Sheria Ndogo ya (Usafi Wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu ya Mwaka, 2024
This section gives the short title of the bylaw: Magu District Council Environmental Sanitation By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya (Usafi Wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu ya Mwaka, 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the bylaw: Magu District Council Environmental Sanitation By-law, 2024. This by-law applies throughout the entire area of Magu District Council. This section defines key terms used in the bylaw, including fees, officers, residents, waste, and sanitation facilities. Mwenye au mkazi wa eneo la nyumba, kiwanja au biashara lazima alisafishe eneo lake, ashughulikie taka kama inavyoelekezwa na Halmashauri, ajenge vyoo na mashimo ya taka yanayokidhi sifa zilizotajwa, na ahakikishe maji ya kunywa ni safi na salama. Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara lazima wawe na karo la kuhifadhia maji taka, walitoe maji taka yanapojaa, na wasimwage au kuyaelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya (Usafi Wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu ya Mwaka, 2024
Showing 34 of 34
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the bylaw: Magu District Council Environmental Sanitation By-law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Magu District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the bylaw, including fees, officers, residents, waste, and sanitation facilities.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya huduma ya kuzoa taka au kupima afya; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa dawa; inayosafishika, banda “choo bora” maana yake ni choo chochote cha maji chenye sakafu la kudumu, limeezekwa, lina mlango imara, bomba la kutolea hewa chafu na lenye mfuniko kwenye tundu la choo na shimo salama na safi kwa ajili ya kutupa kinyesi na mkojo wa binadamu, lililojengwa kwa vifaa vya imara 1 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) kudumu; “chukizo” au kero” maana yake ni kitu chochote kilicho katika hali yoyote ambacho kinatumika, kimewekwa, kimejengwa au ni kichafu kiasi cha kusababisha: (a) hatari kwa viumbe na maisha ya binadamu; (b) harufu mbaya au harufu ya kuudhi au kuleta kinyaa; (c) kuzaliana kwa wadudu hatari kama vile inzi, mende, sisimizi, panya, nyoka, nyuki, kunguni au viumbe wengine hatari; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Magu; “jengo la biashara” maana yake jengo lolote lililojengwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kufanya biashara iliyokusudiwa; “kaya” maana yake mtu mzima anayejitegemea mwanamke au mwanaume, na mtoto au watoto wanaoishi aidha kwenye nyumba nzima au ndani ya chumba kimoja kwenye eneo la Halmashauri; “kizimba cha taka” maana yake ni eneo maalum lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuhifadhi taka ngumu; “mabwawa ya maji taka” maana yake ni mabwawa yaliyojengwa kwa madhumuni ya kuhifadhi na kutakasa maji taka yanayotokana na kuosha vyombo, kutoka vyooni, kutoka bafuni, kufua nguo, kuosha nywele au shughuli zozote za nyumbani na viwanda; Sura ya 191 Sura ya 191 “maji taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo lililoko chini ya mamlaka ya Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu au afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; 2 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) “taka ngumu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira. Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira - 4 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayeishi au
AI-assisted research summary: Mwenye au mkazi wa eneo la nyumba, kiwanja au biashara lazima alisafishe eneo lake, ashughulikie taka kama inavyoelekezwa na Halmashauri, ajenge vyoo na mashimo ya taka yanayokidhi sifa zilizotajwa, na ahakikishe maji ya kunywa ni safi na salama.
4. Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayeishi au anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara kuhakikisha kwamba- (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; zote (b) taka kuondolewa kwa njia Halmashauri; zinakusanywa na kufukiwa au itakayoelekezwa na (c) anachimba shimo la kutupa taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi tatu na upana usiopungua futi mbili; (d) anajenga choo imara cha kudumu kwa matofali na kuezeka kwa bati, tembe, majani au vigae chenye mlango unaofunga na kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na kuna chombo cha maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi; na (f) maji yote yanayotumika kwa kunywa ni safi na salama bila kujali yametoka kwenye chanzo gani cha maji. Uhifadhi wa maji taka - 5 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara lazima wawe na karo la kuhifadhia maji taka, walitoe maji taka yanapojaa, na wasimwage au kuyaelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
5. Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara anatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa ana karo la kuhifadhia maji taka; (b) kunyonya maji taka kila wakati karo linapojaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote ambayo haijatengwa kwa ajili ya kuhifadhia maji taka. 3 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) Utengenez aji na uuzaji wa vyakula Upimaji wa afya Uwezo wa Afisa Mwidhini wa Vifaa vya kuhifadhia taka ngumu - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika,
AI-assisted research summary: Watu wanaotengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula katika eneo la Halmashauri lazima wazingatie masharti na kanuni za afya.
6. Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa kutimiza masharti na kanuni za afya. - 7 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli,
AI-assisted research summary: Hotel, restaurant, bar, guesthouse, butcher, baker, and cooked-food sellers must have their health checked every six months.
7. Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba ya kulala wageni, bucha, muoka mikate au mtu anayeshughulika na kuuza vyakula vilivyopikwa kuhakikisha kwamba anapima afya yake kila baada ya miezi sita. - 8 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa ana uwezo wa kuingia maeneo ya Halmashauri wakati wa saa zilizoainishwa, kutoa ushauri au maelekezo dhidi ya kuishi katika jengo hatarishi, kuzuia shughuli wakati wa mlipuko wa magonjwa, na kufunga au kuagiza kufungwa kwa biashara au majengo yanayokiuka au kutokaguliwa.
8.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika eneo lolote ndani ya Halmashauri kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa tisa na nusu alasiri kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kushauri au kuelekeza watu au mtu kutokuishi katika jengo ambalo linahatarisha afya au maisha ya watu na viumbe hai. (3) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuzuia shughuli mbalimbali wakati wa mlipuko wa magonjwa ikiwa ni pamoja na kukamata vyombo au vifaa vingine vinavyotumika na ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa wakazi wa Halmashari. (4) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kufunga au kuagiza kufungwa kwa biashara yoyote au jengo ambalo halijakaguliwa au limekiuka kanuni na masharti ya afya. lililokaguliwa na kukutwa - 9 Verify source ↗
(1) Kila mmliki wa jengo la makazi, mpangaji wa
AI-assisted research summary: Certain residential property owners, tenants, and anyone doing business in the council area must have a covered waste container and use the designated waste collection points; owners or tenants in green-belt, unmeasured areas must also have a large pit for solid waste on their property.
9.-(1) Kila mmliki wa jengo la makazi, mpangaji wa jengo la makazi au mtu yeyote anayefanya biashara katika eneo lolote ndani ya Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo taka chenye mfuniko na atawajibika cha kuhifadhia kukusanya taka hizo kwenye vizimba vya kuzolea taka katika maeneo yaliyoainishwa. (2) Kila mmiliki wa jengo au mpangaji wa nyumba iliyo katika ukanda wa kijani, katika maeneo ambayo hayajapimwa atalazimika kuwa na shimo kubwa la kukusanya taka ngumu katika eneo lake. 4 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) Ada ya uzoaji taka Ukusanyaj i wa taka ngumu Eneo la kutupa taka Kibali cha kusafirisha taka za plastiki - 10 Verify source ↗
Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikusanye taka ngumu kutoka kwenye vizimba vilivyoainishwa katika kila kata, na wazalishaji taka watalipa ada au ushuru wa ukusanyaji kulingana na viwango vya Jedwali la Kwanza.
10. Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu kutoka katika vizimba vya taka vilivyoainishwa katika kila kata, na wazalishaji taka watalipia ada au ushuru wa ukusanyaji wa taka kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. - 11 Verify source ↗
(1) Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya
AI-assisted research summary: Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye pipa la taka ngumu, chombo chochote cha taka ngumu, au kitu chochote kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara.
11.-(1) Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye pipa au chombo chochote cha taka ngumu au kitu chochote kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara. (2) Taka ngumu zote zitakazokusanywa kwenye pipa au chombo cha taka zitabaki kuwa mali ya mkazi au mmliki wa eneo lile mpaka zitakapokuwa zimefikishwa kwenye kizimba cha taka au zitakapokuwa zimetolewa na Wakala kutoka katika eneo lake. - 12 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupa taka, iweke vyombo maalumu vya kuhifadhi taka, na itoe huduma ya kuzoa takataka kwa malipo hadi dampo.
12. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupa taka; (b) kuweka vyombo maalumu vya kutunza taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji takataka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. - 13 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoa kibali cha kusafirisha taka
AI-assisted research summary: Halmashauri must issue permits for transporting plastic waste for recycling, and certain vehicles and collectors must register or obtain permits and pay an annual fee of TZS 20,000.
13.-(1) Halmashauri itatoa kibali cha kusafirisha taka za plastiki zinazosafirishwa kwa ajili ya urejelezaji . (2) Magari binafsi yatakayokuwa yanasafirisha taka za palstiki kutoka maeneo ya uzalishaji yatapaswa kusajiliwa na kupewa kibali kwa kulipa ada ya shilingi elfu ishirini tu kwa mwaka. (4) Mtu yeyote atakayekusanya taka za plastiki kutoka kwa wanaozichambua katika eneo la uzalishaji au vituo vya kukusanyia atatakiwa kupata kibali na kulipa ada ya shilingi elfu ishirini kwa mwaka. (5) Kibali cha kusafirisha taka za plastiki kitakuwa kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu. 5 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) Wajibu wa mmiliki wa duka la kuuza nyama Siku ya usafi - 14 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa duka la
AI-assisted research summary: Mmiliki wa duka la kuuza nyama lazima ahakikishe duka lina jengo la kudumu lenye sakafu na kuta zilizosakafiwa kwa marumaru nyeupe, lina maji safi na vifaa vya kukatia nyama, lina pipa la taka, na mhudumu ana mavazi maalum na hupima afya kila baada ya miezi sita.
14. Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa duka la kuuza nyama kuhakikisha kwamba- (a) ana jengo la kudumu lililosakafiwa na kuwekwa marumaru nyeupe kwenye sakafu na kuta kwa urefu wa futi sita kutoka usawa wa sakafu; (b) jengo lina maji safi, gogo na misumeno ya kukatia nyama; (c) kuna pipa la kuhifadhia taka; (d) mhudumu ana koti jeupe pamoja na viatu vyeupe aina ya buti; na (e) mhudumu anapima afya kila baada ya miezi sita. - 15 Verify source ↗
(1) Kila jumamosi ya wiki ya pili na jumamosi ya
AI-assisted research summary: Residents in villages and hamlets must join environmental cleanup on the day set by the council, and every person must keep specified nearby areas clean.
15.-(1) Kila jumamosi ya wiki ya pili na jumamosi ya wiki ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku maalamu ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yote ya Halmashauri. (2) Itakuwa ni wajibu kwa kila mkazi katika kijiji na kitongoji kushiriki katika usafi wa mazingira kwa siku iliyopangwa na Halmashauri katika maeneo yao na maeneo ya umma. (3) Kila mtu atahakikisha kuwa eneo lake la makazi, eneo linalomzunguka, eneo analofanyia biashara, eneo la wazi lililokaribu naye kwa umbali wa mita kumi na eneo la mazingira ya ofisi ni safi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Vikundi vya usafi - 16 Verify source ↗
Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi
AI-assisted research summary: The Halmashauri must encourage and recognize community groups so they can help with solid-waste control and environmental cleanliness in villages and hamlets, after contracting with the Halmashauri.
16. Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika vijiji na vitongoji baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Udhibiti wa ubebaji kokoto, mawe na mchanga - 17 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayesafirisha mawe, mchanga au
AI-assisted research summary: Anyone transporting stones, sand, or gravel in the council area must cover the transport container to prevent spilling and environmental pollution.
17. Mtu yeyote atakayesafirisha mawe, mchanga au kokoto katika eneo la Halmashauri atahakikisha kuwa chombo anachotumia kusafirisha kimefunikwa ili kuzuia kumwagika na kuchafua mazingira. Mabaki ya ujenzi - 18 Verify source ↗
Mtu
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kubomoa au kusababisha kubomoka kwa jengo au sehemu ya jengo bila kutoa taarifa ya maandishi kwa Halmashauri siku saba kabla.
18. Mtu yeyote hataruhusiwa kubomoa au 6 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) kusababisha kubomoka kwa jengo au sehemu ya jengo bila kutoa taarifa ya maandishi kwa Halmashauri siku saba kabla ya kubomoa jengo. Udhibiti utupaji wa taka - 19 Verify source ↗
(1) Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi au
AI-assisted research summary: Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi au vya umma hawaruhusiwi kutupa taka nje ya vyombo wanavyotumia au ovyo katika maeneo yaliyotajwa; mtu yeyote au mkazi anatakiwa kuhakikisha taka zinatupwa kwenye vyombo maalumu katika maeneo yaliyotengwa.
