Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2024
This by-law is titled the Korogwe District Council Service Levy By-Law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This by-law is titled the Korogwe District Council Service Levy By-Law, 2024. This provision says the bylaw applies throughout the entire area of Korogwe District Council. This section defines key terms used in the by-law, including the Council, Director, authorised officer, service levy payer, agent, and related accounting terms. Halmashauri lazima itoze na kukusanya ushuru wa huduma kwa 0.3% ya mauzo baada ya VAT na ushuru wa Bidhaa kwa kampuni, tawi la kampuni, au mfanyabiashara mwenye leseni anayewasilisha hesabu za mauzo kwa TRA. Service taxpayers must file accurate sales and final returns, keep records, and pay service tax within the stated deadlines.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2024
Showing 15 of 15
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This by-law is titled the Korogwe District Council Service Levy By-Law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This provision says the bylaw applies throughout the entire area of Korogwe District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe. - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the Council, Director, authorised officer, service levy payer, agent, and related accounting terms.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe; “hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho zinazowasilishwa na taasisi yoyote ya kibiashara baada ya kipindi cha hesabu pamoja na nyaraka au maelezo yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “kampuni” maana yake ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 80 (Linaendelea) “kipindi maalum cha hesabu” maana yake ni muda ambao mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara kwa Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe au afisa yeyote za Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; aliyeteuliwa kutekeleza kazi Sura ya 212 Sura ya 212 Ushuru wa huduma “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara mwenye leseni anayefanya shughuli zake katika eneo la Halmashauri; “tawi la kampuni” maana yake ni tawi la kampuni iliyesajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri au wakala kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara mwenye leseni ya biashara ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne kutokana na huduma anazopata na kutumia miundombinu ya umma inayomuwezesha kufanya biashara katika eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au shirika ambalo limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogohii kwa niaba ya Halmashauri husika. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itoze na kukusanya ushuru wa huduma kwa 0.3% ya mauzo baada ya VAT na ushuru wa Bidhaa kwa kampuni, tawi la kampuni, au mfanyabiashara mwenye leseni anayewasilisha hesabu za mauzo kwa TRA.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu (0.3%) ya mauzo baada ya kutoa kodi ya ongezeko la thamani na ushuru wa Bidhaa kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 80 (Linaendelea) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza kutoka kwa wafanyabiashara wenye leseni za biashara ambao hawawasilishi hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. Wajibu wa mlipa ushuru - 5 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na
AI-assisted research summary: Service taxpayers must file accurate sales and final returns, keep records, and pay service tax within the stated deadlines.
5.-(1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu wa- (a) kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila mwezi endapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania; (c) kuwasilisha hesabu sahihi na za kweli kwa Halmashauri; (d) kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa kwa Halmashauri katika muda uliowekwa; (e) kutunza kumbukumbu, vitabu au hesabu; na (f) kuonyesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi. (2) Kila mlipa ushuru wa huduma atatakiwa kulipa ushuru wa huduma si zaidi ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kuwasilisha taarifa za mauzo ya kila mwezi. (3) Bila kuathiri aya ndogo ya (2), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru huo. (4) Kila mlipa ushuru atatakiwa kuwasilisha kwa Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa kipindi cha hesabu. (5) Iwapo mlipa ushuru hajawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha husika na ametakiwa kufanya hivyo kwa notisi ya siku thelathini, Mkurugenzi inafaa, kuamua anaweza kwa kadri atakavyoona 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 80 (Linaendelea) kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (6) Ushuru uliothaminiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, utalipwa katika kipindi cha siku thelathini tangu tarehe ya kufanya tathmini. (7) ushuru Iwapo mlipa hajawasilisha majumuisho ya hesabu zake kwa mwaka wowote wa mapato, na endapo Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa anafikiri kwamba mlipa ushuru huyo ana wajibu wa kulipa ushuru kwa mwaka huo, anaweza kwa kadri atakavyoona, kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo, isipokuwa tathmini hiyo haitaathiri wajibu wowote wa mlipa ushuru anayostahili kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kwa kushindwa kwake kuwasilisha hesabu hizo. Mamlaka ya Mkurugenzi - 6 Verify source ↗
(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuwataka walipa ushuru wa huduma na watu wengine kuwasilisha taarifa, kumbukumbu, au hesabu; pia anaweza kuagiza ukaguzi na kuteua afisa au kamishna kwa ajili ya tathmini na ukusanyaji wa ushuru.
