Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi za Mwaka 2017
These by-laws are titled the Malinyi District Council Environmental Sanitation By-laws, 2017, and they start to apply after publication in the Government Gazette.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi za Mwaka 2017
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
These by-laws are titled the Malinyi District Council Environmental Sanitation By-laws, 2017, and they start to apply after publication in the Government Gazette. These by-laws apply throughout the entire area under the Malinyi District Council’s jurisdiction. This section mainly defines terms used in the by-laws, including the authorized officer, resident, owner, waste, solid waste, and sanitation-related facilities. Kila mtu, taasisi, au asasi lazima kuweka mazingira safi na salama wakati wote na kushiriki shughuli za usafi wa mazingira. Wakazi na wamiliki wa nyumba au viwanja lazima waweke maeneo yao safi, watumie chombo cha kukusanyia taka, wachangie gharama za taka, na washiriki siku ya usafi ya umma inayoitishwa na Halmashauri.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi za Mwaka 2017
Showing 27 of 27
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za (Usafi wa
AI-assisted research summary: These by-laws are titled the Malinyi District Council Environmental Sanitation By-laws, 2017, and they start to apply after publication in the Government Gazette.
1. Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi za Mwaka 2017 na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: These by-laws apply throughout the entire area under the Malinyi District Council’s jurisdiction.
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa
AI-assisted research summary: This section mainly defines terms used in the by-laws, including the authorized officer, resident, owner, waste, solid waste, and sanitation-related facilities.
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote atakayeteuliwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “Afya” maana yake ni hali timilifu ya kimwili, kiakili na kijamii; “Chakula” maana yake ni kitu chochote kinatumika kwa kuliwa na kunywa na binadamu kujumuisha kitu chochote kinachotumika katika matengenezo ya chakula, kitu chochote kinachoongeza ladha ya chakula, au kitu chochote kinachobadili rangi ya chakula isipokuwa madawa; 1 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) “Choo bora” maana yake ni choo chochote cha maji chenye sakafu, banda imara la kudumu, limeezekwa, lina mlango imara, bomba la lenye mfuniko kutolea hewa chafu na kwenye tundu la choo na shimo salama na safi kwa ajili ya kutupa kinyesi na mkojo wa binadamu, lililojengwa kwa vifaa vya kudumu, lenye vipimo vya futi 4 x 3 na kimo cha futi 12 na zaidi; “Choo cha Umma” maana yake ni choo kilichojengwa na Halmashauri au wakala wake kwa matumizi ya umma; “Eneo la wazi” maana yake ni eneo lililoachwa kama eneo la mapumziko kwa umma au viwanja vya michezo au kwa ajili ya shughuli zozote ambazo sio ujenzi wa kitu chochote; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi; “Hati ya usafi” maana yake ni hati itakayotolewa na Afisa Mwidhiniwa inayothibitisha kukaguliwa kwa maeneo yote yaliyotajwa katika Sheria Ndogo hizi kulingana na Kanuni za Afya. “Kaya” maana yake ni familia ya watu akiwemo baba, mama, mtoto au watoto na mtu mwingine yeyote anayeishi na familia hiyo, au watu wanaokaa katika nyumba moja na kuishi kama familia au mtu yeyote anayeishi peke yake katika chumba au nyumba; “Kero au chukizo” maana yake ni kitu chochote ambacho kipo katika hali yoyote iwe kinatumika, kimewekwa, kimejengwa, au ni 2 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) kichafu kiasi cha kusababisha hatari kwa viumbe na maisha ya binadamu, harufu mbaya na kuudhi, kuzaliana kwa wadudu na wanyama hatari kama vile nzi, mende, sisimizi, panya, nyoka, nyuki, kunguni au aviumbe wengine hatari, mlipuko wa magonjwa au kusababisha madhara ya afya kwa binadamu, na viumbe wengine; “Kituo