AI-assisted research summary: Mwombaji amepewa kibali cha kujenga kituo cha mafuta kwenye Kiwanja Na. 2348, Masanga, Kigoma/Ujiji, lakini lazima akidhi masharti ya usalama na ujenzi yaliyoorodheshwa.
3. Mwombaji anapewa kibali cha ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mafuta kwenye Kiwanja Na. 2348, Kitalu “A”, Eneo la Masanga, Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Mkoa wa Kigoma, kwa kuzingatia masharti yafuatayo: (a) kituo cha mafuta kitajengwa kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania Na. TZS 1115:2009 na TZS 1079:2008; (b) uangalifu wa kutosha utazingatiwa wakati wa uchimbaji na uwekaji wa matenki ya mafuta chini 1 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo Cha Mafuta Kwa Salmo Oil Limited Tangazo La Serikali Na. 129 (Linaendelea) ya ardhi; (c) mpangilio wa kituo cha mafuta utapaswa kukidhi umbali wa kiusalama kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania Na. TZS 1079:2008; (d) ufukiaji wa matenki ya kuhifadhi mafuta pamoja na mabomba chini ya ardhi utapaswa kufanywa kwa namna ambayo italinda usalama wa vifaa hivyo ikiwemo kupata kutu; (e) matenki ya kuhifadhia mafuta, pampu na mabomba husika pamoja na vifaa vyote vinavyounganishwa pamoja navyo vitapaswa kufungwa vizuri ili kuzuia uvujaji wowote wa mafuta; (f) matenki ya kuhifadhia mafuta na pampu za mafuta zitapaswa kufanyiwa uhakiki wa usahihi wa vipimo na Wakala wa Vipimo Tanzania ulioanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo; (g) eneo la mbele la kituo cha mafuta na kuzunguka eneo la pampu litasakafiwa kwa zege madhubuti lisiloweza kupenyeza mafuta na kuhakikisha kuwepo kwa mitaro itakayokusanya maji na mafuta wakati wa mvua na kuyaelekeza kwenye chemba ya kutenganisha maji na mafuta; Sura ya 340 (h) kuweka ya swichi eneo linaloonekana na kufikika kirahisi ili iwe rahisi kuzima umeme wa kituo kizima wakati wa dharura; dharura katika (i) kuhakikisha uwepo wa vyoo vya kutosha vya wanawake na wanaume vilivyo safi wakati wote; (j) kuhakikisha kuwa alama za usalama zinawekwa sehemu ya kuingia na ya kutoka kwenye kituo cha mafuta na eneo la pampu zikijumuisha “zima injini”, “zima simu” na “usivute sigara”; (k) kuhakikisha kila tenki la kuhifadhia mafuta linaunganishwa na bomba la kupumulia lenye urefu usiopungua mita 3.6 kutoka ardhini na bomba hilo linatakiwa kuwa angalau mita 1.5 2 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo Cha Mafuta Kwa Salmo Oil Limited Tangazo La Serikali Na. 129 (Linaendelea) kutoka kwenye mpaka wa kiwanja na angalau mita 4 kutoka kwenye dirisha au kifaa chochote cha kuvuta hewa ikiwemo kiyoyozi; (l) pampu za kuuza mafuta na sehemu ya kushushia mafuta zinatakiwa kuwa angalau mita 4.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja, angalau mita 8 kutoka kifaa chochote ambacho kinaweza kuwa chanzo cha moto ikiwemo jokofu na angalau mita 10 kutoka kwenye nyaya za kusafirishia umeme; (m) kuhakikisha kila pampu ya mafuta inalindwa na kizuizi na kizuizi kitapaswa kuwa na urefu wa mita 1 kutoka juu ya ardhi; (n) mifumo ya upakuaji wa mafuta kwenye kituo cha mafuta itapaswa kujengwa kwa kufuata kanuni na taratibu zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; (o) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na paa linalofunika eneo lote lenye pampu za mafuta na linajengwa kwa mujibu wa viwango na taratibu zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; na (p) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na bango la bei ambalo litawekwa mahala ambapo panaonekana kirahisi ili wateja waweze kuona bei za mafuta kabla ya kuingia kituoni. Ukomo wa kibali cha ujenzi