KANUNI ZA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ZA MWAKA 2016
These regulations may be called the Public Service Employment Secretariat Operations Regulations of 2016.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- KANUNI ZA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ZA MWAKA 2016
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
These regulations may be called the Public Service Employment Secretariat Operations Regulations of 2016. Kanuni hizi zinatumiwa na Sekretarieti ya Ajira kuendesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma, na zinawahusu waajiri, watumishi wa umma, waombaji kazi na wadau mbalimbali wa ajira. This provision defines several terms used in the regulations. Sekretarieti lazima itekeleze majukumu ya kusaidia ajira katika Utumishi wa Umma, ikiwemo kutafuta wataalam, kuandaa orodha za wahitimu na wataalam, kutangaza nafasi wazi, kushirikisha wataalam wa usaili, kutoa ushauri kwa waajiri, na kufanya kazi nyingine inayoelekezwa na Waziri. Secretariat members must carry out specified Secretariat duties, including reviewing and approving work plans, reports, applicant lists, interview results, recruitment procedures, and giving advice after receiving feedback from employers.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of KANUNI ZA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ZA MWAKA 2016
Showing 39 of 39
- 1
AI-assisted research summary: These regulations may be called the Public Service Employment Secretariat Operations Regulations of 2016.
1. Kanuni hizi zinaweza kuitwa Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma za mwaka 2016. - 2
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinatumiwa na Sekretarieti ya Ajira kuendesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma, na zinawahusu waajiri, watumishi wa umma, waombaji kazi na wadau mbalimbali wa ajira.
2. Kanuni hizi zitatumiwa na Sekretarieti ya Ajira kuendesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma na zitawahusu- (a) Waajiri; (b) Watumishi wa Umma; (c) Waombaji kazi pamoja na (d) Wadau mbalimbali wa ajira. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: This provision defines several terms used in the regulations.
3. Katika Kanuni hizi isipokuwa kama mkutadha imetamkwa vinginevyo- “Katibu” maana yake ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma; “Kanzidata” inamaanisha taarifa mbalimbali za mchakato wa ajira zilizohifadhiwa kwenye kompyuta; “Mamlaka ya Nidhamu” inamaanisha Mamlaka ya Nidhamu kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Utumishi wa Umma; 4 Sura ya 298 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) Sura ya 298 Sura ya 298 Sura ya 298 Majukumu ya Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma “Mwajiri” inamaanisha Mamlaka za Ajira kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Utumishi wa Umma; “Sekretarieti” inamaanisha Sekretarieti ya Ajira kama katika Utumishi wa Umma ilivyoainishwa katika Sheria ya Utumishi wa Umma; “Wajumbe wa Sekretarieti” inamaanisha Wajumbe wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kama ilivyoainishwa katika Kifungu (29) (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma. SEHEMU YA PILI MAJUKUMU
Part
SEHEMU YA PILI
- 4
AI-assisted research summary: Sekretarieti lazima itekeleze majukumu ya kusaidia ajira katika Utumishi wa Umma, ikiwemo kutafuta wataalam, kuandaa orodha za wahitimu na wataalam, kutangaza nafasi wazi, kushirikisha wataalam wa usaili, kutoa ushauri kwa waajiri, na kufanya kazi nyingine inayoelekezwa na Waziri.
4. Sekretarieti itatekeleza majukumu yafuatayo kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Utumishi wa Umma- (a) kutafuta wataalam wenye ujuzi maalum na kuandaa kanzidata za wataalam hao ili kurahisisha utaratibu wa kuwaajiri pindi wanapohitajika; (b) kuandaa orodha ya wahitimu wa Vyuo na Wataalam Weledi Vikuu (Professionals) kwa madhumuni ya kurahisisha rejea na ujazaji wa nafasi wazi za ajira katika Utumishi wa Umma; (c) kutangaza kazi nafasi wazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma; maalum wataalam (Appropriate experts) kwa ajili ya kufanya usaili kulingana na mahitaji; (d) kuhusisha za 5 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) (e) kutoa ushauri kwa Waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na ajira; na (f) kufanya yoyote inayoendana na majukumu yake kadri itakavyoelekezwa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma. nyingine kazi Majukumu ya Wajumbe wa Sekretarieti - 5 Verify source ↗
Majukumu ya Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma
AI-assisted research summary: Secretariat members must carry out specified Secretariat duties, including reviewing and approving work plans, reports, applicant lists, interview results, recruitment procedures, and giving advice after receiving feedback from employers.
