maji taka barabarani, uchochoroni kwenye mifereji, mtoni, mabonde, kwenye vyanzo vya maji au sehemu yoyote ambayo haijatengwa kwa ajili ya kuhifadhi maji taka. (2) Kila kiwanda kinachozalisha maji taka kitakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa kinaunganisha maji taka au kujenga mifereji na mabwawa kwa ajili ya kuhifadhi maji taka. (3) Kila mmiliki wa nyumba atapaswa kuwa na karo la kuhifadhi maji taka na atawajibika kunyonya maji taka kutoka katika karo hilo iwapo litajaa na itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kuacha karo kujaa na kutiririsha maji taka barabarani au sehemu yoyote isiyoruhusiwa. - 11 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa kiwanda atakuwa na wajibu
AI-assisted research summary: Kila mmiliki wa kiwanda lazima ahakikishe taka kama vumbi, kelele, harufu mbaya, moshi, maji taka na taka nyingine hazileti kero au madhara kwa watu na viumbe hai wengine.
11.-(1) Kila mmiliki wa kiwanda atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa taka kama vile vumbi, kelele, harufu mbaya, maganda, moshi, maji taka na taka nyingine zinazoweza kuleta kero au adha kwa ujumla haziwafikii, wala hazileti kero au madhara kwa, binadamu na viumbe hai wengine. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya aya ndogo ya (1) atakuwa ametenda kosa. Kutiririsha maji taka Taka za viwanda Taka hatarishi - 12 Verify source ↗
Mtu, kampuni, wakala au taasisi haitaruhusiwa
AI-assisted research summary: Mtu, kampuni, wakala au taasisi haipaswi kuendesha uchomaji wa taka hatarishi bila kibali cha Halmashauri.
12. Mtu, kampuni, wakala au taasisi haitaruhusiwa kuendesha shughuli za uchomaji wa taka hatarishi bila kupata kibali kutoka Halmashauri. Utengenezaji na uuzaji vyakula - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kutengeneza, kuchoma,
AI-assisted research summary: Anyone is prohibited from making, burning, cooking, boiling, or selling any kind of food anywhere or in any house unless health and hygiene rules have been complied with.
13. Mtu yeyote hataruhusiwa kutengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha na kuuza chakula cha aina yoyote mahali popote au kwenye nyumba yoyote isipokuwa kam ametimiza Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) masharti na kanuni za afya. Uuzaji wa vyakula vilivyopikwa Usalama wa matumizi ya maji Makatazo Uzuiaji wa shughuli wakati wa magonjwa ya mlipuko - 14 Verify source ↗
Kila mtu anayeendesha biashara ya vyakula vya
AI-assisted research summary: Mtu anayeendesha biashara ya vyakula vya kupikwa au kukaangwa lazima ahakikishe vyakula hivyo vinahifadhiwa kwenye sanduku la mbao safi na kuwekwa kioo ili kuzuia inzi, vumbi na wadudu.
14. Kila mtu anayeendesha biashara ya vyakula vya kupikwa au kukaangwa atakuwa na wajibu wa kuhakikisha vyakula sanduku vinahifadhiwa lililotengenezwa kwa mbao safi na kuwekwa kioo kuzuia inzi, vumbi na wadudu waletao madhara kwa afya ya binadamu. kwenye hivyo - 15 Verify source ↗
(1) Kila mkazi anapaswa kuhakikisha kwamba
AI-assisted research summary: Kila mkazi lazima ahakikishe maji ya kunywa ni safi na salama; mmiliki wa kisima lazima ahakikishe maji ya kisima yamepimwa ili yawe salama.
15.-(1) Kila mkazi anapaswa kuhakikisha kwamba maji yote yanayotumika kwa kunywa ni safi na salama bila kujali yanatoka kwenye chanzo gani cha maji. (2) Kila mmiliki wa kisima atapaswa kuhakikisha maji ya kisima yamepimwa ili yawe salama kwa matumizi. - 16 Verify source ↗
(1) Mtu anayefanya biashara ya kuuza vyakula
AI-assisted research summary: Wauzaji wa vyakula visivyoiva lazima viweke vyakula juu ya meza na visiwekwe chini; pia hairuhusiwi kupanga vyakula nje ya duka la vyakula, na watu wanaohusika na biashara, hospitali, taasisi, kaya, jengo au kiwanda hawapaswi kusababisha uchafuzi wa hewa kwa kutoa moshi unaodhuru.
