KANUNI ZA AJIRA ZA WATOTO ZA MWAKA 2012
Kanuni hizi zinaweka masharti ya ajira ya watoto, ikiwemo marufuku ya kuajiri watoto wadogo katika hali fulani, mahitaji ya mkataba, mapumziko, ujira, usalama, usajili, na ufuatiliaji.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- KANUNI ZA AJIRA ZA WATOTO ZA MWAKA 2012
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This page preserves the statute’s identified version, provision structure, official source link, and stored legal text for reading and research.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of KANUNI ZA AJIRA ZA WATOTO ZA MWAKA 2012
Showing 1 of 1
- document Verify source ↗
Document text
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinaweka masharti ya ajira ya watoto, ikiwemo marufuku ya kuajiri watoto wadogo katika hali fulani, mahitaji ya mkataba, mapumziko, ujira, usalama, usajili, na ufuatiliaji.
Kanuni za Ajira za Watoto JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ______ SHERIA YA MTOTO [SURA YA 13] TAFSIRI YA KANUNI ZA AJIRA ZA WATOTO ZA MWAKA 2012 Toleo hili la Kanuni za Ajira za Watoto za mwaka 2012, Tangazo la Serikali Na. 196 la tarehe 1 Juni, Mwaka 2012, ni Tafsiri Rasmi iliyosanifiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuchapishwa kwa mujibu wa kifungu cha 84 cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria Mbalimbali, Sura ya 1. Dar es Salaam 28 April, 2016 GEORGE M. MASAJU, Mwanasheria Mkuu Wa Serikali 1 Kanuni za Ajira za Watoto TANGAZO LA SERIKALI NA. 168 la 13/05/2016 SHERIA YA MTOTO (SURA YA 13) ______ KANUNI ZA AJIRA ZA WATOTO ZA MWAKA 2012 1. Jina. 2. Matumizi. 3. Tafsiri. MPANGILIO WA KANUNI SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI SEHEMU YA PILI AJIRA YA MTOTO 4. Umri wa chini wa ajira. 5. Aina za ajira zilizokatazawa. 6. Aina mbaya ya kazi kwa watoto. 7. Ajira hatarishi. 8. Udhalilishaji wa kijinsia. 9. Kazi nyepesi. 10. Afya na usalama. SEHEMU YA TATU VIWANGO VYA CHINI VYA AJIRA 11. Mkataba wa ajira. 12. Mapumziko wakati wa kazi. 13. Ujira. SEHEMU YA NNE WAJIBU WA MWAJIRI 14. Wajibu wa mwajiri. 15. Wajibu wa mwajiriwa au mwangalizi. 1 Kanuni za Ajira za Watoto SEHEMU YA TANO MAFUNZO NA AJIRA YA MTOTO 16. Mafunzo katika Sekta zilizzochaguliwa. 17. Cheti cha mafunzo. SEHEMU YA SITA UTII NA UTEKELEZAJI 18. Wajibu wa Afisa Kazi. USIMAMIZI, UTEKELEZAJI NA MWITIKIO SEHEMU YA SABA 19. Wajibu wa Afisa Ustawi wa Jamii. 20. Adhabu kwa vunja Sheria. 21. Utatuzi wa migogoro. ______ JEDWALI _______ 2 Kanuni za Ajira za Watoto SHERIA YA MTOTO, (SURA YA 13) ______ KANUNI ______ KANUNI ZA AJIRA YA MTOTO ZA MWAKA 2012 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI Jina 1. Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Ajira za Watoto za mwaka 2012. Matumizi Sura ya 366 Sura ya 191, 432, 297 Tafsiri Sura ya 13 2.-(1) Kanuni hizi zitatumika kwa waajiri wote katika sekta ya umma, binafsi na isiyo tengeneza faida ndani ya Tanzania Bara. (2) Kanuni hizi zitasomwa na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sheria ya Taasisi za Kazi, Sheria ya Makosa ya Kujamiiana, Sheria ya Kuzuia Biashara ya Binadamu, Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi, Sheria ya Watu Wenye Ulemavu ya mwaka, 2010 na Sheria au Kanuni zozote nyingine zinazohusika. 