5. Wajumbe wa Sekretarieti watatekeleza majukumu yafuatayo- (a) Kupitia na kuidhinisha mpango kazi wa Sekretarieti; (b) Kupitia na kuidhinisha taarifa ya utekelezaji wa kazi za Sekretarieti; (c) Kupitia na kuidhinisha orodha ya waombaji wa kazi; (d) Kujadili na kuidhinisha matokeo ya usaili; (e) Kupitia za taratibu kuwapata watumishi wapya katika Utumishi wa Umma ili kuhakikisha mchakato wa Ajira unafanyika kwa haki, uwazi, ufanisi na gharama nafuu; na (f) Kupata mrejesho wa mapokezi ya waajiriwa wapya kutoka kwa waajiri na kushauri ipasavyo. SEHEMU YA TATU LUGHA Lugha ya kikao
Part
SEHEMU YA TATU
- 6
AI-assisted research summary: Lugha rasmi ya kikao cha Wajumbe wa Sekretarieti na Menejimenti ya Sekretarieti ni Kiswahili.
6. Lugha rasmi ya kikao cha Wajumbe wa Sekretarieti na Menejimenti ya Sekretarieti itakuwa Kiswahili. 6 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) Lugha ya Usaili - 7 Verify source ↗
Lugha ya Kikao
AI-assisted research summary: Usaili unatazamiwa kufanywa kwa Kiingereza, na Kiswahili hutumika kwa kada za masharti ya kawaida; Katibu pia anaweza kuridhia lugha nyingine au lugha ya alama pale panapokuwa na mahitaji maalum.
7.-(1) Kiingereza. Lugha rasmi ya usaili itakuwa (2) Lugha ya Kiswahili itatumika katika kada za masharti ya kawaida. (3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1) na (2), pale ambapo patakuwa na mahitaji maalum, Katibu anaweza kuridhia usaili ufanyike kwa- (a) lugha ya Kiswahili kwa waombaji wa nafasi zisizokuwa za masharti ya kawaida; (b) lugha ya alama; na (c) lugha zaidi ya zilizoainishwa katika kifungu cha 7(1), 7(2) na 7(3) pae itakapolazimu. (4) Lugha ya alama itatumika kwa watu wenye mahitaji maalum. (5) Pale ambapo patakuwa na mahitaji maalum, Katibu anaweza kuridhia usaili ufanyike kwa lugha zaidi ya zilizoainishwa katika Ibara ya 7(1), 7(2) na 7(3). SEHEMU YA NNE MCHAKATO WA AJIRA UKanuni wa kuwapata waombaji kazi
Part
SEHEMU YA NNE
- 8
AI-assisted research summary: Waajiri must plan for vacant jobs in their annual budgets and, after budget approval, submit employment permits and proposed staffing timings to the Secretariat.
8.-(1) Waombaji wa fursa za ajira wataajiriwa katika Utumishi wa Umma kwa kuzingatia sifa, taaluma, ushindani, uwazi na usawa kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni na taratibu zinazohusu Ajira katika Utumishi wa Umma. (2) Waajiri wanao wajibu wa kutenga nafasi wazi za ajira katika bajeti zao kila mwaka kulingana na mahitaji. (3) Katibu atahakikisha kuwa anapata orodha ya nafasi zote wazi za ajira katika Utumishi 7 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) wa Umma toka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma mwanzoni mwa mwezi Aprili ya kila mwaka, kwa ajili ya maandalizi ya bajeti ya mwaka wa fedha unaofuata. (4) Kila baada ya bajeti kupitishwa na Bunge, Waajiri wanapaswa kuwasilisha vibali vya ajira kwenye Sekretarieti pamoja na mapendekezo ya muda muafaka ambao wangependa wapelekewe watumishi wapya. (5) Katibu ataweka mpango wa kuwapeleka waombaji kazi waliofaulu usaili kwa waajiri kwa kuzingatia mahitaji ya waajiri pamoja na kibali cha ajira kilichotolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. (6) Kila mwaka Sekretarieti itaweka utaratibu wa kukutana na Waajiri, Viongozi wa ili Vyuo, Wanavyuo na Wahitimu wa Vyuo ajira za kuhusu kuwafahamisha zinazopatikana katika Utumishi wa Umma. fursa (7) Endapo Sekretarieti imetumia taratibu zilizoainishwa katika Kanuni hizi za kuwapata waombaji kazi wenye sifa na kushindikana, Katibu kwa kushirikiana na Mwajiri watatafuta mtu mwenye sifa kwa kuwasiliana naye moja kwa moja na hatua za kukamilisha ajira au uteuzi wake zitafanyika. Matangazo ya nafasi wazi za kazi - 9
AI-assisted research summary: Maombi ya kazi lazima yawasilishwe ndani ya siku 14 tangu tangazo la kwanza, kwa posta au kwa njia ya kielektroniki, na mtendaji wa Sekretarieti haruhusiwi kupokea maombi nje ya utaratibu uliowekwa.