cha taka” maana yake ni kizimba au ghuba ya taka kilichowekwa na Halmashauri kwa madhumuni ya kuweka taka ngumu kabla ya kusafirishwa hadi kwenye dampo la taka ngumu la Halmashauri; “Maji taka” maana yake ni sawa na ile iliyotajwa katika Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 kuwa ni pamoja na taka zinazotokana na kinyesi, mkojo na jasho, uchafu wa majimaji kutoka majumbani, Taasisi, majengo ya biashara na viwandani; “Mimea marefu” maana yake ni mazao au mimea inayozidi sentimita 15 kwenda juu kama vile Mtama, Mahindi, Mbaazi, Uwele na mengine yote yale yanayofanana na hayo isipokuwa miti; “Mkazi” maana yake ni mtu yeyote anayeishi katika eneo la Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri. “Mmiliki” maana yake ni mtu yeyote ambaye ana miliki ardhi, sehemu za starehe, nyumba za kulala wageni, nyumba za kuuzia vyakula, 3 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) kumbi za starehe, mpangaji, wakala wa mpangishaji wa nyumba au jengo na makazi yoyote katika mtaa, endapo mazingira husika ni mtaa au barabara za mtaa; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; Halmashauri Afisa au “Mzalishaji wa taka ngumu” maana yake ni Mtu yeyote, kaya, Taasisi, biashara, kiwanda ambacho katika kufanya zao huzalisha taka; shughuli “Pipa la taka” maana yake ni chombo chochote chenye mfuniko kinachoweza kuhifadhi taka ngumu zinazozalishwa majumbani, sehemu za biashara, maofisini ili zisisambae na kuchafua mazingira; “Taka” maana yake ni sawa na ile iliyotajwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, 2004 kwamba kitu chochote kimiminika, kigumu, gesi na mionzi, kinachotoa harufu mbaya, au kilichohifadhiwa katika mazingira ya hali ya ujazo, uozo au hali nyingine yoyote inayosababisha uharibifu wa mazingira, ambayo inajumuisha taka; “Taka Ngumu” maana yake ni sawa na ile iliyotajwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, ya Mwaka 2004 kuwa ni taka ambazo haziko katika majimaji kutoka majumbani, katika majengo ya biashara, viwandani na kutoka katika shughuli za kilimo, pamoja na taka za vyakula, karatasi plastiki au taka laini zinazotokana na ujenzi au 4 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) ubomoaji majengo utengenezaji bustani na shughuli za uchimbaji madini, mizoga ya wanyama na mabaki ya magari mabovu (scraps); “Taka za Majumbani” maana yake itajumuisha mabaki ya chakula, maganda ya matunda, majivu, kinyesi cha mifugo, taka za bustani, marapurapu ya nguo, karatasi za aina mbalimbali na vitu vingine ambavyo baada ya kuvitumia hutupwa; “Taka za Viwandani” kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004, kuwa ni uchafu unaotokana na uzalishaji viwandani au uchafu usiotokana na uzalishaji viwandani ambao ni chanzo cha nishati, maji, mimea iliyotiwa dawa, au mawasiliano, pamoja na taka nyinginezo ngumu kama zilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, 2004 sehemu ya IX; “Uchafu Hatari” kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Mazingira Na 20 ya mwaka 2004, kuwa ni kitu chochote kigumu, chenye majimaji, gesi taka zitokazo viwandani, au mafuta au machafu, ambayo yanaleta athari za kikemia, kwa binadamu au mazingira; “Uchunguzi wa Afya” maana yake ni hali ya Mtu kupima afya yake kwa kuchukuliwa vipimo vya ndani na nje ya mwili ili kubaini kuwepo kwa vijidudu vya magonjwa vinavyoweza kuleta maambukizi kwa watu wengine; Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Kila mtu, taasisi, au asasi lazima kuweka mazingira safi na salama wakati wote na kushiriki shughuli za usafi wa mazingira.
4. Itakuwa ni wajibu wa kila Mtu, Taasisi au Asasi yeyote kuweka mazingira safi na salama wakati wote na kwa 5 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) Kushiriki shughuli za usafi wa mazingira - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Wakazi na wamiliki wa nyumba au viwanja lazima waweke maeneo yao safi, watumie chombo cha kukusanyia taka, wachangie gharama za taka, na washiriki siku ya usafi ya umma inayoitishwa na Halmashauri.