3. Katika Kanuni hizi,isipokuwa kama muktadha unahitaji vinginevyo: “Sheria” maana yake ni Sheria ya Mtoto; “mwangalizi” maana yake ni mzazi yeyote, mlezi, taasisi inayowajibika kwa ajili ya kuangalia watoto, kiongozi wa kijiji au Kamati ya Kijiji inayotambulika, mwalimu au mtu yeyote anayewajibika kwa ajili ya kuangalia mtoto; “mtoto” maana yake ni mtu mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane; “ajira ya mtoto” maana yake ni muundo wowote wa kazi ulioruhusiwa chini ya Kanuni hizi; “nyumba za uangalizi” maana yake ni majengo yaliyosajiliwa na yanayotumika kwa ajili ya uangalizi wa wagonjwa, watoto au wazee; “mkataba wa Ajira” maana yake ni mkataba au maelezo 3 Kanuni za Ajira za Watoto yaliyoandikwa kwa urefu yaliyosainiwa na mwajiri na mwangalizi wa mtoto; “kazi ndogo ndogo za kijamii” ni kazi zinazofanywa katika ngazi ya kaya kama sehemu ya mchakato wa kuwa pamoja; “mwajiriwa” maana yake ni mtu ambaye ameingia katika mkataba wa ajira au ameingia katika mkataba mwingine wowote kwa ajili ya kazi; “mwajiri” maana yake ni mtu yeyote ambaye anaajiri na taasisi binafsi au wakala wa inajumuisha Serikali, Serikali; “ajira” maana yake ni shughuli inayokubalika kisheria ambayo iko ndani ya mpaka wa maelezo ya uzalishaji ya kitaifa; shughuli zinazodhamiria katika kufikia malengo ya kiungwana na kuzalisha kipato sawa na angalau ujira wa chini uliowekwa kisekta; “kazi ya kulazimishwa” maana yake ni kazi au huduma ambayo imewekwa kwa mtoto chini ya kitisho cha adhabu na ambayo mtoto haitekelezi kwa hiyari- (a) biashara ya mtoto kwa ajili ya aina yoyote ya kazi, ikijumuisha kazi ya kijamii, kilimo, sekta ya utalii, madini, kwa ajili ya udhalilishaji wa kijinsia, katika baa au majengo yoyote yanayojulikana kwa kumweka mtoto katika hatari ya kiroho, kisaikolojia, kimwili au nyingine yoyote; (b) kazi ya mtoto fungamani; (c) utumwa au mienendo sawa na utumwa; (d) udhalilishaji wa kijinsia kibiashara; (e) ajira au kumchukua mtoto katika migogoro ya kivita; na (f) kutorosha kwa madhumuni ya ndoa. “kazi za hatari” maana yake ni kazi yoyote ambayo inamuweka mtoto katika hatari ya magonjwa ya kimwili au majeraha ya kiakili; “sekta isiyo rasmi” inajumuisha biashara zote zisizosajiliwa na shughuli za kibiashara zisizo na mpangilio rasmi; “afisa kazi’ maana yake ni afisa aliyeelezewa na Sheria ya Taasisi za kazi; “kazi nyepesi” maana yake ni kazi ambayo haionekani kuwa na madhara kwa afya na maendeleo ya mtoto; na haiathiri mahudhurio ya mtoto shuleni, kushiriki katika maelekezo 4 Sura ya 300 Sura ya 366 Sura ya 366 Kanuni za Ajira za Watoto ya mazingira ya ufundi au mpango wa mafunzo ulioidhinishwa na mamlaka yenye uwezo au uwezo wa mtoto kufaidika kutokana na maelekezo yaliyopokelewa; “umri wa chini wa kufanya kazi” inarejea kwa umri uliowekwa na Kanuni hizi na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, ambao ni umri wa miaka kumi na nne au umri wa kumaliza elimu ya lazima, yoyote iliyo ya mapema elimu yoyote; “majengo” maana yake ni jengo, kiwanda, ofisi, sehemu, shamba, kiwanja na inajumuisha chombo, gari, ndege na eneo jingine lolote ambamo mtoto anafanya kazi; “kazi ya usiku” maana yake ni kazi inayofaywa kati ya saa 2 kamili usiku na saa 12 kamili asubuhi; “mtu mwenye ulemavu” maana yake ni mtu mwenye ulemavu wa