9.-(1) Matangazo ya nafasi za kazi yatatolewa mara tatu kwa mwaka au zaidi pale itakapohitajika. (2) Matangazo ya nafasi wazi za kazi yatatolewa katika tovuti ya Sekretarieti au kupitia 8 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) Redio, Runinga na Magazeti. (3) Waombaji watapewa 14 kuwasilisha maombi yao ya kazi kuanzia tarehe ya kwanza ya kutolewa kwa tangazo. siku (4) Barua za maombi ya kazi zitawasilishwa itakayooneshwa kwenye kwa kutumia anuani tangazo la kazi. (5) Uwasilishaji wa maombi ya ajira utafanyika kwa njia ya posta au kwa njia ya kielektroniki na si vinginevyo. (6) Waombaji wenye mahitaji maalum kutokana na maumbile yao watatakiwa kueleza katika barua zao za maombi ya kazi. (7) Baada ya kumalizika kwa muda wa kupokea barua za maombi ya kazi, Sekretarieti itaandaa orodha itakayowezesha kuwaita waombaji kazi waliokidhi vigezo kwa ajili ya usaili na kutoa taarifa kwa wale ambao hawakufanikiwa. (8) Mtendaji yeyote wa Sekretarieti hataruhusiwa kupokea barua za maombi ya kazi tofauti na utaratibu ulioelekezwa katika Ibara ya 9(4). (9) Waombaji kazi waliokidhi vigezo wataitwa kwenye usaili kwa kutumia njia mbalimbali za mawasiliano. - 10 Verify source ↗
11. Mitihani
AI-assisted research summary: Katibu lazima aunde kamati ya muda ya watu 3 hadi 5 kutoka Sekretarieti kwa ajili ya kuandaa orodha fupi ya waombaji wa kazi.
10.-(1) Katibu ataunda Kamati ya muda ya watu wasiozidi watano na wasiopungua watatu kutoka miongoni mwa watendaji wa Sekretarieti kwa ajili ya uandaaji wa orodha fupi ya waombaji wa kazi. (2) Kamati hiyo ya muda inaweza pia kujumuisha Mtumishi wa Umma ambaye siyo 9 Kamati ya muda Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) mtendaji wa Sekretarieti ili kupata utaalam na uzoefu maalum ambao hautakuwepo miongoni mwa watendaji wa Sekretarieti. (3) Orodha ya waombaji kazi itaandaliwa kwa kuzingatia sifa za mtu anayehitajika kama zilivyoainishwa katika Miundo ya Utumishi wa Umma na tangazo la kazi. Mitihani - 11 Verify source ↗
Mitihani
AI-assisted research summary: Sekretarieti lazima iandae mitihani ya kuandika na ya vitendo.
11. Sekretarieti itaandaa mitihani ya aina mbili ambayo ni ya kuandika na vitendo, na mitihani katika mazingira yafuatayo: itafanyika hiyo (a) Mtihani wa kuandika utafanyika ili kuchuja waombaji wenye sifa, na pia pale ambapo idadi ya waombaji ni kubwa kuliko fursa zilizopo; (b) Mtihani wa vitendo utafanyika kwa baadhi ya fani kama vile madereva, makatibu mahsusi, wataalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano na nyingine zenye mahitaji kama hayo, ili kupima uwezo na ujuzi wa utendaji kazi katika fani husika. Usaili - 12 Verify source ↗
13. Majopo ya Usaili
AI-assisted research summary: Sekretarieti lazima iandae na kufanya usaili wa ana kwa ana au wa vitendo katika hali zilizoelezwa.
12. Sekretarieti itaandaa usaili wa ana kwa ana (mahojiano) au wa vitendo katika mazingira yafuatayo: (a) Usaili wa ana kwa ana utafanyika kwa juu waombaji waliopata alama za miongoni mwa waliofaulu mtihani wa kuandika na pale ambapo idadi ya waombaji wenye sifa italingana na fursa zilizopo; 10 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) Majopo ya Usaili (b) Usaili wa ana kwa ana na wa vitendo utafanyika kwa waombaji wote wenye sifa wa fani zenye mahitaji kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 11(b) ya Kanuni hizi. - 13 Verify source ↗
Majopo ya Usaili
AI-assisted research summary: This section sets who may form interview panels, who may not sit on them, and the minimum and maximum panel size.