5. kuhakikisha kwamba- (a) Mazingira yanayozunguka eneo lake la makazi au biashara yanakuwa safi wakati wote; (b) Anaweka na kutumia chombo cha kukusanyia taka za aina zote; (c) Anachangia gharama za uzoaji wa taka kwenye eneo lake; (1) Kila siku ya Jumamosi ya kila wiki au siku nyingine yoyote itakayotangazwa na Halmashauri itakuwa ni siku ya Wananchi kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira kwa umma katika maeneo yote ya mamlaka ya Halmashauri na atakayeshindwa atakuwa ametenda kosa; (2) Kifungu kidogo cha (1) hakiathiri wajibu wa kila Mmiliki wa nyumba au Kiwanja au eneo lolote kufanya usafi katika eneo lake mara kwa mara. Utupaji wa taka - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Halmashauri must encourage and inspect waste disposal infrastructure in residential and business areas, and in densely populated/high-waste areas it must set special waste disposal and collection arrangements.
6. (1) Halmashauri itahamasisha na kukagua kila eneo la Makazi au Biashara limeweka miundo mbinu na vifaa vya kutupia taka; (2) katika maeneo yenye Watu wengi ambapo uzalisha taka uko kwa wingi, Halmashauri itaweka utaratibu maalum wa kutupa na kuzoa taka ambapo wazalisha taka watawajibika kugharamia huduma taka kwa mujibu wa viwango za uzoaji vilivyowekwa na Jedwali la kwanza la Sheria Ndogo hizi. Kutiririsha maji taka - 7 Verify source ↗
Haitaruhusiwa kutitirisha au kuelekeza maji, kutoka
AI-assisted research summary: It is prohibited to discharge or direct water from toilets, bathrooms, car wash areas, or factories into roads, alleys, rivers, water sources, open areas, storm drains, or any place not designated for storing sewage.
7. Haitaruhusiwa kutitirisha au kuelekeza maji, kutoka vyooni, bafuni, karoni, viwandani, kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote isiyotengwa kuhifadhi maji taka. 6 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) Uendeshaji wa viwanda - 8 Verify source ↗
Ni marufuku kuendesha shughuli za karakana, mashine
AI-assisted research summary: The provision forbids operating certain workshop, milling, woodworking, fruit-juice pressing, welding, or other industrial activities that create wastewater, dust, noise, or bad odor in residential areas without following construction procedures.
8. Ni marufuku kuendesha shughuli za karakana, mashine ya kusaga, kuranda mbao, kukamua maji ya matunda, kuchomelea vyuma au kuendesha shughuli zozote za viwandani zinazozalisha maji machafu, vumbi, kelele au harufu mbaya, uchafu ambao unaleta athari kwa binadamu na viumbe wengi katika maeneo ya makazi ya watu bila kuzingatia taratibu za ujenzi. Kupanda miti - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Watu hawaruhusiwi kupanda mazao au mimea mirefu katika maeneo ya mjini na maeneo mengine yaliyopigwa marufuku na Halmashauri, isipokuwa miti. Pia, mmiliki wa eneo lazima apande na kutunza angalau miti 5, na kila mtu lazima afuate taratibu za kuhifadhi mazingira.
9. (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kupanda au kuotesha mazao au mimea mirefu katika maeneo ya mjini pamoja na maeneo mengine yaliyozuiliwa na Halmashauri isipokuwa kupanda miti; (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1) hapo juu, Kila Mmiliki wa Eneo atatakiwa kupanda na kutunza angalau miti mitano (5) ili kuboresha mazingira; (3) Ni wajibu wa kila Mtu kulima ua kufanya shughuli nyingine za kibinadamu kwa kuzingatia taratibu za kuhifadhi mazingira ikiwa ni pamoja na kutokata miti ovyo, kutolisha mifugo katika maeneo yenye mmomonyoko wa udongo, kulima kwa njia ya matuta au kutumia mbinu yoyote ya uhifadhi wa mazingira. Udhibiti wa mifugo - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatenga maeneo maalum kwa ajili ya
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge maeneo maalum ya kulishia mifugo na kilimo, na watu hawaruhusiwi kuacha au kuendesha mifugo kuzurura katika maeneo yaliyokatazwa.