kimwili, kifikra, kiufahamu, au kiakili na ambaye uwezo wake wa kufanya kazi inakwamishwa na vikwazo vya kitabia, na ukomo wa kimtazamo, kimazingira na vikwazo vya kitaasisi; “ujira” maana yake ni jumla ya thamani ya malipo yote katika pesa iliyolipwa au inayodaiwa na mwajiriwa. “ujira wa chini wa kisekta” maana yake ni ujira uliopangwa na bodi ya ajira ya kisekta kwa kada maalum kwa mujibu wa kifungu cha 39 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini; “afisa ustawi wa jamii” maana yake ni afisa ustawi wa jamii katika utumishi wa Serikali; “wiki” maana yake ni kipindi cha siku sita ambamo wiki ya kufanya kazi ya mwajiriwa huyo kwa kawaida inaangukia. SEHEMU YA PILI AJIRA YA MTOTO Umri wa chini wa ajira 4.-(1) Mtoto ambaye ana umri wa miaka kumi na nne hataajiriwa. (2) Mtoto mwenye umri wa zaidi ya chini ya miaka kumi na nne na bado anahudhuria shuleni hataajiriwa katika mazingira yafuatayo- (a) wakati wa saa za shule au katika siku yoyote ambayo anatakiwa kuhudhuria shuleni; (b) kwa zaidi ya saa mbili katika siku yoyote ambayo 5 Kanuni za Ajira za Watoto anatakiwa kuhudhuria shuleni; (c) kwa zaidi ya saa kumi na mbili kwa wiki wakati wa wiki yoyote ya shule; (d) kufanya kazi usiku; (e) kufanya kazi kwa zaidi ya saa thelathini na sita kwa wiki wakati wa likizo za shule; (f) kufanya kazi yoyote zaidi ya kazi nyepesi; (g) kufanya kazi zaidi ya siku sita katika wiki moja yoyote. (3) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1), mtoto anaweza kufanya kazi wakati wa saa za shule pale ambapo ni sehemu ya utaratibu wa uzoefu wa kazi ulioandaliwa na shule au pale ambapo kazi hiyo ni sehemu ya utaratibu wa kielimu. (4) Kazi ndogo ndogo za kijamiii ndani ya familia au kusaidia wazazi shughuli za kijamii haziharibika kama ni ajira ya mtoto au muundo wa ajira ya mtoto uliokatazwa isipokuwa kama mazingira ya kazi hiyo yanamhatarisha mtoto. 5.-(1) Mtoto hataajiriwa au kushirikishwa kwa madhumuni ya kazi ya kinyonyaji. (2) Kwa madhumuni ya Sheria na Kanuni hizi, kazi ya kinyonyaji inajumuisha aina zote za kazi zilizoainishwa katika kifungu cha 5 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, aina mbaya ya kazi ya mtoto, kazi hatarishi kama zilivyoainishwa katika kifungu cha 82 cha Sheria, kazi za shuruti kama zilivyoainishwa katika kifungu cha 6 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini na kifungu cha 80 cha Sheria, na udhalilishaji wa kijinsia kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 83 cha Sheria. 6. Ajira mbaya za kazi ya mtoto inajumuisha- (a) aina zote za kitumwa au matendo sawa na ya kitumwa, kama uuzaji na usafirishaji haramu wa watoto, dhamana ya deni na ujakazi na kazi iliyolazimishwa au ya lazima ikijuisha kuajiri watoto kwa kulazimisha au kwa nguvu kwa ajili ya kitumika katika mogogoro ya kivita; (b) kumtumia kumsababisha atumike au kumtoa mtoto kwa ajili ya ukahaba, kwa ajili ya kutengeneza picha za ngono au kwa ajili ya uigizaji picha za ngono; (c) matumizi, kusababisha au kumtoa mtoto kwa ajili ya 6 Aina za ajira zilizokatazwa Sura ya 366 Sura ya 366 Aina mbaya ya kazi kwa mtoto Kanuni za Ajira za Watoto shughuli haramu, ususan kwa ajili ya kuzalisha na kufanya biashara ya dawa za kulevya kama kimataifa ilivyotafsiriwa inayohusika; na katiba katika ya Ajira hatarishi Udhalilishaji wa kijinsia Sura ya 16 Kazi nyepesi Sura ya 366 (d) kazi ambayo, kwa asili yake au mazingira ambayo inaweza kudhuru afya, usalama au inafanyika, maadili ya watoto. 