13.-(1) Majopo ya usaili yatapendekezwa na Mkuu wa Idara ya Ajira katika Sekretarieti na kuidhinishwa na Katibu. (2) Wajumbe wa Sekretarieti hawaruhusiwi kuwa Wajumbe katika majopo ya usaili. (3) Majopo ya usaili yataundwa na Watendaji wa Sekretarieti na Wataalam wa ndani ya Utumishi wa Umma. (4) Sekretarieti inaweza kutumia wataalam maalum walio nje ya Utumishi wa Umma (Appropriate experts) endapo atakosekana mtaalam wa aina hiyo katika Utumishi wa Umma ambao watapewa miongozo ya jinsi ya kuendesha usaili kabla ya siku ya usaili na kuchagua mwenyekiti wa jopo kabla ya kuanza usaili. (5) Katibu anaweza kuridhia uundwaji wa jopo maalum endapo patakuwa na sababu za msingi za kufanya hivyo. (6) Jopo la usaili litakuwa na Wajumbe wasiozidi watano na wasiopungua watatu kwa kuzingatia jinsi. (7) Katika kila jopo la usaili litakaloundwa, Katibu wa jopo atakuwa ni mmoja wa Watendaji wa Sekretarieti na endapo kutatokea upungufu wa Makatibu wa majopo, Katibu atatumia Watendaji 11 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) Namna ya uendeshaji wa usaili Uwasilishaji wa matokeo ya usaili wengine wenye sifa waliopo katika Utumishi wa Umma. - 14
AI-assisted research summary: The Secretariat must prepare special interview guidelines, panel secretaries must explain them to members before interviews, interview panel decisions are based on the majority of marks, each panel must publish interview results showing each applicant’s pass level, and panel secretaries must send a report to the Head of the Employment Department in the Secretariat.
14.-(1) Sekretarieti itaandaa miongozo maalum itakayotumika wakati wa usaili na Makatibu wa majopo watakuwa na jukumu la kutafsiri miongozo hiyo kwa wajumbe kabla ya kuanza usaili. (2) Wajumbe wa Sekretarieti wanaruhusiwa kuingia kwenye cha usaili kama chumba watazamaji ili kujiridhisha na uendeshaji wake, endapo watahitaji kufanya hivyo. (3) Uamuzi katika majopo ya usaili utafikiwa kwa wingi wa alama atakazopata msailiwa. (4) Kila jopo la usaili litatoa matokeo ya usaili yakionesha kiwango cha ufaulu kwa kila mwombaji. (5) Makatibu wa majopo ya usaili watawasilisha taarifa ya jinsi usaili ulivyoendeshwa na matokeo ya usaili kwa Mkuu wa Idara ya Ajira katika Sekretarieti. - 15
AI-assisted research summary: Idara ya Ajira lazima ijumuishe matokeo ya usaili na kuyawasilisha kwa Katibu; Katibu lazima ayapeleke kwenye kikao cha Wajumbe wa Sekretarieti kwa idhini; kikao hicho lazima kithibitishe matokeo bila kuyabadilisha, na kikibaini upungufu kiagize usaili urudiwe.
15.-(1) Idara ya Ajira itaunganisha matokeo yote ya usaili kutoka katika kila jopo na kuyawasilisha kwa Katibu ambaye atayawasilisha kwenye kikao cha Wajumbe wa Sekretarieti kwa ajili ya kupata idhini. (2) Katibu atawasilisha kwenye kikao cha Wajumbe wa Sekretarieti taarifa na matokeo ya usaili ili yaidhinishwe kabla ya waombaji waliofaulu kupelekwa kwa waajiri. (3) Kikao cha Wajumbe wa Sekretarieti kitaidhinisha matokeo ya usaili baada ya 12 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) kujiridhisha kuhusu uzingatiaji wa Kanuni, uwazi na utaalam katika uendeshaji wa usaili. (4) Kikao cha Wajumbe wa Sekretarieti hakitabadilisha matokeo ya usaili na endapo kitabaini upungufu kitaelekeza mchakato wa usaili kurudiwa. Alama za ufaulu - 16
AI-assisted research summary: This provision sets interview pass marks at 60%, 70%, and 50% for different cadres.
16.-(1) Alama za Ufaulu (Passmark) katika usaili zitakuwa kama ifuatavyo- (a) Kada ya Watendaji Wakuu (Wakuu wa Taasisi, Wakuu wa Vyuo, Manaibu Wakuu wa Vyuo, Wakuu wa Idara na Vitengo) ni asilimia sitini (60), na utaratibu huu utazihusu Taasisi zilizo chini ya Baraza la Ufundi la Taifa (NACTE); (b) Kada za Wahadhiri na Wakufunzi ni asilimia sabini (70); na (c) Kada za madaraja ya kuingilia kazini na madaraja ambayo mengineyo hayakutajwa katika Ibara ya 16(1) (a) na (b) ya Kanuni hizi alama ya ufaulu ni asilimia hamsini (50). Kupangiwa kituo cha kazi - 17
AI-assisted research summary: The Secretary assigns successful applicants to work stations based on employers’ submitted employment permit requirements, and successful applicants must report to the assigned station within 14 days of receiving the placement letter unless they have a valid reason.