16.-(1) Mtu anayefanya biashara ya kuuza vyakula ambavyo havijapikwa atapaswa kuviweka juu ya meza na kuhakikisha kuwa vyakula hivyo haviwekwi chini. (2) Mtu hataruhusiwa kupanga vyakula nje ya duka la vyakula. (3) Mtu anayehusika na biashara, hospitali, taasisi, kaya, jengo au kiwanda hatafanya shughuli itakayosababisha uchafuzi wa anga hewa kwa kuachilia moshi angani unaoweza kuleta madhara kwa binadamu, mimea na viumbe hai. (4) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu hiki anatenda kosa. - 17 Verify source ↗
(1) Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia
AI-assisted research summary: The Director may prohibit certain activities if they may spread epidemic disease, and may arrest violators and seize related foods.
17.-(1) Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia shughuli yoyote isifanyike kama vile utengenezaji wa vyakula, pombe, mijumuiko, sherehe na mikusanyiko yoyote kwa kutangaza kwa njia ya kipaza sauti, maandishi au kupitia vyombo vya habari endapo atakuwa na sababu ya kuamini kwamba shughuli hiyo inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuleta athari kwa maisha ya binadamu. (2) Mkurugenzi anaweza kumkamata mtu yeyote ambaye atakiuka amri ya zuio la kufanyika kwa shughuli ya uuzaji wa vyakula wakati wa magonjwa ya mlipuko na kumchukulia hatua kwa mujibu wa masharti ya Sheria. (3) Wakati wa utekelezaji wa masharti ya kifungu kidogo cha (2), Mkurugenzi anaweza kukamata vyakula Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) vinavyohusika na ukiukwaji na endapo- (a) ni vyakula vinavyoharibika kwa haraka, kuviharibu vyakula hivyo; au (b) ni vyakula haraka, visivyoharibika kuvihifadhi kwa ajili ya hatua stahiki za kisheria. kwa Machinjio na maduka ya nyama - 18 Verify source ↗
(1) Mtu atakayechinja au kuuza nyama ya aina
AI-assisted research summary: Watu wanaochinja au kuuza nyama hawaruhusiwi kufanya hivyo katika maeneo yasiyo machinjio au maduka ya nyama au maeneo ambayo Halmashauri haijaruhusu. Wamiliki wa maduka ya nyama na wauzaji wa nyama pia wana masharti ya usafi na mavazi.
18.-(1) Mtu atakayechinja au kuuza nyama ya aina yoyote katika maeneo yasiyokuwa machinjio au maduka ya nyama au katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri anatenda kosa. (2) Kila mmiliki wa duka la kuuzia nyama atapaswa kuhakikisha kwamba duka lake- (a) ni jengo la kudumu lililowekwa marumaru nyeupe katika sakafu na ukutani hadi urefu wa futi sita kutoka usawa wa sakafu; (b) lina maji safi na misumeno ya kukatia nyama; (c) lina kabati ya vioo na jokofu la kuhifadhia nyama na sehemu za mizani; (d) lina pipa la kuhifadhia taka; na (e) lina mavazi maalumu kwa ajili ya kuendeshea biashara ikiwemo aproni, mabuti meupe na kofia. (3) Muuzaji wa nyama atatakiwa kuvaa vazi jeupe pamoja na aproni nyeupe na atapaswa kupima afya kila baada ya miezi sita. Uendeshaji wa biashara ya nyumba za kulala wageni na hosteli - 19 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba za kulala wageni na
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba za kulala wageni, hosteli, au nyumba za biashara lazima wapate kibali kutoka Halmashauri kabla ya kuanza biashara.
19.-(1) Kila mmiliki wa nyumba za kulala wageni na hosteli au nyumba za biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha anapata kibali kutoka Halmashauri kabla hajaanza biashara. (2) Endapo mmiliki hajakidhi masharti ya kiafya Halmashauri inaweza kuzuia kibali cha kuendesha biashara ya nyumba za kulala wageni au hosteli mpaka hapo mmiliki na atakapokuwa Halmashauri. amekidhi masharti yaliyotolewa Masharti ya kibali cha biashara ya nyumba ya kulala wageni, n.k. - 20 Verify source ↗
Kibali cha kuendesha biashara ya nyumba ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kutoa kibali cha biashara ya nyumba ya kulala wageni, mgahawa, hoteli au hosteli baada ya kujiridhisha kuwa majengo yanatimiza masharti ya usafi, huduma na vifaa vilivyoorodheshwa.