19.-(1) Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi au vya umma hawataruhusiwa- (a) kutupa taka nje ya vyombo wanavyotumia na taka zote zitawekwa kwenye chombo cha kuhifadhia taka kilichomo kwenye chombo husika; au (b) kutupa taka ovyo katika maeneo ya makazi, biashara, mifereji ya maji ya mvua, hifadhi ya barabara au mahali popote pasipotengwa kwa ajili ya kutupa taka. (2) Mtu yeyote au mkazi atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba anatupa uchafu au taka katika vyombo maalumu vilivyowekwa kwa ajili ya kutunzia taka katika maeneo maalumu yaliyotengwa. - 19 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba
AI-assisted research summary: House owners must keep a sewage storage pit and empty sewage when it fills up. Anyone is prohibited from opening or discharging sewage or faeces into storm drains, ravines, flowing water, or other unauthorized places, especially during rain.
19.-(1) Kila mmiliki wa nyumba anatakiwa kuhakikisha kuwa ana karo la kuhifadhi maji taka na atawajibika kunyonya maji taka pale karo linapojaa. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kufungulia na kutiririsha maji taka au kinyesi kutoka chooni au sehemu yoyote wakati wa mvua au wakati wowote kwenye mifereji ya maji ya mvua, mabonde au maji yanayotembea au sehemu nyingine yoyote isiyoruhusiwa. - 20 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji atakuwa na
AI-assisted research summary: Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji lazima ahakikishe nyumba ina choo, eneo la kunawia mikono lenye maji safi na sabuni ya kimiminika, na choo kijengwe mita 60 kutoka chanzo cha maji.
20. Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba- (a) nyumba yake ina choo boira kwa ajili ya matumizi ya wakazi wa nyumba hiyo; (b) anaweka sehemu maalumu ya kunawia mikono ikiwa na maji safi na sabuni ya kimiminika; na (c) choo kinatakiwa kijengwe umbali wa mita sitini kutoka chanzo chochote cha maji. Uhifadhi wamaji taka Wajibu wa kuwa na choo na kukitumia Vyoo vya - 21 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kujenga choo cha umma
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kujenga choo cha umma au kuwaruhusu watu au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo inayoona yanafaa.
21.-(1) Halmashauri inaweza kujenga choo cha umma 7 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) umma au kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo ambayo Halmashauri itaona inafaa. (2) Vyoo vitakavyojengwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii vitatakiwa kuwa vya kudumu na- (a) matundu yasiyopungua mawili kwa wanawake na mawili kwa wanaume; (b) mfumo madhubuti wa maji na uwepo wa maji ya kutosha yaliyo safi na salama; (c) kuwepo na chombo cha kuhifadhia maji ya akiba; (d) kuwepo kwa bafu ya wanaume na wanawake; (e) kuwepo na sehemu ya haja ndogo kwa wanaume; na (f) kuwepo na chombo maalumu chenye mfuniko cha kuhifadhia taka zisizoweza kusukumwa na maji. Vyoo vya muda katika mikusanyi ko - 22 Verify source ↗
Ni wajibu wa mtu yeyote, kikundi au taasisi yenye
AI-assisted research summary: Mtu, kikundi, au taasisi inayokusanya watu kwa mkutano, sherehe, au mkusanyiko lazima iweke au ijenge vyoo vya muda ikiwa eneo halina choo cha kudumu, na lazima iombe idhini kutoka Halmashauri.
22. Ni wajibu wa mtu yeyote, kikundi au taasisi yenye lengo la kukusanya watu kwa madhumuni ya mkutano au sherehe au mkusanyiko wowote kuweka au kujenga vyoo vya muda endapo eneo hilo hakuna choo cha kudumu na atatakiwa kuomba idhini kutoka Halmashauri. Vyoo katika majengo ya biashara - 23 Verify source ↗
Kila mmiliki wa jengo la biashara atatakiwa
AI-assisted research summary: Mmiliki wa jengo la biashara lazima ajenge vyoo bora vinavyokubalika kwa matumizi ya wateja wake, kwa kuzingatia jinsia zote.