17.-(1) Katibu atawapangia vituo vya kazi Waombaji walioshinda usaili kwa kuzingatia mahitaji ya vibali vya ajira vilivyowasilishwa na Waajiri. (2) Kwa wale waombaji waliopata alama zinazolingana, utaratibu ufuatao utazingatiwa- (i) Iwapo miongoni mwao kuna mtu mwenye ulemavu atapewa kipaumbele kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kazi; 13 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) (ii) Iwapo kutakuwa na waombaji wa jinsi mbili tofauti, mwanamke atapewa kipaumbele; (iii) Iwapo waombaji ni wa jinsi moja, atapewa umri mkubwa mwenye kipaumbele. (3) Mwombaji aliyefaulu usaili anatakiwa kuripoti katika kituo chake cha kazi ndani ya siku kumi na nne (14) tangu tarehe ya kupokea barua ya kupangiwa kituo cha kazi na endapo mwombaji hataripoti ndani ya kipindi hicho bila ya kuwa na sababu za msingi itahesabika kuwa nafasi hiyo iko wazi. (4) Mwombaji aliyepangiwa kituo cha kazi atahesabika kama mwajiriwa kamili mara baada ya kukamilisha taratibu za ajira. (5) lolote Endapo litatokea suala la kiutumishi au kibinafsi kwa mwombaji kazi ambaye alikwishapangiwa kituo cha kazi na kukamilisha taratibu zote za ajira, Sekretarieti haitahusika na taratibu zozote za kikazi zaidi ya kuhifadhi kumbukumbu zake. Kanzidata - 18
AI-assisted research summary: Sekretarieti lazima iandae makanzidata matatu: ya wahitimu na wataalam, ya waliofaulu usaili, na ya waliopangiwa vituo vya kazi.
18.-(1) Sekretarieti itaandaa kanzidata za aina tatu (3) ambazo ni- (a) wahitimu wa Vyuo na Wataalam; (b) waliofaulu usaili; na (c) waliopangiwa vituo vya kazi. (2) Kanzidata ya Wahitimu wa Vyuo na Wataalam itahusisha makundi ya aina mbili ambayo ni- (a) Wahitimu wa Vyuo; na (b) Wataalam wenye ujuzi maalum. 14 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) Kanzidata ya wahitimu wa vyuo - 19
AI-assisted research summary: The graduates database must keep a list of graduates with specified personal details. The Secretariat must contact universities and the higher education ministry each academic year to obtain lists of Tanzanian graduates from inside and outside the country.
19.-(1) Kanzidata ya wahitimu wa Vyuo (Graduates)itatunza orodha ya wahitimu wa vyuo ikionyesha jina, jinsi, picha ya mhitimu, namba ya cheti cha kuhitimu na anuani ya mhitimu. (2) Sekretarieti itawasiliana na Wakuu wa Vyuo na Tume ya Vyuo Vikuu kila mwisho wa mwaka wa masomo pamoja na Wizara yenye dhamana ya Elimu ya Juu ili kupata orodha ya Watanzania waliohitimu mafunzo ndani na nje ya nchi katika utaratibu utakaowekwa na Sekretarieti. (3) Kuwepo kwa orodha ya wahitimu wa vyuo katika kanzidata ya Sekretarieti hakutaondoa uhitaji wa kufanyiwa usaili ili kuajiriwa katika Utumishi wa Umma. Kanzidata ya wataalam wenye ujuzi maalum - 20
AI-assisted research summary: Sekretarieti lazima ipate orodha ya wataalam wanaoweza kuajiriwa, na wataalamu wenye ujuzi maalum wanaweza kuwasilisha taarifa zao kwa Sekretarieti ili zihifadhiwe kwenye kanzidata.
20.-(1) Kanzidata ya wataalam wenye ujuzi maalum itapatikana kama ifuatavyo: (a) Sekretarieti itapata orodha ya wataalam wanaoweza kuajiriwa katika Utumishi wa Umma kutoka katika Bodi za Kitaaluma, Waajiri Taasisi mbalimbali; na (b) Wataalamu wenye ujuzi maalum wanaruhusiwa kuwasilisha taarifa zao katika Sekretarieti ya kuhifadhiwa katika kanzidata ili Serikali iweze kutumia taaluma au ujuzi wao pale inapohitajika. kwa ajili Kanzidata ya waliofaulu usaili - 21
AI-assisted research summary: Katibu must keep the remaining successful applicants’ list in a database, and the Secretariat must use that list to fill vacancies, rank applicants by exam results, and advertise/interview if the list is exhausted or lacks suitable candidates.
21.-(1) Baada ya waombaji waliofaulu usaili kuwapangia vituo vya kazi, orodha itakayobaki itatunzwa na Katibu katika kanzidata ili pale itakapotokea fursa ya ajira orodha hiyo iweze kutumika. 15 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) (2) Orodha ya waombaji walioko kwenye kanzidata itatumika kujaza nafasi wazi kulingana na mahitaji ya waajiri. Hata hivyo, wakati wa upangaji, Katibu atazingatia mpangilio wa matokeo ya alama za ufaulu wa mwombaji kwa aliyepata alama za juu zaidi ya wengine kufikiriwa kwanza. (3) Sekretarieti itatangaza nafasi wazi za ajira na kufanya usaili endapo orodha iliyotunzwa imekwisha au haina katika kanzidata mtumishi mwenye utaalam au sifa zinazohitajika na Mwajiri. itakuwa (4) iliyotajwa Endapo katika orodha kwenye Ibara ya 21(2) kutakuwa na waombaji waliopata utaratibu ulioainishwa katika Ibara ya 14(1) utazingatiwa. zinazolingana, alama Kanzidata ya waliopangiwa na vituo vya kazi Kushindwa kuripoti kituo cha kazi (5) Orodha ya kanzidata itadumu kwa kipindi cha miezi sita (6) tangu kuidhinishwa kwa matokeo na Wajumbe wa Sekretarieti. - 22
AI-assisted research summary: Sekretarieti lazima iendelee kuboresha kanzidata ya watumishi waliopangiwa vituo vya kazi kwa ajili ya kumbukumbu za kiutumishi.