20. Kibali cha kuendesha biashara ya nyumba ya kulala wageni, mgahawa, hoteli na hosteli kitatolewa baada ya Halmashauri kujiridhisha kuwa katika majengo hayo kuna- (a) mwanga na hewa ya kutosha; (b) nafasi na vifaa au samani za kutosha; (c) mfumo wa uondoshaji wa maji taka na taka Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) ngumu wa kuaminika; (d) usafi wa jumla wa jengo na vifaa vyake; (e) vyoo na mabafu kwa jinsia zote; (f) vifaa vya zimamoto; (g) tanki la kuhifadhia maji safi; (h) vyoo na bafu vilivyowekwa marumaru katika sakafu na katika kuta hadi urefu wa futi sita kutoka usawa wa sakafu; (i) kuwa na jozi zaidi ya mbili za mashuka, foronya za mito na magodoro kwa kila kitanda na ziwe na rangi isiyoficha uchafu; (j) kuwepo na sehemu maalumu ya kufulia na kuanikia nguo; na (k) stoo na chumba cha kubadilishia nguo kwa ajili ya wafanyakazi. Upimaji wa afya Uwezo wa kukagua - 21 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa sehemu inayotoa huduma ya
AI-assisted research summary: Owners of listed food and hospitality places must make sure workers get a health check every six months, and they must not let untested workers work.
21.-(1) Kila mmiliki wa sehemu inayotoa huduma ya hoteli, migahawa, baa, bucha, sehemu za kuokea mikate, nyumba za kulala wageni, grosari au mtu yeyote anayetengeneza chakula kwa ajili ya kuuza atapaswa kuhakikisha kuwa wahudumu wake wanapima afya kila baada ya miezi sita. (2) Mmiliki yeyote atakayeruhusu mhudumu yeyote kufanya kazi bila kupimwa afya yake anatenda kosa. - 22 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa anaweza, wakati wowote
AI-assisted research summary: An authorized officer may enter any building during working hours or when a special inspection is needed to check compliance and enforcement. The Director may order closure of a business or building that has not been inspected, or that was inspected and found to violate health rules.
22.-(1) Afisa Mwidhiniwa anaweza, wakati wowote wakati wa saa za kazi na wakati wowote ukaguzi maalumu utakapohitajika, kuingia katika jengo lolote kwa lengo la kukagua uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kufungwa kwa biashara yoyote au jengo ambalo halijakaguliwa au lililokaguliwa na kukutwa limekiuka kanuni na masharti ya afya. Ada ya ukaguzi - 23 Verify source ↗
(1) Ada ya ukaguzi wa afya italipwa kila
AI-assisted research summary: Ada ya ukaguzi wa afya hulipwa mwanzoni mwa kila mwaka wa fedha wa Halmashauri. Asiyeilipa ndani ya miezi miwili baada ya mwaka kuanza lazima alipe deni hilo pamoja na adhabu ya asilimia 50.
23.-(1) Ada ya ukaguzi wa afya italipwa kila mwanzo wa mwaka wa fedha wa Halmashauri. (2) Mtu yeyote atakayeshindwa kulipa ada ya ukaguzi katika kipindi cha miezi miwili baada ya mwaka wa fedha kuanza atawajibika kulipa kiwango hicho pamoja na adhabu ya asilimia hamsini ya kiwango anachodaiwa. Udhibiti wa - 24 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayesafirisha mawe, mchanga au
AI-assisted research summary: Anyone transporting stones, sand, or gravel in the council area must cover the transport container or vehicle to prevent spilling and environmental pollution.
24. Mtu yeyote atakayesafirisha mawe, mchanga au Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) ubebaji kokoto, mawe na mchanga kokoto katika eneo la Halmashauri atahakikisha kuwa chombo anachotumia kusafirisha kimefunikwa ili kuzuia kumwagika na kuchafua mazingira. Ufuaji wa nguo - 25 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekusudia kufanya biashara ya
AI-assisted research summary: Anyone who wants to run a laundry business must get a hygiene certificate before starting.