23. Kila mmiliki wa jengo la biashara atatakiwa kujenga vyoo bora vyenye viwango vinavyokubalika chini ya Sheria Ndogo hii kwa ajili ya matumizi ya wateja wake kwa kuzingatia jinsi zote. Ilani ya kujenga au kurekebish a choo - 24 Verify source ↗
(1) Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika
AI-assisted research summary: If a health inspection finds a house has no toilet, a full toilet, or one unfit for human use, the authorized officer must issue a notice to the owner or occupier requiring corrective action.
24.-(1) Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika kuwa nyumba yoyote haina choo au choo kilichopo kimejaa au hakifai kwa matumizi ya binadamu, Afisa Mwidhiniwa atatoa ilani kwa mmiliki wa nyumba au mpangaji akiainisha masharti ya kurekebisha hali hiyo. (2) Ilani ya kujenga au kurekebisha choo itakuwa katika namna iliyoainishwa katika Jedwali la Nne. Uzuiaji wa shughuli wakati wa magonjwa - 25 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia shughuli fulani ili zisifanyike ikiwa ana sababu ya kuamini kuwa zinaweza kueneza magonjwa ya mlipuko na kuathiri maisha ya binadamu.
25. Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia shughuli yoyote isifanyike kama vile utengenezaji wa vyakula, pombe, mijumuiko, sherehe na mikusanyiko yoyote 8 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) ya mlipuko Ukamataji wakati wa zuio Ilani ya kuondoa kero Uteuzi wa wakala kwa kutangaza kwa njia ya kipaza sauti, maandishi au kupitia vyombo vya habari endapo atakuwa na sababu ya kuamini kwamba shughuli hiyo inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuleta athari kwa maisha ya binadamu. - 26 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri may arrest a person who disobeys a ban on selling food during an epidemic; it must destroy quickly spoiling seized food and store non-perishable seized food until the ban ends.
26.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kumkamata mtu yeyote ambaye atakaidi amri ya zuio la kufanyika kwa shughuli ya uuzaji wa vyakula wakati wa magonjwa ya mlipuko. (2) Endapo mtu aliyekamatwa alikuwa anauza vyakula ambavyo vinaharibika kwa haraka, Halmashauri itaharibu vyakula hivyo. (3) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1) na (2), endapo vyakula vilivyokamatwa vitakuwa haviharibiki kwa haraka, Halmashauri itakuwa na jukumu la kuvihifadhi hadi mwisho wa amri ya zuio. (4) Halmashauri haitahusika na gharama zozote isipokuwa kama uharibifu huo utakuwa zitakazotokea umesababishwa kwa uzembe wa Afisa wa Halmashauri. - 27 Verify source ↗
(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa akigundua eneo alilokagua lina kero, anatakiwa kutoa ilani kwa wahusika ndani ya siku saba.
27.-(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote atatoa ilani ndani ya siku saba kwa mmiliki wa nyumba, mpangaji, mtumiaji au mtu yeyote anayehusika akimtaka kuondoa kero hiyo. (2) Ilani ya kuondoa kero itakuwa katika namna iliyoainishwa katika Jedwali la Pili. - 28 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kumteua wakala kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumteua wakala kutoa huduma ya usafishaji na ukusanyaji wa taka kwa niaba yake, na wakala aliye teuliwa lazima awe na mkataba na Halmashauri na kukusanya na kutupa taka kwenye dampo kuu la Halmashauri.
28.-(1) Halmashauri inaweza kumteua wakala kwa ajili ya kutoa huduma ya usafishaji na ukusanyaji wa taka kwa niaba yake. (2) Wakala atakayeteuliwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa- (a) ameingia mkataba na Halmashauri kwa ajili ya kutoa huduma ya usafi wa mazingira; na (b) anakusanya na kutupa taka hizo kwenye dampo kuu la Halmashauri. 9 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) Makosa - 29 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa anatenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akifanya mojawapo ya vitendo vilivyoorodheshwa kuhusu taka, uchafu, maji machafu, usafi wa nyumba na magari, au shughuli zisizoruhusiwa katika maeneo fulani.