6.-(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa kuwasilisha taarifa ya mauzo chini ya sheria Ndogohii atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo kwa wakati, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka Mlipa Ushuru wa Huduma kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku thelathini kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi. (2) Mkurugenzi kumtaka kwa anaweza taarifa kuhusu maandishi mtu yeyote mwenye mfanyabiashara anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi. (3) Mkurugenzi anaweza kumwagiza kwa maandishi Afisa Mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la taasisi ya kibiashara au la mlipa au mkusanya ushuru yeyote kwa nia ya kufanya uchunguzi na tathmini ya kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa kwa ajili ya kupata na kujua kiwango sahihi cha ushuru anachotakiwa kulipa mlipa ushuru. (4) Mkurugenzi anaweza kumteua Kamishna wa 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 80 (Linaendelea) kodi ya forodha au kodi ya mapato kwa ajili ya kutathmini na kukusanya ushuru wa huduma na kuwasilisha kwa Halmashauri kwa lengo la kupata ushuru wa huduma pamoja na madeni yake. (5) Mkurugenzi kwa taarifa ya maandishi, anaweza kumtaka mlipa ushuru au mkusanya ushuru yeyote kuwasilisha hesabu zenye taarifa kamili za shughuli za kibiashara zikionyesha thamani ya kiasi na thamani ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, kutolewa kusambazwa au kuuzwa kibiashara na taarifa ya fedha katika kipindi maalum kisichozidi siku thelathini tangu tarehe ya taarifa hiyo. (6) Mkurugenzi anaweza, kwa taarifa ya maandishi ya siku saba kumtaka mlipa ushuru kuwasilisha kumbukumbu za kibiashara na vitabu vya hesabu kwa nia ya kupata taarifa kwa ajili ya kufanyiwa tathmini au kukusanya ushuru wa huduma. Ukokotoaji wa ushuru - 7 Verify source ↗
Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikokotoe ushuru wa huduma kwa walipa ushuru wa huduma wanaowasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
7. Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma kwa walipa ushuru wa huduma wanaowasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuzingatia taarifa zinazowasilishwa na walipa ushuru wa huduma katika kipindi maalum cha hesabu. Uteuzi wa wakala Mamlaka ya Afisa Mwidhiniwa - 8 Verify source ↗
Bila ya kuathiri masharti mengine ya Sheria
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru, na wakala huyo lazima awasilishe majumuisho kwa Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa na kuwasilisha ushuru aliokusanya katika kipindi maalum.
8. Bila ya kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo hii, Mkurugenzi anaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri na wakala huyo atakuwa na jukumu la- kuwasilisha majumuisho kwa Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa; na kuwasilisha ushuru aliokusanya katika kipindi maalum. - 9 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa anaweza
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kupokea, kukubali, kukataa, na kufanya tathmini ya hesabu za mlipa ushuru au mkusanya ushuru katika hali zilizoelezwa.
9. Afisa Mwidhiniwa anaweza- (a) kupokea na kukubali hesabu za mlipa ushuru kuzifanyia ushuru na au mkusanya kutathmini; 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 80 (Linaendelea) Makosa na adhabu (b) kufanya tathmini kuhusu kiwango cha hesabu cha mlipa ushuru au mkusanya ushuru endapo hesabu hizo zitakuwa si sahihi; au (c) kukataa hesabu za mwisho na kufanya tathmini kuhusu hesabu hizo iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hesabu hizo siyo sahihi. - 10 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayefanya mojawapo ya vitendo vilivyoorodheshwa hapa anatenda kosa, na akitiwa hatiani anaweza kutozwa faini, kifungo, au vyote viwili.
10. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atashindwa kuwasilisha kwa Halmashauri taarifa sahihi za mauzo katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) atawasilisha kwa Halmashauri taarifa zisizo sahihi; (c) atashindwa kulipa ushuru wa huduma katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (d) atamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru wa Huduma; (e) atamzuia au atajaribu kumzuia Afisa Mwidhiniwa kutekeleza au Wakala majukumu yake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (f) atafanya hesabu za uongo kwa kupunguza au sahihi kwa zisizokuwa kutoa hesabu Halmashauri; (g) atatoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu jambo lolote linaloweza kuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa ushuru; (h) ataandaa au atatengeneza au atasababisha kuandaliwa au kutengenezwa kwa vitabu vya uongo vya mahesabu au kumbukumbu; (i) atashindwa kulipa ushuru wa huduma ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; na 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 80 (Linaendelea) (j) atashindwa kutunza kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya ukaguzi. (2) Mtu yeyote atakayetenda kosa chini yaaya ndogo ya (1) na kutiwa hatiani atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. - 11 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: The Director may compound an offence by charging TZS 200,000 if the offender admits the offence, completes the prescribed form in the Second Schedule, and pays any fee or duty owed.
11. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. Kufifilisha Kosa Kufutwa kwa Sheria Ndogo TS. Na. 75 la 2011 - 12 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Huduma) ya
AI-assisted research summary: The by-law on service levy for Korogwe District Council from 2011 is repealed.
12. Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Huduma) ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2011 imefutwa. ___________ JEDWALI LA KWANZA ____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 4(2)) Na
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: For salons, the annual amount is set between Sh 50,000 and Sh 108,000.
1. Aina ya Biashara Saluni Kiwango Kiasi kisichopungua Shilingi 50,000/= na kisichozidi 108,000/= Muda Mwaka - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: The text lists fee amounts for garages/workshops and several shop or service categories, with amounts ranging from Shilingi 50,000 to 108,000.
6. Gereji na karakana Kiasi kisichopungua Shilingi 50,000/= na kisichozidi Mwaka Duka la jumla Duka la rejareja Bucha Baa 108,000/= Kiasi kisichopungua Shilingi 50,000/= na kisichozidi 108,000/= Kiasi kisichopungua Shilingi 50,000/= na kisichozidi 108,000/= Kiasi kisichopungua Shilingi 50,000/= na kisichozidi 108,000/= Kiasi kisichopungua Shilingi 50,000/= na kisichozidi Mwaka Mwaka Mwaka Mwaka 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 80 (Linaendelea) - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: The text shows annual levy amounts for grocery and other services, and a form for admitting an offence and agreeing to pay the owed fee or levy plus a fine instead of being prosecuted.
8. Grocery Biashara na huduma nyingine 108,000/= Kiasi kisichopungua Shilingi 50,000/= na kisichozidi 108,000/= Kiasi kisichopungua Shilingi 50,000/= na kisichozidi 108,000/= Mwaka Mwaka ___________ JEDWALI LA PILI ____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 11) FOMU YA KUFILILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini…………………..............…… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………….…… Saini………………………….…………………………...…… Wadhifa: ……………………………………………………… Tarehe………………………………………………………… 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Tangazo La Serikali Na. 80 (Linaendelea) Lakari ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe imegongwa kwenye Sheria ndogo hii kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe uliofanyika tarehe 5/11/2021 na kushuhudiwa Lakari hiyo ikigongwa mbele ya:- GOODLUCK A. MWANGOMANGO Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe KALLAGHE S. YUSUPH Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe NAKUBALI L.S Dodoma 31 Oktoba, 2023 MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ya mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in