22. Sekretarieti itaendelea kuboresha kanzidata ya watumishi waliopangiwa vituo vya kazi kwa ajili ya kumbukumbu za kiutumishi. - 23 Verify source ↗
24. Waombaji wanaoweza kufikirika
AI-assisted research summary: Mwombaji asiyeripoti katika kituo cha kazi alichopangiwa bila sababu za msingi anaweza kupangiwa tena kituo kingine, na pia asizingatiwe tena akiomba kazi yenye sifa zilezile katika Utumishi wa Umma.
23. Mwombaji ambaye hataripoti katika kituo cha kazi alichopangiwa bila kutoa sababu za msingi hatapangiwa tena kituo kingine cha kazi. Vilevile, hatafikiriwa kwa mara nyingine pindi atakapowasilisha maombi ya kazi yenye sifa zile zile za kazi aliyoiomba awali katika Utumishi wa Umma. Waombaji wanaoweza kufikiriwa - 24 Verify source ↗
Waombaji wanaoweza kufikirika
AI-assisted research summary: Applicants mentioned in Article 23 may be considered if they have qualifications above the jobs they originally applied for.
24. Endapo waombaji kazi waliotajwa katika Ibara ya 23 watapata sifa za juu ya kazi walizoomba awali wataweza kufikiriwa. 16 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) SEHEMU YA TANO UENDESHAJI WA VIKAO Kikao cha kawaida
Part
SEHEMU YA TANO
- 25
AI-assisted research summary: Secretariat members must convene a regular meeting 4 times a year.
25. Kikao cha kawaida cha Wajumbe wa Sekretarieti kitaitishwa mara 4 kwa mwaka na kitatoa uamuzi katika masuala yafuatayo- (a) Mpango Kazi wa Sekretarieti; (b) Taarifa ya utekelezaji wa kazi za Sekretarieti; (c) Kupitia na kuidhinisha orodha ya waombaji wa kazi; (d) Matokeo ya usaili; na (e) Masuala mengine ambayo yatahitaji idhini ya Wajumbe wa Sekretarieti. Kikao cha dharura - 26
AI-assisted research summary: Sekretarieti inaweza kufanya kikao cha dharura ikiwa Mwenyekiti akishauriana na Katibu ataona kuna haja, au theluthi mbili ya Wajumbe wataomba, au Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma ataelekeza hivyo.
26. Sekretarieti inaweza kuwa na kikao cha dharura katika mazingira yafuatayo- (a) Mwenyekiti baada ya kushauriana na Katibu ataona kuna haja ya kuwa na kikao cha dharura; (b) theluthi mbili ya Wajumbe watataka ya ufanyike baada mkutano huo kushauriana na Katibu; na Uendeshwaji wa kikao cha Sekretarieti (c) Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma ataelekeza hivyo. - 27
AI-assisted research summary: Vikao vya Sekretarieti vinaongozwa na Mwenyekiti; akihudhuria akiwa hayupo, Makamu Mwenyekiti huongoza, na wote wakikosekana wajumbe humchagua mwenyekiti wa muda. Kikao pia hufanyika tu iwapo akidi ni wajumbe watano pamoja na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti.
27.-(1) Vikao vyote vya Sekretarieti vitaendeshwa na Mwenyekiti na endapo Mwenyekiti hatakuwepo, kikao kitaendeshwa na Makamu Mwenyekiti. (2) Pale ambapo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hawatakuwepo, Wajumbe watamchagua Mwenyekiti wa muda miongoni mwao ili kuendesha kikao. 17 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) Namna ya kufikia uamuzi wakati wa kikao Usambazaji wa nyaraka na matumizi yake Kikao cha menejimenti (3) Kikao cha Sekretarieti kitafanyika pale tu akidi (Quorum) itafikia Wajumbe watano akiwemo Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti. - 28
AI-assisted research summary: During a Secretariat meeting, the decision should be reached by agreement; if agreement is not reached, voting is used, and a majority of votes decides. If votes are tied, the Chair has a veto vote.