29. Mtu yeyote atakuwa anatenda kosa endapo- (a) atatupa taka au uchafu wowote au kuacha takataka au uchafu kwenye nyumba, kiwanja, mfereji wa maji ya mvua, barabara au eneo linalopakana na nyumba yoyote au ardhi yoyote au karibu na popote maeneo pasipotengwa kwa shughuli hiyo; au mahali nyumba ya (b) atamzuia au kujaribu kumzuia au kumshawishi mtu au kundi la watu kumzuia Afisa Mwidhiniwa kutekeleza wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii; (c) atamwaga taka barabarani, mtaro wa maji ya mvua, uchochoroni au mahali popote hadharani au katika eneo lolote lisiloruhusiwa; (d) ataendesha biashara ya pombe ndani ya nyumba ya makazi; (e) atatiririsha maji machafu barabarani au katika eneo la nyumba ya jirani; (f) ataosha magari, kufua, kunywesha mifugo na kukoroga dawa za mimea ndani ya mito, mabwawa, lambo au ndani ya chanzo au kisima kinachotumika kwa matumizi ya binadamu; (g) atapika vyakula pembezoni mwa barabara au nje ya majengo mengine; (h) atauza vyakula maeneo yasiyo rasmi na kushindwa kuhifadhi chakula kwenye kabati safi lililofunikwa na lenye kioo; (i) atafanya matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo, katika maeneo ya wazi, makazi, barabarani, uchochoroni au katika maeneo yasiyotengwa kwa shughuli hizo bila kuzingatia taratibu za mipango miji; (j) atavuta sigara hadharani au mahali pa jumuiya au kwenye vyombo vya usafiri; (k) atatema mate hovyo au kutema mate barabarani au mahali pa jumuiya; (l) ataacha nyumba anayoishi au kumiliki au kufanyia shughuli zake katika hali ya uchafu yenye kuleta kero au chukizo; 10 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) (m) ataacha chombo cha usafiri katika hali ya uchafu; (n) ataendesha shughuli za viwanda katika maeneo ya wazi, makazi, barabarani, uchochoroni, au katika maeneo yasiyotengwa kwa shughuli hizo bila kuzingatia taratibu za mipango miji; (o) ataanzisha au kufungua karakana katika majengo au majumba au maeneo ya makazi; (p) ataenda haja ndogo au kubwa hovyo barabarani, uchochoroni au upenuni; au (q) atafanya biashara ya kuosha gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo halikutengwa kwa shughuli lake kutumika kwa hiyo au kuruhusu eneo shughuli za kuosha vyombo vya moto katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hizo bila kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri; Adhabu - 30 Verify source ↗
Mtu atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: A person who violates the bylaw commits an offence and, if convicted, may be fined, imprisoned for up to 12 months, or both.
30. Mtu atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 31 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyefanya kosa chini ya sheria ndogo hii hadi shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Tano.
31. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari yake na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Tano la Sheria Ndogo hii. ________________ JEDWALI LA KWANZA _______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 10) GHARAMA ZA UKUSANYAJI TAKA KATIKA MAJENGO YA BIASHARA NA MAKAZI Namba Aina ya Biashara Kiwango cha Ada (Shilingi) 1 Aina nyingine ya biashara/huduma 10,000 kwa mwezi 11 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 Baa Benki Dahalia (Hostel) Dobi mdogo Dobi Mkubwa 4,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 1000 kwa mwezi 2,000 kwa mwezi Duka la simu, kampuni ya simu kwa mnara 10,000 kwa mwezi Duka dogo la chakula (mini Supermarket) 3,000 kwa mwezi Duka kubwa la chakula (Supermarket) 5,000 kwa mwezi Duka la dawa (rejareja) Duka la dawa (Jumla ) Duka la Jumla Duka la kuuza nyama na samaki Duka la Nguo 5,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 5,000 kwa mwezi 5,000 kwa mwezi 3,000 kwa mwezi Duka la rejareja bidhaa mchanganyiko 5,000 kwa mwezi duka la vifaa chakavu 5,000 kwa mwezi Duka la vinywaji na chakula (grocery) 2,000 kwa mwezi Fundi chuma Fundi Seremala fundi viatu 2,000 kwa mwezi 2,000 kwa mwezi 1,000 kwa mwezi Fundi wa kushona kwa kila cherehani 1,000 kwa mwezi Fundi wa vifaa vya umeme Genge kwa meza moja Gereji pikipiki Gereji ya magari Ghala Karakana 3,000 kwa mwezi 1,000 kwa mwezi 5,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi Kituo cha Afya (taka zisizo hatari) 10,000 kwa mwezi kituo cha baiskeli kituo cha boda boda Kituo cha kuuza mafuta 3,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 50,000 kwa mwezi 12 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44 45 46 47 48 49 50 51 52 53 54 55 56 57 58 59 Kituo cha kuuzia gesi Kituo cha michezo kiwanda cha kuuza mbao Kiwanda kidogo Kiwanda kidogo kwa trip zisizozidi 4 kwa mwezi Kiwanda kikubwa Klabu ya pombe ya asili Klabu ya usiku Kumbi za starehe 5,000 kwa mwezi 5,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 100,000 kwa mwezi 5,000 kwa mwezi 8,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi Lori la Mizigo kushusha (mzigo eneo rasmi) 5,000 kwa tripu moja Maabara ya Vipimo Madawa ya asili Makazi (kaya) kijijini Makazi (kaya) Mjini Mama lishe/baba lishe Mashamba makubwa ya maua, kahawa, kahawa na mazao mengine Mgahawa Mkubwa msikiti/kanisa bila kuwa na shughuli za biashara 10,000 kwa mwezi 5,000 kwa mwezi 1,000 kwa mwezi 2,000 kwa mwezi 1,000 kwa mwezi 100,000 kwa mwezi 5,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi Nyumba ya Kulala wageni 10,000 kwa mwezi Nyumba kwa ajili ya watumishi (Watumishi Housing) 100,000 kwa mwezi Ofisi za ulinzi Saluni 5000 kwa mwezi 3,000 kwa mwezi sehemu za kutengeza chai/uji na vitafunwa 1,000 kwa mwezi Shughuli za vioo 10,000 kwa mwezi Shule ya Msingi ya Bweni binafsi 10,000 kwa mwezi Shule ya Msingi ya kutwa binafsi 10,000 kwa mwezi Shule ya sekondari kutwa binafsi 10,000 kwa mwezi shule ya sekondari ya bweni 10,000 kwa mwezi 13 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) 60 61 62 63 64 65 66 67 68 69 70 Stoo Stoo za Mkaa Taasisi/Idara Uwanja wa michezo 10,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 20,000 kwa mwezi Vibanda kuweka na kutoa fedha 1,000 kwa mwezi Vifaa vya ujenzi vifaa vya umeme, simu, Vipuri na Vifaa Vitabu shajala Vituo vya kuoshea magari Kuuza miwa (kwa kituo) 4,000 kwa mwezi 4,000 kwa mwezi 2,000 kwa mwezi 2,000 kwa mwezi 10,000 kwa mwezi 5,000 Kwa mwezi ____________ JEDWALI LA PILI ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 27(2)) HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ILANI YA KUONDOA KERO SEHEMU ‘A’ kwamba Ndugu……………………………………………… wa Mtaa/Kijiji………………………Kata uliofanyika ya……………….unaarifiwa Tarehe…….....mwezi…………mwaka………… katika nyumba yako ya Biashara/Kuishi/Kutolea Huduma* iliyopo eneo la……………………………….kumekutwa na adha zifuatazo:
Part
JEDWALI LA PILI
- 5 Verify source ↗
………………………………………………………………………
AI-assisted research summary: This notice says you are ordered to do the following in Section B, but the specific steps are not shown here.
5. ……………………………………………………………………… ukaguzi katika SEHEMU ‘B’ Kwa ilani hii unaamriwa kufanya yafuatayo: - 5 Verify source ↗
…………………………………………………………………………
AI-assisted research summary: The notice recipient must follow the instructions in the notice within the stated time, and the council may take legal action if they do not.