10. (1) Halmashauri itatenga maeneo maalum kwa ajili ya kulishia mifugo na shughuli za kilimo; (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuacha mifugo au kusababisha mifugo kuzurura ovyo mitaani, kuchunga kwenye vyanzo vya maji, kwenye eneo la barabara, Hifadhi ya barabara, au kwenye eneo lolote lisiloruhusiwa. (3) Mifugo itakayokamatwa kwa kosa la kuzurua au kuchungwa katika maeneo yasiyoruhusiwa itatozwa faini ya shilingi elfu moja (1000/=) kwa kila Mbuzi, 7 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) Kondoo, au Nguruwe na shilingi elfu tano (5000/=) kwa kila Ng’ombe, Punda au Ngamia. Ilani ya kuondoa kero - 11 Verify source ↗
(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwepo kwa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa akigundua kero, lazima atoe ilani ya siku 7 kwa mwenye nyumba, mpangaji, mtumiaji, au mtu anayesababisha kero hiyo ili waiondoe.
11. (1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwepo kwa eneo kero yoyote atatoa ilani ya siku saba (7) kwa Mmiliki wa nyumba, Mpangaji, Mtumiaji, na/au Mtu yeyote anayesababisha kuwepo kwa hiyo kero akimtaka kuondoa kero hiyo; Wajibu wa kujenga na kukitumia choo Umbali wa kujenga choo Vyoo vya umma (2) Mtu yeyote atakayeshindwa kutekeleza masharti ya ilani aliyopewa ndani ya muda ulioainishwa kwenye ilani atakuwa ametenda kosa; (3) Endapo Halmashauri italazimika kuondoa kero hiyo, gharama za kuondoa kero hiyo zitalipwa na Mmiliki kabla au baada ya kuondoa kero hiyo. - 12 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila Mmiliki au Mpangaji wa
AI-assisted research summary: Kila mmiliki au mpangaji wa nyumba ya makazi au biashara lazima ahakikishe nyumba ina choo safi, imara na madhubuti kwa matumizi ya wakazi, na kiwe kinatumika wakati wote.
12. Itakuwa ni wajibu wa kila Mmiliki au Mpangaji wa nyumba ya makazi au Nyumba ya Biashara kuhakikisha kwamba nyumba yake ina choo safi, imara na madhubuti kwa matumizi ya Wakazi wa nyumba hiyo na kuhakikisha kinatumika wakati wote. - 13 Verify source ↗
Choo kinatakiwa kijengwe umbali wa mita sitini (60)
AI-assisted research summary: A toilet must be built 60 meters away from any well used for domestic water.
13. Choo kinatakiwa kijengwe umbali wa mita sitini (60) cha maji kutoka kisima chochote kinachotumika kwa matumizi ya Nyumbani. chanzo au - 14 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuruhusu watu, vikundi au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo inayoona yanahitaji huduma hiyo.
14. (1) Halmashauri inaweza kumruhusu Mtu yeyote, vikundi vya watu au Taasisi kujenga vyoo vya Umma (Public toilets) katika maeneo ambayo Halmashauri itaona kuwa kuna haja ya kufanya hivyo; (2) Vyoo hivyo vitamilikiwa na Halmashauri au kwa ubia na wajenzi na vitakuwa ni vya kulipia kama itakavyokuwa imeelekezwa na Halmashauri katika Mkataba na Wakala wake watakaopewa kusimamia 8 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) vyoo hivyo. Vyoo katika maeneo ya mikusanyiko ya Watu Maegesho na Matengenezo ya magari mabovu - 15 Verify source ↗
Mtu yeyote, Kikundi, au Taasisi yenye lengo la
AI-assisted research summary: Watu, vikundi, taasisi na wamiliki wa maeneo fulani lazima wajenge choo kinachotenganisha matumizi kwa kuzingatia jinsia.
15. Mtu yeyote, Kikundi, au Taasisi yenye lengo la kukutanisha watu wengi kwa wakati mmoja au Mmiliki hoteli, migahawa au kilabu cha pombe, kanisa misikiti, au Mtu yeyote anayemiliki wa jengo linalotumiwa na watu wengi atatakiwa kujenga choo kitakachotofautisha matumizi kwa kuzingatia jinsi. - 16 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa Mtu yeyote kuegesha, kuosha, au
AI-assisted research summary: It is forbidden for anyone to park, wash, or repair vehicles or faulty machinery on roads, road reserves, sidewalks, streets, open areas, or any place not set aside for that activity.