28.-(1) Ili kufikia uamuzi wakati wa kikao cha Sekretarieti, njia ya makubaliano itatumika na pale ambapo uamuzi hautaafikiwa kwa makubaliano, njia ya kura itatumika. (2) Kigezo cha kufikia uamuzi kitategemea wingi wa kura. (3) Na endapo kura zitalingana Mwenyekiti atakuwa na kura ya turufu. - 29
AI-assisted research summary: Notisi za kikao cha kawaida cha Sekretarieti zinapaswa kusambazwa siku 7 kabla ya kikao; nyaraka za kikao cha dharura hutolewa wakati wa kikao; na Katibu hukusanya na kuhifadhi nyaraka baada ya kikao.
29.-(1) Notisi kwa ajili ya kikao cha kawaida cha Sekretarieti zitasambazwa siku saba (7) kabla ya kikao na endapo itatokea dharura usambazaji wa notisi utategemea hali halisi ya suala husika. (2) Nyaraka kwa ajili ya kikao cha dharura zitagawiwa wakati wa kikao. (3) Nyaraka zote za kikao ni mali ya Sekretarieti, hivyo mara baada ya kikao kumalizika Katibu atazikusanya na kuzihifadhi. (4) Nyaraka zote zinazohusu kikao cha Sekretariati ni siri. - 30 Verify source ↗
Kikao cha kawaida
AI-assisted research summary: Sekretarieti ya Menejimenti lazima ikae kikao mara moja kila wiki.
30.-(1) Menejimenti ya Sekretarieti itakuwa na kikao mara moja kila wiki na katika kikao hicho, cha Katibu Menejimenti na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, atakuwa Katibu. atakuwa Mwenyekiti wa kikao (2) Wajumbe wa kikao cha Menejimenti watakuwa- (a) Wakuu wa Idara; (b) Wakuu wa Vitengo; (c) Wakuu wa Sehemu; na 18 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) (d) Wale watendaji wanaoweza kuingia kwa nafasi zao kwa ridhaa ya Katibu. SEHEMU YA SITA WAJIBU WA MWAJIRI NA MWOMBAJI WA KAZI Wajibu wa Mwajiri
Part
SEHEMU YA SITA
- 31 Verify source ↗
Wajibu wa Mwajiri
AI-assisted research summary: Mwajiri lazima azingatie sheria na miongozo ya ajira ya utumishi wa umma na akamilishe hatua za ajira zinazohitajika.
31. Mwajiri ana wajibu wa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni, taratibu na Miongozo mbalimbali inayosimamia ajira katika Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na- (a) kuainisha na kutenga nafasi wazi za ajira katika bajeti ya mwaka husika; (b) kuomba kibali cha ajira kutoka mamlaka husika; (c) kuwasilisha Sekretarieti kibali cha ajira na sifa zinazohitajika kwa nafasi husika; na (d) kukamilisha Kanuni za ajira baada ya Sekretarieti kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi waliofaulu usaili. Wajibu wa mwombaji wa kazi katika Utumishi wa Umma. - 32 Verify source ↗
Wajibu wa mwombaji wa kazi katika Utumishi wa Umma
AI-assisted research summary: Mwombaji wa kazi lazima azingatie masharti ya tangazo la kazi na aambatishe taarifa na nyaraka zilizoombwa; mtumishi wa umma wa daraja linalolingana katika ofisi nyingine anatakiwa kupitisha maombi yake kwa mwajiri wake.
32.-(1) Mwombaji wa kazi anapaswa kuzingatia masharti yafuatayo wakati na kuomba nafasi za kazi zilizotangazwa pamoja na masharti yaliyoainishwa katika tangazo- (a) wasifu wenye wadhamini wasiopungua watatu ukionyesha anuani zao na mahali walipo; (b) nakala za vyeti halali vya kuhitimu mafunzo; (c) nakala ya cheti halali cha kuzaliwa; (d) picha ndogo (Passport size); (e) anuani/simu/barua pepe/nukushi; (f) umri ulioainishwa katika tangazo; (g) tarehe ya mwisho ya kuwasilisha barua 19 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) ya maombi ya kazi kwa mujibu wa tangazo. haruhusiwi (2) Mwombaji ambaye tayari ni mtumishi wa umma daraja kuomba linalolingana na alilonalo kwenye ofisi nyingine ya Serikali na anapaswa kupitisha barua ya maombi kwa mwajiri wake. kazi ya Udanganyifu (3) Mwombaji ambaye hatazingatia masharti ya jumla ya tangazo la kazi, hatafikiriwa nafasi aliyoiomba. (4) Mwombaji atakayewasilisha taarifa za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria. SEHEMU YA SABA MENGINEYO
Part
SEHEMU YA SABA
- 33
AI-assisted research summary: Kama mwombaji au mhusika akibainika kufanya udanganyifu wakati wa usaili, anaondolewa kwenye usaili na hatua za kisheria huchukuliwa.