7.-(1) Mtoto hataajiriwa au kushirkishwa kufanya kazi yoyote iliyotafsiriwa kama hatarishi katika kifungu cha 82 cha Sheria na chini ya Kanuni hizi: Isipokuwa kwamba, kazi hatarishi kama ilivyofafanuliwa katika Sheria haitochukuliwa kuwa hatarishi kwa mtoto ambaye amefikisha umri wa chini wa miaka kumi na sita ambaye anafanya kazi hiyo chini ya uangalizi na kazi haimuweki mtoto katika hatari ya ustawi wake, elimu, afya ya kimwili au kiakili au maendeleo ya kiroho au kijamii, na ikiwa itafanywa kwa maelekezo maalum au mafunzo ya ufundi katika tawi husika. (2) Orodha ya kazi hatarishi iliyoambatishwa katia Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi itatoa orodha ya shughuli zote hatarishi ambazo mtoto hataajiriwa au kuruhusiwa kuzifanya hata kwa kigezo cha kuridhia. (3) Wazira inaweza kufanya marekebisho kwenye orodha ya shughuli zote hatarishi na marekebisho hayo yatachukuliwa kuwa sahihi na orodha hatarishi inayokwenda na wakati kwa madhumuni ya Kanuni hizi. 8.-(1) Mtu hataajiri au kushirikisha watoto katika shughuli yoyote inayohusiana na matendo ya kingono yoyote au shughuli jinsia za mtoto au inayomuweka mtoto katika mandhari au picha za kigono iwe ni katika majengo ya mwajiri au pengine popote. inayoweka wazi sehemu za (2) Katika kuamua matendo mengine ambayo yanasababisha udhalilishaji wa kingono, rejea ifanywe kwa Sheria ya Kanuni za Adhabu. 9.-(1) Mtoto ambaye amefikisha umri wa chini wa kufanya kazi anaweza kuruhusiwa kufanya kazi nyepesi kama ilivyoelezwa na Sheria na katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. 7 Kanuni za Ajira za Watoto (2) Mamlaka yenye uwezo, katika kuamua kile kinachosababisha kazi nyepesi, itazingatia hatari nyingine zozote ambazo zipo katika majengo au nje ya majengo wakati mtoto amejumuishwa katika aina yoyote ya kazi. (3) Kazi nyepesi hazitajumuisha kazi ambayo itafikiriwa kuwa ni hatarishi kwa namna yoyote na inajumuisha kufanya kazi katika majengo yafuatayo- (a) majengo au mazingira yanayoongeza hatari kwa afya na usalama ikijumuisha maeneo yenye vumbi au moshi, kemikali hatari, kelele kali, mitikisiko, joto, kuinama, kusimama au kukaa chini, maeneo ambayo ni oevu kupita kiasi au yaliyojaa maji, vifaa hatari vya kufanyia kazi kama vile vyenye ncha, mitambo mikubwa, kubeba mizigo mizito mgongoni, kichwani au mabegani au matumizi ya moto au kwenye moto; na (b) majengo ambayo yanamuweka mtoto katika hatari za kiroho na kisaikolojia ikijumuisha uuzaji wa vitu vya ngono au kumweka mtoto katika ukatili wa kimwili au unyanyasaji na udhalilishaji wa kingono au shughuli, mazingira, maneno au tendo lolote ambalo linamweka mtoto katika tabia za uovu au tabia mbaya. Afya na usalama Sura ya 297 Sura ya 182 10.-(1) Kila mwajiri atawajibika kuhakikisha usalama na ustawi wa mwajiriwa yeyote wa mtoto kwa mujibu wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi, na sheria nyingine yoyote inayosimamia afya na usalama kazini. (2) Mwajiri atafanya tathmini ya athari ili kuhakikisha kwamba sehemu ya kazi ni salama na hatari zote zimepunguzwa kwa kiasi kikubwa inavyowezekana au zimeondolewa. (3) Mtoto mwenye ulemavu atapewa haki na stahili kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Watu Wenye Ulemavu na sheria nyingine yoyote inayosimamia ajira ya mtu mwenye ulemavu. 