16. (1) Ni marufuku kwa Mtu yeyote kuegesha, kuosha, au kutengeneza gari, pikipiki au mitambo mibovu kwenye eneo la barabara, hifadhi ya barabara, njia ya waenda kwa miguu, mtaa, eneo la wazi au eneo lolote ambalo halikutengwa kwa shughuli hiyo. (2) Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yatatakiwa kufanyika kwenye karakana, gereji au maeneo yaliyoruhusiwa baada ya kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri. Wajibu wa kuondoa na kudhibiti mazalia ya mbu. - 17 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa mmiliki wa nyumba kuhakikisha
AI-assisted research summary: The house owner must make sure there is no standing water, wastewater, garbage, or other liquid or solid matter that could become a breeding place for mosquitoes or other harmful insects.
17. Itakuwa ni wajibu wa mmiliki wa nyumba kuhakikisha kuwa hakuna mkusanyiko wa maji, maji machafu, takataka au kitu chochote cha majimaji au kigumu ambacho kinaweza kuruhusu kuwepo kwa mazalia ya mbu au wadudu wengine wenye madhara kwa afya ya binadamu. Upulizaji dawa za kuua Wadudu - 18 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakayetaka kupulizia dawa za kuuwa
AI-assisted research summary: A person who wants to fumigate a house or any place must apply for permission from the Council before doing it.
18. (1) Mtu yeyote atakayetaka kupulizia dawa za kuuwa Wadudu au wanyama waharibifu (Fumigation) katika nyumba yoyote au mahali popote atalazimika kuomba kibali cha kufanya shughuli hiyo kutoka Halmashauri. (2) Halmashauri itajiridhisha kwanza kwamba tahadhali zote zinazoweza kuathiri uhai wa viumbe hai wengine zimechukuliwa, na Mtu huyo anao utaalamu wa kupulizia dawa za kuuwa wadudu au 9 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) Wanyama waharibifu. Uendeshaji wa Hoteli, Hosteli na Shule - 19 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni wajibu wa kila Mmiliki wa nyumba za
AI-assisted research summary: Wamiliki wa baadhi ya maeneo ya biashara na shule lazima wapate kibali cha afya kutoka Halmashauri kabla ya kuanza huduma, baada ya kukaguliwa na kuthibitishwa kuwa wanakidhi masharti ya afya.
19. (1) Itakuwa ni wajibu wa kila Mmiliki wa nyumba za kulala wageni, Mgahawa, Hoteli, Hosteli, Shule au Nyumba za biashara kuhakisha anapata kibali cha afya baada ya kukaguliwa na kuonekana kuwa amekidhi masharti ya afya kutoka Halmashauri kabla hajaanza kutoa huduma. (2) Kibali kitatolewa baada ya Halmashauri kujiridhisha kuwa- (a) upo mwanga na hewa ya kutosha katika eneo la biashara; tahadhali ya moto na dharura nyingine; (b) (c) nafasi na vifaa (samani ) za kutosha; (d) uimara wa jengo; (e) kuna mfumo imara wa maji taka, na maji (f) safi, na uhifadhi wa taka ngumu; kuna vyoo na mabafu safi vya kutumika wa jinsi zote; na (g) kama ujenzi wa jengo umezingatia watu hasusan wenye mahitaji maalumu Walemavu. Upimaji wa afya za Wahudumu - 20 Verify source ↗
(1) Kila baada ya miezi mitatu (3), Halmashauri itapima
AI-assisted research summary: Halmashauri must check the health of listed food and hospitality workers every three months and issue a health certificate, and it may charge a health inspection fee.
20. (1) Kila baada ya miezi mitatu (3), Halmashauri itapima afya za Wahudumu wa Hoteli, mgahawa, baa, bucha, Machinjio, sehemu za kuokea mikate, nyumba za kulala wageni, yeyote grosari anayetengeneza chakula kwa ajili ya kuuza na kutoa hati ya afya; au mtu (2) Halmashauri itatoza ada ya ukaguzi wa afya kwa na vitakavyopangwa Mujibu wa kutangazwa na Halmshauri.. viwango Uwezo wa kutoa adhabu ya papo kwa papo - 21 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kutoa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kutoa adhabu ya papo kwa papo kwa mtu anayechafua mazingira kwa kukiuka sheria ndogo za usafi wa mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.