33.-(1) Endapo itabainika kuwa msailiwa amefanya udanganyifu wowote na kwa njia yoyote ile wakati wa usaili ataondolewa kwenye zoezi la usaili na kuchukuliwa hatua za kisheria. (2) Tukio la udanganyifu likibainika aidha baada ya matokeo ya usaili au baada ya kupangiwa kituo cha kazi , ajira ya mhusika itasitishwa na hatua za kisheria zitachukuliwa na Mamlaka yake ya Nidhamu. Sifa za Watendaji wa Sekretarieti - 34 Verify source ↗
35. Mgongano wa kimaslahi
AI-assisted research summary: Sekretarieti inapaswa kuwa na watendaji wenye uadilifu, bidii, ubunifu, na motisha.
34. Sekretarieti itapaswa kuwa na watendaji ambao ni waadilifu, wachapakazi, wabunifu, na wenye motisha. Mgongano wa kimaslahi - 35 Verify source ↗
Mgongano wa kimaslahi
AI-assisted research summary: Mjumbe wa jopo la usaili mwenye uhusiano wa karibu na msailiwa lazima auweke wazi, na anaweza kuhitajika kujiondoa wakati wa usaili ikiwa uwepo wake utaathiri maamuzi.
35.-(1) Ikitokea mmoja wa wajumbe wa jopo la usaili ana uhusiano wa karibu na msailiwa, atapaswa kuweka wazi uhusiano huo kwa wajumbe ili waweze kupima kama utaathiri maamuzi na 20 Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) endapo Wajumbe wataona kuwa uwepo wake utaleta athari itabidi ajiondoe wakati msailiwa huyo anapohojiwa. (2) Pale itakapobainika ya kwamba kuwa mjumbe wa jopo alikuwa na uhusiano na msailiwa na hakuliweka wazi msailiwa ataondolewa katika orodha ya ushindani. (3) Mjumbe wa jopo ambaye alikuwa na uhusiano na msailiwa na hakuliweka wazi mamlaka yake ya Nidhamu itashauriwa kumchukulia hatua zinazostahili. - 36 Verify source ↗
Mrejesho wa majukumu ya Sekretarieti
AI-assisted research summary: Sekretarieti lazima ipange mikutano ya kila mwaka na waajiri na pia na wakuu wa vyuo vikuu/taasisi za elimu ya juu ili kupata mrejesho na kuboresha ajira na mitaala.
36.-(1) Sekretarieti itaweka utaratibu wa kukutana na waajiri mara moja kwa mwaka ili kupata mrejesho wa kazi zake na ubora wa watumishi wanaopelekwa kwa waajiri, kwa lengo la kupata maoni ili kuboresha mchakato wa ajira. (2) Sekretarieti itakuwa inakutana na Wakuu wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu mara moja kwa mwaka ili kuwapa mrejesho wa ubora wa wahitimu wa Vyuo vyao kwa lengo la kusaidia kuboresha mitaala yao ili ikidhi matakwa ya soko la ajira. - 37 Verify source ↗
Kumbukumbu za mwombaji kazi
AI-assisted research summary: Interview records tied to job applications are not to be returned to the applicant; they must be kept for 12 months and then destroyed under government document-destruction procedures.
37. Kumbukumbu za usaili zinazohusiana na maombi ya ajira hazitarejeshwa kwa mwombaji kazi bali zitahifadhiwa kwa kipindi cha miezi kumi na mbili (12) kwa ajili ya rejea baada ya kuisha kwa kipindi hicho zitateketezwa kwa kuzingatia utaratibu wa uteketezaji wa nyaraka za Serikali. - 38 Verify source ↗
Mwenendo mbovu wa mtaalam aliyehusishwa katika mchakato wa
AI-assisted research summary: A recruiter-linked expert who breaches the rules or guidance for the recruitment exercise can be removed, and the Secretary must report the matter to the disciplinary authority.
38. Endapo itabainika kuwa mtaalam aliyehusishwa na Sekretarieti katika mchakato wa ajira amehusika kwa namna yoyote ile kwenda kinyume na Kanuni na miongozo ya zoezi husika, 21 Mrejesho wa majukumu ya Sekretarieti Kumbukumbu za mwombaji kazi Mwenendo mbovu wa mtaalam aliyehusishwa katika mchakato wa ajira Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Taarifa ya Kawaida Na. 196 (linaendelea) ataondolewa katika zoezi hilo na Katibu atatoa taarifa kwa Mamlaka yake ya Nidhamu ili achukuliwe hatua stahiki za kinidhamu. Mapitio - 39 Verify source ↗
Mapitio
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinaweza kufanyiwa mapitio pale itakapohitajika.
39. Kanuni hizi zinaweza kufanyiwa mapitio pale itakapohitajika. Dar es Salaam, 23/ 3/ 2015 XAVIER M. DAUDI Katibu Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma 22
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
KANUNI ZA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ZA MWAKA 2016
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in