8 Kanuni za Ajira za Watoto SEHEMU YA TATU VIWANGO VYA CHINI VYA AJIRA Mkataba wa Ajira Sura ya 366 Sura ya 263 Sura ya 366 11.-(1) Mtoto hataajiriwa bila mkataba au andiko la maelezo mahsusi lililosainiwa na mwajiri na kusainiwa na mwangalizi wa mtoto. (2) Mtoto ataeleza kuridhia kwake vigezo na masharti ya mkataba au andiko la maelezo mahsusi mbele ya mwajiri na mwangalizi. (3) Mkataba utasomwa kwa mtoto na mwangalizi au kiongozi wa Serikali ya Mtaa ambapo mtoto ameajiriwa iwapo haupo asipokuwepo au anaposhindwa kufanya hivyo. (4) Mwajiri atawajibika kwa ajili ya kuandaa mikataba ya ajira. (5) Mwajiri atajumuisha katika mkataba haki zote na stahili kama zilivyotolewa katika Sehemu ya Tatu ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. (6) Kipindi cha mkataba kitakuwa kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini na pale ambapo ni lazima, itaamuliwa zaidi na mwajiri kwa kushauriana na muangalizi kwa niaba ya mtoto na isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo, uhusishaji utakuwa kwa mujibu wa mapatano mengine na mtoto na waangalizi wao. (7) Masharti yanayosimamia afya na usalama mahali pa kazi kama yalivyotolewa na sheria yatakuwa sehemu ya makubaliano. (8) Mkataba utaagiza haki ya uangalizi wa kitabibu kwa ajili ya mtoto ikiwa mtoto atajeruhiwa au kupata ugonjwa akiwa kazini. (9) Mtoto aliyejeruhiwa au kupata ugonjwa kutokana na ajira atalipwa fidia kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi. (10) Mkataba unaainisha kwa muhtasari majukumu ya mtoto na kueleza shughuli mahsusi ambazo mtoto atapewa. (11) Masharti ya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini yanaweza kutumika kuonesha namna ya kuandika mikataba. Mapumziko wakati wa kazi 12.-(1) Mwajiri atampa mtoto ambaye anafanya kazi kwa zaidi ya saa tatu katika siku yoyote chakula au muda wa 9 Kanuni za Ajira za Watoto mapumziko wa angalau saa moja. (2) Ujira wa mtoto hautakatwa kutokana na vipindi vya mapumziko. (3) Kipindi cha mapumziko hakitahesabika katika saa za juu za kazi katika siku moja yoyote. (4) Mtoto hatahitajika au kuruhusiwa kufanya kazi katika muda wa ziada ama kwa malipo au bila malipo. Ujira 13.-(1) Waajiri wana wajibu wa kulipa si chini ya ujira Sura ya 366 Wajibu wa mwajiri wa chini wa kiasi cha kisekta. (2) Ujira kwa ajili ya mtoto utakuwa kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Amri ya Ujira na Kanuni nyingine zozote. (3) Makato kwenye ujira hayatafanyika isipokuwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini na Kanuni za Ujira wa chini wa Kisekta. SEHEMU YA NNE WAJIBU WA MWAJIRI 14.-(1) Mwajiri atamjulisha mtoto haki zote, wajibu, tahfif na njia ya utatuzi wa mgogoro. (2) Mwajiri atasimamia na kuhakikisha kwamba muajiriwa mtoto haendeshi mitambo ya hatari, hatumii vifaa hatari vya kazi au kufanya kazi katika mazingira hatari au hatarishi. (3) Mwajiri hatambagua mwajiriwa mtoto kwa vigezo vya jinsia, kabila, ulemavu, hali ya UKIMWI, uyatima au hali nyingine yoyote. (4) Mwajiri atakuwa na wajibu wa kutoa uangalizi mzuri kwa watoto wenye ulemavu. (5) Mwajiri atakuwa na wajibu wa kutoa