5. ………………………………………………………………………… SEHEMU ‘C’ 14 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) Unapewa muda wa siku ……… tangu siku ya kupokea ilani hii kutekeleza yote yaliyoelezwa katika Sehemu ‘B’ ya ilani hii. Kushindwa kwako kutekeleza ndani ya muda uliopewa Halmashauri italazimika kukuchukulia hatua kali za kisheria bila kulazimika kukupa taarifa nyingine. IMEPOKELEWA NA: Jina……………………………. …… Saini…………………………… …… Wadhifa……………………………… Tarehe…………………………. …… KWA MATUMIZI YA OFISI TU Kimetolewa na: Jina la Afisa Mwidhiniwa…………………………………..Saini……… Wadhifa:……………………………………………………………….. Tarehe:………………… Muhuri:…………………………………………… *futa lisilohusika _____________ JEDWALI LA TATU _____________ KIBALI CHA KUSAFIRISHA TAKA ZA PLASTIKI (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 13(4)) Namba ya Kibali…………………… ……………………………………….. Jina……………………………………………………………………………… Anwani: …………………………………………………………………………………… Umeruhusiwa kusafirisha taka ngumu kutoka: ……………………Kata/Wilaya) Kwenda ……………………………… Kata/Wilaya. Aina ya Gari na Namba ya usajiri wa Gari ……………………………………… Leseni kuanzia………20………………….Hadi……………20………………………… hii lililopewa kibali cha Kusafirisha itatumika Leseni hii imetolewa kwa kuzingatia masharti yafuatayo……………………………………………………………………………………………… ……………………………… 15 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) ………………………………………………………………………………………………………… ……………………………… ………………………………………………………………………………………………………… KWA MATUMIZI YA OFISI TU Kimetolewa na: Jina la Afisa Mwidhiniwa…………………………………..Saini……… Wadhifa:……………………………………………………………….. Tarehe:………………… Muhuri:…………………………………………… *futa lisilohusika _________ JEDWALI LA NNE __________ ILANI YA KUJENGA AU KUREKEBISHA CHOO (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 24(2)) SEHEMU ‘A’ Ndugu…………………………………………wa Mtaa/Kijiji……………Kata ya………………………………………………..Unaarifiwa kwamba katika ukaguzi uliofanyika ya Tarehe………..Mwezi…………Mwaka……………… eneo Biashara/kuishi/kutolea la……………………..………… kitongoji/Mtaa*……………Kijiji Katika cha…………………Kata ya………………… Imekuwa haina choo/choo kimejaa/kimeharibika * hivyo unaamriwa kutekeleza mambo yafuatayo:- (1)………………………………………………………………………………… (2)………………………………………………………………………………… (3)………………………………………………………………………………… (4)………………………………………………………………………………… namba..………………….iliyopo huduma* nyumba Katika yako SEHEMU ‘B’ Unapewa muda wa siku thelathini (30) tu tangu siku ya kupokea ilani hii kutekeleza maelekezo yote yaliyoelekezwa katika sehemu ‘A’ ya Ilani hii. SEHEMU ‘C’ Ukaguzi wa kuthibitisha utekelezaji wa maelekezo uliyopewa utafanyika tarehe…………… endapo utashindwa kutekeleza maelekezo ndani ya muda uliopewa Halmashauri itachukulia hatua kali za kisheria bila kukupa taarifa nyingine. IMEPOKELEWA NA: Jina……………………………. …… Saini…………………………… …… Wadhifa……………………………… Tarehe…………………………. …… 16 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) KWA MATUMIZI YA OFISI TU Kimetolewa na: Jina la Afisa Mwidhiniwa…………………………………..Saini……… Wadhifa:……………………………………………………………….. Tarehe:………………… Muhuri:…………………………………………… *futa lisilohusika _____________ JEDWALI LA TANO ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 31) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi;………………………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya;…………………………………….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Magu, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka;…….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya……….. ya Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe:…....... ya Mwezi:………… Mwaka:………….. Jina:…………………………………..……………………. Saini:…………………………..…………………………… MBELE YANGU: Jina:…………………………….………..…………………… Wadhifa:…………………………………………………..……. Saini:………………………………………………………… Tarehe:……………………………………………………… 17 Sheria Ndogo ya (Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu Tanagazo La Serikali Na. 97 (Linaendelea) Nembo na mhuri wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu umebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika Tarehe 27 Mwezi machi Mwaka 2022 FIDELIKA GABRIEL MYOVELLA Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Magu MPNDALUME S. MPANDALUME Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Magu NAKUBALI, L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB), 2 Februari, 2024 Waziri Wa Nchi - Ofisi Raisi, (Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa) 18
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya (Usafi Wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu ya Mwaka, 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in