25. Mtu yeyote anayekusudia kufanya biashara ya kufua nguo atapaswa kupata hati ya usafi kabla ya kuanza biashara hiyo. Kuchoma au kusababisha moto Uvunaji miti - 26 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: People are prohibited from burning in municipal areas or preparing land by burning, and residents must help extinguish a fire when a major fire occurs if they have no reasonable excuse.
26.-(1) Mtu yeyote ambaye- (a) anachoma moto kwa namna yoyote ile katika maeneo yaliyoko katika eneo la Halmashauri; taka ndani ya eneo la (b) anachoma moto Halmashauri; au (c) anaandaa shamba kwa njia ya kuchoma moto, anatenda kosa. (2) Endapo moto mkubwa utatokea katika eneo la Halmashauri, kiongozi wa eneo husika atawajibika kutoa ishara ya hatari kwa kutumia njia iliyozoeleka na kuhamasisha wakazi wa eneo hilo kushiriki katika zoezi la kuzima moto huo. (3) Mkazi wa eneo la Halmashauri linalowaka moto ambaye atashindwa kushiriki katika zoezi la kuzima moto bila sababu za msingi atakuwa ametenda kosa. - 27 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Watu hawaruhusiwi kukata miti katika eneo la Halmashauri bila kibali maalumu, au kuvuna miti katika msitu uliohifadhiwa kwa viumbe maalumu. Wanaotaka kuvuna miti kwa mkaa, mbao au kuni lazima wawe na eneo lililoidhinishwa na Halmashauri na walipe ada ya uvunaji; Halmashauri pia inapaswa kuhakiki ukomavu wa miti inayovunwa.
27.-(1) Mtu hataruhusiwa- (a) kukata miti katika eneo la Halmashauri kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali maalumu cha Halmashauri; au (b) kuvuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe maalumu ambao ni rasilimali ya Taifa. (2) Halmashauri itatakiwa kuhakiki iwapo miti inayovunwa katika eneo lake imekomaa na inafaa kwa ajili ya matumizi. (3) Mtu yeyote anayetaka kuvuna miti kwa ajili ya kuchoma mkaa, mbao au kuni atatakiwa kuwa na eneo maalumu lililoidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kazi hiyo na atatakiwa kulipa ada ya uvunaji miti kwa kiwango kilichoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. Wajibu wa kupanda miti - 28 Verify source ↗
Mkazi au mmiliki wa jengo la makazi au biashara
AI-assisted research summary: Mkazi au mmiliki wa jengo la makazi au biashara ndani ya eneo la Halmashauri lazima apande na atunze miti katika eneo lake kwa utaratibu uliowekwa katika Jedwali la Pili.
28. Mkazi au mmiliki wa jengo la makazi au biashara Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) ndani yae neo la Halmashauri atawajibika kupanda na kutunza miti katika eneo lake kwa utaratibu ulioainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. Bustani za Halmashauri - 29 Verify source ↗
Mtu hataruhusiwa kufanya biashara yoyote au
AI-assisted research summary: A person may not conduct any business or build a permanent structure in the Council’s park area.
29. Mtu hataruhusiwa kufanya biashara yoyote au kujenga jengo la kudumu katika eneo la bustani la Halmashauri. Ushirikishaji wa jamii katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira - 30 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kutoa kibali au kuingia
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kutoa kibali au kuingia mkataba na watu au taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha bustani, maeneo ya wazi, na usimamizi wa mazingira ndani ya Halmashauri ya Mtaa, Kata au Wilaya.
30. Mkurugenzi anaweza kutoa kibali au kuingia mkataba na mtu yeyote, taasisi, kikundi binafsi au asasi ya kiraia, ndani ya Halmashauri katika ngazi ya Mtaa, Kata au Wilaya katika kuboresha bustani, eneo la wazi, kusimamia uhifadhi na usimamizi wa mazingira. Tathmini ya athari kwa mazingira na jamii Uhifadhi wa mazingira ya mto au bwawa na udhibiti wa rasilimali zake - 31 Verify source ↗
(1) Miradi yote
AI-assisted research summary: Miradi ndani ya Halmashauri haiwezi kuendelezwa bila tathmini ya athari ya mazingira, na mpendekezaji wa mradi lazima alipe Halmashauri 10% ya gharama ya tathmini hiyo kama ada ya ukaguzi na usimamizi.