vifaa vya kutosha vya usafi kwa ajili ya waajiriwa wasichana na wavulana kwa wakati wote. (6) Mwajiri ana wajibu wa kuhakikisha kwamba mtoto anafanya kazi chini ya hali ya usalama, ikijumuisha kuhakikisha, kwamba wanazo zana za kufanyia kazi na hali nyingine zozote za usalama kama zilivyoelezewa katika Sheria za Afya na Usalama Mahali pa Kazi. (7) Mwajiri atawasajili watoto wote wanaofanya kazi 10 Wajibu wa mwajiriwa au muangalizi Mafunzo katika sekta zilizochaguliwa Kanuni za Ajira za Watoto katika majengo yake. (8) Rejesta itakuwa na maelezo ya umri, kabila, jinsia, ulemavu na maelezo ya kuwasiliana na muangalizi. (9) Mwajiri ataachia huru daftari kwa ajili ya ukaguzi pale ikapohitajika na taasisi iliyoidhinishwa. (10) Mwajiri atatii sheria zote na kanuni zinazosimamia ulinzi wa mtoto. 15.-(1) Mwangalizi atakuwa na wajibu wa kutoa taarifa ya udhalilishaji wowote au unyanyasaji kwa afisa ustawi wa jamii au mamlaka za serikali za mitaa pale ambapo mwangalizi anahisi kwamba kuna udhalilishaji au unyanyasaji wa mwajiriwa mtoto. (2) Mtu mwingine yeyote anaweza kutoa taarifa ya udhalilishaji au unyanyasaji kwa afisa ustawi wa jamii au mamlaka za serikali za mitaa pale ambapo mtu huyo anahisi kwamba kuna udhalilishaji au unyanyasaji. (3) Pale ambapo shauri litakuwa limetolewa taarifa kwa mamlaka ya mtaa, mamlaka ya mtaa itakuwa na wajibu wa kutoa taarifa ya shauri haraka kwa afisa ustawi wa jamii kwa hatua zaidi. (4) Mtoto atatoa taarifa ya udhalilishaji au unyanyasaji uliofanywa katika sehemu ya kazi kwa afisa ustawi wa jamii, mamlaka ya serikali ya mtaa au taasisi nyingine yoyote inayofanyia kazi haki za watoto. SEHEMU YA TANO MAFUNZO NA AJIRA YA MTOTO 16.-(1) Mtoto anaweza, kwa mujibu wa kifungu cha 5(5) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini na kifungu cha 82(4) cha Sheria, kuruhusiwa kushiriki katika mafunzo ilimradi kwamba mtoto hawekwi katika mazingira hatarishi. (2) Mafunzo katika kiwanda, meli, au mgodi yatafanyika kwa mujibu wa mtaala ulioidhinishwa na chini ya ukaguzi wa mara kwa mara wa afisa kazi, afisa afya na usalama mahali pa kazi na mkaguzi wa mafunzo ya ufundi. (3) Pale ambapo mazingira ya mafunzo yatakuwa yamethibitishwa kuwa salama na afisa kazi au taasisi nyingine yoyote yenye wajibu wa kuidhinisha viwango, mtoto wa umri wa kufanya kazi atasajiliwa na mtoa mafunzo. 11 Kanuni za Ajira za Watoto (4) Rejesta litajumuisha umri wa mtoto, tarehe ya kuzaliwa, kabila, jina la mtoto, jinsia, hali ya ulemavu, ngazi ya elimu, hali ya afya, majina na mawasiliano ya waangalizi na asili ya mafunzo yaliyotolewa. (5) Rejesta litawekwa wazi kwa ajili ya ukaguzi wa afisa kazi au afisa mwingine yeyote aliyeidhinishwa na Sheria. (6) Kipindi cha mafunzo katika kiwanda, meli au mgodi hakitazidi miaka minne. (7) Matumizi ya nyenzo za usalama katika kipindi cha mafunzo katika kiwanda, meli ya mafunzo au mgodi itakuwa ni lazima. (8) Mkataba kwa ajili ya mafunzo utakuwa sawa na masharti ya Sheria ya Elimu, Kanuni za Mafunzo za mwaka 2011 na kanuni nyingine zozote kuhusiana na makubaliano ya mafunzo. Cheti cha mafunzo Sura ya 300 17.-(1) Mtoto atastahili kupewa cheti cha kuhitimu baada ya kumaliza kozi yote ya mafunzo. (2) Cheti cha mafunzo kitakuwa sawa na viwango vya Serikali kwa ajili ya utoaji wa vyeti. Wajibu wa Afisa Kazi SEHEMU YA SITA UTII NA UTEKELEZAJI 18.