21. (1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kutoa adhabu ya papo kwa papo kwa Mtu yeyote taratibu atakayechafua mazingira kwa kukiuka 10 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) zilizowekwa na Sheria ndogo hizi na; (2) endapo adhabu hiyo itahusisha malipo ya faini, Afisa Mwidhiniwa atamkatia Mkosaji stakabadhi ya malipo kutoka Halmashauri. Makosa - 22 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kufanya vitendo vya uchafuzi, kuzuia afisa, kuuza pombe ndani ya nyumba ya makazi, kufanya shughuli fulani za gari/viwanda nje ya maeneo yaliyotengwa, au kwenda haja ovyo katika maeneo ya umma.
22. Mtu yeyote ambaye- (a) atamzuia au kumzuia Afisa kujaribu Mwidhiniwa asitekeleze wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hizi; au (b) atatiririsha maji machafu au atamwaga takataka katika mtaa, mtaro wa maji ya mvua, uchochoroni, au mahali popote hadharani au katika eneo lolote la wazi bila idhini ya Halmashauri; (c) ataendesha biashara ya pombe ndani ya nyumba ya makazi; (d) ataosha gari, kufua, kunywesha mifugo na kukoroga dawa za mimea ndani ya mito, mabwawa, lambo au ndani ya chanzo maji au kisima kinachotumika kwa matumizi ya binadamu; (e) atauza vyakula vilivyopikwa bila kufuata taratibu za kiafya zilizowekwa na sheria ndogo hizi; (f) atafanya matengenezo ya gari, pikipiki na mitambo, kuendesha shughuli za viwanda katika barabarani, maeneo uchochoroni, au katika maeneo yasiyotengwa kwa shughuli hizo bila kuzingatia taratibu za mipango miji; ya wazi, makazi, (g) ataenda haja ndogo au kubwa hovyo barabarani, 11 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) uchochoroni, upenuni au mahali popote ambapo siyo chooni. (h) atakwenda kinyume na Sheria ndogo hizi Adhabu - 23 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetenda kosa na kupatikana na hatia
AI-assisted research summary: Anyone convicted of an offence may be fined up to 300,000 shillings, jailed for up to 12 months, or given both penalties.
23. Mtu yeyote atakayetenda kosa na kupatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu (300,000/=) au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili (12) jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. Kufifilisha kosa - 24 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote faini isiyozidi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kutoza mtu yeyote faini isiyozidi shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa maandishi na anakubali kulipa faini iliyowekwa chini ya Sheria Ndogo hizi.
24. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote faini isiyozidi shilingi Elfu Hamsini (50,000/=) iwapo mkosaji atakiri kosa kwa maandishi na kukubali kulipa faini iliyoainishwa chini ya Sheria Ndogo hizi. JEDWALI LA KWANZA (Chini ya kifungu cha 6(2) SEHEMU “A” ADA YA KUZOA TAKA NA.
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 17 Verify source ↗
Section 17
AI-assisted research summary: This section lists different business/building types and the monthly fees charged for them.
17. AINA YA JENGO/ BIASHARA Wafanyabiashara wakubwa Maduka ya rejareja Mgahawa mdogo Mgahawa Mkubwa Nyumba ya kulala Wageni Kiwanda cha mbao Fundi Seremala/ Karakana/ Kuchoma vyuma (Mchundo) Kiwanda kidogo Kiwanda kikubwa Bar, klabu za usiku, kumbi za starehe, Duka la nyama na samaki Duka la Dawa Meza za Matunda Mama Ntilie, wauza matunda na miwa Kituo cha kuuzia mafuta Fundi cherehani, Wasusi, Vinyozi Wauza Mkaa, klabu za pombe za kienyeji/ asili ADA KWA MWEZI 10,000/= 5,000/= 10,000/= 5,000/= 10,000/= 6,000/= 10,000/= 20,000/= 50,000/= 10,000/= 5,000/= 5,000/= 2,500/= 3,000/= 10,000/= 2,500/= 5,000/= 12 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) JEDWALI LA PILI (Chini ya kifungu cha 20) ADA YA UKAGUZI WA AFYA Na. Aina ya biashara Kiwango cha ada kwa mwaka
Part
JEDWALI LA PILI
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: This section is titled “Guest Houses and Hotels.”