31.-(1) Miradi yote inayotekelezwa ndani ya Halmashauri haitaendelezwa bila kufanyiwa tathmini ya athari ya mazingira. (2) Kila mpendekezaji wa mradi atawajibika kulipa Halmashauri asilimia kumi ya gharama ya tathmini ya athari za mazingira kama ada ya ukaguzi na usimamizi wa mradi husika. - 32 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Mtu haruhusiwi kutumia baadhi ya njia za uvuvi, kuvua katika maeneo yaliyolindwa bila kibali maalumu, kuvua bila leseni, kutumia chombo kisicho na usajili na leseni, au kufanya biashara/picha ufukweni bila kibali cha Halmashauri.
32.-(1) Mtu hataruhusiwa- (a) kutumia uvuvi wa juva, baruti, sumu au mkuki; (b) kuvulia nyavu kwenye maji mafupi au kwenye miamba; (c) kuvua, kuokota, kuchukua au kufanya kitendo chochote kwenye maeneo tengefu ya samaki isipokuwa kwa kibali maalumu cha Halmashauri; (d) kuvua samaki bila kuwa na leseni ya uvuvi; (e) kutumia chombo cha uvuvi kisichokuwa na namba za usajili pamoja na leseni ya chombo hicho; au (f) kufanya biashara au kupiga picha kwenye ufukwe bila kibali cha Halmashauri. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. Makosa yanayotokana na uharibifu wa misitu - 33 Verify source ↗
Mtu ambaye
AI-assisted research summary: A person commits an offence if they carry out listed forest-related acts without a permit or in protected areas.
33. Mtu ambaye- (a) atachoma au kusababisha moto katika misitu bila kibali; (b) atashindwa kushiriki katika kuzima moto kwenye Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) msitu wa eneo lake; (c) atavuna mazao ya miti katika misitu iliyohifadhiwa bila kibali; (d) atachoma mkaa na kukata kuni katika eneo la msitu bila kibali; (e) atafyeka nyasi, kung’oa visiki kwenye misitu bila kibali; (f) atachunga mifugo lolote lililopandwa miti au misitu iliyohifadhiwa kama bustani ya mtu; kwenye eneo Udhibiti wa utupaji wa taka (g) atakata miti au kuchungia mifugo kwenye miti ailiyopandwa kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko wa udongo au kinga upepo; (h) atabandua magome ya miti kwa ajili ya kueneza vilindo, mzinga na vitu vingine bila ya kuwa na vibali; au (i) atalima au kukata miti katika vyanzo vya maji, milima, kando ya njia, makorongo na sehemu nyingine zozote zinazohifadhiwa ili kupunguza mmomonyoko wa udongo, anatenda kosa. - 34 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: The Council must set aside waste disposal areas, place waste containers in its areas, and provide waste collection for a fee. Residents, household owners, tenants, and business operators must use proper covered containers and dispose of waste in the designated containers. Throwing waste or litter in prohibited places is an offence.
34.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kutenga eneo maalumu kwa ajili ya kutupia taka; (b) kuweka vyombo maalumu vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. (2) Itakuwa ni wajibu kwa- (a) kila mmiliki wa nyumba au mpangaji au mfanyabiashara kuhakikisha kuwa ana chombo imara chenye mfuniko kwa ajili kuhifadhia taka ngumu kabla hazijachukuliwa kwa ajili ya kwenda kutupwa katika eneo lilotengwa kwa ajili ya kuhifadhi taka; na (b) kila mkazi au mtu yeyote kutunza na kuhifadhi vyombo vya kuhifadhia taka vinavyowekwa na Halmashauri. (3) Mtumiaji wa chombo cha usafiri binafsi au cha umma atapaswa kutupa taka kwenye chombo cha kuhifadhia taka kilichomo kwenye chombo cha usafiri husika na mtu taka nje ya chombo cha usafiri yeyote atakayetupa Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) anachotumia anatenda kosa. (4) Mkazi au mtu yeyote atawajibika kutupa taka katika vyombo maalumu vilivyowekwa kwa ajili ya kutunzia taka katika maeneo maalumu yaliyotengwa. (5) Mtu atakayetupa taka au uchafu wowote au kuacha takataka au uchafu katika maeneo ya makazi, biashara, uchochoro, kiwanja, mifereji ya maji ya mvua, barabara, hifadhi ya barabara au mahali popote ambapo hapajatengwa kwa ajili ya kutupa taka anatenda kosa. Ushiriki wa vikundi jamii katika usafi wa mazingira - 35 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na jukumu la kuhamasisha
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ihimize na itambue vikundi vya jamii ili viweze kusaidia udhibiti wa taka ngumu na usafi wa mazingira, baada ya kuingia mkataba na Halmashauri.