-(1) Afisa Kazi atakagua mazingira ya kufanyia kazi na viwango mara kwa mara kama ilivyowekwa kwa ajili hiyo chini ya Sheria ya Taasisi za Kazi na zitakazofuatia. (2) Afisa Kazi atakuwa na mamlaka ya kumsaili mtoto yeyote aliyekutwa anafanya kazi katika majengo yoyote. (3) Usaili utafanyika kwa faragha bila ya mtu mwingine yeyote kuwepo. (4) Afisa Kazi atakuwa na wajibu wa kumtaarifu mtoto kuhusu haki zote za ajira na stahili ikijumuisha njia za kutatua migogoro. (5) Afisa Kazi atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba mwajiri ambaye ameajiri watoto ametimiza viwango vya ajira vilivyowekwa katika Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi na Sheria nyingine zozote zinazohusika. 12 Wajibu wa Afisa Ustawi wa Jamii Kanuni za Ajira za Watoto (6) Afisa Kazi, kwa kushauriana na afisa ustawi wa jamii, atachukua hatua zote za lazima kufuatilia utekelezaji wa masharti ya Sehemu ya Saba ya Sheria. (7) Inapotokea mtoto amekutwa anafanya kazi katika mazingira ya udhalilishaji, Afisa Kazi atatoa taarifa haraka kwa mamlaka zilizoteuliwa jamii, mamlaka za serikali za mitaa na polisi. ikijumuisha afisa ustawi wa SEHEMU YA SABA USIMAMIZI, UTEKELEZAJI NA MWITIKIO 19.-(1) Afisa Ustawi wa Jamii, baada ya kupokea ukiukwaji wa taarifa za Kanuni hizi, atakuwa na wajibu wa kutoa taarifa hizo. (2) Pale ambapo shauri litakuwa limeripotiwa kwa afisa ustawi wa jamii au mamlaka nyingine yoyote iliyoteuliwa, afisa ustawi wa jamii au afisa mwingine yeyote wa Serikali atahakikisha kwamba mtoto ameondolewa au kutolewa kutoka katika ajira hiyo na amepewa huduma za urekebu. (3) Afisa Ustawi wa Jamii atahakikisha kwamba mtoto amepelekwa katika taasisi au mtu mwingine yeyote anayefaa ambaye anatoa malazi ya muda au huduma nyigine yoyote kama itakavyokuwa. (4) Utakuwa ni wajibu wa afisa ustawi wa jamii kukutana na mwangalizi na kujadili mazingira yaliyosababisha kutolewa au kuondolewa kwa mtoto kutoka katika ajira ya udhalilishaji, na matokeo ya udhalilishaji huo. Adhabu kwa kuvunja Sheria Sura ya 16 na 366 20. Pale ambapo mtu anakiuka masharti yoyote yanayohusu ajira ya mtoto, adhabu zote, na adhabu zilizotolewa na Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini na sheria nyingine zozote na kanuni zitatumika. Utatuzi wa migogoro Sura ya 300 21.-(1) Ukiukwaji wowote wa masharti haya au masharti mengine yoyote kuhusu ajira ya mtoto utafunguliwa katika mahakama za sheria kwa mujibu wa Sheria ya Taasisi za Ajira. (2) Mtoto atapewa msaada wa kisheria au mwingine wowote kuwezesha mahudhurio yao kusikiliza kesi mahakamani. (3) Kanuni kuhusu haki ya mtoto zitatumika kwa madhumuni ya kumlinda mtoto. 13 Kanuni za Ajira za Watoto ______ JEDWALI ______ (Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 7(2)) _____ Kazi Hatarishi ____ A: SEKTA YA KILIMO 1. Kunyunyiza dawa za kuulia wadudu ikijumusiha mbolea. 2. Kuvuna na kuchambua pale ambapo anatumia zana na vifaa vya hatari au kuvuna mazao ambayo yanaweza kuwa na madhara. 3. Kupanda mazao pale ambapo mazingira yanaleta tishio au hatari kwa afya ya mtoto. 4. Kuchunga idadi kubwa ya mifugo. 5. Kuendesha mashine za shambani. 6. Kusaidia mafundi sanifu kwenye karakana za shambani ikiwa hatua za kiusalama B: C: hazikuzingatiwa. 