3. Nyumba za Wageni (Guest House) na Hoteli - 5 Verify source ↗
Majengo mengineya Biashara
AI-assisted research summary: Ilani inampa mpokeaji muda wa siku 7 kuondoa au kusafisha uchafu/kero, na muda wa siku 30 kutekeleza maelekezo ya kujenga choo; akishindwa, Halmashauri inaweza kuchukua hatua kali za kisheria bila taarifa nyingine.
5. Majengo mengineya Biashara 5000/= 2,500/= 10,000/= 10,000/= 5,000/= JEDWALI LA TATU (Chini ya kifungu cha 11) ILANI YA KUONDOA KERO Ilani hii imetolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo za Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, 2016. SEHEMU ‘A’ Ndugu…………............... wa Mtaa/Kijiji …………… Kata ya……………Unaarifiwa kwamba katika ukaguzi uliofanyika Tarehe……mwezi………..mwaka…. katika nyumba yako ya Biashara/kuishi iliyopo eneo la……………..kumekutwa machukizo/kero/uchafu kama ifuatavyo; 1) ………………………………………………………………………………….. 2) ………………………………………………………………………………….. SEHEMU ‘B’ Kwa ILANI hii unaamriwa ndani ya muda wa siku saba (7) tangu siku ya kupokea ilani hii, unatakiwa kutekeleza kwa kuondoa/ kurekebisha/ au kusafisha machukizo/ kero/ uchafu uliotajwa hapo juu; kushindwa kwako kutekeleza ndani ya muda uliopewa Halmashauri italazimika kukuchukulia hatua kali za kisheria bila kulazimika kukupa taarifa. 13 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) ………………………………….. AFISA MUIDHINIWA IMEPOKELEWA NA; Jina;…………………………. saini……………………….... wadhifa……………………….. Tarehe………………………... IMETOLEWA NA; Jina;………………………. Saini……………………… Wadhifa…………………... Tarehe…………………….. *Futa lisilohusika JEDWALI LA TATU (Chini ya kifungu cha 12) ILANI YA KUJENGA CHOO Ilani hii imetolewa kwa mujibu wa Kifungu kidogo cha 32 cha Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, 2016 SEHEMU ‘A’ Ndugu…………………...............wa Mtaa/Kijiji……………Kata ya…………Unaarifiwa kwamba katika ukaguzi uliofanyika Tarehe……mwezi………..mwaka….Katika nyumba yako ya Biashara/kuishi/kutolea Huduma la katika ………………katika Kitongoji/Mtaa*………. Kijiji cha……………Kata ya…………. Imekutwa haina choo/ choo kimejaa/kimeharibika* hivyo unaamriwa kutekeleza mambo yafuatayo; ya …………………….. iliyopo eneo (1) ………………………………………………………………………………… (2) ………………………………………………………………………………… SEHEMU ‘B’ Unapewa muda wa siku thelathini (30) tu tangu siku ya kupokea ilani hii kutekeleza maelekezo yote yaliyoelezwa katika sehemu ‘A’ ya Ilani hii, SEHEMU ‘C’ Ukaguzi utafanyika tarehe……………….endepo utashindwa kutekeleza maelekezo ndani ya muda uliopewa Halmashauri itakuchukulia hatua kali za kisheria bila kukupa taarifa nyingine. kuthibitisha utekelezaji maelekezo uliyopewa wa wa 14 Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tangazo la Serikali Na. 22 (linaendelea) …………………….. AFISA MUIDHINIWA IMETOLEWA NA; IMEPOKELEWA NA; Jina ;………………………. Jina ;…………………………. saini………………………….... Saini……………………… wadhifa……………………….. Wadhifa…………………... Tarehe………………………... Tarehe…………………….. Nembo ya halmashauri ya Wilaya ya Malinyi imebandikwa kwenye Sheria ndogo hizi kufuatia azimio iliyotolewa katika kikao kilichofanyika tarehe 23.04.2016 na ilibandikwa mbele ya:- la Halmashauri SAID ALLY MSOMOKA, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi. FADHILI NASSORO LIGUGUDA, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi. NAKUBALI, Dodoma, 09Januari, 2017 GEORGE B. SIMBACHAWENE (MB) Waziri wanchi-or-Tamisemi. 15
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi za Mwaka 2017
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in