35. Halmashauri itakuwa na jukumu la kuhamasisha uundaji wa vikundi jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Ada ya uzoaji taka Wajibu wa kuwa na choo na kukitumia - 36 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ada ya uzoaji taka kila
AI-assisted research summary: Halmashauri hutoza ada ya kila mwezi ya uzoaji taka kwa kaya, biashara, taasisi na kampuni zilizo ndani ya eneo lake, na malipo hufanyika tarehe 30 ya kila mwezi kwa Afisa Mwidhiniwa.
36.-(1) Halmashauri itatoza ada ya uzoaji taka kila mwezi kutoka kwa kila kaya, wamilliki wa nyumba za biashara, taasisi na kampuni zilizopo ndani ya eneo la Halmashauri kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii. (2) Ada ya kila mwezi italipwa kila tarehe 30 ya kila mwezi ndani ya mwezi husika na italipwa kwa Afisa Mwidhiniwa stakabadhi ya malipo atatoa yatakayolipwa kwa njia ya kieletroniki na atajaza katika rejista ya wazalishaji taka. ambaye (3) Endapo mzalishaji wa taka atashindwa kulipia gharama ya huduma ya uzoaji taka kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo, Halmashauri itamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani. - 37 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba au mpangaji lazima ahakikishe nyumba ina choo safi na imara, sehemu ya kunawia mikono yenye maji safi na sabuni ya kimiminika, na choo kijengwe mita 60 kutoka chanzo cha maji.
37.-(1) Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji atahakikisha kwamba nyumba yake ina- (a) choo safi, imara kwa matumizi ya wakazi wa nyumba hiyo na kinatumika wakati wote; na (b) sehemu maalumu ya kunawia mikono ikiwa na maji safi na sabuni maalumu ya kimiminika. (2) Choo kinatakiwa kujengwa umbali wa mita sitini kutoka chanzo chochote cha maji. Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) Vyoo vya umma - 38 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kujenga choo cha
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kujenga choo cha umma au kuruhusu watu binafsi, vikundi au taasisi kujenga vyoo vya umma mahali itakapoona panafaa.
38.-(1) Halmashauri inaweza kujenga choo cha umma au kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo ambayo Halmashauri itaona inafaa. (2) Vyoo vitakavyojengwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii vitatakiwa- (a) kuwa vya kudumu; (b) kuwa na matundu yasiyopungua mawili kwa wanawake na mawili kwa wanaume; (c) kuwa na mfumo madhubuti wa maji na uwepo wa maji ya kutosha yaliyo safi na salama; (d) kuwa na chombo cha kuhifadhia maji ya akiba; (e) kuwa na bafu ya wanaume na wanawake; (f) kuwa na chumba maalumu cha kuvutia sigara; (g) kuwa na sehemu ya haja ndogo kwa wanaume; na (h) kuwa na chombo maalumu chenye mfuniko cha kuhifadhia taka zisizoweza kusukumwa na maji. Vyoo vya muda katika mikusanyiko Vyoo katika majengo ya biashara Notisi ya kujenga au kurekebisha choo - 39 Verify source ↗
Mtu, kikundi au taasisi yoyote yenye lengo la
AI-assisted research summary: Watu, vikundi au taasisi zinazoandaa mkutano, sherehe au mkusanyiko lazima ziweke au zijenge vyoo vya muda ikiwa eneo halina choo cha kudumu, na ziwe na idhini ya Halmashauri.