7. Kubeba mavuno kwa magari ya usafiri. 8. Kubeba uchafu kwa ajili ya kuutupa. 9. Kusafisha nyumba za wanyama za kibiashara. 10. Kusafisha vifaa vya kupulizia. 11. Kuchukua na kubeba kuni kwa ajili ya biashara. SEKTA YA UVUVI 1. Kupanga au kukokotoa nyavu. 2. Kuchambua nyavu. 3. Kupika kwa madhumuni ya kibiashara. 4. Kubeba barafu. 5. Kutoa matumbo, kutoa magamba, kukata samaki. 6. Kuweka chumvi samaki na kukausha. 7. Kukausha boti. 8. Kuvua katika bahari kuu. SEKTA YA MADINI NA KUPASUA MAWE 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. Uchimbaji wa mashimo, mkondo au handaki. Kubeba mawe ya madini kutoka shimoni. Kutoboa na kulipua. Kuponda mawe ya madini. Kusaga mawe ya madini, kuchekecha mawe ya madini. Kupanga mchanga mkavu na uliolowana. Kubeba maji. Kuunganisha na kushughulikia madini. 14 Kanuni za Ajira za Watoto D: SEKTA YA UJENZI 1. Kuchanganya saruji. 2. Kupaka rangi. 3. Kutengeneza Tofali (la kuchoma au la saruji). 4. Kuchimba mfereji. 5. Kubeba maji. 6. Kubeba matofali. 7. Kuendesha mashine ya uchimbuaji. 8. Ubomoaji. 9. Msaidizi wa gari. 10. Zana za kupondea mawe na usafirishaji kwenda kiwanjani. E: SEKTA YA HUDUMA (a) Huduma za jamii 1. Utengenezaji wa vifaa na makazi. 2. Utoaji msaada wa hali na uangalizi kwa nyumba za uangalizi. 3. Ubebaji wa kuni na mafuta mengine. 4. Utoaji ulinzi. (b) Huduma ya Mgahawa na Hoteli 1. Usafishaji madirisha. 2. Uoshaji mashuka na uwekaji fanicha maeneo ya nje. 3. Kubeba maji. 4. Kutandika kitanda. 5. Kuchukua kuni. 6. Upikaji chakula (vyakula vya magenge ya mitaani) 7. Usafishaji bwawa na kuogelea. 8. Uoshaji wa idadi kubwa ya vyombo. (c) Huduma za Jamii 1. Washona viatu. 2. Matengenezo ya umeme 3. Matengenezo ya mashine 4. Upakaji rangi. 5. Uzoaji taka 6. Maduka ya kufulia nguo. 7. Saluni za utengenezaji nywele na urembo 8. Maduka ya kunyoa nywele. 9. Uuzaji maji. 10. Uendeshaji mitambo ya kuchimbia. 11. Uuzaji vyakula mitaani. 12. Uombaji au kutumia watoto kuomba mitaani. F: SEKTA YA BIASHARA 1. Ubebaji na uuzaji bidhaa mitaani. 2. Uuzaji wa picha za ngono. 15 G: H: Kanuni za Ajira za Watoto SEKTA YA USAFIRI 1. Vituo vya huduma. 2. Ubebaji mizigo. 3. Upakiaji bidhaa kwenye magari. SEKTA NYINGINE 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. Useremala na karakana ya vitu vya kudumu. Uchakataji wa pamba katika kinu na utengenezaji wa bidhaa za soksi na fulana. Utengenezaji wa dawa za kusafishia na sabuni. Matanuru ya chokaa na kutengeneza chokaa. Viwanda vya kutengeneza kitani na utengenezaji wa makumbi ya nazi. Utengenezaji na uzalishaji saruji. Ukataji vipande risasi. Utengenezaji wa bidhaa za simenti. Utengenezaji zulia na magodoro. Upakaji rangi nguo na batiki. Vitanda vya mfumi vya mikono na vinavyojiendesha vyenyewe. Utengenezaji kemikali. Kukalibu madini/Utengenezaji Chupa/bilauri Utengenezaji Asidi. Uwekaji madaraja na kubangua korosho na uchakataji. Kutengeneza na ushikaji wa dawa za kuulia wadudu. Kutengeneza terazo na ufinyanzi. Kucheza kwa malipo kwenye baa, hoteli na klabu za usiku. Dar es Salaam, 27 Machi, 2012 HADJI H. MPONDA, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii 16
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
KANUNI ZA AJIRA ZA WATOTO ZA MWAKA 2012
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in