39. Mtu, kikundi au taasisi yoyote yenye lengo la kukusanya watu kwa madhumuni ya mkutano au sherehe au mkusanyiko wowote itapaswa, endapo eneo hilo hakuna choo cha kudumu, kuweka au kujenga vyoo vya muda kwa idhini ya Halmashauri. - 40 Verify source ↗
Kila mmiliki wa jengo la biashara atatakiwa
AI-assisted research summary: Mmiliki wa jengo la biashara lazima ajenge vyoo kwa ajili ya wateja, kwa kuzingatia jinsia zote na viwango vinavyokubalika chini ya Sheria Ndogo hii.
40. Kila mmiliki wa jengo la biashara atatakiwa kujenga vyoo kwa kuzingatia jinsia zote vyenye viwango vinavyokubalika chini ya Sheria Ndogo hii kwa ajili ya matumizi ya wateja wake. - 41 Verify source ↗
(1) Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika
AI-assisted research summary: If a health inspection finds a house has no toilet, an overflowing toilet, or a toilet unfit for human use, the authorized officer must notify the owner or tenant with conditions for building or fixing it. The council may also order the house or building not be used for living or business until the problem is fixed.
41.-(1) Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika kuwa nyumba yoyote haina choo au choo kilichopo kimejaa au hakifai kwa matumizi ya binadamu, Afisa Mwidhiniwa atatoa notisi kwa mmiliki wa nyumba au mpangaji akiainisha masharti ya kujenga au kurekebisha choo husika. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Halmashauri inaweza kuamuru nyumba au jengo husika lisitumike kwa shughuli za makazi au biashara hadi hapo hali hiyo itakapokuwa imerekebishwa. Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) Notisi ya kuondoa kero - 42 Verify source ↗
(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa akiona kero katika eneo alilokagua, lazima atoé notisi ya siku 7 kwa mhusika kuiondoa; kutotekeleza notisi hiyo ndani ya muda huo ni kosa.
42.-(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote atatoa notisi ya siku saba kwa mmiliki wa nyumba, mpangaji, mtumiaji au mtu yeyote anayehusika akimtaka kuondoa kero hiyo. (2) Mtu yeyote atakayeshindwa kutekeleza masharti ya notisi aliyopewa chini ya kifungu kidogo cha (1) ndani ya muda ulioainishwa kwenye notisi anatenda kosa. Eneo maalumu la uvutaji sigara - 43 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa kuvuta sigara kwenye eneo
AI-assisted research summary: People must not smoke in open areas or at gatherings. Building owners for certain business and public/private premises must set aside a special smoking area and provide a container for ash and cigarette filters.
43.-(1) Mtu hataruhusiwa kuvuta sigara kwenye eneo la wazi au kwenye mikusanyiko ya watu. (2) Kila mmiliki wa jengo la biashara za baa, hoteli, mgahawa, kumbi za starehe, viwanja vya michezo na burudani, ofisi za umma na binafsi anatakiwa kutenga eneo maalumu la kuvutia sigara na kuweka chombo cha kuhifadhia majivu na vichungi vya sigara. - 44 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kuteua wakala wa
AI-assisted research summary: Halmashauri may appoint an agent to collect fees on its behalf, and the appointed agent must follow the contract terms and collect approved electronic fees in the assigned area.
44.-(1) Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ada kwa niaba yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Wakala atakayeteuliwa chini ya Sheria Ndogo hii atakuwa na wajibu wa kuzingatia masharti ya mkataba ikijumuisha kukusanya kwa alioingia na Halmashauri kutumia mfumo wa kielekitroniki ada mbalimbali zinazohusiana na afya, usafi na usimamizi wa mazingira kwa niaba ya Halmashauri katika eneo lake alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa chini ya Sheria Ndogo hii. - 45 Verify source ↗
Mtu atakayekiuka masharti yaliyowekwa na
AI-assisted research summary: A person who breaches the conditions set by this bylaw commits an offence and, if convicted, may be fined up to 300,000 shillings or imprisoned for up to 12 months, or both.
45. Mtu atakayekiuka masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na endapo atapatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili jela au vyote kwa pamoja. - 46 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kutoza mtu aliyekiri kosa na yuko tayari kujaza fomu maalum ya Jedwali la Nne.
46. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Nne la Sheria Ndogo hii. Uteuzi wa wakala Makosa Kufifilisha kosa Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) ________ JEDWALI LA KWANZA ________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 27(3)) ADA YA UVUNAJI MITI Na.
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaonyesha viwango vya ada/ushuru kwa huduma mbalimbali, mahitaji ya chini ya kupanda miti, na fomu ya kukiri kosa kwa kukiuka masharti ya sheria ndogo.
3. Aina ya Huduma Kiasi cha ada (Shilingi) Mkaa Mbao Kuni 1,000/= kwa gunia 5,000/= kwa kila ujazo wa mita (1M3) 3,000/= kwa kila ujazo wa mita moja (1M3) Ujazo wa juu Ujazo wa kati Ujazo wa chini ________ JEDWALI LA PILI _______ (Limetengenezwa chini ya aya ya 28) KUPANDA MITI Miti isiyopungua 2 Miti isiyopungua 4 Miti isiyopungua 5 ________ JEDWALI LA TATU _______ (Limetengenezwa chini ya aya ya 36(1)) ADA ZA HUDUMA ZA USAFI Na. Taasisi Kiwango cha Ada na Ushuru kwa Mwaka Kiwango cha Ushuru kwa mwezi 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 Taasisi zote na mashirika Hospitali ya rufaa Viwanda vikubwa Viwanda vya kuoka mikate (bakery) Hoteli za kitalii Migahawa Useremala Wauza mbao Mashine ndogo za kusaga na kukoboa Duka la jumla Duka la rejareja Ghala (godown) Viwanda vidogo vya kukamua mafuta 360,000/= 600,000/= 720,000/= 360,000/= 360,000/= 60,000/= 50,000/= 30,000/= 50,000/= 50,000/= 36,000/= 360,000/= 50,000/= 30,000/= 50,000/= 60,000/= 30,000/= 30,000/= 5,000/= 4,200/= 5,000/= 3,000/= 5,000/= 3,000/= 30,000/= 5,000/= Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 Bucha za samaki au nyama Machinjio Baa Mini-sepermarket Vilabu vya pombe za kienyeji Nyumba ya kuishi Saluni za wanaume na wanawake Grocery (mini-bar) Nyumba za kulala wageni Vituo vya afya na zahanati Vituo vya mafuta Maduka ya vifaa vya ujenzi Maduka ya nguo na viatu Maduka ya dawa (pharmacy) Maduka ya dawa muhimu Maduka ya mikate na vitafunwa Maduka ya vyombo Maduka ya kuuza magodoro na samani Maduka ya kuuza spea za magari, pikipiki na baiskeli Maduka ya kuuza shajaa na kurudufisha (photocopy) Maduka ya kuuza vipodozi Maduka ya kuuza simu au saa Mama na baba lishe 36,000/= 360,000/= 60,000/= 50,000/= 36,000/= 24,000/= 36,000/= 36,000/= 60,000/= 60,000/= 50,000/= 60,000/= 36,000/= 60,000/= 36,000/= 30,000/= 30,000/= 30,000/= 60,000/= 60,000/= 36,000/= 36,000/= 30,000/= 3,000 30,000/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 2,000/= 3,000/= 3,000/= 5,000/= 5,000/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 5,000/= 3,000/= 2,500/= 2,500/= 2,500/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 3,000/= 2,500/= Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) ________ JEDWALI LA NNE _______ (Limetengenezwa chini ya aya ya 46) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi…………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ………………………… ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwamba mnamo tarehe…………… ya mwezi …………….. Mwaka ………………………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ……………………… ya Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ya Mwaka 2023. Hivyo, kwa kuzingatia masharti ya sheria husika, nipo tayari kulipa kiasi cha ada au ushuru ninayodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe ....… ya mwezi …………… mwaka ...............……. Jina …………………………………..….. Saini …………………………………..…. Mbele ya: Jina ……………………………………….. Cheo ……………………………………… Saini ……..……………………………….. Tarehe …………………………………. Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tangazo la Serikali Na.30 (Linaendelea.) Nembo na Chapa ya Halmashauri yaManispaa ya Iringa imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa na Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ulioitishwa na kufanyika tarehe 28 Januari, 2022 na ulibandikwa mbele ya:- KASTORI G. MSIGALA, Mkurugenzi, Halmashauri ya Manispaa Iringa IBRAHIM A. NGWADA, Meya Halmashauri ya Manispaa Iringa L.S NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (Mb.), 30 Novemba, 2023 Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI,
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi Wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ya Mwaka, 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in